Nyumbani » 19/06/2012
Entries posted on “Juni 19th, 2012”
Kusikiliza /

Wawakilishi wa serikali na wadau kutoka kote ulimwenguni wamefikia muafaka kuhusu mswada wa mkataba wa maendeleo endelevu wa Rio+20, ambao unatarajiwa kusainiwa mwishoni mwa mkutano wa viongozi mjini Rio de Janeiro, Brazil, ambao, ambao unaanza rasmi hapo kesho. Katika mswada huo, viongozi wa kimataifa wanaazimia kuunga mkono maendeleo endelevu na kuhakikisha kuwa maendeleo yote ya [...]
19/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa, yametoa wito kwa mataifa wanachama wa G20 kwenye mkutano Mexico kuongeza juhudi zao katika kukabiliana na njaa. Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yenye makao mjini Rome, ni FAO, IFAD na WFP. Yote, kwa taarifa ya pamoja mnamo siku ya Jumanne, yamekaribisha G20 kwa kuendelea kutambua mchango wa [...]
19/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Bado hali kwenye jimbo la Rakhine nchini Myanmar inabaki kuwa tete kutokana na ghasia ambazo zimeshuhudiwa siku 10 zilizopita. Kulingana na makadirio ya serikali karibu watu 48,000 wamelazimika kuhama makwao kufuatia ghasia zilizoanza kushuhudiwa juma lililopita. Kufuatia ombi la msaada lililotolewa na serikali ya Myanmar kwa Umoja wa Mataifa, shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja [...]
19/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limewasilisha mpango mkakati wenye shabaha ya kuinua hali ya kilimo katika nchi zinazoinukia kiuchumi kwa kusisitiza haja ya kuwepo mashirikiano baina ya serikali, wafanyabiashara na wakulima wadogo wadogo. Mpango huo ambao unatupia macho zaidi kilimo endelelevu unapendelea kuona kuwa sehemu hizo zinajenga daraja la pamoja na hatimaye [...]
19/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekaribisha hatua ya Muungano ya Ulaya ya kuzindua mpango kati ya mwaka 2012na 2016 wa kumaliza tatizo la usafishaji haramu wa watu. Mpango huo wa miaka mitano unalenga kutambua waathiriwa wa vitendo vya usafirishaji haramu wa watu , kuwafikisha mbele ya sheria wahusika, kuongeza ushirikiano na mashirika mengine katika [...]
19/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi wa Shirika la bishara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD Supachai Panitchpakdi ametangaza mpango mpya wa masoko ya hisa wa kuwa na uwekezaji wa muda mrefu kwa masoko yao. Makubaliano hayo ni kati ya soko la hisa la Marekani NASDAQ na na masoko ya hisa kwenye mataifa ya Brazil, Misri, Istanbul na Afrika [...]
19/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema mkutano wa kimataifa wa Rio+20 unatoa fursa muhimu kwa ulimwengu kutambua na kufahamu uhusiano uliopo kati ya afya ya mwanadamu na maendeleo endelevu. WHO limesema takriban watu milioni 150 hupitia taabu kubwa kifedha kila mwaka kwa sababu huwa wanaumwa na kutafuta huduma za afya ambazo wanahitajika kulipia papo hapo. [...]
19/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wengine wa kutoa huduma za kibinadamu hii leo wametoa wito mpya wa misaada ya kuwasaiadia watu wa Sahel magharibi mwa Afrika. Wito huo wa pamoja ambao ni wa dola bilioni 1.6 utagharamia huduma za chakula , afya , usafi na usaidizi mwingine ambao utatolewa kwa watu milioni 18.7. Wito [...]
19/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeanzisha shughuli mpya ya dharura ya kusafirisha misaada kwa njia ya ndege kwenda kwa wakimbizi walio kwenye jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini. Shughuli hiyo inalenga kuwapelekea misaada wakimbizi 50,000 ambao wamekimbia mizozo na uhaba wa chakula kwenye jimbo la Blue Nile nchini Sudan. Ndege [...]
19/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wanachama wa Baraza la Usalama la UM wamekaribisha kurejelea kwa mazungunmzo kati ya Sudan na Sudan Kusini chini ya tume maalum ya Muungano wa Afrika. Katika taarifa ilotolewa baada ya mkutano wake wa Jumatatu, wanachama wa Baraza la Usalama wamesema kuwa ghasia zimepunguzwa kwenye maeneo ya mpakani, na kupongeza pande zote mbili kwa hatua zilizopigwa [...]
19/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamewalazimu maelfu ya watu kuhama makwao, amesema leo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadam katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, katika ripoti yake mpya. Bi Pillay ameelezea hofu yake kuwa uhalifu zaidi dhidi ya raia huenda ukatendeka katika eneo hilo na wasiwasi wake kuhusu usalama wa wakazi [...]
19/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »