Hatuwezi kuwa na maendeleo endelevu bila afya nzuri- WHO

Kusikiliza /

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema mkutano wa kimataifa wa Rio+20 unatoa fursa muhimu kwa ulimwengu kutambua na kufahamu uhusiano uliopo kati ya afya ya mwanadamu na maendeleo endelevu. WHO limesema takriban watu milioni 150 hupitia taabu kubwa kifedha kila mwaka kwa sababu huwa wanaumwa na kutafuta huduma za afya ambazo wanahitajika kulipia papo hapo. Kwa sababu hii, wengi huuza mali zao, au kukopa fedha ili kutimiza mahitaji haya, na watu milioni 100 huingia katika umaskini kwa sababu zizo hizo.

WHO imesema kutopata huduma za afya kunawaletea watu umaskini kwa sababu hawawezi kufanya kazi, na kwamba ukosefu wa huduma za afya kunawaweka katika umaskini kwa sababu hawawezi kuzilipia. Hivyo, WHO imesema, kuwalinda watu kutokana na gharama kubwa ya matibabu na kuhakikisha wanapata huduma muhimu za afya kupitia mfumo wa Afya kwa Wote, kuna uwezo wa kuongeza maendeleo ya kiuchumi, kuongeza nafasi za elimu, kuwapa wanawake uwezo zaidi, kupunguza umaskini na kuongeza utengamano wa kijamii, na hivyo, kuchangia maendeleo endelevu.

Baadhi ya wale wanaohudhuria mkutano huo wa Rio+20 wanalitambua hili. Miongoni mwao ni Patricia Kuya anayewakilisha kundi la kina mama wa Afrika na anatokea nchini Tanzania.

(SAUTI YA PATRICIA KUYA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930