Nyumbani » 30/11/2009 Entries posted on “Novemba, 2009”

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

UM umetoa mwito unaopendekeza ifadhiliwe na jamii ya kimataifa mchango wa dola bilioni 7.1, ili kuhudumia kihali watu milioni 48 wanaoishi katika nchi 25 mnamo 2010. Ombi hili lilitangazwa rasmi Ijumatatu, kutokea Geneva, na John Holmes, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA). Taarifa ya Ombi la Msaada wa Kiutu kwa 2010 linawakilisha idadi kubwa kabisa ya msaada unaohitajika kufadhiliwa OCHA kuendeleza shughuli zake katika mwaka ujao, kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu Mfumo wa Ombi la Jumla (CAP) ulipoanzishwa rasmi katika 1991. Kwenye utangulizi wa ripoti ya ombi la OCHA, KM alieleza ya kuwa lengo hasa la taarifa hii lilikuwa ni kusaidia umma wa kimataifa ulio dhaifu kunusurika na maafa ya kihali katika mwaka ujao, ili nao pia waweze kujivua na masaibu hayo kwa hishima, usalama na kwa kujitosheleza, hali ambayo kila mwanadamu ana haki ya kubarikiwa nayo. Kadhalika, ombi la 2010 hujumlisha misaada inayohitajika kuhudumia kihali raia wa Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, maeneo yaliokaliwa kimabavu ya WaFalastina, na katika Usomali, Sudan, Uganda, ukanda wa Afrika Magharibi, Yemen na Zimbabwe. John Holmes, Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu na Mshauri Mkuu ya Misaada ya Dharura alitilia mkazo juu ya umuhimu wa kuilinda misaada ya kiutu na zile shinikizo zinazoletwa na matatizo ya bajeti la hivi sasa, ambayo hukabili serikali mbalimbali wanachama.

30/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Harakati za Ijumatatu kwenye Baraza la Usalama

Edmond Mulet

Baraza la Usalama asubuhi lilisikiliza ripoti kutoka Edmond Mulet, KM Msaidizi kuhusu Operesheni za Ulinzi Amani za UM juu ya Darfur, ambaye alisisitiza hali ya usalama katike eneo bado ni ya kuregarega.

30/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upigaji marufuku minara ya misikiti Uswiss ni kitendo cha ubaguzi dhidi ya WaIslam, asisitiza mtaalamu wa UM wa haki za binadamu

asma jahangir

Asma Jahangir, Mkariri (Mtetezi) Maalumu juu ya uhuru wa kiitikadi na haki ya kufuata dini, ametoa taarifa kwa waandishi habari, kufuatia kura ya maoni iliofanyika Uswiss, ya kupiga marufuku ujenzi wa minara mipya ya misikiti nchini humo, taarifa iliosisitiza kwamba marufuku hayo huwa yanabagua kidhahiri jamii ya WaIslam waliopo katika Uswiss.

30/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa ya Ushikamano na Umma wa Falastina

Tarehe 29 Novemba huadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Ushikamano na Umma wa KiFalastina.

30/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa maututi wa sotoka, uliodhuru wakulima miaka iliopita, unakaribia kufyekwa kimataifa

Imetangazwa kutoka Roma, Utaliana, leo hii, yalipo Makao Makuu ya Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) ya kuwa jamii ya kimataifa inakaribia kufyeka milele lile janga maututi la maradhi ya sotoka, ugonjwa wa kuhara wenye kuambukiza ng’ombe, maradhi ambayo kwa muda wa miaka mingi, yalikuwa yakiwasumbua wakulima, hasa kwenye yale maeneo ya Afrika, kusini ya Sahara.

30/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mfuko wa Global Fund wanusuru maisha ya watu milioni 4.9 duniani

Mfuko wa Kimataifa Kupiga Vita UKIMWI, TB na Malaria (Global Fund) imetangaza leo hii, kutokea Geneva, matokeo ya shughuli zake za mwaka, katika kupambana na maradhi haya matatu.

30/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo kuhusu Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto (Sehemu ya Pili)

unicef-20th-anniv

Kwenye makala ya awali, ya mfululizo wa vipindi vya sehemu mbili kuhusu Mkataba wa Haki za Mtoto, makala iliotangazwa hapo jana, tulikupatieni mahojiano baina ya mwanafunzi wa kidato cha pili, kutoka Kenya, Millicent Atieno Odondo,

27/11/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo kuhusu Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto (Sehemu ya Awali)

millicent-unicef

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) majuzi lilichapisha ripoti muhimu yenye mada isemayo “Hali ya Watoto Duniani kwa 2009″.

26/11/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Alkhamisi KM Ban Ki-moon anatazamiwa kusafiri kwenda Trinidad na Tobago kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM). Kwenye ziara hiyo, itakayochukua siku tatu, KM anatarajiwa kuwahimiza viongozi wa CHOGM kuhudhuria Mkutano Mkuu juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Copenhagen, utakaofanyika mwezi ujao, kikao ambacho kinaandaliwa kujaribu kukamilisha mapatano ya kuanzisha mkataba mpya wa kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Wakuu wa kiserikali watanasihiwa na KM kuwa na mtazamo halisi utakaowawezesha kufikia mapatano yanayoridhisha kwenye Mkutano Mkuu wa Copenhagen, maafikiano yatakayodumishwa, yenye usawa na yanayotimiza matakwa ya kisayansi.

25/11/2009 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO kupitisha mkataba wa kihistoria kudhibiti uvuvi haramu

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limepitisha mkataba mpya wenye lengo la kupiga marufuku vyombo vyote vya baharini na meli zilizoshiriki kwenye uvuvi haramu, kutoegesha kwenye bandari za Mataifa Wanachama.

25/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa Kufyeka Utumiaji Mabavu dhidi ya Wanawake

Tarehe ya leo, Novemba 25 (2009) inaadhimishwa rasmi na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa Kufyeka Matumizi ya Nguvu na Mabavu dhidi ya Wanawake.

25/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kijamii kwa watoto na wanawake Zimbabwe ni mbaya, inasema UM

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) likijumuika na Serikali ya Zimbabwe leo limetangaza takwimu mpya za maendeleo ya jamii, takwimu zenye kuonyesha hali ya wanawake na watoto wadogo katika Zimbabwe inaendelea kuharibika na kuwa mbaya zaidi.

25/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yamehadharisha kuhusu tofani Bukini

Mashirika ya UM yametangaza kuwa na wasiwasi juu ya kunyemelea kwa majira ya matofani na vimbunga katika taifa la Bukini, maafa ambayo kama hayajadhibitiwa yanaashiriwa huenda yakaathiri maisha ya watu 600,000.

25/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP imetangaza marekibisho ya kuhudumia pekee eneo la Kaskazini-Magharibi la JKK na katika Jamhuri ya Kongo

Shirika la UM juu Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kwamba litarekibisha huduma zake katika JKK na taifa jirani la Jamhuri ya Kongo.

25/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama linazingatia JKK na Kamisheni ya Ujenzi Amani

Baraza la Usalama lilikutana leo asubihi kuzingatia kazi za kamati ya vikwazo dhidi ya JKK.

25/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Kwenye maelezo ya tamko la KM juu ya mauaji ya kikatili ya raia 40 ziada, yaliotukia juzi kwenye jimbo la Maguindanao, Ufilipina ya Kusini, Ban Ki-moon alishtumu vikali jinai hii ya kutisha, uhalifu ambao alisema ulioripotiwa kufungamana na kampeni ya uchaguzi wa serikali ya majimbo.

24/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtandao mpya wa kuwasaidia Viongozi Wanaume dhidi ya Udhalilishaji wa Kijinsia, waanzishwa rasmi na KM

Asubuhi ya leo, KM ameanzisha Mtandao wa Viongozi Wanaume wa kukomesha vitendo vya kutumia mabavu na vurugu dhidi ya wanawake, Mtandao utakaojumlisha wanaume vijana pamoja na wale wenye umri mkubwa, washiriki ambao waliahidi kufyeka karaha ya kutumia nguvu ya udhalilishaji wa kijinsia.

24/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF itaandaa warsha maalumu Copenhagen, kwa watoto kuzingatia mageuzi ya hali ya hewa

Warsha Maalumu wa Watoto Kuzingatia Masuala juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani unaandaliwa kufanyika kwenye mji wa Copenhagen kuanzia Novemba 28 mpaka Disemba 04 (2009), kabla ya Mkutano Mkuu wa UM juu ya Udhibiti wa Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa kuanza majadiliano.

24/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya wasiwasi katika Equateur (JKK) imefumsha mapigano ya kikabila: OCHA

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kuzuka kwa hali ya wasiwasi hivi karibuni, kwenye Jimbo la Kaskazini la Equateur, katika JKK, baina ya jamii za makabila ya Boba na Lobala. Hali hii inaripotiwa iliripusha mapigano makali ya kikabila mnamo tarehe 04 Novemba (2009) ambapo watu 37 walisemekana waliuawa, jumla ambayo UM inaamini ilikaribia watu 100 waliouliwa kwa sababu ya uhasama.

24/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya WHO yazuru Usomali kutathminia hali ya afya nchini

Mnamo mwisho wa wiki iliopita, ujumbe maalumu wa hadhi ya juu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ulizuru Usomali kutathminia hali mbaya ya afya ilioselelea nchini humo.

24/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizo mapya ya VVU yateremka kwa 17% duniani – maendeleo zaidi yashuhudiwa kusini ya Sahara

Ripoti iliotolewa wiki hii bia na Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), imethibitisha kwamba ile miradi kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya UKIMWI ndio mipango ilioyawezesha mataifa kuleta tofauti halisi kwenye udhibiti unaoridhisha wa maradhi kwenye maeneo yao.

24/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Ripoti mpya ya Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo imeripoti ya kuwa idadi ya watafiti na wachunguzi wa kitaaluma katika mataifa yanayoendelea imeongezeka, kwa kiwango cha kutia moyo katika miaka ya karibuni. Ripoti ilieleza baina ya miaka ya 2002 hadi 2007, idadi ya watafiti katika nchi zinazoendelea ilizidi kwa asilimia 56, ikimaanisha nchi nyingi zenye uchumi haba zimetambua umuhimu wa kuendeleza tafiti zinazowasilisha ubunifu unaoleta mageuzi ya kiteknolojia kwenye maendeleo yao.

23/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viwango vya gesi chafuzi duniani vinaripotiwa kufurutu ada

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwenye ripoti yake mpya iliochapisha Ijumatatu, imeeleza kwamba kiwango cha ile hewa chafu inayotupwa kwenye anga, kinaeendelea kukithiri katika dunia.

23/11/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

UM imethibitisha mabaki ya mtumishi wa UM aliyepotea miaka mingi Lebanon

Msemaji wa KM ameripoti kwamba Ban Ki-moon amearifiwa kupatikana kwa mabaki ya Alec Collett katika Lebanon mashariki.

23/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi wa haki za watoto asema kasumbuliwa sana na ripoti za watoto wanaoshirikishwa na wapambanaji katika Sudan

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto Walionaswa kwenye Mapigano, ameripotiwa kuwa ana wasiwasi juu ya taarifa alizopokea, zinazoonyesha watoto walio chini ya umri wa utu uzima, wameruhusiwa kujiunga na makundi ya waasi wa katika Sudan.

23/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Urajisi wa wapiganaji wa zamani waanzishwa rasmi katika Darfur

Vile vile kuhusu Sudan, mnamo siku ya leo, katika mji wa El fasher, wapiganaji wa zamani 5000 kutoka makundi kadha yaliotia sahihi Mapatano ya Amani kwa Darfur, wameanza urajisi wa kujumuishwa kwenye maisha ya kawaida nchini.

23/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fafanuzi fupi juu ya mkutano wa UNIFEM kwa wanawake wa Darfur Kaskazini

Mnamo wiki iliopita, wanawake 500 ziada, kutoka fani na kazi mbalimbali walikusanyika katika Chuo Kikuu cha El Fasher, Darfur Kaskazini kusailia amani na utulivu kwenye eneo lao, na taifa, kwa ujumla.

23/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya Redio ya UM na mshindi wa mashindano ya picha ya UNDP/Olympus/AFP kutoka Kenya

Harusi

Ijumatano raia wawili wa kutoka Kenya, pamoja na mzalendo mwanamke kutoka Morocco, walitunukiwa zawadi maalumu, kwa picha zao zilizoonyesha namna watu wa kawaida barani Afrika, wanavyoshiriki kwenye harakati za kutunza na kuhifadhi mazingira – ikijumlisha zile shughuli za kupandisha miti, na huduma za kuigeuza mifuko ya plastiki, iliotupwa kwenye majaa baada ya kutumiwa, kuwa mikoba ya pochi na vikapu, ikiwa miongoni mwa kadhia muhimu zinazochangia kimataifa katika kupunguza athari haribifu za mabadiliko ya hali ya hewa.

20/11/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa Haki za Mtoto wakamilisha miaka ishirini

Tarehe ya leo, Novemba 20, 2009 inawakilisha kumbukumbu ya maiaka 20 ya Mkataba juu ya Haki za Mtoto.

20/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya Hali ya Watoto Duniani 2009 – UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limewasilisha ripoti muhimu Alkhamisi inayosailia: Hali ya Watoto Duniani.

20/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya IFRC inasihi, huduma za misaada ya kihali Afrika zahitajia marekibisho ya hali ya juu

Russian Radio

Ripoti mpya ya Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC), iliochapishwa hii leo, imeonya kwamba misaada ya kiutu inayofadhiliwa bara la Afrika ni ya gharama kubwa, na mara nyingi inashindwa kukidhia mahitaji yanayoendelea kupanuka, kwa zile jamii dhaifu kihali, ziliopo katika sehemu mbalimbali za Afrika.

20/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM imetangaza kuwapatia IDPs wa Zimbabwe hifadhi na misaada ya dharura

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuanzisha mradi mpya wa kuwasaidia kidharura wahamiaji wa ndani (IDPs) waliong’olewa makazi katika Zimbabwe kupata hifadhi wanayohitajia kumudu maisha.

20/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulio ya chuki za wageni Afrika Kusini yamelaaniwa na UNHCR

Mashambulio yaliotukia Ijumanne kwenye eneo la De Doorns, Afrika Kusini yaliochochewa na chuki na hofu dhidi ya wageni wa nchi, ikijumlisha raia wa Zimbabwe wenye kuomba hifadhi ya kisiasa, yaliripotiwa kusababisha baadhi ya wahamiaji 3,000 kukimibia mabanda waliokuwa wakijistiria ili kunusuru maisha, na ni kitendo ambacho kililaaniwa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR).

20/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon ameripotiwa kukaribisha uteuzi wa Herman van Rompuy kuwa raisi wa awali wa Umoja wa Ulaya, na vile vile kupongeza uteuzi wa Catherine Ashton kuwa Mjumbe Mkuu wa Umoja wa Ulaya juu ya Masuala ya Nchi za Kigeni na Sera za Usalama. KM alisema atashirikiana kikazi, kwa ukaribu, na viongozi hawa wa Umoja wa Ulaya, yaani Rompuy na Ashton, na kuimarisha uhusiano baina ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

20/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amemtumia salamu za pongezi Raisi Hamid Karzai wa Afghanistan baada ya kuapishwa Alkhamisi, kuwa Raisi atakayetumikia awamu ya pili ya utawala, kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini katika wiki za karibuni. KM aliunga mkono ahadi za Raisi Karzai za kutumikia raia wote WaAfghani, na kupiga vita vitendo vya rushwa, na katika kuimarisha utawala bora, na pia kuhakikisha hali ya usalama inajiri nchini, na kwamba atajitahidi kuhudumia mahitaji ya taifa, kwa ujumla, kwa kulingana na fafanuzi alizowakilisha kwenye hotuba yake ya kutawazishwa uraisi. KM alisema UM utaendelea kushirikiana na Raisi Karzai na serikali yake, pamoja na umma wa Afghanistan na washirika wa kimataifa katika huduma za maendeleo ya kukuza uchumi na jamii nchini mwao.

19/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yanahudumia kihali WaAngola waliofukuzwa kutoka JKK

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Ofisi ya OCHA imeripoti raia wa Angola waliofukuzwa JKK na waliorejea nchini mwao hivi sasa wanajumlisha watu 51,000.

19/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUC imekaribisha kukamatwa Ujerumani kwa viongozi wawili wa FDLR

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limetangaza kukaribisha kukamatwa nchini Ujerumani, mnamo siku ya Ijumanne, kwa viongozi wawili wa kundi la waasi la FDLR (Forces démocratiques de Libération du Rwanda), wanaoitwa Ignace Murwanashyka and Straton Musoni.

19/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uspeni imeongeza maradufu mchango wake kwa WFP kupambana na njaa katika Pembe ya Afrika

Corne de l'Afrique; horn of Africa WFP adapted graphic

Soraya Rodriguez Ramos, Waziri wa Nchi wa Uspeni kwa Ushirikiano wa Kimataifa, ametangaza siku ya leo kuwa serikali yao imekabidhi Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) msaada wa Yuro milioni 75 (dola milioni 112) kutumiwa kufarajia hali mbaya ya chakula iliolivaa eneo la Pembe ya Afrika.

19/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Benki Kuu ya Dunia inasisitiza miundombinu dhaifu ya Afrika inahitajia misaada maridhawa kukuza maendeleo

Kwenye ripoti ya utafiti wa Benki Kuu ya Dunia kuhusu hali ya miundombinu katika Afrika, imeripotiwa kwamba mnamo miaka michache iliopita, bara la Afrika lilifaidika kujipatia maendeleo muhimu.

19/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF inaunga mkono utekelezaji wa Mkataba wa Haki ya Mtoto kimataifa

Philip O’Brien, Mkurugenzi wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) anayehusika na Uchangishaji Pesa na Mashirkiano aliwaambia waandishi habari Geneva Alkhamisi ya leo,

19/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

Mkutano Mkuu wa UM wa kuzingatia maendeleo kwenye bidii za pamoja katika kudhibiti bora akiba ya chakula duniani, uliofanyika Roma, Utaliana kwa siku tatu, ulihitimisha majadiliano Ijumatano bila ya wajumbe wa kimataifa kukubaliana juu ya mchango wa fedha maridhawa zinazohitajika kupambana na tatizo kuu la njaa katika ulimwengu. Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) – liliotayarisha mkutano – limekadiria mchango wa dola bilioni 44 utahitajika kidharura, kuwekezwa kila mwaka, kwenye kilimo, kupiga vita, kwa mafanikio, matatizo ya njaa duniani.

18/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Matishio ya uharamia Usomali yamejizatiti bado licha ya kuwepo kwa manowari za kimataifa kwenye mwambao wa nchi

Uharamia pwani ya Somalia

Asubuhi Baraza la Usalama liliitisha kikao cha hadhara kuzingatia ripoti ya karibuni ya KM juu ya hali ya uharamia na ujambazi wa baharini unaotendeka kwenye mwambao wa Usomali.

18/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bodi la Uchunguzi juu ya ukiukaji wa haki za binadamu Guinea laanza kazi

Makamishna wa tume ya KM wanajumlisha Mohamed Bedjaoui, Françoise Ngendahayo Kayiramirwa na Pramila Patten ambao wanatazamiwa kuendeleza uchunguzi huru kutathminia ukweli, na kutoa mapendekezo yao juu ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya wale waliowajibika na msiba dhidi ya raia uliotukia Guinea mwezi Septemba. Wajumbe wa tume watazuru Guinea kuendeleza kazi zao kuanzia tarehe 25 Novemba [...]

18/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UNFPA inasisitiza umuhimu wa wanawake katika kupiga vita mabadiliko ya hali ya hewa

UNFPA.United Nations Population Fund logo. UNFPA/U.N. Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNFPA) limeripoti Ijumatano kwamba, kwa kulingana na fafanuzi za taasisi yao, fungu kubwa la jamii ya kimataifa yenye kusumbuliwa, kwa uzito mkubwa kabisa na matatizo yanayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, huwa ni wanawake.

18/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNIDO asema ‘maendeleo ya viwanda ndio ufunguo wa kuiunganisha Afrika na uchumi wa dunia’

Kandeh K. Yumkella, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) amesihi kwamba bara la Afrika linahitajia kudhibiti vizingiti vya kiuchumi vinavyokwamisha maendeleo yao, kwa kukuza uzalishaji wa viwandani, hatua ambayo ikitekelezwa alisema huenda ikamegea Afrika sehemu kubwa zaidi ya natija za kiuchumi kutoka soko la kimataifa, na kunufaisha uchumi mzima wa ulimwengu wetu.

18/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM yahimiza Mataifa Wanachama yote kushirikiana kufyeka njaa duniani

Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP), kwenye risala aliotoa mnamo siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Dunia juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula unaofanyika Roma, Utaliana, alisema raia wote wa kimataifa – na sio viongozi wa dunia pekee – wanawajibika kuhamasishwa wajitayarishe kuwapatia chakula watu bilioni moja ziada wenye kusumbuliwa na tatizo la njaa sugu ulimwenguni.

17/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Natija za ubora wa hewa zitasailiwa kwenye Mkutano wa Sayansi ya Angahewa utakaofanyika Korea Kusini

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limearifu ya kuwa kikao cha kumi na tano cha Kamisheni juu ya Sayansi ya Angahewa, kitaanzisha mijadala maalumu mnamo siku ya Ijumatano, katika Korea Kusini.

17/11/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

ICTR imeamrisha kuachiwa kutoka vizuizini wafungwa wawili

International Criminal Tribunal for Rwanda ICTR/UN Spanish Radio

Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) imeamua kumwachia huru Hormisdas Nsengimana, aliyekuwa padri wa Rwanda, baada ya kuonekana hana hatia juu ya mashitaka ya kushiriki kwenye vitendo vya mauaji ya halaiki na makosa ya jinai dhidi ya utu na kuamrisha afunguliwe haraka kutoka Kituo cha UM cha Kuwekea Watu Kizuizini kiliopo Arusha, Tanzania.

17/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama limelaani ongezeko la mashambulio ya LRA katika JKK

Ijumanne asubuhi, Baraza la Usalama lilifanyisha mashauriano kuhusu masuala ya eneo la Maziwa Makuu na tatizo la waasi wa Uganda wa kundi la LRA.

17/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa Haki za Binadamu aisihi JKK kuwalinda mawakili, na watetezi wa haki za kiutu

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu ametoa taarifa yenye kuihimiza Serikali ya JKK kuhakikisha mawakili na watetezi wa haki za binadamu, ikijumlisha waandishi habari, huwa wanapatiwa ulinzi unaofaa utakaowaruhusu kutekeleza majukumu yao, bila ya kuingiliwa kati kikazi wala kubaguliwa, kutishiwa au kulipizwa kisasi kwa sababu ya shughuli zao.

17/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA inasema, hifadhi ya raia Kivu Kaskazini ndio jukumu muhimu kabisa kwa sasa

Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA), Elizabeth Byrs, aliwaambia waandishi habari Geneva, leo hii, kwamba hali ya usalama katika Kivu, Majimbo ya Oriental na Equateur katika JKK, bado inaendelea kuwa mbaya zaidi.

17/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

un flag

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limeripoti ya kuwa miradi mingi isiochafua hewa, na inayotumia nishati inayotunza mazingira, inalengwa sasa hivi kutekelezwa katika bara la Afrika, licha ya kuwa idadi hiyo bado ni ndogo tukiilinganisha na miradi kama hiyo inayoendelezwa katika mataifa ya Asia na Amerika ya Latina. Miradi hii inajumlisha sehemu ya Mifumo ya Maendeleo Safi (CDM) ya Mkataba wa Kyoto, inayohusikana na mipango mbalimbali ya kuhifadhi mazingira, kuanzia ile miradi ya nishati zinazotumiwa mara kwa mara hadi ile ya kupandisha miti. Miradi kama hii imezisaidia nchi zenye maendeleo ya viwanda kudhibiti vyema matatizo ya hewa chafu na kupunguza halijoto katika dunia, baada ya kuamua pia kuwekeza kwenye miradi ya kupunguza utoaji wa hewa chafu katika nchi zinazoendelea. Miradi 112 ya CDM, inayogharamiwa Yuro milioni 212 kwa mwaka, inasubiri kuthibitishiwa nchi za Afrika kwa sasa, na inasubiri “usajili rasmi”. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na UNEP, inaonyesha kuwepo ongezeko la kutia moyo katika Afrika tukilinganisha na 2008 ambapo miradi 78 ya kutunza mazingira ilisajiliwa kwa Afrika; wakati katika 2004 ni miradi miwili tu ya CDM ilisajiliwa kwa bara zima la Afrika. Asilimia 80 ya miradi ya sasa inayongojea kutekelezwa katika nchi za Afrika kusini ya Sahara – na hujumlisha miradi 28 itakayotendeka Afrika Kusini, ikifuatiwa na miradi ya CDM 14 kwa Kenya. Kuhusu Afrika Kaskazini, Misri inaandaa miradi 13 ya CDM, ikifuatiwa na Morocco ambayo inajitayarisha kutekeleza miradi 10. Wataalamu wanasema Serikali za Afrika zimedhamiria kihakika kuleta mabadiliko yenye natija za kimazingira wiki chache tu kabla ya Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa utakaofanyika Copenhagen kuanzia tarehe 07 mpaka 18 Disemba 2009.

17/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kudhibiti Kisukari Duniani

world diabetes day 14a

Ijumamosi, tarehe 14 Novemba, iliadhimishwa kuwa ni Siku ya Kudhibiti Maradhi ya Kisukari Duniani.

16/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa kimataifa wameakhirisha jukumu la kukamilisha itifaki ya Copenhagen juu ya mabadiliko ya hali ya hewa

Imeripotiwa hii leo kwamba viongozi wa kimataifa wameafikiana kuakhirisha yale majadiliano ya kufikia mapatano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa katika mkutano ujao utakaofanyika mwezi Disemba katika Copenhagen, na badala yake wamekubaliana kwamba mkutano huu wa mabadiliko ya hali ya hewa ujaribu kufikia itifaki isio na uzito “wenye masharti ya kisiasa” ili kuwawezesha wajumbe wa kimataifa kuhakikisha masuala magumu yenye kutatanisha majadiliano yao yatazingatiwa kidhati katika siku za baadaye.

16/11/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya KM inahimiza uharamia usitishwe Usomali na wakosa wafikishwe mahakamani

Ripoti mpya ya KM kuhusu hali ya uharamia na ujambazi katika mamlaka ya maeneo ya bahari ya mwambao wa Usomali, inayoambatana na Azimio 1846 la Baraza la Usalama, imechapishwa na kutolewa rasmi leo Ijumatatu, na imeeleza ya kuwa kuwepo kwa vyombo vya majeshi ya majini vya Mataifa Wanachama kwenye eneo hilo ni hatua muhimu iliosaidia kusawazisha utulivu wa mwambao wa Afrika Mashariki.

16/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dunia wakutana Roma kuzingatia mradi wa kupiga vita njaa

Mkutanao mkuu wa UM, wa siku tatu unaozingataia udhibiti bora wa akiba ya chaklula duniani, umefunguliwa rasmi leo hii kwenye mji wa Roma, Utaliana ambapo KM Ban Ki-moon, kwenye risala yale alionya kwa kukumbusha mnamo siku ya leo pekee watoto 17,000 watafariki duniani kwa sababu ya kusumbuliwa na njaa – ikijumlisha kifo cha mtoto mmoja katika kila nukta tano za dakika – jumla ambayo kwa mwaka inakadiriwa kukiuka vifo milioni 6 vya watoto, licha ya kuwa sayari yetu imebarikiwa chakula cha kuweza kutosheleza mahitaji ya chakula kwa umma wote wa kimataifa, alisisitiza KM.

16/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Alain Le Roy Naibu KM juu ya Operesheni za Ulinzi Amani, akifuatana na Mshauri wa KM juu ya Masuala ya Kijeshi, Jenerali Chikadibia Isaac Obiakor, na Anthony Banbury, KM Msaidizi kwa Huduma za Nje za Mashirika ya Ulinzi Amani ya UM, wiki hii wataelekea Uchina kuhudhuria mkutano maalumu wa kuzingatia operesheni za kulinda amani za UM. Wakati watakapokuwepo Beijing, Le Roy atakutana na wajumbe kutoka Wizara ya Ulinzi ya Uchina na Wizara ya Mambo ya Nje na kusailia nao mchango wa Uchina katika kuimarisha huduma za kulinda amani ulimwenguni.

16/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Baraza la Usalama lilikutana Ijumaa kwenye majadiliano ya hadhara ambapo, awali, lilisikia ripoti kutoka wenyekiti wa kamati tatu zinazohusika na utekelezaji wa mapendekezo ya Azimio 1267 juu ya masuala ya al-Qaeda na Taliban; Azimio 1373 dhidi ya vitendo vya ugaidi; na Azimio 1540, linaloambatana na masuala ya silaha za maangamaizi ya halaiki. Wenyekiti wa kamati hizi tatu ni mabalozi wa kudumu wa UM kutoka Austria, Croatia na Costa Rica ambao waliwasilisha taarifa kuhusu kazi za kamati zao katika miezi sita iliopita.

13/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNFPA itawasilisha ripoti mpya wiki ijayo juu ya idadi ya watu duniani

Russian Radio

Ijumatano ijayo, tarehe 18 Novemba, Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) itawasilisha ripoti mpya kuhusu uhusiano wa mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake kwa wanawake.

13/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA imeonya ‘Hali Chad mashariki inahatarisha usalama wa wahudumia misaada ya kiutu’

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti ya kuwa vitendo vya uharamia na ujambazi mbaya uliofanyika katika wiki mbili zilizopita, kwenye maeneo ya mashariki katika Chad, ni hali inayohatarisha operesheni za kiutu za kunusuru umma muhitaji.

13/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Treni ya ‘Climate Express’ inaelekea Copenhagen kumurika umuhimu wa kuhitimisha mapatano ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Wanaharakati 400 ziada juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, wakijumlisha wapatanishi, viongozi wa mashirika ya kibiashara pamoja na watetezi wa hifadhi ya mazingira wanatarajiwa kusafiri pamoja kwenda Copenhagen kwa treni yenye jina la 'Treni ya Hali ya Hewa ya Haraka’ (Climate Express), kwa madhumuni ya kuwahimiza viongozi wa dunia kufikia makubaliano yalio ya haki, yenye masharti ya kisheria na nia ya kutekelezwa, pale watakapokusanyika Denmark kuhudhuria mkutano mkuu wa UM juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

13/11/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dunia wahimizwa na KM kuhudhuria Mkutano wa Copenhagen ili kuwasilisha mapatano ya kuridhisha

Mapema Alkhamisi Msemaji wa KM alitoa taarifa maalumu kwa waandishi habari, kuhusu Mkutano Mkuu ujao wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa, utakaofanyika mjini Copenhagen.

13/11/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Suluhu hakika yahitajika kudhibiti upungufu wa maji unaosababishwa na hali ya hewa ya kigeugeu

Wiki hii tunajadilia umuhimu wa kuzingatia, kwa kina, mchango wa maji safi na salama, katika udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa.

13/11/2009 | Jamii: Makala za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Hatua ziada zinahitajika Sudan Kusini kudhibiti uhaba wa chakula, anasema Ofisa wa UM

Nembo ya UNICEF

Hilde F. Johnson, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) ametoa mwito unaopendekeza kuchukuliwe hatua ziada Sudan Kusini, ili kudhibiti tatizo la upungufu mkubwa wa chakula, uliojiri kwa sasa, katika baadhi ya sehemu za eneo, ili hali isije ikageuka kuwa janga baya zaidi.

12/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahimiza vitendo hakika kukomesha silaha zinazodhuru raia

Kwenye ujumbe aliotuma Geneva katika Mkutano wa 2009 wa Mataifa Yalioidhinisha Mkataba wa Udhibiti Silaha Maalumu za Kawaida, KM Ban Ki-moon aliyahimiza Mataifa kuendelea kulenga majadiliano yao kwenye zile juhudi za kuimarisha hifadhi bora ya raia dhidi ya madhara yanayoletwa na matumizi ya silaha hizi katili na zisiobagua,

12/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Kwenye mkesha wa Mkutano Mkuu juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani, utakaofanyika wiki ijayo kwenye mjini Roma, Utaliana, kulitolewa ilani maalumu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) yenye kuuhimiza umma wa kimataifa kufanyisha mgomo wa siku moja dhidi ya tatizo la njaa sugu iliokabili mamilioni ya watu kwenye sayari ya dunia yetu. Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jacques Diouf amependekeza kwamba kila mwanadamu mwenye hisia halisi juu ya mateso ya njaa sugu wanaopata watu bilioni moja ulimwenguni, wajaribu kufunga ama katika Ijumamosi au Ijumapili ijayo. Alisema yeye binafsi ataanza kufunga, kwa muda wa saa 24, kuanzia Ijumamosi asubuhi ya tarehe 14 Novemba 2009.

12/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yahimiza ugawaji wa mapema wa dawa kinga dhidi ya H1N1

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza hadhari maalumu kwa madaktari, inayowasihi kutongojea matokeo ya vipimo vya maabara ya afya kuhusu maambukizi, kabla ya kugawa dawa ya kupambana na virusi vya homa ya mafua ya A/H1N1 kwa wanawake wajawazito wanaodhaniwa wameambukizwa na maradhi hayo.

12/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya 2009 juu ya Kuangamizwa Vijibomu Vilivyotegwa Ardhini

Ripoti ya 2009 Inayosimamia Utekelezaji wa Kuangamiza Vijibomu Viliotegwa Ardhini, iliochapishwa Geneva hii leo, imeeleza kupatikana mafanikio kadha kwenye shughuli za kufyeka silaha hizo katika sehemu mbalimbali za dunia.

12/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Global Fund itafadhilia nchi maskini dola bilioni 2.4 kupiga vita maradhi

Logo of the Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis and Malaria. Global  Fund / Spanish Radio

Taasisi ya Mfuko wa Kimataifa Dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria – inayoungwa mkono na UM – yaani Taasisi ya Global Fund, imeidhinisha leo hii msaada wa dola bilioni 2.4 kufadhilia miradi ya kupamabana na mardhi hayo matatu, katika nchi zenye maendeleo haba ya kiuchumi,

12/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Kabla ya kumaliza ziara ya siku moja mjini Washington D.C. mnamo siku ya Ijumanne, KM Ban Ki-moon alifanya mahojiano na waandishi habari, ambapo alitilia mkazo umuhimu wa kukamilisha mapatano yenye nguvu, kwenye mkutano ujao wa Copenhagen, itifaki ambayo itatumiwa kama ni msingi wa mkataba mpya wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa katika ulimwengu. KM alikiri, utekelezaji wa kadhia hiyo utahitajia gharama kadha wa kadha. Lakini vile vile alikumbusha ya kuwa gharama hizo hazitojumlisha fedha nyingi tukilinganisha na gharama zitakazorundikana kwa siku za baadaye, pindi walimwengu watashindwa kuchukua hatua zinazotakikana kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa kimataifa. Wabunge watatu wa Marekani walishiriki kwenye mahojiano hayo na waandishi habari, wakijumuisha Seneta John Kerry, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge juu ya Masuala ya Nchi za Kigeni, Seneta Richard Lugar na Seneta Joe Lieberman, kufuatia mkutano wa maseneta wengine na KM kuzingatia suala la mabadiliko ya hali ya hewa.

11/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uhamishaji usio khiyari wa Wasomali kutoka Djibouti waihuzunisha UNHCR

Somali Refugees Gulf of Aden UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kuhuzunishwa na uamuzi wa karibuni wa serikali ya Djibouti, wa kuwarejesha makwao Mogadishu, kwa nguvu, raia 40 wa Kisomali, kitendo kilichofanyika katika siku za Ijumatatu na Ijumanne, wiki hii.

11/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF inasema watoto wanavia kwa sababu ya upungufu sugu wa chakula

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) nayo pia imewasilisha ripoti maalumu inaozingatia athari za ukosefu wa chakula kwa watoto wachanga.

11/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mchanganyiko wa vitega uchumi na nia ya kisiasa huweza kufyeka njaa – FAO

Ripoti mpya ya Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), iliochapishwa rasmi leo hii, yenye kutathminia maendeleo yaliofanyika kwenye nchi kadha inazozishughulikia, imebainisha kwamba idadi ya watu wasiopata chakula cha kutosha iliteremka kwa kiwango kikubwa, na cha kutia moyo.

11/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umeteua Julai 18 kuwa ni Siku Kuu ya Kimataifa Kumhishimu Nelson Mandela

Ijumanne, kwenye kikao cha Baraza Kuu, kusailia mada muhimu inayohusu “utamaduni wa amani”, Mataifa Wanachama yalipitisha, bila kupingwa, azimio la kuadhimisha tarehe 18 Julai, kila mwaka, kuwa ni 'Siku ya Kimataifa Kumhishimu Nelson Mandela’.

11/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Headquarters UN PHOTO / Spanish Radio

KM Ban Ki-moon siku ya leo anazuru Washington D.C. ambapo asubuhi alikutana na maofisa wa Makao Makuu ya Raisi wa Marekani (White House) wanaohusika na masuala ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni. Alasiri KM vile vile alikutana na viongozi wa Bunge la Marekani na walishauriana juu ya mada zinazofungamana na mabadiliko ya hali ya hewa.

10/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Raia waliong’olewa makazi JKK wafarajiwa kihali na UM

© UNHCR/P.Taggart

Taarifa mpya zimefichuka karibuni, kuhusu mapigano ya kikabila yaliofumka mwezi Novemba, kwenye jimbo la Equateur, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).

10/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lengo la MDGs kupambana na UKIMWI linafanyiwa mapitio na UNAIDS

Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS), kwenye makala iliochapishwa wiki hii katika Jarida juu ya UKIMWI, imezingatia kwa makini zaidi, suala la kama jamii ya kimataifa itafanikiwa kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika 2015, kwa kulingana na pendekezo rakamu ya sita ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

10/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO itafadhaliwa dozi milioni 50 za chanjo kudhibiti A/H1N1 kwa nchi maskini

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza hii leo kwamba kampuni ya GlaxoSmithKline, inayohusika na huduma ya matunzo ya afya, imetiana sahihi na UM, mapatano rasmi ya kufadhilia dozi milioni 50 za dawa ya kupambana na homa ya mafua ya A/H1N1 kimataifa.

10/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA inasihi, misaada ya dharura yahitajika kuunusuru umma wa Usomali na majanga ya kiutu

Ramani ya Somalia

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeihimiza jumuiya ya kimataifa, kuharakisha michango ya dharura inayotakikana kunusuru maisha kwa raia wa Usomali.

10/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi maskini 31 zimedhurika na bei ya juu ya chakula: FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwamba ulimwengu unakabiliwa na uhaba mkubwa, na wa hatari wa chakula, ulioathiri vibaya sana nchi 31.

10/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amesema ana matumaini serikali wanachama katika UM zitaweza kufikia mapatano juu ya masuala ya kimsingi, kwenye mkusanyiko wa Mkutano wa Copenhagen.” Janos Pasztor, Mkurugenzi wa Tume ya KM Kushughulikia Masuala ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa amenakiliwa akisema ana imani mapatano anayoyazungumzia KM yatawakilisha “maudhui yenye sheria ya kuongoza utendaji wa kimataifa unaotakikana kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa katika dunia.”

09/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjumbe Maalumu wa KM Kudhibiti Malaria apongeza mchango wa UNICEF kuhudumia vyandarua vya dawa Afrika

mosquito net Russian Radio

Ray Chambers, Mjumbe Maalumu wa KM Kudhibiti Malaria, ameripotiwa kupongeza mchango wa UNICEF ambapo msaada wa dola milioni 8.5 ulitengwa makhsusi kuhudumia ugawaji wa vyandarua vilivyonyunyiziwa dawa ya kuua vijidudu, katika mataifa ya Afrika yaliopo kusini ya Sahara.

09/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yaripoti watu 16,000 wang’olewa makazi Usomali na mafuriko

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti, kwa akali, watu 16,000 waling’olewa makazi kwa sababu ya mafuriko katika majimbo ya Usomali ya Hiraan, Gedo na Shabelle ya Chini.

09/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laidhinisha Ripoti ya Goldstone juu ya mashambulio ya Ghaza

gaza-mapa

Alkhamisi jioni, Baraza Kuu la UM limepitisha azimio la kuidhinisha ripoti ya tume ya uchunguzi kuhusu ugomvi uliosababisha mashambulio yaliotukia mwanzo wa mwaka, dhidi ya eneo liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza, ripoti ambayo iliwatia hatiani vikosi vya jeshi la Israel pamoja na wapiganaji wa KiFalastina, kwa makosa ya kukiuka pakubwa haki za binadamu dhidi ya raia.

09/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM Ban Ki-moon ahutubia Baraza la Usalama kuzingatia hali katika Afghanistan

Ijumaa alasiri KM Ban Ki-moon alihutubia Baraza la Usalama, kwenye kikao maalumu cha faragha, kuzingatia hali katika Afghanistan.

09/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ijumaa alasiri KM Ban Ki-moon alihutubia Baraza la Usalama, kwenye kikao maalumu cha faragha, kuzingatia hali katika Afghanistan. Alitazamiwa kusailia hali ya usalama na kuwasilisha fafanuzi zake juu ya ziara aliifanya majuzi kwenye mji wa Kabul, Afghanistan kufuatia shambulio la magaidi dhidi ya watumishi wa UM, tukio liliosababisha vifo vya wafanyakazi watano na majeruhi tisa.

06/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sheria kali lazima zitekelezwe kuhifadhi mali ya asili kwenye mazingira ya mapigano, inasema ripoti ya UNEP

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya mazingira (UNEP) limechapisha ripoti mpya, ilioandaliwa na wataalamu wa sheria, inayozingatia kanuni zinazohitajika kubuniwa na kuimarishwa ili kutunza mazingira, wakati wa mapigano, uhasama, vurugu na vita.

06/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM inahamisha na kuwatawanya wafanyakazi wake Afghanistan kuwapatia usalama unaoridhisha

Shirika la UM la Kuisaidia Afghanistan Kurudisha Utulivu (UNAMA) Alkhamisi lilitangaza ya kuwa limeamua kuhamisha baadhi ya wafanyakazi wake, waliopo katika sehemu kadha wa kadha nchini Afghanistan, na kuwapeleka kwenye makazi ya muda ndani ya nchi, na wengine nje ya taifa hilo, kwa matarajio ya kuwapatia ulinzi unaofaa.

06/11/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imeomba ifadhiliwe misaada ya kunusuru maisha ya wahamiaji wa Usomali wanaokabiliwa na mafuriko Kenya

Shirika la UNHCR limetoa ombi maalumu linalowataka wahisani wa kimataifa kuchangisha msaada wa dharura wa dola milioni 2.8 zinazohitajika kushughulikia hatari ya mafuriko, inayowakabili watu 300,000,

06/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umeingiwa wasiwasi juu ya kuzuka mapigano ya kikabila katika JKK kuhusu haki ya uvuvi

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kuingiwa wasiwasi mkubwa juu ya mapigano makali ya kikabila yalizuka wiki iliopita, kwenye jimbo la Equateur, katika JKK, juu ya haki za uvuvi.

06/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ahadi na maelewano yanahitajika kusukuma mbele majadiliano ya hali ya hewa

Kikao cha mwisho, cha mashauriano, kabla ya mkutano ujao wa Copenhagen (Denmark), kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, kimekamilisha mahojiano mjini Barcelona, Uspeni hii leo hii.

06/11/2009 | Jamii: Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Kesi ya Bemba itaanzishwa rasmi Aprili 2010 mjini Hague: ICC

Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) imetangaza kwesi ya Jean-Pierre Bemba itaanza kusikilizwa rasmi mwezi Aprili mwaka 2010.

05/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bagaragaza ahukumiwa kifungo cha miaka minane na ICTR kwa jinai ya halaiki Rwanda

International Criminal Tribunal for Rwanda ICTR/UN Spanish Radio

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imehukumu kifungo cha miaka minane kwa mtuhumiwa Michel Bagaragaza, aliyekuwa mfanya biashara mkuu katika Rwanda, kwa kushiriki kwenye mauaji ya halaiki yaliotukia nchini mwao katika 1994.

05/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjadala wa BK juu ya uchunguzi wa mashambulio ya Tarafa ya Ghaza waingia siku ya pili

Ijumatano Baraza Kuu (BK) la UM lilianzisha majadiliano maalumu kuhusu ripoti ya uchunguzi wa UM, uliofichua vikosi vya Israel pamoja na wapiganaji wa KiFalastina, walipatikana na hatia ya kukiuka haki za kibinadamu wakati wa mashambulio ya katika eneo liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza mapema mwaka huu.

05/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa UNAMA Afghanistan watahamishiwa makazi ya muda kupata usalama

Shirika la UM la Kuisaidia Afghanistan (UNAMA) limetangaza kuwa litawahamisha baadhi ya wafanyakazi wake na kuwapeleka kwenye makazi ya muda, ndani ya nchi au nje ya Afghanistan,

05/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uokozi wa awali wa watoto waliotoroshwa Sudan kusini kupongezwa na UM

UM umepongeza kuokolewa watoto 28 waliotekwa nyara siku za nyuma katika Jimbo la Jonglei, Sudan Kusini.

05/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Leo Alkhamisi KM Ban Ki-moon yupo njiani akirejea New York, baada ya kukamilisha ziara ya Ugiriki. Kabla ya kuondoka Ugiriki asubuhi alihutubia Bunge la Helleniki, na kuwa KM wa kwanza kihistoria kufanya hivyo. Aliwaambia wabunge wa Ugiriki kwamba ziara aliofanya Kabul, mapema wiki hii, ilimtia hamasa sana baada ya kushuhudia ushupavu na dhamana walionyesha watumishi wa UM, wanaohatarisha maisha, kuhudumia umma wa Afghanistan, na alisisitiza kazi muhimu za UM nchini humo hazitopwelewa kwa sababu ya mashambulio ya karibuni, na aliahidi zitaendelea kutekelezwa licha ya kuwepo hatari kadha wa kadha dhidi ya watumishi wa kimataifa. Vile vile KM alizungumzia kuhusu matarajio yake juu ya maafikiano kwenye majajdiliano yaudhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa. Alikumbusha majadiliano ya Copenhagen ni mazito na magumu kwa sababu hujumuisha watendaji wengi na maafikiano ya vipande vipande; na ailitilia mkazo ni muhimu kwa Mataifa Wanachama kuwa na makubaliano ya pamoja, yalio ya jumla, yenye wizani wa kuridhisha, pamoja na usawa na hukumu ya lazima.

05/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

KM azisihi serikali za kimataifa kuzingatia kikamilifu matatizo ya uhamaji

Mnamo siku ya leo, KM Ban Ki-moon ambaye yupo Athens, Ugiriki akihudhuria Mkutano Mkuu wa Tatu wa Dunia juu ya Fungamano kati ya Maendeleo na Tatizo la Uhamaji, alihadharisha kwenye hotuba yake kwamba sera zinazohusu kuruhusu wahamaji wa kigeni kuingia nchini au la, ni lazima zibuniwe kwa kutia maanani zile taarifa zenye uhakika na sio chuki na ubaguzi dhidi ya wageni.

04/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu huru wa UM aihimiza Mauritania kuongeza bidii ya kufyeka milele utumwa mamboleo

UM umeripoti kwamba Serikali ya Mauritania na jumuiya za kiraia zimeshirikiana kuchukua hatua muhimu, ili kupambana na aina mpya ya utumwa mamboleo katika nchi.

04/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ndege za WFP zimeanzisha operesheni za kudondosha chakula Sudan Kusini baada ya mvua kali kuharibu barabara

wfpairplane

Shirika la UM Juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha, Alkhamisi iliopita, operesheni za kudondosha, kutoka angani, misaada ya chakula inayohitajika kuhudumia watu 155,600 katika Sudan Kusini, ambapo barabara hiko zimeharibiwa na mvua kali zilizonyesha katika siku za karibuni, na kukwamisha shughuli za kusafirisha misaada ya kihali kwenye eneo.

04/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo muhimu yamepatikana Sudan Kusini katika upokonyaji wa silaha

Press Conference: Mr. Ashraf Qazi Special Representative for Sudan UN PHOTO / Spanish Unit

Mjumbe Maalumu wa UM kwa Sudan, Ashraf Jehangir Qazi, Ijumanne, kwenye mazungumzo ya duru ya meza nchini Sudan juu ya taratibu za kuwajumuisha kwenye maisha ya kawaida wapiganaji wa zamani, alipongeza mafanikio yaliopatikana mwaka huu kwenye utekelezaji wa mradi wa kupokonya, kutawanya na kuwaunganisha na maisha ya kijamii wale wapiganaji wa zamani wanaokadiriwa 15,000, walioshiriki kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka mingi kati ya Sudan Kaskazini na Sudan Kusini.

04/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

un flags 012b

Kwenye taarifa aliotoa KM Ban Ki-moon Ijumanne, kwa waandishi habari, alielezea kuvunjika moyo juu ya kuendelea kwa vitendo visio halali vya Israel, kwenye eneo liliokaliwa kimabavu la Jerusalem Mashariki, ambapo alisema nyumba za WaFalastina zilibomolewa kihorera, na aila kadha zilifukuzwa kutoka majumbani mwao, mastakimu ambayo baadaye walikabidhiwa walowezi wa Kiisraili waliojisakama, kwa nguvu, katika mitaa ya WaFalastina. Vitendo hivi, alionya KM, ni miongoni mwa mambo yenye kupalilia mazingira ya wasiwasi na kudhoofisha zaidi hali ya kuaminiana miongoni mwa makundi yanayohusika na mvutano wa Mashariki ya Kati. Aliisihi Israel kusitisha, halan, vitendo hivi vya uchokozi. Kadhalika, KM alitoa mwito ziada unaoitaka Israel kutekeleza zile ahadi ilizotoa kabla, kuhusu mapendekezo ya Ramani ya Amani juu ya Suala la Mashariki ya Kati, na kusimamisha shughuli zake zote kwenye makazi ya walowezi, ikijumlisha pia vile vitendo vya kutaka kupanua zaidi majengo yaliopo kwenye maeneo yaliokaliwa; na vile vile Israel ilinasihiwa ing’oe haraka vituo vyote vya mbali vya uangalizi na, hatimaye, iruhusu taasisi za KiFalastina zifunguliwe baada ya kufungwa kwa kitambo, ili zianze kuendesha shughuli zake halali katika eneo la Jerusalem Mashariki.

04/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama limepitisha ajenda ya majadiliano kwa Novemba

Leo asubuhi wajumbe wa Baraza la Usalama walikutana kushauriana juu ya ajenda ya kazi kwa mwezi Novemba.

03/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mvua kali Kenya zimewanyima makazi maelfu ya raia

Kenya Map UN Spanish Radio

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imechapisha taarifa iliobainisha baadhi ya maeneo katika Kenya, hivi sasa yamepigwa na mvua kubwa kabisa, yenye taathira mbaya kieneo, licha ya kuwa sehemu kubwa ya nchi babdo inaendelea kusumbuliwa na athari za ukame uliotanda kwa muda mrefu huko katika kipindi cha karibuni.

03/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa kidini na wasio wa kidini wanasihiwa na KM kuhusu ulazima wa kudhibiti kipamoja taathira za mabadiliko ya hali ya hewa

Kadhalika, Ijumanne, KM Ban Ki-moon alihutubia mkusanyiko wa viongozi wa kidini na wale wasiohusiana na dini, katika Kasri ya Windsor, juu ya ulazima wa kushughulikia kipamoja matatizo yanayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

03/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ana matumaini juu ya matokeo ya Mkutano wa Copenhagen

KM Ban Ki-moon, alinakiliwa akisema anaamini itifaki muhimu itakamilishwa mwezi ujao, kwenye Mkutano Mkuu wa Copenhagen, kuhusu udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

03/11/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

UNHCR yapeleka misaada ya dharura kufarajia Waangola waliofukuzwa JKK

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kuwa Ijumamosi, ilituma Angola, kutoka Afrika Kusini, ndege zilizobeba shehena ya misaada ya kufarajia kihali, makumi elfu ya raia wa Angola waliorejea nchini kwao mwezi uliopita, baada ya kufukuzwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).

03/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Russian Radio

Michele Montas, Msemaji wa KM aliulizwa kwenye mahojiano ya Ijumanne na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu kama kuna ukweli juu ya madai ya ripoti ya shirika lisio la kiserikali, linalochunguza utekelezaji wa haki za binadamu linaloitwa Human Rights Watch, kuhusu ukiukaji wa haki za kiutu uliofanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mwaka huu, ambapo wanajeshi wa brigedi ya 213 ya Vikosi vya Taifa vya FARDC walituhumiwa kushiriki kwenye "mauaji na uvunjaji sheria dhidi ya darzeni ya raia" katika eneo la mashariki la JKK. Alain Le Roy, Naibu KM juu ya Operesheni za Ulinzi Amani za UM, anayezuru eneo la mashariki la JKK, mapema wiki hii, alinakiliwa akisema Ijumatatu kwamba Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) na jeshi la FARDC wanalazimika kuanzisha, haraka, uchunguzi juu ya madai ya ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia ulioendelezwa na wanajeshi wa taifa; na wakati huo huo alitangaza MONUC itasitisha mchango wake kwenye uenezaji na usafirishaji wa wanajeshi wa brigedi 213 ya FARDC kwenye operesheni za pamoja, ili kusubiri matokeo ya uchunguzi juu ya wanajeshi waliohusika na vitendo haramu dhdi ya raia vilivyofanyika katika eneo la mashariki la JKK. Msemaji wa KM Michele Montas aliwaambia waandishi habari wa Makao Makuu, New York kuna "ushahidi unaoaminika" kwamba wanajeshi wa FARDC walihusika na mauaji ya raia 62, ikijumlisha fungu kubwa la wanawake na watoto wadogo, yaliofanyika katika eneo la mapigano la Lukweti, kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, baina ya miezi ya Mei na Septemba 2009. Vikosi vya MONUC katika siku za nyuma vilishirikiana na wanajeshi wa FARDC kwenye operesheni za kuwang'oa waasi Wahutu wa Rwanda waliopiga kambi katika Kivu Kaskazini.

03/11/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mgombea uraisi Afghanistan alijitoa kwenye duru ya pili ya uchaguzi ambayo anasema hairidhishi kisheria

abdullah-abdullah

Mgombea uraisi wa Afghanistan, Abdullah Abdullah, aliripotiwa Ijumapili kujitoa kwenye duru ya pili ya uchaguzi ilioandaliwa kufanyika tarehe 07 Novemba.

02/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahalifu wanane wa makosa ya vita Sierra Leone wahamishiwa kifungoni Rwanda

scsl

Wahalifu wanane waliopatikana na hatia ya kushiriki kwenye jinai ya vita na makosa dhidi ya utu, na Mahakama Maalumu juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone (SCSL), Ijumaa walisafirishwa kutoka vituo vya kufungia watu viliopo Freetown, Sierra Leone na kuhamishiwa kwenye Jela ya Mpanga, iliopo Kigali, Rwanda, kutumikia adhabu yao. Mahakama ya SCSL, inayoungwa mkono na UM, iliamua kuwapeleka wafungwa hawo wanane Rwanda kwa sababu magereza ya Sierra Leone hayatoshelezi viwango vya sheria ya kimataifa.

02/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umeanzisha mradi mkuu wa kusambaza vifaa vya kusajili wapiga kura Sudan

UNMIS. UN Photo/Fred Noy-UN Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS) na Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) yameanzisha operesheni kuu, za kugawa vifaa vya uchaguzi vitakavyotumiwa kusajilia wapiga kura kuanzia Ijumatatu ya leo.

02/11/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930