Taasisi zapanga kuongeza ujenzi wa madarasa Gaza

Kusikiliza /

ujenzi wa darasa Gaza

Taasisi kadhaa za kimataifa zimendua mpango wa pamoja wenye shabaha ya kuimarisha hali ya elimu katika eneo la Gaza.

Shirika la kuhudumia wakimbizi huko Gaza UNRWA, kwa kushirikiana na taasisi nyingine zimeweka shabaha ya kujenga madarasa nane katika shule ya msingi ya Al Durj iliyoko mjini Gaza.

Shule hiyo ya msingi kwa sasa inajumla ya wanafunzi 1,900 ambao huingia shuleni kwa kufuata mikondo ya awamu mbili.Kujenga kwa madarasa hayo kunatazamia kupunguza kwa hali ya msongamano unaoshuhudiwa sasa kwa baadhi ya madarasa.

Ujenzi huo unatazamia kuwaondolewa usumbufu wanafunzi wapatao 630 ambao kwa sasa wanasoma katika hali ya mazingira magumu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031