Wataalamu wa UM Walaani Mauaji yanayoendelea Iran

Kusikiliza /

mauaji, Iran

Wataalam watatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji na utesaji Iran, wamelaani mauaji ya hivi karibuni ya watu wanne kutoka jamii ndogo ya Kiarabu ya Ahwaz kwenye jela ya Ahwaz Karoun, katika jamhuri ya Iran. Kufuatia kesi ambayo hakuendeshwa kwa njia ya uwazi na haki, watu hao walipewa hukumu ya kifo na kuuawa karibu siku ya Juni 19 mwaka huu.

Watu hao waliouawa ni Abdul Rahman Heidarian, Abbas Heidarian, Taha Heidarian and Ali Sharif. Wataalam hao huru wa haki za binadamu wamesema, kutokana na kutokuwepo uwazi katika uendeshaji mashtaka, kuna hofu kwamba shughuli nzima haikuendeshwa kwa njia nzuri na ya haki. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2013
T N T K J M P
« mei    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930