UM wakaribisha hatua ya serikali ya Haiti kuleta usawa
Kusikiliza /Umoja wa Mataifa umesema kuwa unakaribisha kwa furaha hatua ya serikali ya Haiti kuridhia mpango mpya unaokusudia kutoa usawa katika maeneo ya uchumi, jamii na utamaduni.
Serikali ya Haiti imeanza kuuratibu mpango huo ambao pamoja na mambo mengine utatilia uzito maeneo ya kukaribisha usawa wa kijamii na kupunguza bengo la kitabaka. Katika taarifa yake kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH, imesema kuwa kuanzishwa kwa mpango huo ni hatua mujarabu ambayo itahakikisha uhuru wa haki za binadamu sasa unaanza kuzingatiwa nchini humo.
Ama kikosi hicho kimerejelea kauli yake ikisema itaendelea kuiunga mkono serikali ya Haiti hasa wakati huu inapoanza kuteleza mpango huo wa kijamii.
