Ingawa hatua zimepigwa Kifua Kikuu bado ni tisho kubwa Afrika:WHO

Kusikiliza /

Ugonjwa wa kifua kikuu

Machi 24 ulimwengu umeadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na maradhi ya Kifua Kikuu. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO watoto wengi wa umri kati ya kuzaliwa hadi miaka 15 huwa hawachunguzwi na hasa katika nchi zinazoendelea.

Mwaka huu shirika hilo limetoa wito wa kuwepo ushirikiano zaidi baina ya mipango ya kupambana na Ukimwi na ile ya Kifua Kikuu au TB, na hasa kushughulikia mahitaji ya kundi ambalo ni muhimu sana katika jamii la wanawake na watoto.

Ingawa kwa ujumla WHO inasema ingawa juhudi zaidi zinahitajika kukabiliana na Kifua Kikuu kuna baadhi ya nchi kama Burundi, kasi ya maambukizi ya maradhi hayo imepungua kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011 ikiwa ni sawa na asilimia 24 ukilinganisha na mwaka wa 2010.

Hata hivo maambukizi mpya zaidi ya 7000 yanaonekana kwa sehemu kubwa huambatana na ugonjwa wa Ukimwi. Na hii ndio imekuwa changamato kubwa katika vita dhidi ya Kifua Kikuu pamoja na maisha duni ya wananchi katika taifa hilo.

Mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani KIBUGA amefuatilia kwa kina hali ya Kifua Kikuu nchini Burundi na kutuandalia makala hii.

(MAKALA NA RAMADHAN KIBUGA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031