Nyumbani » 29/02/2012 Entries posted on “Febuari, 2012”

Kofi Annan asema yuko tayari kusaidia kutatua mzozo nchini Syria

Kusikiliza / Kofi Annan na Ban Ki-moon

Mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za Kiarabu Bw. Kofi Annan leo amesema wajibu aliokabithiwa ni mgumu lakini yuko tayari kuutekeleza. Akiongea baada ya kukutana na Katibu Mkuu Ban Ki-moon Bw Annan amesema jambo la kwanza kuhimu linalihitajika ni kuhakikisha kwamba misaada ya kibinadamu inawafikia walioathirika. (SAUTI YA KOFI ANNAN) Katibu [...]

29/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Changamoto zaingoja serikali mpya nchini Libya

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Ian Martin anasema kuwa hata baada ya kuwepo ghasia nchini humo suala lililo wazi ni kwamba watu wa Libya wana nia ya kusonga mbele kupata demkokrasia.   Akihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video kutoka nchini Libya, Martin anasema kuwa [...]

29/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Amos asikitika kwa kutozuru Syria

Kusikiliza / Valerie Amos

Mratibu wa huduma za dharura za misaada kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos ameelezea sikitiko lake kutokana na sababu kwamba hajaitembelea Syria mwenyewe ili kujionea hali ya kibinadamu na kufanya mikutano na maafisa wa ngazi za juu wa nchi hiyo. Maelfu ya raia wameuawa kwenye oparesheni za serikali dhidi ya wanaoipinga serikali zilizoanza machi mwaka [...]

29/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM kuongeza shinikizo kukomesha mila ya Ukeketaji

29/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UM umewaleta pamoja wataalamu wa sekta ya habari na mawasilino

Kusikiliza / nishati safi

Kongamano la kimataifa linalowakutanisha wataalamu wa habari, mawasilliano ya teknolojia limeanza huko Barcelona likiwa na shabaha ya kukaribisha mifumo mipya ya ubunifu juu ya maendeleo ya nishati mbadala. Wataalamu hao kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaangazia nafasi ya teknolojia ya habari na mawasilinao inavyoweza kuchochea kasi ya maendeleo yanayozingatia nishati bora. Kongamano hilo linaloratibiwa na Umoja [...]

29/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mshauri wa UM wa michezo aunga mkono mpango wa kuruhusu hijab salama katika soko

Kusikiliza / Wachezaji wa kandanda wa Iran

Katika hatua ya karibuni ya maendeleo katika mchezo wa kandanda kuhusu suala la wachezaji wanawake kuvaa hijab wakati wakiwa kiwanjani , mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu michezo kwa ajili ya maendeleo ya amani Wilfried Lemke amesema anaunga mkono hatua iliyopendekezwa na makamu wa raia wa shirikisho la soka duniani FIFA Mwana mfalme Ali [...]

29/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban awataka watu wa Timor-Leste Kufanya uchaguzi kwa amani

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka watu wa Timor-Leste kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu. Ban amesema uchaguzi ujao wa Rais ni hatua muhimu kwa taifa hilo katika kudumisha demokrasia.  Amesema kufanyika kwa uchaguzi huo ni ishara ya hatua iliyopigwa katika muongo mmoja tangu kurejeshwa kwa uhuru ambapo amani na ukuaji wa [...]

29/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tovuti ni chombo muhimu kwa watu kupata taarifa:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Tovuti imekuwa ni nyenzo muhimu kwa watu kupata taarifa zaidi ya zile zinazotayarishwa na kusambazwa na vyombo vya asili vya habari. Hayo yamesemwa na kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay katika mjadala wa haki ya uhru wa kujieleza katika tovuti uliofanyika Jumatano mjini Geneva. Amesema wakati huohuo tovuti imesuruhusu watumiaji wote kutoa taarifa, [...]

29/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yabaini watoto waliotelekezwa kwenye mpaka wa Chad na Nigeria

Kusikiliza / wakimbizi wa Chad

Tathimini ya pamoja iliyofanywa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Chad imebaini kuwa kwenye mpaka baina ya Chad na Nigeria kuna kundi kubwa la watu wa Chad wanaorejea kutoka Nigeria ikiwemo idadi kubwa ya watoto walio peke yao wa kati ya umri wa miaka 6 hadi 14. Tathimini hiyo imefanyika kwa [...]

29/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei ya chai kuendelea kupanda kutokana na ongezeko la mahitaji:FAO

Kusikiliza / chai

Utabiri wa awali wa mwaka 2012 unaonyesha kuendelea kupanda kwa bei ya chai kwa wasitani wa asilimia 2.2 kwa kilo hapo mwaka 2011 limesema kundi la la shirika la chakula na kilimo FAO la mataifa wazalishaji wa chai. FAO inasema bei za juu za chai zinaashiria ukweli kwamba mahitaji ya chai ambayo inachukua nafasi kubwa [...]

29/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya mkurugenzi wa redio

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga Jumatano amelaani vikali mauaji ya Abukar Mohamed Kadaf, mkurugenzi wa Somaliweyn Radio ambaye amepigwa risasi na kuuawa usiku wa Jumanne katika wilaya ya Wadajir mjini Moghadishu. Balozi Mahiga ameitaka serikali ya mpito ya Somalia kufanya uchunguzi huru mara moja ili kuwafikisha kwenye mkono wa [...]

29/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni wakati wa Afrika kujitengenezea dawa za HIV na ukimwi: Sidibe

Kusikiliza / Michel Sidibe, UNAIDS akutana na rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS Michel Sidibe amesema umefika wakati kwa Afrika kuanza kutengeneza dawa za kupunguza makali ya ukimwi. Sidibe amesema kwa kuzalisha dawa hizo Afrika nchi kama Ivory Coast na jirani zake watakwepa tatizo la upungufu wa madawa na kufaidika na gharama nafuu ya [...]

29/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wazindua mpango wa kupambana na ugonjwa wa Chikungunya

Kusikiliza / virusi vya chikungunya

Maafisa wa afya kutoka Umoja wa Mataifa wametoa mwongozo mpya wa kusaidia nchi kwenye mabara ya Amerika kutambua ugonjwa ujulikanao kama chikungunya uanosambazwa na mbu na ambao tayari umewaambukiza zaidi ya watu milioni kote duniani. Mpango huo uliozinduliwa na shirika la afya duniani WHO ni wa kuwatarisha maafisa wa afya ili kuutambua na kuuzuia ugonjwa [...]

29/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maduka ya madawa ya mtandao yatumia mtandao kuwafikia vijana

Kusikiliza / cocoa

Bodi ya kimataifa inayohusika na madawa INCB inaonya kuwa maduka haramu yanayotumia mtandao kwa sasa yanawalenga vijana kupitia mawasilino ya mtandao. Hii ilikuwa moja ya ajenda ya ripoti ya mwaka 2011 ya bodi hiyo iliyozinduliwa mjini Vienna. Rais wa INCB Hamid Ghadse anasema kuwa maduka ya kuuza madawa ya kupitia mtando ukiwemo wa mawasiliano ya [...]

29/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatma ya mazungumzo ya moja kwa moja Palestina-Israel bado iko "gizani"

Kusikiliza / palestine-1

Umoja wa Mataifa umezitolea mwito Palestina na Israel kuchukua hatua madhubuti kuyatafutia ufumbuzi masuala yanayokwamisha kurejea kwenye meza ya majadiliano na kuongeze kuwa majadiliano yaliyoanzishwa mwezi uliopita yamegota katika wakati hali ya mambo huko Gaza ikisalia kuwa tete. Kwa mujibu wa mwakilishi wa Katibu Mkuu juu ya masuala ya siasa Lynn Pascoe pande hizo zinapaswa [...]

29/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Urusi imesema haitounga mkono jaribio la kufanya HRC kutoa shinikizo la Kisiasa

Kusikiliza / Gennardy Gatilov

  Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Gennandy Gatilov amesema kwamba Urusi haitounga mkono jaribio lolote la kufanyia mabadiliko baraza la haki za binadamu au HRC kuwa chombo cha kutoa shinikizo la kisiasa na kugawanya mataifa iwe kwa vizuri au vibaya. Waziri huyo ameongeza kwamba ni muhimu matatizo yaliyopo yakatatuliwa na watu wenyewe [...]

29/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu limetoa wito wa kuzingatia uhuru duniani kote

28/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wanaoishi kwenye kambi nchini Haiti yapungua

Kusikiliza / makambi nchini Haiti

Idadi ya watu wanaoishi kwenye mahema nchini Haiti kufuatia tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo mwaka 2010 imepungua hadi chini ya watu 500,000. Hii ni kutokana na matokeo ya idara ya nyumba nchini humo wakati shughuli ya kuwahamisha watu hao inapong'oa nanga. Mpango huo ujulikanao kama 16/6 unawasaidia watu waliopoteza makazi yao wakati wa tetemeko hilo [...]

28/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uchimbaji wa makaa watishia haki za binadamu nchini Bangladesh:UM

Kusikiliza / Oliver De Schutter

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Bangladesh kuhakikisha kuwa sera zinazohusiana na uchimbaji wa mgodi wa makaa zinalinda haki za binadamu. Wataalamu hao wanasisitiza kuwa uchimbaji huo wa mgodi wa Phulbari haustahili kuendelea kutokana na matatizo ambayo huenda ukasababisha. Pia wanaonya kuwa ukiwa shughuli hiyo itaruhisiwa huenda ikasababisha kuhamishwa kwa maelfu ya [...]

28/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi ya 30,000 wa Liberia na Ivory Coast kurejea nyumbani

Kusikiliza / Wakimbizi wa Ivory Coast

Zaidi wakimbizi 30,000 kutoka Liberia na Ivory Coast wanatarajiwa kurejeshwa nchini mwao kupitia mpango wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Kuna takriban wakimbizi 79,000 kutoka Ivory Coast walio nchini Liberia na wengine 24 ,000 kutoka Liberia wanaoishi nchini Ivory Coast. Jumbe Omari [...]

28/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aitaka Angola kuunga mkono vilivyo Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Katibu mkuu,UM Ban Ki-moon akutana na Rais Jose E dos Santos, Angola

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekamilisha ziara yake nchini Angola ambapo amelitaja taifa hilo kama kiongozi wa kimataifa siku za usoni. Kwa sasa Angola ndiye mwenyeki wa nchi za SADC na pia kwa jumuiya ya mataifa yanayozungumza lugha ya kireno. Ban anasema kuwa Angola itayafanya mengi kwenye ulingo wa kimataifa kwa ushirikiano na Umoja [...]

28/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna zana 23,000 za nyuklia zinazotishia usalama:Iran

Kusikiliza / Zana za nyuklia

Taifa la Iran limeuambia mkutano kuhusu silaha za maangamizi mjini Geneva kuwa zana za kinyuklia zinaweza kuongezeka hasa wakati baadhi ya mataifa yanaonekana kuwa huru kuyatisha mataifa mengine yakiwemo mataifa yasiyo na silaha hizo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Ali Akbar Salehi amesema kuwa kuna njia mbili za kuushughulikia mpango wa nyuklia nchini [...]

28/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICRC yatoa ombi la Euro milioni 10 kuwasaidia watu 700,000 Mali na Niger

Kusikiliza / Wafanyakazi wa ICRC nchini Mali

Chama cha kimataifa cha msalaba mwekundu na cha mwezi mwekundu ICRC kinatoa wito wa mchango wa Euro milioni 10 zitakazotumika kuwapelekea misaada watu 700,000 nchini Mali na Niger na kugharamia huduma zingine za kibinadamu kwenye mataifa hayo mawili. ICRC inasema kuwa watu nchini Mali kwa sasa wanakabiliwa na matatizo aina mbili ikiwemo ukosefu wa chakula [...]

28/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Syria yajiondoa kwenye mjadala wa baraza la haki za binadamu

Kusikiliza / Faysal Khabbaz Hamoudi

Syria imejiondoa kutoka kwenye kikao cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kinachojadili ghasia zinazoendelea nchini humo. Balozi wa Syria Faysal Khabbaz Hamoudi anasema kuwa ujumbe wake haukitambui kikao hicho na kulishutumu baraza hilo kwa kukiuka sheria zake za uongozi. Balozi Hamoudi anadai kwamba mjadala huo utachochea makundi ya kigaidi yanayoipinga serikali. [...]

28/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi kubwa ya ndovu wauawa nchini Cameroon

Kusikiliza / Uwindaji haramu wa ndovu nchini Cameroon

Katibu anayehusika na biashara ya kimataifa kuhusu sehemu na wanyama walio kwenye hatari ya kuangamia John Scanlon ameelezea hofu iliyopo kutokana na ripoti ya kuuawa kwa karibu ndovu 450 kwenye mbuga ya kitaifa ya Bouba Ndjida iliyo Kaskazini mwa Cameroon. Serikali katika eneo hilo zimepewa usaidizi wa kuwatafuta na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika na [...]

28/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu lataka ghasia zikome Syria:

Kusikiliza / Navi Pillay

Akiongea wakati wa kuanza kwa mjadala wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali nchini Syria mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa hali nchini Syria inazidi kuzorota huku vikosi vya serikali vikiendelea kuwadhulumu maelfu ya waandamanaji na watetesi wa haki za binadamu. Pillay amerejelea [...]

28/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto wengi waishia mitaani mijini:UNICEF

Kusikiliza / Watoto barani Afrika

Zaidi ya watoto bilioni moja kote duniani wanalelewa mijini huku wale wanaoelelewa kwenye familia maskini wakiwa hawapati huduma muhimu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu kuhusu hali ya watoto duniani ya shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. UNICEF inasema kwamba mmoja kati ya watu watatu walio mijini wanaishi kwenye [...]

28/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Migiro ataka vijana wasiendelee kuachwa kando

Kusikiliza / Asha-Rose Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha –Rose Migiro amesema kuwa serikali pamoja na watunga sera wanakazi kubwa ya kufanya ili kutambua nguvu za uzalishaji walizonazo vijana.  Pia amehimiza haja ya kuwepo kwa mageuzi ili kutatua tatizo la kimfumo linaloendelea kuwaacha vijana wengi nje ya ajira.  Katika hotuba yake wakati akifungua kongamano la kimataifa [...]

28/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuna haja ya kuwa na mashirikiano kushinda hujma za kiharamia Pwani ya Guinea-UM

Kusikiliza / Meli iliyokamatwa na maharamia Benin mwaka 2011

Kuna haja ya kuweka mikakati ya dharura kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uharamia katika pwani ya Guinea, na hii itazaa matunda kama nchi husika zimedhamiria kuzishinda hujma za maharamia hao. Akijadilia tishio la kiusalama pamoja na maendeleo ya kiuchumi kwenye eneo hilo, mwakilishi wa Katibu Mkuu katika masuala ya kisiasa Lynn Pascoe amesema kuwa [...]

28/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu lafanya majadiliano

Kusikiliza / Nemba ya Baraza la haki za binadam

Baraza la haki za binadamu limeendesha majadiliano kwa ajili ya kumulika hali ya haki za binadamu huku likiweka zingatio la kuwepo kwa mashirikiano ya kimataifa.  Katika ujumbe wake kupitia video, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi wanachama wa Umoja huo zinawajibika kuheshimu na kuzingatia masuala ya haki za binadamu. Amezitolea mwito [...]

28/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM kuongeza shinikizo kukomesha mila ya Ukeketaji

Kusikiliza / Angelique Kidjo

  Balozi mwema wa Umoja wa Mataifa Angelique Kidjo anatazamiwa kutumbuiza kwenye tamasha maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kutokomeza vitendo vya ukeketaji. Mwanamuziki huyo atapanda jukwaani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kutoa ujumbe unaohamasisha kukomeshwa kwa vitendo hivyo.  Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya wasichana na wanawake milioni 140 wamekeketwa na kuna [...]

28/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupambana na unyanyasaji wa kijinsia:UM

27/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Fursa za wanawake wa vijijini katika kupambana na umasikini zitiliwe maanani

Kusikiliza / wanawake vijijini

Kuwawezesha wanawake wa vijiji ili waashiriki katika  jukumu la kupambana na njaa na umasikini itakuwa ndio ajenda kubwa ya mwaka huu katika mjadala wa kila mwaka kuhusu hali ya wanawake duniani. Tume ya kuhusu hali ya wanawake au CSW imeanza kikao cha 56 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York leo Jumatatu. Wanawake [...]

27/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshindi wa tuzo ya Oscar ataka kutengeneza filamu kuhusu UM

Kusikiliza / Terry George alipopokea tuzo

Mshindi wa tuzo ya filamu yaani Oscar Terry George amesema moja ya mimitadi yake ijayo itakuwa kutengeneza filamu kuhusu mwanadiplomasia wa zamani wa Umoja wa Mataifa Sergio Viera de Mello ambaye aliuawa katika shambulio la bomu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya Iraq mwaka 2003. Bwana George ameshinda tuzo ya filamu bora fupi [...]

27/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wawahamisha kwa muda wafanyakazi wake baada ya shambulio kaskazini mwa Afghanistan

Kusikiliza / Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa unawahamisha kwa muda wafanyakazi wake wa kimataifa kutoka katika ofisi yake ya mpango wa kulinda amani UNAMA iliyoko jimbo la Kuunduz Kaskazini mwa nchi hiyo kufuatia kuongezeka kwa ghasia. Ofisi hizo zilishambuliwa mwishoni mwa juma na waandamanaji wenye hasira kutokana na wanajeshi wa Marekani kuchoma kitabu kitakatifu cha Koran wiki iliyopita. Hakuna [...]

27/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamhuri ya Afrika ya kati yazindua kampeni ya kutokomeza polio

Kusikiliza / chanjo ya Polio kwa mtoto

Kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya polio imezinduliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mwishoni mwa juma ikiwa na lengo la kufikiwa watoto wote nchini humo ikiwa ni pamoja na wale ambao ni vigumu kuwafikia wanaoishi kwenye maeneo ya vita na ambako vita ndio vimemalizika tuu na hivyo huduma za afya ni haba. Kampeni [...]

27/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO na IFAH kukabiliana na biashara haramu ya dawa za mifugo

Kusikiliza / dawa haramu ya mifugo

  Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula la kilimo FAO na shirikisho la kimataifa la afya ya mifugo IFAH wanafanya kazi pamoja ili kuanzisha viwango vya kwanza vya sekta ya madawa kwa ajili ya dawa zinazotumika kutibu ugonjwa unaoathiri mifugo Afrika ujulikanao kama Nagana au malale. Kwa mujibu wa Juan Lubroth mkuu wa shirika [...]

27/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Ivory Coast aridhishwa na uchaguzi mdogo nchini humo

Kusikiliza / Mkuu wa UNOCI, Bert Koenders

Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Ivory Coast UNOCI ameelezea kuridhishwa kwake na jinsi uchaguzi mdogo wa bunge ulivyoendeshwa nchini humo akisema upigaji kura umefanyika katika mazingira ya utulivu. Bert Koenders ameyasema hayo katika mwisho wa ziara yake kwenye vituo mbalimbali vya uchaguzi, ziara ambayo aliambatana na maafisa mbalimbali wa [...]

27/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uturuki kuandaa mkutano wa mwingine wa "marafiki wa Syria"

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz Al-Nasser

Uturuki imesema kuwa iko tayari kuandaa mkutano wa marafiki wa Syria kwa ajili ya kufuatilizia maazimio yaliyofikiwa na mkutano kama huyo uliofanyika wiki iliyopita nchini Tunisia. Tayari rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser ambaye alikuwa nchini humo, amekaribisha uamuzi huo. Uturuki inatazamia kuandaa mkutano huo uliopangwa kufanyika baadaye mwezi March [...]

27/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukaliwaji na watu wa nje hauendani na demokrasia: Nassir

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu, UM, Nassir .A. Al-Nasser

Ukaliwaji na watu wa nje unakwenda kinyume na demokrasia na haki za binadamu hususani haki ya kujitawala amesema Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser alipokuwa akilihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Jumatatu. Amesema hali inayoendelea katika ulimwengu wa Kiarabu isisababishe kupuzwa kwa masuala ya amani na utlivu. Ametaka [...]

27/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Zambia yapongezwa kwa kuimarisha demokrasia

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Nchi ya Zambia imepongezwa kutokana na kufanya vizuri katika maeneo kadhaa ikiwemo ukuzaji wa demokrasia, ongezeko la wanafunzi wanajiunga na elimu ya msingi na kupunguza kwa vifo vya kina mama wajawazito. Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-moon wakati alipokutana na rais wan nchi hiyo Michael Sata, akihitimisha ziara ya kiserikali [...]

27/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa walaani mashambulizo kwenye makao yake nchini Afghanistan

Kusikiliza / ramani ya Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulizi lililotokea kwenye makao yake yaliyo kwenye mji ulio kaskazini mashariki wa Kunduz. Hata hivyo hamna visa vyovyote vya majeruhi vilivyoripotiwa na bado wafanyikazi wote wa Umoja wa Mataifa wako salama. Vyombo vya habari vinaripoti kuwa ghasia kwenye mji wa Kunduz zinahusiana na kuchomwa kwa nakala [...]

27/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Senegal yasubiri matokeo ya awali ya uchaguzi

Kusikiliza / Uchaguzi nchini Senegal

Hali ya wasiwasi bado imetanda kufuatia Senegal kufanya uchaguzi wa Rais wa duru ya kwanza mwishoni mwa juma. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye yuko ziarani barani Afrika amesema ana matumaini kwamba uchaguzi huo utakuwa ni huru, wa wazi, wa amani na unaoheshimu matakwa ya watu wa taifa hilo. Kampeni za uchaguzi [...]

27/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wawili wanaohudumu kwenye kikosi cha UNAMID wajeruhiwa

Kusikiliza / askari wa UNAMID

Walinda amani wawili wanaohudumu kwenye kikosi cha pamoja cha Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan UNAMID walijeruhiwa wakati watu waliokuwa wamejihami walipofyatulia risasi basi walilokuwa wakisafiria karibu na mji wa El Dein ulio magharibi mwa Sudan. Wawili hao walio kwenye kikosi cha polisi cha UNAMID [...]

27/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Angola imekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika vita dhidi ya polio: Ban

Kusikiliza / Katibu mkuu UM, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipongeza Angola kwa juhudi zake za kutokomeza ugonjwa wa polio. Katika risala yake kwenye kituo cha chanjo ya polio mjini Luanda Jumatatu Ban amesema matokeo ya juhudi hizo ni kuwa huru bila polio mwaka 2001, lakini amelaumu kwamba katika kipindi cha miaka minne baadaye virusi vya polio [...]

27/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu lafanya mjadala wa dharura kuhusu Syria

Kusikiliza / Baraza la haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu litafanya mjadala wa dharura kuhusu hali ya Syria licha ya Iran kupinga kufanyika kwa mjadala huo. Mjadala utafanyika Jumanne kwa ombi maalumu la Qatar amesema Rais wa baraza la haki za binadamu Laura Dupuy Lasserre. Rais huyo pia amesema amepokea pingamizi rasmi la mjadala huo kutoka kwa Iran ambayo sio [...]

27/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais mpya wa Yemen aapishwa

Kusikiliza / uchaguzi nchini Yemen

Makamu wa rais wa Yemen amekula kiapo kama kiongozi mpya wa nchi hiyo baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amekaribisha hayo hasa wakati huu ambao taifa hilo linakabiliwa na wakati mgumu. Abbed Rabbo Mansour al-Hadi aliapishwa mwishoni mwa juma. Hii ni baada ya pande zinazozozana [...]

27/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yataka suluhu kwa wakorea wanaozuiliwa nchini China

Kusikiliza / maandamano ya wakimbizi wa Korea kaskazini

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linaifuatilia kwa karibu hali ya watu 25 raia wa Korea Kaskazini waliokamatwa nchini China mwezi huu. UNHCR imekuwa ikiwasiliana na utawala nchini China kuhusu watu hao na kutaka pande zote zinazohusika kujaribu kupata suluhu litakalowahikikishia usalama wa watu hao. UNHCR imesema kuwa itatoa ushirikiano wake na kuendelea [...]

24/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa haki za binadamu wa UM aikaribisha ripoti ya Togo

Kusikiliza / ufungwa

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekaribisha kutolewa kwa ripoti na tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini Togo kuhusu madai ya dhuluma za mateso yaliyotendwa kwa watu wanaoaminika kuhusika na mapinduzi ya mwaka 2009 nchini humo. Ripoti hiyo iligundua kuwa wafungwa hao walidhulumiwa na ikataka hatua kuchukuliwa dhidi [...]

24/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa UM akaribisha kurejea kwa wafanyakazi Kordofan Kusini:

Kusikiliza / wakimbizi,south kordofan Sudan

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Mark Cutts amekaribisha kurejea leo kwa wafanyakazi wa kimataifa ambao ni wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Kordofan Kusini. Hatua hii imefuatia uamuzi uliofanywa awali na serikali ya Sudan wa kuidhinisha kurejea kwa wafanyakazi hao, na wafanyakazi wawili wa kwanza wamewasili leo kwenye [...]

24/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ni wakati wa kutupia macho watoto walioko mijini: UNICEF

Kusikiliza / shirika linaloshughulikia maswala ya watoto UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema zaidi ya watu bilioni 7 duniani hivi sasa wanaishi mijini, na h ii inamaanisha nini kwa watoto? . Kwa mujibu wa shirika hilo ripoti yake ya mwaka 2012 imetenga maalumu kwa ajili hiyo, kuangalia hali ya watoto duniani husani wale wanaokulia mijini. Miji inajulikana kwa kukuza [...]

24/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakusanya nguvu ya pamoja kukabili janga la njaa

Kusikiliza / WFP

Huku kukisubiriwa kwa hamu kubwa kuzinduliwa rasmi kwa filamu inayozungumzia njaa, waandaaji wa filamu hiyo wameanza kukutana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mpango wa chakula WFP kwa ajili ya kuhamasisha ulimwengu juu ya kitisho cha njaa. Tayari wamezindua wavuti ambao ndani yake inapatikana picha za video zinazoelezea mchezo kuhusiana na janga la [...]

24/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa usawa kwenye maeneo ya kazi waongezeka barani Ulaya

Kusikiliza / Nemba ya shirika la ajira duniani, ILO

Shirika la ajira duniani ILO limesema kuwa kutokuwepo usawa kwenye maeneo ya kazi kumeongezeka barani Ulaya hasa kutokana na hali mbaya ya uchumi na hali hiyo inatarajiwa kuendelea wakati nchi nyingi zinapoendelea kufanya mabadiliko kwenye masuala ya ajira. Kulingana na utafiti wa ILO ni kwamba hali kwenye maeneo ya kazi, mishahara na usawa wa kijinsia [...]

24/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa yanayoendelea yatakiwa kuwa na mazingira bora ya kibiashara

Kusikiliza / Picha ya bendera za baadhi ya mataifa yanoyostawi

Mataifa yanayoendelea yametakiwa kufanya jitihada za kuhakikisha kuwepo kwa mazingira mazuri ya kibiashara ikiwa yatahitaji kuwa na fedha za kugharamia miundo msingi yao. Hii ndiyo ilikuwa ajenda kwenye mkutano wa mwaka huu wa watunza sera kuhusu ushirikiano kati ya washika dau wa kibinafsi na wale wa umma PPP. Kwa sasa ushirikiano wa PPP unakabiliwa na [...]

24/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi, Tanzania na UNHCR kuwarejesha nyumbani wakimbizi walioko Mtabila

Kusikiliza / Kambi ya Mtabila

Serikali ya Burundi, Tanzania na na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameazimia kufunga kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Mutabila iliyoko nchini Tanzania ifikapo mwezi wa Disemba mwaka huu. Halmashauri hiyo ya pande tatu imetangaza hatua hiyo katika kikao cha 16 kilichofanyika alhamisi hii mjini Bujumbura Burundi na kutaja kwamba hamna [...]

24/02/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wengi wana nia ya kuhamia nchi za kigeni

Kusikiliza / mchoro unaoashiria uhammiaji duniani

Imebainika kuwa watu wazima milioni 630 duniani wanaweza kuhamia nchi zingine kabisa. Hii ni kulingana na matokeo ya utafiti wa taasisi ya utafiti duniani Gallup. Ripoti hiyo inatoa picha nzuri kwa mara ya kwanza kuhusu maisha ya watu walio na nia ya kuhama kabisa au kufanya kazi kwa muda, wanajiandaa kuondoka na waliorejea nyumbani.  Ripoti [...]

24/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu kuijadili Syria

Kusikiliza / baraza la haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuandaa mjadala wa dharura kuhusu mzozo wa kisiasa unaondelea nchini Syria juma lijalo. Ombi la kutaka kuandaliwa kwa mjadala huo lilitolewa na taifa la Qatar na kuungwa mkono na wanchama kadhaa wa baraza hilo wakiwemo Marekani, Jumuiya ya Ulaya na mataifa kadhaa ya kiarabu. Hiyo [...]

24/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban aihakikishia Zambia usaidizi wa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / biashara katika Soko la vyakula,Zambia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaisaidia nchi ya Zambia katika jitihada zake za kuboresha uchumi za kuhakikisha kuwepo kwa ajira na kupunguza umaskini. Kwenye ujumbe wake kwa bunge la Zambia Ban amesema kwamba kitu muhimu kwa taifa la Zambia ni watu wake akiongeza kuwa Zambia itagundua umuhimu [...]

24/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 130,000 wakimbia makwao kufuatia mapigano yanayoendelea nchini Mali

Kusikiliza / wakimbizi wa Mali

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa zaidi ya raia 130,000 wa Mali wamelazimika kuhama makwao kufuatia mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa Tuareg kwenye eneo la kaskazini mwa nchi. Watu 63,000 wamehama ndani mwa nchini huku waliosalia wakikimbilia nchi majirani zikiwemo Niger, Burkina Faso, Mauritania na Algeria. Shirika la kuratibu masuala [...]

24/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna ongezeko la ukosefu wa usawa sehemu za kazi: ILO

Kusikiliza / Mchoro wa usawa

Utafiti mpya uliotolewa na shirika la kazi ulimwenguni ILO, unaonyesha ongezeko kubwa la ukosefu wa usawa sehemu za kazi. Utafiti huo unasema hali ya kukosekana kwa usawa kwenye sehemu za kazi barani Ulaya ni kubwa na kuonya kwamba mwenendo huo unatazamiwa kuendelea kushuhudiwa kwa kipindi kIrefu. Kwa mujibu wa utafiti huo mabadiliko hayo yamechangiwa pakubwa [...]

24/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kofi Annan akubali kuwa mjumbe wa UM na muungano wa nchi za Kiarabu nchini Syria

Kusikiliza / Kofi Annan

Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amekubali ombi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na katibu mkuu wa muungano wa nchi za kairabu Nabil ElAraby la kuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Muungano huo kuhusu mzozo nchini Syria. Kupitia taarifa yake mjini Geneva Annan amesema kuwa [...]

24/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kofi Annan kwenda kusuluhisha Syria

Kusikiliza / Kofi Annan

Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu umemteua Bwana Kofi Annan kuwa mjumbe maalumu atayeshughulia mzozo wa Syria. Wakati pande hizo mbili zikimtangaza Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa kushughulikia mzozo huo, taarifa kutoka nchini humo zinaeleza hali inavyozidi kuwa mbaya. Mamia ya watu wameendelea kupoteza maisha kutokana na operesheni [...]

24/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuinua maendeleo vijijini:UM

23/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Wahalifu wa ubakaji katika maeneo ya vita watajwa na kuaibishwa:

Kusikiliza / Uhalifu wa kimapenzi

Kukomesha matumizi ya ubakaji na mifumo mingine ya ukatili wa kimapenzi kama kutumika kama silaha za vita bado ni moja ya changamoto kubwa katika kulinda haki za binadamu amesema mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi katika maeneo ya vita. Bi Margot Wallstrom amesema njia moja ya kupambana na ukwepaji wa sheria [...]

23/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNESCO alaani mashambulizi dhidi ya kituo cha habari Homs Syria:

Kusikiliza / Mauaji ya wanahabari

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokobva, Alhamisi amelaani vikali mashambulizi ya jeshi la Syria dhidi ya kituo cha habari mjini Homs. Shambulio lilifanyika tarehe 22 Februari na kusababisha vifo vya waandishi habari wawili na kujeruhi wengine wengi. Bi Bokova ameutaka uongozi wa Syria kuheshimu hadhi [...]

23/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban aongeza muda wa kimamlaka kwa mahakama ya kimataifa juu ya mauwaji ya Hariri Lebanon

Kusikiliza / Rafik al-Hariri ,aliyekuwa katibu mkuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameidhinisha kwa miaka mingine mitatu mahakama ya kimataifa inayofuatilia mauwaji ya aliyekuwa kiongozi wa Lebanon Rafik Hariri, mahakama ambayo ilitazamia kumaliza muhala wake wa kwanza Machi mwaka huu. Mahakama hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inaendesha mashtaka dhidi ya watuhumiwa wa mauwaji ya waziri mkuu huyo [...]

23/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban amtaka msaidizi wake kutembelea Syria kuangalia hali ya misaada ya kibinadamu

Kusikiliza / Valerie Amos

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemwomba mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa kutembelea nchini Syria ili kufanya tathmini namna huduma za kibinadamu kwenye eneo hilo, ambalo linashuhudiwa vikosi vya serikali vikiendelea kuyaandama makundi ya waandamanaji. Ban amemwomba Bi Valerie Amos kwenda nchini humo ili hatimaye kubainisha namna mahitajio ya [...]

23/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laipongeza Yemen kwa kuendesha uchaguzi katika hali ya amani

Kusikiliza / Uchaguzi Yemen

Baraza la usalama limekaribisha hatua ya kufanyika kwa uchaguzi nchini Yemen na limewahimiza vingozi wa kisiasa nchini humo kutorudi nyuma hasa wakati huu kukiwekwa misingi mipya ya kuimarisha demokrasia ya taifa hilo ambalo hivi karibuni lilitumbukia kwenye machafuko ya kiraia. Baraza hilo la usalama limewapongeza wananchi wa Yeme kwa utulivu na usikifu na hatimaye kufanikisha [...]

23/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bahati nasibu ya anwani Uholanza na Sweden yaipa UNHCR karibu euro milioni 4:

Kusikiliza / sweden yafadhili UNHCR

Bahati nasibu za anwani nchini Uholanzi na Sweden kwa mara nyingine zimetoa msaada mkubwa kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Msaada wa karibu Euro milioni 4 kwa shirika la UNHCR unajumuisha fedha kwa ajili ya kuboresha kiwango cha elimu katika kambi kubwa ya wakimbizi duniani. Kwa kusikitishwa na hali katika kambi [...]

23/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakulima wadogowadogo kufaidika na ushirikiano baina ya IFAD na wakfu wa Gates

Kusikiliza / wakulima wadogo wadogo

Taarifa iliyotolewa na mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD inasema ushirikiano imara baina ya wakfu wa Bill na Melinda Gates na mfuko huo unamaanisha kuboresha msaada kwa wakulima wadogowadogo duniani. Taarifa ya muafaka imetiwa saini Alhamisi wakati wa kikao cha baraza la IFAD kwenye makao makuu mjini Roma, kati ya mwenyekiti [...]

23/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mawaziri kwenye mkutano wa UM wakubaliana kuchukua hatua za kuleta maendeleo

Kusikiliza / mkutano, UNEP

Mawaziri wa mazingira kutoka kote duniani wameafikiana kuhakikisha kuwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo utakaoandaliwa nchini Brazil baadaye mwaka huu utafanikiwa kupata suluhu za changamoto za kimazingira duniani.  Mawaziri hao wanasema kwamba mkutano wa Rio +20 ambao utafanyika mjini Rio de Janeiro utakuwa fursa nzuri ya kujadili changamoto za kiuchumi ,kijamii na kimazingira [...]

23/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Togo inafaa kuongeza kiwango cha fedha zinazotumika katika vita dhidi ya Ukimwi:UNAIDS

Kusikiliza / Michel Sidibe

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi Michel Sidibe amesema serikali ya Togo inapaswa kuongeza kiwango cha fedha zinazotumika katika vita dhidi ya ukimwi nchini humo. Sidibe ameyasema hayo alipozuru nchi hiyo na kubaini kwamba Togo inategemea sana fedha kutoka nje ili kufadhili zaidi ya asilimia 80 ya mapambano yake dhidi ya [...]

23/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafungwa 44 wauawa kwenye gereza moja nchini Mexico

Kusikiliza / wafungwa, Mexico

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeutaka utawala nchini Mexico kufanya uchunguzi ulio huru kufuatia mauaji ya wafungwa 44 kwenye gereza moja kaskazini mwa nchi mauaji yaliyotekelezwa na wanachama wa kundi moja lililojihami. Wafungwa wengine 26 wengi wanaokabiliwa na hukumu ya kifo walifanikiwa kutoroka gerezani katika jimbo la Nuevo Leon siku ya [...]

23/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Italia ilikiuka mkataba wa haki za binadamu kwa kuwarejesha wakimbizi wa Somalia na Eritrea

Kusikiliza / wakimbizi wa Somali na Eritrea

Mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya iliyo na makao makuu mjini Strasborg Alhamisi imetoa uamuzi na kuhitimisha kwamba Italia ilikiuka mkataba wa haki za binadamu wa Ulaya ilipoingilia na kuwarejesha Libya kundi la wakimbizi kutoka Somalia na Eritrea. Mahakama imesema Italia ilifanya hivyo mwaka 2009 bila kuangalia endapo kufanya hivyo kutayaweka maisha ya wakimbizi [...]

23/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fursa ya amani imewekwa bayana Somalia: Ban

Kusikiliza / Kongamano la London kuhusu Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameuuambia mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia unaofanyika mjini London kwamba Umoja wa mataifa umefungua mlango kwa ajili ya kupatikana kwa amani na utulivu nchini Somalia. Katika mkutano huo wa Alhamisi unaojumuisha wadau mbalimbali ikiwemo serikali ya mpito ya Somalia, wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa, makundi ya jumuiya [...]

23/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UM yasema kuna ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu Syria

Kusikiliza / wanawake waandamana nchini Syria

Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliosambaa na unaoelekea kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu unatekelezwa nchini Syria kwa ufahamu na ridhaa ya uongozi wa ngazi ya juu wa taifa hilo. Hii ni sehemu ya hitimisho la ripoti ya uchunguzi ya tume iliyoundwa na Umoja wa Mataifa kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria. Grace [...]

23/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maharamia watengeza dola milioni 170 kama fidia kutokana na utekaji nyara wa meli mwaka jana

Kusikiliza / meli iliyotekwa nyara

Maharamia wametengeneza mamilioni ya dola mwaka jana kutokana na utekaji nyara wa meli na wafanyakazi wake. Yury Fedetov ameliarifu Baraza la Usalama juu ya tatizo la uharamia katika pwani ya Somalia, ambalo ni tatizo linaloendelea. Ameonya kwamba biashara hii ya uharamia inafanya bei kuongeza katika pembe ya Afrika. Bwana Fedotov amesema fedha hizi kutoka kwa [...]

22/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakulima wadogo wanaweza kuulisha ulimwengu IFAD

Kusikiliza / Rais wa IFAD Kanayo F. Nwanze

Wakulima wadogo wametakiwa kuchukua wajibu mkubwa katika kuulisha ulimwengu miaka inayokuja. Hili ni kwa mujibu wa wataalamu wanaohudhuria mkutano ulioandaliwa na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD. Huku idadi ya watu duniani ikitarajiwa kugonga watu bilioni 9 ifikapo mwaka 2050 IFAD inasema kwamba wakulima wadogo wanaweza kuchangia kuwepo usalama wa chakula duniani. IFAD inasema [...]

22/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walioathiriwa na mvua wanahitaji msaada nchini Burundi

Kusikiliza / mafuriko nchini Burundi

Takriban watu 2000 waliolazimika kuhama makwao kufuatia mvua kubwa kwenye eneo la Gatumba lililo nje ya mji mkuu wa Burundi Bujumbura kwa sasa wanahitaji chakula na makao. Mvua hiyo iliharibu karibu nyumba 400 na kuna hofu ya kutokea kwa uharibifu zaidi kwenye maeneo yaliyoathirika yakiwemo Kinyinya , Mushasha na Muyange. Nyumba hizo zinazungukwa na maji [...]

22/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Japan yafadhili huduma za afya kwenye kanda ya Gaza

Kusikiliza / Filipo Grandi na balozi wa Japan

Serikali ya Japan imetoa msaada wa dola milioni 10 kwa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA kwa vituo kumi vya afya kwenye ukanda wa Gaza mwaka huu. Makubalino hayo yalitiwa sahihi kwenye mji wa Amman kati ya kamishina mkuuu wa UNRWA Filipo Grandi na balozi wa Japan nchini Jordan Junichi Kosuge.Monica [...]

22/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ziara kuhusu masuala ya nyuklia iliyofanywa Iran yakosa kuzaa matunda

Kusikiliza / Iran

  Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na nishati ya nyuklia limeelezea kuhuzunishwa kwake na kutokuwepo mafanikio wakati wa ziara ya siku mbili iliyofanywa nchini Iran ili na lengo la kubainisha shughuli za kinyuklia za taifa hilo. Kundi la wataalamu kutoka kwa shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA walifanya mazungumzo na maafisa [...]

22/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laongeza wanajeshi wa kikosi cha AMISOM nchini Somalia

Kusikiliza / vikosi vya jeshi, Somalia

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kuongezwa kwa wanajeshi wa kulinda amani kwenye kikosi cha Muungano wa Afrika cha kulinda amani nchini Somalia AMISOM kutoka wanajeshi 12,000 hadi wanajeshi 17,000. Kwenye azimio lililopitishwa leo Jumatano baraza hilo pia liliamua kuongeza usaidizi unaotolewa na Umoja wa Mataifa kwa kikosi hicho. Kikosi cha AMISOM ambacho [...]

22/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko yanahitajika kwenye usimamizi wa masuala ya mazingira duniani

Kusikiliza / nishati safi nchini Afrika

Kunahitajika mabadiliko makubwa ya jinsi ulimwengu unavyosimamiwa iwapo changamoto za dunia zingehitaji kutatuliwa kwa watu bilioni saba. Hii ni kutokana na mapendekezo kutokana na utafiti uliondeshwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kupitia kwa wanasayansi 400 na wataalamu wengine kutoka kote duniani. Mkurugenzi mkuu wa UNEP Achim Steiner anasema kuwa mpango huu [...]

22/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Brazil kufadhili ununuzi wa chakula kwenye nchi tano barani Afrika

Kusikiliza / watoto wanaohitaji chakula

Serikali ya Brazil, inatoa dola milioni 2.3 zitakazotumika kufadhili mpango wa kununua chakula uliobuniwa na shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO na lile la mpango wa chakula duniani WFP ili kuwanufaisha wakulima na watu wanaohitaji chakula kwenye nchi tano barani Afrika zikiwemo Ethiopia, Musumbiji, Niger na Senegal. Mpango huo utanunua chakula [...]

22/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lugha ya Kirusi yakataliwa kama moja ya lugha za taifa nchini Latvia

Kusikiliza / ramani ya Latvia

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa wa masuala kuhusu jamii ndogo Rita Izsak ameitaka serikali ya Latvia kuhakikisha kuwa imelinda haki za jamii ndogo zinazotumia lugha ya kirusi na kufanya mazungumzo baada ya kura ya maoni ya Februari 18 iliyokataa pendekezo la kuitambua lugha ya kirusi kama lugha ya pili ya taifa. Bi Izsak amesema [...]

22/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Brazil ndiyo itakuwa mwandalizi wa siku ya mazingira duniani

Kusikiliza / unep-brasil1

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limetangaza kuwa taifa la Brazil ambalo ni moja ya mataifa yaliyo na uchumi unaokua kwa haraka zaidi duniani itakuwa mwandalizi wa siku ya mazingira duniani mwaka 2012 ambayo itaadhimishwa tarehe 5 mwezi Juni. Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Uchumi usioathiri mazingira: Inakuhusu wewe ?’ ina lengo [...]

22/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ataka mashirikiano ya kimataifa kukabili wimbi la uhalifu na usafirishaji wa madawa ya kulevya

Kusikiliza / Ban Ki-moon, uhalifu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka mashirikiano ya pamoja katika uga wa kimataifa ili kuzikabili hujuma na changamoto zinazotokana na ongeko kubwa la uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha ongezeko la kasi la vitendo vya uhalifu, usafirishaji wa madawa ya kulevya na kukua kwa kasi kwa matukio ya [...]

22/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wataka wahusika wa uchomaji Koran Afghanistan washughulikiwe

Kusikiliza / Mwakilishi UM, Afghanistan, Jan Kubis

Umoja wa Mataifa umesema kuwa unamatumaini umoja wa kujihami NATO uanoongoza vikosi vya kijeshi nchini Afghanistan utachukua hatua muhimu ili kuwawajibisha wale wote waliohusika na uchomaji moto wa vitabu vya Korani Kabul ambako kumesababisha maandamano makubwa na watu kadhaa kupoteza maisha. Sehemu ya vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo imetangaza kuanzisha uchunguzi wa haraka [...]

22/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aitaka Morocco kutekeleza sera zinazozingatia usawa wa kijinsia

Kusikiliza / wanawake, Morocco

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binadamu ameitolea mwito Morocco kuweka mipango mahususi kwa shabaha ya kusogeza mbele mafanikio ya wanawake hasa kwa kuyatupia macho maeneo ya kisheria ambayo yanakwamisha ustawi wao. Kamala Chandrakirana amesema kuwa mifumo ya kisheria na taratibu zilizopo nchini Morocco siyo tu zinawaweka  wanawake kando, lakini pia [...]

22/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanajeshi wa UNAMID warejea nyumbani

Kusikiliza / Ibrahim Gambari, UNAMID

Baada ya mazunguzmo marefu sasa kundi la wanajeshi 55 wa kupiga doria wa kikosi cha pamoja cha Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur UNAMID ambacho kilikuwa kimezuiwa na wanamgambo waliokuwa wamejihami kaskazini magharibi kwa muda wa siku mbili sasa kimeelekea kwenye makao yake kwenye eneo la Umm [...]

21/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa amani wa UM awataka wasanii wachanga kuchora picha za ulimwengu usio na zana za kinyuklia

Kusikiliza / Michael Douglas

Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Michael Douglas ametoa wito kwa watoto kutoka kote duniani kuwasilisha fikra zao kwa njia ya sanaa kuhusu ni vipi ulimwengu  usio na zana za kinyuklia utakavyokuwa. Bwana Douglas ambaye amehudumu kama mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1998 ametoa ujumbe kupitia kwa ukanda wa video [...]

21/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama

Kusikiliza / lugha ya mama

Umoja wa Mataifa hii leo unaadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya mama ambapo ina wajibu wa kuonyesha umuhimu na manufaa ya elimu kwa maendeleo pamoja na katika kulinda lugha za mama. Kwa mujibu wa  shirika la elimu , sayansi na utamadini la Umoja wa Mataifa UNESCO ni kuwa kati ya lugha 6000 za mama [...]

21/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM aitaka Israel kumwachilia huru mfungwa wa Kipalestina aliye kwenye mgomo wa kula

Kusikiliza / khader-adnan,mgomo wa kutokula

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayejishughulisha na haki za binadamu katika mamlaka ya Palestina amerejelea tena mwito wake kuitaka Israel kumwachilia huru mfungwa wa Kipalestina ambaye yupo kwenye mgomo wa kutokula chakula. Mjumbe huyo Richard Falk amesema Israel inapaswa kumwachilia huru mfungwa huyo Khader Adnan ambaye anaripotiwa kudhoofika kwa hali ya afya yake kutokana [...]

21/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Onyo la kutokea mafuriko latolewa Ulaya

Kusikiliza / barafu

Onyo la kutokea kwa mafuriko limetolewa kwenye maeneo ya mashariki na kati kati mwa Ulaya wakati barafu iliyoanguka wakati wa kipindi cha msimu wa baridi inapoanza kuyeyuka. Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mjanga inasema kuwa nchi zinazopakana na mto Danube ziko kwenye hatari kubwa ya kufurika. Ofisi hiyo inasema kuwa inatarajia viwango vikubwa [...]

21/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa kipindupindu wasambaa DRC

Kusikiliza / ugonjwa wa kipindipindu nchini DRC

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa ugonjwa wa kipindupindu umeripotiwa kwenye eneo la Bas-Congo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo tangu mwanzo wa mwaka huu ambapo kumeripotiwa visa 125 na vifo vya watu watano huku ugonjwa huo ukisambaa kwenye mikoa tisa kati ya mikoa 11. Kwa muda wa miezi sita zaidi ya dola milioni [...]

21/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wazitaka pande zinazopigana Sudan Kusini kusaka njia mwafaka ya kutanzua mizozo

Kusikiliza / mjumbe maalum wa UM Sudan,hilde johnson

Maafisa wa Umoja wa Mataifa walioko huko Sudan Kusini wamezionya pande zinazopigana kutafuta njia mwafaka ya kupatikana kwa suluhu na hatimaye kutuma ujumbe utaotafsiri maridhiano yanayoweza kupatikana bila kuendelea kuathiri mamia ya watu. Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa pande zinazozozana zina kila sababu ya kumaliza mkwamo huo kwa njia ya maelewano na [...]

21/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Japan yafadhili miradi ya maji nchini Somalia

Kusikiliza / maji safi

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha uchunguzi wa miezi mitatu kuhusu usambazaji wa maji na usafi kwa wakimbizi wa ndani wanaoishi kwenye vitongoji vya mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Mpango huo umefadhiliwa na taifa moja kutoka Japan ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwepo kwa huduma bora za maji zitakazowafaidi maelfu ya watu kweye mji [...]

21/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na mwanadiplomasia wa Misri

Kusikiliza / Abdulaziz Al-Nasser

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Misri kujadilia hali ya kisiasa nchini humo wakati ambapo vugu vugu la mageuzi katika mataifa ya kiarabu likitoa taswira mpya ya mageuzi. Wakikutana katika mji mkuu Cairo, viongozi hao rais Nassir Abdulaziz Al-Nasser na mwenyeji wake wamejadilia [...]

21/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tanzania yafungua kituo cha uhamiaji kilichojengwa na ufadhili kutoka Japan

Kusikiliza / ramani ya Tanzania

Taifa la Tanzania linatarajiwa kufungua makao mapya ya uhamiaji na polisi kwenye eneo la Kilwa Masoko na Kilwamba yaliyojengwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ikiwa ni sehemu ya mradi wa uhamiaji uliofadhiliwa na serikali ya Japan. Mradi huo ulianzishwa ili kuwasaidi wahamiaji waliokwama hasa kutoka kwa pembe ya Afrika wanaopitia Tanzania wakiwa na [...]

21/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yaomba misaada ya kusaidia mataifa kwenye eneo la Sahel

Kusikiliza / Sahel_watoto

Maisha ya karibu watu milioni moja kwenye eneo la Sahel barani Afrika yako hatarini kutokana na kuwepo utapiamlo na magonjwa yanayoambukiza.Mashirika ya Umoja wa Matifa katika eneo hilo yanasema kuwa ukosefu wa ufadhili wa kutosha umekuwa kizuizi katika utoaji misaada kwa watoto huku hali hiyo ikiendelea kuwa mbaya kila siku. Shirika la afya duniani WHO [...]

21/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM walitaka bara la Afrika kuwekeza zaidi kwenye nishati safi

Kusikiliza / nishati safi barani  Afrika

Sera za serikali zinazochangia uwekezaji wa kibinafsi kwenye kawi ni muhimu katika kupunguza umaskini kwenye bara la Afrika na kulielekeza kwenye maendeleo. Hii ni kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo. Wataalamu wanasema kwamba ikiwa hatua mwafaka hazitachukuliwa nusu ya watu wote kwenye bara la Afrika bado watakuwa bila umeme ifikapo mwaka [...]

21/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dunia kujadili hatma ya Somalia mjini London

Kusikiliza / wakimbizi katika kambi ya dadaab

  Viongozi kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanatarajiwa kukutana mjini London juma hili ili kujadili hatma ya taifa la Somalia ambalo kwa muda wa zaidi ya miaka 20 iliyopita limekumbwa na mapigano na kupelekea mamilioni ya watu kuhama makwao suala ambalo pia limechangiwa na ukame pamoja na njaa.  Taifa la Kenya ambalo linapakana na [...]

21/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM wazungumzia kufungwa kwa watetesi wa haki za binadamu nchini Syria

Kusikiliza / Baraza kuu

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameshutumu kukamatwa kwa takriban watu 16 wakiwemo watetesi maarufu wa haki za binadamu nchini Syria wakisema kuwa huenda watu hao wakateswa. Wanasema kuwa huenda watu hao wamekamatwa kutokana na sababu zinazohusiana na uhuru wa kujieleza na shughuli za kutetea haki za binadamu. Wataalamu hao wanaongeza kuwa utawala nchini Syria [...]

21/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya waandishi habari wawili Brazil

Kusikiliza / magazine

Mkrugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, Irina Bokova, amelaani mauaji ya waandishi habari wawili nchini Brazil mwezi huu na kutoa mwito uchunguzi wa kina ufanywe kuhusu uhalifu huo. Bi. Bokova amesema amesikitishwa sana na vifo vya Paulo Roberto Cardoso Rodrigues, aliyeuawa tarehe 12 Februari, na Mario Randolfo [...]

21/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mataifa ya kusini mashariki mwa Asia yataka uwekezaji zaidi katika kupunguza majanga

Kusikiliza / majanga

Maafisa wa ngazi za juu serikalini kutoka eneo la kusini mashariki mwa Asia wametaka kuwe na uwekezaji katika maandalizi dhidhi ya majanga kwa minajili ya kulinda uchumi na masuala mengine ya kijamii. Wawakilishi kutoka mataifa yakiwemo Brunei, Darusssalam, Cambodia, Jamhuri ya Lao, Myanmar, Ufilipino, Timor-Leste, Thailand na Viet Nam walikutana kwenye warsha iliyoandalia na tume [...]

20/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huenda janga la Ukimwi likawa mbaya zaidi ikiwa halitashughulikiwa:De Lay

Kusikiliza / Paul de Lay

Nchi zinazoendelea zinahitaji kuendelea na jitihada zao za kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwa kuwa huenda janga la ukimwi likawa baya zaidi ikiwa zitasitisha jitihada zao. Onyo hilo limetolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa Paul De Lay ambaye amesema kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa kwenye [...]

20/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suluhu zinahitajika kwa lengo la kuafikia maendeleo:Ban

Kusikiliza / Ban akitembelea kiwanda cha mvuke, Kenya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amewataka viongozi wa dunia kutafuta suluhu kwa minajili ya kuafikia maendeleo. Ban ameyasema hayo kwenye ujumbe wake kwa mkutano wa baraza la shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP uliondaliwa mjini Nairobi nchini Kenya. Monica Morara anaripoti. (SAUTI YA MONICA MORARA)

20/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Saudi Arabia yatoa misaada ya kufadhili huduma kwa wakimbizi wa kipalestina

Kusikiliza / watoto wa shule

Taifa la Saudi Arabia kupitia kwa mfuko wa maendeleo wa taifa hilo umetoa msaada wa dola milioni kumi kufadhili mipango ya shirika la kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina kwenye ukanda wa Gaza na ukingo wa Magharibi. Makubaliano hayo yalitiwa sahihi hii leo mjini Riyadh na fedha hizo zitatumika katika kununua vifaa vinavyohitajika kwenye elimu kama vile [...]

20/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa shirika la misaada ya dharura asikitikia hali mbaya Sudan

Kusikiliza / msaada Sudan Kusini, Kordofan

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa shirika la misaada ya kibinadamu ameelezea kile alichokiita kupindukia kwa hali ya ubinadamu katika jimbo la Kordofan lililoko Sudan Kusini ambalo linaandamwa na machafuko. Bi Valerie Amos amesema hali jumla kwenye jimbo hilo na lile la Blue Nile ni ya kukatisha tama katika wakati ambapo hali ya utengamao wa [...]

20/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha hatua ya kuwahamisha kwenye makazi mapya wahamiaji wa Iran walioko Iraq

Kusikiliza / Martin Kobler

Umoja wa Mataifa umekaribisha mpango ulianza kutekelezwa leo nchini Iraq wa kuwatafutia makazi mapya wananchi wa Iran waliowekwa kwenye kambi moja ijulikanayo Ashraf, na kusema kuwa hatua hiyo ni mwanzo mpya wa matumaini. Jumla ya raia 400 wamehamishiwa kwenye maeneo mapya, ikiwa ni moja ya utekelezwaji wa makubaliano yaliyoingiwa hivi karibuni baina ya Umoja wa [...]

20/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanariadha washiriki katika kuadhimisha miaka 40 ya shirika la UNEP

Kusikiliza / nembo ya UNEP

Mamia ya wanariadha wameshiriki katika mbio za kuadhimisha miaka 40 tangu kuundwa kwa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP. Zaidi ya wakimbiaji 200 wameshiriki katika mashindano ya mbio za nusu-marathon mjini Nairobi, ambao ndio makao makuu ya UNEP, huku wengine zaidi ya 300 wakitimua mbio za kilomita tano kujiridhisha wenyewe, UNEP imesema. Washindani [...]

20/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban asifu makubaliano ya kisiasa nchini Somalia

Kusikiliza / makubaliano nchini Somalia

Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema ameridhishwa na makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa katika mkutano wa kikatiba nchini Somalia. Amesema kwamba ni hatua muhimu katika jitihada za kumaliza kipindi cha serikali ya sasa ya mpito na kuleta mfumo mpya wa kikatiba. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake,  Ban amesema wadau walioshiriki katika mkutano huo uliomalizika Ijumaa mjini [...]

20/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuadhimisha Siku ya Urithi duniani

Kusikiliza / makazi duni

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ametaka kuwepo maendeleo ya kiuchumi ili kuhakikisha kuwepo kwa urithi duniani. Kwenye ujumbe wake wakati wa maadhimisho ya siku ya urithi duniani inayoadhimishwa tarehe ishirini ya kila mwezi Februari kila mwaka Ban amesema kuwa mabadiliko makubwa yameshuhudiwa duniani hasa misururu ya maandamanio iliyoshudiwa kwenye nchi kadhaa. [...]

20/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kongamano la UM juu ya ukuzaji sekta ya madini lafikia tamati Tanzania

Kusikiliza / madini

Kamishna ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya uchumi kwa kanda ya afrika, imehitimisha mkutano wake wa 16 jijini Dar es salaam ambako imesisitiza haja ya kuimarisha sekta ya madini kwa ajili ya kukuza maendeleo barani humo. (SAUTI GEORGE NJOGOPA) Mkutano huo ulioduma kwa muda wa juma moja, umewaleta pamoja mawaziri wa masula ya [...]

17/02/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Walibya wanaelekea kuwa na demokrasia :BAN

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Ban Ki-moon Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki –moon hii leo ameadhimisha mwaka mmoja tangu kuanza mapinduzi nchini Libya ambapo amewataka wananchi wa Libya kushirikiana ili kuwa na demokrasia iliyopatikana kwa njia ya haki. Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kutoa usaidizi wake nchini Libya wakati wa kipindi cha mabadiliko hasa kwenye [...]

17/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WMO yakaribisha matokeo ya mkutano wa radio duniani wa mwaka 2012

Kusikiliza / masafa ya radio

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO hii leo limesema kuwa litalinda matumizi ya masafa ya radio yaliyomuhimu katika kuielewa dunia, anga na bahari na kupunguza hatari zinazotokana na hali ya hewa na maji. Mkutano wa 12 wa radio duniani ulitaka kutumika kwa ahadi za awali za mikutano kuhusu mawasiliano ya radio wakati [...]

17/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wataka kuwepo mkataba dhabiti kuhusu biashara ya silaha

Kusikiliza / Umoja wa Mataifa

Wakuu wa mashirika kadha ya kibinadamu , maendeleo na haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa wanaotoa huduma kubwa wamependekeza masuala kadha yatakayojumuishwa kwenye mkataba wa biashara ya silaha hasa kufuatia athari za kimaendeleo za biashara hii isiyo na usimamizi mwema.Wakuu hao wamesema kuwa sheria za sasa za kudhibiti biashara ya silaha hazina uwezo. Wameongeza [...]

17/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Suala la njaa nchini Niger:UNDP na OCHA

Kusikiliza / njaa Niger

Mratibu wa shirika la maendelo la Umoja wa Mataifa UNDP Helen Clark na mkuu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Valerie Amos wamewasili hii leo kwenye mji wa Niamey kwa ziara ya pamoja ya siku mbili kungazia ukosefu wa chakula nchini Niger na kwenye eneo la Sahel. Idadi kubwa [...]

17/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maafisa kwenye Umoja wa Mataifa wazungumzia kura kuhusu Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na rais wa Baraza Kuu Nassir Abdulaziz Al- Nasser

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameizungumzia kura iliyopigwa siku ya Alhamisi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kushutumu vikali dhuluma na ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini Syria. Ban amesema kuwa wakati wananchi wa Syria wanapoendelea kupitia dhuluma na mateso litakuwa jambo la busara ikiwa ulimwengu utaungana ili kumaliza [...]

17/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

OCHA ina miradi ya kusaidia watu kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / watu wanaohitaji msaada

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limesema kuwa suala la kibinadamu lizalosababishwa na mzozo kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati ndilo lililosahaulika zaidi barani Afrika linalopokea chini ya asilimia 50 ya ufadhili. IOM kwa ushirikiano na serikali na washirika wengine wa kibinadamu wametoa ombi la kufadhili miradi 105 itakayochukua muda [...]

17/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake lazima wafikiwe na huduma za kitabibu-UM

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu UNAIDS, Michel Sidibe

Wanawake lazima wafikiwe na huduma za kitabibu-UM Umoja wa Mataifa umerejelea wito wake wa kutaka wanawake wafikiwa kirahisi na huduma za kitabibu ikiwemo kusambaziwa mipira itayowasaidia kuondokana na mimba zisizo za lazima na kuepuka maambukizi ya virusi vya HIV. Wakikutana kwa pamoja kwenye majadiliano ya kitaalamu yaliyoandaliwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana [...]

17/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ulimwengu usio na zana za nyuklia ndio salama:Ban

Kusikiliza / majaribio ya nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ulimwegu utakuwa salama zaidi bila ya silaha za kinyuklia. Akiongea mjini Vienna Ban amesema kuwa mikataba ya kumaliza zana za kinyuklia ni muhimu katika kuleta amani duniani. (SAUTI YA BAN KI-MOON) Ban alikuwa akuhutubia mkutano wa kusherekea miaka 15 tangu kutolewa marufuku ya majaribio ya silaha [...]

17/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Radio ni daraja la mawasiliano kwa mamilioni ya watu

Kusikiliza / Siku ya Radio duniani

Kwa mara ya kwanza wiki hii dunia imeadhimisha siku ya Radio duniani, ikienda sambamba na miaka 66 tangu kuanzishwa Radio ya Umoja wa Mataifa. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO liliamua kuitenga Februari 13 kuwa siku ya Radio duniani kwa lengo la kusherehekea mchango wa Radio, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa [...]

17/02/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wanawake wa Uganda wanaosafirishwa ng’ambo yaongezeka:IOM

Kusikiliza / usafirishaji kiholela wa binadamu

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeelezea wasiwasi wake kufuatia idadi kubwa ya wanawake wanaosafirishwa kiharamu kwenda nchi za ngambo kutoka nchini Uganda hasa kwenda nchi za bara Asia. Kati ya wale shirika la IOM limesaidia kurejea nchini Uganda wamesema kuwa walipitia mateso, dhuluma za kingono na pia walibakwa. Kwa muda wa miezi minne waathiriwa [...]

17/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yawalazimu wakimbizi kurudi tena mjini Mogadishu

Kusikiliza / kambi ya wasomali Mogadishu

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa maelefu ya wakimbizi wa ndani waliohama makwao nchini Somalia kwa sasa wanazidi kuukimbia mzozo katika eneo la Afgooye lililo Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu. Eneo la Afgooye lililo na barabara yenye urefu wa kilomita 40 iliyo na kambi ni makao kwa karibu watu 410,000 [...]

17/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Waziri wa Kyrgyzstan kujadili amani na usalama

Kusikiliza / Ban kyrgystan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Kyrgstan Ruslan Kazakbaev ambako wamejadili masualambalimbali ikiwemo juhudi za kukabiliana na ongezeko usafirishwaji wa madawa ya kulevya.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, viongozi hao wamejadiliana kuanza hatua ya kurejeshwa hali ya utengamano nchini Kyrgistan, mpaka eneo [...]

17/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Nchi za Amerika Kusini zatakiwa kuboresha hali magerezani

Kusikiliza / vifo magerezani

Nchi zilizo kwenye bara la Amerika kusini zimetakiwa kuboresha hali kwenye magereza yao na vituo vingine kufuatia kisa ambapo wafungwa waliangamia kwenye mkasa wa moto kwenye gereza moja nchini Honduras. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Matifa pia inasema kuwa kuna visa vingi vya ghasia ndani ya magereza suala ambalo inasema linachangiwa na [...]

17/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aonya juu ya kuendelea kupuuza kilio cha wanawake na vijana

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban akiwa Vienna

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea haja ya ulimwengu kuwawezesha wanawake na vijana, ambao ndiyo chimbuko kubwa la wimbi la mageuzi yanayoshuhudiwa sasa ulimwenguni kote. Aidha Ban ameonya juu ya kile alichokiita kuendelea kuyapuzia makundi ya watu hao akisema kuwa ni kukaribisha mkwamo unaweza kuvuruga shughuli za maendeleo kwa taifa. Amesema sauti [...]

17/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza kuu lapitisha mswada wa azimio dhidi ya Syria

Kusikiliza / Baraza Kuu la UM

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Alhamisi jioni limepiga kura kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kupitisha mswaada wa azimio dhidi ya Syria. Azimio hilo linalaani vikali kampeni ya mauaji na utesaji ya miezi 11 inayoendeshwa na utawala wa Rais Bashar Al-Assad. Azimio linamtaka ksitisha mara moja mauaji dhidi ya raia, kuwaachia wafungwa wote [...]

16/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakamilisha ziara ya siku nne nchini Haiti

Kusikiliza / Haiti

Baraza la Usalama linatarajiwa kukamilisha ziara yake nchini Haiti leo Alhamisi. Wanachama wa baraza wamekutana na rais wa Haiti Michel Martelly, na kuitembelea miji iliyoathirika vibaya kutokana na tetemeko la ardhi Januari mwaka 2010 na ambapo watu 200,000 waliuawa. Pia wamekitembelea kijiji ambacho kitajengwa nyumba zitakazo stahimili kimbuga na tetemeko la ardhi kwa ajili ya  familia 200 [...]

16/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu akutana na Waziri Mkuu na maafisa wa serikali ya India

Kusikiliza / RIO+20

Rais wa Baraza Kuu Nassir Abdulaziz Al-Nasser amehitimisha ziara ya siku tatu nchini India. Leo amekuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Dr Manmohan Singh ambapo wamejadili mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa, hali ya uchumi duniani, mkutano ujao wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Rio+20 na hali ya Mashariki ya Kati. Rais [...]

16/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukame Sahel

16/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya UM yatangaza tarehe ya kusikilizwa kesi ya Ratko Mladic

Kusikiliza / chumba cha ICTY

Mahakama ya Umoja wa Mataifa iliyobuniwa wakati wa mizozo ya miaka ya tisini ya Balkan imetangaza kuwa kesi ya aliyekuwa mkuu wa majeshi nchini Serbia Ratko Mladic ambaye anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu mwingine wa kivita itaanza mnamo tarehe 14 mwezi Mei mwaka huu. Kupitia taarifa iliyotolewa na mahakama ya kimataifa [...]

16/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Chama cha posta cha UM chamiliki muhuri wa kwanza duniani

Kusikiliza / muhuri

Chama cha Posta cha Umoja wa Mataifa kimetangaza kuwa kwa sasa kinamiliki kile kilichotaja kama muhuri maarufu zaidi duniani uliotolewa miaka 172 iliyopita na ulio na picha ya Victoria, ambaye ni malkia wa zamani wa uingereza. Kando na muhuri huo pia chama hicho kwa sasa kinamiliki mihuri mingine miwili iliyo na picha za Victoria na [...]

16/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM waonya juu ya misongamano kwenye magereza barani Amerika Kusini

Kusikiliza / haki za binadamu

Maafisa wanaohusuka na masuala ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa wamezitaka nchi za Amerika Kusini kutafuta suluhu la tatizo la misongamano kwenye magereza kufuatia mkasa ambapo mamia ya wafungwa waliangamia baada ya moto kuteketeza gereza moja nchini Honduras. Zaidi ya wafungwa 300 waliripotiwa kuangamia kwenye mkasa huo uliotokea kaskazini mwa mji mkuu Tegucigalpa [...]

16/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yataka msukumo utolewe kutokomeza ukoma pacific

Kusikiliza / wauguzi wa ugonjwa wa ukoma wasubiri matibabu

Shirika la afya duniani WHO limetoa wito wa kuwepo na msukumo wa mwisho ili kutokomeza ukoma ambao ni tishio la afya ya jamii katika kanda ya Magharibi mwa Pacific ambako zaidi ya visa vipya 5000 vya ugonjwa huo unaotibika vinaripotiwa kila mwaka. Idadi ya wanaouugua ukoma duniani kote imepungua tangu mwaka 1991 wakati ambapo WHO [...]

16/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM waeleza masikitiko yake kufuatia vifo vya watoto ukingo wa magharibi:

Kusikiliza / Filippo-Grandi -UNRWA

Filippo Grandi, UNRWA Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA , Alhamisi ameelezea masikitiko yake kufatia taarifa za vifo vya watoto na watu wazima katika ajali ya barabani kwenye Ukingo wa Magharibi. Watoto takribani wanane wamearifiwa kufariki dunia baada ya basi la wanafunzi kugongana na lori la Israel [...]

16/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wadau wa habari wakutana UNESCO kujadili maadili baada ya kashfa ya ‘News of the World’ na ‘Wikileaks’:

Kusikiliza / 'weakileaks' UNESCO

Wataalamu na wakurugenzi wa vyombo mbalimbali vya habari duniani, wanazuoni, wataalamu wa sheria za habari na wawakilishi wa mashirika yanayopigania uhuru wa vyombo vya habari wanakutana kujaribu kudadisi mustakhabali wa taaluma ya uandishi habari katika mazingira ya maendeleo ya teknolojia na mfumo wa ‘digital’. Mkutano huo wa siku mbili utakaomalizika Ijumaa unaofanyika kwenye makao makuu [...]

16/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa kibinadamu umeanza kuwafikia watu wa Homs na Bludan:ICRC

Kusikiliza / nemba ya ICRC

Wafanyakazi wa kujitolea wa shirikisho la chama cha msalaba mwekundu katika nchi za Kiarabu wameanza kusambaza msaada wa chakula, madawa, mablanketi, vifaa vya usfi na vitu vingine kwa maelfu ya watu ambao wameathirika na machafuko yanayoendelea nchini Syria. Msafara uliosheheni msaada huo umewasili kwenye mji wa Homs na Bludan. Kwa mujibu wa mkuu wa ICRC [...]

16/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wabunge wa Afrika na viongozi walioko nje ya nchi wajadili kuimarisha ushirikiano:

Kusikiliza / nemba ya Muungano wa Afrika

Wabunge kutoka Afrika na Waafrika wanaoishi nje wamekutana Alhamisi ya leo mjini New York wakijadili njia za kuwawezesha watu wenye asili ya Afrika duniani kote kuchangia maendeleo ya Afrika. Mkutano huo pia umewaleta pamoja wataalamu na wawakilishi wa jumuiya za kijamii kutoka barani Afrika na za Waafrika wanaoishi ughaibuni. Dr Idriss Mossa Ndele ambaye ni [...]

16/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jinsi suluhu ya mgogoro wa Syria inavyochelewa, maisha ya watu yanazidi kupotea:Ban

Kusikiliza / Mgogoro unaokumba nchi ya Syria

Mgogoro unaokumba nchi ya Syria Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anaendelea kutoa hofu na kiwango cha ghasia na ongezeko la kupotea kwa maisha ya watu nchini Syria. Kwa mara nyingine Ban ameitolea wito serikali ya Syria kutekeleza sheria za kimataifa mara moja na kukomesha mashambulizi na matumizi ya nguvu dhidi ya [...]

16/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na viongozi wa Somalia wajadili katiba mjini Garowe

Kusikiliza / Mahiga na viongozi wa Somalia

Viongozi wa Kisomali wanakutana katika siku ya pili mjini Garowe Puntland kwenye mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa wakijadili suala la katiba. Mktano huo unaoendeshwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga umewaleta pamoja pande zote muhimu za Somalia wakiwemo serikali ya mpito, viongozi wa Puntland na Galmudug, pamoja na [...]

16/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mihadarati ni tishio kwa maendeleo ya Afghanistan na jirani zake:Ban

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Ban Ki-moon Afghanistan inakabiliwa na moja ya matatizo makubwa ya matumizi ya kasumba na watu kuathirika na mihadarati duniani amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Akizungumza Alhamisi kwenye ufunguzi wa mkutano wa tatu wa ngazi ya mawaziri ujulikanao kama Paris Pact mjini Vienna , amesema nchi hiyo pia inakabiliwa na tatizo la [...]

16/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka kuharakishwa zoezi la ugawaji makazi kwa raia wa Iran wanaishi uhamishoni Iraq

Kusikiliza / kambi nchini Iran

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitolea mwito serikali ya Iraq ianzishe mpango wa kugawa upya makazi kwa mamia ya wahamiaji wa Iran wanaoishi nchini Iraq katika kambi inayojulikana Ashraf . Ban amesema kuwa pande zote mbili serikali pamoja wakazi kwenye kambi hiyo kuonyesha mashirikiano ya karibu ili kufanikisha zoezi la ugawaji wa [...]

16/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ahofia machafuko mapya yaliyozuka Bahrain

Kusikiliza / KM Ban Ki -moon

Katibu Mku wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea hofu yake kuhusu taarifa za kuzuka kwa machafuko mapya nchini Bahrain kati ya majeshi ya salama na waandamanaji, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya machafuko yaliyoambatana na wimbi kubwa la maandamano kwa mara ya kwanza Mashariki ya Kati. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban [...]

15/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kamishna ya UM kwa Afrika yaendesha mkutano wake Tanzania

Kusikiliza / nishati barani Afrika

Kamishna ya Umoja inayohusika na masuala ya uchumi kwa kanda ya Afrika, imeanza mkutano wake 16 jijini Dar es salaam ikiwakutanisha wataalamu wa maendeleo na sekta ya nishati na madini ili kujadilia mipango ya kusukuma mbele ustawi wa bara hilo. George Njogopa na taarifa zaidi. ( GEORGE NJOGOPA ANARIPOTI)

15/02/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Muungano wa Afrika kufanya mkutano wa kwanza unaojumuisha waafrika walio ughaibuni

Kusikiliza / nemba ya Muungano wa Afrika

Mwezi Juni mwaka huu Muungano wa Afrika utafanya mkutano wa kwanza utakaohusu Waafrika walio ughaibuni. Mkutano huo wa ngazi ya wakuu wa nchi na serikali unakuwa na jukumu la kuanzisha ushirikiano kati ya wabunge walio Afrika na wabunge wanaoishi katika sehemu mbalimbali duniani. Mkutano huo utakaofanyika Midrand nchini Afrika ya Kusini una lengo la kuweka [...]

15/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walionya bara la Ulaya juu hatari ya kiafya kwa watu maskini

Kusikiliza / barafu

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kuwa kila kati ya watu watano walioko barani Ulaya mmoja kati yao hufariki duniani kutokana na matatizo yanayofungamana na hali ya mazingira. Katika taarifa yake WHO imeongezeka kusema kuwa jamii za watu maskini ndiyo walioko kwenye mkondo hatarishi zaidi. Kwenye ripoti yake mpya iliyoangazia hali ya mazingira na afya [...]

15/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM yatilia shaka juu ya kuzorota kwa hali ya ustawi wa kibidamu Yemen

Kusikiliza / watoto walio na utapiamlo nchini Yemen

Huku mamia ya raia wakiendelea kuathiriwa kutokana na ghasia zinazoendelea kujiri Kusini mwa Yemen, Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kupundukia kwa janga la kibinadamu katika wakati kunarifiwa pia kuanguka kwa huduma za kijamii kama maji, na mahitaji mengine. Kwa mujibu wa kitendo cha Umoja wa Mataifa cha kushughulikia majanga ya kibinadamu OCHA, zaidi ya [...]

15/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Finland zaongoza takwimu za UNCTAD za taarifa na teknolojia ya mawasiliano

Kusikiliza / nembo ya UNCTAD

Finland inaongoza duniani kwa mchango wake wa kichumi utokanao na uzalishaji wa bidhaa na huduma zinazohusiana na taarifa na teknolojia ya mawasiliano ICT, kwa mujibu wa takwimu za karibuni zilizotolewa na tume ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD. Takwimu hizo zilizotolewa Jumatano kwenye mtandao zinaonyesha kwamba teknolojia ya mawasiliano nchini Finland inatoa [...]

15/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshauri wa UM aonya juu ya uwezekano wa mgawanyiko wa kidini Syria

Kusikiliza / Syria

Machafuko ya umwagaji damu yanayoendelea nchini Syria yanatishia kuligawa mapande taifa hilo katika misingi ya kidini na kikabila, ameonya afisa wa Umoja wa mataifa, akiitaka jamii, viongozi wa kidini na makundi ya kijamii kuwa msitari wa mbele katika kupunguza mvutano kwenye jamii. Edward Luck mshauri maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu wajibu wa kulinda amekiambia kituo [...]

15/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aupongeza mkataba wa Tlatelolco uliochangia kutokuwepo zana za kinyuklia Amerika Kusini

Kusikiliza / majaribio ya nyuklia

Ikiwa ni miaka 45 ya kuadhimisha mkataba uliochangia kutokuwepo kwa zana za kinyukilia kwenye bara la America Kusini na Caribbean Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameusifu mkataba huo na kuutaja kama mfano wa jinsi jitihada za maeneo zinaweza kuhakikisha kutokuwepo kwa zana za kinyuklia na matumizi ya amani ya nishati ya [...]

15/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNESCO yaomboleza kifo cha msanii Erik Reitzel

Kusikiliza / mviringo wa dunia

Mkuu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova ametoa heshima zake kwa msanii na mhandisi Erik Reitzel raia wa Denmark aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 71 akisema kuwa msanii huyo alichangia makubwa kwa shirika hilo. Bokova ameelezea huzuni yake kufutia kifo cha msanii huyo ambapo alituma [...]

15/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF na washirika wengine kutoa msaada kwa waathiriwa wa kimbunga nchini Madagascar

Kusikiliza / ramani ya Madagascar

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na ofisi inayohusika na masuala ya dharura na washirika wengine wa kutoa huduma za kibinadamu wanajiandaa kwa oparesheni za kusaidia watu walioathiriwa na kimbunga Giovani kilichoikumba Madagascar hii leo. Kimbunga hicho kulichokuwa kwenye kiwango cha nne kilitokea masaa ya usiku umbali wa kilomita 100 kutoka mji [...]

15/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aikosoa Hungary kwa kufanya kutokuwa na makazi ni uhalifu wa jinai

Kusikiliza / Raquel Rolnik

Watu takribani 35,000 wasio na makazi nchini Hungary wanakabiliwa na faini na vifungo kufuatia hatua ya bunge la nchi hiyo kupitisha sheria zinazofanya hali ya kutokuwa na makazi kama ni uhalifu au kosa la jinai. Wataalamu wawili wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wanasema sheria hizo zinazopinga hali ya kutokuwa na makazi sio [...]

15/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa kimataifa waombwa kwa mfungwa wa Kipalestina aliye katika mgomo wa kula

Kusikiliza / Richard Falk

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu kwenye himaya ya Palestina inayokaliwa tangu mwaka 1967, bwana Richard Falk ameelezea hofu yake kuhusu hali ya mfungwa wa Kipalestina Khader Adnan aliye katika mgomo wa kula. Falk ameitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia ili kusaidia haraka hali hiyo. Amesema mataifa yaliyo na uhusiano [...]

15/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wito wa hatua za pamoja za haraka umetolewa kulinusuru eneo la Sahel:WFP

Kusikiliza / njaa katika eneo la Sahel

Wawakilishi wa mashirika ya msaada wa kibinadamu na serikali wahisani wanakutana mjini Roma Italia kuanzia leo Jumatano kujadili tatizo linalotishia maisha la upungufu wa chakula kwenye eneo la sahel barani Afrika. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambalo ndio mwenyeji wa mkutano huo linafanyia kazi mipango ya kuwalisha watu milioni 8 katika eneo hilo [...]

15/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atoa wito katika mkutano wa biashara wa kukumbatia makampuni ya uendelevu

15/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Usalama waelezea hofu yao kuhusu utapia mlo Kordofan Kusini

Kusikiliza / utapiamlo

Wajumbe wa Baraza la Usalama wameelezea hofu yao juu ya ongezeko la tatizo la utapia mlo na matatizo ya chakula katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan. Wajumbe wamesema hali hiyo inaweza kufikia kiwango cha hatari endapo hatua za haraka hazitochukuliwa na pia kutokana na ukosefu wa fursa [...]

14/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Katika mkutano wa biashara Ban apongeza makampuni na kutaka hatua zaidi

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Biashara binafsi lazima ziingilie na kuzisaidia serikali kutafuta suluhu ya kuwa na ukuaji endelevu wa uchumi. Huo ni ujumbe uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa wafanyabiashara na viongozi watunga sera duniani wanaokutana mjini New York katika maandalizi ya mkutano wa ushirikiano endelevu wa Rio+20. Ban Ki-moon amefungua mkutano huo kwa [...]

14/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha kutiwa sahihi kwa makubaliano kati ya Sudan na Sudan Kusini

Kusikiliza / raia wa Sudan Kusini

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kutiwa sahihi kwa maelewano ya kutoshambuliana na ushirikiano kati ya mataifa ya Sudan na Sudan Kusini na kuyashauri mataifa hayo mawili kushikillia makubaliano kati yao. Makubaliano hayo yaliyotiwa sahihi kwenye mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa mwishoni mwa juma lililopita yanataka kila pande kuheshimiwa pamoja na [...]

14/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mataifa yanayokua yashirikishwe kwenye uongozi wa dunia:Migiro

Kusikiliza / Asha Rose-Migiro

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro ametaka kujumuishwa kwa mataifa yanayokuwa kiuchumi kwenye uongozi wa dunia akisisitiza kwamba wanaotoa maamuzi hawazingatii mchango wa masoko mapya kwenye uchumi wa dunia. Akihutubia mkutano wa kuadhimisha miaka 10 tangu kuzinduliwa mpango wa maendeleo na demokrasia wa Helsinki Migiro amesema kuwa washika dau wote wanahitaji kushirikiana [...]

14/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yawasaidia wakimbizi kutoka Angola kurudi nyumbani

Kusikiliza / wakimbizi kutoka Angola

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limerejelea shughuli ya kusaidia kurejea nyumbani kwa hiari wakimbizi 53,370 kati ya wakimbizi 176,00 ambao bado wanaishi kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Zambia, Namibia , Congo na Botswana ikiwa ni karibu miaka kumi baada ya kumalizika kwa [...]

14/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban azitaka Palestina, Israel kujiepusha na malumbano

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Palestina na Israel zinapaswa kuchagua kufuata njia nyoofu na kutuliza mzuka wa uchokozi katika wakati huu ambapo jitihada za kurejea kwenye mazungumzo ili kutafuta suluhu ya kudumu zikipigiwa upatu. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye amehaidi kuendelea kuunga mkono hatua zozote za kutanzua mkwamo huo. Ban ambaye alikuwa [...]

14/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu azungumzia nafasi ya UM kwenye kutanzua mikwamo

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz Al-Nasser

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser ameelezea mwenendo na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na chombo hicho cha kimataifa hasa katika maeneo yanayotumbukia kwenye mizozo kwa kujenga mustakabali mwema na wa maelewano zaidi. Amesema kwa wakati huu Umoja wa Mataifa unatafakari kuweka hadharani mpango mpya ambao unaweza kutizamwa kama siyo wa kawaida [...]

14/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO inasaidia ujenzi mpya wa mifumo ya umwagiliaji Afghanistan

Kusikiliza / FAO inasaidia ujenzi upya nchini Afghanistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linaboresha msaada wake wa kifundi kwa ajili ya kufufua mfumo wa asili wa umwagiliaji nchini Afghanistan. FAO inachukua hatua hii kwa nia ya kuwasaidia wakulima wa Afghanistan kuongeza uzalishaji wa mazao, na pia kwa lengo la kuboresha ufahamu na elimu ambayo wakulima wanahitaji ili kuendesha [...]

14/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kimbuga Giovanna kukikumba kisiwa cha Madagascar:UNICEF

Kusikiliza / kimbuga Giovanna

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema kimbunga Giovanna kilicho katika daraja la nne kinatarajiwa kukikumba eneo la karibu na kisiwa cha Madagascar Jumanne hii ya Febrari 14. Kimbunga hicho kinaarifiwa kitatua kwenye mji wa pwani ya Mashariki mwa Madagascar wa Toamasina na kisha kuelekea mjini mkuu Antananarivo. Kwa mujibu wa UNICEF [...]

14/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwaingiza kinyemela na kiharamu Wasomali wasio na hatia lazima kukome:UM

Kusikiliza / mashua yanayotumika kuwasafirisha Wasomali kiholela

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Somalia Shamsul Bari, Jumanne ameelezea kushitushwa na zahma nyingine ya boti kwenye Ghuba ya aden ambayo imeuwa watu 11 raia wa Kisomali na wengine 34 bado hawajulikani waliko. Bwana Bari amesema kuwasafirisha kinyemela na kiharamu raia wasio na hatia wa Kisomali imekuwa [...]

14/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR na serikali kuwahamisha maelfu ya wakimbizi wa Mali kutoka mipakani

Kusikiliza / wakimbizi wa Mali

Nchini Niger, Burkina Faso na Mauritania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linashirikiana na serikali kuwahamisha wakimbizi wanaokimbia Mali kuwapeleka kwenye usalama kutoka maeneo ya mipakani. Kaskazini mwa Niger UNHCR inasema imepokea taarifa za kuwasili kwa wakimbizi wapya mwishoni mwa wiki. Shirika hilo linasema watu wanaishi katika mahema, wakikabiliwa joto kali kila [...]

14/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna changamoto kubwa kuwahamisha Wasudan 500,000 kurejea Sudan Kusini:IOM

Kusikiliza / Raia wa Sudan Kusini wakirejea nyumbani

  Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema tarehe 8 Aprili ndio siku ya mwisho iliyowekwa kwa Wasudan Kusini takribani 500,000 kuchagua kati ya kurejea nyumbani kutoka Jamhuri ya Sudan au kusalia Sudan Kaskazini. IOM inasema hali hiyo italeta changamoto kubwa za kiufundi kwa serikali zote mbili na jumuiya ya kimataifa. IOM imekuwa ikitarajia kwamba [...]

14/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake ndio wanaoendesha ukuaji wa Uchumi:Migiro

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa UM Asha Rose-Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose-Migiro amesema mchango wa wanawake ni muhimu sana katika jamii na kuwa wao ndio waendeshaji wakubwa wa hatua zinazopigwa katika uchumi. Akizungumza katika kufunga mkutano wa tatu wa mawaziri kutoka nchi zisizofungamana na upande wowote mjini Doha Jumanne amesema changamoto iliyopo ni kuuweka bayana uwezo walionao wanawake [...]

14/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna hofu kwamba janga la kibinadamu Sahel halijapata ufadhili wa kutoka:UM

Kusikiliza / uhaba wa chakula Sahel

Mashirika mbalimbali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa yanahofia kwamba mgogoro wa kibinadamu katika eneo la Sahel haujapata ufadhili wa kutosha kama ilivyokuwa matatizo yaliyoikumba Pembe ya Afrika. Kwa mujibu wa shirikisho la chama cha msalaba mwekundu duniani IFRC janga la kibinadamu linanyemelea endapo msaada hautopatikana haraka. Shirika hilo linakadiria kwamba kati ya watu milioni [...]

14/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu kujadili hali kwenye eneo la Sahel

Kusikiliza / ukosefu wa chakula, Sahel

Hali ya kuhatarisha maisha ya ukosefu wa chakula kwenye eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika itakuwa ajenda kwenye mkutano wa wataalamu wa haki za binadamu juma hili mjini Rome. Ukame na mavuno duni vimesababisha mamilioni ya watu kukabiliwa na tisho la kufa njaa kwenye nchi tisa kwenye eneo la Sahel kuanzia mashariki hadi magharibi mwa [...]

13/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uhalifu dhidi ya ubinadamu umetendwa Syria

Kusikiliza / Navi Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa huenda uhalifu dhidi ya ubinadamu umetendwa nchini Syria. Akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Pillay amesema kwamba zaidi ya watu 5,400 wameuawa nchini Syria tangu mikakati ya serikali ya kupambana na waandamanaji kuanza mwezi machi mwaka uliopita huku watu wengine 18,000 [...]

13/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maoni kuhusu umuhimu wa Radio ya UM

Kusikiliza / wasikilizaji wa radio watoa maoni

UM ukiadhimisha siku ya Radio duniani hii leo watu kutoka Afrika wametoa maoni kuhusu umuhimu wa Radio, ikiwemo Radio ya Umoja wa Mataifa. Mwandishi wetu kutoka Tanzania alipata kuzungumza na watu mbali mbali waliotoa maoni tofauti tofauti kuhusu umuhimu wa radio ya Umoja wa Mataifa. (MAONI KUTOKA TANZANIA)

13/02/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Bado idadi kubwa ya watoto wako jeshini:UNICEF

Kusikiliza / watoto wanaotumika jeshini

Baada ya siku ya kimataifa ya watoto wanajeshi kuadhimishwa hapo jana tarehe 12 shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto wanajeshi 2,260 waliondolewa kutoka jeshini kwenye maeneo ya Afrika ya kati mwaka 2011. Kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watoto 1900 wakiwemo watoto wa kike 266 waliondolewa jeshini [...]

13/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano kuhusu kuongeza soko kwa bidhaa za kilimo cha kitamaduni kuandaliwa

Kusikiliza / mkutano wa UNCTAD

Maafisa wa ngazi za juu na wataalamu akiwemo mkurugenzi kwenye kitengo cha biashara ya kimataifa ya bidhaa na hudumu kwenye shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD Guillermo Valles wanatarajiwa kujadili hatua zilizopigwa na vizuizi vilivyopo kwenye uuzaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo cha kitamaduni. Kati ya watakaozungumza kwenye mkutano huo ni [...]

13/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM azungumzia ukandamizaji wa upinzani na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Georgia

Kusikiliza / Maina Kiai

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kukusanyika kwa amani Maina Kiai ameelezea wasi wasi uliopo kuhusiana na dhuluma zinazolenga vyama vya kisiasa, vyama vya wafanyikazi na wanachama wa mashirika yasiyokuwa ya umma nchini Georgia. Maina ameonya kuwa mabadiliko kadha yaliyofanywa kwa sheria na bunge la Georgia yamaezuia haki ya kukusanyika. Maina amesema [...]

13/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Rotuba kwenye udongo wa dunia inazidi kutoweka:UNEP

Kusikiliza / UNEP

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP linasema kuwa jinsi ambavyo ulimwengu unavyosimamia udongo wake ndilo jawabu kwa usalama wa chakula, maji na mazingira kwenye karne ya 21. Kulingana na UNEP asilimia 24 ya ardhi ya dunia imepoteza rotuba yake kwa karibu kipindi cha robo karne iliyopita kutokana na matumizi mabaya ya ardhi. Ripoti [...]

13/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sera za Israel kuzuia haki ya kuwa na nyumba:Rolnik

Kusikiliza / Raquel Rolnik

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na nyumba Raquel Rolnik ameonya kwamba hatua ya hivi majuzi ya ubinafsishaji wa mali ya serikali nchini Israel kumesababisha kuwepo kwa sera zinazowazuia wenye kipato cha chini kupata makao suala linalochangia kukiukwa kwa haki zao. Akikamilisha ziara ya wiki mbili nchini Israel na kwenye ya [...]

13/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la UM kukutana kuizungumzia Syria

Kusikiliza / baraza kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana ili kujadili hali nchini Syria wakati kunapoendelea na harakati za kukabiliana na wapinzani. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema kuwa Umoja wa Mataifa una mipango ya kutume ujumbe wake kwa ushirikiana na nchi za kiarabu kwa lengo la kutafuta suluhu la mzozo ulio nchini [...]

13/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu watoa maoni kuhusu Radio ya UM

Kusikiliza / msikilizaji wa redio nchini Burundi

UM ukiadhimisha siku ya Radio duniani hii leo watu kutoka Afrika wametoa maoni kuhusu umuhimu wa Radio, ikiwemo Radio ya Umoja wa Mataifa. Nilipata kuzungumza na watu mbali mbali waliotoa maoni maoni kuhusu umuhimu wa radio duniani. (MAONI KUTOKA KENYA) Nchini Burundi mwandishi wetu Ramadhini Kibuga alipata maoni kutoka kwa waandishi wa habari wenzake nchini [...]

13/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha hatua ya kufunguliwa mashtaka kwa afisa wa jeshi Guinea anayetuhumiwa kuhusika na ubakaji wa halaiki

Kusikiliza / Margaret Wahlstrom

Umoja wa Mataifa umepongeza na kukaribisha kwa furaha hatua ya mahakama moja nchini Guinea ambayo imemfungulia mashtaka afisa moja wa ngazi ya juu wa jeshi anayedaiwa kuhusika na vitendo vya ubakaji wakati wa maandamano makubwa ya amani yaliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo mwaka 2009. Akiielezea hatua ya mahakama kumfungulia mashtaka afisa huyo wa [...]

13/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wataka amani kufuatia mauwaji ya watu kadhaa nchini Libya

Kusikiliza / machafuko nchini Libya

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama nchini Libya, katika wakati ambapo watu saba waliokosa makazi wakiripotiwa kuuwawa. Mashambulizi hayo yamefanyika katika eneo karibu na kituo cha mafunzo uongozaji meli cha Janzur kilichopo karibu na Tripoli. Watoto watatu na wanawake wawili walipoteza maisha kwenye shambulio hilo wakati wengine wane walivamia [...]

13/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM washerehekea siku ya Radio Duniani

Kusikiliza / Irina Bokova

Uwezo wa Radio wa kuwaunganisha watu na kuleta uelewano hii leo unasherehekewa kwenye siku ya kwanza kabisa ya kimataifa ya Radio. Tarehe 13 mwezi Februari ndiyo iliyotengwa na shirika la elimu, Sayansi na uatamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. Mkurugenzi wa shirika la UNESCO Irina Bokova amesema kwamba huku ulimwengu ukiendelea kushuhudia mabadiliko bado Radio [...]

13/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuijadili hali nchini Syria

Kusikiliza / Baraza Kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana siku ya Jumatatu ili kuijadili hali nchini Syria ambapo idadi ya watu wanaouawa inazidi kuongezeka kufuatia mikakati ya jeshi ya kukabiliana na makundi yanayoipinga serikali. Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay atalishauri baraza hilo kuhusu hali ilivyo kufuatia ombi kutoka kwa rais [...]

10/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Manusura wa mauaji ya kimbari wa ndani au nje wanahitaji msaada

Kusikiliza / Eugene Mukeshimana

Manusura wa mauaji ya kimbari ya Rwanda wako wengi na baadhi yao asilani hawatosahau yaliyowasibu ndugu, jamaa, marafiki hata majirani zao katika siku 100 za machafuko yaliyokatili watu zaidi ya laki nane na kuwafungisha virago mamilioni. Wengi wa manusura hao walielekea uhamishoni kuomba hadhi za ukimbizi au hifadhi katika nchi mbalimbali duniani. Tarehe 6 Aprili [...]

10/02/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanainchi wa Haiti wajiandaa kwa gharika nyingine

Kusikiliza / wananchi wa haiti wajiandaa kwa gharika nyingine

Miezi baada ya kuanza kwa kipindi cha gharika kwenye pwani za kisiwa cha Hispaniola, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Hispaniola wameatangaza mpangilio wa kwanza jinsi ya kutumia vituo vya uokoaji. IOM imetoa usaidizi wa kiufundi kwa zaidi ya vituo 500 vya uokoaji kote nchini ili kuhakikisha kuwa vinafanya kazi kwa njia [...]

10/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Afrika Magharibi kuwa jaa la taka ya elektroniki

Kusikiliza / taka la elektroniki

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa eneo la Afrika Magharibi linakabiliwa na hatari ya kuwa jaa la taka ya vifaa vya eletroniki. Kulingana na utafiti wenye kichwa tuko wapi Afrika? Ni kwamba taka ya vyombo vya electronoki vinavyotumika nyumbani inachukua asilimia 85 kwenye nchi za Afrika Magharibi. Kwenye mataifa matano yaliyofanyiwa utafiti kwenye ripoti [...]

10/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwanamuziki 50 Cent aitembelea pembe ya Afrika

Kusikiliza / mwanamuziki 50 Cent akiwa na watoto katika pembe ya Afrika

Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa rap Curtis Jackson anayefahamika kama 50 Cent alikuwa na fursa ya kujionea hali alipofanya ziara nchini Somalia na Kenya. Jackson ambaye mwaka uliopita alitangaza ahadi ya kutoa chakula bilioni moja kwa watu walio na njaa amekuwa akitembelea sehemu tofauti na shirika la mpango wa chakula duniani WFP ikiwemo kambi ya [...]

10/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yapata msaada wa kusadia waathiriwa wa tufani nchini Ufilipino

Kusikiliza / waathiriwa wa tufani

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepokea dola 202,000 zaidi kutoka kwa shirika la kimataifa la maendeleo la Canada ili kuweza kusaidia familia zilizoathiriwa na tufani kwa jina Washi nchini Ufilipino. Fedha hizo zitalisaidia shirika la IOM kutoa makao, fedha na misaada mingine kwenye miji ya Cagayan de Oro na Iligan. Kati ya mashirika yanayochangia [...]

10/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaomba dola milioni 145 kusaidia wakimbizi nchini Sudan

Kusikiliza / wakimbizi nchini Sudan

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaitisha dola milioni 145 zaidi ili kuwasaidia wakimbizi wanaokimbia mapigano kwenye majimbo ya Blue Nile na Kordofa Kusini nchini Sudan na kuingia nchini Ethiopia na Sudan Kusini. Kiasi hicho cha fedha kinalenga kuwasiadia hadi wakimbizi 185,000 kwenye nchi hizo mbili. Tangu Juni mwaka 2011 mapigano makali [...]

10/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yaanzisha kituo kuwasaidia askari wa zamani kurejea uraiani

Kusikiliza / raia wa Sudan Kusini

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vilivyoko huko Sudan Kusin vimepiga jeki uzinduzi wa ujenzi wa kituo maalumu ambacho kinakusudia kutumika kuwasaidia makundi ya askari wa zamani. Kituo hicho kilichoko magharibi mwa nchi hiyo kitawasaidia waliokuwa askari wa zamani namna wanavyoweza kuachana na matumizi ya silaha na kuchangamana upya na jamii katika maisha [...]

10/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM utavuna mengi ukiongeza mashirikiano yake na Umoja wa Ulaya

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Umoja wa Mataifa umeelezewa umuhimu wa kuwa na mafungamano ya karibu na nchi wanchama wa Umoja wa Ulaya ambazo zinaunda jumuiya ya usalama na mashirikiano katika eneo hilo OSCE, kuwa hatua hiyo itazalisha matunda mema. Waziri wa mambo ya nchi za Nje wa Ireland ambaye ndiye rais wa chombo hicho cha usalama kwa nchi za [...]

10/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Majaribio ya matumizi ya Nyuklia ni moja ya agenda ya Ban huko Austrian

Kusikiliza / mkutano ya nuklia mjini Vienna

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anatazamiwa kuwa na ziara ya siku kadhaa nchini Australia ambako anatazamiwa kujadilia masuala ya usalama na namna ya kukabiliana na wimbi la madawa ya kulevya. Ban anatazamiwa kuwasilini mjini Vienna hapo February 15 na baadaye kufungua mkutano wa mawaziri unaozingatia mkataba wa ushirikiano wa Paris juu ya [...]

10/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM yawataka wanasiasa Maldives kuketi kwenye majadiliano

Kusikiliza / Oscar Fernandez

Umoja wa Mataifa umewatolea mwito pande zinazokinzana nchini Maldives kujiweka kando na matumizi ya nguvu na kuanzisha majadiliano ya mezani kwa shabaha ya kutanzua mkwamo wa kisiasa uliojitokeza hivi karibuni. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya siasa Oscar Fernandez-Taranco,amewasili nchini humo kujaribu kutuliza mzuka wa kisiasa katika wakati ambapo rais wan [...]

10/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Afisa wa Serbia kujadilia mkwamo wa Kosovo

Kusikiliza / Ban na waziri wa Nje wa Kosovo Vuk Jeremic

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-moon amekuwa na mazunguzmo na waziri wa mambo ya Nje wa Serbia Vuk Jeremic na kujadilia masuala kadhaa hasa hatua zilizopigwa juu ya utanzuaji wa mzozo wa Kaskazini mwa Kosovo. Viongozi hao wamepongeza maendeleo mema yanayoendelea kujiri wakati huu ambapo Umoja wa Ulaya ukiwa kwenye mstari wa mbele [...]

10/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa haki za binadamu kufanya ziara Palestina Misri na Jordan

Kusikiliza / ramani ya Misri na Jordan

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu kwenye maeneo ya wapalestina yaliyokaliwa tangu mwaka 1967 Richard Falk atafanya ziara kuanzia tarehe 10 hadi 20 mwezi huu akiitembelea Misri, eneo lililokaliwa la Palestina na Jordan ili kukusanya habari kuhusu masuala ya haki za binadamu yanayohusiana na kuwepo kwa Israel kwenye [...]

10/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasomali waangamia kwenye ajali ya mashua kwenye ghuba ya Aden

Kusikiliza / ghuba la Aden

Takriban watu 11 wanaripotiwa kuzama na wengine 34 hawajulikani waliko kufuatia tukio ambapo mashua moja ilizama juma hili kwenye ghuba ya Aden. Manurusa waliopatika kwenye pwani za Somalia walieleza kuwa mashua yao iliyokuwa chini ya uongozi wa walanguzi watatu wa watu na iliyokuwa imebeba abiria 58 ilikuwa safarini kuelekea nchini Yemen. Kisha mashua hiyo ilipata [...]

10/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za afya zakwama kwenye mji wa Homs nchini Syria

Kusikiliza / machafuko nchini Syria

Huduma za afya zinaripotiwa kuathiriwa vibaya kwenye mji wa Homs nchini Syria ambao umekuwa ukishambuliwa na vikosi vya serikali mara kwa mara. Shirika la afya duniani WHO linasema kwamba uvamizi unaoendelea kwenye mji huo sio tu unawawazuia wahudumu wa afya kwenda kazini bali pia umesababisha vituo vingi vya afya kuishiwa na madawa. WHO inasema inasumbuliwa [...]

10/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Libya yakamilisha sheria mpya za Uchaguzi

Kusikiliza / Ian Martin

Kulingana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulioko Afrika Kaskazini, Libya imekamilisha Sheria mpya za uchaguzi ambazo zitaleta demokrasia nchini humo. Sheria hizo zinatoa maelezo juu ya uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa bunge. Bunge litakuwa na jukumu ya kuandika katiba mpya. Wakati huohuo, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa [...]

09/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haiti inapiga hatua zaidi kwa masuala ya haki za binadamu:UM

Kusikiliza / Michel Forst

Haiti imepigiwa mfano kwa kuweka zingatio la kutekeleza utawala wa kisheria lakini hata hivyo kuna shaka kuu moja inayosalia namna kuweka uwiano sawia kwenye baadhi ya maeneo. Kulingana na mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu amesema kuwa Haiti imepiga hatua kubwa ikiwemo maeneo ya kuchaguliwa kwa rais wa mahakama [...]

09/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mashujaa wa misitu kutunukiwa tuzo maalum na UM

Kusikiliza / misitu 2011

Watu ambao wametoa mchango mkubwa katika kulinda misitu na jamii za misitu Alhamisi wametunukiwa tuzo ya mashujaa wa misitu kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa na kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu misitu UNFF. Tuzo hizo zimetolewa katika kuhitimisha mwaka wa kimataifa wa misitu kwenye makao maku ya Umoja wa Mataifa hapa New York. Jan Mc Alpine, [...]

09/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atilia shaka kuzuka kwa ghasia Mali

Kusikiliza / mapigano kaskazini mwa Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea shaka yake kufuatia machafuko yaliyozuka huko Kaskazini mwa Mali baina ya vikosi vya serikali na kundi la waasi laTuareg. Ban amesema hali hiyo inaleta hali ya mkwamo na kutatiza hali ya usamaria mwema juu ya utoaji huduma za kibinadamu. Ripoti zinasema kuwa kumekuwa na hali ya [...]

09/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO na taasisi ya kimataifa ya amani watia saini makubaliano

Kusikiliza / Forest Whitaker

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova amesisitiza kuali ya wahenga kwamba Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Akizungumza katika hafla maalumu ya kusaini makubaliano baina ya UNESCO na taasisi ya kimataifa ya amani iliyoanzishwa na balozi mwema wa UNESCO na mcheza filamu maarufu Forest [...]

09/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afisa wa UM asisitiza haja ya kuimarisha operesheni za amani DRC

Kusikiliza / uchaguzi nchini DRC

Afisa wa ngazi ya juu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa amesisitiza haja ya kuboresha mpango wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kusaidia hatua ijayo ya uchaguzi katika taifa hilo kubwa Afrika na kuwalinda raia katika maeneo ambayo uongozi wa taifa haupo. Katika mkutano na waandishi wa [...]

09/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la UM lataka uungwaji mkono kwa mpango wa nyumba wa Kipalestina

Kusikiliza / mpango wa nyumba

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al- Nasser ameyataka mataifa kuunga mkono mpango wa nyumba wa Umoja wa Mataifa kwa wapalestina akiongeza kuwa mpango huo hautaboresha tu hali yao ya kuishi bali utaleta amani katika eneo hilo. Mpango huo unaoongozwa na shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat tayari umepata [...]

09/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watalamu wa UM kuhusu haki za binadamu wapinga kesi ya Garzon

Kusikiliza / Gabriela Knaul

Wataalamu kadhaa huru wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameshutumu kesi dhidi ya jaji mmoja maarufu nchini Hispania kufuatia jitihada zake za kuchunguza zaidi ya madai 100,000 ya kutoweka kwa watu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe chini ya utawala wa Francisco Franco. Kesi dhidi ya jaji Baltasar Garzon kwa [...]

09/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto nchini Afghanistan wakwama katika viwanda vya matofali ili kulipa mikopo

Kusikiliza / watoto wanaofanya kazi katika viwanda vya matofali

Utafiti mpya uliofanywa na Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuwepo mkakati utakaowaacha huru wafanyakazi watoto wanaofanya kazi katika viwanda vya matofali. Utafiti huo ulioongozwa na shirika la kazi duniani ILO umebaini kwamba asilimia 56 ya watengenezaji wa matofali nchini Afghanistan ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 na ajira wa kazi hiyo [...]

09/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtazamo wa bei ya chakula umepanda Januari:FAO

Kusikiliza / bei ya vyakula imepanda

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema mtazamo wa bei za vyakula umepanda kwa karibu asilimia 2 kuanzia Desemba hadi Januari mwaka huu ikiwa ni ongezeko la mara ya kwanza tangu Julai mwaka 2011. Kwa mujibu wa FAO bei za bidhaa zilizoorodheshwa zimeongezeka huku mafuta yakiongoza kufuatiwa na nafaka, sukari, bidhaa za maziwa na nyama. [...]

09/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi wanachama wa UM waunga mkono mtazamo mmoja dhidi ya uhalifu wa kimataifa

Kusikiliza / ramani ya kimataifa

Mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na madawa na uhalifu UNODC bwana Yury Fedotov amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na uhalifu mkubwa wa kimataifa wa mtandao ambao viwango vyake vinagusa karibu kila nchi. Akitoa taarifa kwa mabalozi mjini New York kuhusu kikosi cha kukabiliana na uhalifu wa kimataifa wa kupangwa na [...]

09/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wito watolewa kusitisha mara moja ukiukwaji wa haki za watoto Syria:Coomaraswamy

Kusikiliza / Radhika Coomaraswamy

Kufuatia siku nyingine ya ghasia na mauaji nchini Syria, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kwa ajili ya watoto kwenye migogoro ya vita Radhika Coomaraswamy amerejea kutoa wito kwa uongozi wa serikali ya Syria kukomesha mara moja mauaji na ukatili dhidi ya watoto. Bi Coomaraswamy amesema katika miezi michache iliyopita idadi ya watoto waliokufa na kuathirika [...]

09/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na Ligi ya Kiarabu wajadili kutuma ujumbe Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kushindwa kwa Baraza la Usalama kuzungumza kwa kauli moja kumaliza umwagaji damu nchini Syria kumekuwa na athari kubwa. Akizungumza kwenye Baraza la Usalama Ban amesema Jumamosi iliyopita azimio la baraza hilo la kulaani ghasia Syria na kumtaka Rais Bashar al-Assad kuwachia madaraka lilipingwa kwa kura ya [...]

09/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha uzinduzi wa utaratibu unaolenga kusaidia kutatua mzozo Darfur

Kusikiliza / Ibrahimu Gambari-Darfur

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo, amekaribisha kuzinduliwa kwa shirika la utawala la Darfur, shirika ambalo linalenga kuimarisha na kuendeleza amani katika eneo la magharibi mwa Sudan linalokumbwa na vita. Ban alisema kwamba uzinduzi wa shirika hilo huko El fasher ni ishara muhimu katika hatua ya kutekeleza malengo ya makubaliano ya [...]

08/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali Kaskazini mwa Kosovo imetulia lakini bado ni ya hatihati

Kusikiliza / Edmond Mulet

Juhudi za kutuliza mvutano Kaskazini mwa Kosovo zimezaa matunda lakini hali bado haijatengamana kabisa. Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Edmond Mulet alipotoa taarifa kwenye Baraza la Usalama leo Jumatano. Kosovo jimbo la zamani la Serbia ilijitangazia uhuru mwaka 2008 na kuwa taifa lililojitenga, lakini sehemu ya Kaskazini mwa nchi hiyo wakazi wake [...]

08/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Pande zote DRC kujiingiza kutafuta suluhu ya mzozo wa uchaguzi:UM

08/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa uvumilivu kwa wanachama wa Baraza la Usalama la UM ulisabaisha kuvunjika kwa azimio kuhusu Syria

Kusikiliza / Vitaly Churkin

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa ameelezea kujuta kwake baaada ya taifa lake kupinga azimio kuhusu Syria mwishoni mwa juma. Vitaly Churkin anasema kuwa nchi yake imesababisha madhara makubwa. Amesema kuwa Baraza la Usalama lingeafikia makubaliano kama wenzake kutoka nchi za magharibi wangekuwa na uvumilivu. Amesema kuwa kinachofanyika nchini Syria ni kitu muhimu akiongeza [...]

08/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maafisa wa UM wataka hatua kuchukuliwa kuokoa uchumi wa dunia

Kusikiliza / Rob Vos

Maafisa wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa wameonya kwamba uchumi wa dunia kwa mara nyingine unaelekea pabaya. Katibu katika kitengo cha sera kwenye idara ya masuala ya uchumi na jamii kwenye Umoja wa Mataifa Robert Vos anasema kuwa dalili hizo tayari zimeanza kuonekana kwenye mataifa yaliyostawi. Naye Rais wa baraza la uchumi na [...]

08/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Shirikisho la soka Afrika na UM waungana kufunga bao kwa ajili ya amani na maendeleo

Kusikiliza / Abou Moussa

Mkuu wa ofisi ya siasa ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Kati na Rais wa shirikisho la soka barani Afrika AFC wamekutana kujadili jinsi gani hamasa ya soka barani Afrika itasaidia kuchagiza amani na maendeleo Afrika ya Kati. Katika mkutano wao wakati mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika likiendelea Gaqbon na Equatorial Guinea, Abou [...]

08/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNODC kutoa mafunzo ya kupambana na ufisadi kwa mashirika ya kijamii ya Afrika

Kusikiliza / mashirika ya kijamii Afrika

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na madawa na uhalifu UNODC imesema wakati matukio ya hivi karibuni kwenye ulimwengu wa Kiarabu yameonyesha kuwa ufisadi unaweza kukandamiza taasisi za kidekomrasia, kudumaza uchumi na maendeleo na kuchangia kutokuwepo usalama, jumuiya za kijamii zinaweza kuwa na jukumu muhimu katika kupambana na ufisadi. UNODC inasema jumuiya hizo hazitokuwa [...]

08/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Luxemborg kutoa msaada wa Euro milioni 15 kwa UNRWA miaka minne ijayo

Kusikiliza / Marie-Josee Jacobs

Serikali ya Luxemborg Jumatano imetangaza msaada wa Euro milioni 15 kwa miaka minne kwa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA. Tangazo la msaada huo ni ongezeko la Euro milioni 3.37 sawa na asilimia 36 ya mchango wake wa kila mwaka hadi mwaka 2015. Alice Kariuki na maelezo zaidi. (RIPOTI [...]

08/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Magene ya uhalifu yatishia uchumi Caribean:UNDP

Kusikiliza / Ripoti ya maendeleo Caribean

  Uhalifu umekuwa moja ya changamoto kubwa zinazotishia uchumi na maisha katika mataifa ya Caribean lakini mchanganyiko wa sera na mipango vinaweza kusaidia kukomesha tatizo hilo imesema ripoti ya maendeleo ya binadamu kwa nchi za Caribean mwaka 2012 iliyotolewa Jumatano mjini Port-a-spain Trinidad and Tobago na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa NDP. Ripoti [...]

08/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yaomboleza kifo cha msaani wa Hispania Antoni Tàpies

Kusikiliza / spanish-painter

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni leo ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mchoraji wa Kihispania Antoni Tàpies, ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88. Bi Irina Bokova amemwelezea msanii huyo kuwa alama kuu inayonogesha taalumu na usanii na ubunifu. Katika salama zake hizo, Mkuu [...]

08/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rais wa Maldives hatimaye akubali kujiuzulu

Kusikiliza / Mohamed Nasheed

Rais wa Maldives hatimaye amesalimu amri na kukubali kuachia madaraka ikiwa ni siku chache tu baada ya kuandamwa na mashinikizo yaliyomtaka kuondoka Ikulu. Rais Mohamed Nasheed amekuwa kwenye shinikizo kubwa toka kwa wale wanaopinga utawala wake na katika siku za hivi karibuni maandamano ya kumtaka atachia ngazi yalivuka mipaka na kuudhorotesha uongozi wake. Amekubali kukabidhi [...]

08/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu wauawa na wengine kukimbia kutokana na machafuko Moyale nchini Kenya

Kusikiliza / machafuko Moyale nchini Kenya

Machafuko yanayoendelea kwenye wilaya ya Moyale nchini Kenya tangu Januari yameshakatili maisha ya watu 21, maelfu kukimbia nyumba zao na takribani 57,316 kutawanywa, wengi wao wakikimbia nchi jiraji ya Ethiopia kupata usalama. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa chama cha msalaba mwekundu nchini Kenya KRCS, mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo OCHA na vyombo vya [...]

08/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watu kukabiliwa na njaa Sudan Kusini

Kusikiliza / watu wanaokabiliwa na njaa Sudan Kusini

Mamilioni ya watu Sudan Kusini watakabiliwa na njaa mwaka huu endapo hatua za haraka hazitochukuliwa, imesema ripoti ya pamoja iliyotolewa na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa. Shirika la chakula na kilimo FAO na shirika la mpango wa chakula duniani WFP yameonya kwamba hali ya usalama wa chakula Sudan Kusini inajongea haraka katika kiwango cha [...]

08/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay ametaka zichukuliwe hatua kukomesha machafuko Syria

Kusikiliza / machafuko nchini Syria

Serikali ya Syria inashutumiwa kwa kufanya mashambulizi makusudi kwenye mji wa Homs katika juhudi za kukandamiza upinzani. Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema kushindwa kwa Baraza la Usalama kuafikiana kwa hatua ya pamoja kunaonekama kuichochea serikali ya Syria kuendelea kuuwa watu wake. Bi Pillay amelaani mashambulizi kwenye mji wa Homs na ametoa [...]

08/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Njaa imeisha Somalia lakini bado nchi hiyo inahitaji msaada:UM

07/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Vijana duniani watiwa hofu na ukosefu wa ajira:UM

07/02/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya UM yamuhukumu mwanasheria wa Bosnia Serbia kwa kuidharau mahakama

Kusikiliza / Jelena Rasic

Mahaka ya uhalifu wa vita ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya vita vya miaka ya 1990 vya Balkan leo imemuhukumu mwanasheria anayetetea Bosnia Serbia kwenda jela miezi 12 kwa kuidharau mahakama. Mahaka inasema Jelena Rasic amepewa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia Jumanne iliyopita ya kujua na kuingilia makusudi kazi za mahakama kwa [...]

07/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakristo wa Iraq waliokimbilia uhamishoni wengi wao hawataki kurejea nyumbani:IOM

Kusikiliza / familia za wakimbizi wa Iraq

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa juu ya uhamiaji IOM inasema kuwa wakati mamia ya wakristo kutoka eneo la Iraq ya Kaskazini wakianza kurejea makwao baada ya kukimbilia uhamishoni kunusuru maisha yao, lakini baadhi yao wanaogopa kurejea nyumbani kwa kuhofia usalama Kundi la wakristo hao waliingia uhamishoni wakikimbia machafuko na kokosekana kwa [...]

07/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNCTAD ataka kufanyika mabadiliko kuhusu masuala ya uchumi

Kusikiliza / nembo ya UNCTAD

Katibu Mkuu wa shirika la bishara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD amesema kuwa kunastahili kuwe mabadiliko kuhusu masuala ya uchumi ya miaka 30 iliyopita ili kuingia kwenye masuala yaliyo na lengo la maendeleo ya ya kiuchumi wakati ulimwengu unapojikwamua kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi. Ripoti hiyo iliyotolewa hii leo inataka kuchukuliwa kwa [...]

07/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shughuli za kufungwa kwa kambi nchini Haiti zaendelea

Kusikiliza / kambi nchini Haiti

Shughuli ya kufungwa kwa kambi nchini Haiti zinaendelea kushika kasi wakati nyingi ya familia zinapoendelea kupata makao na kusaidiwa kurudi makwao. Baadhi ya kambi kwenye mji wa Port-au-Prince zimefungwa au zimekaribia kufungwa kupitia kwa mpango wa serikali ya Haiti. Chini ya mpango huo familia 150 zinazopata usaidizi wa shirika la kimataifa  la uhamiaji IOM zitaondoka [...]

07/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ECOSOC kuwahakikishia ajira vijana

Kusikiliza / mkutano wa ECOSOC

Shirika la uchumi na jamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC linasema kuwa kuhakikisha kuwepo ajira kwa vijana ni moja ya malengo makuu ya shirika hilo mwaka 2012. ECOSOC inaanza mkutano wa siku nne hii leo kujadili hali ya sasa ya uchumi duniani. Mkurugenzi wa ofisi ya kutoa ratiba kwenye shirika la ECOSOC Hanif Navid anasema [...]

07/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya hewa inazidi kuwa mbaya Ulaya:WMO

Kusikiliza / barafu

Kumeripotiwa hali ya baridi kali barani Ulaya hasa kuanzia eneo la Scandinavia na Mediterranean. Hali hiyo ilianza kushuhudiwa mwezi Januari mashariki mwa Urusi na Siberia na kusambaa kuelekea mashariki na kati kati mwa Ulaya na hadi magharibi na kusini mwa Ulaya. Hewa baridi inayotoka kaskazini na iliyo na unyevu kutoka kwa bahari ya Mediterranean ilisababisha [...]

07/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa masuala ya kidini wafanyika kwenye UM

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz Al-Nasser

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema kuwa ni jambo muhimu kuyajumuisha masuala ya kidini katika jitihada za kutafuta amani. Akiongea kwenye kongamano ya kidini duniani liliondaliwa kwenye ukumbi wa Umoja wa Mataifa al Nassaer amesema kuwa masuala ya kidini yametengwa kwenye mikutano ya Umoja wa Mataifa. Lakini hata hivyo [...]

07/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto 400 wauawa nchini Syria

Kusikiliza / maandamano nchini Syria

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa karibu watoto 400 wameuawa nchini Syria kwa muda wa miezi 11 iliyopita. UNICEF pia inasema kuwa ina habari za kuthibitisha kuwa hadi watoto 400 wanazuiliwa kwenye vituo ndani mwa Syria. Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Antony Lake kwa sasa anataka kumalizika kwa ghasia dhidi ya [...]

07/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yawalazimu maelfu kuhama makwao nchini Mali

Kusikiliza / wakimbizi kutoka nchini Mali

Zaidi ya watu 22,000 wamelazimika kuhama makwao kaskazini mwa Mali wakati kunapoendelea kushuhudiwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi ya Tuareg. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa wengi wa watu waliohama makwao wamekimbilia Niger, Burkina Faso na Mauritania. Wengi wanaripotiwa kulala nje na hawana huduma kama [...]

07/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR katika jitihada za kutafuta suluhu kwa wakimbizi kwenye mataifa matatu

Kusikiliza / wakimbizi kutoka Rwanda na Liberia

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaweka mikakati ya kumaliza tatizo la wakimbizi barani Afrika hasa tatizo la wakimbizi nchini Angola, Liberia na Rwanda. Mikakati hiyo ambayo kwanza ilitangazwa mwaka 2009 inalenga kutafuta suluhu la wakimbiz kwenye mataifa hayo matatu inayowalenga pia wakimbizi walio nchini mwao, au nchi za kigeni. Kati ya [...]

07/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

DRC yatakiwa kutatua tofauti za kisiasa kwa amani

Kusikiliza / Roger Meece

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo MONUSCO balozi Roger Meece amewataka wenyeji wa nchi hiyo kutumia njia za kisheria kutatua mzozo wa uchaguzi unaondelea nchini humo. Hii ni baada ya kiongozi mkuu wa upinzani nchini DCR kupinga matokeo ya uchaguzi huo. Akiliarifu baraza la usalama la Umoja wa [...]

07/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna umuhimu wa kuunganisha mifumo wa kiteknolojia-UM

Kusikiliza / Sha Zukang

Mkutano wa usoni wa kimataifa juu ya maendeleo endelevu unatazamia kutupia jicho zaidi kwenye eneo la ujenzi wa miundo mbinu ya teknolojia ili kusukuma mbele ustawi wa kibinadamu na maingiliano sahihi ya kimaendeleo. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya mkutano huo Sha Zukang, amesema kuwa kongamano hilo linalotazamiwa kufanyika mwishoni mwa juma huko [...]

07/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya ICJ yachagua viongozi wake

Kusikiliza / Peter Tomka

Mahakama ya Kimataifa juu ya haki ICJ ambacho ni chombo muhimu cha utanzuaji mizozo inayohusiana na sheria kwa Umoja wa Mataifa kimewachagua watendaji wake wa ngazi za juu ambao wanatazamiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu. Mahakama hiyo imemchagua Jaji Peter Tomka kutoka Slovakia kuwa rais na Jaji Bernardo Sepúlveda-Amor kutoka Mexico anakuwa makamu [...]

07/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na machafuko yanayoendelea Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesikitishwa na kushangazwa na machafuko yanayoendelea nchini Syria, hususani idadi ya vifo na majeruhi katika mji wa Homs, machafuko yakihusisha matumizi ya silaha nzito, vifaru na kuvurumishwa kwa makombora kwenye maeneo ya raia. Machafuko hayo hayakubaliki hata kidogo katika misingi ya kibinadamu. Ban amelaani vikali machafuko hayo. [...]

06/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwanamuziki wa Uingereza Sarah Brightman awa msanii wa amani wa UNESCO

Kusikiliza / Sara Brightman

 Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limetangaza leo kwamba mwanamziki na muigizaji huo wa Uingereza atajiunga kwenye orodha ya wasanii wengine wa amani ambao wanatumia umaarufu wao na mchango wao wa kisanii kuchagiza programu na ujumbe wa UNESCO. Bi Brightman atatawazwa rasmi kuwa msanii wa amani katika hafla maalum itakayofanyika [...]

06/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya raia wanaouwa Afghanistan yaongozeka kwa muda wa miaka mitano iliyopita

Kusikiliza / majeruhi nchini  Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA unasema kuwa mwaka 2011 umetimiza miaka mitano ambapo idadi wa raia waliouawa kwenye mizozo chini Afghanistan imeongezeka. Kupitia kwa ripoti ya pamoja kati ya ujumbe wa UNAMA na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja swa Mataifa ni kwamba kubadilika kwa mbinu kati ya pande zinazozonana ndiko [...]

06/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban atoa wito kwa Israel kuacha kulikalia eneo la Wapalestina

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban aitembelea shule ya wasichana ya UNRWA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Jumatatu amerejea wito wa kuchagiza mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, akitaja athari za kiuchumi na maisha ya Wapalestina zinazochangiwa na Israel kuendelea kukalia eneo la Palestina. Ban amesema maendeleo ya kichumi hayawezi kufikiwa bila kuwepo suluhisho la kisiasa. Ban ameyasema hayo mbele ya washiriki wa [...]

06/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kusafisha mabomu yote ya ardhini Sri Lanka itachukua zaidi ya muongo:UNDP

Kusikiliza / mabomu ya ardhini Sri Lanka

Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP unaohusika na mabomu ya ardhini umesema inatarajiwa kuchukua miaka zaidi ya 10 ili kusafisha na kutegua mabomu yote ya ardhini yaliyosalia nchini Sri Lanka. UNDP inasema zoezi hilo litachukua muda mrefu kutokana na ukosefuawa fedha, vitendea kazi na mfumo wa kazi yenyewe. Hadi kufikia mwisho [...]

06/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jamii 2000 zaidi za Kiafrika zatokomeza ukeketaji mwaka 2011:UNFPA

Kusikiliza / mfumo wa ukeketaji wa wanawake

Takribani jamii 2000 barani Afrika zimeachana na mfumo wa ukeketaji kwa wanawake mwaka 2011. Hatua hii imefanya idadi ya jamii zilizotokomeza mila hiyo barani Afrika kufikia 8000 katika miaka michache iliyopita. Takwimu hizi zimetokana na utafitio uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA na shirika la moja wa Mataifa la [...]

06/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ivory Coast, UM kuanza kuyahakikisha matokeo ya awali ya uchaguzi

Kusikiliza / Bert Koenders

Umoja wa Mataifa umeelezea matumaini yake juu ya uwekezekano wa kutolewa hati ya uhakiki juu ya matokeo ya ubunge kufuatia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana nchini nIvory Coast. Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI amesema kuwa upo wezekano serikali na Umoja wa Mataifa wakaridhia matokeo hayo baadaye wiki hii. Bert [...]

06/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serikali za Asia-Pacific zatafuta njia za kuhakikisha wanakuwa na kizazi huru bila HIV

Kusikiliza / Asia-Pacific kupambana na HIV

Viongozi wa serikali, wawakilishi wa jumuiya za kijamii na watu wanaoishi na virusi vya HIV kutoka mataifa 34 ya Asia-Pacific wameanza majadiliano Jumatatu kutafuta njia za kuhakikisha wanatokomeza ukimwi. Majadiliano hayo ya siku tatu yanafanyika kwenye makao makuu ya tume ya Umoja wa mataifa ya uchumi na jamii kwa nchi za Asia na Pacific ESCAP [...]

06/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano kuhusu Somalia wafanyika Djibouti

Kusikiliza / Balozi Mahiga kwenye mkutano Djibouti

Mkutano kuhusu Somalia chini ya uenyekiti wa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga ulifanyika kati ya tarehe 5 na 6 nchini Djibouti, mkutano uliohudhuriwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf Spika wa bunge la serikali ya mpito nchini Somalia Shariif Hassan Sheikh [...]

06/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yazindua mchezo kwenye mtandao kwa ajili ya kuchangia chakula

Kusikiliza / wfp-freerice-336x280

Mchezo wa kwenye mtandao unaojulikana kama Freerice.com wenye lengo la kukusanya mafungu ya fedha kwa ajili ya kuwakirimu wenye matatizo ya njaa duniani, umeanzishwa rasmi leo na wachezaji wake wakipewa himizo kusajili marafiki zaidi kujiunga kwenye mchezo huo. Shirika la kimataifa la mpango wa chakula WFP limezindua mchezo huo likiwa na ujumbe usemao fikiisha wachezaji [...]

06/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNDP yaidhinisha programu ya kwanza kabisa kwa Sudan Kusini

Kusikiliza / soko nchini Sudan Kusini

Katika hatua nyingine kubwa ya mafanikio kwa taifa jipya la Sudan Kusini, sasa litakuwa na programu yake maalumu iliyoidhinishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP. Mpango huo maalumu kwa ajili ya Sudan Kusini umeandaliwa kwa ushirikiano na serikali na umeidhinishwa rasmi na bodi ya magavana ya UNDP Jumapili usiku. Mpango huo wa [...]

06/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya kisiasa yanofanywa na serikali yanasaidia haki za binadamu Myanmar:UM

Kusikiliza / Tomas Ojea Quintana

Mabadiliko ya kisiasa yanayofanywa na serikali ya Myanmar yamekuwa na athari nzuri katika hali ya haki za binadamu nchini humo, lakini taifa hilo bado linakabiliwa na changamoto nyingi amesema mtaalamu wa Umoja wa mataifa wa haki za binadamu kwa ajili ya Myanmar Tomas Ojea Quintana. Bwana Quintana amesema ya Myanmar lazima iwaachilie mahabusu wote wa [...]

06/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana duniani watiwa hofu na ukosefu wa ajira

Kusikiliza / Ripoti ya ajira kwa vijana

  Vijana kote duniani wanatiwa hofu kutokana na ukosefu wa fursa za ajira na wanatoa wito wa kuongezwa uwekezaji katika eneo hilo la ajira . Hii ni kutokana na ripoti mpya ya kimataifa ya vijana iliyotolewa Jumatatu na Umoja wa Mataifa. Baada ya matatizo ya uchumi yanayoendelea kuighubika dunia tatizo la ajira kwa vijana duniani [...]

06/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asema kupingwa kwa azimio dhidi ya Syria kuutia dosari UM

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikitiko yake kwa Baraza la Usalama kushindwa kuafikiana kuhusu Syria. Wajumbe 13 kati ya 15 wa Baraza la Usalama wamepiga kura kuunga mkono azimio lililowasilishwa na Morocco lakini Urusi na Uchina wakaamua kutumia kura yao ya turufu. Na kura yoyote ya turufu kutoka kwa mmoja wa [...]

04/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Urusi na Uchina wapinga azimio la UM kuhusu Syria

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Urusi na Uchina wamepiga kura leo kupinga azimio kuhusu Syria kwenye Baraza la Usalama, huku wajumbe wengine 13 wamepiga kura ya kuliunga mkono azimio hilo. Azimio hilo limelaani kuendelea kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaotekelezwa na serikali ya Syria. Pia limezitaka pande zote nchini humo yakiwemo makundi ya watu wenye silaha kusitisha ghasia [...]

04/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tatizo la Saratani, adha na athari zake kwa nchi zinazoendelea hasa Afrika

Kusikiliza / kiini cha Saratani

Ugonjwa wa Saratani ndio unaoongoza kwa kuua duniani, huku shirika la afya duniani WHO likisema asilimia 13 ya vifo vyote duniani vilivyotokea mwaka 2008 ambavyo ni watu milioni 7.6 vimesababishwa na aina mbalimbali za saratani. Kila tarehe 4 Februari ambayo ni siku ya kimataifa ya Saratani WHO hushirikiana na muungano wa kupambana na saratani kuchagiza [...]

03/02/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waunga mkono kampeni ya chanjo nchini Cameroon

Kusikiliza / chanjo ya Homa ya Manjano

Umoja wa Mataifa umeunga mkono kampeni kubwa ya kutoa chanjo inayoendelea kaskazini mwa Cameroon ambapo kumeripotiwa mkurupuko wa homa ya manjano. Kampeni hiyo iliyoanza mwezi uliopita kwenye wilaya nane inalenga kuwakinga zaidi ya watu milioni 1.2 walio kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo unaosambazwa na mbu na usio na tiba. Shirika la afya duniani [...]

03/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waanza usambazaji wa chakula kwa waathiriwa wa mafuriko nchini Musumbiji

Kusikiliza / mafuriko nchini Mozambique yasababisha uhaba wa chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza kutoa misaasa nchini Musumbiji ambapo Takriban watu 70,000 wanahitaji kwa dharura usaidizi baada ya taifa hilo kukumbwa na tufani. Usambazaji wa misaada ulianzia kwenye mkoa wa Zambezia ambapo takriban watu 60,000 wanapata misaada ikiwemo unga na bidhaa zingine. WFP inasema kuwa ina matumaini ya kutoa chakula cha [...]

03/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya ugonjwa wa Saratani duniani kuadhimishwa kesho

Kusikiliza / mashine ya kutibu ugonjwa wa Saratani

Siku ya Saratani duniani itaadhimishwa tarehe nne mwezi Februari mwaka huu. Ugonjwa wa Saratani unatajwa kuua watu wengi zaidi duniani ukiwa ulisababisha vifo vya watu milioni 7.6 mwaka 2008. Saratani ya tumbo na maini inatajwa kusabahisha vifo vingi zaidi kila mwaka. Matumizi ya tumbaku ndiyo husababisha ugonjwa wa saratani ikiwa inasababisha asilimia 71 ya saratani [...]

03/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya kimataifa yapanga kuwasomea mashtaka watuhumiwa wa mauji wa Hariri nchini Lebanon

Kusikiliza / mahakama ya Lebanon

Mahakama huru iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuchunguza mauwaji ya aliyekuwa kiongozi wa Lebanon Rafik Hariri imesema kuwa inakusudia kuwapandisha kizimbani watuhumiwa 4 wa tukio hilo. Hata hivyo watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kuendesha mashambulizi hayo watasomewa mashtaka bila wao kuwepo mahakamani. Salim Jamil Ayyash, Mustafa Amine Badreddine, Hussein Hassan Oneissi na Assad [...]

03/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha hatua ya serikali ya Haiti kuleta usawa

Kusikiliza / kikosi cha MINUSTAH

Umoja wa Mataifa umesema kuwa unakaribisha kwa furaha hatua ya serikali ya Haiti kuridhia mpango mpya unaokusudia kutoa usawa katika maeneo ya uchumi, jamii na utamaduni. Serikali ya Haiti imeanza kuuratibu mpango huo ambao pamoja na mambo mengine utatilia uzito maeneo ya kukaribisha usawa wa kijamii na kupunguza bengo la kitabaka. Katika taarifa yake kikosi [...]

03/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kaing Guek Eav ahukumiwa kifungo cha maisha gerezani

Kusikiliza / Kaing Guek Eav

Mahakama ya juu nchini Cambodia hii leo imempa Kaing Guek Eav ambaye pia anajulikana kama Duch kifungo cha Maisha gerezani ambayo ndiyo hukumu ya juu zaidi iliyo kwenye sheria kuhusu kesi za uhalifu wa kibinadamu. Mahakama hiyo ilitupilia mbali kifungo cha miaka 35 kilichotolewa na mahakama nyingine tarehe 26 mwezi Julai mwaka 2010. Mahakama hiyo pia [...]

03/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na wasi wasi wa mapigano mapya kwenye jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini

Kusikiliza / mapigano mapya nchini Sudan Kusini

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi kufutia ripoti za mapigano mapya kwenye jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini. Mzozo huo ambao unatajwa kuwa wa mifugo umesababisha vifo vya watu 78. Ripoti zinasema kwamba zaidi ya mifugo 70,000 ilibwa na kuwaacha zaidi ya watu 40,000 bila chochote cha kutegemea. Hata [...]

03/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mwongozo kuhusu matumizi ya madawa ya homoni

Kusikiliza / matumizi ya madawa ya homoni kwa wanawake

Wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa wa ukimwi lakini hata hivyo wanaoishi na virusi hivyo wanaweza kutumia madawa ya homoni. Hata hivyo shirika la afya duniani linataka wahudumu wa afya duniani WHO linaeleza wazi na kuwataka madaktari kuwakumbusha wagonjwa wao kwamba madawa ya homoni hayamkingi mmoja kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi. [...]

03/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kutoa misaada yaomba dola milioni 39 kuwasaidia waathiriwa wa tufani nchini Ufilipino

Kusikiliza / waathiriwa nchini Ufilipino wapokea mkate

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake wametoa ombi la dola milioni 39 za kusaidia katika utoaji wa huduma kwa zaidi ya watu 300,000 walioathiriwa na tufani Washi katika eneo la Mindanao nchini Ufilipino kwa muda wa miezi 6. Kiasi hicho cha fedha kimeongezeka kwa dola milioni 10.6 zaidi kutoka dola milioni 28.4 kilichoombwa awali. [...]

03/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bado Sudan Kusini inakumbwa na changamoto za kibinadamu:Amos

Kusikiliza / Valeria Amos nchini Sudan Kusini

Mkuu wa oparesheni za kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos amesema kuwa taifa la Sudan Kusini lililo na miundo mbinu duni kwa sasa linakabiliwa na changamoto nyingi za kibinadamu. Bi Amos ambaye analitembelea taifa hivyo jimpya la Afrika anasema kuwa watu 360,000 ambao wamerejea kutoka Sudan wanahitaji kuwa na tegemeo la maisha. Bi Amos [...]

03/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaeleza wasi wasi wake kufuatia ripoti za kuteswa kwa wakimbizi nchini DRC

Kusikiliza / wananchi wa DRC

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limeelezea wasi wasi wake kufuatia ripoti za hivi majuzi kuwa wakimbizi wa ndani wameteswa na kuuawa na makundi yaliyojihami kwenye kambi za wakimbizi wa ndani kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Tangu mwanzo wa mwaka 2011 makundi yaliyojihami yamekuwa yakivamia kambi [...]

03/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Njaa yapungua Somalia lakini bado mamilioni wanahitaji huduma za kibinadamu

Kusikiliza / nchini Somalia

Hali ya njaa imetajwa kuisha nchini Somalia lakini hata hivyo Umoja wa Mataifa unaonya kuwa bado hali nchini humo imesalia tete. Umoja wa Mataifa unasema kuwa jitihada kubwa za utaoaji wa misaada ya kibinadamu na mavuno mengi ya chakula yamesaidia katika kuboresha hali nchini Somalia. Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa [...]

03/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amos asikitikia hali mbaya katika jimbo lililokubwa na mapigano ya kikabila la Jonglei Sudan Kusini

Kusikiliza / jimbo la Jongei

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura  ambaye amefanya ziara katika jimbo lililokubwa na mapigano ya kikabila la Jonglei huko Sudan Kusini amesema hali katika eneo hilo ni mbaya.' Katika ziara yake hiyo Bi Valerie Amos, amejionea namna waathirika wa mapigano hayo ya kikabila walivyotuowa mkono na mahitaji muhimu [...]

03/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na maafisa wa Ufaransa kujadilia maendeleo endelevu

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz Al-Nasser

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekuwa na majadiliano na maafisa wa ngazi ya juu ya Ufaransa wakijadilia masuala mbalimbali lakini lile walilolipa uzito zaidi ni juu ya maendeleo endelevu. Nassir Abdulaziz Al-Nasser amekutana na maafisa wa serikali mjini Paris akiwemo waziri wa mambo ya nje Alain Juppé ambao wote kwa pamoja wametupia [...]

03/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban asikitikia ghasia za kwenye uwanja wa mpira Misri

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moom ameelezea masikitiko yake kufuatia ghasia zilizozuka kwenye uwanja wa mpira na kusabisha watu zaidi ya 70 kupoteza maisha nchini Misri. Katika tukio hilo lililohusisha timu mbili zenye upinzani wa jadi, watu wengi kadhaa walijeruhiwa wakati mamia wengine wakiwachwa katika hali ya kihoro. Ghasi hizo zilizoka katika uwanja [...]

03/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Valarie Amos akaribisha kuachiliwa kwa wafanyakazi saba wa misaada Yemen

Kusikiliza / Valerie Amos

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura leo ametangaza kwamba wafanyakazi saba wa misaada waliotekwa mapema wiki hii nchini Yemen sasa wote wameachiliwa bila kudhuriwa. Katika taarifa yake Bi Valarie Amos amesema wafanyakazi hao waliotekwa siku ya Jumanne wiki hii sasa wako mjini Sanaa na wanawasiliana na familia [...]

02/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wawataka raia wa DR Congo kuepuka ghasia kwa kutatua mzozo wa kura kwa njia ya amani

Kusikiliza / matokeo ya kura nchini DRC

Wakati matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa bunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yametangazwa Umoja wa Mataifa leo umewachagiza wahusika wote kutumia njia za kisheria kutatua madai yote ya uchaguzi na kujizuia kutumia nguvu au ghasia. Mamilioni ya raia wa Congo walipiga kura tarehe 28 Novemba mwaka jana kuchagua Rais na wabnge. Wakati [...]

02/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa ECOSOC waanza mjini New York

Kusikiliza / Balozi Miloš Koterec

Kuangamiza umaskini na ajira kwa vijana yatakuwa kati ya masuala yatayoangaziwa kwenye mkutano wa 50 wa tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na maendeleo ya kijamii ambao unaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Kwa muda wa siku kumi zijazo tume hiyo itafanya vikao kadhaa jinsi ya kufanyia mabadiliko sera kuhusu [...]

02/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wailalamikia Ukraine kuwabana waomba hifadhi

Kusikiliza / Nembo ya UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHRC limeelezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya inayowaandama raia wanaoomba hifadhi ya kisiasa nchini Ukraine ambao baadhi yao sasa wanajikuta wakitupwa kizuizini. Ripoti nyingine zinasema kuwa zaidi ya watu 100 ambao waliomba ukimbizi a kisiasa, walikataliwa na kutupwa kizuizini. Kamishna wa UNHCR amesema kuwa ofisi yake imepokea taarifa [...]

02/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwaka mpya wa utamaduni wa China waanza

Kusikiliza / Bi Asha-Rose Migiro

Mamia ya watumbuizaji wamepanda jukwaani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuashiria kuanzisha mwaka mpya wa China wenye shamra shamra za kila aina. Michezo ya kijadi, burudani za hapa na pale pamoja na shughuli nyingine za kiburudani ni baadhi ya mambo yaliyopambwa wakati wa tukio hilo. Akizungumza kwenye tafrija hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa [...]

02/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Shirika la IAEA kufanya mazungmzo zaidi kuhusu programu ya nyuklia nchini Iran

Kusikiliza / Yukiya Amano

Wataalamu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na nishati ya Nyuklia wamekamilisha ziara yao nchini Iran wakisema kuwa wataendelea na majadiliano baadaye mwezi huu kuhusu mpango wa amani wa nchi hiyo. Wataalamu hao walikutana na mafisa wa Iran kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Tehran kwa lengo la kusuluhisha masuala yenye utata huku mkutano [...]

02/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa haki za wanaopigania amani kuzuru Honduras

ramani ya Honduras

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa amani Bi Margaret Sekaggya atazuru Honduras kuanzia Februari 7 hadi 14 mwaka huu. Lengo la ziara yake ni kutathimini hali ya haki kwa watetezi wa haki za binadamu nchini humo. Bi Sekaggya ameongeza kuwa atakuwa na mazungumzo na serikali ili kuhakikisha kwamba watetezi wote [...]

02/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNIDSR akaribisha juhudi za WMO za mfumo wa kukabili majanga mapema

Kusikiliza / Margaret Wahlstrom

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa mkakati wa kimataifa wa kupunguza majanga UNISDR Margareta Wahlstrom Alhamisi amekaribisha tangazo la shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO la kuanza kufanya kazi kwa mfumo mpya wa taarifa za hali ya hewa. Bi Wahlstrom amesema hatua hiyo ni mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya [...]

02/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wasikitishwa na matumizi mabaya ya sheria za ugaidi kubana uhuru wa kujieleza

Kusikiliza / uhuru wa kujieleza Ethiopia

Wataalamu kadhaa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Alhamisi wameelezea kutoridhika na kuendelea kutumia vibaya sheria za kupambana na ugaidi kubana uhuru wa kujieleza nchini Ethiopia. Wiki iliyopita waandishi habari watatu na wanasiasa wawili wa upinzani walikatiwa vifungo vya miaka 14 hadi maisha jela chini ya sheria za Ethiopia za kupambana na ugaidi. [...]

02/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waendesha oparesheni ya kutwaa silaha nchini Ivory Coast

Kusikiliza / unoci-disarm

Oparesheni ya hiari ya Umoja wa Mataifa ya kukusanya silaha imeng'oa nanga mjini Abidjan nchini Ivory Coast kwa lengo la kukusanya silaha haramu zilizo mikononi mwa raia. Oparesheni hiyo inayoongozwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI ni sehemu ya kampeni kubwa iliyoanza mwezi Juni na inayolenga maeneo kadha nchini humo. Naibu [...]

02/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pillay aitaka serikali, wagombea na wafuasi kupinga ghasia Senegal

Kusikiliza / Bendera ya Senegal

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay Alhamisi amelelezea hofu yake kuhusu uwezekano wa matumizi ya nguvu kupita kiasi unaofanywa na serikali mjini Dakar na miji mingine nchini Senegal. Ameonya kwamba utamaduni wa muda mreru wa kuwa na uchaguzi wa kidemokrasia nchi humo upo kwenye hatihati endapo serikali itashindwa kudhibiti inavyostahili maandamano yanayoendelea. Watu [...]

02/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wito wa uhamasishaji na kutimiza ahadi za haki za wanawake watolewa:Bachelet

Kusikiliza / Michelle Bachelet

Mkurugenzi mtendaji wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake yaani UN Women Bi Michelle Bachelet ametoa wito wa dunia kutimiza ahadi na kuchukua hatua kuhakikisha usawa wa kijinsia kwa wanawake wakati huu ambapo siasa na hali ya uchumi inatishia maendeleo ya haki za wanawake. Akizungumza katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuundwa [...]

02/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makazi ya walowezi wa kiyahudi sio kitovu cha mgogoro:Netanyahu

Kusikiliza / Ban Ki-moon na Benjamin Netanyahu

Ujenzi wa makaazi ya walowezi unaofanywa na Israel katika eneo la Wapalestina linalokaliwa sio kitovu cha machafuko Mashariki ya Kati amesema waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Netanyahu ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon mjini Jerusalem kabla Ban hajaenda Gaza. Ban amesema amemweleza [...]

02/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Gaza ni suala linalopewa kipaumbele na UM:Ban

Kusikiliza / Ban  azuru Gaza

Hali ya utulivu japo mdogo unaojitokeza hivi sasa Gaza lazima iendelee amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari alipozuru mradi wa Khan Yonis mjini Gaza Alhamisi amesema kuendelea kupiga hatua kwa watu wa Gaza kunahitaji hatua kadhaa kuchukuliwa. Hatua hizo amesema ni pamoja na mabadiliko ya [...]

02/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa OCHA awasili Juba Sudan Kusini

Kusikiliza / Valerie Amos

Katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu Sudan Kusini mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Valarie Amos amekutana na wawakilishi wa mashirika ya misaada mjini Juba. Bi Amos na wawakilishi hao wamejadili changamoto mbalimbali za kibinadamu zinazolikabili taifa hilo changa ikiwa inajongea miezi sita tangu [...]

01/02/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wasema kuwa kambi mpya ya wakimbizi kutoka Iran inatimiza viwango vya kimataifa

Kusikiliza / Martin Kobler

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanaohusikia na masuala ya wakimbizi na haki za binadamu wamesema kuwa wamethibitisha kwamba miundo msingi na hali kwenye kambi mpya ambayo ni ya wakimbizi kutoka kwa kambi ambayo awali ilikuwa ikifahamika kama kambi ya Ashraf imetimiza viwango vya kimataifa kulingana na makubaliano kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya [...]

01/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya Yugolavia ya zamani kuendelea na kesi ya Jelena Rasic

Kusikiliza / Jelena Rasic

Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mzozo wa Balkans wa miaka ya tisini imekubali kuendelea na kesi ya Jelena Rasic , ambaye anashutumiwa kwa kupata habari isiyo halali kutoka kwa mashahidi kwa njia ya pesa. Bi Rasic amekiri makosa yote mbele ya mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusu Yugoslavia ya zamani iliyo mjini Hague. [...]

01/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ataka pande zinazo zozana nchini Senegal kuachana na vurugu

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikito yake kufuatia kuendelea kushuhudiwa misukosuko ya kisiasa nchini Senegal. Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa watu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi kufuatia uamuzi wa rais Abdoulaye Wade kuwania urais kwa muhula wa tatu kama rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi. Kwenye taarifa kupitia [...]

01/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wazindua kituo cha upashaji habari ili kukabili majanga ya kimazingira

Kusikiliza / Mabadiliko ya hali ya hewa

Umoja wa Mataifa umezindua kituo cha upashaji habari ambacho kinakusudia kuimarisha na kutawanya taarifa muhimu zinazohusu mabadiliko ya tabia nchi, ikiwa ni kama sehemu ya kuiandaa jamii kukabiliana na majanga ya kimazingira yanayoikumba ulimwengu mara kwa mara. Pia kituo hicho kinawajibika kutoa taarifa zinazohusu hali ya hewa na hivyo kuyaepusha mataifa mbalimbali na janga la [...]

01/02/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

KM Ban Ki-moon afafanua umuhimu wa vitabu akizindua mkataba Ethiopia

Kusikiliza / Watoto wakisoma Ethiopia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezindua mktaba mpya nchini Ethiopia kwa ajili ya kuongeza msukumo wa elimu kwa wanafunzi wa elimu ya msingi huku pia akisherekea mapinduzi makubwa yanayoweza kubadili mitazamo ya vijana kupitia vitabu. Uzinduzi wa maktaba hiyo umefanikiwa kupitia mbinu za kisasa zilizobuniwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwanufaisha wanafunzi [...]

01/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi wa WFP akaribisha hukumu kwa watu waliouwa mfanyakazi wa shirika hilo

Kusikiliza / wafanyakazi wa shirika la  WFP nchini Kenya

Mkurugenzi mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Bi Josette Sheeran amekaribisha uamuuzi wa mahakama kuu ya Kenya kuwahukumu kwenda jela watu watano waliohusika na mauaji ya mfanyakazi wa shirika hilo Silence Chirara nchini Kenya mwaka 2008. Watu hao watano wamehukumiwa kifungo cha miaka 56 kila mmoja. Bi Sheera amesema ingawa hakuna linaloweza [...]

01/02/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya mkuu wa kituo cha radio mjini Moghadishu

Kusikiliza / Kituo cha radio Moghadishu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amelaani vikali mauaji ya karibuni ya mkurugenzi wa kituo cha radio bwana Hassan Osman Abdi na ameutaka uongozi wa Somalia kuchunguza mauaji hayo na kuwafikisha wahusiaka kwenye mkono wa sheria. Mahiga amesema amestushwa sana na mauaji hayo ya mmoja wa waandishi habari mahiri nchini [...]

01/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guinea-Bissau yaachana na migodi isiyostahili

Kusikiliza / migodi ya Guinea

Serikali ya Guinea-Bissau imekuwa nchi ya karibuni kutangaza kwamba imeachana na migodi yote isiyostahili kwa kuzingatia mkataba wa Ottawa unaopinga migodi holela. Mkurugenzi wa Guinea-Bissau anayehusika na programu ya serikali ya kupambana na uchimbaji holela wa madini Lopez de Carvalho amesema inafahari kubwa kutangaza kwamba maeneo yote yanayojulikana kuwa na migosi isiyofaa sasa yamesafishwa na [...]

01/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uzalishaji wa mpunga mwaka 2011 wavunja rekodi:FAO

Kusikiliza / mavuno ya mpunga

Uzalishaji wa mpunga kimataifa unatarajiwa kuvunja rekodi wakati takwimu za uzalishaji kwa mwaka 2011 zikikamilika limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Shirika hilo linasema mavuno ya mpunga yameongezeka kwa tani 700,000 hasa barani Asia. Uzalishaji wa mpunga ulipanda kwa asilimia 3 zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2010. Ongezeko hilo limechangiwa sana na msimu mzuri wa [...]

01/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP imezindua wiki ya kimataifa ya mchele wa bure kupambana na njaa kwa kutumia mtandao

Kusikiliza / mchele wa bure kupitia mtandao wa freerice.com

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limezindua wiki ya kimataifa ya kupambana na njaa kwa kutumia mtandao. Shirika hilo linasema dhana ya mgawanyiko wa nyuzi sita inasema kwamba kila mtu duniani ameungana na takribani watu wengine sita duniani, hivyo kwa kutumia mchezo wa kupambana na njaa iliouanzisha kwenye mtandao uuitwao [...]

01/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Usalama watofautiana kwa utekelezaji wa mswaada wa azimio kuhusu Syria

Kusikiliza / Baraza la Usalama lajadili suala

Maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani, Uingereza, Ufaransa na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa waliokutana Jumanne jioni katika kikao maalumu cha Baraza la Usalama kutoa shinikizo la kupitisha mswaada wa azimio litakalounga mkono mipango ya Umoja wa nchi za Kiarabu kuhusu suala la Syria watofautiana. Mswada huo wa azimio unamtaka Rais Al-Assad [...]

01/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hiki ni kipindi muhimu sana kwa Israel na eneo zima la Mashariki ya kati:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na rais wa Israel Shimon Peres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefanya mazungumzo na Rais wa Israel Shimon Peres mjini Jerusarem Jumatano. Ban na Peres wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo changamoto za hali ya Mashariki ya Kati. Ban amesema ushirikiano wa Israel katika kuleta tangamano kwenye eneo la Mashariki ya Kati ni muhimu sana, kwani Rais Peres amekuwa msitari [...]

01/02/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930