Jinsia Sio Tija ya kutotekeleza Wajibu na Malengo:Migiro

Kusikiliza /

Naibu Katibu Mkuu Asha Rose-Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayemaliza muda wake wiki hii na kuondoka Asha Rose Migiro amesema anaushukuru Umoja wa Mataifa kwa kumpa fursa ya kipekee kutumikia dunia kwa miaka mitano. Migiro aliyeteuliwa mwaka 2007 kushika wadhifa huo kama mwanamke wa kwanza kutoka barani Afrika na mwanamke wa pili katika historia ya Umoja wa Mataifa amesema anaondoka akiwa amejawa na furaha na kujivunia mafanikio yaliyopatikana wakati wa uongozi wake.

Angizungumza na idhaa hii katika mahojiano yake ya mwisho kabla ya kuondoka amesema pamoja na changamoto zilizojitokeza katika uongozi wake anapenda dunia na hususani wanawake watambue kwamba jinsia sio sababu ya kumfanya mwanamke kushindwa kutimiza majukumu au kufanya kazi yake ipasavyo, kwani yeye ni mfano.

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)

Kwa mahojiano marefu na Bi migiro usikose kusikiliza makala yetu ya wiki sehemu ya kwanza juma hili na sehemu ya pili Juma lijalo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031