Nyumbani » 09/07/2012
Entries posted on “Julai 9th, 2012”
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa ufisadi ni kizuizi kikubwa cha maendeleo katika mataifa mengi, na unafaa kukabiliwa kwa uwazi na uajibikaji. Akilihutubia jopo la ngazi ya juu kuhusu uwajibikaji, uwazi na maendeleo endelevu, Bwana Ban amesema tatizo la ufisadi linawaathiri zaidi watu wenye uwezo mdogo, kwani wanalazimika kulipa rushwa ili [...]
09/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Sheria za kuadhibu watu pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu unaongeza vifo kutokana na Ukimwi, uharibifu wa fedha na kuwa kizuizi katika vita vya kimataifa dhidi ya Ukimwi, imesema ripoti ya tume huru ya kimataifa kuhusu Ukimwi na sheria, ambayo inawahusisha viongozi na wataalam. Tume hiyo iliyofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la [...]
09/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kitengo nambari 5 cha Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, leo Julai 9 kimeweka tarehe za kuanza kusikilizwa kesi dhidi ya washukiwa wanne wa machafuko yalotokana na uchaguzi uliopita nchini Kenya kama tarehe 10 na 11 Aprili mwaka 2013. Kuwekwa tarehe ya kesi dhidi ya William Samoei Ruto, Joshua Arap Sang, Francis Muthaura na Uhuru Kenyatta, [...]
09/07/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametuma salama zake za pongezi kwa wananchi wa Timor-Leste, serikali na makundi ya vyama vya kisiasa kwa kufanikisha uchaguzi wa bunge katika hali ya amani na utulivu mkubwa. Ban katika salamu zake, amesema kuwa ametiwa moyo na kuhamasishwa namna wananchi wa taifa hilo walivyojitokeza na kufanikisha uchaguzi [...]
09/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kupitia usaidizi kutoka kwa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP mengi kati ya majimbo kumi nchini Sudan Kusini yameboresha ukusanyaji wa ushuru kwa asilimia 100 baada ya kubuniwa idara za ukusanyaji wa ushuru. Hii ni mojawapo ya hatua zilizizochukuliwa kuboresha ukusanyaji wa ushuru uamuzi uliotolewa baada ya kusitishwa shughuli za usafirishaji wa mafuta [...]
09/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amesema kuwa hali nchini Syria inazidi kuwa mbaya akisema ukiukaji wa haki za binadamu unaendelea nchini humo yakiwemo mauaji. Akihutubia waandishi wa habari Ban amesema kuwa kwa sasa Takriban watu milioni 1.5 wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu. Kwenye mkutano wake wa kwanza mjini Geneva kundi kuhusu Syria liliafikiana [...]
09/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya afya, Anand Grover, amelipongeza bunge la Muungano wa Ulaya kwa kukataa mkataba wa biashara unaohusu bidhaa bandia (ACTA) kama hatua muhimu katika kuhakikisha watu wanaendelea kupata dawa muhimu na za bei nafuu na matibabu, kama sehemu ya kulinda haki zao za afya. Bwana Grover amesema kuzuiwa [...]
09/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Raia wa Timor Leste takribani 600,000 mwishoni mwa wiki wamejitokeza kuwasilisha sauti zao kwa njia ya kura kwenye uchaguzi mkuu wa bunge mwaka 2012. Kama kawaida vituo vya upigaji kura vilifunguliwa mapema asubuhi na kulishuhudiwa misruiru mirefu ya watu wenye hamasa na hamu ya kutekeleza haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka. Katibu Mkuu wa Umoja [...]
09/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu utowekaji wa kulazimu, limeanza kuchunguza tena zaidi ya visa 200 vya utowekaji kama huo. Visa hivyo vinahusisha baadhi ya visa chini ya mkakati wake wa visa vinavyohitaji hatua za dharura na habari kuhusu visa vipya na vya kale vinavyohusu nchi zaidi ya 30. Wataalam hao huru watafanya [...]
09/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu wapiganaji wa haki za binadamu na mauaji kinyume sheria, wametoa wito kwa serikali ya Ufilipino kuweka mikakati ya dharura ili kulinda masilahi ya wanaharakati wa haki za binadamu na kuhakikisha kuwa wanaweza kutimiza majukumu yao. Pia wameitaka serikali ya Ufilipino kufanya uchunguzi huru kwa haraka kuhusu idadi inayoongezeka [...]
09/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza jukumu kubwa lililobebwa na tume huru ya kitaifa ya uchaguzi nchini Libya na maelfu ya wafanyakazi wa tume hiyo ambao wamehakikisha kwamba uchaguzi umefanyika vizuri, kwa amani, uwazi na utulivu. Ban amesema anatarajia kumalizika vyema kwa mchakato huo wa uchaguzi ambao umoja wa Mataifa umekuwa radhi [...]
09/07/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Uvuvi endelevu na kilimo cha samaki vinachukua jukumu kubwa katika usalama wa chakula na lishe na kuendesha maisha ya mamilioni ya watu imesema ripoti mpya iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo FAO ihusuyo hali ya uvuvi na kilimo cha samaki. Ripoti hiyo iliyozinduliwa kwenye ufunguzi wa kikao cha 30cha kamati ya uvuvi ya FAO [...]
09/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya Syria Kofi Annan amefanya mazungumzo na Rais Bashar Al-Assad mjini Damascus. Annan anasema wamejadili haja ya kukomesha machafuko na njia za kufanikisha hilo. Amesema katika majadiliano yao wameafikiana mtazamo wa kuchukua kuhakikisha hilo linafanikiwa mtazamo ambao atajadili pia na [...]
09/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa mjini Tokyo Japan Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitolea wito jumiya ya kimataifa kuendelea kujihusisha na kuisaidia Afghanistan. Ban amesema dunia ni lazima iendelee kushikamana na watu wa Afghanistan katika ombi lao la kuwa na usalama, utulivu na mustakhbali mwema. Amesema endapo Afghanistan itakuwa na amani basi [...]
09/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »