Nyumbani » 21/06/2012 Entries posted on “Juni 21st, 2012”

Fursa ya watu kukusanyika kwa amani inazidi kutoweka-Kiai

Kusikiliza / Maina Kiai

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa, kuhusu haki ya kufanya mikutano ya amani, Maina Kiai, ametoa wito kwa serikali zote na jamii ya kimataifa kuchagiza na kulinda haki ya kuwa na uhuru wa kufanya mikutano ya amani na watu kushirikiana, ambayo hukiukwa au imo hatarini katika baadhi ya mataifa. Amesema, inashangaza jinsi serikali zinavyokiuka haki [...]

21/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa kike wapigia debe usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu Rio+20

Kusikiliza / michelle bach

Viongozi wa kike walioko kwenye mkutano wa Rio+20, wametia saini mchakato unaotoa mapendekezo waziwazi kuyahusisha masuala ya usawa wa kijisia na ukombozi wa wanawake katika mipango yote ya maendeleo endelevu. Katika hafla hiyo maalum, viongozi hao wametoa wito kwa serikali zote, mashirika ya umma na sekta ya kibinafsi kufuata mfano wao na kutoa kipaumbele kwa [...]

21/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa nchini Lebanon

Kusikiliza / lebanon map

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa kati ya viongozi wa kisiasa nchini Lebanon. Kupitia kwa msemaji wake Ban amewashauri viongozi wa kisiasa nchini Lebanon kuendelea na kazi yao kwenye mpango huu muhimu wanapojiandaa kwa mkutano unaopangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu. Kulingana na vyombo vya habari mkutano [...]

21/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uvumbuzi wa kibiashara unaweza kuboresha uchumi nchini Dominica:UNCTAD

Kusikiliza / unctad_logo_copy

Uungwaji mkono ulio imara kwenye shughuli za uvumbuzi kwenye sekta za kibinafsi unaweza kuboresha uchumi nchini Dominica. Hii ni kulingana uchunguzi wa sera za sayansi, Teknolojia na uvumbuzi kwenye Jamhuri ya Dominica uliochapishwa hii leo na shirika la biasahara na maendeleo la Umoja wa Mataiafa UNCTAD. Uchunguzi huo ulifanywa kwa ushirikiano na tume ya uchumi [...]

21/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Brazil, Denmark, Ufaransa na Afrika ya Kusini wanaunda ushirika endelevu wa kutoa taarifa

Kusikiliza / Ushirika endelevu

Mtazamo huo wa ushirikiano unaitwa "Marafikia wa aya ya 47" nasema kwamba kutoa taarifa endelevu iwe ni tabia miongoni mwa makampuni. Aya ya 47 ya matokeo ya nyaraka ya Rio+20 inasema kwamba "wanatambua umuhim wa ushirikiano endelevu wa kutoa taarifa na wanayachagiza makampuni kutafakari kujmisha mfumo endelevu wa ktoa taarifa kuwa kama mzungko wa kawaida. [...]

21/06/2012 | Jamii: Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadilia changamoto zinazowaandama walinzi wa amani

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadilia hali ngumu zinazowandama vikosi vya kimataifa vinavyoendesha operesheni za amani kote duniani.  Baraza hilo limetambua ugumu na vikwazo vinavyowaandama wafanyakazi hao wa kimataifa pindi wawapo kwenye maeneo ya kazi ikiwemo utekelezaji wa miongozo ya utanzuaji mizozo na ulinzi wa amani.  Umoja wa Mataifa unajumla ya wafanyakazi 120,000 [...]

21/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu ataka nchi maskini zisaidiwe kufikia shabaha ya maendeleo endelevu

Kusikiliza / Rais wa GA

  Mashirikiano ya kimaendeleo lazima yaweka kipaumbele kuzisaidia nchi maskini kutekeleza sera zinazoangazia maendeleo endelevu. Huo ndiyo ujumbe mahususi uliotolewa na rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bwana Nasir Abdulaziz Al-Nasser wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa Rio + 20, unaofanyika huko Brazil. Amesema kuwa bado nchi masikini zinapaswa kuungwa mkono kwa kupatiwa [...]

21/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Malawi inahitaji kusikia haki zao zitaheshimiwa:Kang

Kusikiliza / Bi Kyung-wha Kang

Malawi imepitia changamoto kubwa na ngumu katika miaka ya karibuni lakini mabadiliko ya amani ya serikali ni moja ya dalili njema zinazoashirika maisha bora ya baadaye. Kauli hiyo imetolewa na naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu Kyung-wha Kang wakati akikamilisha ziara yake nchini humo. Bi Kang amesema wakati taifa hilo linainuka kutoka katika matatizo [...]

21/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwigizaji Ed Norton atetea bayo-annuai kwenye mkutano wa Rio+20

Kusikiliza / Edward Norton

Mwigizaji filamu, Ed Norton yupo kwenye mkutano wa Rio+20 ili kuchagiza uzingatiaji wa aina za viumbe wanaoangamia.  Norton, ambaye ni nyota wa filamu kama 'Fight Club' na 'The Incredible Hulk,' amekuwa balozi mwema wa shirikisho la Umoja wa Mataifa kuhusu bio anuai, yaani CBD tangu mwaka 2010. Kwenye mkutano wa Rio+20, nyota huyo anatarajiwa kuisaidia [...]

21/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Timor-Leste imepiga hatua za amani na salama lakini umasikini bado upo:UM

Kusikiliza / Magdalena Sepulveda

Timor Leste imepgia hatua muhimu katika kuimarisha amani na usalama, na kushuhudia maendeleo ya kiuchumi kwa kasi, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini wa kupindukia na haki za binadamu Bi. Magdalena Sepulveda Carmona ameliambia Baraza la Haki za Binadamu, mjini Geneva. Licha ya hatua hizo, bado kuna hali ya umaskini uliokithiri na ongezeko la [...]

21/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Rio+20 wahitaji uongozi jasiri na wa kujitolea

Kusikiliza / Bi Noeleen Heyzer

Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa maeneo ya Asia na Pasifiki (ESCAP), imesema muda haupo tena wa kupoteza, na kwamba masuala muhimu ni lazima yazingatiwe na mkutano wa Rio+20, ili kupunguza hali inayochangia uharibifu wa mazingira na kuongeza mabadiliko ya hali ya hewa. Tume hiyo imeyataja masuala hayo kama [...]

21/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya itatimiza muafaka wa Rio+20:Kibaki

Kusikiliza / Rais Mwai Kibaki-Kenya

  Rais Mwai Kibaki wa Kenya amesema jumuiya ya kimataifa imekutana tena Rio Brazili ili kutoka na muafaka wa kisiasa kwa ajili ya maendeleo endelevu na kutokomeza umasikini. Na amweuhakikishia ulimwengu kupitia hoptuba yake kwamba taifa la Kenya litakuwa kinara katika kuhakikisha dunia inakuwa na mstakhbali mzri wenye manufaa kwa wote. Amesema ingawa hatua zimepigwa za [...]

21/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia, Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Kushambulia waandishi ni kushambulia demokrasia

Kusikiliza / Waandishi wa habari

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa wamelaani idadi kubwa ya maaji ya waandishi wa habari au hali ya kutowatendea utu kutokana na uwajibikaji wao. Frank La Rue mtaalamu wa uhuru wa maoni na kujieleza na Christof Heyns mtalamu kuhusu mauaji ya kunyongwa au y kiholea wamezitaka serikali kote dniani kuchukua hatua kuwalinda [...]

21/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aweka malengo matatu kutimizwa ifikapo 2030

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema viongozi wa duunia wamekusanyika Rio ili kuunda mfumo mpya wa kimataifa. Ban ameyasema hayo Alhamisi wakati wa utiaji saini makubaliano ya kuanzishwa taasisi ya kimataiga ya kuaji unaojali mazingira. Amesema ameweka malengo makubwa matatu kwa ajili ya kutimizwa ifikapo 2030. Malengo hayo ni moja fursa ya [...]

21/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya hali ya hewa yanawalimu watu kwenye hatarini:UNHCR

Kusikiliza / Antonio Guterres Rio+20

Ripoti mpya inayotokana na ushahidi wa wakimbizi bifasi kutoka Afrika ya Mashariki inaonyesha kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuwadhoofisha watu zaidi na pia kuchangia kuwalazimu kuhamia maeneo ya migogoro, na hatimaye kuvuka mipaka na kukimbilia nchi nyingine. Ripoti hiyo imewasilishwa kwenye mkutanowa Rio+20 na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja [...]

21/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Juni 2013
T N T K J M P
« mei    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930