UM utavuna mengi ukiongeza mashirikiano yake na Umoja wa Ulaya

Kusikiliza /

Baraza la Usalama

Umoja wa Mataifa umeelezewa umuhimu wa kuwa na mafungamano ya karibu na nchi wanchama wa Umoja wa Ulaya ambazo zinaunda jumuiya ya usalama na mashirikiano katika eneo hilo OSCE, kuwa hatua hiyo itazalisha matunda mema.

Waziri wa mambo ya nchi za Nje wa Ireland ambaye ndiye rais wa chombo hicho cha usalama kwa nchi za ulaya ameliambia baraza la usalama juu ya pande hizo kuwa na mashirikiano yenye mshiko na utengamao.

Eamon Gilmore amesema pande zote mbili zinajongeleana kwa mambo mengi, ambayo kama yatapewa uzito na kutumika ipasavyo yanaweza kufaa kukabili changamoto za kiusalama zinazoikabili dunia kwa sasa.

Jumuiya hiyo inajuka ya nchi wanachama 54 na inachukua jukumu la pekee kuhusiana na masuala ya usalama kwa kanda ya Ulaya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

Kuungana

 

Mei 2012
T N T K J M P
« apr    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031