Maandalizi ya Rio+20 yanaingia manthari ya muda wa dharura

Kusikiliza /

Hali ya dharura imejitokeza katika manthari ya siku ya mwisho ya mazungumzo kuhusu mswada wa kisiasa wa mkutano wa Rio+20 kuhusu maendeleo endelevu. Kauli hii imetoka kwa Nikhil Seth, ambaye ni msimamizi wa makao makuu ya mkutano huo, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Rio de Janeiro, Brazil Ijumaa.Wawakilishi wa serikali wamekuwa wakikutana mjini Rio tangu Jumatano ili kuandaa mswada wa mkataba kabla kuwasili kwa viongozi wa nchi kwa mkutano huo unaoanza tarehe 20 Juni. Tofauti zinatokana na ufadhili, uchumi wenye kujali mazingira na kuimarisha taasisi. Nikhil Seth anasema, adui mkubwa sasa, ni wakati.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29