Nyumbani » 29/06/2012 Entries posted on “Juni 29th, 2012”

UNESCO yaorodhesha Kanisa la Kiasili na barabara ya mahujaji Bethlehem kwenye maeneo ya urithi

Kusikiliza / Kanisa la Kiasili, Bethlehem

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limeorodhesha Kanisa la Kiasili, ambako alizaliwa Yesu, na barabara ya mahujaji iliyopo mji wa Bethlehem, Palestina, kama maeneo ya urithi wa kiasili. Maeneo mengine ambayo yameorodheshwa na UNESCO yanapatikana Israel, Palau, Indonesia na mji wa Rabat, Morocco. Maandishi maalum yanaendelea kuwekwa kwa ajili ya [...]

29/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano Wahitajika ili Kuondoa Tishio la LRA:UNOCA

Kusikiliza / Abou Moussa

Mwakilishi maalum na mkuu wa afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika ya Kati na maeneo yaloathiriwa na waasi wa LRA (UNOCA), Abou Moussa, ametoa wito kwa Baraza la Usalama na jamii ya kimataifa kuunga mkono utekelezaji wa mkakati wa kikanda wa Umoja wa Mataifa, na mchakato wa ushirikiano wa Muungano wa Afrika, ili kukomesha [...]

29/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wengi Wameathiriwa Machafuko ya Rakhine, Myamar:OCHA

walioathiriwa Myanmar

Kiasi cha watu 78 wamepoteza maisha na wengine 87 wamejeruhiwa wakati kulipozuka machafuko katika jimbo la Rakhine liliko nchini Myanmar. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa ofisi za Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia na masuala ya usamaria mwema OCHA kama ilivyozinukuu toka wizara ya habari ya nchini humo. Kiasi cha nyumba 3000 ziliharibiwa na kubomolewa wakati [...]

29/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Taasisi zapanga kuongeza ujenzi wa madarasa Gaza

Kusikiliza / ujenzi wa darasa Gaza

Taasisi kadhaa za kimataifa zimendua mpango wa pamoja wenye shabaha ya kuimarisha hali ya elimu katika eneo la Gaza. Shirika la kuhudumia wakimbizi huko Gaza UNRWA, kwa kushirikiana na taasisi nyingine zimeweka shabaha ya kujenga madarasa nane katika shule ya msingi ya Al Durj iliyoko mjini Gaza. Shule hiyo ya msingi kwa sasa inajumla ya [...]

29/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM Waungana na Sanaa ya Fasheni Kukabili njaa

Kusikiliza / UM na sanaa ya fasheni

Umoja wa Mataifa leo imetangaza kuanzisha mashirikiano ya karibu na waendeshaji wa sanaa za fasheni ili kukabiliana na tatizo la umaskini na kutoa msaada wa chakula kwa mamilioni ya wanawake na watoto wanaotabika duniani kote. Mashirikiano hayo yanayojulikana kama fasheni kwa maendeleo F4D, yanania ya kuongeza msukumo kwenye mpango wa maendeleo ya mellenia ya Umoja [...]

29/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Amos aelezea Wasi Wasi Wake Kutokana na Hali ya Wakimbizi nchini Sudan Kusini

Kusikiliza / Valerie Amos

Mratibu wa huduma za dharura kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos ameelezea wasi wasi uliopo kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu kwenye majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan. Taarifa kutoka kwa Ofisi ya Amos inasema kuwa maelfu ya watu wamekwama kwenye eneo la mzozo wakiwa hawana chakula, maji , makao [...]

29/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yachimba Visima na Kujenga Matenki ya Maji kwenye Kambi ya Wakimbizi ya Doro Sudan Kusini

Kusikiliza / matenki ya maji

Shirika la la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha zoezi la uchimbaji visima na kujenga jumla ya matenki mawili kwa minajili ya kuwahakikishia maji takriban wakimbizi 42,000 kwenye kambi ya Doro kwenye jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini. Inakadiriwa kuwa watu 107,000 wamevuka mpaka na kuingia jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini na sasa [...]

29/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hadhi ya kuwa Mkimbizi kwa Wakimbizi nchini Angola na Liberia kufikia kikomo mwezi huu

Kusikiliza / wakimbizi wa Angola

Wakimbizi wanaoishi kwenye mataifa ya Angola na Liberia huenda wakapoteza hadhi za kuwa wakimbizi itimiapo tarehe 30 mwezi huu. Kunzia wakati huo wakimbizi wanaoishi kwenye nchi hizo mbili hawatambuliwa kama wakimbzi na shirika la kuwahudumia wakimbzi la Umoja wa mataifa UNHCR na pia serikali zinazowapa hifadhi. Nchini Liberia wakimbizi waliolikimbia taifa hilo wakati wa vita [...]

29/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria ya Marekani kuhusu Afya inaweza Kupunguza Mwanya katika Usalama wa Kijamii:ILO

Kusikiliza / huduma za afya Marekani

Shirika la Ajira Duniani, ILO, limesema sheria ya kubadili mfumo wa huduma za afya Marekani inaweza kusaidia kupunguza mwanya wa usalama wa kijamii, ambao kwa sasa unawaathiri hadi watu milioni 30 kote nchini. Mratibu wa sera za afya katika idara ya usalama wa kijamii ya ILO, Dr. Xenia Scheil-Adlung, amesema sheria hiyo mpya bila shaka [...]

29/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yahofia Usalama wa Chakula Kenya kufuatia Uhaba wa Mvua

Kusikiliza / mazao duni nchini Kenya

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema hali ya usalama wa chakula nchini Kenya inatia wasiwasi kufuatia ukame uliofuatiwa na kiwango cha chini cha mvua. Kutokana na hali hiyo, ukaguzi uliofanywa mwezi Juni unaonyesha kuwa hadi watu milioni 2.4 watakumbwa na uhaba wa chakula, kufuatia mvua haba kati ya mwezi Machi [...]

29/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP Kuongeza Msaada wa chakula Sudan Kusini

Kusikiliza / raia wa Sudan Kusini

Baada ya kuwasaidia zaidi ya watu 1.9 Sudan Kusini, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, linapanua utoaji wa msaada kwa watu zaidi wanaokabiliwa zaidi na tishio la njaa, wakati msimu wa njaa ukiendelea. Shirika hilo limepanga kutoa msaada wa chakula kwa watu milioni 2.9 mwaka huu, kupitia ugawaji wa kawaida, na [...]

29/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Biashara lazima Ziheshimu Haki za Binadamu kwa Maendeleo Endelevu ya uhakika:Rio+20

Kusikiliza / nembo ya Umoja wa Mataifa

Chombo cha wataalamu wa Umoja wa Mataifa kinachohusika na kuchagiza biashara zote kuheshimu haki za biinadamu katika sekta zote na katika nchi zote kimeelezea hofu kuhusu hati ya matokeo ya mkutano wa maendeleo endelevu wa Rio+20. Chombo hicho kinasema hati hiyo imeshindwa kueleza kwamba biashara lazima ziheshimu haki za binadamu katika juhudi za kuelekea uchumi [...]

29/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Ban anatumai Mkutano wa Geneva utakuwa Mwanzo wa Mabadiliko kwa Mgogoro wa Syria

Kusikiliza / Kofi Annan na Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasafiri kuelekea Geneva Ijumaa ya leo ili kuhudhuria mkutano Jumamosi wa kundi la kuchukua hatua dhidi ya hali inayoendelea Syria. Mkutano huo umeitishwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu Syria Kofi Annan,na unafanyika wakati ambapo mgogoro wa Syria umeshika kasi [...]

29/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Migiro asema kwaheri Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Asha Migiro na Joshua Mmali

Naibu Katubu Mkuu wa Umoja wa mataifa wiki hii anafungasha virago na kurejea nyumbani Afrika baada ya kuutmikia Umoja wa mataifa kwa miaka mitano. Migiro ambaye ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na kwanza barani Afrika anasema anaondoka Umoja wa Mataifa kifua mbele akijivunia mengi mazri na mafanikio aliyoyapata si kwake binafsi bali kwa [...]

29/06/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031