Nyumbani » 15/06/2012 Entries posted on “Juni 15th, 2012”

Maandalizi ya Rio+20 yanaingia manthari ya muda wa dharura

Kusikiliza / rio-+-20-large

Hali ya dharura imejitokeza katika manthari ya siku ya mwisho ya mazungumzo kuhusu mswada wa kisiasa wa mkutano wa Rio+20 kuhusu maendeleo endelevu. Kauli hii imetoka kwa Nikhil Seth, ambaye ni msimamizi wa makao makuu ya mkutano huo, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Rio de Janeiro, Brazil Ijumaa.Wawakilishi wa serikali wamekuwa wakikutana mjini [...]

15/06/2012 | Jamii: Rio+20 | Kusoma Zaidi »

UM wajadili visiwa vya Falklands(MALVINAS)

Kusikiliza / Cristina Fernandez

Kamati maalum kuhusu kuondoa ukoloni imesema kuwa kuondoa hasa hali maalum ya ukoloni inayohusiana na visiwa Falklands au Malvinas, kunahitaji muafaka kwa njia ya amani baina ya Argentina na Uingereza kuhusu uhuru wa visiwa hivyo. Kwa azimio la pamoja lililopendekezwa na Waziri msaidizi wa Mambo ya nje wa Chile, kamati hiyo maalum imesikitika kuwa, licha [...]

15/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ILO yapendekeza ruzuku wastani kwa wote

Kusikiliza / ILO LOGO

Shirika la Wafanyakazi Duniani, ILO, limependekeza kuwekwe ruzuku wastani ya kijamii kwa watu wote, ili kuwasaidia zaidi ya watu bilioni 5 wasiojiweza kukidhi mahitaji muhimu kama ya afya na mengineyo. Hii ni kwa kufuatia maazimio mapya yaliyokubaliwa mwishoni mwa kongamano la kimataifa la wafanyakazi. Shirika la ILO limesema kuwekwa kwa kiwango cha wastani cha ruzuku [...]

15/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa fedha wahatarisha operesheni Mali:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Mali

Ukosefu wa fedha unatajwa kutishia jitihada za shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR za kusaidia zaidi ya watu 300,000 nchini Mali waliolazimika kuhama makwao kutokana na mapigano na ukosefu wa usalama kaskazini mwa nchi. UNHCR inasema kuwa hadi sasa imepokea asilimia 13 tu na dola milioni 153.7 zinazohitajika kuwasaidia raia waliohama makwao [...]

15/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuna mpango kuzuia dhulma kwa wagonjwa wa akili:WHO

Kusikiliza / matatizo ya akili

Shirika la afya duniani WHO limezindua mpango wenye lengo la kuhakikisha kuwa viwango vya juu vya haki za binadamu vinatumiwa kwenye vituo vinavyoshughulikia walio matatizo ya akili na kijamii kote duniani. WHO inasema kuwa kati yaa ukiukaji wa haki za binadamu kwenye vituo kama hivyo ni pamoja na misongamano na mazingira machafu, ghasia , dhuluma [...]

15/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Utumaji pesa kwa simu unaweza kuboreshwa:UNCTAD

Kusikiliza / Kupokea pesa kupitia simu za mkononi

Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD linasema kuwa kutumika kwa simu ya mkononi katika kutuma pesa na masuala mengine kama kukopa na kuhifadhi pesa ni shughuli ambayo imekuwa maarufu mwenye mataifa ya Afrika Mashariki lakini inaweza kuboreshwa zaidi kupitia usimamizi mwema na ushirikiano. Kulingana na ripoti ya UNCTAD Zaidi ya dola [...]

15/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaanza kuwasafirisha wakimbizi wa Sudan toka Al Damazin

Kusikiliza / wakimbizi wa Sudan Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha shughuli ya kuwahamisha wakimbizi kutoka kituo cha Al Damazin kilicho kwenye eneo la magharibi kati ya mpaka wa Ethiopia na Sudan kwenda kambi mpya iliyo eneo la Benishangul Gumuz kaskazini magharibi mwa Ethiopia. Uamuzi wa kuhamisha wakimbizi hao ulifanywa baada ya kituo hicho ambacho kina uwezo wa kuwahifadhi [...]

15/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dhuluma dhidi ya wazee ni kukiuka haki za binadamu:Ban

Kusikiliza / wazee

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa dhuluma dhidi ya wazee ni ukiukwaji wa utu na haki za binadamu. Takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 4 na sita ya wazee kote duniani wamekumbana na dhuluma ya aina moja au nyingine, kimwili, kihisia au kifedha. Uchunguzi pia [...]

15/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bangladesh yazuia wakimbizi kutoka Myanmar:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi toka Myanmar

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa mamia ya watu wanaokimbia ghasia magharibi mwa Myanmar kwa sasa wamekwama kwenye mashua pwani mwa Bangladesh. Mashua hizo ambazo zinaripotiwa kuwabeba akina mama , watoto na watu waliojeruhiwa wanaokimbia ghasia za kikabila kwenye jimbo la Rakhine zilizuiwa kuingia nchini Bangladesh. UNHCR inaiomba serikali ya [...]

15/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ghasia Syria zinazuia kazi za UNSMIS:Mood

Kusikiliza / Jeneral Mood na Ban Ki-moon

Mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Jenerali Robert Mood, amesema kuwa kuongezeka kwa ghasia kunazuia kazi ya waangalizi hao. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa ndiyo sehemu pekee ya mpango wa amani wa kimataifa wenye lengo la kurejesha utulivu katika taifa hilo ambako mzozo unaendelea [...]

15/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Washauri wa Ban wahofia mauaji yanayoendelea Syria

Kusikiliza / Machafuko Syria

Washauri wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon wanaohusika na kuzuia mauaji ya halaiki na jukumu la kulinda mabwana Francis Deng na Edward Luck wameelezea wasi wasi uliopo kutokana na ripoti za kuuawa kwa watu wengi kwenye uvamizi nchini Syria. Kwenye taarifa yao washauri hao wamesema kuwa uvamizi huo ulihusisha mashambulizi yaliyoendeshwa [...]

15/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ajira ya watoto sio tuu ukikaji wa haki zao bali sheria za kimataifa

Kusikiliza / Ajira kwa watoto

Wiki hii dunia imeadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto. Tathimini ya Umoja wa Mataifa imebaini kwamba ajira za shurutio na dhuluma za kimapenzi ni mambo ya kuyatilia maanani saana na ni tatizo linaloelekea kwa sugu. Zaidi ya watoto milioni 215 wanafanya kazi kote duniani huku zaidi ya nusu yao wakipitia hali ngumu [...]

15/06/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031