Nyumbani » 30/03/2012 Entries posted on “Machi, 2012”

Stemp ya kuelimisha kuhusu Autism yatolewa na UM

Kusikiliza / Stemp ya Autism

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya matatizo ya afya ya akili au Autism hapo Aprili pili uongozi wa huduma za posta wa Umoja wa Mataifa umetoa aina 8 za stempu ili kuelimisha umma kuhusu matatizo hayo. Matatizo ya Autism yanaathiri maendeleo ya ubongo hasa katika Nyanja ya masuala ya kijamii na mawasiliano, na ni matatizo [...]

30/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yapeleka kwa ndege msaada wa chakula Chad

Kusikiliza / WHO yatoa msaada wa chakula,Chad

Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limekamilisha kupeleka kwa ndege msaada wa haraka wa lishe kwa maelfu ya watoto walio katika hatari ya kupata utapiamlo nchini Chad, taifa ambalo limekumbwa na ukame. Ndege mbili zimewasili Ndjamena wiki hii na leo malori yataanza kubeba karibu tani 200 za msaada wa haraka [...]

30/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay kufanya ziara ya kwanza kabisa nchini Barbados

Kusikiliza / NAvi Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay atafanya ziara rasmi nchini Barbados kwa mwaliko wa serikali kuanzia tarehe 3 hadi 5 mwezi Aprili mwaka huu. Ziara hii ndiyo itakuwa ya kwanza kufanywa na mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwenye taifa la Caribbean tangu kubuniwa kwa ofisi hiyo [...]

30/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu 100,000 wakimbia mapigano kaskazini magharibi mwa Pakistan

Kusikiliza / UNHCR yatoa usaidizi nchini Pakistan

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa usaidizi kwa maelfu ya familia nchini Pakistan ambazo zimekimbia mapigano kwenye sehemu kadhaa za makabila nchini humo  kwenye mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan. Takriban watu 101,160 wengi wakiwa  wanawake na watoto wamelazimika kuhama tangu tarehe 20 mwezi Januari wakati vikosi vya serikali vilipoanzisha oparesheni [...]

30/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi utakaoandaliwa nchini Myanmar utakuwa mtihani kwa taifa hilo:Quintana

Kusikiliza / Tomas Ojea Quintana

Mjumbe maalum  wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar Tomas Ojea Quintana amesema kuwa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kundaliwa tarehe moja mwezi ujao nchini Myanmar utakuwa jaribio kwa hatua zilizopigwa na serikali  katika masuala ya mabadiliko ambapo viti 48 vya bunge vitawaniwa. Bwana Ojea Quintana anasema kuwa itakuwa ni fursa muhimu [...]

30/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Raia wa Chad waliorejea nyumbani wanahitaji msaada:IOM

Kusikiliza / Wanaorejea Chad kutoka Libya

Uchunguzi wa IOM kwa wahamiaji kutoka Chad waliorejea kutoka Libya inasema kwamba wengine wanahitaji msaada wa dharura kuunganishwa na jamii zao. Uchunguzi huo pia uligundua kuwa waliorejea nyumbani wamekumbana na changamoto zikiwemo za  kifedha za kujitafutia  na kwa familia zao. Uchunguzi huo uliendeshwa kati ya Januari na Machi mwaka huu kwenye maeneo 14 nchini Chad yaliyo na [...]

30/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afisi ya haki za binadamu ya UM yahuzunishwa na kuuawa kwa msenge nchini Chile

Kusikiliza / Mauaji ya msenge nhini Chile

Afisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea mshangao wake kutokana na kuuawa kwa mwanamme mmoja msenge nchini Chile. Afisi hiyo sasa inatoa wito kwa serikali ya Chile kuweka sheria ambayo itapiga marufuku kutengwa kwa watu kuambatana na tabia zao za kimapenzi. Washukiwa wanne wameshatiwa mabaroni huku mauaji hayo yakizua mjadala mkali  nchini [...]

30/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Surua waua zaidi ya watoto 100 nchini Yemen

Kusikiliza / UNICEF na WHO kuzindua chanjo dhidi ya Surua

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa mkurupuko wa ugonjwa wa surua umewaua watoto 177 nchini Yemen huku wengine 4000 wakiambukizwa ugonjwa huo  kwa muda wa miezi michache iliyopita. UNICEF inasema kuwa kuzorota kwa huduma za afya kufuatia mzozo ulioikumba nchi hiyo na suala la utapiamlo miongoni mwa watoto walio chini ya [...]

30/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

LRA yafanya uvamizi zaidi kwenye Afrika ya kati

Kusikiliza / Wakimbizi wa uvamizi wa kundi la LRA

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa limepokea ripoti za uvamizi unaoendeshwa na kundi la Lord's Resistance Army LRA kwenye eneo la Afrika ya Kati. Tangu machi 6 kumeripotiwa uvamizi mara 13 uliofanywa na LRA kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Watu wawili waliuawa na wengine 13 kutekwa nyara akiwemo [...]

30/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Syria yatakiwa kusitisha ghasia mara moja

Kusikiliza / Maandamano nchini Syria

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kirabu  nchini Syria Kofi Annan amesema kuwa serikali ya Syria ni lazima iwe ya kwanza kutangaza usitishaji wa ghasia na iondoe wanajeshi wake kutoka sehemu waliko raia. Annan anasema kuwa anataraji  nao upinzani kuchukua mkondo huu mara moja ikiwa ni moja ya yale yaliyopendekezwa [...]

30/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mkuu wa IOM kuhutubia kongamano la kimataifa Dubai

Kusikiliza / William Lacy Swing,Mkurugenzi Mkuu,IOM

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wahamiaji IOM William Lacy Swing anatazamia kutoa hotuba maalumu wakati wa uzinduzi kongamano la kimataifa la misaada ya usamaria mwema huko Dubai. Kongamano hilo limeandaliwa kwa msaada mkubwa wa makamu wa rais na waziri mkuu wa Jumuiya ya falme ya kiarabu Sheikh Mohammed Bin Rashid [...]

30/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waathiriwa wa majaribio ya mitambo ya nyuklia Marshall bado wanateseka:UM

Kusikiliza / Calin Georgescu

Mtaalamu mmoja kutoka Umoja wa Mataifa ameonya kuwa jamii za watu walioathiriwa na jaribio la mitambo ya kinyuklia miaka sitini iliyopita katika kisiwa cha Marshall bado wanaandamwa na jinamizi la upweke. Calin Georgescu amezitaka nchi mbalimbali duniani, ikiwemo Marekani na jumuiya za kimataifa kutafuta njia mujaribu kushughulikia kadhia inayowaandama wananchi hao. Ameeleza kuwa jamii kubwa [...]

30/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yakaribisha hatua ya Umoja wa Ulaya kuridhia mpango wa makazi

Kusikiliza / makaazi ya wakimbizi, Ulaya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua ya jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuridhia mpango maalumu wa uwekaji makazi Katika taarifa yake, shirika hilo limesema kuwa hatua hiyo inatoa matumaini na ishara njema kwa jinsi ambavyo Umoja huo na wanachama wake walivyotayari kusaidia mkwamo wa makazi unaoikabili dunia kwa sasa. Nchi [...]

30/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ingawa hatua zimepigwa Kifua Kikuu bado ni tisho kubwa Afrika:WHO

Kusikiliza / Ugonjwa wa kifua kikuu

Machi 24 ulimwengu umeadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na maradhi ya Kifua Kikuu. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO watoto wengi wa umri kati ya kuzaliwa hadi miaka 15 huwa hawachunguzwi na hasa katika nchi zinazoendelea. Mwaka huu shirika hilo limetoa wito wa kuwepo ushirikiano zaidi baina ya mipango ya [...]

30/03/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasikitishwa kuhusu ushirikiano wa kisiasa nchini Yemen

Kusikiliza / Mark Lyall Grant

Viongozi wa kisiasa nchini Yemen wametolewa wito wa kuwa na dhamira katika kipindi cha mpito na kuchukua jukumu katika ujenzi wa mchakato huu. Wito huu umetolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika taarifa iliyoelezea wasiwasi kuhusu kuzorota kwa ushirikiano kutokana na uchaguzi wa urais uliofanyika hivi karibuni. Balozi wa Uingereza Mark Lyall [...]

29/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

China inaongoza kwa kusafirisha nje na kuingiza bidhaa za teknolojia ya mawasiliano

Kusikiliza / Uchina yaongoza katika maswala ya bidhaa za teknolojia

Kwa mara ya kwanza Uchina sio tuu ni msafirishaji mkubwa anayeongoza kwa bidhaa za teknolojia ya mawasiliano (ICT) kama kompyuta na simu za mkononi bali tangu mwaka 2010 imekuwa ni muingizaji mkubwa wa bidhaa hizo. Takwimu mpya za shirika la Umoja wa mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD zinaonyesha kwamba Uchina au Hong Kong ni [...]

29/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kuzuru Chad na Niger

Kusikiliza / Kyung wha-Kang

Naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Kyung-wha Kang, Jumapili ataanza ziara ya siku sita nchini Chad na Niger kujadili  na serikali na wadau wengine masuala mbalimbali ya haki za binadamu. Hii itakuwa ni ziara yake ya kwanza kuzuru nchi hizo mbili na inakuja miezi sita baada ya ofisi ya haki [...]

29/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upungufu wa mafuta waweka maelfu ya wagonjwa hatarani Gaza:ICRC

Kusikiliza / Shirika la ICRC

Kamati ya kimataifa ya chama cha msalama mwekundu ICRC inajiandaa kuipelekea wizara ya afya ya Gaza lita 150,000 za mafuta aina ya diesel. ICRC inasema mafuta hayo yatasaidia kuendesha huduma muhimu katika hospitali 13 za umma katika siku 10 zijazo. Kamati hiyo ilipeleka tena mafuta Gaza mwezi wa Februari. Kwa mujibu wa mkuu wa ICRC [...]

29/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

New York yatunukiwa tuzo ya Miji ya Lee Kuan mwaka 2012

Kusikiliza / Mji wa New York wapewa tuzo

Tuzo ya kimataifa ya Lee Kuan Yew ya miji kwa mwaka 2012 ametunukiwa meya wa jiji la New York Michael Bloomberg na idara ya usafiri, mipango miji, hifadhi na burudani limesema shirika la Umoja wa mataifa la makazi UN-HABITAT. Waandaaji wa tuzo hiyo wamesema mji wa New York umefanya mabadiliko makubwa baada ya mashambulizi ya [...]

29/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni muhimu kuwasaidia wajasiriamali wa mashinani kuhamia uchumi unaojali mazingira:UNEP

Kusikiliza / Wakulima shambani

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP limesema kuwasaidia wajasiriamali wanamazingira wadogowadogo kunaweza kusaidia kukabiliana na changamoto za nishati, kilimo na usalama wa chakula na pia kusaidia kuhamia katika uchumi unaojali mazingira. Huu ni ujumbe uliotolewa kwenye kongamano lijulikanalo kama SEED mjini Pretoria Afrika ya Kusini Alhamisi, kongamano ambalo linasherehekea mafanikio ya mashinani katika [...]

29/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bodi ya kimataifa yakutana kukomesha biashara haramu ya bidhaa za tumbaku

Kusikiliza / Biashara haramu ya bidhaa za tumbaku

Mkutano wa kimataifa unaofanyika mjini Geneva umeamua kuongeza muda wa bodi ya kimataifa ya majadiliano INB kwa lengo la kumalizia awamu ya mwisho ya mkutano unaokamilisha mswada wa sheria ya kukomesha biashara haramu ya bidhaa za tumbaku. Mkutano huo pia umeanzisha kundi lisilo rasmi la kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kabla ya kikao cha mwisho [...]

29/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNIFIL na maafisa wa Israel na Lebanon wakutana

Kusikiliza / Paola Serra, meja generali,komanda wa kikosi cha UNFIL

Mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Lebanon UNIFIL na maafisa wa kijeshi wa Lebanon na Israel wamekutana kujadili masula muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa azimio la Baraza la Usalama ambalo lilimaliza vita vya mwaka 2006 kati ya Israel na kundi la Lebanon lijulikanalo kama Hizbollah. Kwa mujibu wa mkuu [...]

29/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ILO na serikali ya Australia waanzisha mradi wa dola millioni 31 Timor-Leste

Kusikiliza / nemba ya ILO

Shirika la kazi duniani ILO na serikali ya Australia wametangaza mradi mpya utakaogharimu dola milioni 31 kusaidia kuboresha usafiri wa barabara nchini Timor-Leste. Ukifadhiliwa na shirika la kimataifa la maendeleo la Australia AusAID mradi huo wa miaka mine moja ya miradi mikubwa kabisa ya maendeleo ya miundombinu katika eneo la Asia-Pacific. Mradi huo unatekelezwa na [...]

29/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasikilizeni watu, Ban aumbaia mkutano wa Umoja wa nchi za Kiarabu nchini Iraq

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Viongozi kutoka nchi za Kiarabu wameaanza mazungumzo kuhusu mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria, ikiwa ni mkutano wa kwanza wa kimataifa kufanyika nchi Iraq baada ya miongo kadhaa. Mpango huo wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu unataka kushuhudia kumalizika kwa mapigano Syria, majeshi ya serikali kuondoka [...]

29/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMA yaongezwa muda wa kuhudumu nchini Afghanistan

Kusikiliza / UNAMA

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umesema kuwa kuongezwa kwa muda wake wa kuhudumu nchini Afghanistan kunatoa fursa ya kushirikiano na serikali ili kuleta amani, maendeleo na malengo mengine nchini humo. Juma lililopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililiongeza muda wa kuhudumu kwa UNAMA kwa mwaka mmoja zaidi ili iendelee kulisaidia [...]

29/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kijana mkimbizi wa Kisomali ana ndoto ya kuwa nyota wa hip hop

Kusikiliza / Saber kijana wa kisomali

Saber ni kijana mkimbizi kutoka Somalia mwenye umri wa miaka 17 ambaye ana kipawa cha uimbaji wa nyimbo mtindo wa hip hop. Hata hivyo Saber anasema kuwa bila ya kuungwa mkono na familia yake ndoto yake haitafanikiwa. Kijana huyo kwa sasa amekwama kwenye kituo cha kupitishia wakimbizi cha Choucha karibu na mpaka kati ya Tunisia [...]

29/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM aelezea Baraza la Usalama changamoto zilizoko nchini Guinea-Bissau

Kusikiliza / Joseph Mutaboba

Mjumbe wa UM nchini Guinea-Bissau amesema kipindi cha mpito cha sasa nchini ni moja ya changamoto zinazoikabili nchi hiyo. Joseph Mutaboba ameliambia Baraza la Usalama kuwa tangu kifo cha rais Malam Bacai Sanha, suala la kurejesha katiba kamili katika taifa hili la Afrika Magharibi limepewa kipaumbele muhimu. Uchaguzi wa urais ulifanyika mapema mwezi huu, na [...]

28/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAIDS na NEPAD watia sahihi makubaliano ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi barani Afrika

Kusikiliza / UNAIDS na NEPAD watia saini kuhusu hatua zaidi kupambana na Ukimwi

Shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS kwa ushirikiano na shirika la maendeleo la bara Afrika NEPAD wametia sahihi makubaliano ya kutaka   kuchukuliwa hatua zaidi katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi barani Afrika. Makubaliano hayo yalitiwa sahihi na mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michael Sidibe na mkurugenzi mkuu wa NEPAD Dr [...]

28/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IAEA yatoa ripoti kuhusu mipango mipya ya usalama wa nyuklia nchini Japan

Kusikiliza / Ripoti ya usalama wa nyuklia nchini Japan na IAEA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA limewasilisha ripoti yake kuhusu uchunguzi lililoendesha kuhusu usalama wa mipango ya nyuklia wa taifa la Japan baada taifa hilo kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi ambapo kinu cha nyuklia cha Fukushima Daiichi kiliharibiwa. Uchunguzi huo ulifanywa na kundi la wataalamu kutoka shirika la IAEA walioizuru [...]

28/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya UM yahofia hatma ya watu wanaoishi kwenye kambi nchi Haiti huku msimu wa mvua ukiendelea

Kusikiliza / Kuna hatari ya mafuriko kambini, Haiti

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa huku msimu wa mvua ukiendelea nchini Haiti hadi watu 65,000 wanaoishi kwenye kambi kwa sasa wanakabiliwa na hatari ya mafuriko. OCHA inasema kuwa tayari mvua zinazoendea kunyesha zimesababisha uharibifu kwa kambi tano kwenye mji mkuu Port-au-Prince. OCHA inalalamika kuwa haikupata ufadhili wa [...]

28/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuna uwezekano mdogo wa kuendelea na mpango wa amani mashariki ya kati:Serry

Kusikiliza / Robert Serry

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Mashariki ya kati Robert Serry amesema kuwa hali kati ya Wapalestina na Waisrael inasalia kuwa isiyotabirika na ngumu. Akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Serry amesema kuwa kilichoko ni kwamba pande zote mbili hazijapa makubaliano ya kurejea kwenye mazungumzo na uwezekano huo unasalia kuwa [...]

28/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanakandanda wa kimataifa Barani Ulaya wachuana kupinga njaa Sahel:FAO

Kusikiliza / Mchuano wa kandanda dhidi ya njaa

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema kampeni ya "wanakandanda mashuhuri kupambana na njaa" inawasili katika viwanja mbalimbali vya kabumbu barani Ulaya na ujumbe maalumu kwamba hatua zinahitajika sasa ili kuepuka janga la kibinadamu kwenye eneo la Sahel Afrika . Eneo hilo ambako matatizo ya chakula na lishe yaliyosababishwa na ukame, umasikini uliokithiri, bei kubwa [...]

28/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ESCAP kuisaidia Afghanistan kutoka kwenye vita na kuingia katika maendeleo

Kusikiliza / ESCAP

Umoja wa Mataifa uko tayari kuisaidia Afghanistan katika kipindi cha mpito kutoka vitani na kuingia katika maendeleo, hasa kwa kuisaidia kuiunganisha na mikakati ya maendeleo ya kikanda amesema Katibu Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na jamii kwa ajili ya nchi za Asia na Pacific ESCAP. Bi Noleen Heyzer akizungumza katika kongamano [...]

28/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umejidhatiti kuhakikisha usalama na utulivu Kuwait:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban akiwa na Amir nchini Kuwait

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema Umoja wa Mataifa umejidhatiti kuhakikisha kuna usalama na utulivu nchini Kuwait na kwamba kuna kuwa na utekelezaji wa maazimio yote ya Baraza la Usalama ikiwemo kutoweka kwa watu na mali nchini humo, mradi wa mpaka baina ya Kuwait na Iraq na ulipaji wa fidia. Akizungumza mjini [...]

28/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matukio ya hali mbaya ya hewa yanatarajiwa kuongezeka:IPCC

Kusikiliza / Mabadiliko mbaya ya hali ya hewa

Matukio ya kiwango cha juu na ya mara kwa mara ya hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya majira kama joto la kupindukia, mafuriko na ukame yanatarajiwa kuongezeka duniani kote kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa imesema ripoti mpya ya jopo la kimataifa la mabadiliko ya hali ya hewa IPCC. Ripoti hiyo hata hivyo [...]

28/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay apongeza uchaguzi wa Senegal na kuzitaka Mali na Guinea Bissau kufuata nyayo

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay Jumatano ameipongeza Senegal kwa kuendesha duru ya pili ya uchaguzi wa Rais kwa amani, uhuru, haki na kwa uwazi, na amezitaka nchi zingine katika kanda hiyo kufuata nyayo. Pillay amesema katika wakati ambao kuna ghasia zinazoambatana na uchaguzi katika sehemu zingine za Afrika ya Magharibi inatia moyo [...]

28/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kambi ya Kakuma yashuhudia wimbi la wakimbizi kutoka Sudan na Sudan Kusini:UNHCR

Kusikiliza / wakimbizi wawasili katika kambi ya Kakuma

  Kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya imeanza kushuhudia tena wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Sudan na Sudan Kusini. Kambi hiyo ilianzishwa mwaka 1992 kwa ajili ya wakimbizi wa Sudan kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa vikiendelea, lakini kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR miaka 20 baadaye [...]

28/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lazitaka Sudan na Sudan kusini kujizuia kuendeleza machafuko mpakani

Kusikiliza / Mark Lyall Grant

Baraza la Usalama limetoa tahadhari kuhusu mapigano ya kijeshi kwenye maeneo ya mpakani kati ya Sudan na Sudan Kusini, likisema makabiliano hayo yanatishia kuchochea vita baina ya nchi hizo mbili, kuzorotesha zaidi hali ya kibinadamu na kusababisha vifo vya raia. Wajumbe wa Baraza la Usalama wamezitaka Sudan na Sudan Kusini kujizuia na kufanya mazungumzo ya [...]

28/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msafara wa watu wanaorejea nyumbani umekwama katikati ya mapigano Sudan Kusini:IOM

Kusikiliza / ramani ya Sudan

Shirika la wahamiaji la IOM limesema msafara wa magari yanayosafirisha raia wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani kutoka Sudan Kaskazini umekwama katikati ya mapigano kati ya waasi na majeshi ya Sudan Kusini. Kwa mujibu wa IOM watu zaidi ya 1000 hadi hivi sasa wanashikiliwa. Shirika la IOM limesema linashirikiana na mashirika mengine kuwaokoa raia hao. Jumbe [...]

27/03/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban awataka viongozi wa Senegal kuweka ushirikiano mbele

Kusikiliza / Mabano ya rais Wade wakati wa kampeni

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa Senegal, anayeondoka madarakani Abdoulaye Wade, na Bwana Macky Sall ambaye anayeripotiwa kushinda katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma, kushirikiana kwa pamoja kwa maslahi ya watu wa taifa lao. Bwana Ban amewapigia simu viongozi wote wawili akiwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Senegal kutokana na kuendesha [...]

27/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ICTR yaamuru mshtakiwa wa mauaji ya Rwanda arejeshwe Kigali

Kusikiliza / Mahakama kuhusu mauwaji ya Rwanda

Mahakama ya Umoja wa Mataifa ambayo inaendesha kesi dhidi ya watuhumiwa muhimu waliohusika kwenye mauwaji ya mwaka 1994 nchini Rwanda, imetaka mashauri juu ya watuhumiwa kadhaa waliosalia yahamishiwe katika mahakama kuu ya Rwanda. Mahakama hiyo kwa ajili ya uhalifu wa kivita wa Rwanda ICTR, imeamuru keshi dhidi ya mtuhumiwa Charles Sikubwabo irejeshwe nchini Rwanda na [...]

27/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji kwenye kilimo utasaidia kutokomeza umaskini barani Afrika:UM

Kusikiliza / Mkulima shambani

Umoja wa Mataifa umehimiza haja ya kuwekeza kikamilifu kwenye maeneo ya kilimo ikitaja kuwa ndiyo njia mujarabu ya kukabiliana na tatizo la umaskini barani afrika. Kwa mujibu wa rais wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD, Kanayo F. Nwanze kuongeza kasi ya uwekezaji kwenye eneo la kilimo ni hatua muhumu ya [...]

27/03/2012 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Matumizi ya sheria yanaweza kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake:Manjoo

Kusikiliza / Rashida Manjoo

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Rashida Manjoo ametoa wito kwa serikali ya Papua New Guinea kutumia njia za kisheria kwenye harakati zake za kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake. Akikamilisha ziara yake nchini humo Bi Manjoo pia ameushauri utawala wa nchi hiyo kuondoa baadhi ya itikadi za kitamaduni zinazowadhulumu wanawake. Mtaalamu huyo amelitwika jukumu na Baraza [...]

27/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yawasaidia vijana kumaliza masomo yao nchini Ufilipino

Kusikiliza / Usaidizi kwa watoto maskini wa Ufilipino

Mamia ya watu wamefaidika kutoka kwenye mradi uliozinduliwa miaka miwili iliyopita uliokuwa na lengo la kuwasaidia vijana wasiojiweza na watoto wa wahamiaji kwenye baadhi ya mikoa maskini zaidi nchini Ufilipino kumaliza masomo yao. Mradi huo ulioanzishwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na chama cha wafilipino wanaofanya kazi mataifa ya kigeni ulitoa huduma za [...]

27/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yataka kulindwa kwa raia mashambulizi ya roketi yanapoendelea mjini Mogadishu

Kusikiliza / raia wa Mogadishu

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasi wasi ya kuendelea kwa mashambulizi ya maroketi kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu yaliyowaua watu watatu hiyo jana. Maroketi kadhaa yalianguka kwenye eneo la Beerta Darawiishta yaliyo makao kwa wakimbizi wa ndani karibu na bunge la Somalia mapema jana. Inaripotiwa kuwa wakimbizi watatu wa [...]

27/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kuzorota kwa usalama yazua wasiwasi kwenye eneo la Yida, Sudan Kusini

Kusikiliza / Wakimbizi, Yida Sudan kusini

Mapigano ya mara kwa mara kwenye eneo linalozozaniwa la ziwa Jau yanazua wasi wasi hasa kuhusu hatma ya wakimbizi wa Sudan walio kwenye eneo la Yida. Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa mapigano yaliripotiwa hapo jana kati ya vikosi vya serikali ya Sudan na vya Sudan Kusini kwenye ziwa Jau [...]

27/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watafuta hifadhi yaongezeka kwenye mataifa yaliyostawi

Kusikiliza / Wahamiaji

Ripoti kutoka kwa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR inasema kuwa idadi ya watafuta hifadhi kwenye mataifa yaliyostawi iliongezeka kwa asilimia 20 mwaka 2011 hali iliyochangiwa na mizozo kwenye nchi za kiarabu na kaskazini mwa Afrika. Jumla la watafuta hifadhi 441,000 waliandikishwa mwaka uliopita tofauti na watu 368,000 walioandikishwa mwaka 2010 kwenye  [...]

27/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugaidi wa kinyuklia ni tisho kwa dunia:Ban

Kusikiliza / Katika mkutano wa usalama wa nyuklia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa suala la ugaidi wa nyuklia linatishia usalama wa kimataifa. Akiongea kwenye mkutano kuhusu usalama wa nyuklia mjini Seoul nchini Korea Kusini Ban amesema kuwa mataifa yote yameungana katika kukabiliana na tisho hili. Ban pia ana mipango ya kuitisha mkutano wa kimataifa mwezi Septemba  mwaka huu kwenye makao makuu [...]

27/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Syria yakubaliana na mapendekezo ya mpango wa amani yaliyotolewa na Kofi Annan

Kusikiliza / Kofi Annan

  Serikali ya Syria imemuandikia mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo Kofi Annan ikikubaliana na mapendekezo sita kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Annan amemuandikia rais wa Syria Bashar Al- Assad ambapo ameitaka serikali ya Syria kuyatekeleza yote kwenye majibu hayo. Kulingana na Annan hii ni hatua nzuri ambayo itachangia [...]

27/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wana wajibu wa kuhakikisha amani inaendelea hata wakiondoka:Ladsous

Kusikiliza / Herve Ladsous

Walinda amani wana wajibu wa kuhakikisha amani inaendelea kwa muda mrefu hata baada ya kuondoka eneo lenye vita amesema afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa. Akitoa taarifa kwenye baraza la usalama Jumatatu Herve Ladsous ambaye ni mkuu wa idara ya operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa amesema kuondoka kwa walinda [...]

26/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mrembo wa ulimwengu 2011 kuelimisha kuhusu maeneo kame

Kusikiliza / Leila Lopez

Mwanamke mrembo kabisa ulimwenguni atasaidia kuelimisha kuhusu kuporomoka kwa maeneo kame, tatizo ambalo linaathiri zaidi ya watu bilioni moja duniani. Mrembo wa ulimwengu mwaka 2011 Leila Lopes ameteuliwa kuwa balozi mwema wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na hali ya jangwa (UNCCD). Akizungumza mjini New York Jumatatu Bi Leila Lopes amesema maeneo makame [...]

26/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM watoa heshima kwa wale wanaotetea ukweli na haki ya utumwa

26/03/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mapendekezo ya majina ya wagombea urais wa benki ya dunia yasitishwa

Kusikiliza / Ngozi Okonjo-Iweala, mmoja wa wanaogombea urais

Bodi ya wakurugenzi wakuu wa benki ya dunia imethibitishwa kwamba kipindi cha kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea wa nafasi ya urais wa Benki hiyo kimemalizika Ijumaa Machi 23. Bodi hiyo ya wakurugenzi imesema ina furaha kutangaza kwamba majina matatu yatafikiriwa katika nafasi ya Urais ambayo ni Jim Yong Kim raia wa Marekani na Rais [...]

26/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vizazi vijavyo lazima vielimishwe kuhusu biashara ya Utumwa:Al Nasser

Kusikiliza / picha ya watumwa

Rais wa Baraza Kuu wa Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema biashara ya utumwa ilikuwa ni changamoto na mtihani kwa dunia na ili kukabiliana na changamoto kama hiyo unahitajika mshikamano, uwajibikaji, shiriki na ushirikiano wa kila aina katika jamii. Akizungumza katika kumbukumbu maalumu ya kuwaenzi waathirika wa utumwa na biashra ya utumwa katika makao [...]

26/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban ahudhuria mkutano wa usalama wa nyuklia DPRK

Kusikiliza / Bendera ya DPRK

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anakutana na viongozi mbalimbali wa dunia katika mkutano wa siku mbili kuhusu usalama wa nyuklia unaofanyika Korea Kusini. Zaidi ya wakuu wa nchi 50 na mashirika ya kimataifa wamekusanyika Seoul kujadili njia za kukabiliana na tishio la ugaidi wa nyuklia pamoja na kulinda vifaa, zana na mitambo [...]

26/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia itizame upya agenda zake za kimaendeleo

Kusikiliza / Jumuiya ya kimataifa

Jumuiya ya kimataifa imeshawishiwa kuweka upenyo wa pamoja ili kushagihisha agenda za maendeleo ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endeleo. Wakishiriki kwenye mkutano wa kimataifa unaoratibiwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kwa ushirikiano na Uturuki, wajumbe kwenye mkutano huo wametoa wito kwa jumuiya kimataifa kuzitizama upya agenda zinazogusia maendeleo kwa [...]

26/03/2012 | Jamii: Malengo ya maendeleo ya milenia, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban azuru Korea Kusini na kujadilia kitisho cha nyuklia

Kusikiliza / Maswala ya nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na rais wa Korea ya Kusin Lee Myung-bak mjini Seoul. Viongozi hao wawili walituwama katika eneo la mkwamo wa mambo huko Syria, urutubishaji wa silaha za nyuklia kwa usalama wa dunia na kinu cha Peninsula. Ban ambaye kwa sasa yuko kwenye ziara ya kikazi [...]

26/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misitu asilia ya mtiki inapungua wakati ya kupandwa inaongezeka:FAO

Kusikiliza / Mkulima apalilia shamba la mtiki

Matokeo ya tathimini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO iliyofanywa kuhusu rasilimali na soko la mtiki katika nchi 60 yanaonyesha kwamba misitu asilia ya mtiki inapungua duniani na kwamba ubora wa mbao za mtiki asilia unaendelea kushuka. Kwa upande mwingine matokeo hayo yaliyochapishwa Jumatatu yanaonyesha kwamba misitu ya mtiki inayopandwa [...]

26/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Annan na Rais wa Urusi wakutana na kujadili hali ya Syria

Kusikiliza / Kofi Annan na rais wa Urusi Demitri Medvedev

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiaarabu Kofi Annan amewasili Moscow na kukutana na Rais Demitri Medvedev kujadili suala la Syria na njia za kumaliza matumizi ya nguvu na mauaji nchini humo. Annan anajaribu kuishwishi Urusi ambayo ni mshirika muhimu wa Syria ichukue msimamo mkali dhidi ya Rais Bashar al [...]

26/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA kupata msaada kutoka Marekani

Kusikiliza / Msaada zaidi kwa UNRWA

Mshauri maaluum wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton kuhusu masuala ya kimataifa ya vijana ametangaza kwenye mkutano wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ongezeko la msaada wa dola milioni 10 kwa mfuko wa shirika hilo. Ongezeko hilo litafanya mchango wa serikali ya Marekani kwa [...]

26/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumza na viongozi wa Australia na Gabon kwenye mkutano wa nyuklia

Kusikiliza / Katibu mkuu na rais Lee Myung Bak wa Korea kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko Seoul Korea kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa usalama wa nyuklia amefanya mazungumzo kando na mkutano na baadhi ya viongozi wa dunia. Ban alipozungumza na waziri mkuu wa Australia Julia Gillard ameishukuru nchi hiyo kwa mchango wake mkubwa kwa kazi za Umoja wa mataifa na hasa katika [...]

26/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atoa heshima kwa wale wanaotetea ukweli na haki

Kusikiliza / makumbusho ya Tuol Sleng

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza mashujaa kote duniani kutokana na mchango wao katika kulinda haki za binadamu pamoja na kuhakikisha kuwepo ukweli na haki. Machi 24 ni siku ya kimataifa ya haki ya ukweli inayohusiana na ukiukaji wa haki za binadamu kwa minajili ya kuwakumbuka waathiriwa wa vitendo vya ukiukaji wa [...]

26/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msafara wa UNHCR wawasili Kachin Myanmar na msaada wa dharura

Kusikiliza / Wakimbizi katika kambi, Myanmar

Msafara wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ukiwa umesheheni msaada wa dharura wa kibinadamu umewasili eneo lililoathirika na vita la jimbi la Kaskazini la Kachin nchini Myanmar. Msafara huo wa malori manne na magari madogo mawili umebeba matandiko, vyandarua vya mbu na vifaa vya jikoni, pamoja na chakula na misaada mingine [...]

26/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka ulinzi kutolewa kwa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Katibu MKuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyataka mataifa yote kuungana ili kuwalinda maelfu ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaohatarisha maisha yao katika kuwasaidia wanaohitaji msaada kote duniani. Ban amesema kuwa ni mataifa 90 yaliyoidhinisha makubaliano ya mwaka 1994 yanayohusu usalama wa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa huku nchi 27 zikiwa zimetia sahihi makubaliano ya [...]

26/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya UM yaonya kuwa hakutakuwa na ulipizaji kizazi dhidi ya watetea haki za binadamu

Kusikiliza / baraza la haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa hakutakuwa na ulipizaji kisasi dhidi ya wale wanaopigania haki za binadamu nchini Sri Lanka kutokana na kutekelezwa kwa azimio na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu Sri Lanka. Wanaharakati kutoka Sri Lanka waliosafiri kwenda Geneva wamekuwa wakipokea vitisho wakati unapoendelea [...]

23/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO yatoa ombi la kusaidia nchi za pembe ya Afrika

Kusikiliza / Mifugo

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO hii leo limetoa ombi la dharura la dola milioni 50 zitakazotumiwa katika kugharamia shughuli za ufugaji na kilimo kwenye pembe ya Afrika kabla ya msimu wa upanzi unaoambatana na mvua kati ya mwezi Aprili na Juni mwaka huu. Ufadhili huo utahitajika ili kufanikisha mpango wa [...]

23/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wenye viwango vya juu vya joto:WMO

Kusikiliza / Shirika la hali ya hewa duniani

Ripoti ya kila mwaka ya shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kuhusu hali ya hewa inasema kuwa mwaka 2011 uliandikisha viwango vya juu zaidi vya joto na ni mwaka wa 11 kati ya miaka yenye viwango vya joto vya juu zaidi tangu takwimu hizo zianze kuchukuliwa mwaka 1850. Hali hii ilizua athari [...]

23/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM watoa wito wa dola milioni 84 za kusaidia wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake wa kutoa huduma za binadamu hii leo wametoa ombi la dola milioni 84 zitakazotumika kuwasiadia wakimbizi wa Syria walio nchini Jordan, Lebanon Uturuki na Iraq. Mpango huo unakadiria kuwa kwa muda wa miezi sita inayokuja utahitaji kuwashughulikia wakimbizi 100,000 raia wa Syria. Hata hivyo mpango huo hautoi shughuli [...]

23/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu laitaka Syria kuheshimu wito wa wananchi wake

Kusikiliza / Waandamanaji, Syria

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limelaani vikali ukiukaji wa haki za binadamu unaondelea nchini Syria na unaoendeshwa na serikali ya Syria ukiwemo mauaji, matumizi ya nguvu kupita kiasi na mauaji ya waandamanaji, wakimbizi , watetesi wa haki za binadamu na waandishi wa habari.  Baraza hilo limeitaka serikali ya Syria kuheshimu wito wa [...]

23/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushahidi zaidi unahitajika kutambua ugonjwa sugu wa TB:WHO

Kusikiliza / Ugonjwa wa kifua kikuu

Wataalamu kutoka kwa shirika la afya duniani WHO wamesema kuwa kwa sasa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuutambua ugonjwa wa kifua kikuu ulio sugu kwa madawa. Utafiti wa madawa wa kubaini kuwa ugonjwa umekuwa sugu umekosa majibu yaliyo sahihi hasa kwa madawa yanayotumika kutibu aina ya ugonjwa wa kifua kuu ulio sugu. Vile vile kuna [...]

23/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunaifuatilia kwa karibu hali nchini Mali:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Mali

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linafuatilia kwa karibu hali nchini Mali kufuatia tangazo kuwa wanajeshi wamechukua udhibiti wa nchi hiyo. UNHCR inasema kuwa kumeshuhudiwa kuhama kwa wa watu  ndani mwa nchi au kwenda kwa mataifa jirani. Suala linaloisumbua UNHCR kwa sasa ni  jinsi hali itakavyoendelea kuwa na iwapo inaendelea kusababisha kuhama kwa [...]

23/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Annan aelekea Moscow na Beijing

Kusikiliza / Kofi Annan

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Kofi Annan anasema kuwa hana mpango wa kurejea tena nchini Syria na badala yake atachunguza majibu yaliyotolewa na nchi hiyo. Annan anatarajiwa kujadili majibu yaliyotoka nchini Syria baada ya mapendekezo yaliyotolewa na katibu huyo mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa ya kumaliza ghasia na ukiukaji wa [...]

23/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna mabadiliko kwenye uongozi wa dunia:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kumeshuhudiwa nguvu na uwezo wa ushirikiano ambao umechangia kuleta matokeo duniani. Akiongea kwenye taasisi moja nchini Singapore hii leo Ban amesema kuwa nchini Ivory Coast wito wa mabadiliko ulifanywa na  jumuiya ya uchumi ya mataifa ya magharibi mwa Afrika ECOWAS pamoja na Muungano wa [...]

23/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM washirikiana na Indonesia kuzindua mwongozo wa kukabili majanga ya dharura

Kusikiliza / Valerie Amos

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali ya Indonesia umezindua mwongozo maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wananchi wa nchi hiyo kukabiliana na majanga ya kimaumbile. Mwongozo huo unaweka maelekezo na kutoa mbinu juu ya kukabiliana na majanga ya kimaumbile. Unazingatia mpango wa miaka minne, kuanzia mwaka 2010 hadi 2014. Mkuu wa Umoja wa Mataifa [...]

23/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa afya wakaribisha azimio la usajili wa kuzaliwa

Kusikiliza / Usajili wa kuzaliwa

Wataalamu wa masuala ya afya ikiwemo mtandao unatupia macho masuala ya afya pamoja na shirika la afya ulimwenguni WHO wamekaribisha azimio lililopitishwa na baraza la haki za binadamu linalozingatia usajili wa kuzaliwa. Baraza hilo la Umoja wa Mataifa hapo jana lilipitisha rasmi azimio la ulazima wa kusajili uzaliwa kwa kila mtu kwa shabaha ya kupunguza [...]

23/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNAMA yaongezewa muda wa kubaki Afghanistan

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la usalama limeongeza muda wa kuendelea kusalia kwa kamishna  ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan. Kwa maana hiyo kamishna hiyo ya Umoja wa Mataifa UNAMA itaendelea na operesheni zake kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi. Kamishna hiyo imetwishwa jukumu la kuratibu shughuli mbalimbali ambazo zitafanikisha kwa taifa hilo kujiendesha lenyewe. Maeneo yanayotiliwa uzito na [...]

23/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utumwa na biashara ya utumwa yakumbukwa kimataifa Machi 25

Kusikiliza / Minyororo ya utumwa

Machi 25 wiki hii ni maadhimisho ya kimataifa ya kumbukumbu ya waathitika wa utumwa na biashara ya utumwa iliyojulikana kama Transatlantic Slave Trade. Katika maadhimisho hayo Radio ya Umoja wa Mataifa imeamua kuenzi kumbukumbu za mamilioni ya watu ambao waliteseka na kupoteza maisha katika utumwa na biashara ya Transatlantic slave trade. Inafanya vipindi maalumu katika [...]

23/03/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Maji duniani:Matumizi endelevu ya rasilimali muhimu duniani

22/03/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Kuadhimisha Siku ya Maji duniani

Kusikiliza / siku ya maji duniani

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya maji ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni “maji na usalama wa chakula” inaonekana kuwa nchi nyingi zimepiga hatua katika udhibiti wa maji lakini bado juhudi zaidi zinahitajika. Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova ameitaka dunia kuungana pamoja ili [...]

22/03/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UM waadhimisha siku ya watu wenye matatizo ya kiafya

Kusikiliza / UM

Kwa mara ya kwanza Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku ya kimataifa duniani inayohusu matatizo ya kijeneti katika mwili wa binadamu. Maadhimisho hayo ni hatua mojawapo ya kuhakikisha kwamba watu wenye matatizo hayo wanatendewa haki. Hali hiyo inaweza kumfanya mtu kukosa mawasiliano ya moja kwa moja baina ya viungo vyake na akili. Katika ujumbe wake kuadhimisha siku [...]

22/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Iran imekiuka vikwazo vya silaha:UM

Kusikiliza / Nestor Osorio

Mkuu wa kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yenye jukumu la kufuatilia vikwazo vya silaha ilivyowekewa Iran kuhusiana na mipango yake ya kinyuklia imesema kuwa imepokea ripoti za ukiukaji wa baadhi ya vikwazo kwa muda wa miezi mitatu iliyopita. Kwenye ripoti yake ya kila miezi mitatu kati ya tarehe 21 mwezi Disemba [...]

22/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wataka kuwa na ushirikino wa kitamaduni

Kusikiliza / Sherehe za NOWRUZ

Maafisa kutoka Umoja wa Mataifa wanasema kuwa moyo wa amani na Umoja vyote vinavyohusiana na maadhimisho ya Nowruz ambazo ni sherehe katika kalenda ya Iran ni muhimu hasa wakati   kunaposhuhudiwa mabadiliko duniani. Kwenye ujumbe wake wakati wa maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbusho kuwa [...]

22/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban aipongeza Malaysia kwa msaada wake kwa UM

Kusikiliza / Katibu mkuu katika ziara yake Malaysia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelipongeza taifa la Malaysia kutokana na usaidizi wake kwa Umoja wa Mataifa na kulitaka kuendelea na moyo huo. Akiongea wakati wa  chakula cha jioni anapondelea na ziara yake ya mataifa manne Ban amesema kuwa taifa la Malaysia limetoka mbali katika kuujenga uchumi wake akiongeza kuwa utajiri wa [...]

22/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Juhudi zinafanyika kupunguza hatari ya mafuriko Haiti:UNEP

Kusikiliza / Jitihada za kupunguza hatari ya mafuriko, Haiti

Wakati msimu wa mvua ukinyemelea, juhudi zinafanyika kuimarisha uangalizi katika maeneo yaliyo kwenye hatari ya mafuriko kama Port-a-Piment Kusini mwa Haiti ili kupunguza hatari ya majanga kwa jamii. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP mafuriko makubwa yaliyoikumba Haiti mwezi Oktoba mwaka jana yalisambaratisha kabisa baadhi ya jamii na kuwalazimisha maelfu [...]

22/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mlipuko wa ugonjwa wa Sotoka waikumba Misri:FAO

Kusikiliza / Mkulima, Misri

Hatua za haraka zinahitajika kudhibiti mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa mifugo wa miguu na midomo au sotoka  na pia kuzuia kusambaa kwake Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati hali ambayo inaweza kuleta athari kubwa kwa usalama wa chakula katika maeneo hayo limeonya shirika la chakula na kilimo FAO Alhamisi. Wakati kukihitajika chanjo mashirika ya kimataifa [...]

22/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanajeshi waasi wafanya mapinduzi nchini Mali

Kusikiliza / Mapinduzi ya utawala nchini Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anafuatilia kwa karibu huku akitiwa hofu na hali iliyojitokeza nchini Mali Jumatano, ambapo wanajeshi waasi wametangaza kupitia televisheni ya taifa ya nchi hiyo kuwa wamechukua udhibiti wa nchi saa kadhaa baada ya kuvamia kasri la Rais. Wanajeshi hao wametangaza marufuku ya kutotoka nje katika nchi nzima na [...]

22/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za binadamu lataka uchunguzi wa vita Sri Lanka

Kusikiliza / Waziri wa Sri Lanka ahutubia Baraza la Usalama

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuunga mkono azimio linaloitaka Sri Lanka kuchunguza ukiukwaji uliotekelezwa wakati wa sik za mwisho za vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Wajumbe 24 wamepiga kura kuunga mkono azimio hilo linalodhaminiwa na Marekani, wengine 15 wakiwemo Uchina, Urusi na Cuba wamepiga kura ya kupinga [...]

22/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto milioni 111 kuchanjwa dhidi ya Polio kwa siku nne:WHO

Kusikiliza / Chanjo dhidi ya Polio, Afrika

Kampeni inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ina mpango wa kutoa chanjo dhidi ya polio kwa watoto zaidi ya milioni 111 wenye umri wa chini ya miaka mitano katika nchi 20 barani Afrika kwa kipindi cha siku nne. Kampeni hiyo itakayojikita Afrika Magharibi na Kati itakuwa na lengo la kufikia watoto wote waliochanjwa au ambao [...]

22/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya Syria inaendelea kuwa mgogoro mkubwa:Ban

Kusikiliza / Ban akiwa Malaysia

  Hali nchini Syria inaendelea kuwa zahma kubwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameuambia mkutano na waandishi wa habari Alhamisi akihitimisha ziara yake nchini Malaysia. Ban amesema wakati wakijadili amani na utulivu Mashariki ya Kati Syria ni sehemu ya eneo hilo, na kutokuwepo kwa utulivu Mashariki ya Kati kuna athari kubwa katika [...]

22/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa lazima ihakikishe matumizi bora ya maji:Ban

Kusikiliza / Siku ya maji duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiungana na dunia kuadhimisha siku ya kimataifa ya maji, amesema kuzalisha chakula cha kutosha kulisha idadi kubwa ya watu inayoongezeka duniani kutahitaji jumuiya ya kimataifa kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali muhimu ya maji. Amesema matumizi mabaya ya maji yatasababisha kuendelea kwa tatizo la njaa, ukame na matatizo [...]

22/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matumizi mabaya ya maji yatasababisha kuendelea kwa njaa, ukame na matatizo ya kisiasa:UM

Kusikiliza / mtoto anakunywa maji

Miaka 20 ilyopita mkutano wa kwanza wa Rio de Jenairo ulioitwa Rio Earth Summit ulielezea umuhimu wa udhibiti wa rasilimali ya maji katika kuwa na mustakhbali imara wa uhakika wa chakula kwa dunia hii. Wakati nchi nyingi zimepiga hatua katika udhibiti wa maji bado juhudi zaidi zinahitajika amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na [...]

22/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

"Askari wanaoshiriki vitendo vya ubakaji wasipatiwe kinga"

Kusikiliza / Ann-Marie Orler

Mkuu wa shughuli za kipolisi kwenye Umoja wa Mataifa ametaka kukomeshwa tabia ya kukingiwa kifua kwa askari wa kulinda amani ambao mara nyingi wanatumbukia kwenye vitendo vya uvunjaji haki kama kushiriki kwenye matukio ya ubakaji na utesaji wa raia.  Ann-Marie Orler,amewaambia waandishi wa habari kuwa askari wa kulinda amani ambao wanatumbikia kwenye matukio hayo lazima [...]

22/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama launga mkono mageuzi ya kisiasa yatakayoongozwa na Syria

Kusikiliza / Mark Lyall Grant

Baraza la usalama limetoa ujumbe ambao unaweza kutafsiriwa kama imara na wa pamoja kwa serikali ya Syria kuwezesha kukabiliana kwa haraka na mzozo unaoikumba nchi hiyo. Baraza hilo jumanne lilikumbatia taarifa kwa pamoja inayounga mkono pointi 6 za mwongozo uliotolewa na Kofi Annan na tume maalum ya Umoja wa Mataifa na kamati maalum ya kiaarabu [...]

21/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kobler alaani mashambulizi ya mabomu Iraq

Kusikiliza / Martin Kobler

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amelaani vikali misururu ya mashambulizi kwenye miji kadha nchini Iraq ambapo watu kadha waliuawa na wengine kujeruhiwa. Martin Kobla amesema kuwa uhalifu unaotendwa kwa watu wa Iraq hautaruhusiwa ambapo amewataka wananchi wa Iraq kuwa macho na kukataa majaribio ya kuvuruga taifa lao na kuutaka utawala wa nchi hiyo [...]

21/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waonya kuhusu uhusiano baina ya ubaguzi wa rangi na migogoro

Kusikiliza / Ubaguzi wa rangi

Maafisa wa ngazi ya juu wameonya kuhusu hatari ya uhsiano baina ya ubaguzi wa rangi na vita, wakiitaka jumuiya ya kimataifa kushughulikia dalili za hali hiyo kabla haijawa janga kubwa la mgogoro. Katika ujumbe wake kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ubaguzi wa [...]

21/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani vikali mashambulizi kwenye shule ya Kiyahudi Ufaransa

Kusikiliza / Katibu mkuu, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali matukio ya ufyatuaji risasi katika shule ya wayahudi Mjini Toulouse nchini Ufaransa ambako watu wanne walipoteza maisha ikiwemo watoto watatu. Pamoja na kutuma salamu za rambi rambi kwa ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huo, Ban amelishutumu shambulizi hilo akisema ni uharibifu wa hali ya [...]

21/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM yataka kuongeza ufadhili kwenye kukabiliana na majanga

Kusikiliza / Majanga

Kuna haja kubwa kwa makundi ya kihisani kutumia kwa kiwango kikubwa sehemu ya ufadhili wao kugharimia miradi itayopunguza maafa,  na wakati huo huo kuwafikia kwa wakati waathirika wa majanga. Kulingana na ripoti moja iliyozinduliwa leo ambayo imeangazia suala la kudhibiti majanga, makundi mengi ya watu walioathiriwa na majanga ya kimazingira hayajahudumiwa vya kutosha. Utafiti huo [...]

21/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Afghan iko kwenye njia sahihi kuelekea kipindi cha mpito:UM

Kusikiliza / Jan Kubis

Shabaya ya kuifanikisha Afghanistan kuingia kwenye kipindi cha mpito bado inaendelea kupewa zingatio la pekee na Umoja wa Mataifa umehaidi kuendelea kuweka msukumo wake, pamoja na hali ya mikwamo ya hapa na pale iliyojitokeza hivi karibuni. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jan Kubis amesema kuwa kuna hali ya utengamano inavyojidhihiri sasa na [...]

21/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza wananchi wa Guinea Bissau kwa kufanya uchaguzi kwa njia ya amani

Kusikiliza / Sherehe za baada ya uchaguzi, Guinea Bissau

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza wananchi wa Guinea Bissau  kwa kushiriki uchaguzi kwa njia ya amani uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki. Wagombea tisa akiwemo waziri mkuu wa zamani Carlos Gomes Junior na rais wa zamani Kumba Yala walishiriki kwenye uchaguzi huo uliondaliwa miezi miwili baada ya kifo cha rais Malam Bacai [...]

21/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto 200 wanakufa kila siku kwa ugonjwa wa kifua kikuu unaozuilika:WHO

Kusikiliza / Vifo vingi hutokana na ugonjwa wa kifua kikuu

 Ugonjwa wa kifua kikuu miongoni mwa watoto unasalia kuwa ni tatizo lililojificha kwa nchi nyingi ukiuwa zaidi ya watoto 70,000 kila mwaka limesema shirika la afya duniani WHO. Watoto wa chini ya umri wa miaka mitatu na wale wenye utapia mlo au kinga iliyodhoofishwa na virusi vya HIV na maradhi mengine wako katika hatari kubwa [...]

21/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa haki za binadamu ahofia ghasia na usalama wa raia Guatemala

Kusikiliza / Ramana ya Guatemala

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay anahofia hali ya kusambaa kwa ghasia na usalama mdogo kwa raia uliosababishwa na ongezeko la mitandao ya uhalifu wa kupangwa, amesema naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu Kyung-wha Kang akitoa ripoti ya taifa hilo kwenye baraza la haki za binadamu Jumatano. Bi Kang amesema watetezi wa [...]

21/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO na EBRD kuimarisha ushirikiano katika kanda ya Mediteranian

Kusikiliza / FAO na EBRD kuimarisha biashara ya kilmo

Shirika la chakula na kilimo FAO na Bank ya ujenzi na maendeleo ya Ulaya EBRD wanaongeza juhudi kuchagiza sekta binafsi kuwekeza katika biashara ya kilimo kwenye kanda za kusini na Mashariki mwa Mediteranian. Mfululizo wa msaada wa miradi mpya ya kiufundi utachangia kuanzishwa kwa sera  na mfumo wa kisheria ambao utatoa mazingira mazuri ya uwekezaji [...]

21/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushairi una nguvu ya kuonyesha ubunifu wa akili ya binadamu:UNESCO

Kusikiliza / Siku ya ushairi

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya ushairi ambayo kila mwaka hufanyika Machi 21, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limesema linatambua uwezo wa kipekee wa ushairi katika kuleta ubunifuu wa akili ya binadamu. Shirika hilo linasema maadhimisho ya siku hii yanatoa fursa ya kuwaenzi wanawake na wanaume ambao wanajitahidi kuifanya [...]

21/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yazindua ahadi kumi kwa vijana

Kusikiliza / UNRWA

Mkutano wa kimataifa wa siku mbili wenye kichwa "Kuwashirikisha Vijana: Wakimbizi wa Kipalestina katika kuibadilisha mashariki ya kati" ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA umekamilika hii leo mjini Brussels  ambapo kamishina mkuu wa URWA  Filipo Grandi amezindua ahadi kumi kwa vijana kwa niaba ya UNRWA. Mkutano huo ulihudhuriwa [...]

21/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM imeanza kuwasafirisha kwa ndege raia wa Sudan kusini kutoka khartoum

Kusikiliza / IOM yaandikisha wanaosafirishwa kwa ndege

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza Jumatano Machi 21 kuwasafirisha kwa ndege kundi la watu 2200 raia wa Sudan Kusini ambao ni pamoja na wazee, walemavu, wasiojiweza, ndugu wa familia wanaowasindikiza pamoja na wafanyakazi wa afya wa IOM kutoka Khartom kuelekea Wau, Juba na Aweil Sudan Kusini. Operesheni hiyo itakayojumuisha ndege ndogo 50 katika [...]

21/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifo vya raia vimeongezeka kwa mwaka wa tano mfululizo Afghanistan:UNAMA

Kusikiliza / Jan Kubis

Mwaka 2011 umekuwa ni mwaka wa tano mfululizo ambapo vifo vya raia vinaongezeka kutokana na vita nchini Afghanistan, umesema mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo UNAMA katika ripoti yake ya mwaka inayohusu kuwalinda raia kwenye vita vya silaha.  Ripoti hiyo iliyotolewa kwa ushirikiano na ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu inasema mabadiliko [...]

21/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuzuia ghasia kabla hazijatokea ndio ngao ya UM:Ban

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuzuia ndio hisa za Umoja wa Mataifa katika biashara na ndio mwongozo katika miaka ijayo. Ban ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa na usalama wa kimataifa, ushirikiano na ubia unaofanyika mjini Jakarta Indonesia, ukijadili ulinzi wa kimataifa. Ban amesema wakati wa [...]

21/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na washirika wawahamisha raia wa Mali walioko Niger

Kusikiliza / Wakimbizi wa Mali

Shirika la kimataifa  la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na serikali ya Niger pamoja na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR wamewahamisha zaidi ya familia 500 kutoka Mali zilizokuwa zikiishi kwenye makao duni ndani na nje ya kijiji kilicho kusini magharibi cha Sinegodar. Karibu watu 28,000 wakiwemo raia 4,500 wa Mali wamevuka mpaka [...]

20/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNECE kufanya utafiti wa kimazingira nchini Morocco

Kusikiliza / Utafiti wa kimazingira, Morocco

Kupitia ombi la serikali ya Morocco tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kuhusu Ulaya UNECE inatarajiwa kufanya utafiti wa kimazingira nchini humo. Shughuli hiyo inapangwa kufanywa mwezi Septemba mwaka 2012 huku utafiti huo ukitarajiwa kukamilika mapema mwaka 2013. Utafiti huo utafanywa kwenye nyanja 14 tofauti zilizo muhimu kwa taifa la morocco yakiwemo kwenye masuala [...]

20/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kofia ya Samawati ni ishara ya amani:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon pamoja na rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa kofia ya Samawati ni ishara ya matumaini. Akitoa hotuba kuhusu changamoto za kulinda amani nchini Indonesia Ban amesema kuwa  ameajionea jinsi walinda amani wanavyoleta mabadiliko kwa maisha ya watu. Ban amesema kuwa wakati kuna mizozo wanafunzi  hukosa kwenda shuleni  hadi wakati walinda amani wa [...]

20/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Takwimu zatajwa kuwa muhimu katika kukabiliana na njaa:FAO

Kusikiliza / Ripoti ya FAO, 2012

Ufuatiliaji wa takwimu zinazohusiana na chakula pamoja na kilimo ni njia muhimu katika jitihada za kupunguza njaa na katika maendeleo. Hii ni kulingana na kitabu cha takwimu cha kila mwaka cha shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO. Kitabu hicho kimefanya mkusanyiko wa  takwimu kuhusu chakula na kilimo na masuala mengine yakiwemo ya [...]

20/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ubaguzi unachochea ghasia:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Utafiti mmoja unaonyesha kwamba machafuko mengi  yaliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni yamechagizwa vikubwa na hali ya ubaguzi wa rangi. Utafiti huo unasema kwamba wakati  wa machafuko hayo makundi ya watu wachache hasa wahamiaji ndiyo yanayoathiriwa zaidi. Kwa mfano utafiti huo umetaja machafuko yaliyotokea mwaka 2007 na 2009 kuwa ni kielelezo sahihi kinachoeleza namna haki [...]

20/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM na benki ya ADB kuzisaidia nchi zilizokumbwa na mapigano

Kusikiliza / Eugene Richard

Kamishna wa UM juu ya ujenzi wa amani kwa kushirikianan na benki ya maendeleo ya Afrika ADB zimeanza kutupia macho maeneo ambayo yalikumbwa na machafuko ya vita barani Afrika. Balozi Eugène-Richard Gasana ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa bodi amesema kwamba pande zote mbili zinaimarisha mikakati ya namna ya kuzisaidia nchi zilizopitia katika mizozo. Pande [...]

20/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa maji Palestina kufuatia uvamizi wa chemichemi kutoka kwa walowezi:UM

Kusikiliza / Kisiwa karibu na kijiji cha Qaryut

Mamia kwa maelfu ya wapalestina wamekosa vyanzo vya upataji  maji  kufuatia uvamizi uliofanywa na walowezi wa Israel ambao wamehodhi vyanzo vyote vinavyotoa maji katika eneo la ukingo wa Gaza. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na UM vyanzo vingi vya maji sasa vinashikiliwa na wahamiaji wa Israel, na idadi chache ya vyanzo hivyo vipo kwa wapalestina. [...]

20/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waelezea masikitiko yake kufuatia kujiuzulu kwa Jaji mwingine katika kesi ya mauwaji ya Cambodia

Kusikiliza / Mahakama, Cambodia

Umoja wa mataifa umeelezea masikitiko yake kufuatia kujiuzulu kwa jaji mmoja aliyekuwa akisikiliza kesi ya mauaji yaliyotokea  Cambodia na kufanya jumla ya jaji walioacha kazi kufikia wawili. Jaji Laurent Kasper-Ansermet amewasilisha barua yake ya kujiuzulu na kueleza kwamba uamuzi wake unaanza rasmi mei 4. Ametumikia mahakama hiyo kuanzia 2011 akichukua nafasi ya mtangulizi wake Siegfried [...]

20/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Suala la Syria limekuwa tatizo kubwa kwa jamii ya kimataifa:Ban

Kusikiliza / Katibu mkuu, Ban Ki-moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa hali nchini Syria kwa sasa imekuwa ya kutatiza na ni suala ambalo linaloisumbua jamii ya kimataifa. Ban aliyasema haya kwenye mkutano na waandishi wa habari alioufanya na rais wa Indonesia Susilo Bambang Yudhoyono. Ban amesema kuwa  hata kama watu wa Syria wamepitia magumu wamekuwa [...]

20/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zimepigwa katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi:Pillay

Kusikiliza / NAvi Pillay

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameliambia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa kugunduliwa kwa ugonjwa wa ukimwi miaka 30 iliyopita ni suala lililoushutua ulimwengu. Pillay anasema kuwa  watu walishikwa na hofu ya kuambukizwa maradhi hayo kwa kumguza mgonjwa au kwa kupumua hewa moja [...]

20/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muungano wa Ulaya na nchi za kiarabu zataka usaidizi zaidi kwa UNRWA

Kusikiliza / Tuwajumuishe vijana, UNRWA

Jamii ya kimataifa imeombwa kuwa kwenye mstari wa mbele katika kulisadia shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA. Ombi hili lilitolewa kwenye mkutano wa siku mbili wa UNRWA ulioandaliwa mjini Brussels ambapo  mwakilishi wa masuala ya kigeni na sera za usalama kwenye Muungano wa Ulaya amesema kuwa wametambua umuhimu wa  vijana wa [...]

20/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatoa misaada kwa wakimbizi wa Mali walioko eneo la Sahel

Kusikiliza / Msaada wawasili katika kambi ya Mbera, Mauritania

Shirika la  kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linatoa usaidizi kwa maelfu ya wakimbizi wa Mali wanaokimbia mapigano kati ya waasi wa Tuareg wa Mouvement National de Libération de l'Azawad  na wanajeshi wa Mali and  tangu mwezi Januari. Tani sitini za misaada ikiwemo blanketi, matandiko na vyombo vya jikoni  vinasafirishwa kutoka kwa ghala la [...]

20/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yashangazwa na mashambulizi ya mabomu mjini Mogadishu

Kusikiliza / Maeneo ya kambi

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasi wasi wake kutokana na mashambulizi ya mabomu ambayo yamewaua watu wanne siku za hivi majuzi mjini Mogadishi nchini Somalia. Mabomu yalianguka eneo wanakopiga kambi wakimbizi wa ndani kwenye wilaya ya Wardhigley mapema hiyo jana. Inaripotiwa kuwa hadi wakimbizi wanne wa ndani wakiwemo watoto waliuawa. [...]

20/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kulikuwa na ukiukaji wa haki za binadamu kwenye uchaguzi mkuu nchini DRC:UM

Kusikiliza / wakimbizi nchini DRC

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo imetolewa hii leo inaonyesha kuwa kumekuwa na ukiukaji wa haki za binadamu yakiwemo mauaji, kutoweka kwa watu na kufungwa vyote vilivyotekelezwa na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati wa kura za urais na ubunge mwaka uliopita. Ripoti hiyo inayotokana na uchunguzi uliofanywa na ofisi ya haki za [...]

20/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya Bahrain vinatumia nguvu kupita kiasi:UM

Kusikiliza / waandamanaji nchini Bahrain

  Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa imepokea ripoti za kutia wasi wasi zinazohusu matumizi ya nguvu kutoka kwa wanajeshi wa Bahrain hasa matumizi wa gesi ya kutoa machozi na risasi na mipira dhidi ya waandamanaji. Ripoti zinasema kuwa matumizi ya gesi ya kutoa machozi kumesababisha vifo vya waandamanaji kadha [...]

20/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Visiwa vya Solomon lazima vichukue hatua kumaliza ukatili dhidi ya wanawake:UM

Kusikiliza / Rashida Manjoo

Visiwa vya Solomon lazima vichukue hatua zaidi kuwalinda wanawake kutokana na ukatili na kutoa msaada kwa waathirika wa ubaguzi wa kijinsia na kunyimwa haki za kisheria, amesisitiza mtaalamu wa Umoja wa Mataifa baada ya kuzuru nchi hiyo. Rashida Manjoo, mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake, sababu zake na athari zake, [...]

19/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban akitaka Korea Kaskazini kutafakari upya uamuzi wa kuanzisha "satelite"

Kusikiliza / Ramani ya DPRK

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka Jamhuri ya watu wa Korea kutafakari upya mpango wake wa uzinduzi  matumizi ya Satelite, akisema kuwa hatua hiyo lazima izingatie maazimio yaliyopitishwa na baraza la usalama. Korea inakusudia kuzindua rasmi satelite mwezi ujao katika kile inachoeleza kuwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kiongozi [...]

19/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban aipongeza Timor-Leste kwa kuendesha uchaguzi kwa amani

Kusikiliza / Wapigaji kura, Timor-Leste

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza wananchi wa Timor-Leste kwa kuendesha uchaguzi katika mazingira ya amani hatua ambayo ameieleza kuwa ni kukaribisha machipuo mapya ya demokrasia. Wananchi hao mwishoni mwa wiki walimiminika kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi wa rais, uchaguzi ambao unatoa mustakabala mpya wa [...]

19/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP kuwasaidia wanawake na watoto wenye lishe dhaifu Senegal

Kusikiliza / Watoto, Senegal

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linaanza programu mpya ya kuwasaidia wanawake na watoto wenye lishe duni kwenye wilaya ya Cox's Bazaar nchini Senegal ambako takribani asilimia 20 ya watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wana afya dhaifu na lishe duni. Programu hiyo itatoa msaada wa lishe kwa watoto wa chini [...]

19/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ajali ya basi la UWISS lililoua watu 28 liko kwenye ajenda ya usalama barabarani ya UM

Kusikiliza / Eva Monlar

Barabara zinazochukuliwa kuwa ni salama mara nyingi zinaweza kuwacha madereva na mtazamo usio sahihi kuhusu usalama, limesema shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya usalama barabarani. Wiki hii jopo la wataalamu wa usalama barabarani litakutana mjini Geneva na ajali ya basi ya hivi karibuni kwenye tunnel nchini Uswiss iliyouwa watoto 22 na watu [...]

19/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwanamke wa kisomali akimbilia usalama kutokana na mapenzi yake kwa michezo

Kusikiliza / Maymun aonyesha ujuzi wake wa kucheza

Maymun Mahyadine alikuwa anapenda kucheza, kukimbia na pia kucheza kandanda kwenye mitaa ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo baadaye alipata kujishindia medali na kofia. Hata hivyo kundi la wanamgambo la Al Shabaab halikufurahishwa na tabia yake Muhyadine, lilisema kuwa  wanawake hawaruhusiwi kushiriki kwenye michezo ambapo lilimuonya akome na kuvaa hijab. Mwaka uliopita kundi la Al [...]

19/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP inasema itahakikisha msaada wa chakula unawafikia wenye njaa Somalia

Kusikiliza / Wasomali wasubiri kupokea chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema limejizatiti kuhakikisha kwamba msaada muhimu wa chakula unawafikia wenye njaa nchini Somalia. Kwa mjibu wa mkurugenzi mku wa WFP Josette Sheeran wanajua kwamba msaada wa chakula wanaoutoa unawafikia maelfu ya watu wenye njaa ambao wanategemea msaada huo mjini Moghadishu kila siku. Nchini Somalia watu zaidi ya milioni [...]

19/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amewapongeza watu wa Timor-Leste kwa kutekeleza demokrasia

Kusikiliza / Masanduku ya kupiga kura, Timor-Leste

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa Timor-Leste kwa kuonyesha nia ya kudumisha demokrasia na amani waliposhiriki kwenye uchaguzi mkuu wa Rais uliofanyika Jumamosi. Katika taarifa yake Ban amesema inatia moyo kuona uchaguzi umefanyika kwa mpango na mazingira ya utulivu. Ban ameupongeza uongozi wa kitaifa na hasa tume ya uchaguzi kwa [...]

19/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulizi ya mabomu nchini Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekashifu vikali mashambulizi ya mabomu yaliyotekelezwa kwenye mji mkuu wa Syria Damascus mwishoni mwa juma ambapo watu kadhaa waliuawa na wengi kujeruhiwa. Ban pia alituma rambi rambi zake kwa jamaa za waathiriwa na kwa watu wa Syria na kutaka kusitishwa kwa ghasia nchini humo. Ripoti za vyombo [...]

19/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yawarejesha nyumbani wasudan kusini zaidi ya 2300 kwa train

Kusikiliza / Wasudan kusini waelekea nyumbani

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM lilifanya mipango ya usafiri wa train iliyoondoka mji mkuu wa Sudan Khartoum siku 18 zilizopita ikiwa na Wasudan Kusini 2300 wakirejea nyumbani. Train hiyo imewasili salama Jumapili mjini Wau katika jimbo la west Bahr el Ghazal Sudan Kusini. Train hiyo ilikuwa ya kwanza kuondoka Khartom tangu Sudan na Sudan [...]

19/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna kufikia malengo ya kimataifa bila uwajibikaji Rio+20:UM

Kusikiliza / Rio+20

Kundi la wataalamu huru 22 wa haki za binadamu limeandika barua ya wazi likizitaka serikali kujumuisha mila, desturi na viwango vya kimataifa vilivyokubalika vya haki za binadamu pamoja na uwajibikaji wa hali ya juu katika malengo ya mkutano wa maendeleo endelevu wa Rio+20 katikia majadiliano yake ya kwanza yalioanza Jumatatu mjini New York. Wataalamu hao [...]

19/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maisha ya wapalestina yameimarika:Israel

Kusikiliza / Aharon-Leshno-Yaar

   Mwakilishi wa Israel kwenye baraza  la haki za binadamu mjini Geneva balozi Aharon Leshno Yaar amesema maisha ya Wapalestina yameimarika.  Akinukuu takiwmu za benki ya dunia balozi Yaar amesema zinaonyesha kuwa uchumi wa Palestina umekuwa kwa karibu asilimia 6 kwenye Ukingo wa Magharibi na zaidi ya asilimia 25 ukanda wa Gaza.  Amesema umri wa [...]

19/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waitaka Israel kusitisha matumizi ya silaha dhidi ya raia wa Palestina wasiojihami

Kusikiliza / Makazi Israel

Idadi kubwa ya raia wa Palestina ambao hawakuwa na silaha zozote wameuawa katika kipindi cha mwaka mmoja kwenye Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza katika mashambulizi yaliyo kinyume na sheria yaliofanywa na askari wa Israel katika vituo vya kijeshi vya ukaguzi imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu. Kamishina mkuu wa [...]

19/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Timor-Leste iko tayari kwa uchaguzi wa Rais

Kusikiliza / uchaguzi Timor-Leste

Watu wa Timor-Leste wako katika harakati za mwisho kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika Jumamosi hii. Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo (UNMIT) umekuwa ukisaidia masuala ya kiufundi ili wapiga kura zaidi ya 600,000 waweze kushiriki katika uchaguzi huo wa tatu tangu taifa hilo kujipatia uhuru muongo mmoja uliopita. Andres [...]

16/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuitembelea India

Kusikiliza / ramani ya India

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Christof Heyns anatarajiwa kuizuru India kuanzia tarehe 19 hadi 30 mwezi huu ziara ambayo itakuwa ya kwanza kufanywa nchini humo na mtaalamu huru aliyetumwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji ya kikatili nchini humo. Heyns anasema kuwa ziara hii itampa fursa nzuri ya [...]

16/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Annan ataka Baraza la Usalama kuwa na kauli moja dhidi ya Syria

Kusikiliza / Kofi Annan

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya Syria Kofi Annan amekuwa akitoa taarifa kwenye baraza la usalama, kuhusu safari yake ya kusaka amani ya taifa hilo hivi karibuni. Akizungumza mbele ya wandishi wa habari mjini Geneva leo Bwana Annan amesema amekuwa akilitaka baraza la usalama kuwa na kauli [...]

16/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM kuhusu masuala ya dhuluma dhidi ya wanawake kuitembelea Papua New Guinea

Kusikiliza / Komesha vita dhidi ya wanawake

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya dhuluma dhidi ya wanawake, kinachosabisha dhuluma hizo na athari zake Rashida Manjoo anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza nchini Papua New Guinea kati ya tarehe 18 na 26 mwezi huu. Manjoo amesema kuwa ataangazia dhuluma dhidi ya wanawake kwa upana wakati wa ziara yake, kinachosababisha dhuluma hizo [...]

16/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa UNECE waadhimisha miaka 20 tangu kutiwa sahihi

Kusikiliza / UNECE yaadhimisha miaka 20 ya makubaliano

Makubaliano ya tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa ya ulaya kuhusu utunzaji na matumizi ya maji na maziwa ya kimataifa UNECE yaliyoafikiwa mjini Helsinki Finland machi 17 mwaka 1992 hii leo yameadhimisha miaka 20 tangu yatiwe sahihi. Tangu kutiwa sahihi kwa makubaliano hayo bara la Ulaya limepiga hatua kubwa katika masuala ya ushirikiano kwenye [...]

16/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

CERF yatoa dola milioni za kufadhili miradi ya usafi nchini Haiti

Kusikiliza / Ufadhili wa miradi ya usafi, Haiti

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetoa dola milioni moja zitakazotumika katika kufadhili miradi ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ya maji na usafi ili kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya maji wakati unapoanza msimu wa mvua nchini Haiti. Karibu watu  nusu milioni maskini nchini Haiti hadi sasa wanaishi kwenye hema tangu [...]

16/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yakaribisha hatua ya Brazil ya kumfungulia mashtaka mwanajeshi wa zamani

Kusikiliza / Rupert Colville

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha uamuzi wa Brazil wa kumfungulia mashtaka mwanajeshi mmoja wa zamani kutokana na madai ya kutoweka kwa raia wakati wa utawala wa kijeshi nchini humo. Hii ndiyo mara ya kwanza Brazil inawachukulia hatua wale wanaoaminika kutenda uhalifu na ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa utawala [...]

16/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mengi yanahitaji kufanywa ili kukabiliana na ulanguzi wa madawa ya kulevya:Fedotov

Kusikiliza / Yury Fedotov

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayopambana na madawa ya kulevya na uhalifu Yuri  Fedotov amesema kuwa mataifa yanastahili kufanya jitihada  za  kukabilina na ulanguzi na mahitaji ya madawa ya kulevya. Fedotov anesema kuwa kuzuia, matibabu na kuwasaidia wanaotumia madawa hayo kuachana nayo ni kati ya masuala makuu yanayohitajika katika kupambana na matumzi ya [...]

16/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wanaokimbia mapigano nchini Mali yaongezeka: OCHA

Kusikiliza / Wakimbizi Mali

  Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao nchini Mali inazidi kuongezeka wakati hadi sasa watu 195,000 wakiwa wamehama ambao 100,000 kati yao wakiwa ni wakimbizi wa ndani na wengine 95,000 wakikimbilia Mauritania, Burkina Faso na Niger. OCHA inakadiria kuwa huenda watu 200,000 [...]

16/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watoto milioni 1.5 wako kwenye hatari ya kufa njaa kwenhye eneo la Sahel:UNICEF

Kusikiliza / Watoto kutoka eneo la Sahel

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto milioni 1.5 wako kwenye hatari ya kufa njaa kwenye eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika. UNICEF inasema kuwa mzozo uliopo pamoja na  ukame huenda vikawa na madhara makubwa kwa maisha ya watoto walio chini ya miaka mitano. Linasema kuwa lina mipango ya kuwalisha [...]

16/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awasilisha ripoti ya jopo la kuhusu udhabiti wa dunia

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amewasilisha ripoti ya jopo lake kuhusu udhabiti wa dunia yenye kichwa "Watu Imara, Sayari Imara: Siku za baadaye zilizo zenye maana". Lengo la jopo hilo ni kuangamiza umaskini na kupunguza ukosefu wa usawa ili kuchangia kuongezeka kwa uzalishaji na matumzi na pia kuzuia mabadiliko ya hali ya [...]

16/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaanzisha kampeni kuwalenga wahamiaji wasiokuwa wa kawaida katika eneo la Guatemela na Mexico

Kusikiliza / Wahamiaji wasio wa kawaida

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeanzisha  kampeni maalumu inayowalenga wahamiaji wasiokuwa wa kawaida wanakatisha mpaka kutoka Guatemala na kuingia Mexico. Kampeni hiyo inazingatia zaidi habari na taarifa, inafanyika kwa kauli mbiu isemayo " tembea salama: taarifa ndiyo kifurushi chako daima"  Serikali za Mexico, Guatemala, Ecuador pamoja na serikali za Amerika ya [...]

16/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ataka uchaguzi wa amani na huru Guinea-Bissau

Kusikiliza / Upigaji kura

Wakati wananchi wa Guinea Bissau wakielekea kwenye uchaguzi mkuu hapo siku ya jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kuwepo kwa hali ya amani na sura ya uwazi. Jumla ya wagombea 9 akiwemo pia waziri mkuu wa zamani Carlos Gomes Junior na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Kumba Yala wanachuana kwenye kinyang'anyiro [...]

16/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNCTAD yaishauri serikali ya Haiti kuanzisha sera mpya za uwekezaji

Kusikiliza / Uwekezaji nchini Haiti

Wataalamu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa UNCTAD wamemshauri rais wa Haiti pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu kuhusiana na uanzishwaji wa sera mpya ya uwekezaji nchini humo. Ama wataalamu hao wametaka pia nchi hiyo kuifanyia mapitio sera yake ya uwekezaji iliyoko sasa. Hatua hiyo inafuata baada ya wataalamu hao waliobobea kwenye uchumi [...]

16/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatimaye mahakama ya ICC yatoa hukumu yake ya kwanza

Kusikiliza / askari mtoto DRC

Jumatano wiki kwa mara ya kwanza mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC iliyoko The Hague Uholanzi imetoa hukumu yake ya kwanza kabisa tangu kuanzishwa na kuanza kushughulikia kesi za uhalifu wa vita. Mahakama hiyo imemkuta na hatia mbabe wa zamani wa kivita kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga. Lubanga alishitakiwa kwa [...]

16/03/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni mwaka mmoja tangu wimbi la mabadiliko ya kihistoria nchini Syria:Ban

Kusikiliza / maandamano nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema leo ni mwaka moja tangu wimbi la mabadiliko ya Kihistoria kuikumba nchi ya Syria, raia waliposimama katika mitaa ya Damascus na kukata rufaa kwa ajili ya haki zao na uhuru kwa wote. Baada ya siku chache maandamano ya amani yalianza mjini Deraa na kusambaa hadi maeneo [...]

15/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Katika kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku

Kusikiliza / uvutaji sigara

Takribani watu milioni 5 wenye umri wa miaka 30 na zaidi wamekufa kutokana na matumizi ya moja kwa moja ya tumbaku kote duniani, na hiyo ni sawa na kifo cha mtu mmoja kila baada ya sekunde sita. Kwa mujibu wa ripoti  ya WHO maeneo ambayo yana kiwango kikubwa cha vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku [...]

15/03/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM apongeza viongozi wapya Ivory Coast

Kusikiliza / Bert Koenders na walinda amani, UNOCI

Mkuu wa Umoja wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast Bert Koenders amempongeza waziri mkuu mpya na Rais wa bunge wa nchi hiyo waliochaguliwa hivi karibuni na kuwahakikishia kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa UNOCI utaendelea kuwasaidia. Jeannot Ahoussou Kouadio ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa taifa hilo huku bunge [...]

15/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahiga alaani shambulio la kujitoa muhanga Mogadishu

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga nchini Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga katika lango la Villa Somalia upande wa serikali ya mpito mjini Moghadishu Jumatano jioni. Mahiga ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na waliojeruhiwa kuwatakia nafuu ya haraka. Kwa mujibu wa mwakilishi huyo kundi la wanamgambo [...]

15/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Taka za elektroniki ni tatizo kubwa kwa nchi za Afrika:UNEP

Kusikiliza / Taka ya vifaa vya elektroniki

Wakati kukiendelea kushuhudiwa maendeleo katika Nyanja za tekinolojia duniani, nchi nyingi hasa zilizo barani Afrika zimeanza kushuhudia matatizo makubwa ya kuingizwa na kurundikana kwa taka za vyombo na vifaa vya kila aina vya elektronini. Hayo yamesemwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP na kuongeza kuwa endapo hali hiyo haitoshughulikiwa mapema huenda ikaleta [...]

15/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watoa mwongozo wa kuzuia ukwepaji ushuru

Kusikiliza / Wataalamu wa ushuru

Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba umetoa mwongozo mpya wa kuzuia ulipaji ushuru mara mbili kati ya nchi na pia katika kuzuia wanaokwepa kulipa ushuru suala ambalo linagharimu nchi dola trillion tatu kila mwaka. Mikataba ya ulipaji ushuru mara mbili ni makubaliano kati ya serikali ya kuzuia watu kulipa ushuru mara mbili kati ya nchi mbili. [...]

15/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maelfu watawanywa na mapigano Gedo, Somalia

Kusikiliza / Wananchi Gedo

  Taarifa kutoka Somalia zinasema maelfu ya watu wametawanya na mapigano yanayoendelea baina ya wanamgambo wa Al-Shabab na majeshi ya Somalia yanayosaidiwa na Ethiopia na wanajeshi wa Kenya katika jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia la Gedo. Kwa mujibu wa gavana wa Gedo Mohamed Adi Kalili katika wiki chache zilizopita watu 5000 zaidi wametawanywa na [...]

15/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanajeshi watatu wa kulinda amani wa UM wamerejeshwa nyumbani kutoka Haiti

Kusikiliza / kikosi cha MINUSTAH

Walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakihudumu nchini Haiti wamerejeshwa nyumbani kufuatia kesi iliyokuwa ikiwakabili wa inayohusiana na kulawitiwa kwa kijana mmoja wa kiume mwenye umri wa 14. Walinda amani hao kutoka Pakistan wanaohudumu kwenye kikosi cha polisi kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha MINUSTAH walikuwa wakihudumu kwenye mji ulio kaskazini mwa [...]

15/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Taka za elektroniki ni tatizo kubwa kwa nchi za Afrika:UNEP

Kusikiliza / taka barani Afrika

Huku kukiendelea kushuhudiwa maendeleo katika nyanja za kiteknolojia nchi nyingi hasa zilizo kwenye bara la Afrika zimeanza kushuhudia matatizo makubwa ya kuingizwa na kurundikana kwa taka ya vyombo vya kila aina vya elektroniki , Suala ambalo ikiwa halitashughulikiwa mapema huenda likawa lenye madhara makubwa kwa mazingira na pia kwa afya ya binadamu. Jason Nyakundi ana [...]

15/03/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waonya juu ya mienendo ya kulipiza kisasi kwa watetezi wa haki za binadamu

Kusikiliza / Haki za kibinadamu kwa wote

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa ameungana na washirika wa kikanda kuzitaka nchi kukomesha mienendo yao inayokwamisha jitihada za watu binafsi na makundi mengine yanayotaka kushirikiana na Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kutetea haki za binadamu.. Mtetezi huru wa haki za binadamu Margaret Sekaggya amesema kuwa vitendo vya ulipizaji kisasi na visa vingine [...]

15/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kiongozi muasi wa Rwanda ajisalimisha baada ya mashambulizi ya FARDC na MONUSCO

Kusikiliza / walinda amani MONUSCO

Kiongozi muasi wa ngazi ya juu kutoka Rwanda amejisalimisha wakati wa mashambulizi ya kijeshi ya pamoja yaliyofanywa na Mpango wa Umoja wa Mataifa MONUSCO na jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC. Kwa mujibu wa msemaji wa MONSUCO Manodje Mounoubai, Luteni Kanali Idrissa Muradadi anayejulikana kama "Big fish na walinzi wake watatu [...]

15/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan na Sudan Kusini zapongezwa kwa kujaribu kutatua mivutano:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezipongeza serikali za Sudan na Sudan Kusini kwa hatua walizopiga katika majadiliano kuhusu matatizo yaliyopo baada ya Sudan Kusini kujipatia uhuru wake. Ban amesema kuafikiana kuhusu hali ya uraia wa kila nchi na kuweka mipaka ni hatua muhimu ya kusonga mbele na ya kutia matumaini kwa pande [...]

15/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwendesha mashtaka wa ICC ataka Lubanga kufungwa maisha

Kusikiliza / Luis Moreno Ocampo

Mbabe wa zamani wa kivita kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga anakabiliwa na kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia Jumatano na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kwa kushiriki uhalifu wa kivita. Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo Luis Moreno-Ocampo amesema ataiomba mahakama kumfunga Lubanga miaka isiyopungua 30 ambayo ndio [...]

15/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Asilima 12 ya vifo vyote vya watu wazima duniani husababishwa na matumizi ya tumbaku:WHO

Kusikiliza / tumbaku

Asilimia 12 ya vifo vyote vya watu wazima duniani wa umri wa kuanzia miaka 30 na zaidi vinasababishwa na matumizi ya tumbaku imesema ripoti ya kimataifa ya shirika la afya duniani inayohusu vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku. Ripoti inasema mwaka 2004 takribani watu milioni 5 wenye umri wa miaka 30 na zaidi walikufa kutokana [...]

15/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yapongeza uamuzi wa ICC dhidi ya uhalifu wa kivita kwa watoto

Kusikiliza / Nemba ya UNICEF

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limepongeza uamuzi wa leo wa mahakama ya ICC kumkuta na hatia Thomas Lubanga ya uhalifu wa kivita kwa kwaingiza watoto katika jeshi lake nchini DR Congo. UNICEF inasema kuwa uamuzi wa leo Lubanga amekuwa mbabe wa kwanza wa kivita kukabiliana na mkono wa kimataifa wa sheria [...]

14/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uamuzi dhidi ya Lubanga ni hatua kubwa katika vita dhidi ya Ukatili:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay Jumatano amepongeza uamazi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC dhidi ya kesi ya bwana Thomas Lubanga, ambaye amekutwa na hatia ya kuwaingiza na kuwatumia watoto jeshini huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya mwaka 2002 na 2003. Bi Pillay [...]

14/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkutano kuhusu maswala ya uzazi kuandaliwa mjini London

Kusikiliza / Swala la kupanga uzazi

Serikali ya Uingereza, shirika la Bill na Melinda Gates, mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wengine wanatarajiwa kushiriki kwenye  warsha itakayoandaliwa mjini London mwezi Julai ambapo watajitolea  kufadhili mahitaji ya upangaji uzazi kwa wanawake kwenye nchi maskini duniani. Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa [...]

14/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mradi wa shirika la UNESCO waboresha makavazi barani Afrika

Kusikiliza / UNESCO yaboresha makavazi barani Afrika

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO  kwa ushirikiano na shule inayohusika na masula ya utamaduni nchini Benin wamewapa mafunzo watu 33 kutoka makavazi 30 kutoka nchi 17 jinsi ya kutunza makavazi yaliyo kwenye nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara. Programu hiyo inayofadhiliwa na shirika kutoka Japan inahusu mafunzo ya [...]

14/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM eneo la Sahara Magharibi kufanya ziara ya eneo hilo mwezi Mei

Kusikiliza / Christopher Ross

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Sahara Magharibi ametangaza kwamba atalitembelea eneo hilo hasa eneo lilalozozaniwa. Mjumbe huyo wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Sahara Magharibi Christopher Ross ameyasema hayo baada ya mazungumzo ya siku tatu akiongeza kuwa mikutano mingine itaandaliwa barani Ulaya mwezi Juni. Umoja wa mataifa umekuwa [...]

14/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwachilieni mwanamke wa kipalestina aliye katika mgomo wa kula:UM

Kusikiliza / Hamasisho ya kuachiliwa kwa Hana Shalabi

Mwakilishi maalumu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwa hali ya haki za binadamu kwenye himaya ya Palestina inayokaliwa tangu 1967 Richard Falk, ameelezea hofu yake kuhusu Hana Shalabi mwanamke wa Kipalestina anayeshikiliwa na Israel ambaye kwa sasa yuko kwenye mgomo wa kula kwa karibu mwezi mzima. Bwana Falk amesema hali ya Bi [...]

14/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na serikali kukutana katika mikakati ya kikanda dhidi ya LRA

Kusikiliza / Kundi la waasi, LRA

Umoja wa Mataifa na maafisa wa serikali kutoka Afrika ya Kati watakutana nchini Uganda wiki ijayo kukamilisha mkakati wa kikanda wa kukabiliana na kundi la waasi la Lord's Resistance Army LRA, kundi la waasi ambalo limepata sifa mbaya kwa uasi ilioutekeleza nchini Uganda na hivi karibuni kuendesha ghasia kwenye nchi za jirani. Mkutano huo utakaofanyika [...]

14/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa ya kiarabu yanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji

Kusikiliza / Changamoto ya maji katika nchi za kiarabu

Mataifa ya kiarabu sasa yametumbukia kwenye mkwamo wa ukosefu wa maji kutokana na ongezeko la kasi la watu na kuwepo kwa ongezeko la mahitaji ya chakula. Pia kumetajwa mambo mengine ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, matukio yanayokwenda sambamba na mabadiliko ya hali ya hewa na kuharibiwa kwa mara kwa mara kwa miundo mbinu inayosambaza maji, [...]

14/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAIDS, UNDP waipongeza New Zealand kutokana na mbuni zake za kukabili maambukizi ya HIV

Kusikiliza / UNDP, UNAIDS yameipongeza New Zealand

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameipongeza New Zealand kutokana na ilivyochukua mkondo sahihi kushughulikia tatizo la mambukizi ya virusi vya HIV. Wakurugenzi watendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS, na lile la maendeleo UNDP wamesema kuwa serikali ya New Zealand imechukua mkondo wa kuridhisha hasa kutokana na hatua yake ya kutoa kipaumbele [...]

14/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatua kali na sera dhaifu zinaathiri ufufuaji wa uchumi

Kusikiliza / Jomo Kwame Sundaram

Hatua kali, sera dhaifu na ukosefu wa ajira vimeelezewa kutia dosari juhudi za kupunguza umasikini na kufufua uchumi uliokumbwa na mdororo mkubwa na kuchagiza maendeleo endelevu yanayojali mazingira. Hayo yameelezwa wakati wa kuhitimisha mkutano wa kimataifa wa baraza la chumi na jamii ECOSOC uliojumuisha taasisi za uchumi na biashara. Jomo Kwame Sundaram katibu mkuu msaidizi [...]

14/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Utafiti wa usalama wa chakula kuonyesha hali mbaya ya njaa Yemen

Kusikiliza / Upungufu na bei ya juu ya chakula, Yemen

Upungufu wa chakula nchini Yemen umefikia kiwango cha hatari huku watu takribani milioni tano hawawezi kuzalisha au kununua chakula wanachokihitaji. Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya awali ya utafiti uliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiano na kitengo cha taifa cha takwimu cha Yemen na shirika [...]

14/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Syria yampa Annan majibu yaliyomuacha na maswali zaidi

Kusikiliza / Kofi Annan

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu Kofi Annan aliyezuru Syria hivi karibuni amepokea majibu ya mapendekezo yake kwa uongozi wa Syria ya jinsi ya kumaliza machafuko yanayoendelea. Kwa mujibu wa duru za habari za Umoja wa Mataifa majibu hayo yamekabidhiwa kwa Bwana Annan Jumanne jioni na yamemwacha mwakilishi huyo [...]

14/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Coomaraswamy akaribisha hukumu ya kwanza ya ICC dhidi ya kuingiza watoto jeshini

Kusikiliza / Watoto hawapaswi kutumika wakati wa vita

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye migogoro ya silaha Bi Radhika Coomaraswamy amesema leo ukwepaji sheria umefikia tamati kwa mbabe wa kivita Thoams Lubanga na wote wanaoingiza na kutumia watoto jeshini. Bi Coomaraswamy amepongeza hukumu hiyo ya kwanza kabisa ya mahakama ya ICC na kusema huu ni wakati wa mawasiliano ya [...]

14/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya ICC yamkuta na hatia Thomas Lubanga wa DR Congo

Kusikiliza / Thomas Lubanga

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imemkuta na hatia ya uhalifu wa vita bwana Thomas Lubanga. Miongoni mwa makosa yaliyomtia hatiani Lubanga mbabe wa zamani wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni kuwaingiza watoto jeshini ili kushiriki mauaji na mashambulizi kwenye jimbo la Itri Mashariki mwa nchi hiyo. Majaji wanasema alipokuwa mkuu wa [...]

14/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatima ya Thomas Lubanga kujulikana jumatano machi14

Kusikiliza / Thomas Lubanga

Uamuzi wa ama kuwa na hatia au kutokutwa na hatia dhidi ya kesi ya mpiganaji wa zamani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga Dyilo kutolewa Jumatano na majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Mahakama hiyo itatoa uamuzi kwa kuzingatia misingi ya mkataba wa Roma mapema asubuhi mjini Hague katika hukumu itakayotolewa [...]

13/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa fedha watishia oparesheni ya kuhamisha wahamiaji Yemen

Kusikiliza / Wahamiaji kutoka Ethiopia

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM mwezi huu linatarajiwa kuongoza oparesheni ya mwisho ya kusafirisha wahamiaji 277 wa Ethiopia waliokwama nchini Yemen ikiwa ufadhili mpya hautatolewa. Hadi sasa IOM imesaidia zaidi ya wahamiaji 6000 raia wa Ethiopia kurejea nyumbani kutoka mji wa Haradh ulio karibu na mpaka ambao umekuwa ukitumiwa na wahamiaji  kama kituo cha [...]

13/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WMO yaelezea sababu ya kipindi chenye baridi kali zaidi barani Ulaya

Kusikiliza / Msimu wa baridi kali, Ulaya

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO limetoa sababu iliyopelekea kushuhudiwa viwango vya chini zaidi vya baridi mwezi Januari mwaka huu barani Ulaya. Ripoti hiyo inaeleza kwamba hali mbaya ya hewa iliyotokea ilizuia hewa za baharini kupita ulaya zikielekea mashariki hali ambayo si ya kawaida kaskazini mwa dunia wakati wa kipindi cha msimu [...]

13/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yahofia hatma ya watoto waliokumbwa na ghasia Gaza na Israel

Kusikiliza / watoto kwenye kanda ya Gaza na Israel

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeelezea hofu yake kuhusu hatma ya watoto kufuatia ghasia za hivi majuzi kwenye Ukanda wa Gaza na nchini Israel. Jana Jumatatu kijana wa Kipalestina wa umri wa miaka 15 aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa kufuatia mlipiko uliotokea kwenye ukanda wa Gaza. Hadi sasa watoto 14 wa [...]

13/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada mpya zinahitajika kumhakikishia kila mmoja maji safi

Kusikiliza / Maji safi kwa wote

Dunia imetimiza lengo la maendeleo ya milenia la kupunguza kwa nusu idadi ya watu wasio na maji safi ya kunywa. Njia za kuhakikisha kuwa kila moija amepata maji safi ni kati ya masuala yanayoangaziwa kwenye kongamano la sita kuhusu maji duniani linaloendelea mjini Marseille nchini Ufaransa na pia hatua zilizochukuliwa na serikali pamoja na mashirika [...]

13/03/2012 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Marekani yafadhili msaada kwa watoto wa Chad waliokwama kwenye mpaka na Nigeria

Kusikiliza / wakimbizi wa Chad

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM lina mipango ya kutuma msafara unaosafirisha misaada kwa zaidi ya wahamiaji 1000 wengine wakiwa ni watoto wasio na wazazi waliokwama kwenye kijiji cha N'Gbouboua eneo la Lac Magharibi mwa Chad. Ubalozi wa Marekani nchini Chad umekubali kufadhili usafirishaji pamoja na shughuli ya kuziunganisha familia. Pesa hizo pia zitaliwezesha shirika [...]

13/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuituma timu ya wachunguzi wa haki za binadamu kwenye mipaka ya Syria

Kusikiliza / baraza la haki za binadamu

Umoja wa Mataifa utatuma timu ya waangalizi wa haki za binadamu katika nchi zinazopakana na Syria ili kukusanya taarifa za uhalifu na ukikwaji wa haki za binadamu unaotekelezwa nchini Syria. Naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Kyung-wha Kang amesema waangalizi hao watapelekwa baadaye wiki hii. Ameongeza kuwa vyunzo vingi vinavyotoa [...]

13/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNHCR yamteua mratibu wake mpya nchini Syria

Kusikiliza / Wakimbizi kufuatia mzozo ulioko Syria

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limemteua Panos Moumtzis kama mratibu wao wa masuala ya wakimbizi kwa wakimbizi wa Syria. UNHCR inasema kwamba karibu wakimbizi 30,000 kutoka Syria wamekimbilia nchi majirani zikiwemo Jordan, Lebanon na Uturuki. Shirika la mwezi mwekundu nchini Syria linakadiria kuwa karibu watu 200,000 nchini Syria wamelazimishwa kuwa wakimbizi [...]

13/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Annan asema anatarajia kupata jibu kutoka Syria hii leo

Kusikiliza / Kofi Annan

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za kiarabu nchini Syria Kofi Annan anasema kuwa anatarajia kupata majibu kutoka kwa serikali ya Syria kutoka na mapendekezo aliyowasilisha kwao. Akiongea mjini Ankara baada ya kukutana na waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan Annan amesema kuwa mara atakapopokea jibu lao ndipo atakapofanya uamuzi wake. Hata [...]

13/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya watu wa kabila la Lou Nuer wakimbilia Ethiopia

Kusikiliza / Wakimbizi, Sudan

Maelfu ya watu kutoka kabila la Lou Nuer kutoka Sudan Kusini wanatafuta hifadhi Magharibi mwa Ethiopia wengi wakiwa ni wanawake, watoto na watu wazee wanaokimbia kaunti ya Akobo iliyo kwenye mkoa wa Jonglei kufuatia mapigano yaliyoshuhudiwa mapema mwaka huu. Takriban watu 15,000 wameingia nchini Ethiopia tangu mwezi Februari. Wengi wanaokimbia wanahofia njama za kulipiza kisasi [...]

13/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muafaka waafikiwa kuhusu umiliki wa ardhi na fursa za uvuvi na misitu:FAO

Kusikiliza / Ardhi

Mazungumzo ya kimataifa yaliyofanyika kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo FAO wiki iliyopita ili kukamilisha majadiliano ya mapendekezo ya muongozo wa kimataifa kuhusu kudhibiti umiliki wa ardhi na fursa za haki ya kuwa na ardhi, uvuvi na rasilimali ya misitu yamemalizika kwa mafanikio. Muuongozo uliopendekezwa sasa uko tayari kufikiriwa kwa idhini ya [...]

13/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha hatua ya Fiji kujiandaa kuandika katiba

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha uamuzi uliotangazwa na serikali ya Fiji, ambayo inakusudia kuanzisha mchakato wa kuandika katiba, akisema kuwa  mwanga wa matumaini unaanza kuliangazia taifa hilo.  Ban amesifu tangazo hilo la serikali na kuongeza kuwa ni muhimu kwa wananchi wa eneo hilo wakapata fursa ya kushirikishwa na kutoa maoni yao. [...]

13/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu ajadili umuhimu wa UM akiwa kwenye bunge la Ulaya

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz Al-nasser

Akiwa katika bunge la Umoja wa Ulaya, rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser ametaja vipaumbele vinavyozingatia na Umoja huo katika wakati ambapo hali jumla ya dunia ikiwa kwenye mkwamo wa mambo.  Rais huyo amejadilia nafasi ya Umoja wa Mataifa katika kuzishughulikia changamoto na mikwamo inayoendelea kuiandama dunia kwa wakati huu [...]

13/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais wa ECOSOC ataka nchi kuwa na maingiliano ya sera za uchumi

Kusikiliza / Balozi Milos Koterec

Rais wa baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya uchumi na jamii ECOSOC amezitolea mwito nchi mbalimbali duniani kutekeleza kwa vitendo sera zitakazosaidia kustawisha kwa hali ya uchumi. Miloš Koterec, amesema dunia inapaswa kuwa na shabaha moja ya kusukuma mbele uchumi wake na inaweza kufaulu kufanya vyema kama kutakuwa na utashi wa pamoja na [...]

13/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNMISS yalaani mashambulizi kwenye kambi ya Lou Nuer

Kusikiliza / Hilde Johnson

  Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umepokea taarifa zinazoashiria kwamba mashambulizi yamefanyika na watu wasiojulikana dhidi ya makambi kadhaa ya Ng'ome Lou Nuer kwenye maeneo ya karibu na mpaka wa Sudan Kusini na Ethiopia. UNMISS imetuma timu ya kushika doria na wauguzi kwenye maeneo ya Akobo na Wanding ili kutanabahi mazingira [...]

13/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM walaani mauaji ya raia Afghanistan

Kusikiliza / Ramani ya Afghanistan

Umoja wa Mataifa umelaani vikali tukio la mauaji ya raia huko Kusini mwa Afghanistan na kutaka malaka husika kuchunguza mwenendo wa mauaji hayo. Duru za vyombo vya habari zimepasha kuwa, askari wa Kimarekani walioweka kambi katika jimbo la Kandahar ndiyo waliohusika na mauwaji hayo.  Askari hao wanadaiwa kuzishambulia nyumba kadhaa na kusababisha vifo vya watu [...]

13/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban amtaka rais wa Syria kuchukua hatua kumaliza ghasia

Kusikiliza / Ban kwenye baraza la usalama

Rais wa Syria Bashaar Al-Assad ametakiwa kuchukua hatua maramoja kukomesha ghasia, ukiukaji wa haki za binadamu na kushughulikia matatizo ya kibinadamu. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa moja wa Mataifa Ban Ki-moon Jumatatu wakati wa kikao cha baraza la usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati. Assad pia ametakiwa kuchukua hatua muafaka kufuatia mapendekezo [...]

12/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICJ yafungua kesi dhidi ya Rais wa zamani wa Chad Habre

Kusikiliza / Aliyekuwa rais wa Chad Hissene Habre

Mahakama ya Kimataifa ya haki  ICJ inasikiliza ombi la kumtaka rais wa zamani wa Chad Hissene Habre kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za uhalifu wa kivita zinazomkabili. Bw Habre, mwenye umri wa miaka 69, anatuhumiwa kwa mauaji na mateso kwa  maelfu ya wapinzani wake kati ya mwaka 1982 na 1990 tuhuma ambazo anazikanusha. Amekuwa akiishi uhamishoni [...]

12/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yaahidi kuwa na jeshi la serikali lisilohusisha watoto

Kusikiliza / Radhika Coomaraswamy

Kundi la Sudanese People's Liberation Army (SPLA) la Sudan Kusini leo limetia saini makubaliano na Umoja wa Mataifa yaitwayo "mpango wa hatua" wakirejea nia yao ya kuwaachilia watoto wote katika jeshi lao. Mpango huu mpya wa hatua umesainia na wizara ya ulinzi, mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMISS, UNICEF na [...]

12/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waendelea kutoa misaada kwa waathiriwa wa poromoko la theluji Afghanistan

Kusikiliza / Watoto katika makazi ya muda, Kabul

Umoja wa Mataifa unafanya jitihada za kutoa misaada ya huduma za afya,  chakula na makao ya muda kwa watu walioathiriwa na maporomoko ya theluji yaliyokikumba kijiji cha Dispay  kwenye mkoa wa Badakshan kaskazini mwa Afghanistan juma lililopita ambapo watu 50 waliuawa. Mratibu wa huduma za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Michael keating anasema [...]

12/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM waendelea na jitihada za kuwalinda raia kutoka kwa kundi la LRA

Kusikiliza / Wakimbizi kufuatia mashambulizi ya LRA

Katibu kwenye masuala ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema kwamba vikosi vya Umoja wa Mataifa vimekuwa vikitoa huduma za kuwasindikiza wafanyibiashara kwenda sokoni pamoja na wale wanaohudhuria ibada kanisani.  Akielezea jukumu la Umoja wa Mataifa katika shughuli za kukabilina na kundi la Lord's Resistance Army LRA wakati wa mahojiano na kitengo [...]

12/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Quartet yapongeza juhudi za Jordan katika kusaka amani mashariki ya kati

Kusikiliza / Wakuu wa Quartet

Mpango wa kimataifa wa pande nne wenye lengo la kutafuta amani ya kudumu Mashariki ya Kati yaani Quartet unaojumuisha Umoja wa Mataifa, Urusi, Marekani na Muungano wa Ulaya, wamekutana Jumatatu kutathimini maendeleo yaliyopatikana tangu walipotoa taarifa yao Septemba mwaka 20011. Quartet inasema kimsingi bado inazingatia malengo waliyoyaweka katika taarifa yao ya mwaka jana na hivyo [...]

12/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya wafungwa 600 wamenyongwa Iran mwaka 2011

Kusikiliza / Ahmed Shaheed

Zaidi ya wafungwa 600 wamenyongwa nchini Iran mwaka 2011 amesema mtaalamu wa Umoja wa mataifa wa haki za binadamu. Ahmed Shaheed ambaye ni mwakilishi maalumu wa haki za binadamu nchini Iran amesema wafungwa hao wamenyongwa bila kupewa fursa zinazostahili za kisheria ikiwemo uwakilishi wa mawakili. Akihutubia baraza la haki za binadamuu mjini Geneva bwana Shaheed [...]

12/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Makahaba nchini Kenya wataka fursa ya huduma za kisheria na afya

Kusikiliza / Makahaba nchini Kenya

Wanaume na wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba nchini Kenya wameandamana mapema mwezi huu wakidai kuheshimiwa kwa haki zao. Zaidi ya wanaume na wanawake 150 wafanya biashara ya ukahaba wakiwa wamevalia vinyago usoni waliandamana katika mtaa wa Koinange jijini la Nairobi mtaa ambao ni maarufu kwa biashara ya ngono nchini humo na kuelekea kwenye ofisi ya [...]

12/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Upokonyaji silaha ni muhimu katika kumaliza machafuko Sudan kusini:Johnson

Kusikiliza / Hilde Johnson

Serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini Jumatatu imezindua mchakato wa kuwapokonya silaha raia kwenye jimbo la Jonglei. Kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa Sudan Kusini Hilde F.Johnson amesema kuenea kwa umiliki na matumizi ya silaha haramu katika jamii za Sudan Kusini ni tishio kubwa la amani na usalama wa taifa hilo na [...]

12/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya milioni 6 wanakabiliwa na uhaba wa chakula Niger

Kusikiliza / Uhaba wa chakula nchini NIger

Wadau wa masuala ya kibinadamu wanatiwa hofu na kutoweka kwa haraka kwa akiba ya chakula kwa familia nyingi nchini Niger na kuonya kwamba kutakuwa na matatizo makubwa ya chakula cha lishe endapo msaada wa haraka hautapelekwa. Kwa mujibu wa kitengo cha tahadhari ya mapema nchini humo SAP watu zaidi ya milioni 6 nchini Niger wanahitaji [...]

12/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majaji wapya wa mahakama ya ICC waapishwa

Kusikiliza / majaji wapya wa ICC

Majaji wapya watano waliochaguliwa hivi karibuni kwa ajili ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC wameapishwa. Majaji hao walichaguliwa mapema mwezi wa disemba mwaka jana waliapishwa mwishoni mwa wiki na kufuatiwa na tafrija fupi. Walioapishwa ni pamoja na Howard Morrison kutoka Uingereza, Anthony T. Carmona wa Trinidad and Tobago, Olga Herrera Carbuccia anayetoka Jamhuri ya [...]

12/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Annan amtaka rais wa Syria kukumbatia mabadiliko

Kusikiliza / Kofi Annan na Bashar Al-Assad

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya Syria Kofi Annan amehitimisha ziara yake nchini Syria baada ya kuwasilisha mapendekezo muhimu ambayo yatasaidia hali nchini Syria na pia kusaidia kuanzisha mchakato wenye lengo la kukomesha machafuko. Katika taarifa yake baada ya mkutano wa pili na Rais Bashar Al-Assad, [...]

12/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna haja ya kuboreshwa kwa huduma za kijamii Iraq-UM

Kusikiliza / Martin Kobler

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ametaka kuboreshwa kwa mazingira ya utoaji wa huduma za kijamii hasa kwa makundi ya wakimbizi wa ndani akisisitiza kuwa upatikanaji wa huduma hizo katika mazingira rafiki ni jambo linalopaswa kutekelezwa bila vikwazo vyovyote. Amesema kuwepo kwa huduma bora kwa jamii ya wakimbizi wa ndani walioko kwenye kambi [...]

12/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ongezeko la mahitaji na mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia raslimali ya maji

Kusikiliza / Maji

Ongezeko kubwa la mahitaji ya maji duniani linatishia malengo yote ya maendeleo, imeonya ripoti ya karibuni ya Umoja wa mataifa kuhusu maendeleo ya maji iitwayo "kudhibiti maji wakati wa hatari na shinikizo". Ripoti hiyo iliyozinduliwa Jumatatu mjini Marseille Ufaransa na mkurigenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina [...]

12/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kitendo cha kuwarejesha kwa nguvu waomba hifadhi kutoka DPRK kikome:UM

Kusikiliza / waandamanaji wa DPRK

Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kukomesha kitendo cha kuwarejesha kwa ngvu waomba hifadhi wanaoikimbia ukiukaji wa haki za binadamu kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK. Marzuki Darusman ambaye ni mtaalamu wa haki za binadamu DPRK amezitaka nchi majirani wa DPRK kuzingatia misingi ya kutoa [...]

12/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka mmoja baada ya tetemeko la ardhi na tsunami nchini Japan:Ban

09/03/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Sehemu zinazopokea madawa ya Ukimwi zashuhudia viwango vya chini vya maambukizi

Kusikiliza / Mwanaharakati abeba vibango

Watafiti kutoka kwa kituo cha afya na idadi ya watu kimetoa matokeo  yanayoonyesha  kuwa watu kwenye maeneo yanayopata madawa yanayopunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi hawako kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi hayo. Mkurugenzi wa shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la  Umoja wa Mataifa UNAIDS Paul De Lay anasema kuwa matokeo ya utafiti huo [...]

09/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Matokeo ya tume ya uchunguzi ya haki za binadamu nchini Libya

Kusikiliza / wananchi wa Libya washerehekea

Maelfu ya wafungwa nchini libya walinyongwa na kuteswa na wanajeshi wa libya waliokuwa waaminifu kwa rais wa zamani Muammar Qadhafi. Tume ya kimataifa kuhusu uchunguzi wa Libya imesema kuwa mauaji hayo yanalinganishwa na uhalifu wa kivita. Utafiti huo uliwasilishwa kwa tume ya Umoja Wamataifa inayohusika na haki za binadamu. Hakimu Phillippe Kirsch, mkuu wa tume hiyo [...]

09/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko kwenye sheria za maandamano ni tisho kwa haki za binadamu

Kusikiliza / Maina Kiai

Mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa Maina Kiai amekashifu baadhi ya mabadiliko yaliyopendekezwa kwenye sheria za maandamano mjini Geneva akiongeza kuwa huenda mabadiliko hayo yakakandamiza haki ya uhuru wa kukusanyika kwa amani na kujieleza. Sheria hizo zinaruhusu kutolewa faini ya takriban dola 110,000 kwa yeyote ambaye hajapewa ruhusa ya kuandamana au kwa yeyote ambaye aheshimu [...]

09/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO yaomba dola milioni 68.9 ili kukabiliana na hali kwenye eneo la Sahel

Kusikiliza / ukame eneo la Sahel

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa nchi zilizo kwenye eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika zinahitaji usaidizi wa dharura ili kuzuia hali ya uhaba wa chakula iliyo katika eneo hilo kuwa mbaya na kuziokoa jamii zinazotegemea mifugo na kilimo. FAO inatoa ombi la dola milioni 69.8 ili kutoa usaidizi [...]

09/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Japan yatoa dola milioni 26.7 kwa huduma za IOM mwaka 2012

Kusikiliza / Shirika la Uhamiaji lapokea ufadhili

Serikali ya Japan imetoa ahadi ya msaada wa dola milioni 26.7 wa kufadhili huduma za kibinadamu za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM zikiwemo za wahamiaji, jamii zinazowapa hifadhi wahamiaji waliorejea nyumbani, watu wanaosafirishwa kiharamu pamoja na wakimbizi wa ndani.  Miradi itakayofadhiliwa nchini Afghanistan, Ivory Coast, Djibouti, Ghana, Kenya, Rwanda, Somalia na Zimbabwe itasaidia mataifa [...]

09/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yazuru mji wa Baidoa nchini Somalia

Kusikiliza / Mgonjwa hospitalini Baidoa, Somalia

Shirika la afya duniani WHO limeutembelea mji wa Baidoa nchini Somalia ambapo ulitwaliwa na vikosi vya serikali ya Somalia hivi majuzi. WHO inatoa usaidizi kwa hospitali moja inayosimamiwa na shirika moja lisilokuwa la kiserikali la Italia ambapo imeweka vifaa vya upasuaji kwenye hospitali hiyo na kutoa mafunzo kwa wauguzi kuhusu huduma za dharura. Pia WHO [...]

09/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa ndani yaongezeka Yemen

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani, Yemen

Maelfu ya watu wanaendelea kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine nchini Yemen wakati kunapoendelea kushuhudiwa  mapigano ya kikabila kaskazini mwa nchi pamoja na mapigano mapya kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi kusini mwa nchi. Hali inaripotiwa kuwa mbaya kwenye eneo la Haradh lililo kaskazini mwa mji mkuu Sana'a ambapo mapigano yamesababisha kuhama [...]

09/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu 172,000 wamehama makwao nchini Mali:OCHA

Kusikiliza / wakimbizi wa Mali

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 172,000 wamehama makwao kutokana na mzozo unaondelea kaskazini mwa Mali. Watu 82,000 kwa sasa ni wakimbizi wa ndani huku wengine 90,000 wakikimbilia Mauritania na Burkina Faso. Kulingana na OCHA ni kuwa mfuko wa kutoa misaada ya dharura [...]

09/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna usalama wa nishati ya nyuklia:UM

Kusikiliza / Mwaka moja baada ya tetemeko, Japan

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema kuwa taifa la Japan limepiga hatua kubwa. Akiongea wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi nchini Japan katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa taifa la Japan limepiga hatua kubwa ya kuzoa na kutumia taka iliyotokana na [...]

09/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uganda yashuhudia wakimbizi wanaokimbia mapigano nchini DRC

Kusikiliza / wakimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kwamba zaidi ya watu 100,000 hadi sasa wamelazimika kuhama makwao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati mapigano kati ya makundi hasimu yaliyojihami yanapoendelea kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mapigano kati ya vikosi vya serikali na kundi la [...]

09/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 1.5 huenda wakahitaji msaada nchini Syria

Kusikiliza / Wakimbizi wa machafuko, Syria

Umoja wa Mataifa unajiandaa kutoa misaada kwa takriban watu milioni 1.5 nchini Syria walioathiriwa na ghasia zinazoendelea na mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo. Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA hata hivyo linasema kuwa idadi kamili ya waathiriwa wa machafuko hayo bado haijulikani huku  mashirika ya kutoa misaada yakishindwa kuyafikia [...]

09/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Syria ni ya kuhofisha:Amos

Kusikiliza / Valerie Amos

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valeria Amos amesema kuwa ameshtuka kutokana na aliyoyaona nchini Syria . Amos amesema kuwa karibu majengo yote yameharibiwa na hamna watu waliosalia akielezea wasi wasi wake kuhusu hatma ya watu waliolazimika kuhama mji wa Baba Amr. Amesema kwamba alikutana na waziri wa mambo ya kigeni wa [...]

09/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuzuru Sudan Kusini

Kusikiliza / Radhika Coomaraswamy

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu juu ya masuala ya watoto na maeneo yaliyokumbwa na mizozo anatazamiwa kuzuru Sudan Kusini. Radhika Coomaraswamy anatazamiwa kuwasili nchini humo March 11, na ataaendelea kusalia huko hadi March 17. Katika ziara yake hiyo pia atatembelea jimbo la Jonglei ambalo linaandamwa na machafuko ya kikabila mara kwa mara. Anatazamia kutupia macho [...]

09/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ripoti yafichua kuwepo kwa ongezeko la watoto wanaotumbukia kwenye mazingira hatarishi

Kusikiliza / Usalama wa watoto umo hatarini

Ripoti moja inasema kiwango cha watoto watumbukiao kwenye mazingira hatarishi kinazidi kuongezeka na hivyo kuendelea kuzusha kwa hali ya sintofahamu juu ya mustakabala wao. Ripoti hiyo inasema kuwa watoto wanaotengana na familia zao  ama kukosa mahusiano ya karibu, ndiyo wako hatarini zaidi kiasi cha kwamba kuleta wasiwasi wa kuongezeka kwa biashara ya uuzaji watoto na [...]

09/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Haiti inapaswa kumteua Waziri Mkuu haraka iwezekanavyo:UM

Kusikiliza / Mariano Fernandez

Haiti inapaswa kumteua Waziri Mkuu haraka iwezekanavyo ili kuepusha hali yoyote ya mkwamo inayoweza kujitokeza. Akizungumza mbele ya baraza la usalama, mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini humo Mariano Fernandez amesema kuwa taifa hilo haliwezi kusonga mbele katika hali ya amani na utulivu kama nafasi ya waziri mkuu itaendelea kuwa wazi. Waziri Mkuu wa Haiti Garry [...]

09/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kiu yangu ni kumkomboa mwanamke mwenzangu Burundi:Hafsa Mossi

Kusikiliza / Waziri Hafsa Mossi

Wakati ulimwengu wiki hii umeadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake hapo Machi 08 ikiambatana na kauli mbiu kuwawezesha wanawake wa vijijini. Burundi ni mojawapo wa mataifa ya Afrika ambayo yamepiga hatua kwa kuwapa kina mama nafasi kwenye ngazi mbalimbali ikiwemo mashirika, serikalini na taasisi  mbalimbali. Katiba ya nchi hiyo inasema kwa uchache uwakilishi wa akina [...]

09/03/2012 | Jamii: Makala za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Siku ya Wanawake duniani 2012:Michelle Bachelet

08/03/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mwanamke aliyejitolea kuwasaidia watoto wasichana na wanawake kwa jumla:Mukamabano

Kusikiliza / Marie Claudine Mukamabano

Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake duniani kuna wanawake mbali mbali wanaojitoa kusaidia wanawake wenzao na wasichana. Miongoni mwao ni Marie Claudine Mukamabano kutoka nchini Rwanda ambaye anaishi Marekani. Marie ameanzisha kituo cha kuwalea watoto yatima nchini Rwanda. Yeye ni manusura wa mauaji ya kimbari lakini pia ni mwanzilishi wa kituo cha kulea watoto kiitwacho [...]

08/03/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Yemen inapaswa kuendelea na mageuzi katika hali ya amani na utulivu:UM

Kusikiliza / Jamal Benomar

Taifa la Yemen ambalo hivi karibuni lilifaulu kuendesha uchaguzi wa rais katika mazingira huru na ya amani, linapaswa kuendelea kushikilia mkondo huo huo wa mageuzi salama na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizosalia kwa mustakabala wa watu wake. Yemen mapema mwezi uliopita, ilifanya uchaguzi ulioshuhudia mamia kwa maelfu ya wananchi wakimiminika kwenye vituo vya kupigia kura. Katika [...]

08/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yapokea msaada wa Helkopta toka Ukraine

Kusikiliza / MONUSCO yapokea helikopta kutoka Ukraine

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vinavyoendesha operesheni yake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, vimepokea helkopta moja toka kwa serikali ya Ukraine ambayo itasaidia kuimarisha shughuli zake kwenye eneo hilo. Msemaji wa vikosi hivyo pamoja na kusifia hatua hiyo pia ameongeza kuwa kutolewa kwa msaada huo kutawezesha kuboresha shughuli za utoaji huduma [...]

08/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake wako kwenye hali tete

Kusikiliza / Kamala Chandrakirana

Wakati ulimwengu hii leo ukiadhimisha siku ya wanawake, mwaka 2012 unachukua sura ya majuto na misukumisuko mikubwa inayowaandama wanawake hao. Akijadilia siku hii, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa Kamala Chandrakirana, amesema kuwa kuna mikwamo na hali ngumu inayoangukia mikononi mwa wanawake inayochagizwa na misuko suko kwenye maeneo ya siasa na uchumi. Mtaalamu huyo huru ambaye [...]

08/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Umuhimu wa kuwawezesha Wanawake Vijijini

Kusikiliza / Kuadhimisha Siku ya wanawake duniani

Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani ambayo ni kumuwezesha mwanamke wa kijijini, kwa mujibu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake UN Women mchango wa mwanamke wa kijiji umekwa haupewi zito unaostahili ndio maana kauli mbiu ya hiyo imetolewa mwaka huu kutoa msisitizo wa kuthamini na kuenzi juhudi [...]

08/03/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahiga ataka kuwe na usawa wa kijinsia na kuwajumuisha wanawake kwenye masuala muhimu

Kusikiliza / Augustine Mahiga

Siku ya kiamataifa ya wanawake ikiadhimishwa hii leo ofisi inayohusika na masuala ya kisiasa ya Umoja wa mataifa kuhusu Somalia UNPOS imeonyesha uzalendo wake kwa wanawake kote duniani hasa walio kwenye maeneo yanayokabiliwa na mizozo na kuunga mkono jitihada za wanawake za kuleta amani nchini Somalia, kwa wanawake walio ndani mwa Somalia na walio nje. [...]

08/03/2012 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Mikakati zaidi inahitajika kwa mabadiliko nchini Libya:UM

Kusikiliza / Ian Martin

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umelifahamisha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa unapanga kuweka mikakati wakati unapojaribu kutafuta mbinu  na wataaalamu wa kuhakikisha kuwa mabadiliko kwenye taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika  yanafanyika kwa njia ya kidemokrasia. Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa Umoja [...]

08/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNECE kushiriki vilivyo kwenye kongamano la sita la maji

Kusikiliza / Kongamano la sita la kimataifa la maji

Tume ya kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ulaya inatarajiwa kuchangia vilivyo kwenye majadiliano ya  kongamano la sita la kimataifa la maji ambalo linalotarajiwa kuandaliwa kati ya tarehe 12 – 17 mjini Maeseille nchini Ufaransa. Kongamano hilo ambalo ni kubwa zaidi la maji duniani linaandaliwa baada ya miaka mitatu na zaidi ya washika dau 25,000 kutoka [...]

08/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Navi Pillay kuzuru Guatemala kutathimini hali ya haki za binadamu

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay atakwenda nchini Guatemala Jumapili wiki hii kujadili na serikali na jumuiya za kijamii  masuala ya haki za binadamu . Wakati wa ziara yake Bi Pillay atakutana na Rais Otto Perez Molina, makamu wa rais  wa nchi hiyo, waziri wa mambo ya nje, waziri wa ulinzi na viongozi [...]

08/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kupanda mlima Kilimanjaro

Kusikiliza / kupanda mlima Kilimanjaro

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na makundi mengine ya kiharakati pamoja na serikali ya Tanzania umeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupanda mlima kulimanjaro kama ishara mojawapo ya kusuma mbele nafasi ya mwanamke huku ikipinga vitendo vya dhulma dhidi yao. Hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hilo, ambalo pia limewashirikisha vijana kutoka mataifa mbalimbali [...]

08/03/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mifumo ya chakula katika nchi zinazoendelea iko njia panda

Kusikiliza / Changamoto za chakula katika nchi zinazostawi

Mifumo ya chakula katika nchi zinazochipuka iko njia panda, mamilioni ya watu wametolewa kwenye umasikini uliokithiri lakini bado jamii zimebakizwa nyuma ameonya mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusuu haki ya chakula Olivier De Schutter. Akiwasilisha ripoti kuhusuu Uchina, Mexico na Afrika ya Kusini kwenye baraza la haki za binadamu amesema raia takribani milioni 19 [...]

08/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kitabu kipya cha WHO kinaonyesha njia za kulinda dawa

Kusikiliza / Dawa

Kitabu kipya kiitwacho "Tisho la usugu wa dawa na uchaguzi wa kuchukua hatua" kimezinduliwa Alhamisi na shirika la afya duniani WHO, ili kuonyesha mifano ya hatua za kuchukua ili kupunguza usugu wa dawa na kulinda uwezo wa dawa kutibu maradhi mengi ya kuambukiza. WHO inasema hatua zinazochukuliwa na serikali, vituo vya afya, makampuni ya dawa [...]

08/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hukumu ya kifo kwa watoto ni ukiukaji wa haki zao:Pillay

Kusikiliza / Watoto kufungwa

Watoto wa umri wa chini ya miaka 18 kuhukumiwa kifo, kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa msamaha na adhabu nyingine kubwa ni ukikaji wa haki za mtoto amesema kamishina mkuu wa haki za binadamu . Bi Navi Pillay amesema takribani nchi 90 duniani zimehalalisha adhabu ya viboko ikiwa ni pamoja na adhabu zingine kama [...]

08/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Annan ataka wahusika katika mgogoro wa Syria kukomesha machafuko

Kusikiliza / Kofi Annan

Mwakilishi maalumu wa Muungano wa nchi za Kiarabu na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Kofi Annan amesema anamtaka Rais wa Syria Bashar Al-Assad na wengine wanaohusika katika mgogoro wa nchi hiyo kusitisha vita na kutafuta suluhu ya kisiasa. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Cairo amesema atafanya kila linalowezekana kusisitiza na [...]

08/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

AU, UNiTE waadhimisha siku ya wanawake kwa kupanda mlima Kilimanjaro

Kusikiliza / Kumaliza vita dhidi ya wanawake

Umoja wa Mataifa kupitia mpango wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake UNiTE wakishirikiana na makundi mengine ya kupigania haki za wanawake, Muungano wa Afrika na serikali ya Tanzania wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupanda mlima Kilimanjaro. Hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hili kufanyika katika kuchagiza kupinga dhuluma dhidi ya wanawake na [...]

08/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwawezesha wanawake wa vijijini kuna umuhimu gani?

Kusikiliza / Mwanamke wa kijijini

Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani ni kumuwezesha mwanamke wa kijijini, kwa mujibu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake UN Women mchango wa mwanamke wa kijiji umekwa haupewi uzito unaostahili ndio maana kauli mbiu hiyo imetolewa mwaka huu kutoa msisitizo wa kuthamini na kuenzi juhudi za wanawake wa [...]

08/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwekeza kwa wanawake wa vijijini ni uwekezaji mwerevu : Ban

Kusikiliza / Siku ya Wanawake Duniani

  Leo ni siku ya kimataifa ya wanawake na kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwawezesha wanawake wa vijijini. Wanawake wa vijijini wanaweza kuboresha maisha ya jamii nzima endapo watapewa fursa ya kuwa na rasilimali na kutobaguliwa. Hiyo ni kauli iliyosemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika maadhimisho ya siku ya [...]

08/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM wa maswala dharura kuchunguza hasara Brazaville baada ya mlipuko

Kusikiliza / Mlipuko Brazaville, Congo

Wataalam wa majanga  wa Umoja wa Mataifa wametumwa kuchunguza kiwango cha uharibifu kufuatia mlipuko katika bohari la silaha jumapili. Ambapo watu 200 walipoteza maisha yao huku 1,500 zaidi wakijeruhiwa vibaya. Kiwango cha mlipuko huo bado haujabainika, lakini makaazi, majengo na miundo mbinu ya usafirishaji imeathirika. Msemaji msaidizi wa UM Eduardo del Buey amesema kwama wataalam [...]

07/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuwawezesha wanawake ili wawe wawakilishi dhidi ya umaskini na njaa

Kusikiliza / Marion Kamara

Wanawake wa vijijini wanatambuliwa katika UM kama kiungo muhimu kwa maendeleo endelevu na watakaowezesha vita dhidi ya umaskini na njaa. Katika tamaduni tofauti wanawake ndio hufanya kazi mashambani. Na wanjumuisha  asilimia 43 ya watenda kazi katika sekta ya kilimo kote duniani, Marion V. Kamara wa Liberia amewaambia haya wajumbe katika mazungumzo ya Kongamano la Umoja [...]

07/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dini kubwa kitisho kwa dini ndogo: Bielefeldt

Kusikiliza / Baadhi ya Dini za dunia

Mtaalamu mmoja wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba dini kubwa zimetajwa kuwa kitisho cha kuangamia kwa dini zingine ndogo na katika kuwatenga waumini wa dini zingine. Akiongea kwenye mkutano wa baraza la haki za binamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva ambapo aliwasilisha ripoti yake kuhusu uhuru wa dini na imani Heiner Bielefeldt amezitaka serikali [...]

07/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Somalia yaomba kuingia Afrika Mashariki:

Kusikiliza / Bendera za mataifa ya jumuiya ya Afrika mashariki

Somalia ambayo imekua ikijaribu kujikwamua toka vita vya miaka 20 imetuma maombi yakutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Kenya ambayo ndio mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo imethibitisha kupokea maombi ya Somalia. Taarifa kutoka serikali ya mpito ya Somalia inasema kuwa wameamua kujiunga na jumuiya hiyo kutokana na hali ya kiusalama nchini Somalia kuimarika [...]

07/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ataka vizingiti vinavyomkwaza mwanamke kiuchumi viondolewe

Kusikiliza / Ban ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuondolewa vizuizi na vikwazo vinavyowaandama wanawake duniani kutojitokeza kwenye masuala ya ukuzaji uchumi. Ametaja maeneo yanakwamisha wanawake wengi kutoshiriki kikamilifu kwenye masuala ya uchumi kuwa ni pamoja kukosa fursa za kuajiriwa, masoko, upatiaji mikopo pamoja na kukosa fursa ya kumiliki mali. Amesema mazingira kama [...]

07/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kundi la Al- Shabaab lavamia shule mjini Mogadishu

Kusikiliza / shule mjini Mogadishu

Ripoti kutoka eneo la Elasha Biyana lililo kwenye vitongoji vya mji wa Mogadishu ambayo ni ngome ya kundi la wanamgambo wa Al Shabaab zinasema kuwa wanamgambo hao walivamia shule kadhaa za msingi katika eneo hilo na kupora vifaa. Wanamgambo hao walivamia jumla ya shule tano zinazofadhaliwa na shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Umoja [...]

07/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu aipongeza Ubelgiji

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz

Rais wa baraza kuu ameipongeza Ubelgiji kutokana namna inavyokaribisha mafungamano ya kimataifa ikiwemo kuunga mkono kazi za Umoja wa Mataifa kwa njia ya kushiriki kwenye utanzuaji wa mizozo na inavyomulika hali ya mambo huko Mashariki ya Kati. Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema kuwa Ubelgiji ni mshirika muhimu wa Umoja wa Mataifa. Ameeleza hayo kwenye risala yake [...]

07/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake ni muhimu hasa wakati wa mizozo:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Mary Kini, Angela Apa na Agnes Sil wanatoka kwenye familia tatu hasimu kwenye maeneo ya milima ya Papua New Guinea. Awali wanawake hawa walikuwa wamezuizwa na sheria za makabila yao za kufanya mazungumzo kati yao lakini walikiuka sheria hizo kisisiri na kuhatarisha maisha yao ambapo walikuta sokoni na kujadili mipango ya amani na kisha kuwavutia [...]

07/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP na Marekani watafuta mbinu mpya kupambana na Utapia mlo jamhuri ya Lao

Kusikiliza / Wanawake katika mafundisho ya lishe bora, Luangnamtha, Lao

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP na ubalozi wa Marekani mjini Vientiane Lao wameungana na kuzuru jimbo la Luangnamtha kujionea mipango ya ubunifu ambayo inadhihirisha juhudi zao zinazoendelea za kuisaidia Jamhuri ya watu wa Lao na mikakati ya serikali kupambana na utapia mlo. Wakati wa ziara hiyo ya siku tatu mkurugenzi [...]

07/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nepal, Afrika Kusini na Venezuela kupokea tuzo ya elimu ya UM

Kusikiliza / Tuzo la UNESCO la Hamdan Bin Rashid Al-Maktoum

Taasisi tatu nchini Nepal, Afrika ya Kusini na Venezuela zitatambuliwa kwa mchango wake wa kysaidia na kuboresha utendaji wa waalimu katika nchi zinazoendelea limesema shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO. Nchini Nepal mfuko wa Rato Bangala wa shirika lisilo la kiserikali unatoa mpango wa mafunzo kwa waalimu wa shule za [...]

07/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yazindua mradi kuhusu wanawake wanaotengeneza habari 2012

Kusikiliza / Wanawake wa Afghan wakitengeza habari

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO kwa mara nyingine limetoa wito kwa wadau wa habari kuhakikisha kwamba usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake linasalia kuwa la juu katika ajenda zao kupitia mradi wake maalumu wa wanawake wanatengeneza habari 2012. au WMN Kwa mujibu wa UNESCO mradi huo unaozinduliwa kila mwaka [...]

07/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OIC yaliambia Baraza la Haki za Binadamu inapinga mjadala wa mapenzi ya jinsia moja

Kusikiliza / Nembo ya OIC

Na nchi wanachama wa shirika la shirikiano kwa nchi za Kiislam OIC wamesema wanataka kudhihirisha msiamamo wao wa kupinga mada inayojadiliwa katika kazi za baraza la haki za binadamu, mada ambayo ni kukomesha ghasia na ubaguzi dhidi ya wanaofanya mapenzi ya jinsia moja. Kwa niaba ya nchi wanachama wa OIC mwakilishi wa Pakistan kwenye baraza [...]

07/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuharamisha uhusiano wa kingono wa watu wa jinsia moja ni ukiukwaji wa haki za binadamu:Pillay

Kusikiliza / bendera ya watu wa jinsia moja

Takribani nchi 76 zinaendelea na sheria ambazo zinafanya kuwa kosa la jinai kushiriki mapenzi au kuwa na uuhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja. Au sheria ambazo zinazuia hali hiyo na hivyo kubagua na kuwachukulia hatua wanawake na wanauume wanaoshiriki ngono za jinsia moja, wanaoshirikia ngono za jinsia zote na watu waliobadilia jinsia. Kamishina mkuu wa [...]

07/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watoa wito wa kukomesha ghasia na ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

Kusikiliza / Arusi ya watu wa jinsia moja

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomesha ghasia na ubaguzi wa moja kwa moja dhidi ya mashoga, wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na watu waliobadili jinsia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ubaguzi kwa misingi ya mfumo wa kimapenzi na jinsia ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Akihutubia baraza la haki [...]

07/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakurugenzi karibu 400 kuzingatia misingi ya kuwawezesha wanawake

Kusikiliza / business

Wakurugenzi karibu 400 duniani kote wametangaza dhamira yao ya kutekeleza kanuni za Misingi ya kuwawezesha wanawake yaani Women's Empowerment Principles (WEPs) katika miaka miwili iliyopita, Kama vile Katibu Mkuu wa Umoja Ban Ki-moon na Mkurugenzi mtendaji wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake yaani UN Women Bi Michelle Bachelet watakavyoangazia katika mkutano [...]

06/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Njia tano za kukabiliana na matatizo ya afya ya jamii yatokanayo na vyakula visivyofaa

Kusikiliza / Oliver De Schutter

Mifumo ya chakula duniani inasababisha maradhi ameonya mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki ya chakula Olivier De Schutter. De Schutter amesema kila mtu mmoja kati ya saba duniani ana utapia mlo, lakini wengi zaidi wanakabiliwa na matatizo ya njaa ya kukosa vyakula bora, huku watu bilioni 1.3 wanasumbuliwa na matatizo ya kuwa [...]

06/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM kuhamisha watu wanaokimbia mapigano nchini Mali

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Mali

Kwa ushirikiano na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatarajiwa kuanzisha shughuli ya kuwahamisha karibu wakimbizi 5000 kutoka Mali na wengine kutoka Niger kutoka eneo waliopiga kambi kwa sasa la Chinegodar lililo kwenye mpaka kati ya Niger na Mali kwenda wilaya ya Ouallam nchini Niger. Watu [...]

06/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshindi wa tuzo la Grammy kuunga mkono juhudi za UNICEF

Kusikiliza / Lenny Kravitz

Mshindi wa tuzo la GRAMMY Lenny Kravitz anatazamia kuunga mkono juhudi zinazoendelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linalotoa mwito juu ya uboreshaji wa mazingira ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa makundi ya watoto duniani kote. Mshindi huyo ambaye anafahamika pia kwa kazi za utunzi wa nyimbo, uimbaji na [...]

06/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dunia kujadili mawasiliano ya teknolojia mjini Doha

Kusikiliza / Baadhi ya bendera za mataifa ya kiarabu

Wajumbe wakiwemo zaidi ya wawakilishi ishirini wanaowajumuisha marais na wakuu wa serikali, mawaziri 27 na wakuu wa makampuni makubwa zaidi kwenye masuala ya teknolojia ya mawasiliano duniani wanakutana juma hili mjini Doha kujadili mikakati na sera ambazo zitahakikisha kuwepo masoko na maendeleo kwenye eneo lote la nchi za kiarabu. Mkutano huo unaoandaliwa na taifa la [...]

06/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM washangazwa na picha za mateso kutoka nchini Syria

Kusikiliza / kunyanyaswa nchini Syria

  Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa imeshangazwa na picha za video kutoka nchini Syria zinazoonyesha wagonjwa walioteswa wanapoendelea kupata matibabu kwenye hospitali moja ya kijeshi.  Ofisi hiyo inasema kwamba ripoti kama hizo za kuteswa kwa wafungwa pia zimetoka kwa tume ya uchunguzi ya uchunguzi iliyoteuliwa kuchunguza hali nchini Syria. [...]

06/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaelezea hofu yake kufuatia uvamizi wa LRA nchini DRC

Kusikiliza / Waliokimbia vurugu kufuatia mashambulizi ya LRA

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea hofu yake baada ya kuhama kwa maelfu ya watu kufuatia mashambulizi mapya kutoka kwa waasi wa Lord's Resisitance Army LRA katika mkoa wa Orientale ulio kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Baada ya oparesheni za mwaka uliopita zilizopelekea kuimarika kwa usalama kwa watu walio kaskazini [...]

06/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nishati safi vijijini kupunguza uchafuzi wa hewa

Kusikiliza / Mfano wa aina ya nishati safi

Watu wanaoishi sehemu za vijijini kwenye nchi zinazoendelea hivi karibuni wataacha kutumia taa zinazotumia mafuta na mashine za kutumia mafuta aina ya Diesel na kuanza matumizi ya nishati safi kutokana na ufadhili unatokana na moja ya makubaliano ya mkutano wa Kyoto CDM. Miradi iliyoafikiwa kwenye mkutano huo inaweza kuwa na umuhimu wa kupunguza gesi zinazochafua [...]

06/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanadiplomasia wa kimataifa kuzuru Syria

Kusikiliza / Valerie Amos

Wanadiplomasia wa kimataifa wanatazamia kuizuru Syria ikiwa katika jitihada za kuitaka serikali ya nchi hiyo kukomesha mashambulizi na kuruhusu wafanyakazi wa kimataifa kupeleka misaada ya kiutu. Mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos katika ziara hiyo anatazamiwa kuambatana na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan aliyeteuliwa kusaka suluhu. Ujumbe [...]

06/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mapigano kwenye mapaka wa Sudan Kusini wasababisha kuhama kwa watu zaidi

Kusikiliza / wakimbizi wa Sudan Kusini

Mapigano mapya kwenye sehemu za mipaka zenye mizozo kati ya Sudan na Sudan Kusini yamesababisha watu zaidi kukimbilia usalama kwenye jimbo la Upper Nile lililo Sudan Kusini na pia maeneo ya magharibi mwa Ethiopia. Juma lililopita shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR liliandikisha watu 2,287 waliowasili kwenye kambi ya wakimbizi ya Jamman [...]

06/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo ya malengo ya Milenia ya kupatikana kwa maji yatimizwa

Kusikiliza / Mtoto akipampu maji

Ulimwengu umetimiza lengo la maendeleo ya milenia ya kupunguza kwa nusu idadi ya watu wasio na maji safi ya kunywa. Hii ni kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na lile la afya duniani WHO. Ripoti hiyo inaonyesha kwamba kwa muda wa miaka kumi iliyopita zaidi ya watu bilioni mbili [...]

06/03/2012 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Michelle Bachelet kwenda Morocco kuadhimisha siku ya wanawake duniani

Kusikiliza / Michelle Bachelet

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake Michelle Bachelet anatazamiwa kuelekea nchini Morocco ambako anaungana na wananwake wa eneo hilo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Akiwa nchini humo anatazamia kuweka zingatio kubwa juu ya wanawake kushiriki kwenye majukwaa ya maamuzi. Anatazamia kuongeza msukumo kuhusu nafasi ya wanawake kwenye majukwaa [...]

06/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Somalia bado iko hatarini: Ban Ki-moon

Kusikiliza / msikiti nchini Somalia

Ingawa hali ya kibimadamu imeboreshwa nchini Somalia, nchi hii ya Pembe ya Afrika bado iko hatarini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyasema haya  katika mjadala  wa Baraza la Usalama juu ya Somalia ambao umefanyika leo jumatatu. Bw. Ban amesema kumekuwa na maendeleo katika mchakato wa amani, akitoa mfano wa mikutano miwili iliyofanyika [...]

05/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miradi ya FAO inawasaidia watunga sera kuzisaidia jamii za vijijini kuzuia matatizo ya chakula

Kusikiliza / Mitambo ya kunasia miale ya jua

Shirika la chakula na kilimo FAO limetoa nyaraka za muongozo na nyenzo za watunga sera ambazo serikali zinaweza kutumia kusaidia jamii za vijijini kufaidika na maendeleo ya nishati mbadala na kuhakikisha kwamba uzalishaji wa mazao ya nishati ya mimea haufanyiki kwa gharama za kusababisha matatizo ya chakula.  Nyaraka hizo zilizotolewa Jumatatu na FAO ni pamoja [...]

05/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwanadiplomasia mkongwe wa Sweden kuwa naibu mkuu wa UM

Kusikiliza / Jan Eliasson

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza uteuzi wa Jan Eliasson wa Sweden mkongwe katika masuala ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa kuwa naibu Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa. Bwana Eliasson atachukua nafasi ya Asha Rose-Migiro kutoka Tanzania hapo Julai Mosi mwaka huu. Eliasson sio mtu mgeni kwenye Umoja wa mataifa, [...]

05/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UNEP wakamilisha tathmini ya tetemeko lililotokea Japan

Kusikiliza / Ziara ya Japan ya UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP limehitimisha ziara ya ujumbe wa wataalamu wa kimataifa katika maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi na tsunami nchini Japan mwaka 2011. Ziara hiyo ilijikita katika kuangalia jinsi taka zinavyodhibitiwa baada ya tetemeko. Ikiwa katika mkesha wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa tetemeko hilo UNEP inasema kumepigwa hatua [...]

05/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Congo Brazaville yaomba msaada wadharura wa kimataifa

Kusikiliza / wananchi wa Congo

Maaafisa wa serikali ya Jamhuri ya Congo wameomba msaada wa jumuiya ya kimataifa baada ya kutokea ajali ya mlipuko katika bohari la silaha na kukatili maisha ya watu takribani 150 na kujeruhi wengine 1500. Mlipuko huo ulitokea katika mji mkuu Brazzaville na makundi ya waokozi bado yanaendelea kuwatafuta manusura. Mlipuko huo pia umeathiri makazi na [...]

05/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maisha ya mtoto kutoka sehemu maskini mjini Nairobi kuangaziwa

Kusikiliza / Molly kutoka Nairobi, Kenya anayeshirikiana na WFP

Msichana moja wa umri wa miaka 13 pamoja na wenzake wanatarajiwa kuungana na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwenye mawasiliano kwa njia ya video ya moja kwa moja ambapo watazungumzia maisha yao kwenye vitongoji maskini vya mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Molly ameelezea kuhusu maisha yake ya kila siku kwenye mtaa maskini wa [...]

05/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa chai nchini Japan kuteuliwa balozi mwema wa shirika la UNESCO.

Kusikiliza / Sen Geshitsu

Shirika la elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limetangaza kuwa litamteua mtaalamu mmoja wa masusla ya chai Sen Genshitsu kama balozi wake mwema kutokana na mchango alioutoa kwenye masuala ya amani na utamaduni. UNESCO inamtambua bwana sen ambaye alizaliwa mwaka 1923 mjini Tokyo Japan kwa mchango wake kwa amani na utamaduni kupitia [...]

05/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Licha ya matatizo ya kiuchumi uandikishaji hati miliki umevunja rekodi 2011: WIPO

Kusikiliza / Nakala ya ripoti ya WIPO

Licha ya mazingira magumu ya kiuchumi uandikishaji wa kimataifa wa hati miliki umevunja rekodi mwaka 2011, ambapo kumekuwa na maombi 182,000 limesema shirika la kimataifa linalohusika na masuala ya hati milikI WIPO. Ongezeko hilo la maombi linawasilisha ukuaji wa asilimia 10 ikilinganishwa na maombi yaliyowasilishwa mwaka 2010. Mkurugenzi mkuu wa WIPO Francis Gurry anasema ongezeko [...]

05/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna ya uchunguzi pekee haiwezi kukomesha vitendo vya ukatili

Kusikiliza / Juan E. Méndez

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia  vitendo vya utesaji Juan E. Méndez, amesema kuwa kuwepo kwa kamishna ya kufuatilia vitendo vya uonevu na mateso ni chombo muhimu ambacho kinaweza kukabili kizingiti cha watu kotofikishwa kwenye mkono wa sheria. Amesema kuwa pamoja na kazi kubwa iliyoko mbele yake, lakini kamishna hiyo haiwezi kufaulu kukomesha vitendo vya watu [...]

05/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa IAEA atoa taarifa kuhusu Iran, DPRK na Syria

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu, IAEA Yukiya Amano

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA Yukiya Amano Jumatatu ameiambia bodi ya magavana wa shirika hilo kwamba IAEA ina jukumu kubwa katika kuthibitisha mipango ya nyuklia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK. Amesema shirika lake liko tayari kurejea Yonbyong kufuatilia shughuli za nyuklia itakapoombwa na kwa [...]

05/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

HRC yahofia sheria zinazokandamiza haki na kazi za waandishi habari:

Kusikiliza / Wanahabari

Mtaalamu wa haki za binadamu ameelezea hofu yake kuhusu kongezeka kwa serikali kutumia sheria za kuzifanya kuwa uhalifu kazi za waandishi habari na watetezi wa haki za binadamu. Bi Margaret Sekaggya mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu amesema amesikitishwa na ripoti ambayo inawahusisha maafisa wa serikali, majeshi ya [...]

05/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya kulinda amani vya UM vitasalia nchini Liberia lakini kwa shabaha mpya

Kusikiliza / Vikosi vya kulinda amani nchini Liberia

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vitaendelea kusalia nchini Liberia lakini vinaazimia kuanzisha shabaha mpya ambayo itaweka zingatio zaidi kutokana na hali ya mambo ilivyo. Msaidizi wa Katibu Mkuu Edmond Mulet amesema kuwa vikosi hivyo haviwezi kujiondosha moja kwa moja nchini humo, lakini kuanzia sasa vitafanya kazi ya uhakiki ili kutambua namna vyombo [...]

05/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya Libya na waasi wamefanya uhalifu wa kivita:UM

Kusikiliza / Muammar Qadhafi

Jopo la wataalam wa UM limesema Majeshi ya Libya ya utawala wa zamani wa kiongozi Muammar Quadhafi, pamoja na waasi waliokuwa wakipigana wote wamefanya uhalifu wa kivita . Hii ni kutokana na ripoti ambayo imechapishwa leo Ijumaa na tume maalum ya uchunguzi wa Libya. Jopo hili pia limepata kuwa haki za binadamu zilikiukwa na waasi [...]

02/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kwa siku yapungua

Kusikiliza / Nemba ya benki ya dunia

  Benki ya dunia inasema kuwa idadi ya watu wanaoishi kwa chini ya dola 1.25 kwa siku kwenye nchi zinazoendelea inaripotiwa kupungua kati ya mwaka 2005-2008.  Takwimu hizo ambazo utafiti wake ulichukua muda wa miaka mitatu ndio wa kwanza tangu benki ya dunia ianzishe utafiti kuhusu umaskini.  Takriban watu bilioni 1.29 waliishi chini ya dola moja [...]

02/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wanawake kwenye masuala ya kisiasa bado ni ya chini

Kusikiliza / Nemba ya IPU

Chama cha bunge IPU kinasema kuwa hata kama mwaka 2011 ulishuhudia mabadiliko makubwa ya kisiasa na mabadiliko ya kidemokrasia kwenye sehemu tofauti za dunia, mwaka huo hata hivyo ulishuhudia idadi ndogo ya wanawake walioshiriki kwenye siasa. Nchi kama Nicaragua, Ushelisheli, Slovenia, Andora na Uganda zilipiga hatua kubwa katika uwakilishi wa wanawake kwenye masuala ya siasa. [...]

02/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakulima wa vijijini watakiwa kuwa na ushirikino wa kuzalisha chakula

Kusikiliza / Wakulima wadogowadogo

Serikali kwenye nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula zimetakiwa kufanya ushirikiano na wazalisha na pia kuwa na ushirikiano ili kupambana na njaa. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya usalama wa chakula na lishe David Nabarro anasema kuwa mashirika kama hayo yatawawezesha wazalishaji wadogo kuchangia kabisa katika upatikanaji wa chakula kwa [...]

02/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Shirika la wanawake wa UM kutoa dola milioni 10.5 kwa miradi ya kuwainua wanawake

Kusikiliza / wanawake

Shirika la wanawake wa Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kutoa dola jumla ya dola milioni 10.5 kwa minajili ya kuinua masuala ya wanawake ya kiuchumi na kisiasa kwa wanawake wa bara la Afrika, Asia na Pacific , America Kusini Caribbean, Ulaya na Asia ya kati. Shirika hilo linasema kuwa fedha zitaanzisha miradi ambayo itayaboresha maisha ya [...]

02/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Pakistan yatakiwa kukomesha ghasia

Kusikiliza / Rita Izsak

Wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na haki za dini na mauaji ya kinyume na sheria hii leo wameitaka serikali ya Pakistan kuchukua hatua ili kumaliza ghasia na kuboresha usalama kwa dini ndogo kufuatia kutokea mauaji ya waumini wa dini moja mara mbili kwa muda wa majuma mawili. Mnamo Februari 28 basi moja lilishambuliwa [...]

02/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

China na UNESCO zatia sahihi makubaliano ya kuboresha elimu Afrika

Kusikiliza / China na UNESCO yatia sahihi kusaidia elimu Afrika

  Mkurugenzi wa shirika la elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova pamoja na naibu waziri wa ulimu na mwenyekiti wa tume ya kiataifa ya UNESCO nchini China Hao Ping wametia sahihi makubaliano ya kuchangisha dola milioni 8 za kufadhili elimu na maendeleo barani Afrika kwa muda wa zaidi ya miaka [...]

02/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yawasaidia watu 1400 kurudi Sudan Kusini

Kusikiliza / Juhudi za kurudi Sudan kusini, IOM

Gari moshi moja kupitia usaidizi kutoka kwa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na ambalo limewabeba watu 1400 raia wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani kutoka mji wa Khartoum liko njiani kwa safari ambayo itachukua muda wa siku kumi ikielekea maeneo ya Aweil na Wau nchini Sudan Kusini. Hili ndilo gari moshi la kwanza kabisa kuondoka [...]

02/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yazindua mwongozo wa kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu

Kusikiliza / picha ya X-ray ya kifua

Takriban maisha ya watu 910,000 yameokolewa kwa muda wa zaidi ya miaka sita iliyopita kutokana na kuboreka kwa huduma za matibabu dhidi ya maradhi ya kifua kikuu na ukimwi ambazo huwazuia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu. Hii ni kulingana na takwimu za afya za dunia nzima zilizotolewa hii [...]

02/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia zaidi wa Mali wakimbilia Mauritania na Burkina Faso

Kusikiliza / wakimbizi wa kutoka Mali

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa mataifa ya Mauritania na Burkina Faso yamekuwa yakishuhudia idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Mali wanaokimbia mapigano kati ya waasi wa Tuareg na wanajeshi wa Mali. Karibu watu 31,000 wameikimbia Mali na kuingia nchini Mauritania huku wengine 20 wakiandikishwa nchini Burkina Faso. Mataifa hayo mawili yanaripotiwa [...]

02/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yaelezea wasiwasi wake kuhusu hali nchini Syria

Kusikiliza / machafuko nchini Syria

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema imetiwa wasi wasi kutokana na ripoti kutoka wilaya ya Baba Amro ya mji wa Homs baada ya kutwaliwa na wanajeshi wa serikali hiyo jana. Ofisi hiyo inasema kwamba haki za wale wanaozuliwa ni lazima ziheshimiwe na kuongeza uhalifu mkubwa umetendwa nchini Syria tangu mwaka uliopita. [...]

02/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yalaani mauji ya mkimbizi aliyekua katika juhudi za kuomba hifadhi, Indonesia

Kusikiliza / UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limelaani na kuelezea masikitiko yake kutokana na kuuliwa kwa raia mmoja wa Afghanistan ambaye alikuwa katika juhudi za kuomba hifadhi ya kisiasa huko Indonesia. Duru za habari zinasema kuwa, mamlaka ya Indonesia iliwatia kuzuizini raia sita wa Afghanistan ambao waliingia nchini humo katika jitihada zao za kusaka [...]

02/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2011 ulikuwa changamoto kubwa kwa haki za binadamu:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa mwaka 2011 ulikuwa ni mwaka wa changamoto nyingi kwa upande wa haki za binadamu hasa kutokana na hali mbaya ya uchumi duniani, hali mbaya ya hewa na uhaba wa chakula , njaa kwenye pembe ya Afrika, mizozo, ukabila na umaskini. Amesema pia [...]

02/03/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mfumo wa kupokea pesa kupitia simu za mikononi utachangia juhudi za kujenga makaazi: UM

Kusikiliza / Kupokea pesa kupitia simu za mkononi

Manusura wa tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi ya Haiti hatimaye wameanza kupokea fedha kupitia mfumo mpya wa simu za mikononi . Mpango huo ambao unapigwa jeki na shirika la maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNDP unalenga kuzisaidia familia hizo kuanzisha ujenzi wa nyumba ambazo ziliharibiwa wakati wa tetemeko hilo. Inakadiriwa kwamba zaidi ya familia [...]

02/03/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM ni jukwaa muhimu la kujadili changamoto za dunia

Kusikiliza / Abdulaziz Al-Nasser

Umoja wa Mataifa ni mahala pekee paliposalia ambapo kunapatikana fursa ya kuzijadilia kwa usawa changamoto zinazoendelea kuikabili dunia wakati huu. Akihutubu katika chuo kikuu kimoja nchini Uingereza, rais wa baraza kuu Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema masuala yanayohusu uchumi, siasa na mabadiliko ya teknolojia yanasalia mikononi mwa Umoja wa Mataifa. Ameeleza kuwa hata hivyo ili kukamilisha [...]

02/03/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maelfu washiriki katika mbio za marathan za Gaza:UM

Kusikiliza / mbio za marathon, Gaza

Mamia kwa maelfu wamejitokeza huko Gaza kushiriki mbio za marathon ambazo zimeandaliwa maalumu kwa ajili ya kuchangisha fedha kuwakirimu makundi ya watoto. Watoto zaidi 2000, na kundi la watu wazima wapato 500 walijikoza kwenye mbio hizo na kuzunguka katika maeneo kadhaa ya ukanda wa Gaza. Mbio hizo zilizoandaliwa na shirika la kuhudumia wakimbizi wa Palestina [...]

02/03/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wanawake bado wanaendelea kutupa au kutelekeza watoto Afrika

Kusikiliza / Mama na mwana

Kila kunapokucha hasa kwenye nchi za bara Afrika kunaripotiwa visa vya kutupwa kwa watoto wachanga mara wazaliwapo. Na ukatili huo hufanywa mara nyingi na wazazi ambao ama hawana mipango ya kuchukua majukumu ya kuwalea watoto hao au kutokana na sababu moja au nyingine, huku wengi wakiokotwa barabarani , kwenye majaa ya taka na wengine wakiwa [...]

02/03/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Umuhimu na thamani ya mwanamke wa Kijijini

Kusikiliza / wanawake vijijini

Wiki hii kwenye Umoja wa Mataifa kunafanyika kongamano ambalo linajumuisha wanawake kutoka kila pembe kujadili umuhimu na thamani ya kila mwanamke kijijini. Kongamano hili limeandaliwa na kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa UN WOMEN na linashirikisha wanawake viongozi na wanaharakati wa kupigania haki za wanawake na wadau wengine ambao wanachagiza haki za wanawake. Miongoni [...]

01/03/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930