Mashirika ya kutoa misaada yaomba dola milioni 39 kuwasaidia waathiriwa wa tufani nchini Ufilipino

Kusikiliza /

waathiriwa nchini Ufilipino wapokea mkate

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake wametoa ombi la dola milioni 39 za kusaidia katika utoaji wa huduma kwa zaidi ya watu 300,000 walioathiriwa na tufani Washi katika eneo la Mindanao nchini Ufilipino kwa muda wa miezi 6. Kiasi hicho cha fedha kimeongezeka kwa dola milioni 10.6 zaidi kutoka dola milioni 28.4 kilichoombwa awali.

Tufani Washi iliingia nchini Ufilipino na sehemu zilizo karibu kati tarehe 16 na 18 mwezi Disemba mwaka uliopita na kusababisha mvua kubwa ambayo pia ilisabaisha kutokea kwa mafuriko na maporomoko ya udongo. Karibu nyumba 48,000 ziliharibiwa huku karibu watu 625 wakiathiriwa. Zaidi ya watu 550,000 pia walilazimishwa kuhama makwao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

Kuungana

 

Mei 2012
T N T K J M P
« apr    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031