Licha ya mashambulizi, Ivory Coast iendeleze maridhiano

Kusikiliza /

Doudou Diène katikati

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Ivory Coast , Doudou Diène, amewatolea wito Wa Ivory Coast wote na jumuiya ya kimataifa, kuendelea kutoa msaada wao kuunga mkono maridhiano ya kitaifa, baada ya mashambulizi ya Ijumaa iliyopita ambayo yalikatili maisha ya walinda amani saba wa Umoja wa Mataifa, raia wanane na mwanajeshi mmoja wan chi hiyo.

Bwana Diene amesema mashambulizi haya yanatoa changamoto kubwa kwa watu wa Ivory Coast na kwa jumuiya ya kimataifa, na licha ya hofu ya usalama iliyosababishwa na mashambulizi haya, watu wa Ivory Coast wakabiliane nayo kwa kujizatiti na kuimarisha demokrasia, usawa katika mfumo wa haki na sheria, kufufua uchumi na upatanisho wa kitaifa.

George Njogopa na taarifa kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031