UNSMIL yaitaka Libya kumalia mizozo iliyopo nchini humo

Kusikiliza /

Ian Martin

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lybia amelezea wasi wasi uliopoa kutokana na kushuhudiwa mapigano mapya kwenye sehemu kadha ambapo watu wameuawa , kujeruhiwa na kulazimika kuhama makwao na kutaka tawala husika kuwalinda raia.

Ian Martin ambaye pia ni mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL amesema kuwa ni jambo muhimu iwapo serikali itachukua hatua za haraka kuzima mizozo hii na kuwahakikishia usalama raia.

Hata hivyo Martin alikaribisha hatua ambazo tayari zimechukuliwa na akaushauri utawala wa Libya na pande zote

husika kumaliza mapigano hasa kwenye maeneo la Kufra na Zintam–Shaqiqa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2013
T N T K J M P
« mei    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930