Nyumbani » 31/08/2011 Entries posted on “Agosti, 2011”

Vifo vya watoto wachanga vyapungua lakini bara la Afrika lasalia nyuma

infant

Utafiti Mpya kutoka kwenye shiririka la afya duniani WHO pamoja na washirika wake unaonyesha kuwa idadi ya watoto wanaokufa baada ya mara baada ya kuzaliwa imeungua kote duniani lakini hata hivyo maendeleo yanajikokota huku bara la Afrika likiachwa nyuma. Vifo vya watoto wanaozalia vilipungua kutoka watoto milioni 4.6 mwaka 1990 hadi watoto milioni 3.3 mwaka [...]

31/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya ICC yakataa ombi la Kenya la kutaka kutupiliwa mbali kesi

ICC KENYA

Mahakama ya kimataiga kuhusu uhalifu wa kivita ICC imetupilia mbali wito wa serikali ya Kenya wa kutaka kutupiliwa mbali kwa kesi zinazowakabili maafisa sita wa ngazi za juu serikalini zinaohusiana na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Sita hao ni pamoja na naibu waziri mkuu Uhuru Muigai Kenyatta, wabunge William Samoei Ruto na Henry Kiprono Kosgey , [...]

31/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulizi nchini Nigeria halitavuruga shughuli za UM: Migiro

Asha-Rose Migiro

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha–Rose Migiro amesema kuwa shambulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye mji mkuu wa Nigeria Abuja juma liilopita haliwezi kuuzuia Umoja wa Matifa katika kuendeleza shughuli zake nchini humo. Bi Migiro aliyatamka haya mara baada ya kurejea kutoka nchini humo alikokwenda kushuhudia [...]

31/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu 200,000 huenda wakakabiliwa na janga kwenye jimbo la Kordofan Kusini

Kordofan

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa huenda zaidi ya watu 200,000 walioathirika na mapigano ya hivi majuzi kwenye eneo la Kordofan Kusini wakabiliwa na hali mbaya ya utapiamlo na vifo baada ya serikali ya Sudan kuzuia mashirika ya kutoa misaada kusambaza misaada hiyo. Mratibu wa masuala ya kibindamu kwenye Umoja wa Matifa Bi Valerie Amos amesema [...]

31/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi kuhusu hatari inayokabili makao yake

Katibu Mkuu Ban

Umoja wa Mataifa hivi karibuni unatarajiwa kuendesha uchunguzi kuhusu hatari inayokabili makao yake sehemu mbali za ulimwengu kufuatia shambulizi lililotekelezwa kwenye makao ya Umoja wa Mataifa kwenye mji mkuu wa Nijeria Abuja ambapo watu 23 waliuawa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon aliliambia baraza la usalama ka Umoja wa Mataifa kuwa kuwa [...]

31/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban kuanza ziara ya kutembelea mataifa manne

mabadliko ya hali ya hewa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anajiandaa kwa ziara ya kuyambelea mataifa manne itakayomchukua kuanzia Australia hadi katika visiwa na Solomon ambako anatazamiwa kutilia uzito masuala ya mabadiliko ya tabia nchi. Katika ziara hiyo inayotazamiwa kuanza mwishoni mwa juma hili, Ban mbali ya kuzitembelea nchi hizo mbili, lakini pia atatembelea New Zealand,na Kiribati [...]

31/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa kibiashara kati ya Kosovo na Serbia

Farid Zarif akilieleza Baraza la usalama mgogoro wa Kosovo na Serbia

Mvutano uliosababishwa na mgogoro wa kibiashara kati ya Kosovo na Serbia unaendelea. Kaimu mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo, Farid Zarif amelieleza Baraza la Usalama kwenye  mkutano hii leo. Amesema Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyopelekwa mbele ya  Baraza la Usalama inaonyesha mawasaliliano mazuri kati ya Kosovo na Serbia wakati wa [...]

30/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wataka mataifa yote duniani kukomesha " Uhalifu wa kupindukia"

mkimbizi kutoka nchi yake kwa ajili ya vita

Umoja wa Mataifa umetoa zingatia la kuyataka mataifa yote duniani kuachana na kile ilichokiita " uhalifu wa kupindukia"kwa kuendesha mwenendo wa chini chini kuwaangamiza watu waliokimnbia uhamishoni kwa shabaya ya kupata hifadhi mpya katika nchi ngeni. Alice Kariuki  na taarifa kamili . Umoja huo wa mataifa umesema kuwa baadhi ya dola duniani zinaendesha fagio la [...]

30/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNHCR aenda kula Eid pembe ya Afrika

Antonio Guterres kusherehekea Eid kule pembe ya Afrika

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi António Guterres yuko katika ziara eneo la pembe ya Afrika kuungana na wananchi wa eneo hilo kusherekea sikukuu ya Eid El Fitr. Kamishna huyo amechukua fursa hiyo kukutana na wananchi walioko kwenye mazingira magumu kuonyesha uungaji mkono wake hasa katika kipindi hiki cha kumalizika [...]

30/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza kuu kujadili shambulizi la bomu kwenye majengo ya UM Abuja

mashambulizi ya bomu Abuja

Watu waliofariki dunia kwenye shambulizi la bomu lililolenga ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Abuja, Nigeria sasa wameongezeka na kufikia 23. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, idadi hiyo ya vifo inajumuisha watumishi 10 wa Umoja huo ambao ni raia wa Nigeria na mmoja raia wa Norway. Watu wengine nane waliouwawa walikuwa [...]

30/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahisani wengine wawasaidia waathirika wa mapigano ya kikabila Sudan Kusini:IOM

Sudan kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limefanikiwa kusambaza huduma mbalimbali za kijamii kwa mamia ya raia wa Sudan Kusini ambao waliondoka kwenye maskani zao na kwenda uhamishoni kutokana na hali mbaya ya usalama katika jimbo la Jonglei. Ikisaidiana na Jamhuri ya Sudan Kusini, shirika hilo la umoja wa mataifa limesambaza vifaa vinavyojumuisha [...]

30/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM washtushwa juu ya mauwaji ya kutisha yaliyofanyika Libya

Gadaffi-Libya

Umoja wa Mataifa umesemwa kuwa umeshtushwa juu ya ripoti zinazosema kuwepo kwa mauwaji ya mamia ya watu pamoja na vitendo vya ukandamizwaji wa haki za binadamu matukio yanayodaiwa kufanyika nchini Libya. Uhalifu huo kwa kiasi kikubwa unadaiwa kufanywa na vikosi vitiifu kwa utawala wa Gaddafi licha kwamba ripoti nyingine zinavitaja vikosi vya waasi kuwa ni [...]

30/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waanza kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu Libya

vyakula kutoka mashirika ya UM kusaidia walibya

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameanza kuweka zingatio la utoaji wa misaada ya dharura kwa mamia ya wananchi wa Libya ambao wanakabailiwa na uhaba wa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula. Tayari shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetuma tani kadhaa za chakula na misaada mingine ya kibinadamu ikiwemo madawa na nishati ya mafuta mjini Tripoli. [...]

30/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya kimataifa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya vyombo vya habari vya kijamii

30/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Wabolivia wenye asili ya Afrika bado wanajikuta wakiishi kando ya jamii

30/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Wahusika wa mashambulio ya bomu Abuja lazima wapelekwe mbele ya sheria: Migiro

Naibu Katibu Mkuu Bi. Asha Rose Migiro, Nigeria

Naibu Katibu Mkuu wa UM Bi Asha Rose Migiro amelaani vikali mashambulio yaliyolenga majengo ya Umoja wa Mataifa nchini Nigeria. Asha –Rose Migiro aliwasili Abuja mwishoni mwa wiki – pamoja na Gregory Starr, mkuu wa idara ya usalama ya Umoja wa Mataifa kujionea uharibifu uliosababishwa na tukio hilo ambako watu kadhaa walipoteza maisha na wengine [...]

29/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuelekea dunia yenye usalama mwema:UM

29/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UM walaani mashambulizi ya bomu kwenye eneo la UM nchini Nigeria

29/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UM waanza kuwapa chanjo mifugo huko Darfur

mifugo, Darfur

Umoja wa Mataifa umeanza utoaji chanjo katika maeneo kadhaa ya jimbo la Darfur kama shabaha ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali. Zaidi ya mifugo milioni moja inatazamiwa kufaidika na mpango huo ambao unashabaha ya kuwaepusha kuambukizwa na magonjwa ya msimu hasa kwenye msimu huu wa mvua. Shirika la mpango wa chakula na kilimo la Umoja wa [...]

29/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua ya Darfur kuwapa msamaha wafungwa yapongezwa na UNAMID

UNAMID yapongeza hatua ya Darfur kuwapa msamaha wafungwa

Muungano wa vikosi vya kulinda amani vya kimataifa katika jimbo la Darfur nchini Sudan vimetoa taarifa ya kuonyesha kuridhishwa kwao kufuatia mamlaka ya nchi hiyo kuwaruhusu masheik kadhaa waliokuwa wakipata hifadhi kwenye maskani ya vikosi hivyo wakihofia usalama wa maisha yao kurejea kwenye maskani zao. Masheikh hao wapatao 5 walilazimika kuomba hifadhi kwenye majengo ya [...]

29/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF kusambaza maji Tripoli

ukosefu wa maji Tripoli

  Shirika la kuhudumia watoto UNICEF leo linatazamiwa kutoa chumba za maji zinazofikia 90,000 mjini Tripoli ikiwa ni nyongeza ya chumba nyingine 90,000 zilizotolewa hapo kabla. Hatua hiyo inalenga kukabili mkwamo wa ukosekanaji wa maji ambao unaiandama maeneo mbalimbali ya Libya hasa mji mkuu wa Tripoli. Hadi sasa kiasi cha lita milioni 5 za maji [...]

29/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yawaokoa wahamiaji 850 waliokwama Tripoli

boti ya IOM inayowasafirisha wahamiaji kutoka Tripoli

Meli iliyopelekwa na shirika la kimataifa la wahamiaji IOM kwa ajili ya kuwakwamua wahamiaji waliokwama kwenye maeneo mbalimbali nchini Libya,imefanikiwa kuondoka katika mji mkuu Tripoli ikiwa na wahamiaji 850. Wengi walinusuriwa ni pamoja na raia wa Libya. Makundi mengine ni wanawake na watoto. Meli hiyo hivi inapiga kasi kuelekea katika mji wa Benghazi na inatazamiwa [...]

29/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kusambaa zaidi kwa ugonjwa wa mafua ya ndege:FAO

ndege waliohatarini kutokana na mafua ya ndege

Shirika la kimataifa la chakula na kilimo FAO limetahadharisha juu ya uwezekano wa kusambaa upya kwa ugonjwa wa mafua ya ndege kufuatia ripoti inayoonyesha kuzuka kwa ugonjwa huo katika maeneo ya bara la Asia. Imeonyesha wasiwasi wake ikisema kazi ya virusi vya ugonjwa huo vinaweza kuvuka mipaka kuanzia bara la asia hadi maeneo mengine na [...]

29/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya upigaji marukufu matumizi ya Nyuklia

siku ya upigaji marufuku matumizi ya Nyuklia

Leo ni siku ya kimataifa ya kukabiliana na majaribio ya mifumo ya kinyuklia. Siku ya leo ndiyo inayoadhimishwa kupitishwa kwa sheria ya kimataifa inayopiga marafuku matumizi ya mitambo ya nyuklia duniani kote. Tibor Toth ambaye ni Katibu Mkuu Mtendaji anayeindaa Kamishna juu ya azimio hilo la upigaji  marafuku  huo anaelezea umuhimu wa siku hii. (SAUTI YA [...]

29/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya wajadiliwa

katibu Mkuu Ban Ki-moon

Ban amejadili hali nchini Libya kupitia video na viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu, Shirika la Ushirikano wa Kiislamu, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya. Amewaambia waandishi wa habari kuwa wote walioshiriki katika majadiliano haya pamoja na serikali ya mpito wamesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika kuisaidia Libya kutekeleza mipango yake baada [...]

26/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umezindua kampeni kuonyesha mataifa shida ya kukosa uraia

26/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lajadili operesheni za kulinda amani

Balozi Hardeep Singh Puri (kulia)

  Watendaji wote wanaoshiriki katika oparesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa wanapaswa kutoa maoni yao na kusikilizwa wakati maamuzi yanafanyika juu ya mamlaka ya kulinda amani. Hii ni kulingana na taarifa ya Baraza ya Usalama iliyotolewa kwenye mkutano hii leo kujadili hali ya operasheni za kulinda amani. Taarifa hiyo inathibitisha kuwa chini ya [...]

26/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi kubwa ya wasomali yawasili Yemen

wakimbizi wa kisomali

Zaidi ya Wasomali 3700 wamewasili Yemen wakibebwa na mashua kupitia Ghuba ya Aden. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kwamba hilo linajitokeza wakati wakimbizi wa ndani wanaendelea kupungua ndani mwa Somalia yenyewe, na idadi ya wakimbizi wanaoingia Kenya na Ethiopia pia imepungua. Shirika hilo linasema kuwasili kwa Wasomali Yemen ni ushahidi [...]

26/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amekaribisha uchaguzi wa rais Cape Verde

Mkuu wa UM Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kurudiwa kwa uchaguzi wa rais katika nchi ya Cape Verde uliofanyika Jumapili iliyopita. Ban amempongeza Jorge Carlos Fonseca kwa ushindi wa uchaguzi huo, ambao waangalizi wa kimataifa wamesema ulifanyika kwa njia ya amani na uaminifu. Pia amewapongeza watu wa Cape Verde kwa kupiga kura kwa [...]

26/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kimbunga Irene chaanza kuleta madhara

kimbuga Irene chaanza kuleta madhara

Shirika la Kimataifa linalohusika na upimaji wa hali ya hewa, limeonya juu ya uwezekano wa kutokea maafa zaidi wakati kunapojiri kimbunga Irene, ambacho tayari kimesababisha vifo vya watu 2 nchini Haiti na kusababisha uharibifu wa nyumba na mali nyingine ikiwemo bara bara. Tayari watu 1,000 wameokolewa na kuwekwa kwenye vituo maalumu wakati kimbunga hicho kilipopiga [...]

26/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama, Katibu Mkuu Ban walaani mashambulio ya bomu Abuja

baraza laomboleza waathirika wa shambulio, Abuja

Umoja wa Mataifa umelaani vikali mashambulizi yaliyolenga majengo ya umoja wa mataifa  nchini Nigeria ambako watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Bomu hilo lilitengwa kwenye gari lililipukia jengo la umoja wa mataifa lililoko kwenye mji mkuu Abuja ambako kunapatikana ofisi kadhaa za mashirika ya umoja wa mataifa. Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mkuu wa Umoja [...]

26/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame kulizorotesha eneo la Pembe ya Afrika

ukame pembe ya Afrika

Pamoja na juhudi zinazochukuliwa na mashirika ya misaada ya kibanadamu yanayojaribu kukabiliana na hali ngumu inayojiri kwenye eneo la Pembe ya Afrika ambayo inaandamwa na ukame usiowahi kushuhudiwa, lakini hata hivyo hali inazidi kuzorota. Kwa mujibu wa maafisa wa shirika la utoaji misaada ya kibinadamu OCHA, eneo hilo linaandamwa na mkuanyiko wa matitizo kuanzia kuwepo [...]

26/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaendelea juhudi za kuwakwamua wahamiaji waliokwama Libya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limetuma boti yake ya pili nchini Libya kwa ajili ya kuwakwamua wahamiaji waliokwama kwenye eneo hilo kufuatia mapigano ambayo sasa yamefikia kwenye kitovu cha kuangusha utawala wa Gaddafi. Boti hiyo imeanza kuondoka toka katika mji wa Benghazi ulioko kaskazini mwa Libya na kuelekea katika mji mkuu Tripoli. Ndani yake [...]

26/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za kitabibu ndiye kipaumbele chetu cha kwanza Libya: UM

afisa wa UM Ian Martin

Utoaji wa huduma za kibinadamu kama madawa, ni kipaumbele cha kwanza kinachozingatiwa nchini Libya. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa hivi sasa kunaandaliwa mpango mkakati wa siku 30 ambao utashughulikia mahitajio ya eneo hilo. Afisa wa Umoja wa Mataifa Ian Martin ameuambia mkutano maalumu unaofanyika huko Uturuki kuwa, mashirika ya misaada ya kibinadamu yanafanya [...]

26/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahisani ni muhimu sana kwa mamilioni ya watu duniani:UM

Wafanyakazi wa hisani ni muhimu

Ijumaa ya tarehe 19 Agosti Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla waliungana kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahisani watu ambao mchango wao, kujitolea kwao na juhudi zao zimeokoa na zinaendelea kuokoa mamilioni ya watu katika maeneo yenye matatizo ya vita, njaa, majanga ya asili na kadhalika. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "watu kusaidia [...]

26/08/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuumaliza mgogoro baina ya Israel na Palestina kumechelea sana:UM

Lynn Pascoe

Kumaliza mgogoro baina ya Israel na Palestina na kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina kumechelewa sana. Hivyo ndivyo alivyosema mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Lynn Pascoe alipokuwa akitoa taarifa kwenye baraza la usalama kuhusu Mashariki ya Kati hii leo. Bwana Pascoe amesema kwamba Waisrael na Wapalestina bado wako njia panda kuhusu [...]

25/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ICC yakaribisha hatua ya Grenada kuwa mwanachama mpya wa mahakama hiyo

bendera ya Grenada

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imekaribisha hatua ya Grenada ambayo wiki hii imeridhia mkataba wa Roma unaotambua uwepo wa mahakama hiyo. Ikikaribisha hatua hiyo ICC imefanya tafriji maalumu mjini  Hague kama njia ya kupongeza uamuzi uliochukuliwa na Grenada kuridhia mkataba huo. Kama ishara ya kukubalika kuwa mwanachama, rais wa mahakama hiyo Jaji Sang-Hyun Song [...]

25/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP kuanza kusambaza msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

wakimbizi wa Sudan kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linajiandaa kuanza kusambaza msaada wa chakula kwa mamia ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wanakabiliwa na hali ngumu baada ya kusitishiwa misaada. WFP pamoja na washirika wake inatazamiwa kutumia ndege ili kudondosha misaada ya chakula kwa wahitajio hao ambao ustawi wao unazidi kuzorota. Familia zaidi ya 4,000 zilizoko [...]

25/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauwaji ya mwandishi wa Pakistan

vyombo vya mwandishi wa habari

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya elimu, sayansi, na utamaduni ambalo pia linawajibika na utetezi wa uhuru wa vyombo vya habari UNESCO limelaani vikali mauwaji ya mwandishi wa habari wa Pakistan aliyeuwawa kwa kupigwa risasi wakati akirejea nyumbani. Mwandishi huyo wa habari Munir Shakar alipigwa risasi na watu wasiojulikana mnano Agosti 14 wakati [...]

25/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Urithi wa kitamaduni kulindwa Libya wakati wa mpito:UNESCO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova amewataka watu wa Libya na pande zote zinazohusika na sanaa za kimataifa na biashara ya vitu vya kale kulinda urithi wa kitamaduni wa nchi hiyo. Bi Bokova amesema kupora, kuiba na kusafirisha kiharamu vitu vya kitamaduni ni ukiukaji wa [...]

25/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wasafirishwa kutoka Tripoli:IOM

boti ya shirika la IOM bandarini Tripoli

Wafanyakazi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wameanza kuwapakia wahamiaji wanaotaka kuondoka mjini Tripoli Libya ili kuwapeleka Benghazi. Boti ya shirika hilo iliyozuiliwa kuuingia bandarini tangu Jumanne wiki hii hatimaye imetia nanga asubuhi ya leo baada ya hali ya usalama kuimarika bandarini hapo. Wahamiaji hao wamekusanywa bandarini wakitokea maeneo mbalimbali ya Libya kama anavyofafanua [...]

25/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji maji una manufaa kwa afya ya binadamu, usalama wa chakula na ukuaji wa uchumi:UNEP

maji yana manufaa kwa afya ya binadamu

Matokeo ya utafiti yaliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa yanasema kuwekeza asilimia 0.16 ya pato la taifa kwenye sekta ya maji kutapunguza matatizo ya maji na kupunguza kwa nusu idadi ya watu wasio na fursa ya kupata maji safi ya kunywa na mahitaji muhimu ya usafi katika kipindi cha chini ya miaka minne. Utafiti huo [...]

25/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban achagiza malengo matatu ya nishati kubadili uchumi wa dunia

ziara ya Ban kwenye maabara ya nishati mbadala

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuna mambo matatu muhimu ya kuzingatia ambayo ni malengo ya nishati ili kubadili uchumi wa dunia na kufungua njia ya kuwa na mustakhabali bora, safi, salama na wenye matumaini. Akizungumza kwenye mjadala maalumu  kuhusu nishati endelevu kwa wote mjini Denver Colorado hapa Marekani, Ban amesema mambo [...]

25/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia imetakiwa kuonyesha mshikamano zaidi kwa serikali ya mpito ya Somalia:UM

Balozi Augustine Mahiga

Mkutano wa maalumu kuhusu Somalia uliohudhuriwa na kuwezeshwa na mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Somalia, Balozi Augustine Mahiga, Muungano wa Afrika na wadau wengine umekamilika mjini Moghadishu. Mkutano huo ambao umefanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Somalia umetoka na mapendekezo kadhaa ikiwemo pongezi kwa serikali ya mpito ya Somalia kuwa hatua iliyopiga kwa [...]

25/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

fadhili kwa ajili ya kufufua kilimo unasuasua:FAO

ufugaji nchini Ethiopia

Wakati viongozi wa serikali mbalimbali duniani wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mkutano wa kimataifa wa kuomba fedha kusaidia Pembe ya Afrika, shirika la kilimo na chakula FAO limeonya kwamba juhudi za kuwafanya wakulima na wafugaji kuendesha shughuli zao ili kuzuia matatizo zaidi hazipati ufadhili wa kutosha. Mikutano miwili ya dharura iliyoendeshwa na [...]

25/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 12 wasio na utaifa wahitaji msaada wa haraka:UNHCR

msichana Nina asiyekuwa na utaifa

Watu milioni 12 duniani kote wanaishi bila uraia wa nchi yoyote hali inayowaweka katika mazingira ya kunyonywa na kunyimwa haki za msingi za binadamu limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Ingawa kutokuwa na utaifa ni tatizo la dunia lakini linaathiri zaidi Kusini Mashariki mwa Asia, Asia ya Kati, Ulaya Mashariki na Mashariki [...]

25/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watoa wito kwa michango ya ukarimu kwa pembe Afrika

25/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga Irene yaikumba Haiti:UM

kimbuga irene nchini Haiti

Kimbunga Irene kimeleta mvua kubwa Kaskazini mwa Haiti na kusababisha mafuriko na kuharibu mashamba imesema ripoti rasmi ya Umoja wa Mataifa na kuongeza kwamba maeneo 160 ya kuhifadhi watu yamefunguliwa endapo watahitaji hifadhi na misaada mingine. Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imesema [...]

24/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza ya haki za binadamu yaamrisha uchunguzi

24/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UM iko tayari kusaidia serikali ya mpito:Libya

24/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Tuzo la ulinzi wa amani la Umoja wa Mataifa

Afisa UNPOL Shazadi Gulfam (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro na Mshauri wa Polisi wa Umoja wa Mataifa Ann-Marie Orler

Afisa wa polisi wa Pakistan ambaye amekabiliana na changamoto kadhaa wakati akitekeleza majukumu yake ya kipolisi ametunikiwa tuzo la Umoja wa Mataifa juu ya utunzaji amani. Polisi huyo Shahzadi Gulfam anaelezwa kuzishinda changamoto mbalimbali na wakati wote ametekeleza majukumu yake huku akiweka mbele shabaya ya kujituma na uchangamfu mkubwa. Kwa hivi sasa Gulfam anaongoza kikosi [...]

24/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkakati wa matumizi ya maji ya ziwa Victoria wazinduliwa Rwanda

ziwa la victoria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi UN HABITAT limezindua awamu ya pili huko Rwanda yenye shabaya ya kuijengea uwezo nchi za Afrika mashariki juu ya matumizi ya maji ya ziwa Victoria. Ikiwakusanya washirika na wadau kutoka kada zote, mpango huo unashabaha ya kutoa mafunzo na maelekezo ya kitaalamu kwa ajili ya kusaidia nchi [...]

24/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban aitaka Sudan Kusini kurejesha utulivu kwenye eneo kulikozuka mapigano ya kikabila

ramani ya sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa mwito kwa serikali ya Sudan Kusini kurejesha hali ya utulivu katika jimbo la Jonglei ambalo limeshuhudia watu zaidi ya 600 wakifariki dunia kufuatia machafuko ya kikabila yaliyozuka wiki iliyopita. Taarifa nyingine zisizo rasmi zimesema kuwa katika machafuko hayo ambayo yalihusisha watu wa kabila la Murle na [...]

24/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu wa UM ahutubia chuo kikuu cha Denver kuhusu maendeleo na nishati

Katibu Mkuu wa UM atoa hotuba kule Denver, Coloraro

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo yuko Denver Colorado hapa Marekani kutoa hotuba maalmu kwenye chuo kikuu cha Denver Josef Korbel kuhusu maendeleo na nishati . Akiwa huko amekutana na wakuu wa eneo hilo na kuchagiza matumizi ya vyanzo ya nishati mbadala, pia amepokea tuzo ya kimataifa kutoka katika chuo hicho kwa [...]

24/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maji ni muhimu kwa usalama wa chakula:FAO

maji ni muhimu kwa kilimo cha asili

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limesema maji ni muhimu sana katika kuhakikisha usalama wa chakula. Akizungumzia wiki ya maji mkurugenzi msaidizi wa mali asili wa FAO Alexander Meller amesema ni muhimu kutofautisha kilimo cha asili kinachotegemea mvua na kile cha umwagiliaji. Umwagiliaji unabadili kila kitu, unaongeza uzalishaji wakati wote bila kutegemea msimu wa [...]

24/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna viumbe millioni 8.7 duniani sasa:UNEP

viumbe duniani

Utafiti mpya uliofanywa na shirika la Umoja wa mataifa la mazingira UNEP kuhusu sensa ya viumbe duniani umebaini kuwa kuna vimbe milioni nane na laki saba vinavyoishi duniani hivi sasa. Utafiti huo ni wa kwanza kutolewa hasa kwa kutanabaisha takwimu. Utafiti huo uliofanywa na UNEP unasema viumbe milioni 6.5 viko nchi kavu na milioni 2.2 [...]

24/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikwazo vya Israel vinadumiza uchumi Palestina:UNCTAD

vikwazo-Gaza

Ukuaji wa uchumi katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa umeonyesha kuimarika kwa mwaka 2010, ingawa ukosefu wa ajira, umasikini na matatizo ya chakula vinaendelea kwa kiwango cha juu umesema mpango wa Umoja wa mataifa wa biashara na maendeleo UNCTAD. Mwaka jana uchumi umekuwa kwa asilimia 9.3 lakini ulichagizwa na msaada kutoka kwa wahisani kuliko uzalishaji katika [...]

24/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara sasa kufanyika kupitia simu ya mkononi Liberia:ITC

biashara Liberia kufanyika kupitia simu ya mkono

Kituo cha biashara cha kimataifa ITC kwa ushirikiano na Angie Brooks International ABIC leo wamezindua mradi nchini Liberia ambao utaruhusu wafanyabiashara kununua na kuuza bidhaa kupitia simu za mkononi. Mradi huo unaoitwa "biashara mkononi T@H umetangazwa na Rais wa Liberia Bi Ellen Johnson Sieleaf kwenye hafla maalumu iliyofanyika mjini Lofa ambako mawaziri mbalimbali pia wamehudhuria [...]

24/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo ya fedha yameifanya WFP kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi wa DRC

wakimbizi wa DRC

Upungufu wa fedha umelifanya shirika la mpango wa chakula duniani WFP kupunguza kwa nusu mgao wa chakula kwa maelfu ya wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walioko Rwanda kuanzia Septemba mosi mwaka huu. Kwa mujibu wa Abdoulaye Balde mwakilishi wa WFP nchini Rwanda uamuzi huo ni mgumu lakini shirika halina fedha za kutosha kugawa [...]

24/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unasimama bega kwa bega na AU kusaidia pembe ya Afrika:Migiro

Asha Rose Migiro

Mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kuomba msaada wa kukabiliana na matatizo yanayoikabili pembe ya Afrika hivi sasa utafanyika kesho Alhamisi mjini Addis Ababa Ethiopia. Lengo la mkutano huo ni kuonyesha mshikamano kwa waathirika wa ukame na njaa kwenye pembe ya Afrika, na Umoja wa Afrika umeziomba nchi wanachama kukusanya [...]

24/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kuomba msaada kwa ajili ya pembe ya Afrika kufanyika Addis Ababa

Asha Rose Migiro

Mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kuomba msaada wa kukabiliana na matatizo yanayoikabili pembe ya Afrika hivi sasa utafanyika kesho Alhamisi mjini Addis Ababa Ethiopia. Lengo la mkutano huo ni kuonyesha mshikamano kwa waathirika wa ukame na njaa kwenye pembe ya Afrika, na Umoja wa Afrika umeziomba nchi wanachama kukusanya [...]

24/08/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Madai ya askari wa UM kusaidia kutorosha madini huko DRC yaanza kuchunguzwa

kikosi cha askari cha MUNUSCO

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Congo vimeanza kushirikiana na mamlaka za nchi hiyo ili kuendesha uchunguzi kuhusiana na tuhumu za mfanyakazi mmoja wa vikosi hivyo kujihusisha na vitendo kutorosha madini kwa njia ya panya. Maafisa wa vikosi hivyo MUNUSCO wamesema kuwa mwajiri mmoja wa vikosi hivyo anadaiwa kuhusika kutorosha tani moja [...]

23/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kupambana na ukimwi zajikita kwenye mpaka na Msumbiji na Malawi

Ukimwi mpakani Msumbiji na Malawi

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wiki hii limezindua mfululizo wa vipindi vya radio vinavyojikiya na elimu ya kuzuia virusi vya HIV kwenye eneo la Nacala moja ya eneo muhimu la safari linalounganisha bandari ya Nacala Kaskazini mwa Msumbiji kuelekea Blantyre Malawi. Vipindi hivyo vya radio vilivyopewa jina "Mukwaha n'Ekumi" ikimaanisha safari salama vimeandaliwa na [...]

23/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yanajiandaa kwa kimbuga Irene, Haiti

kimbuga Irene

Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO limesema kimbunga Irene kimeshika kasi na kupanda hadi daraja la 2 na maeneo kitovu ya kimbunga hicho ni Jamhuri ya Dominican na Haiti, na baadaye leo kinatarajiwa kupiga visiwa vya Turks na Caicos na Kusini mwashariki mwa Bahamas. WMO imesema tayari mipango imeandaliwa na inafuatilia [...]

23/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM ataka tathimini baada ya Marekani kuhusika na ukiukaji wa haki

Umoja wa Mataifa

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ukatili dhidi ya wanawake, sababu zake na athari zake Rashida Manjoo ameitaka serikali ya Marekani kuzipitia upya sera zake zinazohusika na ukatili dhidi ya wanawake. Wito wake unafuatia maamuzi ya tume ya Marekani ya haki za binadamu kubaini kwamba serikali ya Marekani inawajibika na ukiukaji wa [...]

23/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi za kuokoa maisha zinaendelea pembe ya Afrika

shirika la UNHCR, nchini Ethiopia

Nchini Ethiopia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepeleka timu ya dharura kwenye eneo la Gode kilometa 250 Kaskazini mwa kambi ya wakimbizi ya Dollo Ado. Kwa ushirikiano na serikali ya Ethiopia, mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na NGO's, UNHCR inachukua hatua kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi wapya 18,000 walioingia [...]

23/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Historia ya utumwa yaweza kusaidia watu kujifunza utu:UNESCO

Bi Irina Bokova

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO leo amewataka watu kujifunza historia ya udhalilishaji ya biashara ya utumwa ili kubaini utu wao na kuongeza juhudi za kupambana na unyanyasaji na ubaguzi wa rangi. Bi Irina Bokova amesema kila mtu anapaswa kupewa uwezo wa kujifunza yaliyopita na kuyatafakari kama njia [...]

23/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yanayoendelea Tripoli ni kikwazo cha kusafirisha wahamiaji

wahamiaji wanaokimbia Tripoli, Libya

Hali bado ni tete kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli huku kukiarifiwa mapigano makali baina ya waasi na majeshi ya serikali. Leo mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Abdel Elah Al-Khatib na mshauri wa masuala ya Libya Ian Martin wanakutana mjini Doha Qatar na uongozi wa baraza la mpito la serikali ya Libya [...]

23/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu laitaka Syria kusitisha ghasia

baraza la haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa litapeleka tume ya kimataifa ya uchunguzi nchini Syria kuuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati wa kuwasaka waandamanaji wanaoipinga serikali . Wakati wa hitimisho la kikao maalum cha siku mbili kuhusu Syria baraza hilo limepitisha azimio ambalo linalaani vikali kuendelea kwa ukiukwaji wa haki za [...]

23/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 600 wauwawa katika mapigano ya kikabila Kusini mwa Sudan

mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu

Watu wapatao 600 wameripotiwa kuuwawa na kiasi kingine cha watu 700 kujeruhiwa kufuatia mapigano ya kikabila yaliyozuka huko Kusini mwa Sudan katika jimbo la Jonglei. Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ustawi wa Sudan UNMISS machafuko hayo yamezuka kuanzia alhamisi iliyopita. Jamii ya watu wa Murle na ile ya Lou-Nuer inazozana kuhusiana [...]

23/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yaingilia kati kunusuru afya za wakimbizi wa Somalia

wakimbizi wa Somalia

Wakati kukiripotiwa kuzidi kufumuka magonjwa yanayo waandama wakimbizi wanaokimbia nchini mwao Somalia na kuelekea katika nchi za jirani, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wahamiaji IOM, limetangaza kuanza kusambaza huduma za kitabibu kwa wakimbizi hao. Shirika hilo likishirikiana na washirika wake, limesema kuwa limelazimika kuingilia kati kusambaza huduma za kiafya ili kunusuru maisha ya [...]

23/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Brazil yatakiwa kuwalinda majaji wake, kufuatia kuuawa kwa jaji mmoja

ramani ya Brazil

Umoja wa Mataifa umeitaka Brazil kuhakikisha inatoa ulinzi wa kutosha kwa watendaji wake wa kwenye baraza la maamuzi ikiwemo majaji, mahakimu na maafisa wengine, kufuatia tukio la kuuliwa kwa jaji mmoja aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana. Jaji huyo Patrícia Lourival Acioli alipigwa risasi hadi kufa katika eneo karibu na nyumbani kwake huko Rio de Janeiro. [...]

22/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waafiki kukusanya fedha ili kulinda kupotea kwa tembo barani Afrika

tembo walio hatarini kutokana na uwindaji

Mkutano uliwajumuisha wataalamu mbalimbali umemalizika huko Geneva, na kuafikia kutengwa kwa fungu la fedha kwa ajili ya kufadhilia miradi ya kuvilinda viumbe vilivyopo hatarini kutoweka . Mkutano huo uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa umeazimia kutenga fungu maalumu ili kusaidia kuwalinda wanyama jamii ya tembo walioko barani afrika ambao wapo hatarini kuadimika kutokana na wimbi la [...]

22/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM, Quartet yashutumu mashambulizi ya Israel

washirika wa Quartet

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake wa kusaka amani katika eneo la mashariki ya kati wameshutumu vikali matukio ya mashambulizi yaliyotekelezwa kusini mwa Israel na imezitaka mamlaka husika kujiepusha na matukio ya jinsi hiyo. Vile vile Umoja wa Mataifa umelaani juu ya mwenendo wa matukio ya kigaidi yanayoendelea kujiri mara kwa mara kwenye eneo [...]

22/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uhusiano wa viumbe na mazingira ni muhimu kwa usalama wa chakula:UNEP

kilimo cha mazao mbalimbali

Kutambua mfumo bora wa mahuasiano ya viumbe na mazingira kwa ajili ya vyanzo vya maji na salama wa chakula kunaweza kusaidia kuzalisha zaidi chakula, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuleta faida kubwa za kiuchumi kwa jamii masikini. Hayo yamo kwenye ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira [...]

22/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Somalia akutana na vingozi mjini Moghadishu

Balozi Augustine Mahiga

  Ujumbe maalum ukiongozwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Agustine Mahiga leo Jumatatu umewasili mjini Moghadishu Somalia. Kwa mujibu wa duru za habari kutoka nchini humo ujumbe wa Umoja wa mataifa umekutana na viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia na kujadiliana kuhusu mipango ya kufanyika kwa mkutano unaoungwa mkono na [...]

22/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Boti ya IOM yawasili Tripoli kusafirisha wahamiaji waliokwama Libya

boti ya IOM itakayosafirisha wahamiaji waliokwama Libya

Boti ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM inaelekea mjini Tripoli Libya ili kuwasafirisha wahamiaji waliokwama mjini humo. Boti hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 300 imeondoka kwenye mji wa Mashariki wa Benghazi leo asubuhi baada ya kukamilisha kuwahamisha wahamiaji 124 siku ya Jumapili kutoka Misrata. Boti hiyo Tasucu itawasili Tripoli Jumanne na itaondoka kuelekea [...]

22/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imetoa wito wa usalama kwa raia wa kigeni Libya

raia wa kigeni nchini Libya

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ametoa wito wa kuhakikisha usalama kwa raia wa kigeni nchini Libya. Kamishina Antonio Gutetrres ametoa wito huo leo na kuziomba pande zote kwenye mgogoro wa Libya kuhakikisha kwamba maelfu ya raia wa kigeni waliokwama mjini Tripoli na maeneo mengine ambako mapigano yanaendelea kulindwa. [...]

22/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waasi wadhibiti mji mkuu wa Tripoli nchini Libya

Saif Al-Islam Qadhafi

Taarifa kutoka nchini Libya zinasema wapiganaji waasi wanaopinga utawala wa Rais Muammar Gaddafi hivi sasa wanaushikilia mji mkuu Tripoli baada ya majeshi ya serikali kusambaratika. Viongozi wa dunia wamekuwa wakitoa wito kwa Rais Gaddafi kuachia madaraka ili kunusuru maisha ya watu yanayoendelea kupotea kila siku. Wakati huohuo mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu [...]

22/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Operesheni za kijeshi dhidi ya raia zinaendelea Syria:UM

jeshi la Syria pamoja na waandamanaji

Uongozi wa Syria unaendelea kutumia nguvu za kijeshi kuwatawanya watu wanaoandamana kwa amani amesema kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay. Amesema watu takriban 40 wameuawa kati ya Alhamisi na Ijumaa iliyopita na mauaji hayo yametekelezwa na majeshi ya ulinzi na usalama ya Syria, siku moja tu baada ya Rais [...]

22/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM ni muhimu sana kwa kila jambo duniani:vijana

Mwezi huu mwaka wa kimataifa wa vijana umekamilika ambapo Umoja wa Mataifa kwa miezi 12 umekuwa ukipiga debe kuzitaka nchi wanachama kutoa nafasi kwa vijana kushiriki katika masuala muhimu yanayoisumbua dunia. Na kwa vijana wenyewe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mikutano nao na kuwachagiza kuwa wakati wao umewadia kutatua matatizo [...]

19/08/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani vikali shambulio la kujitoa muhanga msikitini Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga lililofanyika leo kwenye msikiti Kasjkazini Magharibi mwa Pakistan na kuuwa watu zaidi ya 40 na kujeruhi wengine zaidi ya 100. Duru za habari zinasema shambulio hilo limefanyika wakati wa swala ya Ijumaa kwenye msikiti wa kijiji cha Ghundi jimbo la Khybernchini [...]

19/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Shahidi muhimu juu ya mauwaji ya Yugoslavia akabidhiwa kwa mahakama ya kimataifa

Shefqet Kabashi

Shahidi muhimu katika mashtaka ya uhalifu wa kivita huko Yugoslavia hatimaye leo amekabidhiwa kwenye mahakama ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu huo. Shefqet Kabashi, ambaye ni afisa wa zamani wa jeshi la ukombozi la Kovoso KLA hapo nyuma alikataa kuleta ushahuidi wake dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Kosovo Ramush Haradinaj. Mahakama ya uhalifu wa kivita [...]

19/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lataka jitihada zaidi kuleta utengamao Jamhuri ya Afrika ya Kati

mwakilishi maalumu wa katibu mkuu Afrika ya kati, Abou Moussa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limetoa mwito likitaka kuchukuliwa na hatua za haraka ili kuleta hali ya utulivu katika nchi ya Jamhuri ya Kati ambayo inakabiliwa na mkwamo wa kisiasa. Baraza hilo la usalama limeitaka ofisi yake inayohusika na ustawi wa eneo hilo UNOCA kuangalia uwezekano kwa kuungana na mashirika mengine ili [...]

19/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maafisa wa serikali ya Syria wapatao 50 watuhumiwa kupalilia mauwaji

Navi Pillay

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloangazia haki za binadamu Bi Navi Pillay amesema kuwa jumla ya watu 50 wanatuhumiwa kuwa nyuma ya uendeshaji wa vitendo vya mauwaji ya raia nchini Syria. Bi Pillay ametoa kauli hiyo kwa kuzingatia ripoti ya waaangalizi iliyofuatilia hali jumla ya mambo nchini humo ambako serikali imeendelea kuyadhibiti na [...]

19/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP inawasaidia waathirika wa mafuriko Bangladesh

mafuriko Bangladesh

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linatoa msaada wa dharura wa chakula unaohitajika kwa watu 57,000 walioathirika na mafuriko Kusini mwa Bangladesh. Shirika hilo linasema maefu ya familia masikini zimeathirika na mafuriko hayo ambayo pia yamewaacha wengi wakiwa wamekwama kwenye nyumba zao bila chakula na malazi. Maeneo mengi ya wilaya ya Satkhira yamefunikwa na [...]

19/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya wahamiaji bado wanahitaji kuhamishwa Libya:IOM

wahamiaji wa kigeni mjini Tripoli, Libya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linafanya juhudi za kuendelea kuwahamisha maelfu ya wahamiaji wanaohitaji msaada kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli. Shirika hilo linasema limepokea maombi mengi ya kuwahamisha wahamiaji wa kigeni mjini Tripoli ambao wako katika hali mbaya na sasa wanataka kuondoka. Idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Misri bado wako Tripoli na Magharibi [...]

19/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yaonya juu ya kutoweka na kutekwa kwa watu Pakistan

familia za waliotekwa nchini Pakistan

Ofisi ya Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imesema tangu mwaka 2007 imekuwa ikipokea ripoti za watu kutekwa, kutoweka, na mauaji nchini Pakistan. Kwa mujibu wa ofisi hiyo wiki moja iliyopita kumekuwa na taarifa za kuawa kwa waandishi habari na wengine kutekwa Balochista na Kaskazini mwa Waziristan. Takwimu zinaonyesha kwamba 2010 [...]

19/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imezindua wavuti maalumu kwa ajili ya pembe ya Afrika

msaada wa UNHCR kwenye pembe ya Afrika

Leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limezindua wavuti mpya ili kutoa taarifa za kila mara za shirika hilo na washirika wake wa kikazi kuhusu wakimbizi na wanaosambaratishwa na hali ya dharura ya njaa kwenye pembe ya Afrika. Wavuti hiyo data.nhcr.org/horn-of-africa/ unatoa taarifa za kina kwa washirika wote wa UNHCR ambao wanatoa [...]

19/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi zinaendelea kuokoa maisha ya mamilioni pembe ya Afrika

wakimbizi wakisomali walioko kambi ya Dadaab

Ugawaji wa misaada katika pembe ya Afrika inayoghubikwa na njaa kali unaendelea ingawa ukosefu wa fedha na milipuko ya magonjwa vinatia dosari juhudi hizo kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa pande wake linaimarisha lishe kusaidia [...]

19/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa ya Uhisani UM wasisitiza umuhimu wa watu kuwasaidia watu

'watu kuwasaidia watu'

Leo Umoja wa Mataifa unaadhimisha mwaka wa tatu tangu kuanzishwa siku ya kimataifa ya wahisani, huku hafla zikifanyika duniani kote. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "watu kusaidia watu", siku hii inaadhimishwa wakati mashirika ya misaada yakiongeza juhudi kuwasaidia mamilioni ya watu walio katika hali mbaya kwenye pembe ya Afrika na kwingineko, na wakati ambapo [...]

19/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu sita wauawa kwenye shambulio la kigaidi Kusini mwa Israel

basi lililoshambuliwa kusini mwa Israel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika leo Kusini mwa Israel. Kwa mujibu wa duru za habari katika eneo hilo mtu mwenye silaha amelifyatulia risasi basi lililokuwa likisafiri karibu na mpaka baina ya Israel na Misri na kuuwa watu sita na kujeruhi wengine wengi. Magari mengine mawili yaliyokuwa [...]

18/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatekeleza mradi wa usambazaji kadi kwa wakimbizi walioko India

UNHCR

UNHCR Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR limeanza kutekeleza mradi wa usambazaji wa kadi maalumu kwa wakimbizi wa Afghanistan walioko India ikiwa ni moja ya juhudi zake za kuboresha ustawi wa wakimbizi hao. Tangu kuanza hatua hiyo mwezi July mwaka huu, hadi sasa jumla ya wakimbizi 1,500 wamepatiwa kadi hizo ambazo pia zinawafaidi [...]

18/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wataka kuharakisha utoaji misaada kwa wananchi wa Pembe ya Afrika

Bi Valeria Amos akiwa nchini Somalia

Umoja wa Mataifa umetaka kuongeza kasi ya usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo la pembe ya Afrika ambalo linaandamwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula hali iliyosababisha mamia ya watu kuishi kwenye hali ya taabu. Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kibinadamu OCHA, Bi Valerie Amos ameonya kwa [...]

18/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zingatio la usalama na usafi kwa viwanda vya nguo vya Cambodia bado liko chini-Ripoti ya UM

wafanyakazi wa viwanda vya nguo Cambodia

wafanyakazi wa viwanda vya nguo Cambodia Ripoti moja iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imetaja kuwepo kwa baadhi ya vitendo vinavyohatarisha afya za watu kwenye viwanda vya uzalishaji nguo nchini Cambodia. Ripoti hiyo ambayo hata hivyo imeridhika na namna viwanda hivyo vinavyopiga hatua kuzingatia viwango vya kimataifa, imesema kuwa kwenye baadhi ya maeneo bado hali ya [...]

18/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM wa masuala ya haki za binadamu kuzuru Myanmar

ramani myanmar

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Tomas Ojea Quintana atazuru nchi hiyo kwa mpango maalumu. Quintana atatembelea maeneo ya Yangon na Naypyitaw kuanzia Agosti 21 hadi 25 kwa mwaliko maalum wa serikali. Bwana Quintana amesema ziara hii itafanyika katika mazingira tofauti ya kisiasa kwani sasa kuna serikali mpya [...]

18/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka hatua zichukuliwe kwa waliotekeleza shambulizi la kigaidi Iraq

Balozi wa India Hardeep Singh Puri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyokatili maisha ya watu wengi nchini Iraq na kujeruhi wengine mapema wiki hii na kusisitiza kwamba wahusika lazima wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Akisisitiza kuhusu hilo jambo balozi wa India kwenye Umoja wa Mataifa ambaye ndiye Rais wa wa baraza kwa mwezi [...]

18/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi ya anga yanayoendelea yanauwa raia:Coomaraswamy

Bi Radhika Coomaraswamy

Mashambulizi ya ndege na watu wasiojulikana lazima yaepukwe kwani yanaua raia hususani wanawake na watoto, ameonya afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ambaye ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kwa ajili ya watoto kwenye maeneo ya vita ameyataka majeshi yote ya kimataifa kuongeza juhudi zake kuhakikisha kwamba mauaji ya raia yanakoma na [...]

18/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aendelea kumuasa Rais Assad kuhusu machafuko Syria

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon azungumza na Rais Assad wa Syria

Wakati huohuo katika mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Bashar Al-assad wa Syria hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon ameelezea hofu yake kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya raia nchini humo. Ban amesema vitendo vya ukiukwaji vinavyofanywa na majeshi ya [...]

18/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yachapisha ripoti ya uchunguzi kuhusu Syria

waandamanaji wa Syria

Ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo Alhamisi imechapisha ripoti ya tume maalumu ya uchunguzi iliyokwenda Syria. Tume hiyo iliundwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa wakati wa kikao maalum kuhusu Syria April 29 ili kuchunguza madai yote ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa za [...]

18/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM utaendelea kusaidia Somalia kusaka amani ya kudumu:Mahiga

Balozi Augustine Mahiga nchini Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amewaambia wajumbe wa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Somalia kuhakikisha inapata amani ya kudumu. Mahiga amesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kisiasa kwa ajili ya Somalia [...]

18/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO imeanza mkutano Roma kujadili hali ya njaa pembe ya Afrika

mkutano wa FAO mjini Roma

Mkutano wa dharura wenye lengo la kuchukua hatua za kimataifa kukabiliana na hali mbaya ya njaa kwenye pembe ya Afrika umeanza leo mjini Roma Italia. Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la chakula na kilimo FAO umewaleta pamoja mawaziri wa kilimo kutoka nchi zote 191 wanachama wa FAO, maafisa wa mashirika ya kiuchumi ya kikanda, Muungano [...]

18/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

"Nitakuwa pale ninapohitajika": asema mfanyakazi wa UM

18/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

"Nitakuwa pale ninapohitajika": wasema wafanyakazi wa UM katika maeneo wanayotoa huduma:

Dr Omar saleh amtibu mgonjwa Somalia

Dr wa Kimisri nchini Somalia Domar Saleh alikuwa anaishi maisha ya amani na ya kawaida kama mtaalamu wa upasuaji na mkufunzi wa chuo kikuu nchini Misri wakati alipopokea simu kutoka shirika la afya duniani WHO na kuambiwa madaktari wanahitajika haraka nchini Somalia, na hakufikiria mara mbili. Dr Saleh leo wakati Umoja wa Mataifa ukijiandaa na [...]

17/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya uholanzi yaachilia euoro milioni 100 za Libya

wanawake wa Libya

Serikali ya Uholanzi imeamua kuachilia baadhi ya fedha za Libya inazozizuilia na kuzitoa kwa shirika la afya duniani WHO. WHO imesema itapokea kiasi cha Euro milioni 100 kununulia madawa kwa ajili ya watu wa Libya wanaoteseka na machafuko yanayoendelea nchini mwao, na msaada huo utakwenda kwa pande zote serikalini na maeneo yanayodhibitiwa na waasi. Shirika [...]

17/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Athari za kilele za binadamu kwa viumbe wa majini kujadiliwa:UM

viumbe wa majini

Kelele zinazosababishwa na shughuli za binadamu zimeelezewa huenda zinaathiri maisha ya viumbe vya majini pengine kwa kupunguza uwezo wao wa kutafuta chakula, kupata wenzi au kukwepa maadui. Kutokana na hali hiyo Umoja wa Mataifa unafanya mkutano ili kuzindua muongo wa uchunguzi wa matatizo na athari hizo. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la [...]

17/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO kufanya mkutano kuthathimini hali katika pembe ya Africa

ramani ya pembe ya Afrika

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limendaa mkutano wa nchi wanachama, wahisani na wada wengine wa maendeleo kwa lengo la kuimarisha hatua za kimataifa za kukabiliana na hali mbaya ya njaa kwenye pembe ya Afrika. Mkutano huo utakaoanza Alhamisi Agosti 18 utaangalia pakubwa matatizo  ya mahitaji na mapungufu kwenye kadhia hiyo [...]

17/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UN-HABITAT yazawadia vikundi vya vijana 59

un habitat logo

Ikiingia mwaka wake wa 3 tangu kuanza kutoa tuzo zinazochochea ukuaji wa kiustawi katika maeneo ya mijini, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi UN-HABITAT limevizawadia vikundi kadhaa ambavyo vimepiga hatua kwenye uboreshaji makazi. Vikundi hivyo 59 ambavyo vinaundwa na vijana vinatajwa kupiga hatua kwenye endelezaji wa miradi inayochochea makazi bora na utengamano wa [...]

17/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mpango wa Israel kujenga nyumba za makazi ni batili:UM

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon katika mkutano wa pamoja na washirika wa quartet

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wanaozingatia hali ya mambo katika eneo la mashariki ya kati, umelaani vikali hatua ya Israel iliyoweka shabaya ya kuendesha ujenzi wa makazi katika eneo la Gaza. Serikali ya Israel imetangaza kusudia lake la kufanya ujenzi wa makazi kwenye eneo la ukingo wa Gaza, kitendo ambacho kinapingwa vikali na Umoja [...]

17/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uwindaji haramu wa tembo na meno yake unazidi kushamiri

Uwindaji wa tembo na meno yane

Ripoti moja iliyotolewa na wakfu wa umoja wa mataifa unaojihusisha na viumbe vilivyopo hatarini kupotea, imesema kuwa vitendo uwindaji haramu wa tembo na meno yake vinazidi kuongezeka. Ripoti hiyo mpya ambayo imeangazia kwa mapana yake suala hilo la uwindaji haramu inaonyesha ongezeko hilo ni la kasi lililoanza kumea mizizi tangu mwaka 2002. Eneo la afrika [...]

17/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ivory Coast kuchukua hatua zaidi kuelekea utawala wa sheria:UM

Gereza mjini Abidjan, Ivory Coast

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI wameisaidia nchi hiyo kukarabati gereza kubwa mjini Abidjan baada ya kusalia tupu kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu hivi karibuni. Ukarabati huo ni katika juhudi za kuisaidia Ivory Coast kurejesha utawala wa sheria nchini humo. Kwa mujibu wa afisa wa UNOCI Francoise Simard hatua [...]

17/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muongozo mpya wa UM unalengo la kuimarisha msaada wa kisaokolojia kwa waathirika wa majanga

muongozo wa huduma za kwanza

Shirika la afya duniani WHO na washirika wake wamezindua kitabu cha muongozo mpya kuwasaidia wafanyakazi katika maeneo mbalimbali kutoa msaada muhimu wa kisaikolojia kwa watu walioathirika na majanga na hali za dharura. Kwa mujibu wa WHO katika miaka mitano iliyopita athari za kisaikolojia zilizosababishwa na tsunami, matetemeko ya ardhi, ukame na vita zimedhihirisha kuwa ni [...]

17/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya bado inakabiliwa na changamoto katika kutokomeza umaskini ambao ni chachu ya ubaguzi

bendera ya Kenya

Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kutokomeza ubaguzi wa rangi imehitimisha kutathimini ripoti ya serikali ya Kenya ya utekelezaji wa mkataba wa kimataifa kuhusu utokomezaji wa mifumo yote ya ubaguzi wa rangi. Ripoti ya Kenya imewasilishwa mbele ya kamati hiyo na waziri wa sheria na katiba wa Kenya bwana Mutula Kilonzo ambaye amesema tangu [...]

17/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umeondoa wafanyakazi wake wasio wa lazima nchini Syria

Waandamanaji wa Syria

Umoja wa Mataifa leo umeondoa baadhi ya wafanyakazi wake wasio wa lazima walioko nchini Syria ambako Rais Bashar al-Assad anaingia katika mwezi wa tano wa maandamano ya kupinga utawala wake. Kauli ya kuondolewa kwa wafanyakazi hao imearifiwa na mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Michael Williams ambaye katika taarifa yake amesema wafanyakazi 26 [...]

17/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama maalumu ya Lebanon imechapisha mashitaka kamili kuhusu mauaji ya Rafiq Hariri

mauaji ya Rafiq Hariri

Mwendesha mashitaka katika mahakama maalumu ya Lebanon inayoshughulikia kesi ya mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Rafiq Hariri bwana Daniel A. Bellemare amekaribisha amri ya hivi karibuni ya jaji wa mahakama hiyo ya kuchapisha mashitaka kamili. Mwendesha mashitaka huyo amesema amri hatimaye itatanabaisha umma na waathirika wa maaji ya Hariri madai kamili [...]

17/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Egypt: Uandishi wa historia

17/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Kuna uwezekano uhalifu wa kivita umefanyika kusini mwa Kordofan: UM

16/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wengi waishio Libya hawana huduma muhimu-IOM

Wahamiaji kwenye kambi ya Al-Kufrah ilioko Libya

Kundi kubwa la wahamiaji wanaishi huko Libya wanaendelea kusota bila huduma muhimu ikiwemo maji, nishati ya umeme na usalama wa hali za afya.Kulingana na tathmini iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, wahamiaji hao ambao wapo kwenye kambi iliyoko kwenye mji wa Al-Kufrah ulioko Kusin mashariki mwa Libya, wapo kwenye wakati [...]

16/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yatuma wataalamu wake Angola kuchunguza ugonjwa wa ajabu

wagonjwa wapokea huduma kwenye hospitali - Angola

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetuma timu ya watalaamu wake nchini Angola kwa ajili ya kubaini ugonjwa mpya wa ajabu uliozuka nchini humo na kusababisha hali ya taharuki kwa mamia ya wanafunzi. Ugonjwa huo umearifiwa kuwakumba wanafunzi katika mji mkuu wa Luanda na maeneo mengine ya jirani. Taarifa zinasema kuwa wanafunzi waliokumbwa na ugonjwa huo [...]

16/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wengi warejea Sudan Kusini-UM

bendera ya Sudan kusini yapepea kwenye ofisi kuu ya Umoja wa Mataifa

Zaidi ya raia 330,000 waliokuwa wakiishi nchini Sudan wamerejea Sudan Kusini katika kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba mwaka jana. Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya usamaria mwema, wengi wa raia hao wamerejea kwa usafiri wa mabasi, treni na ule wa majini wakiwa wameambatana na mafurushi yao. Sudan Kusini ilijipatia [...]

16/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yahofia kubomolewa kwa jengo la taasisi ya amani Azerbaijan

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea hofu yake juu ya uharibifu uliofanywa dhidi ya jengo la taasisi ya amani na demokrasia mjini Baku Azerbaijan Agosti 11. Uharibifu huo umehusisha ofisi zingine mbili zisizo za kiserikali ili ya kampeni ya kupinga mabomu ya kutegwa ardhini na kituo cha wanawake, ambacho kilikwa kituo [...]

16/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makampuni binafsi yanawajibu wa kuwalinda wafanyakazi wake wa kigeni Iraq:IOM

mfanyikazi wa kigeni nchini Iraq

Wakati shirika la kimataifa la uhamiaji IOM likitoa msaada kwa kundi la wafanyakazi 35 wa kutoka Ukraine na Bulgaria waliotelekezwa na waajiri wao nchini Iraq, IOM imetoa wito kwa makampuni binafsi kutekeleza wajibu wao wa kuwahudumia wafanyakazi wao na kufuata sheria za kitaifa za uhamiaji, za kazi na haki za binadamu. Wito huo umekuja wakati [...]

16/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufadhili wa vita dhidi ya ukimwi umepungua 2010:UNAIDS

shirika la umoja wa mataifa kupambana na ukimwi UNAIDS

Msaada wa fedha kutoka nchi wahisani kwa ajili ya vita dhidi ya ukimwi kwenye nchi za kipato cha chini na cha wastani umepungua kwa asilimia 10 mwaka 2010 ikilinganishwa na miaka mingine . Takwimu hizo zimetokana na tathimini iliyofanywa na mfuko wa kimataifa wa Kaiser kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana [...]

16/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamia ya watu wapya wawasili Italia kutoka Libya na Tunisia

Chombo kilichowabeba watu waliowasiri Italia

Watu takribani 2000 wamewasili kwenye kisiwa cha Lampedusa nchini Italia wakitokea Libya na Tunisia limesema shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Watu 1800 kati yao wanasemekana kutoka eneo la Janzor kilometa 12 magharibi mwa mji mkuu wa Libya Tripoli ambako walisubiri kwa zaidi ya wiki moja hali ya bahari itulie kabla ya kuanza safari. Miongoni mwa [...]

16/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID na wahisani wengine wahitimisha ziara ya wiki moja Jebel Mara

Walinda amani wa UNAMID

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na ya kimataifa ikiwemo OCHA, UNICEF, UNHCR, WHO na baraza la wakimbizi la Denmark DRC wamehitimisha operesheni maalumu ya wiki moja kwenye eneo la Magharibi la Jebel Marra. Eneo hilo [...]

16/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP imelaani taarifa ya wizi wa chakula cha msaada na inafanya uchunguzi

magunia ya chakula cha msaada cha WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limelaani vikali hatua zozote za kuiba chakula cha msaada kwa ajili ya mamilioni ya Wasomali wanaokabiliwa na njaa. Shirika hilo limesema linachunguza madai hayo ya wizi unaodaiwa kufanyika mjini Moghadishu. WFP inasema nia yake ni kuhakikisha chakula cha msaada kinawafikia walengwa lakini haliwezi kufuta uwezekano wa wizi wa [...]

16/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Surua na utapiamlo unauwa watoto wakimbizi wa kisomali Ethiopia

Watoto wa kisomali wanaougua kutokana na surua na utapiamlo

Mamia ya watoto wa Kisomali wamekufa katika miezi miwili iliyopita kutokana na mchanganyiko wa mlipko wa surua na utapiamlo uliokithiri, kwenye kambi ya wakimbizi wa Kisomali iliyoko Ethiopia limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Shirika hilo limesema takribani watoto 10 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanakufa kila siku kwenye [...]

16/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi kuongoza wanajeshi kulinda amani Somalia

Wanajeshi wa AMISOM

Rais wa Burundi Pierre Nkrunziza amesema nchi yake itaongeza idadi ya vikosi vyake vinavyolinda amani nchini Somalia chini ya mwamvuli wa vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM. Tamko la Rais Nkurunziza limekja baada ya ziara ya Rais Sheikh Shariff Sheikh ahmed wa Somalia mjini Bujumbura na kutanabaisha umuhimu wa vikosi hivyo vya kulinda amani kongezwa. [...]

15/08/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa OCHA ataka msaada uongezwe Somalia

Valarie Amos

Mratibu mkuu wa masuala ya kibinadamu na ya dharura wa Umoja wa Mataifa OCHA Valarie Amos ametoa wito wa kongeza msaada zaidi kwa ajili ya mamilioni ya Wasomali wanaokabiliwa na njaa. Bi Amos ambaye amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Somalia na Kenya amesema bado Wasomali wanakimbilia nchi jirani ya Kenya, watoto wanakabiliwa na utapia [...]

15/08/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani vikali mashambulizi ya mabomu Iraq

Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mlolongo wa mashambulizi ya mabomu katika miji kadhaa nchini Iraq yaliyofanywa hii leo kuuwa watu zaidi ya 70 na kujeruhi wengine wengi. Ban amesema hivyo ni vitendo vya kinyama hasa kwa mashambulizi haya ktokea wakati wa mwezi mtukuf wa Ramadhan. Katibu Mkuu wamewataka watu wa [...]

15/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa ya vijana

15/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Shughuli za utoaji misaada zarejea tena Gaza

Robert serry afisa wa Umoja wa Mataifa

Shughuli za utaoji wa misaada ya kibinadamu zimerejea upya katika eneo la ukanda wa Gaza, na tayari afisa wa Umoja wa Mataifa amekaribisha hatua hiyo akisema kuwa sasa hatua hiyo ni nukta muhimu hasa panapohusika na ustawi wa jamii. Kulingana na duru kwenye eneo hilo, shirika la kimataifa lisilolo la serikali linalojihusisha na misaada ya [...]

15/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Fuatilizieni masuala ya dunia-Ban awaasa Wakorea

Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa ziarani Korea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametembelea eneo la nyumbani kwake huko Korea ya Kusini na kuwatolea mwito wakaazi wa eneo hilo juu ya kujishughulisha na masuala ya dunia. Akitembelea eneo lake la nyumbani mwishoni mwa wiki, Ban alisema kuwa ni muhimu kwa wananchi wakatambua jinsi inavyofaa kwa wao kuendelea kufuatilia masuala ya [...]

15/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Eneo la Somalia lililokumbwa na njaa lina mahitaji makubwa

Wakimbizi wakisomali

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya kiutu ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya utoaji misaada ili kuokoa maisha ya mamia ya watu wanaosota kwa njaa huko Somalia. Mamia ya watu ambao hawana jimudu kimaisha wanalazimika kukatiza mipaka na kuingia nchini Kenya kila kukicha na kuifanya kambi ya Dadaab inayohifadhi wakimbizi [...]

15/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Majeshi ya Syria yashambulia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina Latakia

waandamanaji Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeelezea hofu yake juu ya taarifa za majeshi ya serikali ya Syria kufanya mashambulizi kwenye kambi ya wakimbizi kwenye mji wa Kaskazini wa Latakia. Kwa Mujibu wa msemaji wa UNRWA Chris Gunness mawasiliano mabovu yanafanya kuwa vigumu kuthibitisha idadi kamili ya waliokufa au [...]

15/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi kuongeza vikosi kulinda amani Somalia

Askari wa AMISOM katika soko la Baraka ,mjini Mogadishu

Serikali ya Burundi imekubali kutuma vikosi vya ziada nchini Somalia kufuatia wito wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kutaka idadi ya vikosi hivyo viongezwe baada ya wanamgambo wa Al Shabab kuondoka Mogadishu. Hayo yamethibitishwa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika mazungumzo na Rais wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed aliyefanya ziara nchini [...]

15/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjadala kufanyika kuokoa maisha ya viumbe vilivyo hatarini :UM

Kuokoa pembe za ndovu na vifaru kutoka kwa maharamia na wafanya biashara haramu ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa kwenye mkutano ulioandaliwa na mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kulinda viumbe vilivyo katika hatari ya kutoweka CITES. Nchi 175 duniani zimetia saini mkataba huo. CITES hukutana kila baada ya miaka mitatu kujadili mapendekezo ya biashara ya [...]

15/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wapitishwa kulinda bahari ya Caspian kutokana na mafuta:UNEP

Bahari ya Caspian

Nchi tano zinazopakana na bahari ya Caspian zimekuabaliana kuimarisha hatua mpya za pamoja za kikanda za kukabiliana na kuvuja kwa mafuta na kuboresha njia za kuangalia vyanzo vya uchaguzi wa mazingira miongoni mwa nchi hizo na mipaka yake. Muafaka huo ulipitishwa wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa wawakilishi wa serikali za Azerbaijan, Iran, [...]

15/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa OCHA ahitimisha ziara nchini Kenya na Somalia

wakimbizi wa kisomali katika kambi ya Dadaab

  Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa OCHA Bi. Valarie Amos amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Kenya na Somalia.Jumapili ambayo ilikwa siku ya mwisho ya ziara yake Bi. Amos alizuru kambi kubwa kabisa ya wakimbizi ya Dadaab Kaskazini mwa Kenya inayohifadhi wakimbizi zaidi ya 400,000 na 70,000 [...]

15/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jeshi la Sudan na waasi washutumiwa kwa uhalifu wa vita Kordofan

Jimbo la Sudan la Kordofan kusini

Ripoti iliyotolewa leo na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba ikithibitika, ukiukwaji wa sheria za kimataifa za uhalifu na sheria za kimataifa za haki za binadamu unaodiwa kufanywa kwenye jimbo la Sudan la Kordofan Kusini mwezi Juni mwaka huu huenda kawa ni uuhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita. [...]

15/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huu ni wakati wenu vijana kutatua matatizo ya dunia:M

youth year

Ijumaa hii Agosti 12 Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla wameadhimisha siku ya kimataifa ya vijana kwa kauli mbiu "Badili dunia yetu" wito mahsusi kuwachagiza vijana kjitoa kimasomaso kushiriki masuala yahusyo maendeleo ya jamii zao. Ikiwa pia ni siku ya mwisho wa mwaka wa Umoja wa Mataifa wa vijana Katibu Mkuu wa Umoja wa [...]

12/08/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Afghanistan, Iraq walioko Iran wapatiwa bima ya afya

Mkimbizi wa Afghan apokea huduma ya afya

Mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa unatazamiwa kuwafaidia jumla ya wakimbizi milioni moja kutoka nchi za Afghanistan na Iraq ambao wanaishi huko Iran.Chini ya mpango huo mpya, wakimbizi hao sasa wanatazamiwa kupata bima ya afya ambayo itawasaidia kugharamia huduma za matibabu. Hata hivyo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR,limesema litaongeza ufadhili [...]

12/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Askari wa UNAMID wazidi kushambuliwa- Gambari

Askari wa kulinda amani wa UNAMID

Vikosi vya kulinda amani vya kimataifa vinavyoendesha opereshani zake kwenye jimbo lenye mzozo Darfur wameendelea kuandamwa na matukio ya mashambulizi .Kulingana na Mkuu wa vikosi hivyo ambavyo muungano wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID, Bwana Ibrahim Gambari amesema kuwa askari kadhaa wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na makundi korofi. Amesema katika kipindi [...]

12/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM inawasafirisha zaidi ya Wasudan 4000 wanaorejea nyumbani Sudan kusini

basi la IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linajiandaa kuwasafirisha hadi watu 4000 raia wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani, ambao wamekuwa kambini kwenye mpaka baina ya Sudan Kaskazini na Kusini kwa miezi kadhaa. Kundi la kwanza la watu takribani 2000 litaondoka eneo la Renk kuanzia Jumamosi hii kwa njia ya mashua pamoja na mizigo yao kama anavyofafanua [...]

12/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na maafisa mbalimbali wa serikali ya jamhuri ya Korea kusini

Ban akizungumza na maafisa wa serikali ya jamhuri ya Korea Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na wanadiplomasia na maafisa mbalimbali wa uongozi wa Jamhuri ya Korea mjini Seoul. Katika mazungumzo yao ameainisha masuala yatakayopewa kipaumbe na Umoja wa Mataifa katika miaka ijayo na kujulisha kwamba kuna muafaka mkubwa miongoni mwa nchi wanachama wa mambo gani ya kushughulikia kwa maendeleo endelevu. [...]

12/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR kuhamisha baadhi ya wakimbizi kutoka kambi ya Dadaab Kenya

wakimbizi wa Kisomali

Mwishoni mwa wiki hii shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR  litaanza kuhamisha baadi ya familia za wakimbizi wa Kisomali kutoka kambi ya Dadaab Kenya na kuwahamishia kwenye eneo jipya la kambi hiyo. Eneo hilo jipya liitwalo Kambioos liko karibu na kambi ya Hagadera na lina uwezo wa kuhifadhi wakimbizi 90,000. Mahema na [...]

12/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindupindu sasa kimesambaa miongoni mwa wakimbizi wa ndani Somalia:WHO

Mlipuko wa kipindupindu miongoni mwa wakimbizi wa ndani nchini Somalia

Mlipuko wa kipindupindu umethibitishwa miongoni mwa wakimbizi wa ndani nchini Somalia ambao wamekimbilia mjini Moghadishu limesema shirika la afya duniani WHO. Hadi sasa visa 18 vimebainika na wagonjwa wanapata tiba. WHO inasema hatua ya watu kuhamahama itafanya kuwa vigumu kudhibiti ugonjwa huo. Dr Michel Yao kutoka WHO anasema watoto waliodhoofu sana na utapia mlo wako [...]

12/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usalama bado ni tatizo kwa watoa msaada ya kibinadamu Mogadishu:OCHA

Mkuu wa OCHA Valeria Amos

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limesema hali ya usalama bado inatia hofu kwa watoa misaada ya kibinadamu mjini Moghadishu Somalia. OCHA inasema kujiengua kwa wanamgambo wa kiislamu wa Al-Shabaab hakutarajiwi kumaliza matatizo ya usalama na kufungua njia kwa watoa misaada mara moja kunakoshindwa kufikika. Kwa [...]

12/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katika siku ya kimataifa ya vijana UM waandamisha mchango wa vijana kutatua matatizo

Vijana walioshiriki katika siku ya kimataifa ya vijana

Umoja wa Mataifa umeadhimisha leo siku ya kimataifa ya vijana kwa kauli mbiu ya "Badili dunia yetu" huku Katibu Mkuu Ban Ki-moon akisisitiza jukumu lililobebwa na vijana mwaka uliopita katika kun'goa madarakani tawala za kidikteta. Ban katika ujumbe maalum kuadhimisha siku hii amesema vijana zaidi ya bilioni moja duniani wanakosa elimu, uhuru na fursa wanazostahili, [...]

12/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Deiss azungumzia chumi wa kimataifa nchini Argentina

Héctor Timerman

Udhibiti wa uchumi, utandawazi na jukumu la Umoja wa Mataifa ndio mada zilizotawala katika ziara ya sik moja ya Rais wa baraza la Umoja wa Mataifa Josef Deiss nchini Argentina. Akiwa mjini Buenos Aires Jumatano bwana deiss amekutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Héctor Timerman, watunga sheria bungeni, wanadiplomasia vijana na [...]

11/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu waathirika kutokana na ghasia dhidi ya vituo na wahudumu wa afya

11/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Rais wa Syria akiri kufanyika makosa wakati wa kukabiliana na waandamanaji

Rais wa Syria Bashar al-Assad na KM wa umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Rais wa Syria Bashar al-Assad kwa mara ya kwanza amekiri vikosi vyake vilifanya makosa wakati vikishughulikia maandamano ya raia wanaoupinga utawala wake.Rais Bashar ametoa kauli hiyo mbele ya ujumbe maalumu kutoka nchi za India, Brazil na Afrika Kusini unaotembelea nchi hiyo kwa ajili ya kupeleka ushawishi mpya wa maafikiano. Mataifa hayo matatu ni wanachama wa [...]

11/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu la UM asema mageuzi hayakwepeki ndani Umoja huo

Rias wa Baraza la Usalama Joseph Deiss

Vyombo muhimu vya Umoja wa Mataifa ikiwemo baraza la usalama, vinapaswa kufanya mageuzi ili kuleta nguvu na ushawishi muhimu katika enzi hii ya karne ya 21.Hayo ni kwa mujibu wa rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bwana Joseph Deiss ambaye ameonya kuwa utendaji wa umoja huo wa mataifa kwenye enzi hii mpya hauwezi [...]

11/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Chombo cha kupima tsunami chafuzu jaribio la kwanza

Mediterranean

Chombo kilichotumwa na Umoja wa Mataifa katika bahari ya Mediterranean na Atlantic kwa ajili ya kufanya utambuzi wa mapema juu ya uwezekano wa kutokea janga la tsunami, kimefaulu katika jaribio lake la kwanza.Hatua hiyo sasa inafungua milango ya kuanzishwa rasmi kwa chombo hicho kwenye eneo hilo. Chombo hicho cha utambuzi wa mapema juu ya janga [...]

11/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa UM wa amani ya mashariki ya kati asikitishwa na na hatua ya Israel

Robert Serry Mratibu Maalumu kwa Mchakato wa amani Mashariki ya Kati

Mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Robert Serry anatiwa hofu na tangazo la leo la serikali ya Israel la ujenzi wa nyumba moja Jerusalemu Mashariki zikiwemo nyumba 1600 mjini Ramat Shlomo ambazo zililaaniwa vikali na Qartet March 12 mwaka jana wakati wa mipango ya ujenzi huo. Serry [...]

11/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Balozi wa Uingereza kwenye UM apuuza mlinganisho wa ghasia za Uingereza na Syria

Balozi Philip Parham wa Uingereza

Balozi wa Uingereza ameitaka serikali ya Syria kusitisha matumizi ya nguvu na kuwakamata waandamanaji wanaouunga mkono demokrasia. Balozi Philip Parham ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya majadiliano kuhusu Syria kwenye baraza la salama mjini NewYork. Parham pia amesisitiza haja ya uongozi wa Syria kusikiliza wito wa baraza la usalama na kanda nzima [...]

11/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Assad amepoteza uhalali wake asema balozi wa marekani UM

Balozi wa marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice

Marekani inataka kwepo na vikwazo zaidi ili kusitisha machafuko nchini Syria. Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice akizungumza na waandishi wa habari mjini NewYork ameyaelezea machafuko na ghasia dhidi ya raia nchini Syria ni kama vitendo vya kutisha. Bi Rice amesema anatiwa moyo na kauli za kimataifa za kulaani hali ya Syria [...]

11/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amezitaka pande husika kuhakikisha suluhu ya kisiasa ya mgogoro wa Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon- Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Libya Baghdadi al-Mahmudi Jumatano jioni. Ban amefahamishwa kwamba baraza la salama limempa taarifa ya hali inayoendelea nchini Libya na limerejea kusisitiza masikitiko yake kuhsu kuendelea kupotea kwa maisha ya watu na kusambaratishwa kwa miundo mbinu. Ban pia ameelezea [...]

11/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake Wasomalia wanaotafuta hifadhi wanakabliwa na ubakaji:UM

Wakimbizi Wakisomali

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya ukatili wa kimapenzi Margot Wallstrom amesema wakati hali ya njaa ikizidi kuwa mbaya nchini Somalia anatiwa hofu na ripoti za visa vya ubakaji kufuatia kukimbia kwa wimbi kubwa la Wasomali na kuuingia Kenya. Vita, uukame na kukimbia makazi yao kunabainisha hali mbaya ya katili wa kimapenzi unaowakabili [...]

11/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kwenye kongamano la kimataifa la wanafunzi Ban awataka vijana kuleta mabadiliko

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon akihutubia vijana - Korea

Vijana wametakiwa kujitoa na kushiriki kikamilifu katika kupata suluhu ya matatizo yanayoisumbua dunia hivi sasa. Akitoa wito huo kwenye mkutano wa tatu wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa mfano yaani UN Model mjini Incheon Korea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kila siku wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wako katika maeneo [...]

11/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia lazima iisaidie Somalia katika kipindi hiki cha kihistoria kuelekea amani ya kudumu

Balozi Augustine Mahiga

Hatua zilizopigwa hivi karibuni kisiasa na kijeshi katika taifa la Somali lililoghubikwa na vita zinatoa fursa muhimu ya kupiga hatua na kukabiliana na changamoto zikiwemo wabbabe wa kivita na magaidi amesema leo afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa. Balozi Augustine Mahiga ambaye ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia ameitolea wito [...]

10/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UN-HABITAT yaandaa mkutano kujadili ongezeko la watu wanaohamishwa kwa nguvu toka kwenye makazi yao

un habitat nemba

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi linajiandaa kuwa na mkutano mkubwa ikiwahusisha wataalamu wa kimataifa wa makazi ambao watakuwa na shabaya ya kuangazia mtizamo wa wale wanaohamishwa kwa kulazimishwa. Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika kuanzia Septemba 20-23 mjini Nairobi unazingatia mpango wa kimataifa ambao umeweka hadi mwaka 2025 kuwa na makazi bora naya uhakika. [...]

10/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wamlilia rais wa zamani wa baraza kuu Holker

Harri Holkeri na aliyekuwa KM wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan(2003)

Maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wanaomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Finland Hariri Holker ambaye pia hapo nyuma amewahi kufanya kazi na Umoja wa mataifa kama rais wa mkutano wa 55. Pia amewahi kufanya kazi huko Kosovo akiwa kama mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa [...]

10/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wataka mashirikiano zaidi kukabili janga la kimazingira

mafuriko

Mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake yametoa mwito yakitaka kuongezwa kwa mashirikiano ya pamoja ili kukwamua janga la kuangamia kwa misitu duniani kote kunakosababishwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya tabia nchi . Hali inayojitokeza sasa inatajwa kuzua kitisho kikubwa kwenye mazingira ikiwemo usababishwaji wa majanga kama mafuriko, kujiri kwa [...]

10/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tathmini ya chakula ya FAO mwezi Agosti yajikita katika Pembe ya Afrika

Ukame imeathiri sana mifugo katika eneo la Pembe ya Afrika

  Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula la kilimo FAO leo limetoa mtazamo wa kufuatilia bei za chakula kwa mwezi huu wa Agosti. Mtazamo huo safari hii umejikita kwenye pembe ya Afrika inayokabiliwa na njaa kali iliyosababisha maelfu ya watu kuzidi kukimbia makwao hususani nchini Somalia na Kenya. FAO inasema bei za kimataifa za [...]

10/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yatakiwa kuchukua hatua baada ya utafiti wa ukatili dhidi ya watoto:UNICEF

ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania

Umoja wa Mataifa umeichagiza serikali ya Tanzania kushughulikia haraka matatizo ya ukatili dhidi ya watoto baada ya matokeo ya utafiti uliofanywa na serikali ambapo zaidi ya robo tatu ya wasichana na wavulana wamesema wamekabiliwa ukatili na kuumizwa kimwili kabla ya kufikia umri wa miaka 18. Kutokana na taarifa iliyotolewa leo na shirika la kuhudumia watoto [...]

10/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watu waathirika kutokana na ghasia dhidi ya vituo na wahudumu wa afya

chama cha msalaba mwekundu ICRC

Mashambulizi dhidi ya mawafanyakazi wa afya, vituo na magari ya wagonjwa kwenye maeneo ya vita na machafuko yamewaacha mamilioni ya watu duniani bila huduma muhimu wanayoihitaji. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliyotolewa leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva na kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC. [...]

10/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wazindua muongozo kwenye mtandao kusaidia kukabili mifumo ya utapia mlo

mtoto mchang'a mikonono mwa mamake

Serikali na wafanyakazi wa afya sasa wanaweza kupata taarifa za mpango mya ulioanzishwa na shirika la afya duniani WHO kwa njia ya mtandao, wenye lengo la kutoa mwongozo mpya wa kisayansi kudhibiti vitisho vya afya vinavyosababishwa na utapia mlo. Mpango huo mpya wa WHO uitwao e-mkataba ambao ni ushahidi kuwa hatua za lishe (eLENA) na [...]

10/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miji iliyoghubikwa na machafuko Darfur kupata msaada

wakimbiaji kutoka Darfur Sudan

Wafanyakazi wa miasaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo linaloghubikwa na machafuko la Darfur Sudan wako katika mpango maalmu wa wiki moja kugawa misaada katika miji ya jimbo hilo. Mpango wa pamoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika UNAMID unasema chakula, madawa na misaada mingine inagawiwa kwa watu [...]

10/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awataka wanazuoni kutafuta suluhu ya kimataifa ya njaa, umaskini na kuvumiliana

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon nchini Korea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameitolea wito jumuiya ya kimataifa ya wanazoni kutafuta suluhu ya matatizo ya njaa na utapia mlo yanayoisumbua dunia,  kuchangia mawazo ya kuchagiza maendeleo endelevu na yanayojumuisha wote na kuimarisha masuala ya kuvumiliana katika jamii kwa kuheshimiana na maelewano. Ban ameyasema hayo kwa washiriki wa kongamano la [...]

10/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wawahisha misaada kwa waliokumbwa na njaa Moghadishu

10/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Bi Asha-Rose Migiro Jijini dar es salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr Asha Rose Migiro leo amezindua ripoti juu ya utokomezaji wa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto, na kubainisha nama vitendo hivyo vinavyipindukia mipaka. Uzinduizi wa ripoti hiyo ni utekelezaji wa azimio lililowekwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2006, alipotaka mataifa yote duniani kuendesha [...]

09/08/2011 | Jamii: Mahojiano, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Juhudi zinaendelea kufanywa ili kuwahamisha wakimbizi walioko Ethiopia

wakimbizi wakisomali wasubiri msaada

Huku hali ikizidi kuzorota katika eneo la Pembe ya Afrika inayoandamwa na ukosefu wa chakula, juhudi zinaendelea kufanywa kwenye makambi ya wakimbizi wa Somalia walioko Ethiopia kufuatia mlundikano mkubwa wa wakimbizi hao waliokwama kwenye kambi moja. Ikiwa leo ni siku yake ya nne, tayari juhudi za kuwaondosha baadhi ya wakimbizi kutoka katika kambi ya Dollo [...]

09/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wachezaji nyota wa Barcelona wawatia moyo vijana

Mpira wa soka

Wanasoka wa kilabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania ambao wanaunga mkono juhudi zinazochukuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamejitokeza hadharani kuwapa moyo watoto wakisema kuwa wanaweza kufika mbali kama wataweka mapenzi yao kwenye soka. Nyota hao wa dimba David Villa na Thiago Alcántara walijitokeza huko Dallas Marekani na kuwapa [...]

09/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lalani vikali mashambulizi kwa askari wa UNAMID Darfur

walinda amani wa UNAMID- Darfur

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali tukio la mashambuli yaliyowalenga vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID vinavyoendesha operesheni zake katika jimbo la Darfur nchini Sudan, ambako  askari mmoja raia wa Sierra Leone alifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa. Katika taarifa yake juu ya kadhia hiyo, [...]

09/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dk.Migiro azindua ripoti ya kupinga ukatili dhidi ya watoto Tanzania

Naibu Katibu Mkuu wa UM Bi. Asha Rose Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro leo amezindua ripoti ya utokomezaji ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania. Uzinduzi huo ni utekelezaji wa azimio lililowekwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon mwaka 2006 alipozitaka nchi zote wanachaka kufanya utafiti wa kina ili kubaini miondo na mifumo ya unyanyasaji dhidi ya watoto. [...]

09/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha hatua zilizotangazwa na Marekani kusaidia kuzuia mauaji ya kimbari

Kumbukumbu mauaji ya kimbari

Juhudi zilizotangazwa na Rais Barack Obama wa Marekani hivi karibuni za kuimarisha uwezo wa serikali yake kusaidia kuzuia mauaji ya kimbari na unyama mwingine ni mipango inayotia matumaini amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Amesema ili jukumula la kuwalinda watu litekelezeke ipasavyo basi chi wanachama lazima wabuni mikakati mipya na kitekeleza kuanzia [...]

09/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia sasa ina watu wa asili milioni 370

Mashujaa wa kimaasai

Umoja  wa Mataifa na dunia kwa ujumla leo imeadhimisha siku ya kimataifa ya watu wa asili ambayo mwaka huu inachagiza masuala ya ubunifu na kauli mbiu ni "ubunifu wa asili, kusherehekea hadithi na utamaduni kwa kuunda maisha ya baadaye". Katika ujumbe maalumu ya kuadhimisha siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema [...]

09/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaonya juu ya idadi kubwa ya watoto kuacha shule Somalia

wanafunzi darasani mjini Mogadishu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limekadiria kwamba watoto milioni 1.8 wa umri wa kati ya miaka 5 hadi 17 tayari wameshaacha shule Kusini na Katikati mwa Somalia .  Hii ni kutokana na tathimini iliyofanywa na kituo cha elimu katika mikoa kumi na imeonya kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka sana wakati shule [...]

09/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO Inawachagiza Wasomali kutohama walipo

somalis

Maelfu ya Wasomali wameikimbia nchi yao ili kutafuta msaada na ukimbizi katika mataifa ya jirani tangu kuanza kwa mwaka huu, huku zaidi ya 100,000 wamekimbia kuanzia mwezi Mai. Hali ya njaa inazidi kuwa mbaya Kusini na Katikati mwa Somalia limesema shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, hata hivyo shirika hilo linawachagiza [...]

09/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wawahisha misaada kwa waliokumbwa na njaa Moghadishu

Ndege yabeba misaada ya dharura kwa maelfu ya watu waliokimbia makazi yao mjini Mogadishu

Wakati hali ikizidi kuwa mbaya kwenye pembe ya Afrika na husani Somalia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR sasa linaelekeza juhudi zake katika kuwahamisha wakimbizi kwenye makambi ya muda yaliyofurika. Tangu kuanza kwa operesheni hiyo Agost 5 wakimbizi takribani 4000 wamehamishwa kwa ndege kutoka kambi ya Dollo mjini Ado Ethiopia na kupelekwa [...]

09/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bokova alaani shambulizi kwenye kituo cha runinga Libya

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Irina Bokova

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililotwikwa jukumu la kutetea uhuru wa vyombo vya habari amelaani shambuli lililoendeshwa na jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO kwenye kituo cha kitaifa cha runinga nchini Libya mwezi uliopita, ambapo wafanyikazi watatu waliuawa na wengine 21 kujeruhiwa. Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu , sayansi na [...]

08/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asema Israel inaendelea kukiuka sheria za kimataifa

Makaazi ya Israel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa amevunjwa moyo kuona Israel ikiidhinisha mpango mpya unaoruhusu kuendelea na ujenzi wa makazi katika eneo la mashariki wa Jerusalem. Chini ya mpango huo mpya, Israel inakusudia kujenga nyumba zipatazo 900 katika eneo ambalo bado linaendelea kuzua mzozo mkubwa. Ban katika taarifa yake amesema kuwa hatua [...]

08/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Askofu wa Sudan asema " kuna maauwaji ya kikabila

Askofu Andudu Adam Elnail

Askofu mmoja ambaye anatoka katika mji wa Kadugli mji ulioko Kusini mwa Sudan ameyaelezea mauwaji yanayoendelea sasa kama mauji ya kikabila. Askofu huyo  Andudu Adam Elnail amesema matukio hayo ya mauwaji ni sawa na kusema ni mauwaji ya kimbari yenye shabaya ya kuangamiza kabila fulani. Amelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua [...]

08/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amtaka rais wa Syria kukomesha mabavu dhidi ya waandamaji

KM wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon azungumza na rais wa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtaka rais wa Syria kukomesha vitendo vya dhuluma dhidi ya waandamanaji wanaopinga utawala wake akisema kuwa mamlaka hiyo inapaswa kuachana na vitendo hivyo mara moja. Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na rais Bashar al-Assad Ban amemwambia rais huyo kuwa anapaswa kuchukua jukumu la kukomesha matumizi [...]

08/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Surua wasambaa kwenye kambi za pembe ya Afrika

wanawake na watoto kutoka Somalia

Umoja wa Mataifa umeelezea kusikitishwa kwake na hali ya wakimbizi kutoka Somalia walio kwenye kambi ya Dollo Ado Kusini Mashariki kwa Ethiopia kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa Surua ambapo umetoa wito kwa msaada wa dharua ili kuwasaidia walioathiriwa. Hadi sasa kumeripotiwa visa 47 na vifo vitatu vilivyosababishwa na ugonjwa wa Surua kwenye kambi ya Kobe [...]

08/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasema wakimbizi katika pembe ya Afrika wakabiliwa na athari za kiafya

Nembo ya UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa  UNHCR, limesema wakimbizi wengi waliokimbia makwao sasa wanakabiliwa na tisho la afya. UNHCR imesema kuna uwezekano wa kutokea matatizo kama magonjwa ya utapiamlo na kwashakoo yanayotokana na  uhaba wa chakula. Wengi wanapata chakula kisicho cha kuridhisha huku wengine wakikosa kabisa. Wataalamu wa afya wanasema kuwa maeneo mengi [...]

08/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanamgambo wa Al-Shabaab waanza kuondoka mji wa Mogadishu

Balozi Augustine Mahiga

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Agustine Mahiga amekaribisha habari kuwa kundi la wanamgambo la Al-Shabaab limeanza kuondoka mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo ametoa wito kwa serikali ya nchi Somalia kutumia fursa hiyo kuhakikisha kuwa misaada imewafikia raia. Mahiga amesema kuwa kundi la Al-Shabaab tayari lishaondoka kutoka maeneo muhimu kwenye mji wa [...]

08/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atembelea eneo la Fukushima nchini Japan

KM Ban Ki-moon asalimia na Sato,gavana wa mkoa wa Fukushima

Akiwa ziarani nchini Japan Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amepeleka ujumbe wa umoja na mshikamano kwenye sehemu za mashariki mwa Japan ambazo bado zinapitia athari zilizosababishwa na majanga ya kiasili yaliyoikumba nchi hiyo yakiwemo tsunami, tetemeko la ardhi na ajali ya kinu cha kinyuklia.Ban amesema  kuwa hata kama alihuzunishwa na mkasa [...]

08/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya haki za binadamu bado mbaya nchini Iraq: UM

waandamanaji nchini Iraq

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Iraq imeonya kuwa ghasia na ukiukaji wa haki za binadamu uliofichika vinaendelea kuwaathiri watu wengi nchini Iraq. Ripoti hiyo iliyotolewa hii leo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI pamoja na ofisi ya kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa iliangazia [...]

08/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya ukweli na maridhiano kuundwa nchini Burundi mwaka ujao

ramani ya Burundi

Makala yetu wiki hii inamulika kuundwa kwa tume ya ukweli na maridhiano nchini Burundi mwaka ujao ikiwa ni moja ya maazimio ya mkataba wa amani wa Arusha uliofikiwa mwaka wa 2000. Nchini Burundi,  serikali ya nchi hiyo imetangaza kwamba tume ya ukweli na maridhiano itaundwa tarehe mosi january mwaka wa 2012. Taasisi hii ya kisheria [...]

05/08/2011 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atangaza nia ya kumteua mwanadiplomasia wa kijerumani kama mjumbe wake nchini Iraq

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon na Martin Kobler

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa ana nia ya kumteua Martin Kobler kutoka nchini Ujerumani kama mjumbe wake maalum nchini Iraq na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMIS. Bwana Kobler atachukua mahala pa Ad Melkert kutoka uholanzi ambaye amehudumu kama mjumbe maalum wa katibu mkuu nchini Iraq tangu Julai [...]

05/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM waitaka Belarus kuhakikisha inazingatia ustawi wa mtetezi wa haki za binadamu anayeshikiliwa

ramani ya Belarus

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kwa serikali ya Belarus ambayo imemweka kizuizini mtetezi wa haki za binadamu Ales Bialatski na imeitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inazingatia ustawi wake. Bwana Bialatski ni rais wa taasisi ya Viasna. Lakini pia anashika wadhifa wa makamu wa rais katika taasisi ya kimataifa ya haki za binadamu. Kwa mujibu wa [...]

05/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Afisa Mkuu wa vikosi vya kulinda amani amaliza muda wake na kutaja mafanikio

Afisa wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia  vikosi vya ulinzi wa amani Bwana Le Roy ambaye anajiandaa kumaliza muhula wake, amebainisha mafanikio yaliyofikiwa na idara hiyo na kusema kuwa kuna hatua kubwa zimepigwa ikiwemo utoaji ulinzi kwa mamia ya raia ulienda sambamba na utengamao katika mataifa kadhaa duniani. Vikosi hivyo vya kulinda amani vimehudumu katika mataifa [...]

05/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sudan yachelewesha helkopta ya uaokoaji-UM

Helikopta ya Umoja wa Mataifa

Mamlaka ya Sudan imetoa tishio kali la kutaka kuidungua helikopta itakayokwenda kwenye eneo la Abyei kwa ajili ya kutoa msaada wa kitabibu kwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao wamejeruhiwa vibaya hatua ambayo imesababisha operesheni hiyo ya uokoaji kuchelewa kwa zaidi ya saa tatu.Hapo majuzi askari 3 wa Umoja wa Mataifa raia [...]

05/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu dawa za kulevya nchini Kenya

wakaazi wa Mombasa nchini Kenya, wandamana dhidi ya madawa ya kulevya

Wasomi wa kiislamu barani Afrika pamoja na wenzao kutoka bara Asia wamekamilisha mkutano wa siku nne mjini Mombasa, Kenya, kuzungumzia njia muafaka za kukabili utumiaji wa dawa za kulevya.Baadhi ya maafikiano katika mkutano huo ni kushirikisha jamii nzima katika kutatua tatizo la dawa za kulevya, hasa kwa kufuata maadili ya kidini. Kongamano hilo lilishirikisha wajumbe [...]

05/08/2011 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM waitaka Syria kutoendesha ghasia dhidi ya raia

Waandamanaji nchini Syria

Huku ghasia zinazoendeshwa na serikali ya Syria dhidi ya raia zikizidi kundi la wataalamu wa haki za binadam kutoka Umoja wa Mataifa wamerejelea wito  wao kutaka kusitishwa kwa ghasia hizo. Wito wa wataalamu hao unajiri baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kulaani ukiukaji wa haki za binadam unaoendelea nchini Syria na matuumizi [...]

05/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uingereza yatakiwa kutafuta suluhu la kuhamishwa kwa familia 86 kutoka Ireland

Wataalamu wawili wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa wanaohusika na masula ya makoa wametoa wito kwa serikali ya uingereza kuwatawafutia makao jamii 86 kutoka nchini Ireland ambazo huenda zikahamishwa kutoka shamba moja lijulikanano kama Dale Farm eneo la Essex kabla ya mwisho wa mwezi huu. Mtaalam anayehusika na masuala ya haki ya kuwa [...]

05/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwanajeshi wa UNAMID auawa Darfur

Wanajeshi wa UNAMID katika Darfur,Sudan

Mwanajeshi mmoja wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika AU kinacholinda amani kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan UNAMID ameuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya wakati gari lao lililokuwa na wanajeshi watano liliposhambuliwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha Duma kilomita 37 kaskazini mashariki mwa nyala kusini mwa Darfur. Eneo la [...]

05/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba msaada ya dola milioni 26 kuwasaidia walio na njaa pembe ya Afrika

Nemba ya IOM

Kufuatia kutangazwa kwa njaa kwenye maeneo matano kusini mwa Somalia, ukame nchini Kenya , Ethiopia na Djibouti wakiwemo wakimbizi wanaokimbia njaa na kuingia nchini Kenya na Ethiopia pamoja na kupanda kwa bei cha chakula katika maeneo hayo.  Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatoa wito kwa wafadhili kwa msaada wa dola milioni 26 ili kugharamia [...]

05/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaongeza usambazaji wa misaada Daadab

mtoto ala 'plumpynut'

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeongeza usambazaji wa misaada wa chakula ndani na nje ya kambi ya Daadab nchini Kenya wakati mahitaji ya misaada yanapozidi kuongezeka. UNICEF inasambaza chakula cha watoto kilicho na dawa na kilicho tayari kutumika kwenye mahospitali na vituo vingine vya lishe kwenye kambi ya Daadab na kwa [...]

05/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa kipindupindu wasambaa kwenye maeneo yanayokumbwa na ukame nchini Somalia

familia ya kisomali

Shirika la afya duniani WHO linasema kwa kumetokea mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye maeneo yanayokumbwa na ukame pamoja na njaa nchini Somalia. WHO inasema kuwa mamilioni ya watu wako kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu, ugonjwa ambao unaweza kusababisha kifo kwa haraka kama mogonjwa hatapata tiba. Mtaalamu wa WHO Dr Michel Yao anasema [...]

05/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wazitaka pande za kisiasa nchini Haiti kuafikia makubaliano

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Mariano Fernández na Rais wa Haiti Michel Martelly

Umoja wa Mataifa umezishauri pande zote za kisiasa nchini Haiti kuafikia makubaliano wakati ambapo kuna mvutano kati ya rais Michel Martelly na bunge kuhusu kuthibitishwa kwa waziri mkuu mpya. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH ulikubaliana na uamuzi wa bunge wa kumkataa Bernard Gousse ikiwa ndio mara ya pili bunge kukataa uteuzi wa [...]

04/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laani mauwaji ya askari wa kulinda amani Abyei

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa washika doria katika mitaa ya mji wa Abyei

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali juu ya kuuliwa kwa askari wa kulinda amani wanaohudumu katika jimbo lenye mzozo la Abyei,Sudan.Askari hao wanne walipoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu la kutengwa ardhini wakati wakiwa kwenye operesheni za ulinzi wa amani.Wote wa askari hao ni raia wa Ethiopia. Katika tukio hilo askari [...]

04/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM yatoa chakula cha ramadhani kwa Wa-Libya 55,000

mvulana mkimbizi apokea chakula cha chakula jioni wakati huu wa Ramadhan

Umoja wa Mataifa umeanza kusambaza msaada wa chakula kwa mamia ya wananchi wa Libya walioko kwenye mfungo wa mwezi wa ramadhani. Kulingana na shirika la umoja huo wa mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR,misaada hiyo ya chakula imewafikia zaidi ya Wa-Libya 55,000 walioko katika nchi jirani ya Tunisia ambao walikimbilia nchi hiyo kufuatia kuzorota [...]

04/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakulima wa Togo wafaulu kuleta faida-UM

mkulima Togo

Mpango ulioendeshwa na Umoja wa Mataifa kwa pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya ambao ulilenga kuboresha hali ya uzalishaji chakula kwa Togo, unaaerifiwa kuzaa matunda mara mbili.Taasisi hizo za kimataifa lilisambaza pembejeo mbalimbali ikiwemo mbegu za kisasa kwa zaidi ya wakulima 20, 000 walioathiriwa na matokeo ya hali mbaya ya hewa. Shabaya kubwa katika [...]

04/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wasaidia Belize kupambana na HIV na Ukimwi

Ukimwi

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP lina mpango wa kutekeleza makubaliono ya gharama ya dola milioni 3.1 na taifa Belize ili kutibu na kuzuia ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa vijana na watu wengine wazima kwenye taifa hilo lililo na idadi kubwa zaidi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwenye eneo la Amerika [...]

04/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya UM nchi Haiti kwenye tahadhari ya kutokea dhoruba

MINUSTA-Haiti

Karibu walinda amani 12,000 wako katika hali ya tahadhari nchini Haiti wakati dhoruba kwa jina Emily inapoelekea katika taifa hilo la Caribbean linalojaribu kurudi kwenye hali ya kawaida baada ya tetemeko kubwa kuikumba nchi hiyo mwaka uliopita na kuwaua zaidi ya watu 200,000 na kuwaacha wengine 2.3 bila makao. Baadhi ya wanajeshi kutoka kwa kikosi [...]

04/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wachunguza madai ya mashumbulizi kwenye mitandao

Msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky

Uchunguzi umeanzishwa kufuatia madai kuwa mitandao ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikiingiliwa. Wataalam wa masuala ya usalama wamedhibitisha kuwa kushambuliwa kwa mitandao kwa muda wa miaka mitano iliyopita kumeathiri mashirika mengi likiwemo shirika la Umoja wa Mataifa. Msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky anasema kuwa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini [...]

04/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watu maskini kumiliki namba za simu za mkononi

mfugaji mmaaasai aonyesha simu lake

Watu milioni tatu maskini barani Afrika na kusini mwa Asia wengi wakiwa ni wanawake watarajiwa kupata namba za simu za mkononi zenye gharama ya chini kama moja ya maelewano kati ya kampuni ya Movirtu na mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Matiafa katika juhudi za kupambana na umaskini. Wale watakaopata namba hizo watakuwa wakitumia simu [...]

04/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takriban watoto 20 wafa nchini Somalia kila siku

watoto wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya

Takriban watoto 20 walio chini ya miaka mitano kati ya watoto 10,000 wanakufa kila siku kwenye sehemu zilizoathiriwa na ukame nchini Somalia. Hii ni mara tano zaidi ya idadi iliyotumika kubaini kuwa eneo liko kwenye njaa. Ripoti kutoka kwa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Matifa FAO zinasema kuwa njaa kusini mwa Somalia [...]

04/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchafuzi wa mazingira katika eneo la Ogoniland hatari kwa afya

Ogoniland, Nigeria

Ripoti iliyotolewa hii leo na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mafuta katika eneo la Ogoniland nchini Nigeria umehatarisha zaidi afya ya binadamu. Ripoti hiyo inasema kuwa huenda ikachukua hadi miaka 30 kusafisha maeneo hayo yaliyochafuliwa. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kiwango cha uchafuzi wa mazingira ni cha [...]

04/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani matumizi ya nguvu dhidi ya raia nchini Syria

Hardeep Singh

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani ghasia zinazoendeshwa na serikali ya Syria dhidi ya raia . Kulingana na taarifa iliyotolewa na balozi wa India kwenye Umoja wa Mataifa Hardeep Sing Puri ni kuwa wanachama wa baraza hilo walitaka kusitishwa mara moja kwa ghasia nchini Syria. Mamia ya watu wameuawa tangu kuanza kwa ghasia [...]

03/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wabakaji lazima wakabiliwe na sheria sio maripota:UM

Margot Wallström

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu  wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kingono kwenye mizozo Margot Wallström ameelezea kusikitishwa kwake baada ya mahakama nchini Sudan kumfunga mwandishi mmoja wa habari aliyeripoti tukio ambapo mwanaharakati mmoja alibakwa na wanajeshi akisisitiza kuwa wahusika ndio wanastahili kufungwa na wala sio wanaoripoti. Wallstrom amesema kuwa hukumu kama hizo sio [...]

03/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watangaza njaa sehemu tatu zaidi nchini Somalia

03/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Chombo cha kung'amua majanga kuanza kujaribiwa wiki ijayo

uharibifu mkubwa wa pwani ya Indonesia uliosababishwa na tsunami katika bahari ya Hindi mwaka 2004

Jaribio la kwanza kupima uwezo wa chombo kinazoweza kutambua uwezekano wa kutokezea janga la Tsunami linatazamiwa kufanywa wiki ijayo katika maeneo ya bahari ya Atlantic na Mediterranean.Chombo hicho ambacho kinaratibiwa na Umoja wa Mataifa ni cha kwanza kuwekwa kwenye eneo hilo kikiwa na shabaya ya kutoa ung'amuzi wa mapema uwezekano wa kutokea janga la tsunami. [...]

03/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM Libya akutana na mwanadiplomasia wa juu wa China

Abdel-Elah Al-Khatib

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa maalumu kwa ajili ya Libya amekuwa na majadiliano na waziri wa mambo ya nje wa China katika jaribio la kutaka kumaliza mzozo unaoendelea kufukuta katika  taifa hilo na wakati huo amesifia juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Beijing ambayo inajisogeza kumaliza mkwamo huo wa kisiasa. Abdel-Elah Al-Khatib ambaye yupo katika ziara ya [...]

03/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM watangaza njaa sehemu tatu zaidi nchini Somalia

Maelfu ya Wasomali wamekimbia nchi yao kuepuka njaa

Umoja wa Mataifa hii leo umetangaza njaa kwenye sehemu tatu zaidi nchini Somalia na kufikisha idadi ya maeneo ambayo sasa yametangazwa kukumbwa na njaa kuwa matano kwenye pembe ya Afrika ambapo utapiamlo na njaa umesababisha vifo vya maelfu ya watu. Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia Mark Bowden amesema kuwa maeneo ya Afgoye Corridor [...]

03/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM aonya kuwa makabiliano kati ya wanajeshi wa Israel na Lebanon huenda yakaleta vita

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Michael Williams

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Michael Williams amesema kuwa makabiliano ya risasi yaliyoshuhudiwa wiki hii kati ya wanajeshi wa Lebanon na wale wa Israel waliovuka eneo la Blue Line linalotenganisha nchi hizo mbili huenda yakaleta vita. Akiongea alipokutana na waziri mkuu wa Lebanon Najib Mikati mjini Beirut Williams amesema kuwa makabiliano hayo yalikuwa [...]

03/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalam wa UM aitaka Iran kutoa ushirikiano katika kushughulikia masuala ya haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu

Mtaalamu mpya wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu nchini Iran ametoa wito kwa nchi hiyo akiitaka ishirikiane naye katika kutatua masuala yaliyopendekezwa na jamii ya kimataifa. Ahmed Shaheed amesema kuwa ana matumani kuwa utawala nchini Iran utaitambua kazi yake kama fursa ya kukabiliana na sheria za kimataifa za haki za [...]

03/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM nchini Somalia asema mapigano yametatiza utoaji wa misaada nchini humo

Balozi Augustine Mahiga

Mjumbe wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga ametoa wito kwa Wasomali wanaoshi nchi za ng'ambo pamoja na jamii ya kimataifa kuchanga fedha zinazohitajika kwa dharura ili kuwasaidia watu wanaokufa njaa nchini Somalia. Hata hivyo Mahiga ameonya kuwa mapigano yanayoendeshwa na wanamgambo na makundi mengine yanayoipinga serikali huenda yakaifanya hali [...]

03/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha vikwazo wa wale watakaokiuka haki za watoto Somalia

Mjumbe maalum- Radhika Coomaraswamy

Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na mizozo Radhika Coomaraswamy amekaribisha uamuzi wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baada ya kukubali kumwekea vikwazo yeyote ambaye atakiuka haki za watoto nchini Somalia. Mjumbe huyo amesema kuwa ikiwa yeyote atamuua , kumuajiri , kumdhulumu kingono mtoto, au kama yeyote atashambulia [...]

03/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi dhabiti vya kulinda amani vyahitajika: Le Roy

Alain Le Roy

Mratibu wa masuala ya kulinda amani  kwenye Umoja wa Mataifa Alain Le Roy amesema kuwa kuna mahitaji ya kuwepo vikosi dhabiti vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa akiongeza kuwa hili limeshuhudiwa kwenye Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, nchini Ivory Coast na Sudan. Amesema kuwa uungwaji mkono wa baraza la usalama la umoja wa Mataifa [...]

03/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanajeshi wanne wa UM wa kulinda amani eneo la Abyei wauawa

walinda amani

Wanajeshi wanne wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan wameuawa hii leo na wengine saba kujeruhiwa baada ya bomu kulipuka walipokuwa kwenye shughuli ya kupiga doria. Wanajeshi hao kutoka Ethiopia walio miongoni mwa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda katika eneo la Abyei walikuwa wakipiga doria kwenye eneo la Mabok kusini mashariki [...]

02/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNRWA yasema hali inazidi kuzorota ukingo wa Gaza

nemba ya UNRWA

Kumejitokeza adhari mbaya inayochagizwa na hatua inayochukuliwa na mamlaka za Israel ambayo huendesha bomoa bomoa ya majengo katika maeneo ya ukingo wa Gaza.Kwa kuzingatia taarifa iliyotolewa na shirika la kimataifa linalohiusika na wakimbizi wa Palestine UNRWA vitendo hivyo vya ubomoaji sasa vimepindukia mipaka. Taarifa ya shirika hilo imesema kuwa hali hiyo imewaathiri zaidi ya watu [...]

02/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mpango wa ujenzi wa endelevu wapigwa jeki

matumizi ya nishati

Mpango unaendeshwa na shirika la kimataifa wenye shabaya ya kuanzisha vigezo vya kimataifa ambavyo vitahusika na upigamaji wa wazi wa matumizi ya gezi kwenye ujenzi leo umepata msukumo mpya kufuatia shirika la kimataifa la viwango ISO kukubali kuweka vifaa vipya vitavyoupa uhai mpango huo. ISO imesema kuwa imekubali kuangalia namna ya kuingiza vifaa vya kisasa [...]

02/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hali ya misaada ya kibanadamu inazidi kuzorota Somalia– UNHCR

wakimbizi katika kambi ya Dagahaley

Mkwamo wa kisiasa unaendelea kujiri nchini Somalia katika wakati ambapo hali ya usalama ikizidi kuzorota kunaarifiwa kuongezeka kwa makundi ya watu wanaoingia mtawanyikoni huku huduma za kibinadamu zikianguka.Kulingana na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi,makundi ya watu wameendelea kukatiza katika mji wa Mogadishu kufuatia hali mbaya ya ukosefu wa chakula ambayo pia imesababishwa [...]

02/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Akina mama waliohuzunika kwenye hatari kuwa na watoto wasiokua

mam mwenye huzuni

Kulingana na utafiti uliochapishwa hii leo kwenye makala ya shirika la afya duniani WHO inaonyesha kuwa wanawake ambao wanaonyesha dalili za kuhuzunika wako kwenye hatari ya kuwa na watoto walio na uzito mdogo au ambao hawatakua, tofauti na akina mama walio na afya nzuri kifikra. Watafiti wameendesha uchunguzi huu kwa karibu akina mama 17,000 na [...]

02/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban kuzuru kinu cha Fukushima nchini Japan

timu ya uchunguzi ya IAEA ya chunguza uharibifu katika kinu cha Fukushima Daiichi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kufanya ziara juma hili kwenda Japan ambapo atakizuru kinu cha Fukushima kujionea uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi na tsunami vilivyoikumba Japan mapema mwaka huu ambapo pia ataitembelea Korea. Tetemeko kubwa la ardhi na tsunami vilivyoikumba Japan tarehe 11 mwezi Machi vilisababisha vifo vya watu kadha na kuharibu [...]

02/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasafirisha wahamiaji kutoka Libya

Wakimbizi - Lybia

Oparesheni ya shirika la kimataifa la uhamiji IOM ya kusafirisha mamia ya wahamiji raia wa Chad waliokwama kwenye mji ulio kusini mwa Libya wa Sebha na kuwarudisha kwenye mji mkuu wa Chad N ‘Djamena imekamilika. Oparesheni hiyo ilikamilika tarehe 30 mwezi uliopita iliwasafirisha wahamiaji 1,398 na raia wan chi zingine wakiwemo wanawake , watoto na [...]

02/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 25 kutoka Libya wafa wakijaribu kuingia ulaya

wafanyikazi wa kujitolea na madaktari kwenye mashua ambapo maiti zilipatikana

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa maiti za wahamiaji 25 zimepatika kwenye meli moja iliyokuwa ikiwasafirisha watu 300 kwenda kwa kisiwa cha Italia cha Lampedusa. IOM inasema kuwa watu 270 waliokolewa na walinzi wa pwani ya Italia. Asilimia kubwa ya wahamiaji waliokuwa kwenye meli hiyo wametoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. [...]

02/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulimwengu uko macho kwa ghasia zinazondelea Syria: Pillay

Waandamanaji katika Homs, Syria

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameionya serikali ya Syria kuwa ulimwengu umeielekezea macho kutokana na ghasia inazoendesha dhidi ya raia wake na kuitaka isitishe umwagikaji wa damu. Pillay amesema amesikitishwa kufuatia ripoti kuwa takriban watu 145 wameuwa na wengine wengi kujeruhiwa tangu siku ya ijumaa. Karibu watu 120 waliripotiwa [...]

02/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wafanya mkutano wa dharura kuijadili Syria

Baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeita mkutano wa dharura kufuatia hatua ya serikali ya kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji na vikosi vya serikali . Mamia ya waandamanaji wanaondamana kwa amani wanaripotiwa kuuawa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani ghasia akiutaka utawala nchini Syria kukoma kutumia nguvu dhidhi ya raia. Mataifa kama vile [...]

02/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wito wa kusafirishwa kwa misaada watolewa

Ghala la UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watu nusu milioni kwenye pembe ya Afrika huenda wakafa kwa majuma mchache yajayo ikiwa hawatapa usaidizi . UNICEF kwa sasa inatoa wito kwa mashirika ya ndege yasaidie kusafirisha misaada ya chakula bila malipo au kwa malipo kidogo kwenda kwa watoto wanaokufa njaa [...]

02/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unyonyeshaji unachangia katika kupunguza vifo vya watoto

01/08/2011 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Makundi ya kiislamu yakusanyika Tahrir Square

mwandamanaji katika eneo la Tahrir square

Makundi ya kiislamu nchini Misri yalikusanyika katika eneo la Tahrir Square mwishoni mwa juma yakitaka kuwepo kwa taifa linaloongozwa na sheria za kiislamu za Sharia.Kulingana mkurugenzi wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa mjini Cairo Khawala Matter ni kuwa mkutano huo uliandaliwa na makundi yanayounga mkono demokrasia ili kuitisha mabadiliko ya haraka na kuandikwa [...]

01/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Oparesheni ya Israel yasababisha vifo vya Wapalestina wawili

watoto wakipalestina katika eneo la West Bank

Mratibu wa masuala ya amani kwenye eneo la mashariki ya kati Robert Serry ametoa wito kwa utawala nchini Israel kujizuia baada ya Wapalestina wawili kuuawa wakati wa oparesheni ya kijeshi kwenye kambi moja katika eneo la West Bank. Wanajeshi watano wa Israel nao pia walijeruhiwa kwenye oparesheni hiyo iliyoendeshwa na wanajeshi wa Isreal kwa madai [...]

01/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama larefusha muda kwa vikosi vya UNAMID kuendelea kusalia Sudan

UNAMID inasambaza maji kwa watoto katika El Srief, nchini Sudan

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limerusha muda wa kuendelea kusalia vikosi vyake vya ulinzi wa amani huko Darfur vikosi ambavyo vinafanya kazi kwa nguvu ya pamoja baina ya Umoja huo wa Mataifa na Umoja wa Afrika.Vikosi hivyo UNAMID sasa vimeongezewa muda wa mwaka mmoja zaidi ili kuendelea na operesheni zake za amani katika [...]

01/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ECOSOC yataka utekelezwaji wa malengo ya kielimu

Lazarous Kapambwe-Rais wa baraza la uchumi na kijamii la uUM

Rais wa baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa Lazarous Kapambwe ametaka kuwepo kwa shabaya ya dhati juu ya utekelezwaji wa maazimio yaliyofikiwa na baraza hilo ambalo liliweka zingatio la uimaishwaji wa mifumo ya elimu kw amaelezo kuwa ndiyo mwarubaini wa kukabiliana na tatizo la umaskini unaoikabili dunia. Rais huyo wa ECOSOC amesema [...]

01/08/2011 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ataka mafungamano zaidi ya kirafiki

friends

Kwenye siku ya kwanza ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya urafiki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon imeitolea mwito jamii ya kimataifa juu ya kile alichotaka ujenzi wa amani mpya ili kuleta ustawi wa maridhiano kwa dunia.Amesema kufikia shabaya ya kuwa na dunia yenye mafungamano ya mafanikio lazima kwanza wanajamii kutambua umuhimu [...]

01/08/2011 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Makabiliano yashuhudiwa kati ya vikosi vya Lebanon na Israel

mlinda amani wa UNIFIL

Umoja wa Mataifa unasema kuwa umeanzisha uchunguzi kufuatia ufyatulianaji wa risasi uliotokea mapema leo kati ya wanajeshi wa Lebanon na Israel kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili. (SAUTI YA MAUREEN KOECH) Kulingana na kikosi cha kulinda amani nchini Lebanon UNIFIL, ufyatulianaji huo ulitokea katika eneo lijulikanalo kama Blue Line linalotenganisha hizo hizo mbili. Kamanda [...]

01/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mauaji yanayoendeshwa na wanajeshi wa serikali nchini Syria

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kushangazwa kwake na ripoti kutoka nchini Syria kuwa mamia ya waandamanaji wameuawa kwenye mji wa Hama na miji mingine kote nchini Syria. Ban amelaani vikali matumizi ya nguvu dhidi ya raia na kutoa wito kwa serikali ya Syria kusitisha ghasia hizo mara moja. Ban amesema kuwa serikali ya [...]

01/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria za kuzuia uchafuzi wa bahari katika eneo la Antarctica kuanza kutekeleza leo

unep-antartica

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO limesema kuwa marufuku iliyowekwa ya kuzuia uchafuzi wa mazingira kutoka kwa bidhaa za mafuta katika eneo la Antarctic imeanza kutekelezwa hii leo. Shirika hilo limesema kuwa mabadiliko kwenye mkataba wa kuzuia uchafuzi wa mazingira kutoka kwa meli unaeleza ni aina gani ya mafuta ambayo [...]

01/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

India yataka kusitishwa mapigano nchini Libya wakati wa mwezi wa Ramadhan

H.E Mr. Hardeep Singh PURI

India imetoa wito wa kusitishwa mapigano nchini Libya wakati wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan inapochukua urais wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa sasa mapigano yanaendeklea kwenye taifa hilo la kaskazini mwa Afrika wakati waasi wanapojaribu kumuondoa madarakani rais Muammar Gadhafi. Mwezi Machi mwaka huu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa [...]

01/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya njaa yaweza kusambaa:yaonya Umoja wa Mataifa

Valarie Amos

Mratibu wa masuala ya kibinadamu kwenye moja wa Matifa Valeria Amos hii leo anatarajiwa kuwahutubia waandishi wa habari hapa kwenye kikao kikuu cha Umoja wa Mataifa kuhusu hali katika pembe ya Africa. Umoja wa Mataifa unaonya kuwa njaa kwenye maeneo mawili nchini Somalia itasambaa katika eneo lote la kusini kwa muda wa mwezi mmoja au [...]

01/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unyonyeshaji wa watoto wapunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano

mama amnyonyesha mwanae

Wakati kunaposherehekewa wiki ya kunyonyesha duniani shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeungana na washirika wake kote duniani likitoa wito wa kutangazwa kwa Umma manufaa ya kumnyonyesha mtoto ili kuhakikisha kuwa vijana kwenye nchi zinazoendelea na zilizostawi wanaelewa umuhimu wa kunyonyesha mtoto kabla hawajakuwa wazazi. Unyonyeshaji unaaminika kuchangia katika kupunguza vifo vya [...]

01/08/2011 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930