Nyumbani » 27/06/2012
Entries posted on “Juni 27th, 2012”
Kusikiliza /

Makundi mbalimbali yanayojumuisha wanawake yamehudhuria mkutano wa Rio+20 uliomalizika tarehe 22 Juni nchini Brazil. Musimbi Kanyoro kutoka Kenya ni miongoni mwa wanawake waliohudhuria mkutano huo. Akizungumza na Monica Grayely wa Radio ya UM amefananua kilichompeleka Rio kwenye Mkutano: (MAHOJIANO
27/06/2012 | Jamii: Mahojiano, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesimamia kikao cha kamati maalum kuhusu usalama wa chakula duniani. Ban amekaribisha matokeo thabiti ya mkutano wa Rio+20 kuhusu usalama wa chakula na lishe. Kufuatia kuzinduliwa kwa mchakato wa kutokomeza njaa wiki ilopita, kamati hiyo maalum itaelekezwa tena kuzingatia malengo matano muhimu ya mchakato huo, kama mwongozo [...]
27/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Juma moja baada ya kukamilika kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu sasa kikao cha tume ya maadili, Sayansi na Teknolojia ulimwenguni kitatoa fursa kwa wataalamu, serikali na jamii ya wanasayansi kuweza kujadili ni kwa njia ipi madili yaweza kuchangia maendeleo endelevu kupitia sayansi na Teknolojia. Suala la mchango uliotolewa na sayansi na [...]
27/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kiasi cha watu 52,000 wamekosa makazi kutokana na machafuko yaliyoibuka hivi karibuni katika jimbo la Rakkhine, nchini Myanmar ambayo yalisababisha mamia ya watu kuyahama makazi yao. Kwa mujibu wa maafisa wa serikali watu hao sasa wamepatiwa hifadhi katika vijiji vipatavyo 66. Wakati wa machafuko hayo yaliyoanza May 28 watu 50 walipoteza maisha huku wengine 54 [...]
27/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limezindua chapisho lake la rangi lilaolezea mafanikio iliyoyapata wakati ikitekeleza majukumu yake ya kimaendeleo duniani kote. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa machapisho hayo 18, mtendaji mkuu wa shirika hilo Bi Helen Clark amesema kuwa,jambo la kutiliwa maanani kwenye machapisho hayo ni namna yalivyoweza kugusa moja kwa moja [...]
27/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la chakula na kilimo, FAO pamoja na shirika la kimataifa la afya ya wanyama, (OIE), yamezindua kwa pamoja mchakato wa kimataifa, wa kukabiliana na ugonjwa wa shuna, unaoathiri midomo na miguu ya mifugo. Mashirika hayo mawili yamesema dhamira na hatma ya mchakato huo ni kutokomeza kabisa ugonjwa huo duniani. Hata hivyo, mashirika hayo yamesema [...]
27/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kufuatia kuzinduliwa kwa mchakato wa kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV na afya ya uzazi kwa vijana wa Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika mwaka 2011, serikali ya Ujerumani, Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI, UNAIDS na Shirika la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, yameweka kamati ya viongozi wa kisera na wataalam ambao [...]
27/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Serikali ya Myanmar na Umoja wa Mataifa leo wametia sainiampango wa kuchukua hatua ya kuzuia uingizaji na utumiaji wa watoto katika majeshi ya Myanmar Tatmadaw na kuruhusu kuachiliwa kwa askari watoto. Mpango huo umetiwa saini mjini Na Pyi Taw kati ya meja jenerali Ngwe Thein mkurugenzi wa wizara ya ulinzi, meja jeneral Tin Maung Win [...]
27/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Uchunguzi uliofanywa na Shirika la Ajira Duniani, ILO, umebainisha kuwa idadi ya watoto wa Kifilipino walio kwenye ajira ya watoto ilipanda na kufikia milioni 5.5 mwaka 2011. Watoto hawa ni wenye umri wa kati ya miaka 5 na 17. Takriban milioni tatu ya watoto hao walikuwa kwenye mazingira ya hatari, ambayo ni mojawepo ya aina [...]
27/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa Richard Falk ameonya Jumatano kwamba idadi ya watu walioathirika na bomoabomoa ya majengo ya Wapalestina imeongezeka kwa asilimia 87 ikilinganishwa na mwaka jana. Bwana Falk pia ameitaka serikali ya Israel kusitisha mara moja ubomoaji wa nyumba za Wapalestina [...]
27/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Inahitaji zaidi ya mtazamo wa jadi wa usalama kupambana na tatizo la ugaidi amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo kwenye kongamano maalumu linalozungumzia elewa na njia za kukabili ugaidi. Ban amesema dunia lazima ishirikiane kuzima moto wa chuki na kutovumiliana ambao ndio chachu ya kuzalisha ghasia za kigaidi. Ameongeza kuwa [...]
27/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na majeshi ya serikali na makundi ya upinzani Syria unaongezeka wakati mapigano yakisambaa nchi nzima limeelezwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Jumatano. Katika ripoti yake kwa baraza tume ya uchunguzi kuhusu Syria imesema jeshi la serikali na washirika wake wamehusika na mauaji ya raia , [...]
27/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu Kofi Annan ametangaza Jumatano kwamba kutakuwa na mkutano maalumu wa kundi la kuchukua hatua kuhusu masuala ya Syria mjini Geneva hapo June 30. Mwaliko umetumwa kwa mawaziri wa wajumbe watano wa kudumu wa Baraza la Usalama pamoja na nchi zingine wanachama wanaohusika. Lengo [...]
27/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »