Duunia yapata hasara kubwa kutokana na majanga

Kusikiliza /

Majanga

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kupunguza majanga Margaret Wahlstrom hii leo amewataka wanachama wa Umoja wa Mataifa kuangazia athari ambazo zimesababishwa na majanga ya kiasili tangu kufanyika mkutano wa dunia mjini Rio de Janeiro miaka ishirini iliyopita.

 Wahlstrom amesema kuwa mkutano wa mwezi huu kuhusu maendeleo endelevu utaangazia hasara ambayo imeshuhudiwa duniani kwa muda wa miaka ishirini iliyopita tangu kufanyika kwa mkutano wa aina hiyo.

Amesema kuwa tangu kufanyika mkutano huo inakadiriwa kuwa majanga yamesababisha vifo vya watu milioni 1.3 , yamewaathiri watu bilioni 4.4 na kuleta hasara ya dola trillioni mbili.

Wahlstrom amesisitiza kuwa mkutamno wa Rio+20 unastahili kuweka malengo ambayo yatamaliza hasara zinazooshuhudiwa zikiwemo za kibinadamu , kijamii na kiuchumi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930