Nyumbani » 05/07/2012
Entries posted on “Julai 5th, 2012”
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limesema hali nchini Mali inatishia amani ya kimataifa na usalama katika kanda nzima, na kuazimia kuunga mkono juhudi za muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, katika kushirikiana na serikali ya mpito nchini Mali ili kurejesha uongozi wa kikatiba. Katika azimio lake namba 2056 (2012), Baraza [...]
05/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama leo limekaribisha kuanza kazi kwa kitengo cha Arusha cha mfumo wa kimataifa wa kushughulikia makbaki ya kesi za amauaji ya kimbari IRMCT likisisitiza kwamba ni muhimu khakikisha ahakuna atakayekwepa mkono wa sheria hasa wale waliohusika na uhalifu uliotekelezwa Rwanda na Balkans miaka ya 1990s. Baraza limeunda vitengo hivyo Desemba 2010 kna kuvipa [...]
05/07/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwaka mmoja baada ya janga la njaa kuanza nchini Somalia, kijana mmoja, Aden Yusef Kabey, anaweza kucheka akikumbuka uchungu aliopitia, alipokonda kupindukia, akawa hawezi kutembea, kula wala kulala. Sasa anaweza kufanya hivyo, baada ya afya yake kurejea. Mwaka mmoja uliopita, Kabey alilala kwenye kijinyumba cha babake, akiwa amefunikwa kiraga tu. Alikuwa amewasili kutoka Ethiopia, kupitia [...]
05/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO na shirika moja lisilokuwa la kiserikali wametoa wito wa msaada wa dharura utakaofadhili ujenzi wa mbuga moja ya wananyapori iliyovamiwa na wawindaji haramu nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo. Kulingana na UNESCO mbuga ya wanyamapori ya Okapi inayopatikana kwenye msitu wa Ituri ni makao [...]
05/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mjini Kingston, Jamaica, Kwame Boafo, ameelezea kusikitishwa kwake na kuendelea kuwepo sheria za uchongezi kwenye katiba za nchi za eneo la Caribbean, na kuzitaka nchi hizo kuziondoa sheria kama hizo ambazo zinabana uhuru wa vyombo vya habari. Bwana Boafo amesema hayo kwenye kongamano liloandaliwa na Taasisi [...]
05/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ubaguzi wa rangi, chuki za watu wa kigeni na aina zingine za ubaguzi, ametoa wito kwa mataifa kote ulimweguni kuzingatia kwa karibu sana ishara za mwanzo za ubaguzi wa rangi, ambao hatimaye huenda ukakolea na kusababisha mizozo na ukiukaji mbaya zaidi wa haki za binadam. Mtaalam [...]
05/07/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kiwango wastani cha bei ya chakula kimeshuka kwa mwezi wa tatu mfululizo mnamo mwezi Juni mwaka 2012. Kiwango hicho kimeshuka kwa kwa pointi 4, ambazo ni asilimia 1.8 kutoka mwezi Mei, na hivyo kufikia kiwango cha chini zaidi cha kipimo wastani cha bei ya chakula tangu mwezi Septemba 2010. Kiwango wastani cha kipimo cha bei [...]
05/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Maendeleo yanaweza kupatikana tu kupitia ushirikiano na uiano, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, siku ya Alhamis kwenye ufunguzi wa kongamano la Baraza la masuala ya kiuchumi na ya kijamii ya Umoja wa Mataifa, ECOSOC kuhusu ushirikiano katika maendeleo. Amesema mataifa yanayoendelea yanasaidiana kwa kutumia uzoefu yaliyonayo binafsi kuendeleza ushirikiano wa mataifa [...]
05/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa unapendekeza kodi ya kimataifa, na ubunifu wa njia zingine za kupata fedha, ili kuchangisha dola bilioni 400 kila mwaka kwa ajili ya kufadhili maendeleo, na changamoto zingine zinazoikabili dunia, kama vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mapendekezo hayo yamo kwenye ripoti ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo [...]
05/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mpango wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria UNSMIS uko tayari kuzisaidia pande za Syria katika kuchkua hatua zinazohitajika kuelekea katika mazungumzo ya amani amesema mku wa mpango huo Jeneral Robert Mood siku ya Alhamisi. Mood amesema wanauimarisha mpango wa UNSMIS ili uweze kuwasaidia vyema watu wa Syria katika siku zijazo. Ameongeza kuwa watarejesha [...]
05/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesema taifa hilo limepitia kipindi kigumu katika mwaka wake wa kwanza wa uhuru. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Hilda Johnson amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi Alhamisi kwamba Juba itaadhimisha mwaka wa kwanza wa uhuru kutoka Sudan Julai 9 huku ikiwa [...]
05/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »