Nyumbani » 07/06/2012 Entries posted on “Juni 7th, 2012”

Ban na Annan wasema umewadia wakati wa kuchukua hatua Syria

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon na Kofi Annan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amewaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa Syria imo hatarini ya kuingia vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe, na athari yake itakuwa ni janga kubwa kwa Syria na kanda nzima. Amesema, hakuna maana tena kuendelea kulaani kwa maneno tu kile kinachotendeka Syria [...]

07/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamhuri ya Afrika ya kati ina fursa nzuri ya kupata utulivu:Vogt

Kusikiliza / Margaret Vogt

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati Margaret Vogt amesema inahitaji kuboreshwa kwa hatua zilizopigwa nchini humo zikiwemo kwenye masuala ya kisiasa , usalama na kukusanya silaha. Akilihutubia kundi la nchi 15 la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati, Vogt amesema [...]

07/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Haki na usalama ni muhimu kwenye vita:UNDP

Kusikiliza / Nembo ya UNDP

Ripoti moja iliyotolewa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP,imeeleza kuwa kuwepo kwa hali ya usalama na utawala wa kisheria ni maeneo muhimu yanayoweza kutoa mustakabala mwema wa kurejesha hali ya utengamao kwenye maeneo yaliyokumbw a na mizozo. Ripoti hiyo iliyochapishwa kwa mara ya kwanza New York inasema kuwa suala la usalama na [...]

07/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ujenzi wa makazi ya Walowezi ni kinyume na sheria:Serry

Kusikiliza / Robert Serry

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mpango wa amani wa Mashariki ya Kati, Robert Serry, ameongeza sauti yake kwa mtazamo wa jamii ya kimataifa kwamba, majengo yote katika maeneo ya makazi, yawe kwenye ardhi binafsi ya Palestina, au kwingineko kwenye maeneo yalokaliwa kwenye ardhi ya Palestina, ni kinyume na sheria za kimataifa. [...]

07/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei ya chakula imeshuka kote duniani:FAO

Kusikiliza / Bei ya chakula imeshuka

Bei ya chankula kote duniani imeshuka ghafla mwezi Mei kwa sababu ya kuongezeka uzalishaji, uchumi kuendelea kuyumbayumba na kupanda kwa dhamana ya dola ya Kimarekani, limesema leo shirika la Mazao na Chakula, FAO. Kipimo cha bei ya chakula cha FAO, kinachotizama mabadiliko katika bei ya kapu la bidhaa za chakula ulimwenguni, kilishuka kwa asilimia nne [...]

07/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pakistan yakabiliwa na changamoto kubwa:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameelezea kusikitishwa kwake na hali ya haki wanawake nchini Pakistan, pamoja na hofu kuhusu mifumo ya sheria nchini humo, ambayo inaonyesha kuhitilafiana. Bi Pillay amesema haya wakati akihitimisha ziara yake ya siku nne nchini humo, ambako amefanya mikutano na Waziri Mkuu, Yousou Raza [...]

07/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vyandarua vya bei nafu vitapunguza gharama:UNICEF

Kusikiliza / Chandarua cha mbu

Kupunguza bei ya vyandarua vya kuzuia mbu wanaosababisha malaria kunaweza kulisadia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kuokoa hadi dola milioni 22 za matumizi yake katika kipindi cha mwaka mmoja ujao, amesema leo mkuu wa shirika hilo.  Wakati wa mkutano wa halmashauri ya UNICEF wa kila mwaka mjini New York, Mkurugenzi huyo [...]

07/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Matatizo ya madeni barani Ulaya ni tishio kubwa kwa uchumi wa dunia:DESA

Kusikiliza / Mtazamo wa ukuaji uchumi

Madeni barani Ulaya yanasalia kuwa tishio kubwa kwa uchumi wa dunia, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Alhamisi na Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo: Mwelekeo na mtazamo wa Umoja wa Mataifa wa hali ya uchumi na matarajio ya katikati ya mwaka 2012 (yaani WESP 2012) inasema kuendelea kwa matatizo hayo kutasababisha hali mbaya [...]

07/06/2012 | Jamii: Habari za wiki, Rio+20 | Kusoma Zaidi »

Licha ya changamoto UNSMIS itaendelea na wajibu wake Syria:Mood

Kusikiliza / Neja Jenerali Robert Mood nchini Syria

Msimamizi Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria (UNMIS), Jenerali Robert Mood, amesema kuwa UNMIS imepeleka waangalizi wa Umoja wa Mataifa Mazraat al-Qubeir, ili kuthibitisha habari za mauaji ya halaiki katika kijiji hicho. Hata hivyo, waangalizi hao bado hawajafika kwenye kijiji hicho, kwani ujumbe wao unakumbana na vizuizi vitatu. Cha kwanza, anasema Jenerali [...]

07/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aitaka jumuiya ya kimataifa kushikamana na kuchukua hatua pamoja dhidi ya Syria

Kusikiliza / Kikao cha Syria baraza kuu

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka jumuiya ya kimataifa kushikamana na kuchuka hatua za pamoja katika saa na kipindi hii kigumu kwa Syria. Ban amesema hali ya Syria inaendelea kuzorota na kila siku mambo mapya yanazuka yanayoongeza zahma katika mauaji na uhalifu. Akizungumza katika kikao maalumu cha Baraza Kuu Ban amesema [...]

07/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031