Wakati chakula kikiongezeka, Sahel kusalia na njaa:FAO

Kusikiliza /

usalama wa chakula barani Afrika

Mtazamo wa robo ya mwaka wa shirika la chakula na kilimo FAO kuhusu kilimo na usalama wa chakula unatoa matumaini kwa uzalishaji wa nafaka duniani, lakini unaonya kwamba maeneo mbalimbali yanatarajiwa kukabiliwa na athari za mvua haba, hali mbaya ya hewa , vita na wakimbizi.

Mtazamo huo ambao ni ripoti ya matarajio ya uzalishaji mazao na hali ya chakula inasema kuna ongezeko la asilimi 3.2 ya uzalishaji wa nafaka duniani kwa mwaka 2012 na hivyo kufikisha tani milioni 2419 hasa kutokana na mahidi Marekani, huku bei ya ngano ikishuka mwezi Mai kwa sababu ya ongezeko la uzalishaji.

Hata hiyo maeneo ya Sahel, Yemen na Syria yanatarajiwa kusalia katika matatizo ya chakula. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031