Nyumbani » 31/10/2011 Entries posted on “Oktoba, 2011”

UNODC na UNHCR watia saini muafaka kukabili usafirishaji haramu wa watu na wahamiaji

human-trafic1

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu na madawa UNODC leo wametia saini muafaka wenye lengo la kupambana na usafirishaji haramu wa watu na uingizaji haramu wa wahamiaji. Muafaka huo uliotiwa sahihi na kamishina mkuu wa wakimbizi Antonio Guterres na mkuu wa UNODC Yuri Fedotov [...]

31/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Saif Al Islam huenda akajisalimisha ICC

Saif Al Islam Qadhafi

Kuna taarifa kuwa huenda mtoto wa pili wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Qadhafi, akajisalimisha kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Kwa mujibu wa mkuu wa mashtaka kwenye mahakama hiyo Luis Moreno Ocampo, mtoto huyo wa Qadhafi, Saif Al Islam Qadhafi, kumeanza kufanywa mawasiliano ambayo yanaashiri kuwepo kwa uwezekano wa kujisalimisha kwake.  Saif pamoja na [...]

31/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mauwaji ya waandamanaji Syria

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali tukio la kushambuliwa waandamanaji wa Syria iliyosababisha watu kadhaa kupoteza maisha na ameitaka serikali nchini humo kuzuia matumizi ya nguvu kudhibiti maandamano hayo. Wananchi wa Syria wameendelea kujitokeza bara barani wakisisitiza haja ya kufanyika mageuzi ya kisiasa ili kufungua fursa zaidi za kidemokrasia. Ikiweka shabaya [...]

31/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yajiunga na UNESCO

Nemba ya UNESCO

Shirika la elimu , Sayansi , na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limelikaribisha taifa jipya la Sudan Kusini ambayo ndiyo nchi iliyo na viwango vya chini zaidi vya elimu duniani. Kwenye sherehe zilizofanyika mjini Paris yaliyo makao makuu ya UNESCO bendera ya Sudan Kusini ilipandishwa kando na za wanachama wengine 193 wa UNESCO. Sherehe [...]

31/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Operesheni za Kenya na serikali ya mpito dhidi ya Al-Shabaab zikikamilika mambo yatakuwa shwari:Mahiga

Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalmu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema ana matumaini operesheni za pamoja za kijeshi za serikali ya mpito na Kenya dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab zikikamilika hali ya amani itakuwa shwari Somalia. Balozi Mahiga akizungumza na mwandishi wa habari wa radio ya Umoja wa mataifa mjini Nairobi Kenya Jason Nyakundi [...]

31/10/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mkuu mpya wa mipango ya Usalama wa UM azuru Darfur

mkuu wa mipango ya usalama wa UM Hervé Ladsous

Mkuu mpya wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa amezuru kwa mara ya kwanza kituo kimoja kati ya 16 vya operesheni za Umoja wa Mataifa duniani. Herve Ladsou amechagua kituo kikubwa cha operesheni ambacho ni Darfur Sudan na amekutana na maafisa wa serikali wa eneo hilo, jumuiya za kijamii na wafanyakazi wa mpango [...]

31/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa UNHCR wauawa katika shambulio Afghanistan

afisi ya UNHCR nchini Afganistan

Leo asubuhi shambulio la kupangwa lililohusisha watu wa kujitoa muhanga kwenye mji wa Kandahar nchini Afghanistan limeuwa wafanyakazi watatu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kujeruhi wengine wawili. Shambulio hilo limefanyika katika eneo la ofisi za UNHCR. Katika taarifa iliyotolewa leo na kamishina mkuu wa wakimbizi Antonio Guterres, UNHCR inatafuta [...]

31/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirika katika kilimo ni muhimu kwa kupunguza umaskini na njaa:FAO, IFAD WFP

washiriki katika kilimo

Wakulima wadogowadogo wanafaidika sana kwa ushirika wa kilimo ikiwemo uwezo wa kushawishi masuala ya bei na kushirikiana rasilimali ambazo zinasaidia kupunguza umasikini na kuleta usalama wa chakula kwa mamilioni ya watu limesema shirika la chakula na kilimo FAO, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Tamko [...]

31/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchini Somalia hali bado ni tete lakini matumaini ya amani bado yapo:Mahiga

Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema hali ya usalama nchini Somalia bado ni tete lakini kuna matumaini kuwa punde mambo yataanza kuwa shwari. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Nairobi Kenya hii leo balozi Mahiga amesema maeneo yanayoshikiliwa na wanamgambo wa Al-Shabaab bado kuna hofu sana, watu wanaendelea kukimbia [...]

31/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia inaelekea mtafaruku mkubwa wa ajira:ILO

ukosefu wa ajira duniani

Tathimini iliyotolewa na shirika la kazi duniani ILO katika mkesha wa kuanza kwa mkutano wa viongozi wa G-20 inasema uchumi wa dunia uko katika hatihati ya kutumbukia katika mtafaruku mkubwa wa ukosefu wa ajira. ILO inasema hali hiyo itachelewesha zaidi kuchipuka upya kwa uchumi baada ya mdororo na huenda ikachochea machafuko zaidi katika nchi mbalimbali. [...]

31/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa Haki za Binadamu akaribisha mwanahaki wa bilioni 7

mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay leo amekaribisha mtoto aliyezaliwa na kuifanya idadi ya watu duniani kufikia bilioni saba kwa ahadi ya kuzingatia azimio la kimataifa la haki za binadamu. Amesema kisheria mtoto huyo awe wa kike au wa kiume amezaliwa huru na usawa katika utu na haki za binadamu. Ameongeza kuwa tangu [...]

31/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu duniani imetimu bilioni 7:Ban

Idadi ya watu imefika bilion 7

Idadi ya watu duniani leo imetimu rasmi bilioni 7 amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York katika hafla maalmu ya kusherehekea tukio hilo. Ban amesema siku hii ya kutimiza watu bilioni saba sio kuhusu kuzaliwa kwa mtoto mpya [...]

31/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano mkuu wa UNESCO umepiga kura kuijumuisha Palestina katika uanachama

Palestine yajumuishwa kama mwanachama wa UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO leo limepiga kura kwenye mkutano mkuu wa shirika hilo na kuijumuisha Palestina kama mwanachama wake mpya. Kura hiyo inaifanya Palestina kuwa mwanachama wa 195 wa UNESCO. Wanachama 107 wamepiga kura kuunga mkono, 14 wamepinga na 52 hawakupiga kura kabisa. Kwa mujibu wa UNESCO uanachama [...]

31/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia ghasia kati ya Israel na Ukanda wa Gaza

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa hisia zake kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa kusini mwa Israel na kwenye ukanda wa Gaza ambapo watu kadha wameuawa. Kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban amelaani shambulizi la roketi lililoendeshwa kutoka ukanda wa Gaza ambalo lilisabaisha kifo cha raia mmoja wa Israel. Ban pia ameitaka Israel kujizuia [...]

31/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo kuhusu Cyprus yapiga hatua

Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Dimitris Christofias (kushoto) na Dervis Eroglu (kulia)

Kumeripotiwa mafanikio kwenye mazungumzo ya siku mbili kati ya viongozi wa Cypriot nchini Ugiriki na Uturuki pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Mshauri maalum wa katibu mkuu kuhusu Cyprus Alexander Downer amesema kuwa Umoja wa Mataifa umefurahishwa na jinsi mazungumzo kati ya kiongozi wa Cypriot nchini Ugiriki Dimitris Christofias na kiongozi [...]

31/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vijana barani Afrika wanasema wakati umefika wa kusikilizwa

Vijana wa Kiafrika

Kila mwaka Novemba mosi vijana kote barani Afrika wanaadhimisha siku yao kwa hafla na shughuli mbalimbali ikiwemo mijadala na maandamano.  Mwaka huu kimataifa siku hii inaadhimishwa nchini Afrika ya Kusini ambako vijana kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika watakutana kuanzia Novemba mosi na pili Gauteng mjini Johanesburg. Mbali ya maadhimisho vijana hao watajadili pia matatizo yanayowakabili [...]

28/10/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila watu saba, watano kati yao hawana uhakika wa ustawi wa kijamii

kila watu saba, watano hawana uhakika wa kijamii

Kundi la wataalamu wa mambo limetoa mwito likizitaka serikali duniani kuongeza mafungu ya kipato na kuboresha hali ya ustawi wa kijamii ili hatimaye kufadhilia amani na usalama pamoja na ukuzaji uchumi. Kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO, zaidi ya watu bilioni 5 duniani kote hawana uhakika wa ustawi wa kijamii. Wakati huo huo [...]

28/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wataka kuweko shabaha ya pamoja kukabili tatizo la ukosefu wa kazi duniani

Rais Lazarous Kapambwe wa ECOSOC

 Jamii ya kimataifa imehimizwa kuweka zingatio la pamoja kwa kushagihisha mifumo yake ili hatimaye iweze kufaulu kukabili tatizo la ajira linaloiandama dunia kwa sasa.  Kwa mujibu wa rais wa baraza la uchumi na la kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC Bwana Lazarous Kapambwe kuna haja kubwa kwa jamii ya kimataifa kufungamanisha mifumo yake ya ukuzaji [...]

28/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuondosha ziada ya risasi kwenye nishati ya mafuta kutanufaisha afya za wengi-Utafiti

kuondoa zaidi ya nishati ya mafuta

Utafiti mmoja unaonyesha kuwa iwapo kutowekwa zingatia la kuondoa ziada ya risasi inayowekwa kwenye nishati ya mafuta, ulimwengu unaweza kupiga hatua kubwa na kufanikiwa kuzikwepa gharama zizozo za lazima.  Kwa mujibu wa utafiti huo unaungwa mkono na Umoja wa Mataifa,matokeo kadhaa yamejidhihirisha ikiwemo kupunguza gharama za uzalishaji, kuokoa vifo visivyo vya wakati vinavyojiri sasa pamoja [...]

28/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasafirisha misaada kwenda nchini Uturuki

msaada kutoka Shirika la UNHCR

Ndege nne zilizosheheni misaada kutoka shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR zinatarajiwa kutua kwenye mji wa Erzurun kuanzia hii leo ili kuwapelekea misaada waathiriwa wa tetemeko la ardhi kwenye eneo la mashariki mwa Uturuki. Ndege ya kwanza inatarajiwa kusafirisha tani 37 kutoka ghala la UNHCR mjini Dubai huku ndege zingine tatu zikitarajiwa [...]

28/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kitabu kuhusu malengo ya milenia chapata tuzo

kitabu cha malengo ya milenia

  Jumla ya mashirika sita ya Umoja wa Mataifa yametunukiwa tuzo la mwaka huu la amani na michezo kutokana na mradi wao wa kitabu cha vichekesho chenye kichwa 'Funga mabao – Kuungana katika kutimiza malengo ya milenia'. Tuzo hiyo ilitolewa mjini Monaco kwenye kongamano la kimataifa kuhusu amani na michezo mbele ya watu 500 mashuhuri [...]

28/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM kusambaza misaada nchini El Salvador, Guatemala na Nicaragua

wasaidize wa IOM nchini El Salvador

Fedha kutoka kwa mfuko wa huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa nchini El Salvado zinasaidia shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuendelea na usimamizi wa vituo 42 vinavyotoa makao ya muda kwa watu 1,895 kuhakikisha kuwa kuna usafi ya mazingira na pia usambazaji wa misaada miongoni mwa waathiriwa. Kiasi kikubwa cha mvua ambayo imenyesha [...]

28/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Norway kupoteza kutambuliwa kwake kama mtunzi wa haki za watu wa asili

Norway kupoteza kutambuliwa kama mtunzi wa haki za watu wa asili

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya haki za watu wa asili James Anaya ameonya kuwa ikiwa taifa la Norway litafanyia marekebisho sheria na sera zinazowalenga watu wa jamii ya Sami huenda ikapoteza kutambuliwa kwake kama taifa linaloongoza katika kulinda haki za watu wa asili. Sami ni watu wa asili wanaoishi Kaskazini mwa [...]

28/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yatoa wito wa hatua za kuiokoa Niger kutoka kwenye njaa

njaa nchini Niger

Hali ya ukosefu wa chakula nchini Niger inaendelea kutia wasiwasi huku ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi ikiwa hatua za mapema hazitachukuliwa. Familia nyingi kwa sasa hawana uwezo wa kukabiliana nayo baada ya ya hali kama hiyo kushuhudiwa mwaka mmoja uliopita. Kulingana na shirika la mpango wa chakula duniani WFP ni kwamba watu milioni moja wanahitaji msaada [...]

28/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi yasema haitavunjika moyo licha ya wanajeshi wake kuuawa Somalia

Wanajeshi wa AMISOM

Huko Burundi, Jeshi la nchi hiyo limesema kwamba halitavunjika moyo licha ya tukio la hivi karibuni nchini Somalia ambako walinda amani wake katika kikosi cha Amisom waliuwawa wiki iliopita. Hata hivo giza linaendelea kutanda kuhusu idadi ya wanajeshi waliouwawa. Taarifa za kutofautiana zilitolewa, Al Shabab wakidai kuwauwa wanajeshi wa Burundi zaidi ya 70 huku Jeshi [...]

28/10/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mamia ya wakimbizi kutoka Sudan walikimbia eneo la Blue Nile na kuingia Ethiopia

wahamiaji kutoka Sudan

Mashambulizi ya anga kwenye jimbo la Blue Nile nchini Sudan yamewalazimu wakimbizi zaidi kuhama eneo hilo na kukimbilia Ethiopia. Kwa muda wa siku nne zilizopita karibu wakimbizi 2000 kutoka Sudan wamewasili magharibi wa Ethiopia huku Wengi wakiwa ni wanawake, watoto na watu wazee. Ripoti zinasema kuwa wapiganaji waliojihami kutoka upande wa Sudan wanajiandaa kulipiza kisasi. [...]

28/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa UM wa kupinga ufisadi kufika kikomo leo

kupambana na ufisadi

Zaidi ya washiriki 1000 walikusanyika kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kupinga ufisadi juma hili nchini Morocco kujadili njia bora za kukabiliana na ufisadi duniani. Mkutano huo ulioandaliwa kwenye mji wa Marrakech kuanzia tarehe 24- 28 mwezi huu. Kati ya ajenda kuu zilizozungumziwa kwenye mkutano huo ni pamoja na kuzuia ufisadi, kutwaa mali yaliyoibwa [...]

28/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili ripoti kuhusu wanawake, amani na usalama

wanawake kuhusishwa katika juhudi za kuleta amani na usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejadili ripoti kuhusu wanawake, amani na usalama. Ripoti hiyo inahusu mchango kutoka kwa wanachama 38, mashirika manne ya kimaendeo na idara 27 za Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshauri nchi wanachama kuongeza idadi ya wanawake kwenye nafasi za juu katika masuala [...]

28/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama kumaliza operesheni za NATO nchini Libya

27/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu duniani ikielekea bilioni 7 UM unahakikisha maendeleo kwa wote

27/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Theluji na mvua yaikumba uturuki ambako waliokufa na tetemeko wamefikia 532

tetemeko la ardhi Uturuki

Theluji na mvua vinatatiza shughuli za uokozi kufuatia tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki huku idadi ya waliokufa ikizidi 500 umesema uongozi wa nchi hiyo. Tetemeko lililikumba eneo la Mashariki la Van Jumapili iliyopita na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu. Umoja wa mataifa umepongeza juhudi za haraka za serikali kukabiliana na janga [...]

27/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama limepiga kura kumaliza operesheni za NATO Libya

Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo Alhamisi limepiga kura kumaliza operesheni za kimataifa za kijeshi za NATO nchini Libya. Wajumbe 15 wa baraza hilo wameamua kumaliza idhini yake ya vikwazo vya safari za anga kama hatua ya kuwalinda raia kuanzia Jumatatu ijayo. NATO wiki iliyopita ilitangaza kwamba ingekomesha operesheni zake za kijeshi Libya [...]

27/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa mpya za matumizi ya maji kwa kilimo zitalinda usalama wa chakula

mto Nile

Ongezeko la idadi ya watu na kumomonyoka kwa mali asili kwenye bonde la mto Nile kunaleta hatari ya kuzuka kwa njaa na umasikini kwenye kanda hilo na hivyo mipango madhubuti ya kuzuia kuzuka kwa janga hilo inahitajika limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Onyo hilo limetolewa wakati FAO ikiwasilisha matokeo ya mradi wa miaka [...]

27/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Israel na Palestina waafiki kutoa mapendekezo ya amani:UM

washirika wa Quartet

Umoja wa Mataifa na washirika wake wa kidiplomasia katika kutafuta amani ya Mashariki ya Kati wamekutana katika nyakati tofauti na maafisa wa Israel na Palestina mjini Jerusalem, na pande zote kuafiki kutoa mapendekezo ya kina ya utaifa na usalama ndani ya miezi mitatu. Jopo hilo lijulikanalo kama Quartet linalojumuisha Umoja wa Mataifa, muungano wa Ulaya, [...]

27/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Waliberia wametakiwa kuendesha duru ya pili ya uchaguzi kwa amani na utulivu

uchaguzi nchini Liberia

Baraza la Usalama limewataka Waliberia kuendesha duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika Novemba 8 kwa amani na usalama. Matokeo ya awamu ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 11 na kutangazwa Jumanne ya wiki hii yameonyesha kwamba rais aliyeko madarakani Ellen Johnson-Sirlef anaongoza kwa asilimia 43.9 ya kura zote akifuatiwa na bwana Tubman [...]

27/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya dola bilioni moja kwa waathirika wa uvamizi wa Iraq nchini Kuwait:UM

Iraq-tanker

Zaidi ya dola bilioni moja zimetolewa na tume ya fidia ya Umoja wa Mataifa UNCC hii leo kwa ajili ya kulipa fidia madai manane ya walioathirika na kupoteza kila kitu wakati Iraq ilipoivamia Kuwait mwaka 1990. Malipo ya leo ya dola bilioni 1.3 yanafanya jumla ya fidia iliyolipwa na tume hiyo hadi sasa kufikia dola [...]

27/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usalama wa chakula ni muhimu:Ban

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema siku ya chakula duniani mwaka huu imeadhimishwa wakati ambapo Pembe ya Afrika inakabiliwa na ukame mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 60. Amesema na sehemu zilizoathirika zaidi ni zile za Kusini mwa Somalia ambazo ni vigumu wafanyakazi wa misaada kuzifikia. Kwengineko amesema hali bado ni [...]

27/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yaweka lugha ya kichina kwenye mtandao

lugha ya kichina yaongezwa kwenye mtandao wa WFP

Shirika la kimataifa linalohusika na mpango wa chakula WFP, limeongeza gia kwenye harakati zake za kukabiliana na tatizo la njaa dunia kwa kuanzisha mpango wa lugha ndani ya mtandao. Watumiaji wa mtandao huo sasa wataweza kujifunza lugha na maneno mapya ambayo yamefungamanishwa katika lugha ya kichina. Waratibu wa mpango huo wamesema kuwa sasa raia wa [...]

27/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban azipongeza taasisi zisizo za kiserikali

Katibu Mkuu Ban Ki-moon kwenye mkutano na mashirika yasiyo ya kiserikali

  Uwepo wa taasisi zisizo za kiserikali ni muhimu hasa wakati huu ambapo dunia inalenga shabaya ya kufikia amani na usalama. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye alikuwa akizungumza kwenye kongamano moja lililoyaleta pamoja mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali. Ban amepongeza mchango mkubwa kutoka kwa taasisi hizi [...]

27/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ushirikinao wa Kimataifa suluhu la hali mbaya ya uchumi:Al Nasser

rais wa Baraza Kuu Nassir Abdulaziz Al-Nasser

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser ameelezea umuhimu uliopo kwenye ushirikiano wa kimataifa katika kukabilina na hali mbaya ya uchumi duniani. Akiongea alipoongoza mkutano kwenye makao makuu ya UM wa kujadili mkutano wa mataifa tajiri na yanayoinukia kiuchumi ya G20 utakaondaliwa wiki ijayo Al-Nasser amesema kuwa masuala mmakuu kama haya [...]

27/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ICC yaelezea ushirikiano kati yake na UM

rais wa ICC Sang-Hyun Song

Rais wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC amesema kuwa uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Umoja wa Mataifa unaendelea kuwa wenye umuhimu. Akihutubia nchi wanachama wa mahakama hiyo Jaji Sang Hyun Song amesema kuwa kati ya wajibu wa ICC na Umoja wa Mataifa ni pamoja na kuzuia na kuwaadhibu waliotenda uhalifu [...]

27/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu 500,000 hufa kila mwaka kutokana na ghasia zinazohusisha silaha:UM

vurugu kutokana na silaha

Ripoti ya kimataifa ya mzigo utokanao na ghasia za kutumia silaha kwa mwaka 2011 inasema takribani watu 526,000 wanakufa kila mwaka kutokana na ghasia zinazohusiha matumizi ya silaha, ikiwa ni zaidi ya watu 1,400 kila siku. Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu wanaokufa katika vita kila mwaka ni 55,000, hii ni ndogo sana ikilinganishwa na [...]

27/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Thamani ya urithi wa matukio ya sauti, video na picha ni kubwa kwa dunia:UNESCO

askari wa MONUC atumia video

Umoja wa Mataifa leo umetanabaisha umuhimu wa kuhifadhi urithi wa dunia katika sauti, video na picha, ukisisitiza hatari ya kuharibika matukio yaliyorekodiwa kwa njia ya sauti, filamu au video, na kusema kuna haja ya juhudi za kuhakikisha kwamba zinahifadhiwa vizuri kwa ajili ya vizazi vijavyo. Likiadhimisha siku ya kimataifa ya urithi wa sauti na filamu [...]

27/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazingira ya kifo cha Gaddafi lazima yachunguzwe asema mwakilishi wa UM

Ian Martin

Kiongozi wa zamani wa Libya kanali Muammar Gaddafi na mwanaye wa kiume hawakutendewa vyema na wameuawa katika mazingira ya kutatanisha ambayo lazima yachunguzwe amesema afisa wa Umoja wa Mataifa. Ian Martin, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Libya ameliambia Baraza la Usalama leo Jumatano kwamba mauaji kama hayo mjini Sirte pia ni kinyume na maagizo [...]

26/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wawatunuku wanafunzi kutokana na uvumbuzi wao

Washindi wa Tuzo la UM

Jiko ndogo ambalo linaweza kutumiwa kwenye mapishi ya nyumbani na linalotumia majani yaliyokaushwa na makaratasi ni kati ya miradi miinne iliyobuniwa na wanafunzi na ambayo inapata tuzo la Umoja wa Mataifa la uvumbuzi wa kimazingira. Sara Rudianto kutoka Indonesia , Maria Rosa Reyes Acosta kutoka Ecuador , Michael Muli kutoka Kenya na Mary Jade Gabanes [...]

26/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM kutoa usadizi zaidi kwa nchi zinazofanya uchaguzi

Lynn Pascoe

Mkurugenzi wa masuala ya kisiasa kwenye Umoja wa Mataifa Lynn Pascoe amesema kuwa Umoja wa Mataifa utahitaji kutoa usaidizi zaidi kando na usaidizi wa kiufundi kwenye uchaguzi kwa kuwa changuzi nyingi huwa zinafautiwa na ghasia. Akihutubia wajumbe kwenye kamati inayohusika na masuala ya kijamii na kibinadamu Pascoe amesema kuwa mara nyingi uchaguzi ndio unakuwa mwanzo [...]

26/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mataifa yatoa wito mpya wa kuindolea Cuba vikwazo

Vikwazo Cuba

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeitaka Marekani kuiondolea Cuba vikwazo ilivyoiwekea karibu nusu karne iliyopita. Kwa mwaka wa 20 sasa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa likipitisha azimio la kuitaka Marekani kuondoa vikwazo vikiwemo vya kiuchumi na vya kifedha ilivyoiwekea nchi hiyo ya Caribbean. Mwaka huu wanachama 186 kati ya wanachama 193 [...]

26/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misitu inaweza kulisha walio na njaa duniani:UM

msitu

Misitu inaweza kuwa na jukumu muhimu la kuilisha dunia kwa mazao yake kuanzia majani yenye vitamin hadi matunda na mizizi, kwa mujibu wa ushirikiano wa kimataifa wa ubia wa misitu CPF unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. CPF imezitaka serikali kuwekeza zaidi katika utunzaji na uhifadhi wa misitu. Kwa mujibu wa CPF yenye wanachama 14 [...]

26/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zakubaliana kupiga marafuku masalia ya bidhaa zenye kuleta sumu

Masalia ya bidhaa zenye kuleta sumu

Kuna uwezekano wa kuanza kutumika kwa azimio la pamoja linalotaka kuzuia usafirishaji wa masalia ya vitu ambavyo ni hatari kutoka katika nchi zilizoendelea kupelekwa katika nchi zinazoendelea. Makubaliano hayo ambayo yanajulikana kama “Ban Amendment” yanaweza zingatio la uzuiaji usafirishaji wa bidhaa zozote zilizokwisha tumika ambazo zinaweza kuleta madhara pale zinaposafirishwa hadi katika nchi za dunia [...]

26/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waasi wajumuishwe kwenye mchakato wa amani Darfur:UM

Herve Ladsous

Wakati hatua muhimu zimepigwa katika mchakato wa amani kwenye jimbo la Darfur Sudan, juhudi zaidi zinahitajika ili kuwajumuisha waasi kwenye mchakato huo ambao bado wanapambana na majeshi ya serikali amesema mkuu wa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. Herve Ladsou ameliambia Baraza la Usalama kwamba anazitaka pande zote ambazo hazijasitisha vita kufanya hivyo [...]

26/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa UM Libya amesema ukombozi wa Libya ni ukurasa mpya

Georg Charpentier

  Mratibu wa masauala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya George Charpentier amezuru mji wa Sirte Libya leo akifungua njia ya mpango wa tathimini ya mji huo na Ban walidi utakaohitimishwa siku mbili zijazo. Mpango huo unafuatia zoezi la kuandaa usambazaji wa misaada ya kibinadamu karibu na maeneo hayo katika maandalizi [...]

26/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makampuni ya dawa na taasisi za utafiti zatoa utaalamu wa kutibu Malaria na TB:WIPO

kutibu ugonjwa wa malaria

Shirika la kimataifa la kuhodhi taaluma WIPO kwa ushirikiano na makampuni makubwa ya dawa na wadau wengine wa afya duniani leo wamezindua muungano mpya waliouita WIPO Re:Search ambapo mashirika ya sekta za umma na za binafsi yataweza kushirikiana utaalamu. Muungano huo utaziwezesha sekta hizo kubadilishana utaalamu na uzowefu na jumuiya ya kimataifa ya utafiti wa [...]

26/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya pamoja ya UNCTAD, OECD na WTO yasema kuna haja ya G20 kuchukua hatua haraka

G20

Ripoti ya pamoja ya shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo na biashara UNCTAD, shirika la kimataifa la biashara WTO na shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD imebaini kwamba uchipukaji wa uchumi baada ya mdororo unakabiliwa na changamoto mpya na huenda ukuaji wa uchumi katika nusu ya pili ya mwaka 2011 ukapungua. Kufuatia [...]

26/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Changamoto zilizo mbele ya G20 zinahitaji mshikamano na hatua za pamoja:Ban

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mataifa ya G20 yana fursa na wajibu wa kihistoria wa kutoa sukluhisho na kuongoza katika kukabili changamoto nyingi zinazoikabili dunia hivi sasa. Katika barua yake kwa G-20 iliyotolewa kwa vyombo vya habari Ban amesema karibu duniani kote matatizo ndio hali ya kila siku na kuoengeza pamoja [...]

26/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati watu kufikia bilioni 7, juhudi zahitajika za maendeleo kwa wote:UNFPA

Watu kufikia bilioni 7

  Katika siku tano zijazo idadi ya watu duniani inatazamiwa kufikia bilioni 7, na jinsi hatua zitakavyochukuliwa sasa itatanabaisha endapo kuna mstakhabali mzuri wa afya, endelevu na wa matuamaini ya baadaye au mustakhabali tuakaoghubikwa na kutokuwepo sawa, uharibifu wa mazingira na matatizo ya kiuchumi. Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya hali ya idadi ya [...]

26/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulanguzi wa dola trilioni 1.6 ulifanyika mwaka 2009:UM

money

Ripoti mpya ya shirika la kupambana na uhalifu na madawa ya kulevya la Umoja wa Mataifa UNODC inasema kuwa wahalifu walifanya ulanguzi wa takriban dola trilioni 1.6 mwaka 2009 asilimia kubwa ikitoka kwa biashara ya madawa ya kulevya. Ripoti hiyo inasema kuwa fedha hizo huwa zinatumiwa kwa kutoa hongo na kufadhili uhalifu ukiwemo ugaidi. Fedha [...]

25/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watoto duniani wakosa masomo ya shule ya upili:UM

25/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya ulinzi wa amani vinapaswa kubadilika kulingana na wakati- Hervé Ladsous

Herve Ladsous

Mkuu wa shughuli za operesheni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa amejadilia ulazima wa kuwepo kwa mwelekeo mpya na mabadiliko ya haraka hasa wakati wa utekelezaji wa majukumu ya ulinzi wa amani kutokana na hali ya kubadilika badilika kwa mazingira ya utendaji kazi. Amesema kutokana na mkangaiko mkubwa wa mambo unaoendelea kujitokeza, kuna [...]

25/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha uchunguzi wa kifo cha Qadhafi

Muammar al-Qadhafi

Kamisheni ya haki za binadamu imesema kuwa imepongeza na kukaribisha hatua inayotaka kuchukuliwa ya kuanzishwa kwa kamishna huru kwa ajili ya kuchunguza mazingira yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar al-Qadhafi. Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya haki za binadamu ilitilia shaka juu ya mauwaji ya kiongozi huyo hasa pale picha [...]

25/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nchi 21 zachaguliwa kwenye ECOSOC

kikao cha ECOSOC

Nchi 21 zimechaguliwa kujumuika kwenye baraza la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya uchumi na jamii ECOSOC, kwa shabaya ya kuweka msukumo zaidi kwenye chombo hicho. Kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, nchi wanachama zilipiga kura na kuzipitisha nchi 18 kuanza kutumika kwenye chombo hicho kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwakani. Na [...]

25/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tume ya UM yaweka malengo kwenye teknolojia ya kisasa

teknolojia ya kisasa

Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na maendeleo ya teknolojia ya kisasa imefanya mkutano wake wa nne ambapo iliweka malengo mapya na kutoa changamoto kwa dunia nzima. Tume hiyo ilikubaliana kwenye malengo manne ambayo nchi kote duniani zinahitaji kujitahidi kuyafikia ili kuhakikisha kuwa wananchi wao wamefahamu yanayojiri siku za usoni. George Njogopa na taarifa kamili

25/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali inazidi kuwa mbaya nchini Uturuki

tetemeko Uturuki

Hali inaripotiwa kuendelea kuwa mbaya nchini Uturuki baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi . Maelfu ya watu bado wanakisiwa kukwama nchini ya vifusi huku bado ikiwa haijatolewa idadi ya watu ambao bado hawajulikani walipo. Inakadiriwa kuwa majengo 2,256 yameharibiwa wakati wa janga hilo. Shughuli kuu kwa sasa ni kusambaza mablanketi, chakula na vifaa [...]

25/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mvua yasababisha madhara nchini El Salvador, Guatemala, Honduras na Nicaragua

mvua kubwa yasababisha mafuriko

Mataifa ya El Salvador, Guatemala, Honduras na Nicaragua yako kwenye hali ya tahadhari kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo tangu tarehe 12 mwezi huu ambapo zaidi ya watu milioni 1.2 wameathirika. Elisabeth Byrs kutoka ofisi la kuratibu masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa anasema kuwa ombi mpya la dola milioni 15.7 litatolewa [...]

25/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuchunguza kunyongwa kwa watu 53 nchini Libya

baraza la haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanyika uchunguzi kwenye ripoti inayoeleza kunyongwa kwa watu 53 kwenye mji wa Sirte nchini Libya. Shirika la Human Rights Watch linasema kuwa lilishuhudia maiti za wafuasi wa aliyekuwa rais wa Libya Muammar Gaddafi ambao mikono ilikuwa imegungwa na kuachwa kwenye hoteli moja mjini Sirte. Msemaji [...]

25/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana kutoa maoni kuhusu ugonjwa wa ukimwi

Michel Sidibe

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la UNAIDS linazindua mradi kwenye mtandao unaowalenga vijana na ugonjwa wa ukimwi. Mradi huo unatumiwa kuwawezesha idadi kubwa ya watu kuweka mikakati, kutatua matatizo au kutoa maoni mapya. Wakati ambapo vijana 3000 walio kati ya miaka 15-24 wakiambukizwa na ugonjwa wa ukimwi kila siku [...]

25/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa misaada kuathiri nchi zinazoendelea

Joseph Stiglitz

Mashirika ya kiuchumi kwenye Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa nchi zinazoendelea huenda zikakabiliwa na ukosefu wa misaada. Haya yalisemwa na kamati ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya uchumi ilipoandaa mkutano wa pamoja na baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC. Wajumbe kwenye mkutano huo walielezea uwezekano wa [...]

25/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanafunzi wengi hawapati masomo ya shule ya upili Afrika

watoto shuleni

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa kumekuwa na mahitaji makubwa ya elimu ya shule ya upili ikiongeza kuwa serikali nyingi hususan zilizo kusini mwa jangwa la sahara zina wakati mgumu huku wanafunzi wakiwa hawaendi shuleni. Kulingana na shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ni kuwa kuna asilimia [...]

25/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia huru bila nyuklia inawezekana Ban

Dunia ya nyuklia

Wakati dunia ikijiandaa kufikia idadi ya watu bilioni 7 wiki ijayo Katibu Mkuu leo amesisitiza haja ya kufikia ya jamii nzima ya dunia hii kuwa na mustakhbali wa kizazi huru bila silaha za nyuklia. Ban amesema wote tunafahamu kuwa dunia ya kesho inategemea sana maamuzi tunayofanya leo hivyo dunia bila silaha za nyuklia ni suala [...]

24/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni lazima kulinda haki ya kutetea haki za binadamu:UM

Baraza Kuu

Mwakilishi maalmu wa Umoja wa Mataifa Margaret Sekaggya leo amewasilisha kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ripoti yake ya nne na muongozo wa haki ya kutetea haki za binadamu. Ripoti hiyo ni muhimu na inalenga kuwasaidia ambao wanapigania haki kwa kuongeza uelewa wa azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1998 linalohusu watetezi wa [...]

24/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Myanmar yatakiwa kuachia huru wafungwa wa kisiasa

Thomas Quintana

Serikali ya Myanmar imeendelea kubinywa iwaachilie huru wafungwa wa kisiasa ikiambia kuwa hiyo ndiyo hatua muhimu itayofungua njia ya mpito kwenye kuelekea katika demokrasia ya kweli. Wito huo umetolewa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu nchini humo Tomás Ojea Quintana ambaye amesisitiza kuwa taifa hili linapaswa kuimarisha [...]

24/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban atoa heshima kwa jaji Antonio Cassese

Jurist

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa heshima zake kwa jaji Antonio Cassese ambaye ni mtaalamu maarufu wa sheria aliyeaga dunia ijumaa iliyopita akimtaja kama bingwa wa sheria ya kimataifa na rafiki wa Umoja wa Mataifa. Jaji Cassese ambaye amekuwa mwalimu wa sheria kwa miaka mingi sehemu mbali mbali za dunia aliaga dunia [...]

24/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Guatemala, Morocco, Pakistan na Togo zateuliwa wanachama kwenye Baraza la Usalama la UM

uchaguzi kwenye Baraza la Usalama

Guatemala, Morocco, Pakistan na Togo zitakuwa wanachama wasio wa kudumu miongoni mwa wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2011-2013 baada ya kushinda viti hivyo kwenye uchaguzi mwishoni mwa juma lililopita kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Wanachama wa Umoja wa Mataifa walipiga kura ya [...]

24/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Cambodia inastahili kuwa na mahakama huru:UM

askari wa Cambodia (CPAF)

Mtaalamu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa hata kama kumeshuhudiwa maendeleo ya miaka 20 nchini Cambodia tangu kumalizika kwa mapigano, mengi bado yanasalia kutekelezwa ikiwemo kubuniwa kwa mahakama huru. Cambodia imepiga hatua kwa muda wa miaka ishirini iliyopita ambapo amani na utulivu vimeleta usawa kwenye ugavi wa utajiri na kwenye maendeleo. Hayo ni kwa mjibu [...]

24/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban amlilia kiongozi wa Saudia

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametuma salamu zake za rambi rambi kufuatia kifo cha mwanamfalme wa Saudia Arabia Prince Sultan bin Abdul-Aziz Al aliyefariki dunia mwishoni mwa juma kwa maradhi ya saratani. Prince Sultan ambaye alikuwa mdogo wa mfalme wa Saudia Abdullah mpaka umati unamkuta alikuwa akitumika kama waziri wa ulinzi. Alifariki [...]

24/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awapongeza watunisia kwa kufanya uchaguzi kwa mpango na amani

sanduku la kupiga kura nchini Tunisia

Watunisia na serikali ya mpito ya nchi hiyo wamepongezwa kwa kuendesha uchaguzi wa kihitoria wa bunge Jumapili ya October 23. Katika taarifa yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema huu ni uchaguzi muhimu na hatua kubwa kuelekea demokrasia ya Tunisia, na ni maendeleo katika mabadiliko ya kidemokrasia Afrika ya Kaskazini na Mashariki [...]

24/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa UM wajadili njia bora za ufikishaji taarifa za kijographia kwa maendeleo

GGIM-logo

Wawakilishi kutoka nchi 90 na wajumbe kutoka mashirika mbalimbali na jumuiya za kiraia wanakutana katika mji mkuu wa Jamhuri ya Korea leo kwa ajili ya mikutano kadhaa ya Umoja wa mataifa. Mikutano hiyo inajikita katika kuboresha teknolojia ya udhibiti wa ukusanyaji, utunzaji, uendeshaji na ufikishaji taarifa za kijografia au geospatio na kuzitumia taarifa hizo kukabiliana [...]

24/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM kuendelea kusaidia Libya wakati viongozi wapya wakitangaza ukombozi

serikali ya mpito ya Libya

Umoja wa Mataifa umerejea kusisitiza nia yake ya kuwasaidia watu wa Libya kujenga mustakhbali mzuri wa taifa lao wakati viongozi wa baraza la mpito NTC walitangaza ukombozi kamili wa taifa hilo la Afrika ya Kaskazini ikiwa ni miezi minane tangu kuanza kwa vuguvugu na machafuko. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema tangazo la ukombozi [...]

24/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM uko tayari kusaidia waathirika wa tetemeko Uturuki

uharibifu wa tetemeko la ardhi Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amestushwa na kuhuzunishwa na athari za tetemeko la ardhi lililotokea Jumapili nchini Uturuki na kupoteza maisha ya watu, kujeruhi wengine na kuharibu miundombinu. Ban amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada kama utaambwa kufanya hivyo. Watu zaidi ya 200 wamearifiwa kufa na 1,300 kujeruhiwa wakati [...]

24/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania inajiandaa kwa kufanya sensa ya kitaifa:UNFPA

UNFPA

Idadi ya watu nchini Tanzania inakuwa kwa kiwango cha asilimia 2.9 ikiwa ni wastani wa watu milioni 1.3 kila mwaka kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA. Mwaka 2012 taifa hilo la Afrika ya Mashariki limepanga kuendesha sensa ya kitaifa ambayo inakadiriwa kugharimu dola milioni 76. Kama sehemu ya [...]

24/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM athamini maandalizi ya uchaguzi mkuu DR Congo

vifaaa vya uchaguzi vimewasili nchini Congo

Mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amezuru mashariki mwa nchi hiyo katika mji wa Bukavu jimbo la Kivu ya Kusini kutathimini maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao katika taifa hilo kubwa la Afrika. Katika ziara yake ya siku mbili Roger Meece ambaye ni mwakilishi maalumu na [...]

24/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya chakula inazidi kuwa mbaya DPRK:Amos

Valeria Amos akiwa katika nyumba ya watoto Korea Kusini

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura wa Umoja wa Mataifa Bi Valarie Amos amesema hali ya chakula inazidi kuwa mbaya katika jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK. Amesema licha ya mavuno kuwa mazuri bado watu wanajaribu kuishi kwa kula mchanganyiko wa vyakula ambavyo vina lishe duni. Bi amos amesema amezuru [...]

24/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwa UM miaka 66 iliyopita

kuadhimisha siku ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema dunia imepiga hatua kubwa tangu kuzaliwa kwa Umoja wa Mataifa miaka 66 iliyopita. Ban amesema siku chache kuanzia sasa dunia itamkaribisha mwanachama mpya ,mtoto atazaliwa na kuifanya idadi ya watu duniani kufikia bilioni 7. Ameongeza kuwa watakuwa watu bilioni saba wenye nguvu, kwani sasa watu wanaishi [...]

24/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tusiwasahau watu wa DPKR wanaokabiliwa na matatizo ya chakula:Amos

21/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tusiwasahau watu wa DPRK wanaokabiliwa na matatizo ya chakula:Amos

mama na mtoto nchini DPKR

Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK haiwezi kulisha watu wake katika siku zijazo, kwa mujibu wa mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Valarie Amos. Ameitaka dunia kuongeza misaada ya kibinadamu na sio kuwapa mgongo watu hao ambao takribani milioni sita sasa wanategemea msaada wa chakula. Bi [...]

21/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haja ya kushughulikia matatizo ya mmomonyoko wa udongo yasisitizwa kwenye mkutano wa kimataifa

mmomonyoko wa udongo mjini Changwon, Korea

Kipindi cha miaka 25 ijayo mmomonyoko wa udongo utapunguza uzalishaji wa chakula kwa takribani asilimia 12 huku idadi ya watu ikiendelea kuongezeka. Onyo hili limetolewa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kukabiliana na hali ya jangwa yaani COP 10 uliohitimishwa leo Ijumaa mjini Changwon, Korea ya Kusini Korea. Mwandishi wa radio ya [...]

21/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vita dhidi ya malaria bado ni changamoto kubwa Tanzania

Mbu anaeeneza malaria

Lengo namba sita la maendeleo ya milenia ni kupambana na maradhi ya ukimwi, kifua kikuu na malaria. Umoja wa Mataifa uliweka malengo 8 ya maendeleo ya milenia mwaka 2000 na yanapaswa kutimizwa ifikapo 2015. Nchi nyingi zimepiga hatua lakini kwa Tanzania suala la malaria bado ni changamoto japo wanajitahidi. Mwandishi wetu wa Tanzania George Njogopa [...]

21/10/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania italikubali baraza la mpito Libya pale tuu litakapounda serikali

Bendera ya Tanzania

Serikali ya Tanzania leo imesema haitolitambua baraza la mpito la Libya hadi pale litakapounda serikali mpya. Tanzania imechukua msimamo huo pamoja na mataifa mengi ya Afrika baada ya kukubaliana kwa pamoja kwenye muungano wa Afrika yaani AU. Baraza la mpito la Libya liliundwa baada ya kuzuka vuguvugu la kutaka kumng’oa madarakani Kanali Muammar Gaddafi aliyekuwa [...]

21/10/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Botswana kuwa mwenyeji wa mkutano kuhusu uhamiaji

ramani ya Botswana

Mkutano wa kujadili masuala ya uhamiaji unatarajiwa kuandaliwa kwenye mji mkuu wa Botswana Gaborone, mkutano unaotarajiwa kuyaleta pamoja mashirika kadha kutoka kote duniani. Mkutano huo wa siku mbili unaong'oa nanga tarehe 25 mwezi huu ni wa watu wa aina yake kuandaliwa ukiwa na lengo la kuboresha uhamiaji baina ya nchi na masuala mengine ya kuboresha [...]

21/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yapeleka misaada kwa shirika la majanga ya dharura nchini Thailand

Mafuriko Thailand

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM hii leo linatarajiwa kuwapelea msaada waathiriwa wa mafuriko nchini Thailand, msaada wa gharama ya dola laki tano unaofadhiliwa na shirika la kimataifa la maendeleo la Marekani USAID. Msaada huo unajumuisha mashua mbili, mashine 10 za kuondoa maji na jenereta 10. IOM inafanya jitihada za kupata mashua zaidi ili kuisadia [...]

21/10/2011 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Jitihada za kuokoa maisha zaendelea Dadaab

Wakimbizi Dadaab

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pamoja na washirika wake wanaendelea kuwahudumia maelfu ya wakimbizi kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya. Kunashuhudiwa idadi ndogo ya wakimbizi wanaoingia kwenye kambi hiyo kutoka Somalia suala ambalo huenda limechangiwa na oparesheni za kijeshi zinazoendelea au mvua kubwa inayonyesha. Zaidi ya wahudumu 30 wa UNHCR bado [...]

21/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya Kenya vyapambana na Al shabaab nchini Somalia

Balozi Augustine Mahiga

Vikosi vya Kenya kwa sasa viko nchini Somalia kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab ambao mara kwa mara wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia nchini Kenya ambapo wanatekeleza vitendo vikiwemo vya utekaji nyara na mauaji. Akithibitisha hayo mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema kuwa idadi kubwa ya [...]

21/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasomalia zaidi wakimbilia Yemen:UNHCR

wasomali wakimbilia Yemen

Hali ikizidi kuwa mbaya nchini Somalia watu zaidi wanaendelea kuihama nchi hiyo, ikikadiriwa kuwa zaidi ya wasomali 318,000 wamehama nchi hiyo mwaka huu. Huku idadi kubwa ikiwa inaingia nchini Kenya na Ethiopia kutafuta hifadhi wengine wengi wanafanya safari zilizo hatari baharini kupitia kwa ghuba ya Aden. Tangu mwezi Junauari wakimbizi 20,000 wameingia nchini Yemen wakisema [...]

21/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatulitambui baraza la mpito la Libya mpaka itakapoundwa serikali:Tanzania

ramani ya libya

  Serikali ya Tanzania leo imesema kuwa bado inaendelea kutia ngumu ya kutolitambua baraza la mpito la Libya ambalo hapo jana liliutangazia ulimwengu juu ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Kanali Muamar Gaddafi. Akitoa msimamo wa serikali ya Tanzania kuhusiana na hali ya Libya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa [...]

21/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kifo cha Gaddafi kitaleta utulivu Libya:Pillay

Navi Pillay

Mkuu wa haki zabinadamu kwenye Umoja wa mataifa Navi Pillay amesema kuwa kifo cha Muammar Gaddafi na kutekwa kwa miji ya Sirte na Bani Walid ndio mwisho wa ghasia ambazo zimedumu kwa muda wa miezi minane na mateso kwa watu wa Libya. Pillay amesema kuwa awamu nyingine mpya imeanza ambao itayajali maslahi ya wananchi, kuleta [...]

21/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naibu kamishna wa haki za binadamu akamilisha zile yake

Kyung-wha Kang

Naibu Mkuu wa kamishna ya haki za binadamu Kyung-wha Kang,amehitimisha ziara yake ya kwanza iliyomchukua kuanzia nchini Paraguay na Uruguay na Chile. Katika ziara yake hiyo ya siku tatu, kiongozi huyo ameweka zingatio la udumishaji misingi ya haki za binadamu na kusisitiza haja ya kukaribisha mashirikiano kwa pande zote. Amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi [...]

21/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu lamteua mtaalamu wake wa masuala ya haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu leo limeendelea na majadiliano yake yaliyosimamishwa hapo nyuma na kumchagua Mutama Ruteere kuwa mtaalamu wake mpya atayeshughulikia masuala yanayohusu ubaguzi wa rangi. Bwana Ruteere raia kutoka Kenya ana uzoefu mkubwa katika maeneo yanayohusu haki za binadamu na amepata kufanya kazi katika taasisi mbalimbali. Anashahada ya uzamifu katika eneo la sayansi [...]

21/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wathibitisha vikosi vya Kenya kuingia Somalia

Balozi Augustine Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augstine Mahiga leo amethibitisha kwamba vikosi vya jeshi la Kenya vimeingia Somalia. Balozi Mahiga amesema amezungumza na maafisa wa Kenya na Somalia kuhusu hatua hiyo ambayo Kenya inasema imechukua kwa ajili ya usalama na  kukabili uhalifu unaoendeshwa na kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al-shabaab.  Wanamgambo wa [...]

21/10/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Utoaji makazi ya muda huko Saloum Misri kukoma

nemba ya UNHCR

Kuanzia jumapili makundi ya watu wanaowasili katika kambi moja iliyoko mpakani mwa nchi ya Misri, wakitokea nchini Libya sasa hawatapatiwa hadhi ya makazi kwenye eneo hilo. Hata hivyo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa wale waliowasili kwenye kambi hiyo Saloum kabla ya jumapili bado wataendelea kupata uangalizi. Hatua hiyo inakuja [...]

21/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Walibya lazima waje pamoja kwa maridhiano baada ya kifo cha Gaddafi:Ban

21/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Ukame unaendelea Ethiopia

21/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada Somalia

Waziri Membe na Asha Rose-Migiro

Serikali ya Tanzania imeitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi na kunyoosha mkono zaidi kusaidia kunusuru maisha ya mamilioni ya watu nchini Somalia. Somalia ambayo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili sasa inakabiliwa pia na tatizo kubwa la njaa, utapia mlo kwa watoto na kame. Waziri wa mambo ya nje [...]

20/10/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Matarajio ya ajira kwa vijana ni duni:UM

20/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kirai yataka ukomeshwaji uporaji wa ardhi

ramani ya mji wa Changwon Korea Kusini

Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa unaojadilia hali ya ukame, yametaka ukomeshwaji mienendo wa upokaji ardhi unaendelea kufanywa katika mataifa kadhaa. Mashirika hayo ambayo yanakutana katika mji wa Changwon, Korea Kusini yamesema kuwa pamoja vitendo vya uchukuaji ardhi vinavyopaliliwa na baadhi ya tawala za kidola na makundi ya kibiashara havipaswi kuendelea [...]

20/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Adha kwa watoto wa kipalestina kutokana na kukaliwa imalizwe

watoto wa Kipalestina

Mwakilishi maalmu wa Umoja wa Mataifa kwa hali ya haki za binadamu kwenye himaya ya Palestina Richard Falk ameitaka serikali ya Israel kufuata muongozo wa kuwalinda watoto wa Palestina wanaoishi katika maeneo yanayokaliwa ambao hukamatwa na kushikiliwa. Ameitaka serikali hiyo kuzingatia sheria na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu. Akizungumza Alhamisi kwenye Baraza Kuu [...]

20/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Familia 24,000 zinaendeshwa na watoto Msumbiji:UNICEF

watoto wanaoendesha familia zao

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema familia zipatazo 24,000 nchini Msumbiji ni za watoto pekeyao. Kwa mujibu wa shirika hilo watoto wengi kati ya hao ambao wamepoteza wazazi wote kutokana na ukimwi huachwa bila msaada wowote . Lakini sasa kuna shinikizo kubwa kutoka UNICEF na jamii kwa ujumla ya kutaka familia [...]

20/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

OCHA yataka misaada zaidi kwa wakimbizi nchini Ivory Coast

wakimbizi nchini Ivory coast

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa fedha zaidi zinahitajika ili kugharamia misaada kwa maelfu yawakimbizi nchini Ivoyr Coast. OCHA sasa inatoa wito wa kutolewa kwa misaada ya kuwasaidia wakimbizi kurudi makwao na kuanza upya maisha yao. Kulingana na OCHA hadi sasa kuna zaidi ya wakimbizi wa ndani 194,000 [...]

20/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban na Bi Karman wajadili haki za binadamu nchini Yemen

Katibu Mkuu Ban Ki-moon pamoja Tawakkul Karman, mshindi wa tuzo ya Nobel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amefanya mkutano na mwandishi wa habari na mwanaharakati ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu raia wa Yemen Tawakkul Karman na kujadili masuala ya haki za binadamu na kudorora kwa masauala ya kibinadamu na uchumi nchini mwake. Wakati wa mkutano huo uliofanyika [...]

20/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ICC yaitaka Malawi kueleza sababu ya kutomkamata rais Bashir

Jumba la ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya Hague imeitaka Malawi kueleza sababu zilizoifanya kutomkamata rais wa Sudan Omar Hassan al- Bashir ambaye anatafutwa na mahakama hiyo kutokana na mashataka ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki baada ya ripoti kuwa alifanya ziara nchini Malawi. Haya yanajiri baada ya ripoti za vyombo vya habari [...]

20/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kanali Muammar Gaddafi ameuawa

Kanali Muamar Gadaffi

Baraza la mpito la Libya NTC limesema aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi ameuawa leo mjini Sirte. Taarifa za kifo hicho zimetolewa baada ya majeshi ya Baraza la Mpito kutangaza yanaudhibiti mji wa Sirte, mji alikozaliwa kiongozi huyo. Kwa mujibu wa afisa wa Baraza la Mpito Abdel Majid kiongozi huyo alikamatwa na kujeruhiwa [...]

20/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Myanmar bado inaendelea kukandamiza haki za binadamu-UM

Tomas Ojea Quintana

Myanmar ikiwa imepiga hatua kubwa pamoja na kupunguza mbinyo kwa vyombo vya habari na kupewa nafasi kwa vyama vya siasa, hata hivyo kwa kiasi kikubwa Myanmar inaendelea kuziendea kinyume haki za binadamu. Hayo ni kwa mujibu wa mtaalamu mmoja wa Umoja wa Mataifa ambaye amelitaka taifa hilo kufanya haraka ili kuwaachia huru wafungwa kadhaa wa [...]

20/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban aelezea kusikitishwa kwake kufuatia kuuwa kwa askari wa Uturuki na vikosi vya Kurdistan

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea shaka  juu ya taarifa za kuwepo machafuko yaliyoshuhudia askari 26 wa Uturuki wakipoteza maisha baada ya kuvamiwa na vikosi vya Kikurd katika eneo la KusinI mashariki mwa nchi hiyo. Ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa mashambulizi hayo yalifanyika katika jimbo la Hakkari na askari wa [...]

20/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwanakandanda maarufu wa Brazili aelimisha vijana kuhusu Ukimwi

Ronaldo de Assis Moreira

Ronaldo de Assis Moreira mwanasoka maarufu kutoka nchini Brazili ambaye pia anajulikana kama Ronaldinho amekubali mwaliko kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na wizara ya afya ya Brazil kuchagiza vita dhidi ya ukimwi kwa kutumia michezo. Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe amesema Ronaldinho anamvuto mkubwa miongoni mwa vijana duniani [...]

20/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msafara wa wahamiaji wa Afrika kutoka Libya umewasili Chad:IOM

wahamiaji wa Libya

Zaidi ya wahamiaji 1220 kutoka nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara waliohamishwa kutoka mjini Sebha Kusini mwa Libya wiki mbili zilizopita sasa wamewasili Chad baada ya safari ndefu. Wahamiaji hao walisafirishwa kwa msafara wa malori 15 kutoka kwenye kituo cha shirika la kimataifa la uhamiaji IOM mjini Sebha kwa msaada wa shirika hilo. [...]

20/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuimarisha jamii zinazoishi katika maeneo makavu

jamii inayoishi katika maeneo makavu

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP inasema kuongeza uwekezaji katika maeneo makavu, kuimarisha uhusiano baina ya sayansi na sera na maisha mchanganyiko kwa jamii ili kupunguza shinikizo kwa mali asili ni miongoni mwa suluhu ya kutambua umuhimu wa maeneo makavu. Ripoti hiyo ya UNEP iitwayo ‘Global Drylands: A UN System-wide response’ [...]

20/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia Somali

waziri wa mambo ya inje Tanzania, Bernard Membe

Serikali ya Tanzania leo imeitolea wito jumuiya ya kimataifa kutolipa kisogo eneo la Pembe ya Afrika ambalo wakati huu inaandamwa na hali ngumu ya ukosefu wa chakula na kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi kutorokea katika nchi za jirani. Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Bwana Bernad Memba ambaye amesema jumuiya za kimataifa [...]

20/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo yanayoikabili pembe ya Afrika bado ni makubwa:UNICEF

mtoto apata matibabu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema msaada wa kimataifa kuokoa maisha ya watoto kwenye Pembe ya Afrika unaonyesha matumaini lakini bado juhudi zaidi zinahitajika ili kuokoa maisha ya maelfu ya watoto walioko kwenye hatari ya kufa na utapiamlo na magonjwa mengine. UNICEF imeyasema hayo katika ripoti yake inayoelezea hatua zilizopigwa miezi [...]

20/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu la UM ahofia waathirika wa mafuriko Thailand, Cambodia na nchi zingine za Kusini Mashariki mwa Asia:

mafuriko kusini mashariki mwa Asia

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser, ameelezea hofu, huruma na huzuni yake kufuatia kupotea kwa maisha ya mamia ya watu nchini Thailand, Cambodia na nchi za jirani za Kusini Mashariki mwa Asia kutokana na mafuriko. Hivi sasa inakadiriwa kwamba mafuriko hayo yameshakatili maisha ya mamia na kuwacha mamilioni wakikosa makazi [...]

19/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uchumi wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kukua kwa asilimia 6:IMF

uchumi wa Afrika  Kusini mwa Sahara

Uchumi wa nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara unatarajiwa kukua kwa asilimia 6 mwaka 2012 kwa mujibu wa shirika la fedha duniani IMF. Shirika hilo linasema ukuaji wa uchumi katika eneo hilo umesalia kuwa imara wakati nchi nyingi za kipato cha chini zilisongwa na matatizo ya kudorora kwa uchumi. Katika makadirio ya [...]

19/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Timor-Leste pamoja na UM waanza kuteketeza masalia ya silaha

Timor-East

Serikali ya Timor-Leste kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa zimeanzisha mkakati wenye shabaya ya kutegegua silaha zilizoendelea kusalia kwenye eneo la Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambazo zilikuwa bado kulipuka. Pande zote mbili zinaendesha shabaya ya pamoja kuhakikisha kwamba silaha hizon zinaondoshwa kabisa kabla ya kuletan madhara mengine kwenye siku za usoni. Maafisa wa polisi [...]

19/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wa kimaendeleo ni muhimu sana wakati huu misaada inasuasua:ECOSOC

Lazarous Kapambwe rais wa  ECOSOC

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa maendeleo na kuifanya misaada kutumika ipasavyo hasa katika wakati huu ambapo serikali nyingi duniani zinakaza mikanda na kupunguza bajeti za misaada. Akizngumza Luxembourg katika kufunga kongamano la kimataifa linalozungumzia kuongeza athari nzuri za maendeleo ktokana na misaada , Rais wa baraza la kiuchumi na masuala [...]

19/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shirika lisilo la kiserikali lawasaidia waafrika wanaoomba hifadhi marekani

Joseph Chuman

Shirika lisilo la kiserikali lililoko Kaskazini mwa jimbo la New Jersey hapa Marekani liitwalo Begen County Sanctuary kamati kwa ajili ya waoomba hifadhi wa kisiasa linawasaidia waomba hifadhi kutoka Afrika ili kupewa hadhi za kisheria za kuishi nchini Marekani. Waomba hifadhi hao wanakuja Marekani kutokana na mazingira na sababu tofauti, lakini karibu wote wamekuwa waathirika [...]

19/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Asia-Pacific na jumuiya za kijamii wakutana katika maandalizi ya RIO+20

RIO+20

Zaidi ya wajumbe wa serikali na jumuiya za kijamii 250 kutoka mataifa zaidi ya 40 ya Asia-Pacific wamekutana leo mjini Seoul Korea ili kuafikiana msimamo na taarifa ya kikanda itakayowasilishwa kwenye mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu maendeleo endelevu (UNCSD) ambao pia hujulikana kama Rio + 20 unaotarajiwa kufanyika kwakani. Mkutano huo unaandaa tamko la [...]

19/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mfuko wa kimataifa umeokoa maisha ya watu 830,000 kutoka kwa malaria

vyandarua vya umbu

Mfuko wa kimataifa yaani Global Fund unasaidia kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria unasema tangu mwaka 2002 umewekeza dola bilioni 4.1 kupambana na malaria. Global Fund inasema fedha hizo zimetumika kusaidia kuokoa maisha ya watu 830,000 kufikia mwishoni mwa mwaka 2010 kwa kuongeza matumizi ya dawa za kuua mbu kwenye vyandarua na kufanya kazi [...]

19/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo yanayosababisha kutokuwepo usawa katika afya:WHO

nemba ya WHO

Wawakilishi kutoka nchi na serikali 100 duniani, wataalamu wa afya, jumuiya za kijamii na wadau wengine wanakutana mjini Rio de Janeiro Brazil kwa siku tatu kujadili jinsi gani hali za kijamii, kiuchumi na kimazingira zinaweza kuboreshwa ili kupunguza mapengo ya kiafya ndani ya nchi na baina ya mataifa. Mkutano huo wa kimataifa wa ulioandaliwa na [...]

19/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uharamia umepita mipaka na nia za kiuchumi:Ban

uharamia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema uharamia umevuka mipaka ya kitaifa na haja za kiuchumi. Akizungumza kwenye Baraza la Usalama ambalo leo limekutana kujadili uharamia katika ghuba ya Guinea, amesema uharamia huo una athari mbaya kwa biashara ya Afrika ya Magharibi na dunia nzima kwa ujumla hususani kwa washirika wakubwa wanaofanya biashara [...]

19/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yaonya juu ya matatizo ya ajira kwa vijana

vijana wasio na ajira

Shirika la kazi duniani ILO limeonya juu ya kuwa na kizazi cha vijana kilichoghubikwa na tatizo kubwa la ajira, ongezeko la kukosa shughuli za kufanya, kupata kazi zisizo za maana katika nchi zilizoendela na kazi za kimasikini au kutokuwa na kazi kabisa katika nchi zinazoendelea. Katika takwimu za ripoti ya shirika hilo zilizotolewa leo ziitwazo [...]

19/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yajitolea kuinua wanawake wa vijijini

Michelle Bachelet

Wakuu wawili wa mashirika ya Umoja wa Mataifa akiwemo Michelle Bachelet mkurugenzi wa idara ya Umoja wa mataifa inayohusika na usawa wa kijinsia(UN WOMEN) na Kanayo Nwanze aliye rais wa mfuko wa kilimo wa kimataifa IFAD wamekubalina kushirikiana katika kuwanua wanawake wa vijijini kwa kuwekeza kwenye kilimo, uchumi na kwenye masuala ya usalama. Wakiwa mjini [...]

19/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kifungo cha upweke kinastahili kupigwa marufuku:Mendez

Juan Mendez

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na masuala ya mateso ametoa wito kwa mataifa kupiga marufuku kifungo cha upweke kwa wafungwa. Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Juan Mendez amesema kuwa kifungo cha upweke kinahitaji kupigwa marufuku kama njia ya kutesa akisema kuwa hayo ni mateso makali. Mendez amesema kuwa utafiti wa kisayansi unaonyesha [...]

19/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ana imani kuwa kubadilishana kwa wafungwa kati ya Israel na Palestine kutaleta amani

18/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UM wamtunuku Maya Angelou

Maya Angelou

Mshairi na mwandishi wa Kimarekani Maya Angelou ametunukiwa heshima na Umoja wa Mataifa kama mmoja wa wazee wa busara wa jamii ya wanazuoni mahiri na watetezi wa haki za binadamu na za jamii. Mwaka 2011 umetangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa ni mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Afrika kwa [...]

18/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mfuko mpya wa UM watoa dola 300,000 kusaidia waathirika wa usafirishaji haramu wa watu

usafirishaji haramu wa watu

Mashirika kutoka nchi 12 yanayosaidia waathirika wa usafirishaji haramu wa watu ili waweze kupata haki, kurejea nyumbani na kurejea katika maisha ya kawaida kwa pamoja yamepewa dola 300,000 leo msaada kutoka mfuko mpya wa Umoja wa Mataifa. Mtazamo huo umechukuliwa na Umoja wa Mataifa ili kutoa msaada wa fedha unaohitajika kwa waathirika wa uhalifu wa [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanamazingira vijana kwenye maonyesho nchini Ujerumani

vijana kwenye maonyesho nchini Ujerumani

Viongozi vijana wanaohusika na masuala ya kimazingira kutoka mataifa 18 yanayokua wanakusanyika nchini Ujerumani ili kuonyesha uvumbuzi wao kuhusu maendeleo. Kuanzia kubuni jiko lisilotumia makaa nchini Kenya pamoja na miradi ya watalii nchini Chile wavumbuzi hawa wanahusika na masuala ya mazingira kwenye nchi zao. Vijana hao 47 walichaguliwa kutoka kwa wengine 800 waliotuma maombi ili [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

EMPRETEC katika kuboresha biashara na kubuni ajira

Empretec

Mkutano wa 18 wa wakurugenzi wa EMPRETEC ambao ni mpango wa kibiashara kwenye nchi zinazoendelea utafanyika mjini Pretoria nchini Afrika Kusini kuanzia tarehe 18 hadi 21 mwaka 2011 mkutano ambao utawaleta pamoja wafanyibiashara kutoka Afrika. Mkutano huu utatoa fursa ya kujadili masuala ya kubuniwa nafasi za ajira kupitia biashara na pia kuimarisha ushirikiano kati ya [...]

18/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Huduma bora za hali ya hewa zitakabiliana na ukame:WMO

hali ya hewa

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO limesema kuwa maendeleo ya kisayansi yameweka msingi bora wa sera za kukabiliana na kiangazi na kuenea kwa majangwa. Usalama wa chakula na maji ni kati ya sehemu zitakazoshughulikiwa kwenye mpango wa hali ya hewa wa WMO na washirika wake. Mpango huo una lengo la kuhakikisha kuwepo [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali zatakiwa kutambua uhamiaji kama suala la kubaini hali ya kiafya

nemba ya IOM

Huku wajumbe kutoka mataifa mbali mbali wakikusanyika mjini Rio de Janeiro kwenye mkutano wa kwanza kabisa kuhusu masuala ya kijamii kwenye afya, shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezitaka serikali kutambua suala la uhamiaji kama suala linalobainisha afya ya wahamiaji. Mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing amesema kuwa inahitaji kukubalika kuwa wakati wahamiaji wanapochangia [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji nchini Yemen

Waandamanaji Yemen

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani mauaji ya waandamanaji wenye amani kwenye miji ya sanaa na Taiz nchini Yemen. Ghasia zilizuka mwishoni mwa juma na ofisi hiyo ya haki za binadamu inasema kuwa mauaji hayo yalitokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi kutoka kwa vikosi vya usalama. Hata hivyo ghasia zinaendelea [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifo vinavyosababishwa na Malaria vyapungua kwa asilimia 20

mtoto atibiwa kutokana na ugonjwa wa malaria

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria vimeshuka kwa asilimia 20 kote duniani kwa muda wa miaka kumi iliyopita. Pia wataalamu wanasema kuwa ikiwa hatua zitachukuliwa maisha ya watu milioni 3 zaidi yataokolewa. Malaria ndio moja ya magonjwa hatari zaidi hasa barani Afrika. Kulingana na WHO watu 781,000 waliaga [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waomba hifadhi kwenda nchi zilizostawi waongezeka

mtoto

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa nchi zilizostawi zimeshuhudia kuongezeka kwa asilimia 17 watu wanaoomba hifadhi wakati wa nusu ya kwanza ya mwaka ambapo idadi kubwa ya maombi ya hifadhi inapotoka kwenye nchi zilizo na mizozo ya muda mrefu. Kulingana na ripoti ya UNHCR maombi 198,300 yalitumwa kati ya mwezi [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ahadi za kimaendeleo ni lazima zitimizwe:Migiro

Naibu katibu mkuu wa UM Asha Rose Migiro

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro ameyataka mataifa kuacha kutegemea misaada. Akiongea kwenye mkutano kuhusu ushirikiano katika maendeleo mjini Luxembourg Bi Migiro amesema kuwa ahadi za kimaendeleo zilizowekwa ni lazima zilindwe na kutimizwa. Pia amesema kuwa ni lazima kuwe na ushirikiano katika kuhakikisha kuwa misaada inachangia katika maendeleo. Mkutano huo pia unaangazia [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aelezea mafanikio yaliyopo katika ubadilishanaji wa wafungwa kwenye eneo la mashariki ya kati

Ban atoa taarifa juu ya kubadilishana kwa mfungwa kati ya Iarael na Palestina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anaamini kuwa kubadilishana wafungwa kati ya Israeal na Palestina kutaleta matokeo mema kwenye mpango wa amani wa mashariki ya kati uliokwama. Ban amesema kuwa amefurahishwa na shughuli ya kubadilishana wafungwa baada ya miaka mingi ya majadiliano. UM umekuwa ukitoa wito wa kuachiliwa kwa Gilad Shalit na [...]

18/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amtaka rais wa Syria kuchukua maamuzi dhabiti

Yakin Ertürk, Paulo Pinheiro,  Karen Abu Zayd

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtaka rais wa Syria kuchukua hatua madhubuti kusitisha vitendo vya ukandamizaji waandamanaji na wakati huo huo akubali kuwaruhusu wataalamu wa haki za binadamu wanaotaka kwenda kufanya uchuguzi wa uvunjivu wa haki za binadamu nchini humo. Ban amemtaka rais Bashar-Al Assad kuanza kutekeleza mabadiliko ya kisiasa kabla wakati [...]

18/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mshikamano wa Olimpiki kufufuliwa

Baraza Kuu

Jukumu la michezo katika kuleta mshikamano miongoni mwa watu kutoka mataifa mbalimbali na imani tofati za kidini limejadiliwa leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Sebastian Coe, ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki, mapema mwaka huu alipigia upatu kuanzishwa kwa azimio la amani kwenye michezo hiyo. Azimio hilo la [...]

18/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka uchaguzi huru na haki DRC

Baraza la Usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kuwepo kwa uchaguzi wa uhuru na waki katika wakati ambapo wananchi wa Jamhuri ya Congo wakijiaanda katika uchaguzi mkuu ujao. Baraza hilo limeweka zingatio lake likizitaka mamlaka nchini humo kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kufanikisha uchaguzi huo. Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mwakilishi maalumu wa [...]

18/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kutokomeza umaskini duniani:UM

17/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Kubadilishana wafungwa baina ya Israel-Hamas ni hatua nzuri:Ban

Ban Ki-moon akiwa Switzerland

Tangazo la hivi karibuni la Israel na kundi la Palestina la Hamas la kubadilishana wafungwa ni hatua ya kukaribishwa ambayo itachagiza zaidi juhudi zinazoendelea za kutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Israel na Hamas walitangaza wiki iliyopita kwamba wameafikiana kuwa Hamas itamwachilia askari wa Israel Gilad [...]

17/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usalama wa chakula duniani:UM

shirika la UM la chakula na kilimo FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la mpango wa chakula duniani WFP wameungana kuadhimisha siku ya chakula duniani. Siku hii huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuchagiza dunia kukabiliana na matatizo ya chakula, kauli mbiu mwaka huu ni "usalama wa chakula [...]

17/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa OCHA aelezea hofu ya mafuriko kusini mashariki mwa Asia

Valerie Amos

Mkuu wa masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura wa Umoja wa Mataifa ameelezea hofu yake kuhusu kuongezeka kwa athari za mafuriko kwa mamilioni ya watu Kusini Mashariki mwa Asia. Bi Valarie Amos ambaye yuko ziarani katika eneo hilo amesema hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi wakati vina vya maji vya mito vikiongezeka na mvua bado [...]

17/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa ndani wa kigeni hawatathminiwi Lebanon:UM

Gulnara Shahinian

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa anayefuatilia mifumo ya kisasa ya utumwa Gulnara Shahinian leo ameitaka serikali ya Lebanon kuweka sheria ya kuwalinda wafanyakazi wa nyumbani takribani 200,000 nchini humo. Shahinian ameonya kwamba bila ulinzi wa kisheria wafanyakazi hao wataendelea kuishi katika hali mbaya ya kunyanyaswa, kuwa tegemezo kwa waajiri wao kwa kunyonywa kiuchumi, kuathirika [...]

17/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano zaidi watakiwa kukabili hali ya jangwa:UM

jangwa

Hali ya jangwa inaathiri takribani watu bilioni moja kote duniani kila mwaka na asilimia moja ya ardhi yenye rutuba hupotea. Kutokana na hali hiyo Umoja wa Mataifa kupitia mkataba wake wa kupambana na jangwa COP unaendesha mkutano kwa wiki mbili nchini Korea Kusini. Mkutano huo ulioanza leo unajadili jinsi ya kupambana na hali ya jangwa [...]

17/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake katika ulimwengu wa Kiarabu lazima wawezeshwe:Bachelet

Michelle Bachelet

Kitengo maalumu cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake UN-Women kupitia mfuko wa usawa wa kijinsia leo kimetangaza mapendekezo mapya ya kuzishirikisha mashirika ya serikali na mashirika yanayosaidia wanawake kuomba fedha kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kisiasa na kiuchumi. Mfuko huo ulianzishwa na serikali ya Hispania kwa lengo la kuchagiza haki za wanawake na [...]

17/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe mpya wa UM nchini Iraq akaribishwa nchini humo

Martin Kobler akiwa na Ban Ki-moon

Mwakilishi maalum mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler amepokewa na waziri mkuu wa nchi hiyo Nuri Ak- Maliki akisema kuwa atashirikiana na utawala nchini Iraq kuisadia nchi hiyo kupiga hatua. Bwana Kobler aliye pia mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq (UNAMI) alimshukuru bwana Al- Maliki kwa [...]

17/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ajionea kupungua kwa theluji nchini Uswisi

kupungua kwa theluji

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alijionea mwenyewe akitumia ndege aina ya helkopta kupungua kwa theluji kwenye mji wa Bern nchini uswisi na baadaye kujadiliana na rais Micheline Calmy- Rey kuhusu maendeleo na mkutano wa UM kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa utakaoandaliwa nchini Afrika Kusini. Akiwa nchini Uswisi ambapo alihudhuria kikao cha [...]

17/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mpango wa Isreal kuanzisha ujenzi wa makazi Jerusalem

makazi ya Israel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonyesha wasiwasi wake kufuatia tangazo la serikali ya Israel la kutaka kuweka makazi mapya ya majengo katika eneo inalokalia kwa nguvu la Jerusalame Mashariki akisema kuwa kitendo hicho ni sawa na kukaribisha machafuko. Ban amesema kuwa juhudi zozote za kutaka kuendeleza makazi hayo ni hatua isiyokubalika hasa [...]

17/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa ta kutokomeza Umaskini

mtu maskini

Zaidi ya watu bilioni moja duniani ni masikini na wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku, hali ambayo imetiwa mkazo leo katika siku ya kimataifa ya kutokomeza umasikini. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "kutoka katika umasikini kuelekea maisha bora:watu ndio kitovu cha maendeleo kwa wote".  Akitoa ujumbe maalumu kuhusu siku hii Katibu Mkuu [...]

17/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Changamoto kubwa hii leo ni upungufu wa imani:Ban

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema serikali zote duniani zinakabiliwa na shinikizo kubwa la kukabiliana na matatizo ya bajeti kutokana na kuyumba kwa uchumi, lakini amesisitiza changamoto kubwa zaidi sio upungufu wa rasilimali bali ni upungufu wa imani. Ban ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa muungano wa wabunge IPU mjini Berne Switzeland. [...]

17/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuadhimisha siku ya kuona duniani

17/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa ya chakula yaadhimishwa

14/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kupambana na upofu nchini Kenya

daktari atibu mgonjwa wa macho nchini Kenya

  Makala yetu ya wiki hii inaangazia siku ya kuona duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba. Shirika la afya duniani WHO limesema katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuona kwamba mkazo wa kimataifa unapaswa kuelekezwa katika kupunguza upofu, matatizo ya kutoona mbali au karibu na kuwasaidia wasioona. Maadhimisho ya mwaka [...]

14/10/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika yaomba misaada kusaidia Pakistan kupambana na mafuriko

waathiriwa wa mafurikoPakistan

Wafadhili wanaombwa kutoa msaada kuwalisha wapakistani milioni 2.5 walioathiriwa na mafuriko kwenye jimbo la Sindh kusini mwa Pakistan. Shirika la chakula duniani WFP limesema tayari limeshatoa lishe kwa watu zaidi ya milioni moja katika wilaya nane Sindh. WFP inasema dola milioni 27 zilizopokelewa hadi sasa zitawasaidia kuwalisha walioathiriwa mpaka mwisho wa mwezi wa Novemba. Zaidi [...]

14/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatua kubwa kulinda idadi ya watu nchini somalia hasa mikoa ya kati na kusini

mbu anayeambukiza malaria

Inakadiriwa kuwa watu millioni 2.5 nchini Somalia, wameathirika na ukame, njaa, na vita. Watu hawa sasa wapo katika athari ya kuambukizwa na ugonjwa wa malaria endapo msimu wa mvua utakapoanza. Kuzuia vifo vya watu kutokana na ugonjwa huu, hususani watoto wadogo walio na utapiamlo na watu walioathiriwa na vita, hatua thabiti zimeanza kuchukuliwa. Shirika la [...]

14/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ataka nchi zinazoendelea kuongeza kasi juu ya mipango ya afya kwa wanawake na watoto

Ban Kimoon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka nchi zinazoendelea kutopoteza mwelekeo wa kushughulikia vipaumbele vya afya za wanawake na watoto akionya kuwa kuna kazi kubwa inayopaswa kufanywa mbeleni.  Akizungumza kwenye hafla ya ushirikiano wa Kusin-Kusin Mjini New York Ban amesema kuwa ametia moyo sana na hatua zilizopigwa na nchi hizo tangu kuanzishwa kwa [...]

14/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa ya kumaliza umaskini yaadhimishwa

umaskini

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu na umaskini Magdalena Sepulveda ameyataka mataifa kupunguza mwanya uliopo kati ya matajiri na maskini . Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumaliza umaskini Sepulveda amesema kuwa pengo lililopo kati ya matajiri na maskini limesababisha kutokuwepo uwiano wa kijamii na kuchangia kudorora [...]

14/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya kulinda amani vinahitaji usalama zaidi- UM

Bw. Herve Ladsous

Mkuu mpya wa kamandi ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa amezungumzia umuhimu wa watendakazi kwenye vikosi hivyo kuhakikishiwa usalama wa maisha wao pindi wanawajibika. Umoja wa Mataifa unajumla ya maafisa 120,000 wanaofanya kazi za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, mkuu huyo mpya Hervé [...]

14/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP kupungukiwa na chakula inapotoa misaada kwa wakimbizi kutoka DRC

wakimbizi wa DRC

Wakimbizi 120,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo walio nchini Congo wakakosa chakula kuanzia mwezi ujao. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiano na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR yamekuwa yakiwandaa wakimbizi kurudi makwao. WFP imekuwa ikitoa chakula kwa wakimbizi katika eneo la Likouala nchini Congo. Kwa sasa karibu [...]

14/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Balozi wa hisani Zidane aenda Mali kujadili umaskini

balozi mwema wa UM  Bw. Zidane

Mwanasoka mashuri wa enzi hizo ambaye sasa ni mjumbe wa hisani wa Umoja wa Mataifa Zinédine Zidane,anatazamiwa kuelekea nchini Mali kwa ajili ya kuweka zingatio la kukabiliana na tatizo la umaskini  Zidane ambaye safari yake imepangwa kufanyika wiki ijayo amesema kuwa anakwenda huko kwa shabaya moja ya kujadilia na kuhimiza mikakati inayoendelea kuchukuliwa ya kukabiliana [...]

14/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuwekeza kwa wanawake wa vijijini kutaangamiza njaa na umaskini:Ban

wanawake vijijini

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwainua wanawake wa vijijini sawia na wanaume akisema kuwa hatua hiyo itachangia kuongezeka kwa chakula na kupungua kwa watu walio na njaa duniani. Akiongea kabla ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake wa vijijini Ban amesema kuwa hata baada ya [...]

14/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na serikali ya Kenya watoa chanjo kwa wakimbizi kutoka Somalia

chanjo kwa wakimbizi kutoka Somali

Zaidi ya wakimbizi 2000 wa Kisomali wanaowasili nchini Kenya kupitia kwa mji wa Liboi ulio kwenye mpaka kati ya Kenya na Somalia wamepata chanjo dhidhi ya ugonjwa wa polio na surua kufuatia ushirikiano kati ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Kenya. IOM na wizara ya afya nchini Kenya walizindua shughuli hiyo [...]

14/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres aomba kuachiliwa kwa madaktari waliotekwa nyara Kenya

mkuu wa UNHCR António Guterres

Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa ameelezea mshangao wake kutokana na kutekwa nyara kwa wafanyikazi wawili wa kike wa kutoa misaada kutoka kwenye kambi ya Daadab nchini Kenya baada ya dereva wao kupigwa risasi. Antonio Geterres amesema kuwa kutekwa nyara kwa wafanyikazi hao kutoka kwa shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka [...]

14/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka jamii ya kimataifa kuchukua hatua nchini Syria

waandamanaji nchini Syria

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuwalinda raia nchini Syria ambapo idadi ya waliouawa sasa imefikia watu 3000 wakiwemo watoto 180. Pillay amesema kuwa tangu kuanza kwa ghasia nchini Syria serikali imekuwa ikitumia nguvu kupita kiasi wakati kuvunja maandamano ya amani. [...]

14/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa ya kuosha mikono kuadhimishwa

kusisitiza umuhimu wa kuosha mikono kwa sabuni

  Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF litajiunga na mamilioni ya watu kote duniani wakati wa siku ya kimataifa ya kuosha mikono katika kusisitiza umuhimu wa kuosha mikono kwa sabuni kama moja ya njia rahisi ya kuzuia magonjwa. Shughuli zinatarajiwa kuandaliwa ambapo walimu, wazazi, watu mashuhuri na maafisa wa serikali watawatia moyo [...]

14/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa yatakiwa kuwahakikishia watoto lishe bora

siku ya chakula duniani

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linatarajiwa kuyaunganisha maisha ya watoto kutoka nchi zinazoendelea duniani wanaoishi kwa njaa kwa wahisani wanaoweza kuwasaidia wakati wa maadhamisho ya siku ya chakula duniani. Mkurugenzi mkuu wa WFP Jesette Sheeran anasema kuwa chakula kizuri ndiyo nguzo ya kukua kwa mtoto aliye na afya akiongeza kuwa huu ndio wakati [...]

14/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watoto 500,000 wa Iraq watapata chakula mashuleni

watoto nchini Iraq

Watoto nusu milioni wa shule za msingi nchini Iraq watafaidika na mpango wa chakula mashuleni wakati utakapoanza muhula mpya wa masomo limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Watoto watakaofaidika ni wale wanaotoka katika wilaya zilizo na matatizo na chini ya mpango huu wapata chakula cha mchana. Chakula hiki kitawawezesha watoto kuhudhuria shule na [...]

13/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko katika jeshi na polisi ni muhimu kwa kuzuia migogoro:Baraza Kuu

13/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji wa kimataifa katika kupunguza hatari ya majanga:UM

13/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Ban atoa heshima kwa mtangulizi wake

Ban akiwa mjini Uppsala nchini Sweden

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa heshima zake kwa mtangulizi wake Dag Hammarskjöld, aliyefariki miaka 50 iliyopita akimtaja kama msuluhishi. Akiongea kando na kaburi lake mjini Uppsala nchini Sweden Ban amesema kuwa Hammarskjöld aliyatenda aliyoyaamini kuwa mema. Bwana Hammarskjöld aliliongoza shirika la Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 1953 hadi kifo chake mwaka [...]

13/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM kuondoa mabomu ya kutegwa ardhini Sudan Kusini

Sudan kusini

Wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa wanaotegua mabomu nchini Sudan Kusini wanafanya mikakati ya kupanua oparesheni zao kwenda eneo la Kaskazini mwa nchi baada ya mlipuko wa bomu kuwaua karibu watu 20 hivi majuzi. Raia 18 na wanajeshi wawili waliuawa wakati basi walilokuwa wakisafiria lilipokanyaga bomu siku ya Jumapili kwenye barabara ya kutoka Mayon kwenda Mankien. [...]

13/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Afisa wa UM azuru DRC kufuatia kuuawa kwa wafanyikazi wa kutoa misaada

wafanyakazi wa kutoa misaada nchini DRC

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa yuko kwenye ziara ya wiki moja katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa mazungumzo na serikali pamoja na maafisa wanaohusika na misaada kufuatia kuuawa kwa wafanyikazi watano wa shirika moja lisilokuwa la kiserikali. Mkurugenzi katika kitengo cha kuratibu na hatua kwenye shirika la kuratibu masuala ya [...]

13/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mataifa mengi sasa yafuatia athari za uwekezaji katika Uchumi wao:UNCTAD

uwekezaji katika uchumi

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo ya kiuchumi na biashara UNCTAD limesema kuongezeka kwa matatizo ya kichumi duniani bado hakujaathiri sera za uwekezaji toka nje ingawa kuna dalili kwamba nchi nyingi zinazidi kuwa na hofu kuhusu athari za uwekezaji wa ndani na nje wa uchumi wao. UNCTAD inasema hofu ya karibuni ya [...]

13/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO kuthathmini athari za mafuriko kwenye eneo la makumbusho la Ayutthaya

Ayutthata Thailand

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limeombwa na serikali ya Thailand kufanya tathimini ya athari ziliazosababishwa na mafuriko kwenye eneo la makumbusho na miongoni mwa urithi wa dunia la Ayutthaya. Makumbusho ya Ayutthaya yamekumbwa na mafuriko kwa wiki nzima sasa, minara na madhabahu katika makumbusho hayo vimeathirika. Kwa mujibu wa [...]

13/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazoendelea zinahitaji msaada kukabiliana na majanga

Janga la mafuriko

Nchi nyingi zinazoendelea bado hazijamudu kukabiliana na athari za majanga ya asili na hata yanayosababishwa na shughuli za binadamu. Hayo yamesemwa na Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya kimataifa hii leo ya kupunguza majanga. Mkazo umetiwa katika kpunguza athari za majanga hayo na kwenda sambamba na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Tatizo kubwa [...]

13/10/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

FAO imeanza miradi kuwasaidia wakulima wa Kenya kudhibiti ukame

ukame nchini Kenya

Wakati msimu wa mvua ukianza nchini Kenya, shirika la chakula na kilimo FAO limeanza mradi wa kusaidia zaidi ya kaya 5000 za wakulima Mashariki mwa nchi hiyo kuandaa matuta katika mashamba yao ili kuhifadhi maji ya mvua kwa ajili ya mazao na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Mradi huo pia unawasaidia wakulima kujenga visima ambavyo vitavuna [...]

13/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhamiaji wa Kusini-Kusini umesambaa kama wa Kusini-Kaskazini:Nasser

rais wa Baraza Kuu Nassir Abdulaziz Al-Nasser

Uhamiaji kutoka Kusini kwenda Kusini umesambaa sana kama ilivyo ule wa kutoka Kusini kuelekea Kaskazini amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Nassir Abdulaziz Al-Nasser ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu uhamiaji na mawasiliano unaofanyika mjini Helsinki Finland. Al-Nasser amesema maeneo mapya ya uhamiaji yanajitokeza barani Asia, Afrika na Amerika Kusini [...]

13/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay apongeza kukamilika kwa tathmini ya kwanza ya haki za binadamu kwa mataifa 193

Navi Pillay

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, leo amepongeza Baraza la haki za binadamu kwa kukamilisha tathimini ya hali ya haki za binadamu kwa mataifa yote wanachama 193. Bi Navi Pillay amesema sasa anatarajia matokeo mazuri kwa mataifa hayo katika kulinda na kuchagiza haki za binadamu. Mchakato huo mpya wa tathimini umekamilika leo [...]

13/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupunguza matatizo ya kutoona:WHO

siku ya kimatifa ya kuona

Shirika la afya duniani WHO limesema katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuona kwamba mkazo wa kimataifa unapaswa kuelekezwa katika kupunguza upofu, matatizo ya kutoona mbali au karibu na kuwasaidia wasioona. Siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba ni maalumu kwa kuelimisha jamii kuhusu upofu, athari zake na njia za [...]

13/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wanapaswa kujifunza kuishi kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa

watoto wacheza kwenye uchafu baada ya tetemeko

Hatari ya kukabiliwa na majanga inakuwa haraka kuliko maandalizi ya kujikinga nayo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa ya kupunguza majanga. Ban amesema mwaka uliopita dunia imeshuhudia majanga makubwa kuanzia mafuriko, matetemeko ya ardhi, tsunami na ukame. Na majanga mengine kama usalama wa nyuklia na [...]

13/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utalii wa kimataifa kufikia bilioni 1.8 ifikapo mwaka 2030:UM

katibu mkuu UNWTO Taleb Rifai

Ripoti zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonyesha idadi ya watalii watakaosafiri toka sehemu moja hadi nyingine inatazamiwa kufikia bilioni 1.8 katika kipindi cha miongo miwili ijayo.  Hali hiyo itakuwa na mafungamano makubwa na ongezeko la ukuaji wa hali ya uchumi kwa baadhi ya mataifa. Katika taarifa yake shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii [...]

13/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wananchi wa Haiti washiriki kikamilifu kusafisha maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko

wananchi wa Haiti watoa uchafu baada ya tetemeko

Mamia kwa maelfu ya wananchi wa Haiti wamejitokeza kushiriki kikamilifu kusafisha masalia ya zaga zaga zilizoachw awakati wa tetemeko la ardhi iliyoikumba nchi hiyo mwaka uliopita. Taarifa za awali zinasema kuwa tetemeko hilo lililosababisha maafa makubwa limeacha masalia mengi ya taka taka ambazo sasa zimeanza kusafishwa katika mpango unaratibiwa na shirika la maendeleo la Umoja [...]

13/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko katika jeshi na polisi ni muhimu katika kuzuia migogoro

Hervé Ladsous

Kufanyia mabadiliko jeshi na mashirika mengine ya usalama ni muhimu kwa kuzuia kuzuka tena kwa migogoro. Hayo yamesemwa leo na mkuu wa operesheni za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous, wakati Baraza la Usalama lilipokutana kujadili mabadiliko katika sekta ya usalama Afrika. Akitolea mfano Liberia bwana Ladsous amesema kuwa sababu matatizo ya usalama [...]

12/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aipongeza Cameroon kwa kuendesha uchaguzi wa amani

uchaguzi Cameroon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza Wacameroon kwa kuendesha uchaguzi mkuu wa Rais wa amani na utulivu lakini kushughulikia malalamiko yote yaliyojitokeza. Uchaguzi huo uliofanyika siku ya Juumapili namuhusisha Rais aliyeko madarakani tangu mwaka 1982 Paul Biya, akichuana na wagombea wengine 22. Katika taarifa yake Ban amezitaka pande zote za siasa kutumia [...]

12/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Masuala ya fedha ya Umoja wa Mataifa yameimarika

Angela Kane

Hali ya kifedha kwenye Umoja wa Mataifa imeonyesha kuimarika mwaka huu licha ya mdororo wa uchumi unaoitikisa dunia, huku nchi wanachama zikilipa madeni yake yote kwa Umoja huo kwa mujibu wa mkuu wa idara ya uongozi ya Umoja wa Mataifa. Angela Kane akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa taarifa ya kamati ya tano [...]

12/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabalozi wema wa UNAIDS wachagiza vita dhidi ya Ukimwi

kongamano lajadili vita dhidi ya ukimwi

Katika siku ya ufunguzi wa kongamano la kimataifa mjini Moscow, Urusi kuhusu lengo namba 6 la maendeleo ya milenia ambalo ni kupambana na ukimwi, malaria na magonjwa mengine, mcheza filamu wa Inda Preity Zinta, mshindi wa kombe la dunia la kandada ya wanawake Lorrie Fair na mwanaharakati wa ukimwi kutoka Urusi Alexander Volgina wakishirikiana na [...]

12/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Liberia yapongezwa kwa kupiga kura kwa amani:UM

kupiga kura Liberia

Waliberia wamepongezwa na Umoja wa Mataifa kwa kuendesha uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge hapo jumanne kwa amani na utulivu ikiwa ni hatua kubwa kwa taifa hilo katika juhudi za kudumisha amani na demokrasia karibu muongo mmoja tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Katibu Mkuu wa Umoja [...]

12/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Aisa Kirabo Kacyira kutoka Rwanda ateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi mtendaji wa UNHABITAT

Bi Aisa Kirabo Kacyira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Bi Aisa Kirabo Kacyira kutoka Rwanda kuwa naibu mkurugenzi mtendaji na katibu mkuu msaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UNHABITAT. Bi Kirabo anayechukua nafasi ya Bi Inga Bjork hivi sasa ni gavana wa jimbo la Mashariki ambalo ni jimbo kubwa kabisa nchini Rwanda [...]

12/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulimwengu kupata mtu wa bilioni 7 mwishoni mwa mwezi

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ulimwengu unastahili kujitahidi zaidi wakati idadi ya watu duniani inapotimia watu bilioni 7 baadaye mwezi huu. Akihutubia mkutano wa kimataifa kuhusu nishati safi mjini Copenhagen unaowaleta pamoja viongozi wa serikali , biashara na mashirika ya umma Ban amesema kuwa watoto wanaozaliwa ni lazima wapate maisha [...]

12/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuwa maskini ni gharama kubwa:UNDP

Rebeca Grynspan

Afisa Mtendaji wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP ametaka kuongezwa juhudi za uzalishaji wa nishati mbadala kwa kutumia vyanzo rafiki ili kulinda mazingira. Bi Rebeca Grynspan, ambaye alikuwa akizungumza kwenye kongamano la kimataifa huko Oslo amesema kuwa kuna haja ya kuongeza mashirikiano kwa sekta zote ili kufikia shabaha ya nishati mbadala. Ameongeza [...]

12/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Haki za binadamu walaumiwa na Syria

Faysal Mekdad naibu waziri wa mambo ya nje wa Syria

Ripoti ya tathimini ya hali ya haki za binadamu nchini Syria imepitishwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa lakini si kimya kimya, kwani Syria imewashutumu baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kuingiza siasa katika tathimini hiyo. Tathimini hiyo ya Syria ni sehemu ya muendelezo wa tathimini inayoendelea kupitia utekelezaji wa hali [...]

12/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika iko njiani kufufua uchumi wake:Migiro

mchuuzi wa mboga

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amesema bara la Afrika liko njiani kufufua uchumi wake na kwamba kiwango cha ukuaji wa uchumi kinatarajiwa kuendelea. Akizungumza kwenye kongamano la kimataifa kuhusu ufahamu na elimu mjini Seol Korea Bi Migiro amesema uchumi wa Afrika unatarajiwa kukua kwa asilimia 6 mwaka 2012 ambayo itakuwa [...]

12/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taifa la Yemeni lakabiliwa na njaa kubwa wakati pia likikumbwa na matatizo ya kibinadamu

watoto wa Yemen

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo limeonya kwamba kuzorota kwa hali ya usalama wa chakula iliyochangiwa na kupanda kwa bei, upungufu wa mafuta na matatizo ya kisiasa kunazifanya familia nyingi kushindwa kulisha watu wake. Mkurugenzi mkuu wa WFP Bi Josette Sheeran amesema hasa ongezeko la gharama za chakula na machafuko ya kisiasa yamewaacha [...]

12/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani vikali mauaji ya walinda amani wa UNAMID Darfur

Baraza  la Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mashambulizi dhidi ya walinda amani wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika UNAMID kwenye jimbo la Darfur Sudan. Mashambulizi hayo yaliyofanyika Oktoba 10 yamekatili maisha ya wanajeshi wawili kutoka Rwanda na mshauri mmoja wa polisi kutoka Senegal. Wanajeshi wengine [...]

12/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizi ya Kifua Kikuu yamepungua:UM

12/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia kuwarejesha nyumbani raia wa Sudan Kusini

Wakimbizi wa Sudan Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasaidia maelfu ya raia wa Sudan Kusini kurejea nyumbani. Kwa mujibu wa shirika hilo maelfu ya raia hao wengi walikuwa wamekwama katika eneo la Kosti na wengine ni wale walioishi Kaskazini kwa muda na sasa wanataka kurudi nyumbani. Hata hivyo IOM inasema licha ya kuanza kuwasafirisha watu hao ni [...]

11/10/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uzalishaji wa Kasumba waongezeka Afghanistan:UNODC

Kilimo cha kasumba Afghanistan

Uzalishaji wa kasumba umeongezeka kwa asilimia 60 nchini Afghanistan kwa mwaka huu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa na serikali ya Afghanistan. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uhalifu na Madawa UNODC inasema kilimo cha kasumba nchini humo kimeongezeka kwa asilimia 7 mwaka 2011 kutokana na usalama mdogo, matatizo [...]

11/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa Sri Lanka kungo'a nanga

wakimbizi wa Sri Lanka

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Linatarjia kupokea kundi la kwanza la wakimbizi raia wa Sri Lanka watakaosafiri kwa mashua kutoka nchini India hapo kesho kwenye mpango unaoungwa mkono na Sri Lanka pamoja na India. Hadi sasa wakimbizi wote wa Sri Lanka wamekuwa wakirejea nyumbani kwa njia ya ndege. Watakaorejea nyumbani ni [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OHCHR yahuzunishwa na kunyongwa kwa watu nchini Saudi Arabia

Rupert Colville

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imehusunishwa na hatua ya Saudi Arabia ya siku ya ijumaa ya kuwanyonga hadharani wanaume 15, 8 kati yao wakiwa ni wahamiaji wafanyikazi raia wa kigeni. Ofisi ya haki za binadamu ya UM inasema kuwa kati ya watu 58 walioripotiwa kunyongwa nchini Saudi Arabia mwaka huu 20 [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yawasaidia raia wa Sudan Kusini kurudi nyumbani

nemba ya IOM

Msafara wa nne wa mashua zinazowasafirisha raia 1800 wa Sudan Kusini kutoka mji wa Kosti ulio kusini mwa mji mkuu wa Sudan Khartoum umewasili kwenye mji wa mkuu wa Sudan Kusini Juba. Oparesheni hiyo imefikisha idadi ya wale waliosafirishwa na IOM kuwa watu 7000 tangu Julai 26 baada ya Sudan Kusini kutangazwa huru Julai 9 [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Marekani yatoa msaada wa kuwasaiadia wanaoishi na virusi vya ukimwi Ethiopia

mkurugenzi mkuu wa WFP Josette Sheeran

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha msaada wa jumla ya dola milioni 56 kutoka kwa shirika la mpango wa dharura la ukimwi la rais wa Marekani PEPFAR msaada ambao utachangia katika kuongeza ufadhili wa programu za kusaidia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini Ethiopia. Mkurugenzi mkuu wa WFP Josette Sheeran anasema kuwa [...]

11/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa kipindupindu waua watu Afrika Magharibi

vitanda vya wagonjwa wa kipindupindu

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa kuna zaidi ya visa 85,000 kipindupindu Magharibi na kati kati mwa Afrika hasa nchini Chad, Cameroon na Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Hali hiyo inatia wasi wasi kutokana na sababu kwamba ugonjwa huo unaripotiwa kwenye maeneo makubwa ambapo watu hawaelewi njia zozote za kuuzuia na kuutibu [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani watatu wa UNAMID wauawa Darfur

Walinda amani wa UNAMID

Walinda amani watatu wa mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika kulinda amani Darfur Sudan UNAMID wameuawa usiku wa kuamkia leo kwenye shambulio katika kambi ya wakimbizi wa ndani. Ukithibitisha mauaji hayo mpango wa UNAMID umesema askari hao walikuwa katika shughuli za kila siku za kushika doria waliposhambuliwa na kundi la watu wenye [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia nchini Liberia wapiga kura

vifaa vya kupiga kura nchini Liberia

Raia nchini Liberia hii leo wamepiga kura kwenye uchaguzi wa urais na ubunge, uchaguzi unaoonekana kama kiungo muhimu katika kudumisha amani na demokrasia nchini Liberia . Hii ndiyo mara ya kwanza Liberia inajisimamia na kujiendelezea uchaguzi baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 kusimamiwa na Umoja wa Mataifa. Wagombea 16 akiwemo rais Ellen Johnson Sirleaf wanawawania [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka kuwepo matumizi ya nishati safi

nishati safi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa matumizi ya nishati safi duniani ni lazima yaambatane na changamoto za kijamii, kiuchumi na za kimazingira. Akizungumza kwenye mkutano kuhusu matumizi ya nishati safi mjini Copenhagen Ban amesema kuwa kwa sasa ulimwengu unakabiliwa na changamoto za chakula , mafuta na uchumi kwa hivyo masuala [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu kutokana na ghasia kwenye Ukingo wa Magharibi:UM

Palestinian-attacks

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na ghasia zinazoendeshwa na walowezi wa kiyahudi dhidi ya raia wa kipalestina kwenye ukingo wa magharibi tangu mwezi Septemba. Kijiji cha Qusra karibu na mji wa Nablus kaskazini kwa ukingo wa Magharibi kimekuwa kikilengwa na walowezi kwa muda wa karibu majuma [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNCTAD yakutana na viongozi wa Asia Kusini

Dr Supachai Panitchpakdina

Viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wameanzisha majadiliano ya pamoja huko Bangkok yakihusisha nchi za Kusini mwa Asia kwa shabaha ya kusaka mustabala mwema wa eneo hilo kwa siku za usoni. Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya biashara UNCTAD, Dr Supachai Panitchpakdina mwenzie anayeshughulia ustawi wa [...]

11/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Miji ya Pakistan yajiunga kwenye mpango wa UM

mwakilishi wa UM Margaret Wahlstrom

Zaidi ya miji 30 nchini Pakistan imejiunga kwenye mpango unaendeshwa na Umoja wa Mataifa wenye shabaha ya kupiga kampeni ya kujiandaa na majanga ya kimazingira. Mpango huo unaendeshwa na Umoja wa Mataifa ni hatua ya awali ya kuyaandaa maeneo yanayokumbwa mara kwa mara na matukio ya majanga ya kimaumbile yakijiweka sawa kwa hali yoyote inayoweza [...]

11/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ataka utulivu Misri

maandamano ya wakristo nchini Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa mwito akitaka kuwepo kwa hali ya utulivu nchini Misri ambako kumejitokeza machafuko na kusabisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa. Vurugu hizo, zilijitokeza pale waumini wa dhehebu la kikristo la Coptic walipokwaruzana na vikosi vya polisi wakilalamikia hatua askari hao hivi karibuni [...]

11/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maambukizi ya kifua kikuu yamepungua duniani:WHO

Mgonjwa wa TB akichomwa sindano

Shirika la afya duniani WHO limearifu kwa mara ya kwanza kwamba idadi ya watu wanaougua kifua kikuu inapungua kila mwaka. Takwimu mpya zilizochapishwa leo na WHO kwenye ripoti yake iitwayo 2011 Global Tuberclosis Control zinaonyesha kwamba idadi ya watu wanaokufa na maradhi hayo kwa mwaka huu imepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka kumi. [...]

11/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei za chakula kuendelea kupanda:FAO

10/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mahabusu wa vita wanateswa Afghanistan:UNAMA

gereza la Afganistan

Mahabusu nchini Afghanistan wanakabiliana na baadhi ya mifumo ya utesaji imesema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa. Mpango wa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA umesema hayo baada ya kuwahoji mahabusu wanaoshikiliwa kwa sababu zinazohusiana na vita ambao walikamatwa na posili au idara ya upelelezi ya nchi hiyo. UNAMA inasema inatarajia ripoti hiyo [...]

10/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Thailand yatakiwa kufanyia marekebisho sheria zake za uhuru wa kujieleza

Bw. Frank De La Rue

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya uhuru wa maoni na wa kujieleleza Frank La Rue ameitaka serikali ya Thailand kufanyia marekebisho sheria zake zinazohusu uhuru wa maoni ambazo kwa mujibu wa kifungu namba 112 cha nchi hiyo mtu yeyote anaye mdaharau, kumtukana au kumtishia mfalme, malkia au mwana mfalme ataadhibiwa kwenda jela [...]

10/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

DR. Congo inaweza kuendelea sana ikitumia misitu yake vyema:UNEP

Hali ya misitu Congo

Utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP unasema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaweza kuwa na maendeleo makubwa sana barani Afrika endapo itapunguza shinikizo na kushughulikia haraka matatizo yanayoikabili sekta yake ya mali asili. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio yenye nusu ya misitu ya bara la Afrika, ina vyanzo vikubwa [...]

10/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wawasili Iraq

Martin Kobler akiwa na Ban Ki-moon

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenda nchini Iraq umeanza mkutano na maafisa wa ngazi za juu kutoka kwa serikali ya nchi hiyo kujadili jinsi Umoja wa Mataifa unavyoweza kulisaidia taifa hilo la mashariki ya kati kujijenga na kuwa dhabiti. Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler akiandamana na maafisa [...]

10/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utalii bora utasaidia kufikia malengo ya maendeleo ya milenia:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa UM Bi. Asha Rose Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amezitaka serikali, wahisani na taasisi za fedha za kimataifa kutumia uwezo wa utalii kwa ajili ya maendeleo. Migiro amesema sekta ya utalii ina uwezo mkubwa wa kutoa nafasi za ajira, kuchagiza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini. Akihutubia kikao cha 19 cha Baraza Kuu la [...]

10/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wanawake haukubaliki duniani:Manjoo

Rashida Manjoo

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Rashida Manjoo amesema kuota mizizi na kusambaa kwa ukatili dhidi ya wanawake ni sala lisilokubalika popote dniani. Akihutubia Baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Bi Manjoo amewasilisha ripoti ya katili huo, chanzo chake na athari zake. Amesema haijalishi unatokea wakati gani uwe [...]

10/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umaskini wa nishati ni tishio la kufikia malengo ya milenia:Ban

Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa kwa mkutano mjini Oslo

Umasikini wa nishati ni tishio kubwa la kufikia malengo yote ya maendeleo ya milenia ameonya Katibu Mkuu wa UMoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa nishati mjini Oslo wenye mada "nishati kwa wote, kufadhili upatikanaji kwa nchi masikini" Ban amesema umasikini wa nishati unadumaza ukuaji wa uchumi na upatikanaji [...]

10/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtu 1 kati ya 4 atahitaji huduma ya afya ya akili duniani:WHO

siku ya kimataifa ya afya ya akili

Serikali zote zimetakiwa na shirika la afya duniani WHO kuongeza fedha zaidi katika huduma za afya ya akili. Mtu mmoja kati ya wanne watahitaji huduma ya afya ya akili katika wakati fulani wa maisha yao limesema shirika hilo. WHO imetoa ramani ya afya ya akili kwa mwaka 2011 hii leo Oktoba 10 ikiadhimisha pia siku [...]

10/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati njaa ikinyemelea Sudan Kusini kila mbegu ni muhimu:FAO

kila mbegu ni muhimu Sudan Kusini

Baadhi ya sehemu za Sudan Kusini janga la kibinadamu linanyemelea kutokana na ukosefu wa chakula limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Tathimini ya karibuni imeonyesha kuwa taifa hilo jipya litaweza kuzalisha nusu tu ya idadi ya nafaka inayohitajika kulisha watu wake, hali ambayo itasababisha watu takribani milioni 1.3 kukabiliwa na njaa. Kupitia mradi maalumu [...]

10/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya njaa 2011 yasema bei za chakula kuendelea kupanda:FAO

bei ya vyakula kuendelea kupanda

Gharama na bei za chakula zitaendelea kuwa juu na pengine kuongezeka na kusababisha wakulima masikini, wachuuzi na nchi nyingi kuwa katika hali mbaya ya umasikini zaidi na ukosefu wa chakula imesema ripoti ya hali ya njaa duniani iliyotolewa leo mjini Roma. Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa yaliyotoa ripoti hiyo ya pamoja lile la chakula [...]

10/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yajadilia ombi la Palestina kuwa mwanachama UM

bodi ya watendaji ya UNESCO

Bodi ya watendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu,sayansi, na utamaduni imekamilisha majadiliano ya wazo yaliyoshuhudia yakiweka usoni ombi la Palestina kwenye Umoja wa Mataifa na bila kuweka kando ahadi ya bodi hiyo juu kujitawanya zaidi barani Afrika. Bodi hiyo ya wakurugenzi inaundwa na jumla ya wanachama 58 wanazunguka kwa muhula wa miaka [...]

10/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Washindi wa Nobel wamedhihirisha uwezo wa wanawake kuchangia amani

10/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Hatua zimepigwa kimaendeleo Afrika baada ya miaka 10:NEPAD

Abdulaziz Al-Nasser

  Nchi za Afrika zimepiga hatua tangu kupitishwa kwa mpango mpya wa ushirikiano kwa ajili ya maendeleo barani Afrika NEPAD amesema afisa wa Umoja wa Mataifa. Cheick Diarra ambaye ni mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika amesema lengo kubwa la NEPAD ambayo ilianzishwa Julai mwaka 2001 ni kuisaidia Afrika katika umasikini na kutokuwa [...]

07/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Utafiti zaidi utahitajika kukabilia NCD’s Afrika

Waziri Haji Mponda

Maradhi ya kisukari, moyo, saratani na matatizo ya kupumua kwa miaka mingi yamekuwa yakizikumba zaidi nchi zilizoendelea na ndio maana hata kuna baadhi ya nchi waliyachukulia kama ni magonjwa ya matajiri, lakini mtazamo umebadilika. Mkutano wa wakuu wa nchi kwenye Umoja wa Mataifa mwezi uliopita kwenye mjadala wa Baraza Kuu la 66 ulifahamishwa kwamba magonjwa [...]

07/10/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yazindua kampeni kukabili biashara haramu ya usafirishwaji watu

gari la kampeni ya  kukabili biashara haramu ya usafirishwaji watu

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji leo limezindua kampeni maalum huko Berlin yenye shabaha ya kukabiliana na tatizo la usafirishaji haramu wa binadamu. Shirika hilo IOM limesema kuwa kampeni hiyo inatazamiwa kudumu kwa muda wa mwezi wa Novemba katika maeno yote ya Ujerumani. Zingatio kubwa linalowekwa kwenye kampeni hiyo ni kukabili vitendo vya [...]

07/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Peru yatakiwa kuweka zingatio kwenye sayansi na ubunifu ili kukuza uchumi wake

mkutano peru

Wataalaamu wa masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu ambao hivi karibuni waliendesha utafiti wao katika nchi ya Peru, wamesema kuwa nchi hiyo inapaswa kuanzisha sera mbadala zitazosaidia kusuma mbele shughuli za kiuchumi. Kwa mujibu wa wataalamu hao ambao walipewa dhima hiyo na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD, nchi ya Peru [...]

07/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yajiunga na UPU na kuwa mwanachama wa 192

bendera ya sudan

Shirika la posta duniani limesema kuwa linaikaribisha Jamhuri ya Sudan Kusin kwenye jumuiya hiyo kwa furaha kubwa, hasa inapozingatiwa kuwa taifa hilo linakuwa mwanachama wa 192 kwenye umoja huo wa posta UPU. Jamhuri ya Sudan Kusin wiki hii yaani Octoba 4, ilijiunga rasmi kwenye umoja huo baada ya maombi yake kukubaliwa na maafisa wa ngazi [...]

07/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IRB na WFP katika juhudi za kumaliza njaa duniani

WFP-IRB

Mashindano ya Ragbi ya kuwania kombe la dunia mwaka huu yatakayoandaliwa nchini New Zealand yanatarajiwa kuunga mkono jitihada za shirika la mpango wa chakula duniani WFP baada ya kuongezwa muda wa kampeni ya kumaliza njaa duniani na bodi ya kimataifa ya mchezo wa Ragbi. Kampeni hiyo iliyozinduliwa mwaka 2003 ina lengo la kutoa hamasisho ya [...]

07/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia maelefu ya wakimbizi kwenye jimbo la Puntland nchini Somalia

wavuvi nchini Somalia

Takriban wahamiaji 500 wameandikishwa kwenye eneo la Bossaso ambayo ndiyo bandari kubwa zaidi kwenye jimbo la Puntland nchini Somalia. Maelfu ya watu waliohama makwao kutoka sehemu zinazokumbwa na ukame kusini mwa Somalia pia wamepiga kambi sehemu mbali mbalia za eneo hilo. Kwa muda wa miezi miwili iliyopita shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limewapa wahamiaji [...]

07/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yamuenzi Steve Jobs wa Apple

Steve Jobs

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamadni NESCO Bi Irina Bokova leo amemuenzi na kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanzilishi mshiriki na aliyekwa mwenyekiti wa kampuni ya Apple Inc Steve Jobs ambaye amefariki dunia Oktoba 5 mwaka huu. Bi Bokova amesema Jobs sio tuu ameleta mapinduzi katika [...]

07/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi kutoka Sudan waingia nchini Ethiopia

wakimbizi wa Sudan waingia Ethiopia

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limeweka kambi mpya Magharibi mwa Ethiopia ili kuto hifadhi kwa wakimbizi wanaokimbia mapigano na kuvuka mpaka kutoka jimbo la Blue Nile nchini Sudan. Kambi hiyo ina uwezo wa kuwahifadhi watu 3000 huku ikitarajiwa kupanuliwa zaidi. Kwa mwezi mmoja uliopita zaidi ya watu 27,000 wamelikimbia mjimbo la Blue [...]

07/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kuisadia Sudan Kusini kwenye ujenzi wa barabara

ukosefu wa barabara Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linaendelea kuisadia serikali ya Sudan Kusini katika ujenzi wa barabara kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma za kibinadamu na kwa vyakula kufikishwa kwa urahisi sokoni. WFP ina mipango ya kujenga barabara zenye urefu wa kilomita 500 kote nchini Sudan Kusini ikiwa na lengo la kuimarisha maendeleo ya [...]

07/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia kwenye mji wa Sirte nchini Libya wapitia hali ngumu

raia wa Libya

  Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC inasema kuwa raia kwenye mji wa Sirte nchini Libya wanakabiliwa na changamoto za ukosefu mkubwa wa chakula na mafuta. Pia hospitali iliyo kwenye mji huo haina uwezo wa kuhudumia idadi kubwa ya majeruhi ikiwa pia inakabiliwa na ukosefu wa nguvu za umeme. ICRC inatoa usaidizi kwa takriban [...]

07/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurupuko wa Surua waripotiwa barani Ulaya, Afrika na Marekani

watoto hospitalini wangoja utambuzi wa surua

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa mkurupuko mkubwa wa ugonjwa wa surua umeripotiwa barani Ulaya, Afrika na Marekani. Takriban visa 160,000 vya ugonjwa huo vimeripotiwa kote duniani tangu mwezi Januari mwaka huu. WHO inasema kuwa Afrika ndiyo imeathirika zaidi ikiwa na visa 130,000 wakati ambapo Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ikiwa na visa vingi [...]

07/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Merkel na viongozi wa mashirika watoa wito wa kubuniwa ajira zaidi

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, mkurugenzi wa shirika la kazi duniani ILO Juan Somavia na wakuu wengine wa mshirika matano ya kimataifa kwa pamoja wametoa wito wa kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa uchumi wa dunia unaaminika. Wakitoa wito huo kabla ya kuandaliwa kabla ya mkutano wa mataifa tajiri zaidi duniani na yanayoinukia kiuchumi ya G20 [...]

07/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR na Rwanda wajadili hatma ya wakimbizi

Wakimbizi wa Rwanda

Serikali ya Rwanda na kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la wakimbizi UNHCR wamektana mjini Geneva kujadili hatua zilizopigwa kupata sukluhu ya wakimbizi wa Rwanda. Pande hizo mbili zilikwa kwenye kikao cha 62 kamati kuu ya UNHCR zimesema bado zimejidhatiti kupiga hatua ya suluhu ya wakimbizi na kuuafikiana kwamba mkutano wa pande zote [...]

07/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tuzo ya amani ya Nobel yaenda kwa wanawake watatu wanaharakati wa haki za binadamu

Leyma Gbowee wa Liberia, Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, na Tawakkul Karma wa Yemen

Mwanamke wa kwanza kuchagulia kuwa Rais barani Afrika, mwanaharakati wa kupinga ubakaji Liberia na mwanamke wa Yemen aliyesimama kidete dhidi ya utawala wa nchi hiyo ndio washindi wa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka huu iliyotangazwa mapema leo asubuhi. Wanawake hao watatu Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, mwanaharakati wa haki za binadamu Leyma [...]

07/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Abyei inaweza kuwa chanzo cha mvutano baina ya Sudan na Sudan Kusini:UM

wakaazi wa Abyei

Kuwepo kwa majeshi yenye silaha kutoka Sudan na Kusini Kusini kwenye jimbo lenye utajiri wa mafuta linalozozaniwa la Abyei inaweza kuwa chanzo cha mvutano baina ya nchi hizo mbili jirani. Mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa Herve Ladsous ameliambia Baraza la Usalama leo kwamba makubaliano yaliyoafikiwa mwezi Juni ya kuondoa vikosi [...]

06/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa UM wa kupunguza vifo vya wavuvi kuanza kutumika Septemba ijayo

wavuvi waandaa mashua yao

Mkataba unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wenye lengo la kupunguza takriban vifo 24,000 vinavyotokea wakati wa shughuli za uvuvi kote duniani unatarajiwa kuanza kutumika mwezi Septemba mwaka ujao ikiwa ni zaidi ya miaka 17 tangu upitishwe na shirika la kimataifa la mabaharia IMO. Mkataba huo ulipata sahihi yake ya 15 kutoka kwa taifa la [...]

06/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mambo zaidi ya kale kwenye orodha ya UM

ongezeko kwenye orodha ya mambo ya kale

Miswada ya karne ya tano kutoka nchini Georgia, Amri ya kifalme ya mwaka 1537 kutoka nchini Ufaransa na utafiti wa anga wa karne ya ishirini ni kati ya mambo saba yaliyoorodheshwa kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya mambo ya kale. Kujumuishwa kwa masuala hayo kunafikisha idadi ya mambo ya kale yaliyo kwenye orodha hiyo [...]

06/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujerumani yatakiwa kukoma kuendelea kuwazuia wafungwa

jela za ujerumani

Serikali ya Ujerumani imetakiwa kuchunguza mfumo wake wa kuendelea kuwazuia wafungua hata baaada ya wafungwa hao kukamilisha vifungo vyao. Wito huo unajiri baada ya ziara ya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ujerumani. Wakati wa ziara hiyo wataalamu hao waliwahoji watu kadha wanaoendelea kuzuiliwa chini ya mfumo wa kuzuia baada ya kukamilisha kifungo. [...]

06/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vijana waueleza UM hofu yao kuhusu athari za matatizo ya kiuchumi

vijana kutoka mataifa 22

Vijana kutoka mataifa 22 wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wiki hii ili kutanabaisha athari za mdororo wa kiamatifa wa uchumi kwa vijana duniani kote. Ukosefu wa ajira, kupunguza kwa ufadhili wa elimu na haja ya kuwahusisha vijana katika maamuzi ni miongoni mwa masuala ambayo ujumbe wa vijana hao wamekwa wakiwasilisha kwa viongozi [...]

06/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNICEF ataka ulinzi wa haraka kwa watoto Yemen

watoto wa Yemen

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ametoa wito wa ulinzi wa haraka kwa watoto nchini Yemen ambao wamejikuta katika hatari ya mapigano kufuatia kuzuka machafuko mapema mwaka huu. Bwana Anthony Lake amesema watoto hao wanapaswa kuwa mashuleni katika kipindi hiki cha mwaka lakini badala yake wanakabiliwa na watu wenye silaha [...]

06/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na Baraza la Usalama kutoafikiana kuhusu Syria

Baraza la Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amesikitishwa na kitendo cha Baraza la Usalama kushindwa kuafikiana kuhusu azimio dhidi ya Syria. Jumanne siku Uchina na Urusi walipiga kura ya turufu kupinga azimio linalotishia kuiwekea vikwazo Syria endapo haitositisha mashambulizi ya kijeshi dhiri ya raia wanaoandamana kwa amani. Wajumbe wengine wane wa baraza hilo [...]

06/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Soko la nafaka linatarajiwa kusalia kuwa juu licha ya ongezeko la uzalishaji:FAO

uzalishaji wa nafaka

Licha ya kuongezeka kwa matarajio ya uzalishaji, soko la dunia la nafaka linatarajiwa kusalia kwa la juu kwa mwaka 2011/2012 limesema leo shirika la chakula na kilimo FAO. Ripoti ya FAO ya matarajio ya hali ya mazao kwa robo ya mwaka inaonyesha kuwa uzalishaji wa nafaka duniani utafikia tan milioni 2301 katika msimu huu ikiwa [...]

06/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afisa wa UM atembelea Pakistan kukagua mkwamo uliosababishwa na mafuriko

mafuriko Pakistan

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na upunguzaji majanga kwenye maeneo yaliyokumbwa na matukio mabaya, amewasili nchini Pakistan ambako anatazamiwa kukutana na maafisa wa serikali kwa ajili ya kujadilia hatua za dharura zitakazosaidia kupunguza mkwamo uliosababishwa na mafuriko ambayo yameharibu mfumo mzima wan chi hiyo. Bi Margareta Wahlström,akiwa nchini humo anatazamiwa kukutana na [...]

06/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNEP yajiunga na kampeni ya watu bilioni 7 kuonyesha fursa na changamoto

kampeni ya watu bilioni 7

Idadi ya watu duniani itafikia bilioni 7 hapo Oktoba 31 mwaka huu na kuleta changamoto ya kuhakikisha maendeleo endelevu na usawa katika kugawana rasilimali kukidhi idadi hiyo ya watu. Kwa kulitambua hilo shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP leo limejiunga na kampeni ya kuchukua hatua kukidhi matakwa ya watu bilioni 7 kwa kuwachagiza [...]

06/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Masuala ya nishati na kujali mazingira ndio agenda za ziara ya Ban Norway, Denmark na Sweden

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon atazuru nchi za Scandinavia wiki ijayo ili kuhudhuria mikutano kuhusu nishati, maendeleo endelevu, mabadiliko ya hali ya hewa na mikakati ya uchumi inaojali mazingira. Pia atakutana na wakuu wa nchi na viongozi mbalimbali wa serikali nchini Norway, Denmark na Sweeden. Katika kituo chake cha kwanza Oslo Norway [...]

06/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji yako katika kiwango cha juu marekani na Afrika:UNODC

Homicide2

Matokeo ya kwanza ya utafiti uliofanywa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC kuhusu mauaji na kutolewa leo yanaonyesha kwamba vijana wa kiume hususani Amerika ya Kati na Kusini, visiwa vya Caribbean na Afrika ya Kati na Kusini wako katika hatari ya kuwa wahanga wa mauaji kimataifa. Utafiti huo ulioitwa "utafiti [...]

06/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuuimarisha utawala wa sheria ni muhimu sana:Migiro

Asha -Rose Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa kujihusisha katika kuimarisha utawala wa sheria, jambo ambalo limeleta matunda yaliyoshuhudiwa katika nchi mbalimbali hasa kuchagiza uwajibikaji na uwazi. Akizungumza kwenye kamati ya Baraza Kuu inayoshughulika na masuala ya sheria ambayo pia hujulikana kama Sixth Committee au kamati ya sita, Asha-Rose [...]

05/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Shambulizi la kujitoa mhanga lalaaniwa kwenye UM

kikosi cha kulinda amani AMISOM

Mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Shamsul Bari amelaani vikali shambulizi la kujitoa mhanga mjini Mogadishu na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kutuma kikosi kitakachosaidia kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) ili kiweze kuwalinda raia kutoka kwa vitendo hivi viovu. Bwana Bari [...]

05/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awashauri wanafunzi kuimarisha sheria kwenye mataifa yanayokua

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa ulimwengu unastahili kuwa mahala penye uwajibikaji na pia mahala ambapo sheria na uzuiaji wa uhalifu vinatekelezwa kwa minajili ya kuweka amani. Ban pia amewashauri wanafunzi kujiunga na huduma za kuleta amani za Umoja wa Mataifa kwenye nchi ambazo zinakuwa kidemokrasia ili kusaidia kuimarisha mifumo [...]

05/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM waipongeza Mexico kutokana na mpango wake wa kuwalinda raia wake dhidi ya tetemeko la ardhi

mji wa Mexico

Umoja wa Mataifa umeipongeza Mexico ambayo hivi karibuni imetangaza kuchukua hatua madhubiti za kuwanusuru raia wake kutoka kwenye majanga ya kimaumbile kama tetemeko la ardhi. Kupitia sheria yake mpya, serikali imeridhia kutoa uangalizi wa karibu pamoja na kutoa hifadhi salama za nyumba wakati kunapojiri matukio kama tetemeko la ardhi. Wiki iliyopita serikali hiyo ilipitisha sheria [...]

05/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UN-HABITAT yatoa mafunzo kuhusu ardi, nyumba na haki za nyumba

nemba ya UN-HABITAT

Kufuatia shirika la Umoja wa Mataifa la makaazi UN-HABITAT kuzindua mwaka 2010 mafunzo maalumu kuhusu ardhi, nyumba na haki za nyumba kwenye ulimwengu wa Kiarabu, sasa mpango wa shirika hilo nchini Somalia umeendesha mafunzo kwa wakufunzi kuanzia Aprili mwaka huu mjini Nairobi. Siraj Sait mwandishi na mchangiaji mkubwa wa mafunzo hayo aliendesha mafunzo kwa wafanyakazi [...]

05/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umezindua mradi wa kutumia simu za mkononi kusaidia masikini kwa chakula Ivory Coast

simu za mkono nchini Ivory Coast

Umoja wa Mataifa umezindua mradi wa majaribio ambayo inatumia teknolojia ya simu za mkononi kutuma fedha za kusaidia maelfu ya watu masikini ambao waliathirika vibaya na machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Ivory Coast kununua chakula. Zaidi ya familia 10,000 kwenye wilaya za Abobo na Yopougon mjini Abuja zitapata ujmbe kwenye simu zao za mkononi [...]

05/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo ya chakula yafukuta Sudan Kusini:FAO

msaada wa chakula kutoka WFP

Msaada wa haraka unahitajika ili kuzuia janga la kibinadamu na matatizo ya chakula yanayofukuta kwenye majimbo mawili ya mpakani kati ya Sudan na taifa jipya la Sudan Kusini, limeonya leo shirika la chakula na kilimo FAO. Kwa mujibu wa shirika hilo upatikanaji wa chakula katika jimbo la Blue Nile na Kordofan Kusini unatarajiwa kupungua kufuatia [...]

05/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama kujadili jukumu muhimu la wanawake kuzuia vita

Joy Ogwu, Balozi wa Nigeria

Jukumu muhimu la wanawake katika kuzuia migogoro itakuwa miongoni mwa masuala matatu muhimu yanayotarajiwa kujadiliwa na Baraza la Usalama mwezi huu wa Oktoba. Hayo yamesemwa na Balozi Joy Ogwu wa Nigeria ambaye anachukwa jukumu la Rais wa Baraza la Usalama mwezi huu, alipokuwa akifafanua yatakayojitokeza kwenye baraza hilo mwezi huu. Amesema moja ya mijadala itakuwa [...]

05/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taifa changa kabisa duniani Sudan Kusini lajiunga na ITU

bendera ya Sudan Kusini

Muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU umesema unafuraha kubwa kutangaza kwamba taifa changa kabisa duniani Sudan Kusini limejiunga na ITU na kuwa taifa mwanachama wa 193 kuanzia Oktoba 3 mwaka huu. Taifa hilo ambalo limejinyakulia uhuru wake Julai 9 mwaka 2011 tayari limeshapewa namba ya kimataifa ya nchi hiyo ambayo ni +211, baada ya nchi [...]

05/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lashindwa kupitisha azimio kulaani Syria

Baraza la Usalama

Baraza la Usalama jumanne usiku limeshindwa kupitisha azimio ambalo lingelaani ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea nchini Syria, azimio ambalo lingeonya kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya utawala wa Rais Bashar al-Assad ikiwemo vikwazo endapo hali hiyo ingeendelea. Azimio hilo limeshindwa kupitishwa kutokana na kura mbili za turufu kutoka kwa wanachama wawili wa kudumu wa [...]

05/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia katika sekta ya elimu ni chachu ya mafanikio:UM

siku ya waalimu

Umuhimu wa kuwapa elimu bora wasichana na wavulana ndio kiini cha siku ya kimataifa ya waalimu ambayo kauli mbiu yake mwaka huu ni "elimu kwa ajili ya usawa wa kijinsia". Siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka ni ya kuwaenzi mamilioni ya waalimu kote duniani ambao wamejitolea maisha yao kufundisha, watoto, vijana na watu wazima umesema [...]

05/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Angelina Jolie atoa wito wa kuongeza juhudi kusaidia Pembe ya Afrika

Angelina Jolie

Angelina Jolie Mcheza filamu maarufu na balozi mwema wa Umoja wa Mataifa Angelina Jolie ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi za kukabiliana na matatizo yanayolikumba eneo la Pembe ya Afrika. Ametoa witi huo kwenye mkutano wa kila mwaka wa kamati kuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia wakimbizi UNHCR mjini Geneva leo. [...]

04/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa ndani 600,000 wanakabiliwa na shida Haiti:Amos

Valerie Amos

Takriban wakimbizi wa ndani 600,000 waliosambaratishwa na tetemeko la ardhi la mwaka jana nchini Haiti wako katika hatari ya kukabiliwa na njaa, kipindupindu na majanga ya asili amesema mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa. Valarie Amos ambaye amerejea kutoka Haiti alikozuru kwa siku mbili amesema uongozi wa taifa hilo la Caribbean, watu [...]

04/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF na washirika wajadili mahitaji ya lishe

Mama na watoto

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limewaleta pamoja takriban washirika 100 kujadili kuendendelea kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za lishe na kutoa wito wa kuwepo ushirikiano miongoni mwa mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya umma, wasomi na sekta ya lishe. UNICEF huwa inachukua asilimia 80 ya chakula kilicho tayari kutumika duniani [...]

04/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yazindua mpango wa kusaidia jamii za wafugaji

Mifugo kaskazini mwa Kenya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeendesha shughuli ya kununua mifugo kutoka kwa jamii ya Kulan Kaskazini mwa Kenya ambapo wafugaji 1000 katika eneo hilo walifaidika na zoezi hili. IOM ina lengo la kuisaidia jamii hiyo kuepukana na athari za ukame katika eneo hilo na hatari inayokodolea macho mifugo wao. Jamii za wafugaji zimeathirika na [...]

04/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maelfu wahama makwao kutokana na mashambulizi kaskazini mwa Iraq

Nemba ya ICRC

Takriban wakimbizi 600 wamepokea usaidizi kutoka kwa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC kaskakazini mwa Iraq. Familia hizo ni miongoni mwa wale waliohama makwao kutokana na kuwepo mashambulizi ya mabomu ambayo yamekuwa yakiendelea katika eneo hilo tangu miiezi mitatu iliyopita. Familia hizo 98 kutoka vijiji 98 kutoka eneo la Kurdistan ziliwasili kwenye wilaya ya [...]

04/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yalaani maandamano nchini Bulgaria

Bulgaria

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea hisia zake kufuatia maandamano ya kupinga jamii ya Roma nchini Bulgaria baada ya kijana mmoja kuuawa alipogongwa na gari inayomilikiwa na mtu kutoka jamii hiyo.  Maandamano hayo yaliyoanza Septemba 23 yamesambaa kwenda miji mingine. Ofisi ya haki za binadamu ya UM inasema kuwa inajutia kifo [...]

04/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usalama mdogo, na barabara mbaya ni adha kwa wakimbizi Sudan Kusini

wakimbizi wa Kisomali wakosa matibabu

Wafanyikazi wa kutoa huduma za matababu kutoka shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwenye jimbo la Western Equatoria nchini Sudan Kusini wanaendelea kutoa huduma za matibabu kwa wakimbizi wa ndani ambao hawana njia yoyote ya kufika kwenye vituo vya afya. Makundi hayo yamekuwa yakisafiri mwendo mrefu kwenye barabara mbovu kuwafikia wakimbizi hao kwenye maeneo yaliyo [...]

04/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO kwenye jitihada za kuangamiza minyoo nchini Guinea

minyoo nchini Guinea

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa hata kama kumepigwa hatua kubwa ukosefu wa fedha umetatiza juhudi za kuuangamiza ugonjwa wa Guinea Worm nchini Guinea ugonjwa unaosabaisha ulemavu. Karibu visa 1800 viliripotiwa mwaka 2010 ikilinganishwa na visa milioni 3.5 wakati kulianza mpango wa kuuangamiza ugonjwa huo mwaka 1980. WHO inasema kuwa bado kuna visa vya [...]

04/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Oktoba 4 hadi 10 ni Wiki ya Anga Duniani

anga

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limetangaza Oktoba 4 hadi 10 kama Wiki ya Anga Duniani ambayo ni wiki ya kimataifa ya kuadhimishwa kila mwaka ya kusherehekea mchango wa Sayansi ya Anga na teknolojia ya anga kwa manufaa ya binadamu. Tarehe 4 mwezi Oktoba mwaka 1957 ndiko kulifanyika uzinduzi wa mtambo wa Satellite wa Sputnik 1 [...]

04/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano mapya yasababisha watu kuhama nchini Somalia

wakimbizi nchini Somalia

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasisi uliopo kufuatia ghasia zinazoendelea kusini mwa Somalia. Ghasia hizo mpya ni kati ya makundi hasimu suala ambalo limechangia hali iliyopo sasa ya njaa kuwa mbaya zaidi. Hata hivyo makundi yote yaliyojihami nchini Somalia yametakiwa kukoma kulenga maeneo waliko raia na kuhakikisha kuwa maisha ya [...]

04/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani shambulio la kujitoa muhanga Moghadishu

Shambulio la bomu Moghadishu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine Mahiga amelaani vikali shambulio la bomu la kujitoa muhanga hii leo kwenye ofisi za serikali ya mpito mjini Moghadishu ambalo limekatili maisha ya watu wengi na kujeruhi wengine. Balozi Mahiga amesema ameshtushwa na kusikitishwa sana kitendo hicho cha kikatili na kisichostahili, amesema mauaji ya raia [...]

04/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola trilioni 1.6 zitumikazo kila mwaka kwenye masuala ya kijeshi, zingeweza kuchochea maendeleo-UM

Sergio Duarte

Kiasi cha dola za kimarekani trilioni 1.6 kinachotumika kila mwaka kwa ajili ya kugharimia shughuli za kijeshi kingeweza kusaidia pakubwa kusukuma mbele maendeleo na kukabiliana na janga la umasiki. Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa anayehusika masuala ya uondoshwaji wa silaha ambaye ameongeza kuwa kuna haja sasa kwa mataifa makubwa [...]

04/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yajiaandaa kuwasaidia waathirika wa mafuriko Sindh

waathirika wa mafuriko Pakistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la linalohusika na uhamiajii linapanga kusambaza huduma za dharura ikiwemo maladhi na misaada mingine isiyo ya chakula kwa mamia ya wananchi wa Pakistan ambao makazi yao yameharibiwa vibaya na mafuriko. IOM imesema kuwa inamendea kupata msaada wa fedha wa kiasi cha dola za kimarekani milioni 1.5 kutoka kwa mfuko wa [...]

04/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kupambana na ubaguzi wa rangi

04/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Kuadhimisha siku ya kimataifa ya makazi duniani

03/10/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Uchumi wa kimataifa usiokumbatia uzembe unahitajika(GA 66)

Thomas Stelzer

Serikali kote duniani zimetakiwa kujitahidi kuchangia uchumi wa dunia ambao utaleta mustakhabali mzuri na sio kuwatunuku wasiojali. Wito huo umetolewa na Thomas Stelzer naibu katibu mkuu wa kamati ya pili inayohusika na masuala ya uchumi ambayo imeaanza kazi yake. Bwana Stelzer amesema kuwa kukumbuka mwaka 2008 alipoanza mtafaruku wa chakula, nishati, uchumi na kuanguka kwa [...]

03/10/2011 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wazindua shindano kwa ajili ya kumbukumbu ya biashara ya utumwa

kumbukumbu ya biashara ya utumwa

Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza umezindua shindano la kimataifa kwa ajili ya kuwakumbuka waathirika wa biashara ya utumwa. Shindo hilo linatazamiwa kuchukua fursa ya pekee kwa ajili ya kuwakumbusha wana ulimwengu namna mamilioni ya waafrika walivyoteseka kutokana na biashara hiyo ya utumwa. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni [...]

03/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka kuongezwa kwa vikosi vya kulinda amani Somalia

kikosi cha kulinda amani Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeutaka Umoja wa Afrika kuongeza idadi ya askari wa kulinda amani nchini Somalia ambako kunashuhudia mkwamo wa kisiasa pamoja na kukosekana kwa utulivu na usalama. Somalia kwa hivi sasa inapata msaada mkubwa wa ulinzi wa amani kutoka kwa muunganiko wa vikosi vya kimataifa AMISOM ambavyo hata hivyo vinashindwa [...]

03/10/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Juhudi zahitajika kulinda misitu mijini:FAO

miti yahitaji kulindwa

Sera bora na uwekezaji kwa lengo la kulinda na kudhibiti misitu na miti mijini zinahitajika, ili kuimarisha maisha ya mijini na kuboresha mazingira limesema shirika la chakula na kilimo FAO kwani miji inakuwa kwa kasi duniani. Ujumbe huo umetolewa na ushirikiano wa kimataifa wa misitu CPF na FAO wakati leo ikiadhimishwa siku ya makazi. George [...]

03/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watumiaji wa ardhi wasiojiweza lazima walindwe na sheria za kimataifa:UM

mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki ya chakula Oliver De Schutter

Haki za ardhi ni kikwazo cha kwanza katika kufikia lengo la usalama wa chakula, na bila kufikia muafaka wa kimataifa wa jinsi gani ardhi idhibitiwe basi haki za matumizi ya ardhi kwa watu wasiojiweza zitaendelea kuwekwa kando. Onyo hilo limetolewa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki ya chakula Oliver De Schutter, ikiwa [...]

03/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC kuchunguza mauaji yaliyotekelezwa Ivory Coast:Ocampo

mwendesha mashataka ICC Luis Moreno Ocampo

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC leo Jumatatu imempa idhini mwendesha mashitaka mkuu kuanzisha uchunguzi dhidi ya ghasia na mauaji yaliyofanyika Ivory Coast baada ya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka jana. Mwendesha mashitaka huyo Luis Moreno Ocampo aliomba kupewa haki mwezi Juni ya kufanya uchunguzi dhidi ya madai kwamba majeshi yaliyokuwa yanamuunga mkono Rais aliyetolewa [...]

03/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vita na ongezeko la majanga ni kikwazo cha suluhu ya wakimbizi:Guterres

mkuu wa UNHCR Antonio Guterres

Kuongezeka kwa migogoro na vita na kukumbwa na majanga ya asili kunafanya kuwa vigumu kupata suluhisho la watu milioni 43 duniani ambao ni wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wale wasio na utaifa limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Kwa mujibu wa mkuu wa shirika hilo Antonio Guterres, juhudi kubwa za jumuiya [...]

03/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji waliokwama Sebha Libya waanza safari kurejea nyumbani:IOM

wahamiaji kutoka Sebha, Libya

Zaidi ya wahamiaji wa Kiafrika 1200 ambao walikuwa wamekwama katika mji wa Sebha Kusini mwa Libya wameanza kuhamishwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na kupelekwa Chad. Wahamiaji hao wameanza kuondoka Sebha kwa msafara wa malori 15 Jumapili Oktoba pili na safari hiyo inatarajiwa kuchukua siku saba hadi kuwasili Chad. Kundi hilo ni sehemu [...]

03/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ziongeze juhudi kukabili mabadiliko ya hali ya hewa:Figueres

mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa

Serikali lazima zitambue haja ya kuongeza juhudi kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kujua kwamba majadiliano ya wiki hii Panama ni muhimu katika kuandaa mazingira ya kuelekea hatua nyingine ya kufikia malengo ya Durban amesema afisa wa Umoja wa Mataifa. Bi Christiana Figueres ambaye ni mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika [...]

03/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa kidingapopo waripotiwa Pakistan

kunyunyiza kemikali ili kumaliza mbu wanaosambaza kidingapopo

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa zaidi ya visa 12,000 vya ugonjwa wa kidingapopo vikiwemo vifo 125 vimeripotiwa nchini Pakistan hasa kwenye mkoa wa Punjab. Msemaji wa WHO Tarek Jasarevic anasema kuwa WHO inayasaidia makundi yaliyobuniwa na serikali ya Pakistan kutoa hamasisho kwa umma. Pia amesema kuwa WHO imekuwa ikisaidia katika utoaji wa mafunzo [...]

03/10/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza mafanikio ya mradi wa vijiji vya milenia

mradi wa vijiji vya milenia

Mafanikio ya mradi wa vijiji vya milenia ni mfano dhahiri kwamba kufikia malengo ya maendeleo ya milenia katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara sio tu inawezekana bali ni bayana. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi huo. Ban amesema [...]

03/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukuaji wa miji ni lazima uzingatie mabadiliko ya hali ya hewa:Migiro

siku ya makazi duniani

Kuadhimisha siku ya kimataifa ya makazi duniani ujumbe umetolewa kwamba ukuaji wa miji unapaswa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa. Siku hii ambayo imetengwa na Umoja wa Mataifa kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba kauli mbiu ya mwaka huu ni "miji na mabadiliko ya hali ya hewa" lengo likiwa kutathimini hali ya miji na [...]

03/10/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930