Afya ya wanawake na watoto muhimu kwa maendeleo:Migiro

Asha-Rose Migiro

Kuwekeza katika afya ya wanawake na watoto kunasaidia kuchagiza maendeleo na kujenga jamii bora zenye matumaini.

Hayo yamesemwa na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro akilieleza baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii leo lililokuwa likijadili lengo la maendeleo la milenia la kutokomeza umasikini na njaa ifikapo mwaka 2015

Bi Migiro amesema katika wakati ambapo serikali nyingi zinabana matumizi na kupunguza huduma za jamii ni muhimu kuendelea kwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye.

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)

Ni lazima tuangalie yale yatakayotoa faida mara nyingi pale tunapoweza. Na hakuna kilicho muhimu, na kilicho na faida kama kuwekeza kwenye afya ya wanawake na watoto. Wanawake wenye afya njema huzaa watoto wenye afya bora ambao watahudhuria shule na kuwa sehemu ya nguvu kazi. Nguvukazi yenye afya inazalisha vyema, inaweza kutimiza wajibu wake wa ujenzi wa jamii zenye matumaini mazuri.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930