Nyumbani » 31/03/2010 Entries posted on “Machi, 2010”

Dola bilioni 8 zimeahidiwa leo kwenye mkutano wa kuisaidia Haiti

haiti-conference

Nchi na mashirika mbalimbali wameahidi kutoa zaidi ya dola bilioni nane hii leo ili kuisaidia Haiti katika ujenzi mpya baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi.

31/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nusu ya watu wa Niger wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula

Nusu ya watu wa Niger wanakabiliwa na matatizo makubwa ya chakula kutokana na mvua za masika kutonyesha na mavuno hafifu mwaka jana.

31/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO imetoa wito wa kuwepo na mfumo wa haki kwa wafanyakazi wahamiaji

Utafiti uliofanywa na shirika la kazi duniani ILO wakati huu wa mtafaruku wa kiuchimi duniani umeainisha kuwa kuna haja ya kuwa na mtazamo wa haki ili kuwapa usawa wafanyakazi wahamiaji milioni 105 kote duniani.

31/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umeonya kuwa ahadi za kupungua gesi ya viwanda hazitoshi kufikia malengo ifikapo 2020

Katibu mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa Yvo de Boer amesema ahadi zilizotolewa na nchi mbalimbali kupunguza gesi za viwandani hazitoshelezi kufikia malengo ifikapo mwaka 2020.

31/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICRC imeridhishwa na kuachiliwa kwa mateka mwingine wa Colombia

redcross-cn

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu ICRC, limesema limeridhika na limefurahishwa na kuachiliwa kwa Sajenti Pablo Moncayo.

31/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa wahisani kuisaidia Haiti umeanza leo mjini New York

Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 130 leo wameanza mkutano katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York kwa lengo la kukusanya fedha za kuisaidia Haiti baada ya kukubwa na tetemeko la ardhi mwezi Januari.

31/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haiti inahitaji dola bilioni 11ili kujijenga upya katika miaka kumi ijayo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo katika mkutano wa wahisani hapa New York amesema katika miaka kumi ijayo Haiti itahitaji dola bilioni 11 kujijenga upya baada ya tetemeko la ardhi la Januari.

31/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yatoa ruksa kufanyika uchunguzi wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya

icc-chamber

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoko The Hague Uholanzi leo limetoa ruksa kwa ombi la waendesha mashitaka kuchunguza uhalifu dhidi ya binadamu unaodaiwa kufanyika Kenya katika ghasia za baada ua uchaguzi mkuu miaka miwili iliyopita.

31/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa unachunguza mauaji ya raia yanayoendelea Congo RDC

Umoja wa Mataifa unaendelea na uchunguzi wake kufuatia kundi la Lords Resistance Army kufanya mauaji ya raia Kaskazini Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya congo Desemba mwaka 2009.

30/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM imezindua wavuti Georgia kuwasaidia wanaotaka kuwa wahamiaji

mapa-georgia-rusia

Wakati huohuo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linazindua wavuti nchini Georgia kuwasaidia wanaotaka kuwa wahamiaji kufanya uamuzi wa mipango yao ya kusafiri ng’ambo kutafuta kazi.

30/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shirika la IOM linawasaidia waathirika tetemeko la ardhi Chile

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Chile linampango wa kuzisaidia familia 2100 zilizoathirika na tetemeko la ardhi la Februari 27.

30/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

El-nino bado inaendelea kuathiri sehemu mbalimbali duniani

Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO limesema matukio ya Elnino yanaendelea kusambaa na kuwa na athari kubwa.

30/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujenzi mpya wa Haiti hautofanikiwa endapo haki za binadamu zitapuuzwa

Mtaalamu binafsi wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Haiti leo amesema endapo haki za binadamu zitapuuzwa nchni humo basi ujenzi mpya hautofanikiwa.

30/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wiki chache zijazo ni muhimu sana katika historia ya Sudan

Haile Menkerios ASSISTANT SECRETARY-GENERAL FOR POLITICAL AFFAIRS. UN Photo/UN Spanish Radio

Mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Haile Menkerios amesema wiki chache zijazo ni muhimu sana katika historia ya Sudan tangu nchi hiyo ipate uhuru.

30/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukaji wa haki za binadamu unachangia umasikini mkubwa Afganistan

afghan-streets1

Ripoti ya ofisi ya kamishna mkuu wa tume ya haki za binadamu iliyochapishwa leo inasema ukiukaji wa haki za binadamu unaongeza ufukara nchini Afghanistan.

30/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwanajeshi ameachiliwa huru kwa msaada wa chama cha msalaba mwekundu

daniel-calvo

Mwanajeshi wa Colombia aliyekuwa akishikiliwa na wapiganaji wa kundi la Armed Forces of Colombia (FARC) ameachiliwa huru kwa msaada wa kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC.

29/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vikwazo vya usafiri kwa wetu wenye virusi vya HIV viondolewe:UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS na wabunge kutoka kote duniani wamezitaka serikali kuondoa vikwazo vya usafiri kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV.

29/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waziri mkuu wa Iraq aukosoa UM kwa kutounga mkono kuhesabu upya kura

Waziri mkuu wa Iraq ameukosoa Umoja wa Mataifa kwa kutounga mkono madai yake ya kutaka kura za uchaguzi wa bunge wa Machi 7 zihesabiwe upya.

29/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabomu zaidi ya 1700 yameteguliwa na UNAMA nchini Afghanistan

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Afghanistan UNAMA umesema miezi miwili ya mwanzo ya mwaka huu wa 2010 umetegua mabomu zaidi ya 1,700.

29/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikwazo dhidi ya Iran itakuwa ajenda kuu kwenye mkutano wa G-8 leo

Waziri wa mambo ya nje wa Canada amesema mipango ya nyuklia ya Iran inatia mashaka na ndio itakuwa ajenda kuu kwenye kikao cha mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi nane tajiri duniani G-8.

29/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulio la kigaidi lauwa zaidi ya watu 30 mjini Moscow Urusi

Mashambulio mawili ya mabomu leo yameukumba mfumo wa usafiri wa treni za chini ya ardhi mjini Moscow Urusi na kukatili maisha ya watu zaidi ya 30 na wengine wengi kujeruhiwa.

29/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tathimini yafanywa kuhusu WHO ilivyokabiliana na homa ya mafua ya H1N1

Kamati ya kujitegemea itathimini jinsi shirika la afya duniani WHO lilivyokabiliana na homa ya mafua ya H1N1.

29/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu limepitisha hatua za kuisaidia Congo DRC na Guinea

Baraza la haki za binadamu leo limepitisha masuala saba muhimu ikiwemo njia za kuzisaidia kiufundi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Guinea.

26/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR imerejea saada Yemen baada ya miezi minane

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limepata fursa kuingia kwenye jimbo la Saada Yemen kwa mara ya kwanza tangu kuzuka machafuko mwezi Agust mwaka jana.

26/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu limeelezea hofu yake juu ya sheria za uchaguzi Myanmar

Human Rights Council

Baraza la haki za binadamu leo limepitisha azimio la kuelezea wasiwasi wake juu ya sheria za uchaguzi nchini Myanmar.

26/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimatifa wa ukuaji wa miji na makazi umemalizika Rio de Jeneiro

Russian Radio

Mkutano huo uliomalizika Ijumaa Machi 26 umetoka na maazimio mbalimbali likiwemo la kuzisaidia serikali za nchi zinazoendelea kufikia malengo ya miji bora. Miji mingi katika nchi zinazoendelea hususani Afrika haiko katika mpangilio unaofaa, kwani nyumba zimejengwa kiholela na huduma muhimu ni nadra kupatikana au hakuna kabisa. Tunazungumza na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya [...]

26/03/2010 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Usaili wa maombi ya ukimbizi barani Ulaya umebainika kuwa na dosari

Nembo ya UNHCR

Utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR umebaini kuwa mfumo unaotumiwa na nchi za umoja wa Ulaya kusaili wanaoomba hifadhi ya ukimbizi una dosari.

26/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu karibu milioni moja wanakabiliwa na upungufu wa chakula nchini Uganda

Mfumo wa tahadhari ya mapema ya baa la njaa FEWS Net umesema takribani watu laki tisa katika eneo la Karamoja Kaskazini Mashariki mwa Uganda wanakabiliwa na upunguvu wa chakula.

26/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO inakabiliwa na upungufu wa fedha za kuisaidia Somalia

somalia

Shirika la afya duniani WHO linakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha katika mradi wake wa dharura wa kuisaidia Somalia.

26/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ki-moon yuko ziarani Libya kuhudhuria mkutano wa jumuia ya nchi za kiarabu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili nchini Libya leo asubuhi kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa jumuiya ya nchi za Kiarabu. Mkutano huo unaanza kesho.

26/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uharibifu wa misitu duniani umepungua lakini bado ni tatizo kwa nchi nyingi

Hali ya uharibifu wa misiti duniani imepungua kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita,lakini ukataji miti unaendelea katika nchi nyingi.

25/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya kumbukumbu ya waathirika wa biashara ya utumwa duniani

slavery

Katika kuadhimisha siku ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema utumwa na matendo ya kitumwa bado yanaendelea katika sehemu mbalimbali duniani.

25/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umetoa wito wa Afghanistan kufuta sheria inalowalinda wahalifu wa kivita

Umoja wa Mataifa leo umetoa wito kwa Afghanistan kuifuta sheria yenye utata ya msamaha ambayo inatumika kama ngao ya kutowahukumu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wa kivita.

25/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa siku mbili wa uchumi na maendeleo umemalizika New York

Umoja wa Mataifa una jukumu kubwa la kuhakikisha nchi mbalimbali zinahusishwa katika mchakato wa kujua umuhimu wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo.

25/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO inachunguza madai ya kuzuka ugonjwa wa ndui nchini Uganda

Shirika la afya duniani WHO limekuwa likifanya kazi kwa karibu na wizara ya afya ya Uganda kufuatilia visa vinavyodaiwa kuwa ni ugonjwa wa ndui.

25/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Israel imetakiwa kuwalipa fidia watu wa Gaza kwa uharibifu ilioufanya

Israeli strikes on gaza strip

Baraza la haki za binadamu limependekeza kwamba Israel iwalipe fidia Wapalestina kwa hasara na uharibifu walioupata wakati wa vita kwenye ukanda wa Gaza.

25/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu kuchunguza ukiukaji haki Israel na Palestina

Human Rights Council

Baraza la haki za binadamu leo limepiga kura ya kuunda kamati itakayofuatilia uchunguzi wa Israel na Palestina katika madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita.

25/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Craig David ateuliwa kuwa Balozi Mwema wa mapambano dhidi ya Kifua Kikuu (TB)

craig_david_20101

Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya pop Craig David ameteuliwa kuwa balozi mwema wa mapambano dhidi ya Kifua Kikuu (TB).

24/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya kisiasa Jerusalem ni ya vuta ni kuvute baada ya mapigano

gaza

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema hali ya kisiasa mjini Jerusalem ni ya wasiwasi kufuatia mapigano baiana ya Israel na Wapalestina.

24/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya haki za binadamu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado ni mbaya

walter

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wakimbizi wa ndani amesema hali ya haki za binadamu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado haijaimarika.

24/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa haki za binadamu anataka vikosi vya UM vipelekwe Somalia

somalia

Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufikiria tena wazo la kupeleka vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa Somalia

24/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi Sudan unajongea na hofu imeanza juu vya vitisho kwa wapinzani

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake juu ya taarifa kwamba baadhi ya wajumbe wa upinzani na wafuasi wao wanatishwa nchini Sudan.

24/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani

tb-day

Leo ni siku ya kimataifa ya ya ugonjwa wa kifua kikuu, inayoadhimishwa kila mwaka kote duniani.

24/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada ya malazi imewafikia waathirika milioni moja wa tetemeko Haiti

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC linasema robo tatu ya watu milioni 1.3 wasio na makazi kutokana na tetemeko nchini Haiti sasa wamepata msaada wa vifaa vya malazi kama mahema na nguzo za ujenzi.

24/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatma ya maisha ya sokwe barani Afrika bado iko njia panda

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP na jeshi kubwa la kimataifa la polisi INTERPOL wamesema hatma ya sokwe barani Afrika bado iko njia panda.

24/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kwa mara ya kwanza Jamhuri ya Korea imempa mkimbizi hadhi ya uraia

unhcr

Kwa mara ya kwanza tangu kupitishwa mkataba wa wakimbizi 1951 Jamuhuri ya Korea imempa mkimbizi hadhi ya uraia. Mkumbizi huyo alikuwa anatambulika nchini humo na hatua ya leo ya kumpa uraia imepongezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

23/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mpango wa kimataifa wa kuongeza nafasi za kazi utasaidia uchumi:ILO

Afisa wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi Helen Clark amesema mpango wa kazi wa kimataifa wa shirika la kazi duniani ILO utasaidia kufungua njia kwa nchi nyingi zilizoathirika na mdororo wa uchumi kuanza kujerea katika hali ya kawaida.

23/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na Ujerumani kusaidia waathirika wa kubakwa nchini Sierra Leone

Mpango wa serikali ya Ujerumani unaofadhili shirika la kimataifa la uhamiaji IOM unatoa msaada wa kiufundi na kitaalamu kwa mradi maalumu nchini Sierra Leone.

23/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa upokonyaji silaha watakiwa kuzuia kusambaa silaha za nyuklia

Mwakilishi wa Marekani kwenye mkutano wa upokonyaji silaha unaofanyika mjini Geneva, Laura Kenedy amesema mkutano huo ni lazima uwe msitari wa mbele katika kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia.

23/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afghanistan inaongoza kwa wanaoomba ukimbizi nchi za Magharibi

Imebainika kwamba idadi ya Waafghanistan wanaoomba hifadhi ya ukimbizi katika nchi za magharibi zilizoendelea kiviwanda imeongezeka karibu mara mbili mwaka uliopita.

23/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unasema uko Afghanistan kwa ajili ya kusaidia sio kutawala

Peacekeeping - UNAMI

Mwakilsi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Staffan de Mistura amesema watu wa Afghanistan wameteseka kiasi cha kutosha katika miongo miwili iliyopita.

23/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa

Leo ni siku ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa duniani, kauli mbiu ikiwa ni miaka 60 ya huduma kwa ajili ya maisha na usalama wako”

23/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sierra Leone yachukua hatua kali kupambana na ufisadi

sierra-leone

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mahusiano ya kujenga amani nchini Sierra Leone UNIPSIL inasema nchi hiyo imechukua hatua kali katika miezi michache iliyopita kupambana na ufisadi.

22/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wameshawishi kiongozi wa waasi kujiunga katika mchakato wa amani

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ameshawishi kiongozi wa waasi wa Sudan kujiunga na mchakato wa amani.

22/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dr Anna Tibaijuka afafanua ripoti ya ukuaji wa miji, makazi na mitaa ya mabanda

tibaijuka

Mkutano wa tano kuhusu hali ya miji na makazi umeanza mjini Rio de Janeiro nchini Brazil, ukijumuisha washiriki kutoka kila pembe ya dunia.

22/03/2010 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Fedha zinahitajika katika kufufua uchumi na maendeleo ya Darfur

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan amesema hali ya walioathirika na machafuko ya Darfur ni mbaya na juhudi kubwa zinahitajika kuleta maendeleo ya jimbo hilo.

22/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa tano kuhusu ukuaji wa miji na makazi umeanza Brazil

tibaijuka

Mkutano wa tano kuhusu hali ya miji na makazi umefunguliwa leo mjini Rio de Janeiro nchini Brazili.

22/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shirikisho la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu kuisaidia Niger

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC imetoa wito wa msaada wa dola zaidi ya laki tisa ili kusaidia kukabiliana na hali ya upungufu wa chakula iliyotokana na mavuno mabaya mwaka jana nchini Niger.

22/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya maji duniani, na maji ni haki ya kila mmoja

Leo ni siku ya maji duniani na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNFPA katika kuazimisha siku hii, inasema kuwekeza katika maji safi kutakuwa na manufaa ya kuhakikisha mzunguko wa maisha ulio bora na jamii nzima kwa ujumla.

22/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya haki za binadamu yatathmini ripoti ya Katibu Mkuu wa UM

Human Rights Day logo

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa inatathmini ripoti ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon inayohusu eneo la Syria la Golan linalokaliwa na Israel.

22/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon ataka Israel kuondoa vikwazo dhidi ya ukanda wa Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekosoa vikwazo vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza alipokuwa ziarani jana kwenye ukanda huo uliosambaratishwa na vita.

22/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake Zanzibar wanajivunia hatua zilizopiga katika usawa wa kijinsia.

asha-juma

Makala yetu ya wiki leo inazungumzia hatua zilizopigwa katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza malengo ya Beijing.

19/03/2010 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Silaha bado zinauzwa Afrika kinyemela

Licha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa silaha bado zinaingizwa kinyemela katika maeneo ya vita Afrika. Taarifa iliyowasilishwa kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na Rosemary A Dicarlo mwakilishi wa Marekani kwa masuala ya kisiasa ya uingizaji haramu wa silaha Afrika ya Kati inasema kila mwaka maelfu ya silaha ya thamani ya mamilioni ya dola yanaingizwa kinyemela katika maeneo yenye migogoro barani Afrika.

19/03/2010 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Magonjwa ya kuambukiza yamedhibitiwa Port-au-Prince Haiti

Shirika la afya duniani WHO linasema hakujakuwa na ongezeko lolote la magonjwa ya mlipuko katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince.

19/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kwanza wa kidini kujadili ukimwi utaanza Jumatatu

HIV-AIDS logo

Viongozi wa kidini na kiroho kutoka sehemu mbalimbali duniani watakunata nchini Uholanzi kuanzia jumatatu ijayo tarehe 22 Machi hadi 23 kwa mkutano wa kwanza kabisa kuwahi kufanyika wa viongozi wa kidini kujadili ukimwi.

19/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa unawasaidia waathirika wa maporomoko Madagascar

Umoja wa Mataifa na washirika wake wanapeleka misaada ya dharura kwa watu walioathirika na maporomoko ya ardhi yaliyotokana na hali mbaya ya hewa na mvua kubwa nchini Madagascar.

19/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maji safi na salama ni haki ya kila mtoto wasema Umoja wa Mataifa

Taarifa ya pamoja iliyotolewa kwa ajili ya kuazimisha siku ya maji duniani itakayokuwa Jumatatu ijayo tarehe 22 Machi inasema maji safi ni haki ya kila mtoto.

19/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kombe la dunia litasaidia mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema michuano ya kombe la dunia la mpira wa miguu itakayofanyika mwezi June mwaka huu nchini Afrika ya Kusini itatoa fursa ya kuliangalia upya suala la ubaguzi wa rangi.

19/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo baiana ya Israel na Palestina ni chachu ya amani Mashariki ya kati

Mkutano wa kujadili hatma ya amani ya mashariki ya kati uliokuwa unafanyika Moscow Urusi umemalizika.

19/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chama cha msalaba mwekundu limethibitisha kuachiliwa kwa mfanyakazi wake Darfur:

Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC imethibitisha kwamba mmoja wa wafanyakazi wake aliyetekwa mgharibi mwa Darfur mwaka jana ameachiliwa huru.

18/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yashikamana kupigania haki za wasichana

Wajumbe wa Umoja wa mataifa wa kundi linalopigania haki za wasichana Adolescent Girls Task Force, leo kwa pamoja wametoa ombi la kuongeza juhudi la kupigania haki za binadamu kwa waasichana.

18/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kundi lingine la waasi Sudan latia saini mkataba wa amani Doha

Waasi Sudan

Maafisa wa serikali ya Sudan leo wametia saini mkataba wa kusitisha vita kwa miezi mitatu na kundi lingine la waasi la Liberation and Justice Movement (LJM).

18/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa walaani shambulio la roketi dhidi ya Israel

Israel attacks Gaza Ashkelon Israel Embassy

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la roketi lililovurumishwa leo dhidi ya Israel kutoka ukanda wa Gaza.

18/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amekutana na viongozi wa Urusi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mikutano na Rais wa Urus Demitry Medvedev na waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov mjini Moscow.

18/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO imestushwa na moto ulioteketeza makumbusho Uganda

uganda-unesco

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaoshughulikia masuala ya elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ameelezea huzuni yake kufuatia moto ulioteketeza makaburi ya wafalme wa Uganda ambayo ni moja ya maeneo yaliyoorodheshwa kama urithi wa dunia nchini Uganda.

18/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu milioni 200 wamekwepa kuishi katika mitaa ya mabanda

Russian Radio

Ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT inayoelezea hali ya miji duniani kwa mwaka 2010/2011 inasema, watu milioni 227 wameepuka maisha ya mitaa ya mabanda katika muongo mmoja uliopita.

18/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon ataka itikadi kali zikomeshwe kote duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito kwa watu kukataa itikadi kali. Na amesema nchi zaidi ya 100 wanachama wa kundi la nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) zinajukumu kubwa katika kuchagiza maelewano katika jamii.

17/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tatizo la ubakaji DRC linaathiri wanawake na jamii kwa ujumla

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA linasema matatizo ya ukatili wa kimapenzi dhidi ya wanawake nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni makubwa na athari zake sio kwa wanawake tuu bali hata kwa jamii nzima.

17/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF imeipa msaada wa vifaa vya shule Jamuhuri ya Afrika ya Kati

books

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati limekabidhi vitabu vya hesaabu elfu 60,vya Kifaransa elfu 60 na vya muongozo wa walimu elfu mbili na mia nne kwa wizara ya elimu, elimu ya juu na kitengo cha utafiti.

17/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon kukutana kuzungumza na viongozi wa Urusi Moscow

moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili mjini Moscow kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Urusi kuhusu mahusiano katika muundo wa Umoja wa Mataifa.

17/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazochafua zaidi mazingira ziko tayari kuwajibika

Cutting Fossil Fuel Subsidies Can Cut Greenhouse Gas Emissions Says UN Environment Report UNEP

Nchi ambazo zinahusika na uchafuzi wa mazingira kutokana na gesi ya viwandani kwa zaidi ya robo, sasa zimeamua kuunga mkono mkataba ulioafikiwa kwenye mkutano wa mwaka jana Copenhagen Denmark.

17/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko Somalia yanaiweka amani ya nchi hiyo njia panda

Ripoti ya kamati ya baraza la usalama kuhusu Somalia na Eritrea iliyowasilishwa leo inasema shughuli za kuleta amani na usalama nchini Somalia zinakabiliwa na vizingiti vingi ukiwemo ufisadi katika taasisi za serikali.

17/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshauri wa UM wa kuzuia mauaji ya kimbari amekwenda Afrika magharibi

Mshauri maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Kimbari amekwenda Afrika ya magharibi leo.

17/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya misaada yanajitahidi kufikia malengo Haiti

Mashirika ya misaada yanafanya kila juhudi kugawa misaada inayohitajika kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Haiti ili kufikia malengo ya tarehe mosi May.

16/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kina mama Sierra Leone yaiuzia WFP chakula

Jumuiya ya kina mama wakulima wa mbogamboga nchini Sierra Leone iitwayo Koinadugu women’s vegetable farmers cooperative, kwa mara ya kwanza imeliuzia mchele shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

16/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umezindua jopo la kuangalia masuala ya kulinda amani

peace

Umoja wa Mataifa unaimarisha mipango yake ya kulinda amani kwa kuanzisha jopo la ushauri litakalotathmini shughuli za kimataifa za kulinda amani.

16/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malengo ya milenia lazima yafikiwe asema Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema bado kuna kazi ngumu ya kuhakikisha malengo ya milenia yanatimizwa.

16/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Somalia yaanza kupiga hatua kuelekea amani ya kudumu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Ahmedou Ould-Abdallah ameipongeza serikali ya mpito ya Somalia na kundi la Ahlu Sunnah wal Jamaa kwa kutia saini rasmi makubaliano ya amani kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika.

16/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahaka ya ICTR imepupilia mbali rufaa ya Leonidas Nshogoza

ictr

Kitengo cha rufaa cha mahakama ya kimataifa inayohukumu kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ICTR iliyoko Arusha Tanzania leo imetupilia mbali rufaa ya wakili wa zamani aliyetaka hukumu yake ibadilishwe au kifungo kipunguzwe.

16/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wa hali ya hewa wa Afrika kukutana kwa mara ya kwanza

climate-change-logo-k

Mawaziri wanaohusika na masuala ya hali ya hewa kutoka barani Afrika watakutana kwa mara ya kwanza katikati ya mwezi Aprili kuanzia tarehe 12 hadi 16 mjini Nairobi Kenya.

16/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upinzani Sudan walalamika kwa Ban Ki-moon kuhusu uchaguzi

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Umma Reform and renewal Party (URRP) nchini Sudan Mubarak Al-Fadil amemtumia barua rasmi ya malalamiko katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

16/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tovuti kutumika katika kampeni ya kupambana na malaria

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria leo amezindua kundi jipya la watumiaji wa tovuti ,kuchagiza na kushirikisha vyombo vya habari na wasikilizaji,watazamaji na wasomaji wao katika vita dhidi ya malaria.

16/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

serikali ya Junta Myanmar bado inakiuka haki za binadamu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Myanmar Tomas Ojea Quintana ameongeza shinikizo dhini ya serikali ya Junta ya Myanmar.

15/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamhuri ya Korea yanyooshewa kidole kuhusu haki za binadamu

korea

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu imeisonta kidole Jamuhuri ya watu wa Korea kwa ukiukaji wa haki.

15/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanasayansi wanakutana kujadili biashara ya vitu vitokanavyo na mimea

CITES (the Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Fauna and Flora) is an international agreement between governments. Its aim is to ensure that international trade in specimens of wild animals and plants does not threaten their su CITES - Spanish Radio

Wanasayansi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanakutana Doha Qatar kujadili biashara ya kimataifa ya viumbe vilivyoko katika hatari ya kutoweka Flora na Fauna.

15/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haiti bado inahitaji msaada kurejea katika maisha ya kawaida

ban-ki-moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Haiti bado inakabiliwa na hali ngumu na matatizo makubwa , na juhudi kubwa za msaada zinahitajika kuikwamua katika hali hiyo.

15/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa magereza Sudan

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika nchini Sudan UNAMID kwa kushirikiana na mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNDP na na uongozi wa magereza wa Darfur kaskazini wameanza mpango mpya wa mafunzo kwa wafanyakazi wa magereza na wafanyakazi wa jamii.

15/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia iko mbioni kufikia malengo ya milenia ya maji safi ya kunywa

maji

Shirika la afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamesema hivi sasa asilimia 87 ya watu wote duniani ambayo ni karibu watu bilioni 5.9 wanatumia maji safi ya kunywa.

15/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haiti inakabiliwa na matatizo makubwa ya mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la linalohusika na mazingira UNEP limesema Haiti inakabiliwa na changamoto kubwa za mazingira baada ya tetemeko la ardhi la Januari 12.

12/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kusaidia kufufua mchakato wa uchaguzi Ivory Coast

Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast leo amekutana na rais mpya wa tume ya uchaguzi katika nia ya kuupa nguvu mchakato wa uchaguzi, ambao umecheleweshwa zaidi na maandamano na kuvunjwa kwa serikali mwezi uliopita.

12/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yanazidi kukatili maisha ya watu Somalia

wfp-somalia2

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema watu zaidi ya 70 wameuawa wiki hii kufuatia mapigano makali baiana ya vikosi vya serikali ya mpito ya Somalia na wanamgambo mjini Moghadishu na hasa juzi na jana.

12/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko makubwa yamewaacha maelfu bila makazi Kenya: OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Kenya zimesababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo na kuwaathiri watu takribani 10,000.

12/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Israel imefunga ukingo wa magharibi kwa saa 48 kuzuia wapalestina kuingia

Israel imefunga mpaka wa Ukingo wa Magharibi ili kuwazuia Wapalestina wasiingie Israel wakihofia kuzuka kwa ghasia. Kumekuwa na mapigano baada ya sala ya leo Ijumaa katika miskiti mbalimbali mjini Jerusalem na kwengineko pia ghasia zimekuwepo wiki nzima hii.

12/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matokeo ya awali yaashiria mchuano mkali nchini Iraq

Kwa mujibu wa matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge yaliyotolewa leo nchini Iraq, waziri mkuu Nour al-Maliki anaonekana kuwa mbele kwa kura chache dhidi ya mpinzani wake wa Kishia.

12/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika imejitahidi katika usawa wa kijinsia

Makala yetu ya wiki leo inazungumzia kumalizika kwa kikao cha 54 cha wanawake hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, ambapo imebainika afrika imepiga hatua katika kumkomboa mwanamke.

12/03/2010 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wa kimataifa wahitajika kukomesha ukatili dhidi ya wanawake

violence

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ukatili dhidi ya wanawake unaharibu kabisa maisha ya watu na kuacha athari kubwa kwa jamii.

11/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zimbabwe inahitaji msaada wa haraka wa chakula

MDG. Zimbabwe. UNDP/UN Spanish Radio

Wito wa msaada wa fedha umerejewa tena ili kuwasaidia haraka maelfu ya Wazimbabwe wnaohitaji msaada wa chakula.

11/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matokeo ya awali nchini Iraq yamuweka pazuri waziri mkuu

Iraq elections Russian Radio

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge yaliyotolewa na tume ya uchaguzi nchini Iraq, yanaashiria kwamba waziri mkuu Nour al-Maliki anashinda katika majimbo mawili ya Washia kusini mwa Iraq.

11/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Timor Mashariki sasa yajivunia amani na utulivu baada ya machafuko

Jose Ramos Horta 25a

Rais wa Timor ya Mashariki Jose Ramos Horta leo ameuambia Umoja wa mataifa katika baraza la haki za ninadamu mjini Geneva kuwa, nchi yake sasa inajivunia amani na utulivu baada ya machafuko.

11/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko yawafanya maelfu kukosa makazi zambia na Msumbiji

Mvua kumbwa zinazoendelea kunyesha kaskazini mwa Msumbiji na kaskazini mwa zambia zimesababisha vina vya maji katika mito kujaa na hivyo serikali kuamua kufungua maji ya bwawa la Kariba nchini Zimbabwe na Kahora Bassa nchini Msumbiji.

11/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon aitaka Myanmar kujumuisha wapinzani katika mfumo wa kisiasa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejea wito wake kwa serikali ya Myanmar kuhakikisha pande zote zinajumuishwa katika mchakato wa kisiasa katika kuelekea uchaguzi.

11/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa shughuli zake Somalia

wfp-somalia

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa chakula duniani WFP leo umesema uko tayari kutoa ushirikiano kwa uchunguzi binafsi dhidi ya shughuli zake za misaada ya chakula nchini Somalia.

11/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 123 zahitajika kuisaidia Nepal

childrennepal

Mashirika ya misaada yametoa wito wa kupata dola milioni 123 kuwasaidia watu nchini Nepal. Fedha hizo zitafadhili miradi ya kuwasaidia zaidi ya raia milioni tatu kwa msaada wa kuokoa maisha yao ikiwa ni pamoja na chakula kwa mwaka mzima.

10/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wahofia kuzuka magonjwa baada ya mafuriko nchini Kenya

kenya

Shirika ya Umoja wa Mataifa linalohusika na kuratibu masauala ya kibinadamu OCHA linasema maeneo ya Kenya yaliyofurika hivi karibuni huenda yakakumbwa na magonjwa ya kuambukiza yatokanayo na maji.

10/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ghasia zachelewesha kampeni ya chanjo Nigeria

Polio Vaccine Africa WHO

Kampeni ya chanjo ya polio katika jimbo la Jos lililoghubikwa na ghasia katikati mwa Nigeria itachelewa kuanza.

10/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO inawasaidia walioathirika na maporomoko nchini Uganda

Mpango wa kimataifa wa dharura wa afya HAC umeidhinisha dola elfu 50 kwa shirika la afya duniani WHO nchini Uganda ili kusaidia mahitaji ya madawa na matibabu kwa walioathirika na maporomoko ya ardhi yaliyoanza tarehe 25 Februari.

10/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waasi 90 wa FDLR wauawa mashariki mwa Congo DRC

Waasi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUC umesema majeshi ya serikali mashariki mwa Congo yamewaua wanamgambo 90 wa kihutu kutoka Rwanda katika mashambulizi yaliyoanza mwezi uliopita.

10/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon alaani hatua ya Israel kuongeza makazi ya Walowezi

israel

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mipango ya Israel ya kuongeza kujenga makazi ya walowezi 1,600 katika eneo linalokaliwa la Wapalestina wanaodai kuwa na taifa lao.

10/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu lajadili haki za watoto

Baraza la haki za binadamu leo limeanza mkutano wake wa kila mwaka kuhusu haki za mtoto na ukatili wanaotendewa.

10/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chakula cha msaada kwa mamilioni ya Wasomali chatoweka

Karibu nusu ya chakula cha msaada kilicholengwa kuwafikia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa nchini Somalia kimetowekea mikoni mwa wahandisi mafisadi, wanamgambo wa Kiislam na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

10/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafunzo maalumu yazinduliwa kuinua teknolojia ya mawasiliano

cambodia-it

Umoja wa Mataifa na Cambodia leo wamezindua mafunzo ya kusaidia uwezo wa nchi hiyo wa kutumia teknolojia ya mawasiliano kwa mipango yake ya maendeleo.

09/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakulima wa Afrika wanafaidika na kuuza mazao yao nje

Wakulima wa Afrika wameanza kufaidika na ongezeko la watu kutaka chakula kisichorutubishwa na madawa.

09/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ongezeko la wanawake kumiliki ardhi ni muhimu sana:FAO

FAO. Internaional Day of Rural Women.  FAO/UN Spanish Radio

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema ongezeko la wanawake katika umilikaji ardhi ni muhimu sana hasa katika mapambano dhidi ya umasikini na njaa.

09/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa haki za binadamu amesema amestushwa na mauaji Nigeria

nigeria

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo amesema ameshtushwa na mauaji yaliyofanyika nchini Nigeria. Amesema eneo hilo lilipaswa kulindwa vyema ili kuzuia mauaji hayo ya kikatili.

09/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unahitaji dola milioni 59 kuwasaidia wakimbizi wa DR Congo

drc-refugees

Umoja wa Mataifa na washirika wake leo umezindua wito wa kuomba dola zipatazo milioni 59 ili kusaidia mahitaji ya haraka ya wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

09/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO inatoa utaratibu mpya wa kutibu malaria

malaria

Shirika la Afya Duniani WHO linatoa utaratibu mpya wa matibabu ya malaria . Utaratibu huo utakuwa ni wa kwanza ulio salama wa dawa za kuzuia malaria.

09/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa Umoja wa Mataifa aruhusiwa kuzuru Gaza

Wizara ya mambo ya nje ya Israel jana iliamua kulikubali ombi la katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwakilishi wa sera za nje wa umoja wa Ulaya Catherine Ashton la kuzuru Ukanda wa Gaza.

09/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wawakumbuka wafanyakazi wake waliokufa Haiti

Memorial Ceremony

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na familia za watu 101 waliofariki dunia katika tetemeko la Januari nchini Haiti, leo wamekusanyika katika makao makuu ya UM mjini New York kuwakumbuka wahanga hao na pia kukumbuka pigo kubwa kabisa la kupoteza watu wengi kwa mara moja katika historia ya Umoja wa Mataifa.

09/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu mkuu wa UM ahofia mauaji yaliyotokea Nigeria

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema anahofia ghasia za kidini katika mji wa Jos nchini Nigeria ambazo zmekatili maisha ya mamia ya watu.

08/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaahidi nafasi zaidi za wanawake katika uongozi

jenista

Wakati siku ya wanawake kimataifa imeazimishwa leo kote duniani, Tanzania kuna mambo ya kujivunia na pia changamoto ambazo bado zinahitaji juhudi kufikia malengo ya Beijing ya ukombozi wa mwanamke.

08/03/2010 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban ki-moon ahitimisha ziara Chile na kuahidi msaada

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehitimisha ziara yake katika maeneo yaliyoathirika nchini Chile, kwa ahadi ya kuisaidia nchi hiyo katika juhudi za kurejea katika maisha ya kawaida baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi.

08/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakosoa mfumo wa upekuzi katika viwanja vya ndege

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema matumizi ya mashine za upekuzi wa mwili katika viwanya vya ndege kufuatia jaribio la shambulio la kigaidi siku ya Krismas mwaka jana, ni hatua za kisiasa zaidi kuliko hatua muafa za kiusalama.

08/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watalaamu wa mateso walezea yanayotendeka

Mwakilishi maalumu kuhusu masuala ya mateso Manfred Nowak leo ameliambia baraza la haki za binadamu katika ripoti yake kwamba mfumo wa mateso, hali isiyo ya kibinadamu katika mahabusu za polisi na kutokuwepo kwa ushirikiano wa serikali ndio yanayoendelea Equatorial Guinea.

08/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya kimatifa ya wanwake

Siku ya kimataifa ya wanawake

Leo ni siku ya wanawake duniani, na siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.

08/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya nusu ya walioathirika na tetemeko Haiti wamepata malazi

Ikiwa ni chini ya miezi miwili tangu tetemeko kubwa kulitikisha eneo la kusini mwa Haiti na kuwaacha watu wapatao milioni 1.3 bila makazi, mashirika ya misaada ya kibinadamu yanayogawa vifaa kwa ajili ya malazi yanasema yamewafikia watu 650,000 ambao ni zaidi ya nusu ya waathirika.

08/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Inawezekana kutokomeza maambukizi ya HIV kwenda kwa mtoto

Lengo la kutokomeza mambukizi ya virusi vya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ifikapo mwaka 2015 ni jambo linalowezekana.

08/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serekali ya Chile imewahakikishia matababu waathirika wa tetemeko

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo atakutana na Rais wa Chile Michele Bachelet na mrithi wake ili kuwahakikishia azma ya kimataifa ya kuwasaidia baada ya kukumbwa na tetemeko.

05/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wataka marekebisho ya uwiano baina ya wakulima wadogo na wafanya biashara

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki ya chakula Oliver De Schutter amesema biashara ya kilimo inaweza kuwa kiungo muhimu katika kutambua haki ya chakula.

05/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP imelazimika kupunguza nusu ya mgao wa chakula mashuleni nchini Ivory Coast

Mpango wa chakula duniani WFP leo umesema umelazimika kupunguza nusu ya mgao wa chakula mashuleni kwa watoto zaidi ya lakini nne na nusu nchini Ivory Coast kutokana na upungufu wa fedha.

05/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabomu ya ardhini ambayo hayajaripuka Afghanistan yatia hofu

Kamati ya kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu ICRC imeelezea wasiwasi wake juu ya mabomu ya ardhini ambayo hayajaripuka na mabaki mengine ya silaha za vita nchini Afghanistan.

05/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya waliokufa Haiti haijaongezeka na misaada inaendelea kupelekwa

Ofisi ya kuratibu masauala ya kibinadamu OCHA inasema kwamba idadi ya watu waliouawa kwenye tetemeko la ardhi la Januari 12 nchini Haiti haijabadiliaka.

05/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampenii kubwa ya polio imeanza katika nchi za Afrika ya Kati na Magharibi

Polio Vaccine Africa WHO

Watoto zaidi ya milioni 85 walio chini ya umri wa miaka mitano watapata chanjo ya polio katika nchi 19 za Afrika ya magharibi na Afrika ya kati kuanzia kesho Jumamosi. Chanjo hiyo inatolewa katika kampeni kabambe yenye lengo ya kuonyesha ushirikiano baina ya nchi hizo katika nia ya kutokomeza ugonjwa huo uliosumbua kwa mwaka mzima.

05/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania imepiga hatua katika ukombozi wa mwanamke

Makala yetu ya wiki leo inazungumzia hatua zilizopigwa na nchi ya Tanzania katika kumkomboa mwanamke miaka 15 tangu mkutano wa Beijing wa 1995.

05/03/2010 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda akana mashitaka ya mauaji ya kimbari

Aliyekuwa afisa wa jeshi la Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 leo amekanusha mashitaka ya kuhusika na mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

05/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ICC yataja majina 20 ya waliohusika na machafuko Kenya

kenya-violence

Kufuatia ombi la maelezo zaidi mapema mwezi huu kutoka mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoko The Hague Uholanzi, waendesha mashitaka wake wametaja majina ya watu 20 wanaodai walihusika na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya.

04/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afisa wa UNHCR anafafanua kuhusu msaada kwa Waganda walioathirika na maporomoko.

uganda

Idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya ardhi nchini Uganda inatarajiwa kuongezeka kwani shughuli za ukozi bado zinaendelea.

04/03/2010 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Maandalizi wa msimu wa kupanda yameanza Haiti:FAO

Maaandalizi ya msimu wa kipupwe wa kupanda yameanza nchini Haiti, na ni katika juhudi za muda mrefu za kuirejesha katika hali ya kawaida nchi hiyo amesema meneja wa FAO wa mpango wa dharura wa Haiti Alex Jones.

04/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF kusaidia Waeritrea zaidi ya milioni moja 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa maombi ya msaada wa karibu dola milioni 25 ili kupanua wigo wa shughuli zake nchini Eritrea.

04/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR kuwasaidia waathirika wa maporomoko ya ardhi Uganda

Nembo ya UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekubali kutoa msaada wa dharura kwa Waganda walioachwa bila makazi kufuatia maporomoko makubwa ya ardhi mashariki mwa nchi hiyo.

04/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo Togo wanapiga kura kumchagua Rais

togo-election

Wananchi wa Togo leo wanapika kura katika uchaguzi mkuu wa Rais baada kusubiri kwa muda mrefu. Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limekuwa msitari wa mbele kuhakikisha kwamba uchaguzi wa leo wa Rais ambao siku za nyuma ulighubikwa na machafuko baada ya kuzuka utata mwaka 2005 unafanyika kwa amani na kuheshimu haki za binadamu.

04/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Japan inasema upokonyaji wa silaha za nyuklia lazima uwe na mtazamo maalumu

chinami-nishimura

Wakati huohuo mwaka huu ni muhimu saana katika kuelekea kuwa na dunia isiyo na silaha za nyuklia, wakati ukijongea mkutano wa kimataifa wa usalama wa nyuklia na kuupitia mkataba wa kutozalisha nyuklia.

04/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapendekezo ya vikwazo vipya kwa Iran yameanza kusambazwa

Mataifa muhimu ya magharibi na yenye nguvu yametuma mapendekezo ya vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa Urusi na Uchina. Vikwazo hivyo vitakilenga kikosi chenye nguvu nchini Iran cha wanamgambo wanamapinduzi, na kukaza uzi kwa vikwazo vilivyopo dhidi ya usafirishaji ,masuala ya bank na sekta ya bima.

04/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon ataka UM uwe mfano katika kuwapa nafasi wanawake

Akiwa katibu mkuu amehakikisha kumekuwa na wanawake wengi katika nafasi za juu za uongozi sasa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Umoja wa Mataifa. Miaka 15 tangu mkutano wa kimataifa wa wanawake wa Beijing amesema kuna hatua zimepigwa.

03/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zimepigwa katika kumkomboa mwanamke duniani

Kikao cha 54 cha kimataifa cha wanawake kinachojadili hali ya wanawake duniani baada ya mkutano wa Beijing kinasema hatua zimepigwa katika kumkomboa mwanamke

03/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umezindua mpango wa miaka 5 kuwasaidia wanawake kupambana na Ukimwi

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS kwa kushirikiana na msanii na mwanaharakati wa masuala ya wanawake na ukimwi Annie Lenox wamezindua mpango waliouita “Ajenda ya kuzichagiza nchi kuchukua hatua kwa ajili ya wanawake, wasichana, usawa wa kijinsia na HIV mwaka 2010 hadi 2014″.

03/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi ya 30 wameuawa nchini Iraq katika shambulio la kujitoa mhanga

Mashambulizi yaliyofuatana ya kujitoa muhanga katikati ya mji wa Bauba nchini Iraq leo, yamewaua watu 33 na kujeruhi wengine 55. Mashambulizi haya yamefanyika siku chache tuu kabla ya taifa zima kupiga kura ya uchaguzi wa bunge utakaofanyika mwishoni mwa wiki.

03/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yanayoendelea Darfur yaongeza hofu kwa wakimbizi wa ndani

Wiki kadhaa za mapigano yanayoendelea katika baadhi ya sehemu za jimbo la Darfur Sudan yameongeza wasiwasi kwa usalama wa raia, hasa baada ya ukosefu wa usalama kuyafanya mashirika ya misaada ya kibinadamu kusitisha shughuli zake katika baadhi ya sehemu.

03/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umetanga muongo mmoja wa kudhibiti usalama barabarani

Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umetangaza muongo mmoja wa kuchukua hatua za kudhibiti usalama barabarani, na kipindi hicho ni kuanzia 2011 hadi 2020.

03/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Urusi yatoa wito wa suluhu ya kidiplomasia dhidi ya mipango ya nyukilia ya Iran

Serikali ya Urusi imesema ni lazima kutafuta suluhu ya kidiplomasia kutatua masuala ya nyuklia ya Iran na cha muhimu ni kutatua mzozo huo kwa njia ya amani.

03/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati kwingineko duniani wanawake wamepiga hatua kujikomboa Congo DRC bado inasuasua

Wanawake kutoka sehemu mbalimbali duniani tangu tarehe mosi March wanakutana hapa New York kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika Kikao cha 54 cha kimataifa cha wanawake kinachojadili hali ya wanawake duniani baada ya mkutano wa Beijing .Congo DRC bado inajikongoja.

03/03/2010 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban ki-moon awataka Watogo kufanya uchaguzi kwa amani

togo-election

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amesema kwamba uchaguzi mkuu wa Rais utakaofanyika wiki hii nchini Togo ni fursa nzuri kwa nchi hiyo kuendeleza juhudi za kuleta demokrasia.

02/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ICRC imeanza kusafirisha matufaa kwenda Syria

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC leo imeanza kusafirisha matufaa kupitia Kuneitra kuvuka mpaka baiana ya eneo la Golan na Syria.

02/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa dharura wahitajika kusaidia wanafunzi Mongolia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema msaada wa haraka unahitajika kuwasaidia wanafunzi takribani 4000 katika eneo lililoathirika vibaya na msimu wa baridi nchini Mongolia.

02/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko yanawazuia raia kupata msaada Darfur

Shirika linaloratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema machafuko yanayoendelea Darfur yanasababisha maelfu ya raia kushindwa kupata msaada wanaouhitaji.

02/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO inasema maradhi ya kuambukiza yamepungua Haiti

Shirika la afya duniani WHO linasema tathimini yao inaonyesha kuwa hakuna ongezeko la maradhi ya kuambukiza nchini Haiti.

02/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watathmini hali ya Chile na kuanza kutoa msaada

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu OCHA imesema tathmini yao ya awali inaonyesha kuwa watu milioni mbili wameathirika na tetemeko la ardhi lililoikumba Chile na wengine 723 wamefariki dunia.

02/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waitaka Misri kuacha kutumia nguvu dhidi ya wahamiaji

egypt-sinai

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Navi Pillay leo ametoa wito kwa serikali ya Misri kuamuru mara moja vikosi vyake vya usalama kuacha kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wahamiaji wasiokuwa na silaha, ambao wanajaribu kuingia Israel kupitia jangwa la Sinai.

02/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa mataifa waipongeza Somalia

Mwakilishi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ameisifia serikali ya mpito ya Somalia kwa kuwa na umoja na nguvu katika mwaka mmoja wa utawala wake.

01/03/2010 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 54 cha wanawake kimeanza New York

Asha-Rose Migiro

Leo kikao cha 54 cha wanawake kimeanza hapa mjini New York Marekani. Kikao hicho kinachohudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka sehemu mbalimbali duniani na mashirika ya Umoja wa Mataifa, kitatathmini ajenda za mkutano wa Beijing uliofanyika mika 15 iliyopita.

01/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UN bado inahofia mswaada wa mapenzi ya jinsia moja Uganda

Wawakilishi maalumu wawili wa Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi wao kuhusu mswaada wa mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda.

01/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 13 cha baraza la haki za binadamu kimeanza

Baraza la usalama la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeanza kikao chake cha 13 mjini Geneva leo.

01/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za dharura zimetangazwa Chile kufuatia tetemeko la ardhi

01-03-2010-chili

Rais wa Chile Michelle Bachelete ametangaza hatua za dharura ili kukabiliana na uharibifu uliofanywa na tetemeko kubwa la ardhi siku ya Jumamosi .

01/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano mkubwa wa masuala ya Darfur wafanyika Rwanda

Leo mkutano mkubwa wa masuala ya Darfur unaosimamiwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan unafanyika mjini Kigali Rwanda.

01/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA yaonya juu ya Iran kutotoa ushirikiano wa mipango yake ya nyuklia

Mkuu wa shirika la kimataifa la masuala ya nyuklia IAEA Yukiya Amano amesema Iran haitoi ushirikiano wa kutosha kwa shirika la kimataifa la nguvu za atomic katika uchunguzi wake wa shughuli za nyuklia za Jamuhuri hiyo ya Kiislam.

01/03/2010 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930