fadhili kwa ajili ya kufufua kilimo unasuasua:FAO
Wakati viongozi wa serikali mbalimbali duniani wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mkutano wa kimataifa wa kuomba fedha kusaidia Pembe ya Afrika, shirika la kilimo na chakula FAO limeonya kwamba juhudi za kuwafanya wakulima na wafugaji kuendesha shughuli zao ili kuzuia matatizo zaidi hazipati ufadhili wa kutosha.
Mikutano miwili ya dharura iliyoendeshwa na FAO mjini Roma tarehe 25 Julai na 18 Agosti imesaidia kuandaa mazingira ya mkutano muhimu wa Muungano wa Afrika hii leo, ukiitanabaisha dunia umuhimu wa kusaidia Pembe ya Afrika sio tu kwa chakula bali pia kusaidia uzalishaji na kukufua kilimo katika Pembe hiyo haraka iwezekanavyo.
(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)
