Nyumbani » 11/06/2012
Entries posted on “Juni 11th, 2012”
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, hii leo amewasilisha ripoti yake ya kila mwaka kuhusu watoto kwenye maeneo ya migogoro ya silaha kwa Baraza la Usalama, ambayo inatoa picha ya hali ya watoto katika maeneo ya vita na hatua zilizochukuliwa kuwalinda. Akiwasilisha ripoti hiyo, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwa watoto katika maeneo [...]
11/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa kila taifa kote ulimwenguni kutimiza wajibu wake katika kuhakikisha kuwa watoto hawaambukizwi virusi vya UKIMWI na wanawake wazazi hawafariki kutokana na UKIMWI. Amesema wanawake na watoto wanafaa kuzingatiwa kwa njia maalum katika vita hivi. Ameyasihi mataifa kuongeza kasi na juhudi, kwa kuunga mkono mpango [...]
11/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA limesema kuwa hakuna hatua zozote zilizopigwa wakati wa mkutano na maafisa kutoka Iran mwishoni mwa juma jinsi ya kutatua mzozo kuhusu mpango wa nyuklia nchini Iran. Maafisa wa ngazi za juu kutoka IAEA walikutana na ujumbe kutoka Iran mjini Vienna yaliyo makao makuu ya [...]
11/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza Kuu la Umoja wa Mataiafa limemteua waziri wa mambo ya kigeni wa Serbia Vuk Jeremic kuwa raia wa kikao kinachokuja cha 67 cha bazara kuu la Umoja huo. Kwenye shughuli ya kupiga kura ya kuchagua rais mapema leo bwana Jeremic alipata kura 99 ambapo mpinzani wake balozi Dalius Cekuolis kutoka Lithuania alipata kura 85. [...]
11/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, Ertharin Cousin, ameanza leo ziara ya siku tano kwenye mataifa ya Dominican Republic, Haiti na Nicaragua ili kuimarisha ushirikiano wa shirika hilo la WFP na serikali za eneo hilo katika kuimarisha usalama wa chakula na lishe. Atakutana na rais mpya wa Dominican Republic, Danilo Medina, na kuzuru [...]
11/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Singapore imetia saini mkataba wa Shirika la Kazi Duniani ILO wa kuchagiza afya na usalama wa wafanyakazi kazini. Tangazo hilo limetolewa Jumatatu na waziri wa kazi na maendeleo ya nchi hiyo Tan Chuan-Jin wakati wa mkutano wa ILO unaoendelea mjini Geneva. Amesema Singapore imekuwa ikijitahidi kuimarisha usalama wa wafanyakazi wake tangu kulipofanyika mabadiliko ya sheria [...]
11/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, ameelezea kuhuzunishwa kwa shirika hilo na kifo cha Profesa George Saitoti, ambaye alikuwa waziri wa usalama nchini Kenya. Bwana Saitoti alifariki dunia mwishoni mwa wiki kwenye ajali ya ndege, pamoja na waziri msaidiz katika wizara ya usalama wa ndani, Joshua Orwa Ojode na watu [...]
11/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti kutoka nchini Myanmar zinasema kwamba Umoja wa Mataifa unaondoa wafanyakazi wake wasio wa lazima kutoka Maghjaribi mwa nchi hiyo ambako kumekwa na ghasia za kidini zilizosababisha vifo na serikali imetangaza amri ya kutotoka nje. Kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini humo wafanyakazi 44 na familia zao wanaondoka hasa kwa ajili ya [...]
11/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC imesema inahofia usalama wa wafanyakazi wake ambao haijawasiliana nao tangu walipokamatwa Libya Alhamisi iliyopita. Maafisa wanne wa mahakama hiyo wanashikiliwa kwa karibu juma zima sasa na tayari Rais wa mahakama hiyo Sang-Hyung Song ametoa wito akitaka waachiliwe mara moja. Maafisa hao pamoja na kuwa na kinga waliwekwa kizuizini walipo [...]
11/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Bado kuna pengo kubwa kati ya uridhiaji mkataba wa kupinga ajira kwa watoto na hatua za utekelezaji zinazochukliwa na nchi kukabiliana na tatizo hilo imesema ripoti ya shirika la kazi duniani ILO iliyotolewa kuadhimisha mwaka wa 10 wa sik ya kimataifa ya kupinga ajira ya watoto. Kwa mjib wa mkurugenzi mkuu wa ILO Juan Somavia [...]
11/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu, Kofi Annan, ameelezea kusikitishwa kwake na ripoti za hivi karibuni za ghasia na kuongezeka kwa mapigano baina ya serikali na upinzani nchini Syria. Amesema anahofia zaidi hasa urushaji wa mabomu kwenye mji wa Homs, pamoja na matumizi ya mizinga, ndege za helkopta katika [...]
11/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Maafisa wanne wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kiivita ICC wanashikiliwa nchini Libya katika kipindi cha wiki moja sasa na tayari rais wa mahakama hiyo Jaji Sang-Hyun Song, ametoa mwito akitaka waachie huru mara moja. Maafisa hao waliwekwa kizuizini kuanzia June 7 mwaka huu wakati walipokuwa kwenye ziara ya ujumbe maalumu nchini humo. Pamoja [...]
11/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »