Nyumbani » 02/07/2012
Entries posted on “Julai 2nd, 2012”
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa siku ya Jumapili dhidi ya makanisa mawili kwenye mji wa Garissa nchini Kenya, na ambayo yalisababisha vifo vya watu 17 na kuwajeruhi wengine wengi. Bwana Ban amesema, mashambulizi hayo ambayo yalilenga maeneo ya ibada kwa kukusudia, ni kihalifu na yanafaa kukemewa [...]
02/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Viongozi wa Libya wamewaachilia huru wafanyakazi wanne wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, ambao walikuwa wamezuiliwa Zintan, baada ya kumzuru Saif Al-Islam Gaddafi, Juni 7. Rais wa mahakama ya ICC, Jaji Sang-Hyun Song, ambaye alisafiri kwenda Zintan, amekaribisha uamuzi wa Libya kuwaachilia huru wafanyakazi hao. Bwana Song aliwashukuru viongozi wa Libya na mamlaka za [...]
02/07/2012 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Mali na hivyo kukwamisha juhudi za utoaji wa misaada ya usamaria mwema katika upande wa kaskazini mwa taifa hilo. Ghasia zinazoendelea kuzuka kwenye eneo hilo zimesababisha pia kubomolewa kwa moja ya jengo lenye historia ya [...]
02/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la uchumi na masuala ya jamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC limesema kuwa litajadili hali ya ukosefu wa ajira duniani linapoanza mkutano wake hii leo. Zaidi ya wajumbe 500 wakiwemo mawaziri wa serikali na wakuu wa mashirika ya umma , mashirika ya kimataifa na sekta za kibinafasi watahudhuria mkutano huo ambao utazungumzia masuala kadha [...]
02/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Nchi 13 tatu zinazoendelea zimechukuwa hatua ili kuimarisha sera za utamaduni na viwanda, kwa mujibu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO. Nchi ambazo tayari zimefaidika kutokana na usaidizi wa kitaaluma wa UNESCO, unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya, ni Argentina na Ushelisheli. Miradi kama hiyo ya mwongozo wa wataalam katika [...]
02/07/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Watu 16 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuvamia makanisa mawili katika mji wa Garissa, kaskazini mashariki mwa Kenya hii Jumapili. Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu walifika eneo hilo, na haraka waliwapeleka majeruhi hospitali. Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi nchini Kenya, Muhoro Ndegwa, watu waliouawa saba [...]
02/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Malengo muhimu matatu ya milenia yamefikiwa miaka mitatu kabla ya wakati ambayo ni umasikini, mitaa ya mabanda na maji, imesema ripoti ya ya malengo ya maendeleo ya milenia iliyozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon. Ban amesema ingawa kufikia malengo mengine yaliyosalia ni changamoto, itawezekana tuu kuyafikia ikiwa serikali zitatimiza majukumu [...]
02/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wahamiaji, François Crépeau, ametoa wito kwa Uturuki na Muungano wa Ulaya kutoa kipaumbele kwa haki za binadamu za wahamiaji, katika muktadha wa ushirikiano wao katika kudhibiti uhamiaji. Mtaalam huyo amesema, anakaribisha mabadiliko muhimu ya kisheria na kitaasisi katika sera za uhamiaji za Uturuki, yakiwemo [...]
02/07/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linalohusika na ubaguzi wa wanawake kisheria na katika vitendo, limesema kuwa vipindi vya mpito kisiasa hutoa fursa ya kipekee ya kuendeleza haki za binadamu za wanawake, licha ya kuwepo hatari kurudi nyuma na aina mpya za ubaguzi. Wakitoa ripoti yao ya kwanza ya kila mwaka kwa Baraza la [...]
02/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya Wapalestina waliowekwa chini ya ulinzi wa Israel imepanda na kufikia 309, kwa mujibu wa mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Richard Falk ambaye ni mtaalam wa hali ya haki za binadam katika maeneo ya Kipalestina, amesema watu wanaozuiliwa ni wafungwa wa dhana, na kwamba hawakuhusika na vitendo vyovyote vya ghasia. [...]
02/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkutano kuhusu mkataba wa kimataifa wa biashara ya silaha umeanza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kwa mara ya kwanza nchi wanachama wamekusanyika kujadili mkataba utakaokuwa ukifuatilia utaratibu wa kimataifa wa biashara ya silaha. Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kila aliyehudhuria mkutano huo anaandika historia, kwani ni [...]
02/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Umoja wa Mataifa la masuala ya uchumi na jamii ECOSOC limeanza kikao chake cha ngazi ya juu Jumatatu likijadili masualua kadhaa lakini kubwa ni matatizo ya ajira duniani. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wanakutana wakati ambapo dunia inaendelea kufunikwa na kivuli cha [...]
02/07/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »