
Wiki iliyopita, raia 214 wa Afghanistan waliuawa au kujeruhiwa katika matukio 48 tofauti. Mashambulizi ya makundi yanayoipinga serikali yalisababisha asilimia 98 ya vifo vya raia. Matukio mawili ya mashambulizi ya kujitoa mhanga yalisababisha vifo vya raia 38 wa Afghanistan, huku 38 wengine wakijeruhiwa vibaya kwenye mji wa Khost na kwenye hoteli moja kwenye Ziwa Qargha. [...]

Takriban jamaa 25 na watu 200 binafsi wanaendelea kuingia kwenye jimbo la Kikurdi la Iraq na kujiandikisha na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, na idara ya uhamiaji ya jimbo hilo kila wiki, limesema shirika la UNHCR. Kuongezeka kwa idadi ya watu wanaowasili upya ikilinganishwa na wiki iliyopita, kumeshuhudiwa katika kipindi cha [...]

Kiasi cha dola za kimarekani 770,000 na kingine 70,000 kinatazamiwa kutolewa kwa ajili ya kulipiga jeki shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR ambalo linatazamia kutoa misaada ya dharura kwa zaidi ya familia 25,000 zilizokosa makazi nchini Mali kutokana na machafuko yaliyozuka katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Kiasi hicho cha fedha [...]

Kamishna ya kitaifa juu ya mpango wa kijamii imeanza kutoa fidia ya malipo ya fedha kwa waathirika zaidi ya 10,753 walioathiriwa na machafuko mabaya yaliyoikumba Sierra Leone miongo kadhaa iliyopita. Machafuko hayo yaliyofikia ukomo mwaka 2000 yaligharimu maisha ya watu kadhaa huku wengine wakilazimika kukimbia uhamishoni kwa ajili ya kunusuru maisha yao. Malipo hayo ambayo [...]

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-Moon, amesema kwamba madawa ya kulevya na mitandao husika ya uhalifu inachangia kwa kiasi kikubwa ukiukaji wa sheria. Katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye siku ya kimataifa dhidi ya matumizi na ulanguzi wa madawa ya kulevya, Bwana Ban amesema mabilioni ya fedha zinazotokana na [...]

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema watu wengi wenye uraibu wa madawa huwa hawapati matibabu na huduma za afya wanazohitaji. Hayo ni kwa mujibu wa mfumo mpya wa WHO wa habari, ambao kwa mara ya kwanza unatoa maelezo zaidi kuhusu rasilmali zinazotengwa kwa ajili ya kuzuia na kutibu matatizo yanayotokana na uraibu wa madawa ya [...]

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa bado haijabainika ni watu wangapi walioaga dunia kutokana na ugonjwa wa homa ya nguruwe wa H1N1 kati ya mwaka 2009 na 2010. Hii hi kutokana na sababu kwamba ugonjwa wa H1N1 hauorodheshi kama unaosababisha vifo kama maradhi mengine. Hata hivyo kulingana na utafiti wa makala ya Lancet ni [...]

Kumeshuhudiwa kuongezeka kwa idadi wakimbizi wa ndani kwenye siku za hivi karibuni nchini Somalia ambao wanalalamikia ugumu wanaopitia katika kujitafutia riziki. Kwa muda wa majuma saba yaliyopita shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeandikisha wasomali 6000 ambao wamepitia magumu kama hayo hali inayosababishwa na ukosefu wa mvua na kutokuwepo usalama wa chakula. [...]

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema utesaji wa watu bado upo, miaka 25 tangu mkataba wa kimataifa wa kupinga utesaji kutiwa saini. Bwana Ban ameyasema haya katika ujumbe wake kwenye siku ya kimataifa ya kuwasaidia waathirika wa mateso. Amesema kila siku, wanaume, wanawake na hata watoto, huteswa au kudhulumiwa na lengo la [...]

Shirika la kimatiafa la uhamiaji IOM linasema kuwa karibu watu 400,000 bado wamesalia kambini nchini Haiti miaka miwili baada ya taifa hilo kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi. IOM inasema kuwa hata baada ya kupungua kwa idadi ya watu waliohama makwao inahitaji wale ambao bado hawajapata makoa kwenye kambi 575 kushughulikiwa. Mkurugenzi mkuu wa IOM [...]

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linajiandaa kutoa huduma za dharura kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa ujulikanao kama Peste des Petits ruminants ugonjwa unaoathiri mbuzi na kondoo. Ugonjwa huo unatajwa kuhatarisha usalama wa chakula nchini DRC na huenda ukasaamba kwenda mataifa ya kusini mwa Afrika [...]