Nyumbani » 06/07/2012
Entries posted on “Julai 6th, 2012”
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na chama cha mwezi mwekundu nchini Chad wanapeleka misaada ya dharura kwenye mji ulio kaskazini mwa nchi wa FayaLargeau ambapo tayari wahamiaji 300 wamewasili kutoka Libya siku mbili zilizopita. Jumbe Omari Jumbe wa Shiriko hilo anazungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo.
06/07/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limemteua John knox kama mjumbe maalum wa haki za binadamu na mazingira na pia kutangaza kundi la kushughulia ujenzi wa makao ya walowezi kiyahudi nchini Israel kabla ya kukamilika kwa kikao chake cha 20. Uteuzi huo ulitangazwa na rais wa baraza la la haki za binadamu [...]
06/07/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mshauri maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu michezo kwa maendeleo na amani, Wilfried Lemke, amekaribisha uamuzi uliotolewa na bodi ya kandanda ya kimataifa IFAB kwa kuwaruhusu wanawake wanamichezo kuvaa hijabu iliyo salama kwenye michezo iliyo chini ya usimamizi wa shirika la kandanda duniani FIFA. Amesema kuwa uamuzi huu ni hatua kubwa mbele [...]
06/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM William Lacy Swing anatazamiwa kuwa na ziara ya kikazi Dakar Mji Mkuu wa Senegal ziara inayotazamiwa kuanza hapo jumatatu. Akiwa nchini humo atahudhuria mkutano wa majadiliano ya wazi kwa nchi za afrika magharibi ulioandaliwa na jumuiya ya eneo hilo ECOWAS. Mkutano huo unashabaha [...]
06/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza eneo la Asia ya kati kuanzia tarehe 8- 12 mwezi huu. Pillay ataanzia ziara yake nchini Kyrgyzstan ambapo shirika lake liliweka Ofisi mwaka 2008. Akiwa nchini humo Pillay anatarajiwa kukutana na rais Atambayev, mawaziri, mahakama, watetesi wa [...]
06/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula Dunia, FAO, Jose Graziano da Silva, amesema ulimwengu unafaa kuzingatia jinsi utabiri unaofanywa na wataalam kwenye masoko ya fedha na hisa unavyoathiri bei za chakula. Bwa da Silva amesema hayo kwenye mjadala wa ngazi ya juu kuhusu swala la mfumko wa bei ya chakula kwenye makao makuu [...]
06/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pamoja na washirika wengine wanakutana juma lijalo mjiji Geneva kutafuta njia za kuwasaidia wakimbzi 859,000 kote duniani ambapo makao yanatajwa kuwa suluhu pekee kwao. Mkutano huo ambao utakuwa nchini ya uenyekiti wa Australia na kuleta pamoja waakilishi wa nchi zinazotoa makao, mashirika yasiyokuwa wa serikali na [...]
06/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na chama cha mwezi mwekundu nchini Chad wanapeleka misaada ya dharura kwenye mji ulio kaskazini mwa nchi wa FayaLargeau ambapo tayari wahamiaji 300 wamewasili kutoka Libya siku mbili zilizopita. Wahamiaji hao 300 ni kati ya kundi la watu 1000 waliorejeshwa nchini Chad na utawala wa Libya kwa kuishi nchini [...]
06/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wakati huo huo, Baraza hilo la Haki za Binadam pia limelaani ukiukaji wa haki za binadam unaotendeka kaskazini mwa Mali, na ambao unaenezwa na waasi, makundi ya kigaidi na mitandao mingine ya kihalifu kutoka nchi mbalimbali. Limelaani hasa ukatili unaoetendewa wanawake, mauaji, utekaji nyara, uporaji na uharibifu wa maeneo ya urithi wa kiasili na ibada, [...]
06/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Haki za Binadam la Umoja wa Mataifa, leo limelaani vikali ukiukaji mkubwa wa haki za binadam nchini Syria, pamoja na mauaji na mashtaka yanayoendelezwa dhidi ya waandamanaji, wanaharakati wa haki za binadam na waandishi wa habari. Katika azimio lililoungwa mkono na nchi 41 wanachama, Baraza hilo limesisitiza umuhimu wa kuwafikisha wale wanaopanga na [...]
06/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, linasema kuwa makundi yaliyojihami yanaendelea kuwaingiza kwenye jeshi watoto kwenye maeneo ya kaskazini mwa Mali. UNICEF inaelezea hofu yake kuhusu hatma ya watoto kaskazini mwa Mali, kufuatia ripoti zinazosema kuwa kumeripotiwa visa ya ubakaji wa watoto wasichana. Shirika hilo linasema kuwa ukosefu wa usalama umewalazimu karibu [...]
06/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa wito wa haki na maisha ya watoto kupewa kipaumbele cha haraka katika maendeleo ya nchi wakati maadhimisho ya mwaka mmoja wa uhuru wa Sudan Kusini yakijongea. UNICEF inasema wakati nusu ya watu wa taifa hilo jipya wana umri wa chini ya miaka 18 uwekezaji kwa [...]
06/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kama tulivyowafahamisha Juma lililopita Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Migiro amemaliza muda wake na kurejea nyumbani Afrika baada ya kuutumikia Umoja wa Mataifa kwa miaka mitano. Migiro alikuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na wa kwanza kutoka barani Afrika. Ameondoka akiacha sifa kemkem ya mambo mengi ya kuigwa aliyoyafanya tangu alipoteuliwa [...]
06/07/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »