Wanainchi wa Haiti wajiandaa kwa gharika nyingine
Kusikiliza /Miezi baada ya kuanza kwa kipindi cha gharika kwenye pwani za kisiwa cha Hispaniola, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Hispaniola wameatangaza mpangilio wa kwanza jinsi ya kutumia vituo vya uokoaji. IOM imetoa usaidizi wa kiufundi kwa zaidi ya vituo 500 vya uokoaji kote nchini ili kuhakikisha kuwa vinafanya kazi kwa njia inayohitajika. IOM ilijenga na kukarabati jumla ya vituo 29.
Suala la kutoa mpango wa kutumika kwa vituo hivyo ulipendekezwa wakati wa ujenzi wake kufuatia madai ya njia za kusimamiwa kwa vituo wakati kunapotokea jambo la dharura.
