Nyumbani » 14/06/2012
Entries posted on “Juni 14th, 2012”
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula, FAO, José Graziano da Silva, amefanya mazungumzo na Papa Benedict XVI leo katika mkutano wa faragha, Vatican. Wakati wa mkutano huo, Bwana da Silva amemwambia Papa Benedict kuwa, kutokomeza njaa ni muhimu, siyo tu kisiasa, kiuchumi na kijamii, bali pia ni wajibu wa kimaadili. Ametoa wito kwa [...]
14/06/2012 | Jamii: Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mashirika hamsini ya kimaifa ya kutoa misaada pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa kauli moja ya kuondelewa kwa vikwazo Gaza. Mashirika hayo yamechapisha taarifa fupi katika kuadhimisha kukumbukumu ya miaka mitano ya kuongeza nguvu vikwazo hivi. Taarifa hiyo inasema; Kwa zaidi ya miaka mitano Gaza, zaidi ya watu milioni 1.6 wameishi chini [...]
14/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ametoa mwito akitaka serikali ya taifa hilo kusaka njia mjarabu itayobainisha chanzo cha kujiri matukio ya mashambulizi ya mara kwa mara. Pamoja na kuelezea masikitiko yake kutokana na mashmbulizi hayo, Martin Kobler amesema serikali inapaswa kujua chanzo cha kujirudia rudia kwa hali hiyo ambayo amesema kuwa inazorotesha [...]
14/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Tathmini ya haraka iliyofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali katika eneo la Afrika ya Kati imebaini kuwepo kitisho kikubwa cha ukosefu wa chakula. Mashirika hayo yamebainisha kuwa kiasi cha watu 45,000 wanaoishi katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo wapo kwenye hali ngumu wakikabiliwa na ukosefu wa chakula. Wa mebainisha kuwa hali ni mbaya [...]
14/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mshauri wa katibu mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wa michezo kwenye mandeleo na amani Wilfried Lemke yuko mjini Berlin Ujerumani ambapo amehutubia kikundi cha kamati ya michezo cha bunge la Ujerumani kuhusu sera za kimataifa za michezo ambapo aliangazia shughuli zake kwa muda wa mwaka mmoja uliopita. Mwishoni mwa juma bwana [...]
14/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kupunguza majanga Margaret Wahlstrom hii leo amewataka wanachama wa Umoja wa Mataifa kuangazia athari ambazo zimesababishwa na majanga ya kiasili tangu kufanyika mkutano wa dunia mjini Rio de Janeiro miaka ishirini iliyopita. Wahlstrom amesema kuwa mkutano wa mwezi huu kuhusu maendeleo endelevu utaangazia hasara ambayo imeshuhudiwa [...]
14/06/2012 | Jamii: Rio+20, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema msukosuko wa kisiasa mjini Bamako na ktokuwepo salama Kaskazini mwa Mali kunaendelea kuzusha wimbi la wakimbizi wanaoingia Burkina Faso, Niger na Mauritania. Shirika hilo linasema tangu katikati ya mwezi wa Mai wakimbizi wa Mali 20,000 wamewasili katika nchi hizo jirani na mipaka katika nchi zote [...]
14/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkutano wa Kimataifa wa kuchagiza juhudi zaidi kuzuia vifo vya watoto ambavyo vinaweza kuzuiliwa, umeanza leo mjini Washington, Marekani. Mkutano huo wa hali ya juu uitwao Child Survival Call to Action, umeitishwa na serikali za Ethiopia, India na Marekani, zikishirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF. Mkutano huo unawajumuisha wawakilishi kutoka [...]
14/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Muungano wa wa teknolojia ya mawasiliano ITU umesema katika mktano wa Rio+20 unasisitiza kwamba teknolojia ya habari na mwasiliano ICT ni kiungo muhimu katika kupiga hatua na kutokomeza umasikini, hivyo ni lazima itamblike kama muundombinu muhimu unaoweza kuunganisha masuala ya kijamii na kuleta maendeleo endelevu. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ITU Hamadoun Toure teknolojia [...]
14/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kilimo kinachotegemea zaidi nishati za kisukuku kinapunguza uwezo wa sekta hiyo kuzalisha chakula cha kutosha, na hivyo kuongeza umaskini na kudhoofisha juhudi za kuweka uchumi endelevu kote ulimwenguni, limesema shirika la kilimo na chakula, FAO. Onyo hili limetolewa katika ripoti ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa kufuatia utafiti kuhusu uzalishaji chakula wenye kutumia nishati [...]
14/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Waziri wa mambo ya nje wa Brazil Antonio Patriota amesema nchi yake inajitahidi kwa kila hali kuhakikisha kwamba wanafikia muafaka mapema kuhsu matokeo ya mkutano wa Rio+20. Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa amesema nchi yake imekuwa ikijihusisha zaidi na juhdi za kondoa tofati zilizopo na kshughulikia vipengee na mada ambazo bado zinahitaji kufanyiwa [...]
14/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kiongozo anayeunga mkono masuala ya demokrasia nchini Myanmar Aung San Suu Kyin amesema kuendeleza mchakato wa mabadiliko nchini humo ni jukumu la pamoja la watu wa Myanmar, serikali, viongozi wa siasa na jeshi. Akizungumza mjini Geneva Bi Suu Kyi amesema hata chuki yoyote dhidi ya utawala wa kijeshi yaani Junta uliomuweka katika kifungo cha nyumbani [...]
14/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Majadiliano ya matokeo ya mwisho ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu au Rio+20 yako yako katika hata za mwisho. Majadiliano hayo yanaanza rasmi Juni 20 hadi 22 mjini Rio Dejaneiro Brazili ambako wakuu wan chi na serikali mbalimbali wanatarajiwa kutia saini nyaraka muhimu kwenye mkutano huo. Mkutano huo pia unahudhuriwa na makundi [...]
14/06/2012 | Jamii: Mahojiano, Rio+20 | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa wito kwa watu wengi zaidi kujitokeza na kutoa damu mara kwa mara, ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya damu kote ulimwenguni. Katika ujumbe wake kwenye siku ya utoaji damu duniani, WHO inasema kuwa mamilioni ya watu hutegemea ukarimu wa watu wanaotoa damu kila mwaka, lakini viwango vya utoaji [...]
14/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »