Nyumbani » 01/06/2012
Entries posted on “Juni 1st, 2012”
Kusikiliza /

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mauaji ya watu zaidi ya 100 katika kijiji cha Houla, katikati mwa Syria na kuagiza uchunguzi huru ufanyike. Baraza hilo lililokutana mjini Geneva Ijumaa limepitisha azimio kwa njia ya kura huku wajumbe 41 wakiunga mkono, na watatu wakiwemo Urusi, Uchina na Cuba wakipinga, na [...]
01/06/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Serikali ya Burundi kwa ushirikiano na shirika la Afya Duniani WHO wameanzisha kampeni kabambe dhidi ya ugonjwa wa polio. Hii ni baada ya Burundi kujikuta katika kitisho kikubwa cha kuvamiwa na maradhi hayo baada ya nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuonyesha dalili za Polio katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi [...]
01/06/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (IFRC), limesema kuwa tetemeko la ardhi la siku ya Jumanne kaskazini mwa Italy, limewaua watu 17 na kuwajeruhi wengine 350. Wengi wa waathirika wa tetemeko hilo walikuwa wafanyakazi katika viwanda na vyumba vya kuhifadhi shehena, kama vile ilivyokuwa kwenye tetemeko la siku tisa zilizopita. Shughuli za kutafuta manusura na [...]
01/06/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, limezindua kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu siku ya kimataifa ya kulinda watoto, dhidi ya usafirishaji haramu wa watoto na kuwatumia katika kuombaomba. Kampeni hiyo inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani, USAID, itawalenga mashabiki wa kandanda wanaozuru miji ya Ukraine ya Donetsk, Kharkiv, Kyiv na [...]
01/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mamia ya watoto wanaosoma katika shule za msingi katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara wanatajwa kuandamwa na matatizo chungu mbovu ikiwemo kuwepo kwa mlundikana mkubwa wa wanafunzi katika darasa moja jambo linalowafanya washindwe kupata elimu bora. Hali ya wasiwasi nyingine inayowaandama watoto hao ni pamoja na kukosekana kwa walimu wa kutosha wenye mafunzo [...]
01/06/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa takriban wakimbizi 20,000 kwa sasa wamekusanyika kwenye mpaka wa Sudan Kusini baada ya kukimbia mizozo na uhaba wa chakula kwenye jimbo la Blue Nile majuma machache yaliyopita. Kwa sasa UNHCR na washirika wake wanafanya hima kuwahamisha maelfu ya wakimbizi hao na kuwapa misaada ya [...]
01/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametoa tahadhari kufuatia kundelea kuongezeka kwa ukatili unaondeshwa na makundi ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ukiwemo mauaji, ubakaji, uporaji wa mali na kuchomwa kwa vijiji ambapo ameitaka serikali kuchukua hatua za dharura za kuzuia ukatili huo. Maafisa wa haki [...]
01/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Kazi Duniani ILO linasema kuwa karibu watu milioni 21 kote duniani ni waathiriwa wa kazi za lazima. ILO inasema kuwa eneo la Asia- Pacific ndilo lenye kiasi kikubwa zaidi cha watu wanaolazimishwa kufanya kazi duniani likiwa na watu milioni 11.7 wanaofanya kazi walizohaidiwa kufanya na ambazo ni ngumu kwao kuziacha. Mabara ya Afrika [...]
01/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Utafiti Kuhusu Saratani (IARC), umeonyesha kuwa kuimarisha hali ya maisha ya watu ni sehemu muhimu katika kupunguza mzigo wa saratani uliopo sasa. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ilyochapishwa leo katika jarida la Lancet Oncology. Utafiti huo unaonyesha si tu jinsi mzigo wa saratani utayaathiri zaidi mataifa yanayofanya [...]
01/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa linafanya kikao cha dharura cha kujadili mzozo na kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini Syria. Kikao hicho kinatarajiwa kuangazia kisa cha hivi karibuni cha mauaji ya raia 108 wakiwemo watoto 49 na wanawake 34 kwenye kijiji cha EL-Houle mauaji ambayo yanakisiwa kutekelewa na makundi ya [...]
01/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa ijitolee kuisaidia Somalia kwa kipindi kirefu ili kusaidia kuikarabati nchi hiyo iloathiriwa na migogoro kwa zaidi ya miongo miwili. Bwana Ban amesema haya wakati akilihutubia kongamano la pili la kimataifa kuhusu Somalia, linalofanyika mjini Istanbul, Uturuki. Ameongeza kuwa Somalia inahitaji taasisi [...]
01/06/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »