Nyumbani » 31/12/2009 Entries posted on “Disemba, 2009”

Watetezi huru wa haki za binadamu waishtumu Thailand kwa kufukuza nchi watu wa makabila ya Hmong

Wakimbizi-IOM

Wataalamu wawili wanaowakilisha mashirika yanayotetea haki za binadamu wametangaza taarifa ya pamoja, iloilaumu vikali Serikali ya Thailand, kwa kuwahamisha kwa nguvu, wahamiaji 4,000 wa makabila ya Hmong na kuwarejesha kwenye taifa jirani la Laos, bila ya idhini yao.

31/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO inasema homa ya mafua ya H1N1 imegundiliwa kuenea zaidi Ulaya ya Mashariki kwa sasa

Nembo ya WHO

Mataifa ya Ulaya ya kati na mashariki yameripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ndio maeneo ya ulimwengu yaliosumbuliwa zaidi sasa hivi na maambukizo ya homa ya mafua.

31/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP inayashukuru mataifa kwa kusaidia kuhudumia chakula wenye njaa katika 2009

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limetoa taarifa maalumu, ya shukurani, kwa Mataifa Wanachama katika sehemu zote za dunia, kwa kazi ngumu na misaada waliochangisha katika zile huduma za kupiga vita njaa ulimwenguni mnamo 2009.

31/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu anasema “kashtushwa” na miripuko ya ghasia katika Iran

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu kwenye taarifa aliotoa kwa vyombo vya habari Ijumatano alisema ya kuwa alishtushwa na kile alichokiita “mfumko wa vifo, majeraha na watu kukamatwa” katika Jamhuri ya KiIslam ya Iran.

30/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP itaisaidia Yemen kitaaluma, kwa kupitia mtandao, kudhibiti mazingira nchini

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limetangaza kuwa litaipatia Yemen fursa ya kupokea makala muhimu za kisayansi, kwa kutumia taratibu za mtandao, ikiwa miongoni mwa miradi ya kujiendeleza na maarifa ya sayansi ya kisasa kwenye nchi zinazoendelea, katika kipindi ambacho mataifa haya huwa yanakabiliwa na matatizo kadha wa kadha, yanayozushwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

30/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa mataifa jirani katika Sudan wanahitajia huduma za msingi haraka kumudu maisha, imeonya UNHCR

Wahamiaji kutoka Sudan

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeeleza UM kwamba liliwajibika kushughulikia kihali jumla ya wahamiaji 66,000 waliomiminikia kwenye kambi za wahamiaji ziliopo Sudan mashariki, kutokea Eritrea, Ethiopia na Usomali.

30/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID/Sudan waahidi ushirikiano kuimarisha usalama Darfur

Wawakilishi wa Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) pamoja na wawakilishi wa Serikali ya Sudan wameripotiwa kutiliana sahihi makubaliano ya jumla, kuhusu mradi wa utendaji, uliokusudiwa kuhakikisha watumishi wa UNAMID pamoja na mali zao, huwa watapatiwa usalama wanaostahiki kwenye jimbo la mvutano la Sudan Magharibi la Darfur.

30/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ijumanne, wawakilishi wa kutoka Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) walitiliana sahihi na Serikali ya Sudan makubaliano ya jumla kuhusu mradi wa utendaji, uliokusudiwa kuhakikisha usalama wa watumishi wa UNAMID pamoja na mali zao. Taadhima ya utiaji sahihi mapatano haya ilifanyika kufuatilia kikao cha utendaji kazi, kilichokutana Khartoum Ijumapili ya tarehe

29/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

“Ukomeshaji wa janga la H1N1 ulimwenguni huenda ukachukua mwaka”, ameonya Mkuu wa WHO

WHO. Dr. Margaret Chan UN Spanish Radio

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwenye mahojiano mjini Geneva na gazeti la Le Temps, Ijumanne alinakiliwa akisema janga la homa ya mafua ya H1N1 halitofanikiwa kudhibitiwa kikamilifu mpaka mwaka 2011.

29/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia masikini Burundi watasaidiwa na UM kupata vitambulisho vya kura bila malipo

Raia wa Burundi milioni moja, waliotimia umri wa kupiga kura, watafadhiliwa bure vitambulisho vya uraia vitakavyowaruhusu kushiriki kwenye uchaguzi utakaofanyika nchini mwao mnamo mwezi Mei 2010.

29/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa MONUC akumbusha, vikosi vya UM katika JKK huhami maelfu ya raia kila siku

Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), na pia Mkuu wa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) kwenye makala aliochapisha mapema wiki hii, katika gazeti la kila siku la Marekani linaloitwa The Washington Times, alieleza kwamba UM huchangisha pakubwa katika kuwatekelezea haki za kimsingi, takriban kila siku, kwa maelfu ya raia wanaoishi kwenye mazingira ya wasiwasi ya JKK.

29/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakusanyisha makabila yanayohasimiana Sudan Kusini kujadiliana amani

Nembo ya UNDP

UM umeripoti hali ya wasiwasi inaendelea kuselelea kwenye jimbo la Sudan la Abyei, miaka mitano baada ya makundi yaliokuwa yakihasimiana yalipokubaliana kutia sahihi mapatano ya amani yaliosaidia kusitisha Mapigano ya Pili ya Wenyewe kwa Wenyewe ya katika Sudan.

29/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), na pia Mkuu wa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) leo alichapisha kwenye gazeti la kila siku la Marekani, linaloitwa The Washington Times, insha yenye maelezo maalumu yaliokumbusha mchango wa kila siku wa UM, katika kuwatekelezea maelfu ya raia haki zao za kimsingi, kwenye mazingira ya

28/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

EU imechangisha Yuro milioni 5.5 kuisaidia UNRWA kuimarisha afya bora kwa wakazi wa Tarafa ya Ghaza

Ijumatatu, Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kufadhilia msaada wa Yuro milioni 5.5 kulipa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kihali kwa WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) uliokusudiwa kuhudumia miradi ya afya na mazingira safi kwenye Tarafa ya Ghaza.

28/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuzorotwa kwa suluhu Ghaza, mwaka mmoja baada ya mapambano, kwahatarisha maisha ya umma, anasema KM

Tarehe ya leo, inakamilisha mwaka mmoja tangu majeshi ya Israel yalipovamia eneo la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza, mnamo Disemba 27 mwaka 2008, ambapo kwa wiki tatu kuliendelezwa operesheni za kijeshi zilizopewa jina la “Operesheni ya Kumwaga Risasi”.

28/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lafanikiwa kupitisha bajeti la 2010-2011 kwa shughuli za UM

Alkhamisi iliopita, Baraza Kuu la UM lilifanikiwa kupitisha bajeti la UM kwa miaka miwili ijayo, miaka ya 2010-2011, bajeti ambalo linagharamiwa dola bilioni 5.16.

28/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hekaheka za Mkutano wa COP15 zazingatiwa na mtaalamu wa kimazingira kutoka Tanzania

Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen, au Mkutano wa COP15, uliofanyika mwezi Disemba, na yaliochukua wiki mbili, yalipambwa na michuano, mivutano na mabishano yasiotarajiwa juu ya itifaki ya kuzingatiwa na wajumbe wa kimataifa, ili kuimarisha kipamoja Mkataba wa Kyoto, na kuyasaidia Mataifa Wanachama kuwa na chombo cha sheria ya kudhibiti bora athari zinazozalishwa na hali ya hewa ya kigeugeu.

24/12/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi Huru wa Haki za Wafalastina atoa mwito kwa marafiki wa Israel kuishinikiza ikomeshe, halan, vikwazo angamizi dhidi ya umma wa Ghaza

Richard Falk, Mtetezi Maalumu wa UM juu ya Haki za Wafalastina wa Maeneo Yaliokaliwa Kiamabavu na Israel, kwenye taarifa aliotoa kabla ya kumbukumbu ya kutimia mwaka mmoja wa uvamizi wa vikosi vya Israel katika Tarafa ya Ghaza, alisihi mataifa rafiki wa Israel ya Amerika ya Kaskazini na Ulaya kutumia vitisho vya kuweka vikwazo vya kiuchumi [...]

24/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNICEF anajiandaa kumaliza kazi mapema

Ann Veneman Unicef 019a

KM Ban Ki-moon, ametangaza taarifa ya masikitiko yenye kueleza Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kwamba hana azma ya kuendelea kazi tena baada ya muda wake kumalizika.

24/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID kujihusisha na huduma za kuwasaidia vijana Sudan kuelewana kwa amani

Vikosi vya Mchanganyiko vya UA-UM kwa Darfur (UNAMID) vimeripoti kuwa vitaisaidia Wizara ya Ilmu ya Sudan, kuandaa Mashindano ya 21 ya Taifa, ambapo wanafunzi 7,000 ziada, wanaowakilisha skuli za sekandari za kutoka majimbo 25 ya Sudan hushiriki kwenye mashindano ya kitaaluma na riadha.

24/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

BU lapitisha azimio kuidhinisha MONUC kutumia “nyenzo zote za lazima” kuwahami raia katika JKK

Ijumatano wajumbe wa Baraza la Usalama (BU), wanaowakilisha mataifa wanachama 15, walipitisha, kwa kauli moja, azimio lenye kuruhusu Vikosi vya Ulinzi Amani vya UM katika JKK (MONUC), kutumia “uwezo wote walionao”, chini ya Mlango wa VII wa Mkataba wa UM, unaoruhusu kutumia nguvu, ili kuwapatia raia hifadhi wanayostahiki, dhidi ya mashambulio kutoka makundi yote yenye kuhatarisha usalama wao.

24/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa misaada ya dharura ahimiza hifadhi bora kwa raia wa JKK dhidi ya mashambulio ya waasi wa LRA

John Holmes, Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu na Mratibu wa Misaada ya Dharura, ametoa mwito maalumu unaopendekeza jamii ya kimataifa ichukue hatua za nguvu zaidi zitakazohakikisha raia wanaokabiliwa na hatari ya kushambuliwa na waasi wa Uganda, wa kundi la LRA, huwa wanapatiwa ulinzi na hifadhi inayofaa kuwanusuru kimaisha.

24/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Baraza Kuu Alkhamisi limepitisha bajeti la UM kwa 2010-2011, linalogharamiwa dola bilioni 5.16, hatua iliopongezwa na KM Ban Ki-moon kwa kukamilishwa kwa wakati. Kwa mujibu wa taaarifa iliotolewa kwa waandishi habari, Msemaji wa KM alisema Mkuu wa UM, binafsi, aliahidi “mchango wa bajeti liliopitishwa

24/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Mashirika ya UM yanayohudumia misaada ya kiutu wiki hii yameanza kufarajia vifaa vya kunusuru maisha katika Malawi kaskazini, kufuatia mitetemeko ya ardhi iliopiga huko mwezi huu na kuua watu wanne, kujeruhi watu 300 ziada na kuharibu au kubomoa nyumba karibu 4,000. Wilaya ya Karonga, Malawi kaskazini iliathirika vibaya zaidi kufuatia msururu wa zilzala zilizopiga kuanzia tarehe 06 mpaka 20 Disemba, mitetemeko iliokadiriwa kuvuka vipimo vya baina ya 5.4 na 6.0 Richter, kwa mujibu wa taarifa ya Shrika la UM juuya Misaada ya Dharura (OCHA). Tume ya kiufundi ya pamoja, ikijumuisha watumishi wa shirika la UM juu ya maendeleo ya watoto, UNICEF; miradi ya chakula, WFP; huduma za chakula na kilimo, FAO, pamoja na taasisi juu ya udhibiti wa watu, UNFPA Ijumatano walielekea Karonga kufanya tathmini halisi juu ya mahitaji ya kiutu, hasa yale yanayohusu afya na lishe, maji salama, usafi, vifaa vya ilmu na akiba ya chakula. Mashirika ya UM yanayohudumia misaada ya kiutu yameeleza kushirikiana, kwa ukaribu zaidi, na mashirika yasio ya kiserikali pamoja maofisa wa Seikali ya Malawi katika kusimamia huduma za kufarajia waathirika wa mitetemeko ya ardhi nchini.

23/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Matukio katika Baraza la Usalama

Baraza la Usalama asubuhi limepitisha azimio la kuiwekea vikwazo Eritrea. Azimio linapiga marufuku kuiuzia silaha Eritrea au kununua silaha kutoka taifa hili.

23/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM amatangaza kuteua naibu mpya wa MONUC kutoka Cote d’Ivoire

Walinzi amani wa MONUC

KM leo ametangaza kumteua Fidele Sarassoro wa Cote d’Ivoire kuwa Naibu Mjumbe Maalumu wa KM kwa Shirika la UM Kulinda Amani katika JKK (MONUC).

23/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yachapisha maelekezo kukabili utovu wa ustahamilivu na ubaguzi wa wageni wahamiaji

Nembo ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limechapisha, kutoka Geneva, leo hii maelekezo maalumu ya kutumiwa kukabili matatizo ya ubaguzi wa rangi na chuki, dhidi ya wageni, matatizo ambayo husababisha watu kuhama na kuhatarisha juhudi za UNHCR katika kuwapatia hifadhi watu waliokosa uraia, wahamiaji na wale wenye kuomba hifadhi za kisiasa.

23/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa BK asema karidhika na shughuli za kikao cha 2009

Ali Abdussalam Treki wa Libya, Raisi wa kikao cha 2009 cha Baraza Kuu (BK) la UM – kikao cha 64 – Ijumanne adhuhuri, alikuwa na mahojiano ya kufunga mwaka, na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu.

23/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

Terje Roed-Larsen, mjumbe wa UM anayehusika na utekelezaji wa Azimio 1559 (2004) la Baraza la Usalama, ameripotiwa na Msemaji wa KM, Martin Nesirky, kwamba huwa anashauriana mara kwa mara na maofisa wa Lebanon kadha pamoja na washirika wengine wa Ki-Arabu katika eneo, na vile huwa anashauriana na mataifa yote mengine yanayohusika na utekelezaji wa azimio hilo la Baraza la Usalama. Taarifa hii ilitolewa kujibu suala kujua nani hushirikiana na mjumbe wa UM juu ya utekelezaji wa Azimio husika. Azimio 1559 la Baraza la Usalama lilipopitishwa 2004 lilikusudiwa hasa kuunga mkono pendekezo la kufanyisha uchaguzi wa uraisi Lebanon, ulio huru na wa haki; na lilitilia mkazo kuondoshwa kwa "vikosi vya kigeni" viliopo Lebanon, kwa wakati huo, ikimaanisha, kwa lugha ya kidiplomasiya, vikosi vya Syria. Kwa hivi sasa Syria imekataa kabisa kujihusisha, wala kushiriki kwenye mashauriano ya aina yoyote yale yanayosimamiwa na mjumbe wa UM, Terje Roed-Larsen.

22/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO imeripoti ‘bei ya chai kwenye soko la kimataifa imevunja rikodi’

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limechapisha ripoti mpya yenye kuonyesha bei za chai duniani zimefikia kiwango kilichovunja rikodi, kwa mwaka huu.

22/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu laitisha Mkutano Mkuu mwakani kuharakisha utekelezaji wa MDGs

UN Millennium Development Goals

Baraza Kuu la UM limepitisha azimio la kuitisha, katika mwezi Septemba mwakani, mkutano mkuu, utakaohudhuriwa na wawakilishi wote wa kimataifa, kwa madhumuni ya kusailia maendeleo kwenye utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

22/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlinzi wa majengo ya UM Usomali auawa

wfptrucksomalia

UM imeripoti Ijumanne majambazi kadha walimpiga risasi na kumwua ofisa raia wa usalama nchini Usomali, aliyekuwa akitumikia Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), kitendo kilichotukia kwenye mji wa Beledweyn, Usomali.

22/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Chad Mashariki yazidi kuharibika, kuhadharisha OCHA

United Nations Mission in the Central African Republic and Chad. MINURCAT. MINURCAT/UN Spanish Radio

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali ya usalama katika Chad Mashariki inaendelea kuwa mbaya zaidi. Mnamo mwisho wa wiki iliopita, msafara wa UM wa magari matatu ya kiraia, wa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika Jamuri ya Afrika ya Kati na Chad (MINURCAT) uliohusika na ugawaji wa misaada ya kihali kwa umma waathirika wa mapigano, ulishambuliwa na majambazi wasiojulikana wanane. Ofisa mmoja wa Vikosi vya Ulinzi wa Mchanganyiko, aliyekuwa akiongoza msafara wa UM, alijeruhiwa.

22/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aweka muda kwa mataifa kutia sahihi Itifaki ya Copenhagen kudhibiti hali ya hewa ya kigeugeu

KM Ban Ki-moon jana alitangaza mwito maalumu kwa mataifa makuu, unaoyanasihi kuongeza bidii zao ili kuhakikisha, katika 2010 kutapatikana maafikiano ya kimataifa yenye sharti kisheria, juu ya udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa katika ulimwengu.

22/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Russian Radio

Msafara wa Shirika la UM juu ya Amani katika Jamhuri ya AfrIka ya Kati na Chad (MINURCAT), unaohusika na ugawaji wa vitu na watu, uliojumuisha magari ya kiraia matatu, ulishambuliwa Ijumapili na watu wanne wasiotambulika waliochukua silaha, kwenye eneo la kusini-mashariki katika Chad. Vikosi vya MINURCAT vilipelekwa haraka kwenye eneo, pamoja na wahudumia tiba ili kuokoa watumishi waliopatwa na ajali hiyo, pamoja na kuyaokoa magari ya MINURACT yalioharibiwa na mashambulio.

21/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya fujo Guinea yakabidhiwa makundi husika na KM

Msemaji wa KM ameripoti kwamba Ban Ki-moon leo amewatumia makundi kadha husika na tukio la Guinea, ripoti maalumu ya Tume ya Uchunguzi ya Kimataifa juu ya hatua kali za kinidhamu zilizochukuliwa na vikosi vya usalama dhidi ya raia waliokuwa wakiandamana, bila ya fujo, kwenye mji wa Conakry, mnamo mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo raia wanaokadiriwa 150 waliuawa, na wingi kujeruhiwa.

21/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM imelaumu vikali waasi wa LRA kwa mauaji na mateso ya raia katika JKK

Vile vile hii leo, kumewasilishwa ripoti nyengine ya apmoja ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) na Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC) kuhusu mashambulio ya kikatili yaliofanywa na waasi wa LRA katika JKK.

21/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OHCHR inasema mashambulio ya LRA Sudan Kusini ni “madhambi yanayokiuka ubinadamu”

OHCHR-Logo2

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) Ijumatatu imechapisha ripoti mpya juu ya Sudan, ilioeleza ya kwamba mashambulio katili, dhidi ya raia, yalioendelezwa na wapiganaji waasi wa Uganda wa kundi la LRA katika Sudan Kusini, ni vitendo vilivyofananishwa “sawa na makosa ya jinai dhidi ya ubinadamu.”

21/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwanaharakati wa Kenya juu ya Mazingira awakilisha maoni binafsi juu ya Mkutano wa Copenhagen

kiswahili-interviewee-small

Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen, unaojulikana kama Mkutano wa COP15, yaliendelezwa kwa wiki mbili, kwa kasi ambayo wajumbe wengi, hasa wale wa kutoka nchi zinazoendelea, walilalamika ilikuwa ni ya polepole sana, hali ambayo iliwakatisha tamaa juu ya uwezekano wa kufikia mapatano ya mwisho yanayoridhisha.

18/12/2009 | Jamii: Makala za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Tarehe ya 18 Disemba huadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Wahamaji. Risala ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), iliowasilishwa kuadhimisha siku hii, ilihimiza mataifa kuonyesha bidii za mbele zaidi, kupita Mkutano wa Copenhagen, na kukabili masuala magumu ya uhamaji unaochochewa na uharibifu wa mazingira na uchafuzi wa hali ya hewa. Taarifa ya IOM ilieleza wanasayansi wa kimataifa walishathibitisha kihakika kwamba mabadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi wa mazingira ni mambo yanayozusha uhamaji wa dharura na kusababisha watu kung’olewa mastakimu, katika sehemu mbalimbali za dunia, hasa katika nchi masikini, maeneo ambayo ndio yenye kudhurika zaidi na maafa ya kimaumbile. Kwa mujibu wa IOM kuna pengo kubwa la maarifa na uzoefu juu ya ujuzi unaofaa kushughulikiwa, ili kudhibiti vyema matokeo na athari kubwa za uhamaji unaoletwa na maafa ya kimazingira.

18/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR imetangaza watu 74,000 wa Pembe ya Afrika wamehajiri Yemen 2009 kuomba hifadhi

Nembo ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti raia 74,000 waliwasili kwenye mwambao wa taifa la Yemen mwaka huu, kutoka eneo la Pembe ya Afrika, watu waliokuwa wakikimbia hali ya mtafaruku uliozuka na kujiepusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, pamoja na uegugeu wa kisiasa, hali duni ya maisha, ikichanganyika vile vile na baa la njaa na ukame.

18/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi wa Haki za Binadamu Sahara Magharibi aruhusiwa kurejea nchini

Taarifa iliotolewa na KM Ban Ki-moon, baada ya saa sita za usiku ya Ijumaa, imeeleza kuwa amefarajika na pia kupata nafuu baada ya kupokea ripoti ilioleza mtetezi wa uhuru wa taifa la Sahara ya Magharibi, Aminatou Haidar, aliruhusiwa kurejea kwao kwenye mji mkuu wa Laayoun.

18/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yajihusisha Kenya kudhibiti mripuko wa kipindupindu Turkana Mashariki

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti Alkhamisi jioni kwamba taasisi kadha za UM zinazohudumia misaada ya kiutu, hivi sasa zinajitahidi kuipatia Serikali ya Kenya misaada ya dharura inayohitajika kupambana na mripuko wa maradhi ya kipindupindu, yaliozuka kwenye eneo la kaskazini-magharibi, ambapo tumearifiwa watu karibu 30 walifariki kutokana na ugonjwa huo, kwenye zile sehemu za mbali zenye matatizo kuzifikia.

18/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa Dunia wamo mbioni kuleta maafikiano ya kuridhisha kutoka Mkutano wa COP15

Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa UM wa kuleta mapatano yatakayosaidia Mataifa Wanachama kudhibiti bora, kipamoja, athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika ulimwengu, Ijumaa yalishindwa kuwasilisha maafikiano ya kuridhisha, yaliotarajiwa kutiwa sahihi na viongozi wa Kitaifa na serikali 120 ziada waliokusanyika sasa hivi kwenye mji wa Copenhagen, Denmark.

18/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Shughuli za Baraza la Usalama kwa Alkhamisi

Mapema asubuhi ya leo, Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza muda wa shughuli za Ofisi ya UM juu ya Mchanganisho wa Huduma za Amani Burundi (BINUB) ambazo zinatazamiwa kuendelezwa hadi mwisho wa mwaka 2010.

17/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya Kamisheni ya Uchunguzi wa vurugu la Septemba katika Guinea imekabidhiwa rasmi KM

KM amekabidhiwa ripoti ya Kamisheni Maalumu ya Uchunguzi ya Kimataifa kuhusu vyanzo vya matukio ya fujo mnamo tarehe 28 Septemba 2009 katika taifa la Afrika Magharibi la Guinea, ambapo raia wapinzani kadha waliripotiwa kuuawa kihorera na vikosi vya ulinzi, kufuatia maandamano yaliofanyika kwenye mji mkuu wa Conakry.

17/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM akutana na viongozi wanaohudhuria COP15

KM Ban Ki-moon leo alianzisha mazungumzo ya kina, ya pande mbili, na viongozi kadha wa kadha wa kimataifa, ikijumlisha Waziri Mkuu wa Uchina Wen Jinbao. Alipokutana na waandishi habari Alkhamisi,

17/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Mabadiliko ya Halihewa unanyemelea hatima

Wakati huo huo, majadiliano yameanzishwa tena kuhusu maafikiano mapya ya kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa, baada ya mzoroto na mivutano ya siku mbili baina ya mataifa yenye maendeleo ya viwanda na mataifa yanayoendelea.

17/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Matumaini yafifia juu ya itifaki ziada kutoka Mkutano wa COP15

Taarifa tulizopokea kutoka Mkutano wa COP15, zinasema matumaini ya kuwakilisha itifaki ziada, kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, yanaanza kufifia,

17/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Alkhamisi asubuhi, mataifa 11 yaliripotiwa kuidhinisha na kuridhia Mapatano ya Kimataifa ya 2006 juu ya Mbao za Tropiki (2006 International Tropical Timber Agreement). Nyaraka za Mapatano ziliokusudiwa kukabidhiwa KM, ziliwakilishwa kwenye tafrija iliofanyika katika Ofisi ya UM juu ya Masuala ya Sheria. Mataifa 11 yalioridhia Mapatano ya Mbao za Tropiki ni kama ifuatavyo: Bulgaria; Jamhuri ya Ucheki; Finland; Ujerumani, Ireland; Ureno; Romania; Slovakia; Slovenia na Uspeni. Mapatano ya Mbao za Tropiki, bado hayajakuwa chombo rasmi cha kimataifa na sasa hivi kinajumlisha Makundi Yalioridhia mapatano kutoka nchi arobaini na moja.

17/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lapitisha maazimio mawili ya Mahakama za Kimataifa na kuhusu Milima ya Jolan

Baraza la Usalama, leo asubuhi, vile vile limeptiisha maazimio matatu, kwa kauli moja. Azimio la awali liliongeza muda wa operesheni za vikosi vya UNDOF kwa miezi sita zaidi,kwenye eneo la Milima ya Jolan, katika Syria, hadi mwisho wa Juni 2010.

16/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Operesheni za kijeshi Kongo Mashariki zitakamilishwa mwisho wa mwezi, asema Baraza la Usalama limearifiwa na Mjumbe wa UM katika JKK

Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM kwa JKK, asubuhi aliwaeleza wajumbe wa Baraza la Usalama ya kuwa vikosi vya Serikali ya Kongo vimefanikiwa kuteka tena mji wa Dongo, katika jimbo la Equateur.

16/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

A. Guterres anakumbusha, mabadiliko ya hali ya hewa yanahusiana na watu kung’olewa mastakimu, mapigano na uhamaji

Antonio Guterres 06a

Vile vile tukizungumzia matukio kwenye Mkutano wa COP15 unaofanyika Copenhagen, Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, aliwaambia wajumbe wa kimataifa Ijumatano kwamba zipo fungamano halisi kati ya watu kuhamahama makwao, kung’olewa makazi na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa.

16/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Mwanaharakati wa mazingira Kenya atawazwa na KM kuwa Mjumbe wa Amani mpya kwa UM

Ijumanne alasiri, KM Ban Ki-moon, alimjulisha rasmi mjini Copenhagen, kwenye Mkutano wa COP15, Profesa Wangari Maathai wa kutoka Kenya, kuwa ni Mjumbe wa Amani mpya wa UM, atakayehusika na masuala yanayoambatana na hifadhi ya mazingira na udhibiti manufaa wa mabadiliko ya hali ya hewa katika dunia.

16/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Mtetezi wa Haki za Chakula afananisha madhara ya halihewa ya kigeugeu na “bomu liliotegwa dhidi ya udhamini wa chakula”

Olivier De Schutter, Mkariri Maalumu wa UM juu ya haki za mtu kupata chakula, amehadharisha Ijumatano mjini Copenhagen ya kwamba sera za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, zenye uwezo wa kutekelezwa kwa mafanikio ni zile zinazozingatia kidhati haki za binadamu,

16/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa kimataifa wanaohudhuria COP15 wamo mbioni kuharakisha mapatano kabla ya mwisho wa wiki

Viongozi wa kimataifa, wamo mbioni, wakijaribu kukamilisha mazungumzo ya kuleta itifaki mpya, Ijumaa ijayo, itakayoyasaidia Mataifa Wanachama kudhibiti kihakika, madhara yanayochochewa na hali ya hewa ya kigeugeu.

16/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa za dharura | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon Ijumatano alihudhuria tafrija maalumu mjini Copenhagen, Denmark kuanzisha mradi wa Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) wa kubuni “jiko la stovu salama” ambalo litatumiwa bila kuunguza kuni. Jiko hili litasaidia kutunza miti kwa kuhakikisha haitokatwa, na litapunguza tatizo la kumwaga gesi chafu kwenye anga kwa sababu ya kuchoma kuni, na vile vile kuyanusuru maisha ya wanawake na watoto wa kike, ambao mara nyingi hulazimika kwenda masafa marefu kukusanya kuni, shughuli ambazo husababisha wanawake kushambuliwa, kuibiwa mali zao na hata hunajisiwa kimabavu na wavunjaji sheria. Mradi wa WFP hasa umekusudiwa kuwasaidia wanawake wa Uganda na Sudan. Jiko la stovu salama jipya litatengenezwa mwaka ujao, na litagaiwa wahamiaji milioni 6, waliopo katika nchi 36, wakijumuisha vile vile watu waliong’olewa makazi na wale raia wanaorejea makwao kutoka nchi za nje ambapo walipatiwa hifadhi na usalama.

16/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa KM kwa JAK azungumzia hali nchini na wajumbe wa Baraza la Usalama

Jamhuri ya Afrika ya Kati

Sahle-Work , Mjumbe Maalumu wa KM kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK), asubuhi aliwasilisha mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama ripoti kuhusu mpango wa amani katika nchi.

15/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya Malaria Duniani kwa 2009 yachapishwa na WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO), leo limetangaza Ripoti ya 2009 juu ya Malaria Duniani. Ripoti ilieleza kwamba muongezeko wa misaada ya fedha, mnamo miaka ya karibuni, kuhudumia malaria, umeyawezesha mataifa kadha kufanikiwa kudhibiti maradhi,

15/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watumishi wawili wa UNAMID waachiwa huru Darfur

Watumishi wawili wa Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID), wanaoitwa Patrick Winful wa kutoka Nigeria pamoja na Pamela Ncube wa Zimbabwe, wameripotiwa kuachiwa huru na hivi sasa wanaelekea makwao.

15/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa JKK wakithiri katika taifa jirani kutafuta hifadhi baada kuzuka mapigano ya kikabila

Nembo ya UNHCR

Shirika la UM Juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti idadi ya raia wanaohajiri kutoka jimbo la Equateur, la kaskazini-magharibi katika JKK, inaendelea kuzidi kwa sababu ya kufumka kwa mapigano ya kikabila kwenye eneo lao.

15/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

EMG yatangaza rasmi sera ya kupunguza utoaji wa gesi chafu wa taasisi za UM

Vile vile kutoka Copenhagen, UM umetangaza rasmi utaratibu wa kupunguza gesi chafu zinazozalishwa na mashirika na taasisi mbalimbali za UM.

15/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Kuwasili kwa KM Copenhagen kunatazamiwa kuhamasisha mataifa kukamilisha mapatano ya COP15

Ilivyokuwa majadiliano ya Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa yanaonekana kupwelewa, na yamezorota kwenye mabishano ya kiutaratibu, pamoja na mivutano na mgawanyo mkubwa wa kimasilahi baina ya nchi tajiri na mataifa maskini,

15/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ofisi ya UM Juu ya Misaada ya Dharura (OCHA), imetangaza ripoti yenye kuelezea utaratibu wa sheria unaotumiwa na utawala wa kimabavu wa Israel katika kugawanya ardhi za WaFalastina ziliopo kwenye kanda mbalimbali za sehemu ya Ukingo wa Magharibi ya Mto Jordan, sehemu inayotambuliwa kama Eneo la C. Chini ya mfumo huo, WaFalastina huwa hawaruhusiwi kuendeleza ujenzi wa aina yoyote kwenye asilimia 70 ya maeneo yao. Wakati huo huo, ile asilimia 30 iliosalia ya maeneo ya WaFalastina, kumewekwa msururu wa vizuizi na vikwazo aina kwa aina ambavyo vinafuta, takriban, fursa zote za mtu kupata kibali cha kujenga. Kutokana na vikwazo kama hivi, makumi elfu ya WaFalastina wenye azma ya kujenga kwenye Eneo la C hunyimwa, kwa makusudi na kwa mipangilio, fursa ya kisheria ya kujenga na kutosheleza mahitaji ya makazi yao. Kwa sababu hizo,WaFalastina hulazimika kuendeleza ujenzi wa makazi yao bila ya kibali kutoka kwa watawala walowezi. Kwa hivyo, raia wa KiFalastina hukabiliwa na hatari ya majumba yao kubomolewa na, halafu, hung’olewa makazi na watawala wa Israel waliokalia kimabavu ardhi yao.

15/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

KM Ban Ki-moon ametangaza kwenye mkutano na waandishi habari Ijumatatu kwamba Wangari Maathai, mzalendo wa Kenya, aliotunukiwa Tunzo ya Amani ya Nobel na mtetezi wa mapinduzi ya kijani ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Amani wa UM mpya, atakayeshughulikia majukumu ya kuhifadhi mazingira na udhibiti bora wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani. KM aliwaambia wanahabari wa Makao Makuu, Profesa Maathai atatambulishwa rasmi kama Mjumbe wa Amani Ijumanne alasiri, kwenye taadhima maalumu itakaofanyika Copenhagen, ambapo Mkutano wa UM kuzingatia itifaki mpya ya kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa bado unaendelea na majadiliano yake. KM alisema uteuzi wa Profesa Maathai ulikuwa ni wa bora kabisa, kwa sababu ya mafanikio kadha aliopata kwenye bidii za muda mrefu za kutunza mazingira, na katika kuimarisha maendeleo. Profesa Wangari Maathai ni mwanamke wa KiAfrika pekee aliyetunukiwa Tunzo ya Nobel, na ameshatumikia Serikali ya Kenya kama waziri, na vile vile aliwahi kuwa mbunge, ni mwanataaluma na mtetezi shupavu wa haki za wanawake kwa zaidi ya miaka arobaini.

14/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wakusanyishwa Geneva na UNCTAD kuzingatia ushirikiano wa mataifa ya Kusini kuhudumia maendeleo

Nembo ya UNCTAD

Shirika la UM juu ya Maendeleo na Biashara (UNCTAD) linalosimamia ukuzaji wa biashara miongoni mwa nchi zinazoendelea, ili kupiga vita ufukara na hali duni, limeanzisha mjini Geneva mkutano wa siku tatu, wenye makusudio ya kutafuta taratibu zinazofaa kuimarisha ushirikiano

14/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM apongeza usajili wa amani wa wapiga kura Sudan

Ashraf Qazi, Special Representative of the Secretary-General for the Sudan and Head of the United Nations Mission in Sudan (UNMIS), addresses the Security Council on the current situation in the Sudan. UN PHOTO - Spanish Radio

Mjumbe Mkuu wa UM kwa Sudan, Ashraf Jehangir Qazi, ametangaza kukaribisha mwisho mzuri, wa utaratibu wa kusajili wapiga kura, kwa uchaguzi wa vyama vyingi, utakaofanyika nchini Sudan mwaka ujao. Asilimia 75 ya watu waliofikia umri wa kupiga kura walirajisiwa, sawa na raia wa Sudan milioni kumi na tano. Baina ya tarehe 1 Novemba mpaka Disemba 07 (2009), mamilioni ya watu walifanikiwa

14/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Baada ya mazungumzo kusimamishwa kwa muda Copenhagen, wajumbe wa kimataifa warudia tena majadiliano

Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen, au Mkutano wa COP 15, yalisimamishwa kwa muda baada ya nchi wanachama wa Kundi la G-77, linalowakilisha mataifa yanayoendelea, zilipoamua kutoshiriki kwenye mazungumzo, hususan nchi za KiAfrika. Wawakilishi wa bara la Afrika waliopo

14/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

UM yathibitisha robo tatu ya vifo vya maafa duniani husababishwa na majanga ya kimaumbile

margareta-wahlstrom

Margareta Walhstrom, Mjumbe Maalumu wa KM anayehudumia Mpango wa Kupunguza Athari za Maafa amenakiliwa akisema hali ya hewa mbaya kabisa iliojiri ulimwenguni, katika miezi 11 iliopita, ndio matukio yaliosababisha asilimia 75 ya vifo vinavyoambatana na majanga na maafa ya kimaumbile.

14/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Wakati wa kukamilisha itifaki mpya kudhibiti athari za hali ya hewa ni sasa, anasema KM

Kwenye mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu, Ijumatatu asubuhi, KM Ban Ki-moon alitoa mwito maalumu kwa viongozi wa dunia wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Copenhagen, unaowasihi waongeze, mara mbili zaidi, juhudi zao za

14/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya raia wanaendelea kuhajiri Yemen Kaskazini kukwepa mapigano, imeripoti UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti maelfu ya raia katika Yemen kaskazini bado wanaendelea kuyahama makazi yao hivi sasa, kwa sababu ya kushtadi kwa mapigano baina ya vikosi vya Serikali na wapiganaji wa Al Houthi, uhasama ambao umeingia mwezi wa tano.

11/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM na wafanyakazi wa UM wahudhuria kumbukumbu ya wenziwao waliofariki Algiers 2007

Algiers Attack

KM Ban Ki-moon na wafanyakazi wa UM leo asubuhi walikusanyika kwenye Makao Makuu kuhudhuria taadhima maalumu ya Siku ya Kumbukumbu kwa watumishi 17 waliouawa na shambulio la bomu, kwenye ofisi za UM katika Algiers, Algeria mnamo miaka miwili iliopita.

11/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matokeo ya utafiti wa FAO, yathibitisha shughuli za uvuvi ulimwenguni zahitajia marekibisho kudhibiti athari za hali ya hewa ya kigeugeu

Ripoti ya utafiti ulioendelezwa karibuni na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), iliochapishwa leo hii, inaeleza shughuli za uvuvi wa baharini zinakabiliwa na matatizo mbalimbali yanayoambatana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa,

11/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Copenhagen umewakilisha fursa ya kuleta maisha bora kwa umma wa kimataifa, anasema mkuu wa IFRC

Bekele Geleta, KM wa Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) ametangaza taarifa maalumu ya taasisi yao kuhusu wasiwasi unaoambatana na maendeleo kwenye majadiliano ya Mkutano wa Copenhagen.

11/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNFCCC abainisha mapatano yamefikiwa kwenye teknolojiya kinga dhidi ya gesi chafu angani

Mkuu wa Taasisi ya UM juu ya Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) kwenye mahojiano ya Alkhamisi na waandishi habari mjini Copenhagen, alisema wajumbe wa kimataifa, kwa sasa, wameshafikia makubaliano juu ya taratibu za kuanzisha mfumo mpya wa teknolojiya ilio imara na madhubuti,

11/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Kwenye Mkutano wa UM Kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, unaofanyika Copenhagen, wapatanishi wa kimataifa sasa wanazingatia nyaraka mpya zilizowasilishwa kwenye meza ya mahojiano, na Wenyekiti wa makundi kadha yanayozingatia mada mbalimbali chini ya Itifaki ya Kyoto na Mkataba wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa. Kwa mujibu wa Taasisi ya UM juu ya Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC), nyaraka zinazozingatiwa huwakilisha hatua muhimu ya majadiliano na haziathiri matokeo ya mwisho ya mkutano, au mfumo wa sheria wa matokeo hayo.

11/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waziri Mkuu wa Kenya anazungumzia maendeleo ya uchumi kijani nchini usiochafua mazingira

Wiki hii, mjini Vienna, Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) lilifanyisha kikao maalumu kuzingatia uwezekano wa Kufufua Uchumi wa Dunia kwa kutumia Viwanda Kijani, yaani viwanda vitakavyotunza mazingira.

11/12/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Baraza la Usalama Alkhamisi liliendeleza shughuli zake, awali, kwa kuzingatia taarifa mpya ya Kamati ya Vikwazo kuhusu azimio 1737, linaloambatana na “uzuiaji wa uenezaji wa silaha za kinyuklia na Iran.” Balozi Yukio Takasu wa Ujapani, mwenyekiti wa kamati, aliwakilisha ripoti kwenye Baraza. Baada ya hapo, Mwakilishi Mtendaji wa KM kwa Burundi, Youssef Mahmoud alihutubia Baraza la Usalama na kuelezea kupatikana kwa maendeleo ya kutia moyo kwenye mpango wa amani na katika matayarisho ya uchaguzi wa 2010 nchini Burundi. Alisema kuna matatizo kidogo kuhusu msaada wa fedha zinazohitajika kusimamia uchaguzi ujao, kwa sababu alisema mataifa kadha yalioahidi kuchangisha fedha za kuendesha uchaguzi hayajatimiza ahadi zao bado. Baadaye, Baraza la Usalama liliendeleza majadiliano juu ya Burundi kwenye kikao cha faragha.

10/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ayahimiza mataifa kujikinga na madhara thakili ya ubaguzi

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, kwenye risala yake kuiadhimisha Siku ya Haki za Binadamu, naye pia alitoa mwito wenye kuzihimiza Serikali na watu binafsi, kote ulimwenguni, kuchukua hatua hakika, na za kudumu, kutokomeza na kukomesha janga la ubaguzi milele duniani.

10/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unaadhimisha Siku ya Haki za Binadamu

Tarehe ya leo, 10 Disemba (2009) inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Haki za Binadamu. Kwenye risala ya KM juu ya taadhima za siku hii, alihadharisha kwamba hakuna hata taifa moja duniani liliosalimika hivi sasa na tatizo la ubaguzi, tatizo linaloendelea kujiwasilisha kwenye mifumo na miundo aina kwa aina ya kijamii.

10/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kiashirio cha awali kupima uchafuzi wa gesi za kaboni kimewakilishwa Copenhagen

Shirika la Kimataifa juu ya Usimamizi wa Fedha (IFC), likiwa miongoni mwa taasisi za Kundi la Benki Kuu ya Dunia, likijumuika na Kampuni ya Kimarekani ya Standard & Poor, ambayo hushughulikia ugunduzi wa viashirio vya uwekezaji wa kimataifa, wamebuni kiashirio cha kwanza duniani chenye kupima mabaki ya gesi ya kaboni kwenye masoko ya mataifa yanayoanza kuibuka kiuchumi,

10/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Ripoti fupi kuhusu matukio ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen

KM Ban Ki-moon amenakiliwa akifuatilia, kwa ukaribu zaidi, hekaheka na harakati za kijumla kwenye Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya hewa, wakati majadiliano yakipamba na kuendelea miongoni mwa wajumbe wa kimataifa.

10/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Wawakilishi wa G-77 waamini kuna rasilmali za kutosha ulimwenguni kukomesha madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa

Wawakilishi wa Mataifa wanachama wa Kundi la G-77 na Uchina, wamesisitiza kwenye kauli kadha walizowasilisha kwenye majadiliano ya Copenhagen ya kuwa umma wa kimataifa, kwa ujumla, katika karne ya ishirini na moja, umebarikiwa rasilmali ya kutosha kushughughulikia, kwa mafanikio, matatizo

10/12/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Mkutano wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, unaofanyika Copenhagen, hivi sasa umeingia kwenye hatua ya kuratibu mswada wa jaribio la mapatano ya mwisho. Kwa mujibu wa Mfumo wa Mkataba wa UM juu ya Udhibiti wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC), wajumbe wa kimataifa wameonyesha hamu na shauku kuu ya kujumuika pamoja kukamilisha mapatano yao muhimu kabla ya mawaziri wa kutoka Nchi Wanachama kuwasili Copenhagen wiki ijayo.

09/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya FAO yanonyesha bei za chakula zimeanza kupanda tena kwenye soko la kimataifa

Nembo ya FAO

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti iliochapishwa Ijumatano kwamba bei za juu za chakula, zimeanza kupanda tena katika dunia.

09/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM awaambia wajumbe wa Mkutano juu ya Mfuko wa CERF “twahitajia misaada zaidi kukabili athari za gesi chafuzi”

Asubuhi kwenye Makao Makuu, kulifanyika kikao maalumu kuzingatia shughuli za ile Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF.

09/12/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hatua ziada zatakikana dhidi ya matumizi ya tumbaku duniani, inahimiza WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ripoti mpya inayoeleza kwamba licha ya kuwa idadi kubwa ya umma wa kimataifa huhifadhiwa na zile sheria za kupiga marufuku uvutaji sigara kwenye mazingira ya umma, hasa katika 2008, juu ya hayo tumearifiwa kwamba bado tutahitajia kuchukua hatua ziada za dharura, za kuwalinda watu na maradhi pamoja na vifo vinavyoletwa na athari za moshi wa sigara.

09/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa kimatafia wanajiandaa kubuni viashirio vipya juu ya mifumko ya ukame duniani

Kuhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa zilizoshuhudiwa kutukia ulimwenguni mnamo miaka ya karibuni, Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani, (WMO), limebashiria kutatukia muongezeko mkubwa wa marudio ya ukame mkali, katika sehemu mbalimbali za dunia katika miaka ijayo.

09/12/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Waraka wa siri uliofichuliwa Copenhagen waonyesha mgawanyo wa matarajio kati ya nchi tajiri na zile zenye maendeleo haba

Majadiliano ya Mkutano wa UM juu ya taratibu za kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, Ijumanne yalikabiliwa na mtafaruku na vurugu lisiotarajiwa, baada mataifa yanayoendelea kuonyesha ghadhabu kubwa juu ya waraka wa siri uliofichuliwa na vyombo vya habari,

09/12/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amenakiliwa asubuhi ya leo, alipokutana na waandishi habari wa Makao Makuu, kushtumu vikali msururu wa mashambulio ya mabomu yaliotukia Ijumanne kwenye sehemu kadha za Baghdad, ambapo watu 120 ziada wanaripotiwa waliuawa pamoja na makorja kadha ya raia walijeruhiwa. KM alilaani, kwa kauli nzito kabisa, mashambulio haya na alisema alishtushwa kabisa na kiwango kikubwa cha ukatili uliodhihirishwa dhidi ya raia, matukio ya kigaidi ambayo alisema “yalikuwa ni ya kutisha, na yasiokubalika katu!” Alisema “hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha mashambulio ya kikatili dhidi ya raia.” Anaamini hujuma hizi zilikusudiwa hasa “kudhoofisha mpango wa uchaguzi pamoja na maendeleo ya kisiasa yaliopatikana siku za karibuni katika Iraq.” KM aliwatumia mkono wa pole aila za watu waliouawa, na pia kuwaombea majeruhi wapone haraka na kwa ukamilifu. Alisihi raia wa Iraq wasife moyo na kuwahimiza kuonyesha ushupavu dhidi ya mashambulio ya kigaidi, na aliutaka umma kuongeza bidii katika kuleta mapatano ya kitaifa yenye natija kwa wazalendo wote. KM aliwaahidi WaIraqi kwamba UM utaendelea kuwasaidia kwa kila njia kwenye utekelezaji wa malengo ya kurudisha utulivu, amani na maendeleo kwenye taifa lao.

08/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mradi wa DOTS wafanikiwa kutibu TB watu milioni 36

Katika miaka 15 iliopita, watu milioni 36 wanaripotiwa walitibiwa, kwa mafanikio, maradhi ya kifua kikuu, au TB, ulimwenguni, kwa kutumia utaratibu mkali wa kuhudumia afya bora uliotayarishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

08/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kutumia msaada Umoja wa Ulaya kufyeka utapiamlo mkali unaofukuta Kenya Kaskazini

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba yuro milioni 7.5 (sawa na dola milioni 11.3) ilizopokea kutoka Idara ya Misaada ya Kiutu ya Kamisheni ya Mataifa ya Ulaya, zitatumiwa kuhudumia kihali matatizo ya utapiamlo wa kima cha juu, yaliojiri miongoni mwa watoto wadogo, mama wajawazito na mama wanaonyonyesha wanaoishi katika maeneo ya ukame, Kenya Kaskazini.

08/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Halijoto duniani, kwa mwongo wa 2000, imefurutu kawaida, imehadharisha WMO

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limetangaza ripoti iliobainisha, kihakika, kwamba mwaka 2009 ni miongoni mwa vipindi 10 vilivyoshuhudia kiwango kikubwa kabisa cha halijoto katika dunia, kuanzia 1850, mwaka ambao WMO ulipoanzisha ukusanyaji wa takwimu juu ya kumbukumbu ya halijoto.

08/12/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Uchina inahimiza nchi tajiri kutimiza haraka ahadi za kupunguza utoaji wa gesi joto na haribifu kwenye anga

Climate Change. Emission of greenhouses gases. IMF/UN Spanish Radio

Kwa upande mwengine, mjumbe wa Uchina, alitoa mwito maalumu kwa zile nchi zenye maendeleo ya viwanda, unaozihimiza kutimiza, kwa uaminifu, ahadi walizotoa siku za nyuma na kuongoza kwenye kadhi ya kupunguza utoaji wa hewa chafu kwenye anga, kwa viwango vilivyo vikubwa,

08/12/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UM kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, ahimiza wapatanishi kuandaa kidharura marekibisho ya kifedha na kitaaluma kumudu bora athari za gesi chafuzi

Yvo de Boer, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM ya Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) kwenye mahojiano aliofanya Ijumanne na waandishi habari, alisema ufunguzi wa Mkutano Mkuu ulianza kwa “hatua ya kutia moyo, na katika nafasi muafaka,

08/12/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Matokeo ya uchunguzi ulioendelezwa na Nicholas Stern, Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti ya Grantham juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, iliopo kwenye Chuo Kikuu cha London School of Economics (LSE), akijumuika na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) yameonyesha dhahiri kuwepo uwezekano wa kutia moyo, kwa nchi zilizokusanyika Copenhagen, Denmark kuhudhuria Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, kufikia itifaki ya kupunguza utoaji wa gesi chafu angani. Hatua hii itausaidia ulimwengu kuepukana na madhara ya kuongezeka kwa halijoto, kwa kiwango cha daraja 2 ya sentigredi. Fafanuzi za ripoti ya utafiti ziliochapishwa kwenye mkesha wa Mkutano wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, zimethibitisha kuwepo pengo la tani bilioni chache tu kuhusu kiwango kinachotakikana kupunguzwa kila mwaka, kitaifa, cha zile gesi chafuzi zinazomwagwa angani. Imetangazwa na Ofisi ya Msemaji wa Ban Ki-moon hii leo kwamba KM atawasili Copenhagen wiki ijayo kuhudhuria kikao cha hadhi ya juu cha Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, kikao ambacho kinatarajiwa kuanza Ijumanne alasiri, katika tarehe 15 Disemba 2009. KM anaamini Mkutano Mkuu wa Copenhagen utawasilisha kipindi muhimu cha mabadiliko kwenye bidii za kimataifa za kudhibiti athari za hewa chafuzi kabla mageuzi haya kutuponyoka, tukishindwa kuwakilisha enzi mpya ya “ukuaji wa kijani” wa uchumi na jamii wenye natija za kimaisha kwa wote.

07/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bidhaa za ndizi, kwenye soko la kimataifa, hazijaathirika na migogoro ya uchumi, imeripoti FAO

Mazao ya ndizi ni bidhaa ya kilimo inayotarajiwa kutoathirika na mizozo ya kifedha, iliotanda karibuni kwenye soko la kimataifa, kwa mujibu wa ripoti iliochapishwa mapema wiki hii na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO).

07/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR inasema nusu ya wahamiaji duniani huishi mijini

Nembo ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba zaidi ya asilimia 50 ya wahamiaji milioni 10.5 wanaosaidiwa na taasisi hii ya kimataifa, huwa wanaishi kwenye maeneo ya miji na miji mikuu ya sehemu mbalimbali za dunia.

07/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ana matumaini juu ya itifaki ya kupunguza utoaji wa gesi chafu angani

KM Ban Ki-moon kwenye mahojiano na gazeti la kila siku la Denmark, linaloitwa Berlingske Tidende – yaliochapishwa Ijumapili, alisema ana “matarajio ya matokeo mazuri kutokana na majadiliano ya wawakilishi wa kimataifa” kwenye mkusanyiko wa Copenhagen.

07/12/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa wafunguliwa rasmi Copenhagen

Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, unaojulikana kama Mkutano wa COP 15, umefunguliwa rasmi Ijumatatu ya leo, kwenye mji wa Copenhagen, Denmark ambapo viongozi wa kimataifa walinasihiwa na Mkuu wa Mkutano, Yvo de Boer, kwamba, baada ya muda mrefu wa mivutano na majadiliano ya huko na kule, wakati umewadia kwa walimwengu kuchukua vitendo halisi dhidi ya athari haribifu zinazochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa katika dunia.

07/12/2009 | Jamii: Matatizo ya mifumko ya bei ya chakula | Kusoma Zaidi »

UM inahimiza kujumuishwa kwenye miradi ya MDGs mahitaji ya walemavu na walionyimwa uwezo

Kama mlivyosikia kwenye taarifa za habari wiki hii, kwamba Alkhamisi ya tarehe 03 Disemba (2009) iliadhimishwa hapa Makao Makuu ya UM, kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Watu Walemavu na Wenye Kunyimwa Uwezo wa Kimaumbile.

04/12/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinzi amani wawili wauawa Darfur na shambulio la watu wasiotambuliwa

Vikosi vya Pamoja vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) vimetoa ripoti ya mwanzo, yenye kueleza wanajeshi wake wawili, walinzi amani wa kutoka Rwanda, waliuawa wakati walipokuwa wanateka maji kwenye eneo la Saraf Umra, Darfur Kaskazini.

04/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Cartagena umepitisha azimio la kukomesha mateso ya silaha zilizotegwa

Kwenye Mkutano Mkuu wa Mapitio juu ya Ulimwengu Huru dhidi ya Silaha za Mabomu Yaliotegwa Ardhini, unaofanyika kwenye mji wa Cartagena, Colombia, Mataifa Wanachama yalioidhinisha na kuridhia Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu Yaliotegwa, yameahidi tena kukomesha usumbufu na madhara yanayoletwa na silaha hizo.

04/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulio la Mogadishu ni pigo adhimu kwa maendeleo ya afya Usomali, imeonya WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kupitia msemaji wake wa Geneva, Fadela Chaib, limeripoti leo Ijumaa ya kuwa shambulio la Alkhamisi la bomu la kujitoa mhanga, liliotukia Mogadishu, ni pigo lenye msiba mkubwa katika sekta ya afya ya Usomali.

04/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shirika la Afya la UM laanzisha juhudi mpya kudhibiti matumizi ya tumbaku Afrika

Imeripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba kuna haja kuu katika Afrika, kwa sasa hivi, kuanzisha haraka udhibiti wa matumizi ya sigara kwenye maeneo yao.

04/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Photo

Alkhamisi Baraza la Usalama lilisikilia taarifa ya faragha, iliowasilishwa kwenye ukumbia wa majadiliano, na Haile Menkerios, KM Msaidizi Juu ya Masuala ya Kisiasa, kuhusu shambulio la bomu la kujitoa mhanga liliofanyika asubuhi kwenye mji mkuu wa Usomali wa Mogadishu. Baada ya hapo, Baraza liliitisha kikao rasmi cha hadhara ambacho kilipitisha azimio la Maelezo ya Raisi (Presidential Statement), taarifa iliolaani shambulio la kigaidi kwa kauli kali kabisa, na kusisitiza kufanyike uchunguzi kamili kuhusu tukio hilo na kutaka wakosaji wote washikwe na kupelekwa mahakamani, haraka iwezekanavyo. Baraza la Usalama limetilia mkazo ya kuwa litaendelea kuunga mkono umma wa Usomali na Serikali ya Mpito, utawala ambao Mawaziri wake watatu walikuwa miongoni mwa watu waliouawa na shambulio la bomu la mhanga.

04/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lazingatia hali katika Usomali, na kazi za Mahakama za ICTY na ICTR

Alasiri Baraza la Usalama linatarajiwa kukutana kujadilia maendeleo ya karibuni katika Usomali.

03/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na mashirika ya misaada ya kiutu yaomba yafadhiliwe $689 kuisaidia Usomali kwa 2010

Vile vile kuhusu hali katika Usomali, kutokea Nairobi, kumeanzishwa hii leo kampeni maalumu ya kuchangisha misaada ya kiutu inayokaribia dola milioni 700, fedha zinazohitajika kufadhilia miradi 174 katika 2010,

03/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulio la kujitoa mhanga Usomali kulaaniwa na mashirika ya kimataifa, ikijumlisha UM

Hii leo, kutoka mjini Nairobi, Kenya mashirika kadha yenye kujumuisha jumuiya ya kimataifa yametoa taarifa ya pamoja, iliolaani kwa kauli kali, tukio la bomu la kujitolea mhanga liliofanyika Alkhamisi kwenye mji mkuu wa Usomali wa Mogadishu ambapo maofisa kadha wa Serikali ya Mpito waliuawa pamoja na wanafunzi, waandishi habari na raia wengine.

03/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UM inasema vifo vya shurua vimeteremka kwa 76% duniani

Taasisi inayohusu miradi wa kudhibiti maradhi ya shurua, ulioanzishwa 2001 na washiriki wa kimataifa, ikijumlisha Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) na Shirika la Afya Duniani (WHO),

03/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji maradufu kwenye uzazi wa majira unaweza kupunguza kwa nusu vifo vya uzazi ulimwenguni: UNFPA

Russian Radio

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNFPA) likishirikiana na Taasisi ya Guttmacher yamechapisha ripoti ya utafiti ulioendelezwa bia wenye kuthibitisha kwamba tunaweza kupunguza, kwa viwango vikubwa kabisa, vifo milioni nne ziada, vinavyotokea kila mwaka, vya watoto wachanga na vifo vya uzazi,

03/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wahimiza kuwapatia mamlaka ya kujitegemea watu wenye ulemavu

UM leo unaadhimisha rasmi Siku ya Kimataifa kwa Watu Walemavu na Wenye Upungufu wa Uwezo.

03/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

Ripoti mpya ya KM kuhusu shughuli za Ofisi ya UM ya Huduma za Mchanganyisho za Amani Burundi (BINUB) imewakilishwa Alkhamisi ya leo hapa Makao Makuu. Ndani ya ripoti KM alibainisha kwamba tangu BINUB kuanzishwa nchini kulishuhudiwa maendeleo mengi, ya kutia moyo. Lakini ilisema ripoti hali bado ni ya wasiwasi na dhaifu. Kwa mujibu wa ripoti, mwaka ujao utakuwa muhimu kwa Burundi, na taifa litahitajia kusaidiwa na jamii ya kimataifa ili kuhakikisha maendeleo yaliofikiwa hadi sasa kuwa yataimarishwa vizuri zaidi kabla, na baada, ya uchaguzi wa 2010, na wakati wa upigaji kura, hali kadhalika. Kwa hivyo, KM amependekeza shughuli za Ofisi ya BINUB ziendelee kutekelezwa Burundi kwa mwaka mmoja zaidi, baada ya muda uliodhaminiwa na Baraza la Usalama kwa sasa kumalizika mnamo tarehe 31 Disemba 2009.

03/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mataifa yanayoendelea yamefikia makubaliano ya kupunguza ushuru wa bidhaa zao

OMT Logo Organizacion Mundial Turismo / World Tourism Organization UNWTO OMT / Spanish Radio

Mataifa yanayoendelea, yalioridhia ule Mfumo wa Dunia wa Kufaidia Uhusiano wa Kibiashara (GSTP), ambayo yanakutana sasa hivi Geneva, kwenye kikao cha hadhi ya mawaziri, yameafikiana kupunguza kwa asilimia 20, viwango vya ushuru wa bidhaa wanazouziana baina yao,

02/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Stevie Wonder, msanii aliyepoteza nuru ya macho, ateuliwa na KM kuwa Mfadhili wa Amani mpya wa UM

Alkhamisi KM anatazamiwa kumteua msanii maarufi wa Marekani, Stevie Wonder kuwa Mjumbe wa Amani wa UM atakayejihusisha zaidi na huduma za kusaidia walemavu kote ulimwenguni.

02/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa ya Kuondoshwa Utumwa kuhishmiwa na UM

Tarehe ya leo, Disemba 02 (2009) huhishimiwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Uondoshaji wa Utumwa.

02/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC imerekibisha tena uamuzi wa kuachiwa kwa muda Bemba

Mapema Ijumatano Korti Ndogo ya Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), iliopo Hague, Uholanzi imebatilisha uamuzi wa siku za nyuma wa kumwachia Jean-Pierre Bemba kutoka kizuizini.

02/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM adhamiria kumteua I. Gambari kuwa Mjumbe wa Pamoja wa UM-UA kwa Darfur

Ibrahim Gambari, United Nations Special Envoy for Myanmar. UN Photo/UN Spanish Radio

KM amewajulisha wajumbe wa Baraza la Usalama leo hii ya kwamba anaazimu, baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, kumteua Ibrahim Gambari wa Nigeria kuwa Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UM/UA kwa Operesheni za Amani kwa Darfur, na kusimamia operesheni za vikosi vya pamoja vya UM-UA vya UNAMID, kuanzia tsarehe 01 Januari 2010.

02/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majadiliano ya kibiashara yanahitaji kuzingatia kidhati tatitzo sugu la njaa, asihi mtetezi wa haki ya chakula

Profesa Olivier De Schutter, Mkariri Maalumu wa UM anayetetea haki za mtu kupata chakula, amepongeza taarifa za wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO),

02/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Sera mpya ya Marekani, iliotangazwa Ijumanne usiku na Raisi Barack Obama juu ya Afghanistan ilipokelewa kwa matumaini na KM, kwa sababu, alisema iliwakilisha wizani baina ya juhudi za kijeshi na mchango wa raia unaotakikana kufufua utulivu wa taifa hilo. Mwelekeo huu mpya wa Marekani, aliongeza kusema KM, unatilia mkazo zaidi uwezo wa taasisi za KiAfghani zenyewe, ikichanganyika na vikosi vya usalama vya taifa kuwa vitahusishwa kwenye huduma za kurudisha utulivu na ujenzi wa taifa lao. Alikumbusha ya kuwa ujenzi wa taasisi za utawala, kufuatilia mazingira ya uhasama, ni kadhia inayochukua muda mrefu kutekelezwa, na kadhi hiyo ni muhimu sana katika kuhakikisha juhudi za pamoja zitadumishwa na jamii ya kimataifa katika ujenzi wa amani Afghanistan. UM umeahidi kuwa upo tayari kuunga mkono bidii zote zinazohitajika kuwapatia WaAfghani madaraka ya kujitegemea kizalendo, na kutekeleza majukumu yao kwa uongozi utakaowaletea amani ya kudumu, utulivu na maendeleo ya kiuchumi na jamii katika nchi yao.

02/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

The United Nations Secretariat Building is lit with the Red AIDS ribbon, demonstrating the Organization's commitment to the battle against HIV/AIDS, and to spotlight the General Assembly Special Session on HIV/AIDS on June 25-27.

Ripoti ya KM aliotumia Baraza la Usalama siku ya leo, imeelezea hali mpakani kati ya Syria na Israel ya kuwa ni shwari, kwa ujumla. KM amependekeza kwenye ripoti zile operesheni za Vikosi vya UM vya Uangalizi wa Kusimamishwa Mapigano kwenye Milima ya Jolan Syria (UNDOF) ziongezewe muda wa shughuli zake kwa miezi sita ziada – hadi mwezi Juni 2010.

01/12/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msemaji wa awali wa Ban Ki-moon astaafu na kuhishimiwa na UM

Msemaji wa awali wa KM Ban Ki-moon, yaani Michèle Montas, amestaafu rasmi kuanzia Ijumatatu, tarehe 30 Novemba.

01/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mkuu mpya wa IAEA aanza kazi rasmi Vienna

Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) ameanza kazi rasmi, hii leo, Ijumanne mjini Vienna. Kwenye taarifa kwa waandishi habari ameeleza ya kuwa “mazingira yaliozikabili shughuli za taasisi yao kwa sasa ni ya zahma tupu.”

01/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA inahadharisha, Chad Mashariki yatota kwenye hali ya wasiwasi

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba hali katika eneo la Chad Mashariki inaendelea kuzongwa na ukosefu wa usalama na wasiwasi, ulioselelea kwenye eneo katika kipindi cha karibuni, mazingira ambayo yanazorotisha shughuli za kukidhia mahitaji ya kiutu kwa waathirika wa hali ya msukosuko na vurugu.

01/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Siku ya Ukimwi Duniani’, UM kuhimiza mataifa kufuta sheria za kibaguzi dhidi ya waathirika wa VVU

UM unaiadhimisha tarehe ya leo kuwa ni Siku ya UKIMWI Duniani. Mada ya taadhima za mwaka huu inatilia mkazo Upatikanaji wa Haki za Binadamu kwa Wote.

01/12/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031