Nyumbani » 18/06/2012
Entries posted on “Juni 18th, 2012”
Kusikiliza /

Kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa UN women kupitia mkurugenzi wake mkuu Michele Bachelet kimesisitiza kwamba sauti za wanawake lazima zisikilizwe. Akizungmza kwenye mkutano wa Rio+20 Bi Bachelet amesema dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kimazingiza na ili kukabiliana nazo ni lazima wanawake washirikishwe na sati zao zipewe [...]
18/06/2012 | Jamii: Makala za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huku nusu ya watu wote duniani wakiwa chini ya umri wa maiaka 25 na hali mbaya ya uchumi ikiendelea, kuwepo kwa ajira za kisasa ili kupunguza athari za shughuli za uchumi kwa mazingira ni kati ya masuala yatakayopewa kipaumbele na vijana ambao watahudhuria mkutano kuhusu maendeleo endelevu wa Rio+20. Kwenye mkutano uliondaliwa na shirika la [...]
18/06/2012 | Jamii: Rio+20, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali matukio ya mashambulizi yaliyofanywa na kundi la askari walioasihuko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kusababisha mauwaji ya watu kadhaa. Askari hao wameripotiwa kufanya mashambulizina kuwauwa raia kadhaa wakiwemo wanawake na watoto na kushiriki vitendovya kuwanyanyasa wananchi. Katika eneo hilo la kusini na kaskazinimwa jimbo la [...]
18/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu Umoja wa MataifaBan Ki-moon ametoa mwito akitaka kuweko kwa mikakati madhubuti ili kuhifadhi udongo ambao ndiyo tegemeo kuu la maisha ya binadamu. Ban amesisitiza kuwa kunapaswasasa kuchukuliwa hatua za haraka kurejesha kwenye ubora wake udongo huoambao kwa kiwango kikubwa umekubwa na uharibifu. Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye kuadhimisha siku ya kimataifa ya [...]
18/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Waangalizi wa kimataifa kwa ajili ya mzozo wa Syria wamesitisha shughuli zake nchini humo kutokanana idadi ya mashambulizi ya silaha kuwa ya kiwango cha juu. Taarifa iliyomkariri Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Generali Robert Mood imesemakuwa kuwamekuwa na ongezeko la mashambulizi karibu katika eneo nzima laSyria na hivyo kuzuai kwa kiwango [...]
18/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea husuni yake kutokana na kifo cha mwana wa kifalme Nayef bin Abdulaziz al-Saud ambaye pia alikuwa ni waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani nchini Saudi Arabia. Kwenye taarifa kupitia kwa msemaji wake Ban amasema kuwa Prince Nayef alijitolea kuhakikisha kuwepo usalama nchini Saudi Arabia [...]
18/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lybia amelezea wasi wasi uliopoa kutokana na kushuhudiwa mapigano mapya kwenye sehemu kadha ambapo watu wameuawa , kujeruhiwa na kulazimika kuhama makwao na kutaka tawala husika kuwalinda raia. Ian Martin ambaye pia ni mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL amesema kuwa ni jambo muhimu iwapo [...]
18/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mazungumzo ya mwiso kuhusu hati ya kisiasa ya mkutano wa Rio+20 yataongozwa naBra zil ambaye sasa amechukua rasmi urais wa mkutano kuhusu maendeleo endelevu. Waakilishi wa serikali walimaliza awamu ya tatu na ya mwisho ya maandalizi yake kabla ya kuandaliwa kwa mkutano huo wakiwa wamekubaliana asilimia 40 ya hati hiyo. Waziri wa mambo ya nje [...]
18/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha shughuli ya kuwahamisha wakimbizi kutoka kituo cha Al Damazin kilicho kwenye eneo la magharibi kati ya mpaka wa Ethiopia na Sudan kwenda kambi mpya iliyo eneo la Benishangul Gumuz kaskazini magharibi mwa Ethiopia. Uamuzi wa kuhamisha wakimbizi hao ulifanywa baada ya kituo hicho ambacho kina uwezo wa kuwahifadhi [...]
18/06/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Naibu Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Kyung-wha Kang, ameanza ziara ya siku nne nchini Malawi ili kujadili masuala kadha wa kadha ya haki za binadamu na rais Joyce Banda na wadau wengine nchini humo. Hii ndiyo ziara ya kwanza ya aina yake nhcini humo, ya afisa mkuu wa haki za [...]
18/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women Bi Michele Bachelet, akizungumza na waandishi wa habari mjini Rio De Jenairo Brazili, ameelezea mustakhbali wanaotaka wanawake. Katika mkutano huo wa Rio+20, amesema wakati wanawake wakifurahia haki sawa, fursa sawa na ushirikishwaji, wanaweza kuchangia pakubwa katika maendeleo endelevu. Ameongeza kuwa [...]
18/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Takriban wafungwa 10,000 wa kisiasa wapo katika jela nchini Eritrea, kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay. Katika hotuba yake kwa Baraza la Haki za Binadamu, Bi Pillay amesema kuwa hatma ya wafungwa hawa haijulikani, kwani Eritrea imekataa kushirikiana na afisi yake na mifumo mingine ya haki za binadamu ya kimataifa [...]
18/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Misitu kote duniani ina nafasi muhimu katika hatua za kuweka uchumi mpya wenye kujali mazingira, kwa mujibu wa ripoti mpya ya FAO. Uchumi wenye kulinda mazingira ni mojawepo ya maudhui muhimu katika mazungumzo ya mkutano wa Rio+20 kuhusu maendeleo endelevu. Lakini ili kufanya hili litimie, FAO inasema ni lazima serikali ziweke mikakati na sera ambazo [...]
18/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wakati huo huo raia wanaendelea kukwama kutokana na machafuko yaliyoshika kasi Syria amesema mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa uangalizi Syria UNSMIS Jenerali Robert Mood. Katika taarifa yake iliyotolewa Jumapili jioni Mood amesema katika mji wa Homs juhudi za kuwaondoa raia wanaozingirwa na mapigano zimeshindwa kuzaa matunda. Amezitaka pande zote husika katika vita [...]
18/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuungana ili kushirikiana kukomesha ghasia, na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Syria. Bi Pillay ameelezea kusikitishwa kwake na kushindwa kwa waangalizi wa Umoja wa Mataifa, UNSMIS kutekeleza majukumu yao kwa sababu ya kuonegezeka kwa ghasia nchini [...]
18/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti mpya ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, inasema mwaka wa 2011 uliweka rekodi kwa kushuhudia idadi ya wakimbizi 800,000, ambayo ndio idadi kubwa zaidi ya watu kuwahi kuvuka mipaka kama wakimbizi,tangu mwaka 2000. Ripoti hiyo ambayo imetolewa leo iitwayo 2011 Global Trends, inaonyesha kwa mara ya kwanza kiwango cha ukimbizi uliotokana na mizozo ya [...]
18/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »