Nyumbani » 30/10/2009 Entries posted on “Oktoba, 2009”

Hapa na pale

Ijumaa asubuhi KM Ban Ki-moon, akijumuika na wafanyakazi wa UM waliopo kwenye Mkao Makuu, pamoja na maofisa wa vyeo vya juu, ikijumlisha Naibu KMAsha-Rose Migiro walikusanyika kwenye Ukumbi wa Baraza la Udhamini kuwakumbuka watumishi wenziwao watano waliouawa Ijumatano, na wapinzani wa Taliban, ndani ya nyumba ya wageni, kwenye mji wa Kabul, Afghanistan. Watumishi waliouawa walitokea Philippines, Marekani, Ghana na Liberia. Mtu wa tano hajatambuliwa bado uraia wake, ikisubiriwa matokeo ya vipimo vya afya vinavyoendelezwa na madakatari kuthibitisha asili ya maiti. Kabla ya wafanyakazi wa UM kusikiliza taarifa ya KM juu ya tukio, na miradi inayoandaliwa kuimarisha usalama wa watumishi wa UM waliopo nje, hasa katika Afghanistan, walisimama wima kimya kwa dakika moja kuwakumbuka na kuwaombea wenziwao waliouawa na shambulio la bomu la kujitoa mhanga. Baadaye mke wa askari wa usalama aliyeuawa kutoka Ghana alihutubia mkusanyiko huo na aliomboleza juu ya kifo cha mumewe, marehemu Lawrence Mefful. Kwenye risala yake, KM alisema UM sasa hivi unafanya mapitio ya dharura juu ya mazingira ya usalama, kwa ujumla, nchini Afghanistan. Alisema UM unazingatia vile vile uwezekano wa kupeleka vikosi ziada vya usalama kuhakikisha majengo ya UM yanapatiwa ulinzi na hifadhi bora kujikinga na mashambulio.

30/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu milioni moja huuawa kila mwaka na maradhi ya chakula kisio salama, imehadharisha WHO

Nembo ya WHO

Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), wanaohusika na maradhi yanayosababishwa na chakula, wamekusanyika wiki hii mjini Geneva kujadilia hatari ya vyakula visio salama, na hadhi ya maisha bora yanayohitajika kwa umma wote wa dunia.

30/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa mpya ya WHO kuhusu homa ya A/H1N1

Hii leo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza taarifa mpya juu ya maendeleo, katika udhibiti bora wa homa ya mafua ya A/H1N1.

30/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa Kudhibiti Nimonia

Tarehe 02 Novemba, itaaadhimishwa, kwa mara ya kwanza na walimwengu, kuwa ni Siku ya Kimataifa Kudhibiti Homa ya Vichomi/Nimonia.

30/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM aomba msaada ziada kuhudumia usalama kwa watumishi wa UM

Alkhamisi, KM Ban Ki-moon ametoa onyo lenye kuhadharisha ya kuwa, hivi sasa, watumishi wa UM hivi sasa tumegeuzwa kuwa “walenghwa dhaifu”, na yale makundi yalionuia kutuhujumu kihorera, bila kujali adhabu.

30/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa wanachama 187 yalaumu vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba kwenye Baraza Kuu

Mnamo Ijumatano ya wiki hii, kwa mwaka wa 18 mfululizo, wawakilishi wa kimataifa kwenye Baraza Kuu la UM walipiga kura ya kuunga mkono, kwa mara nyengine tena, azimio la kuishtumu Marekani kwa vikwazo vyake vya kiuchumi, kifedha na kibiashara dhdi ya Cuba.

30/10/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA imepokea jawabu ya awali ya Iran kuhusu yuraniamu halisi kwa viwanda vya utafiti wa tiba

Mohamed ElBaradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Nishati ya Nyuklia kwa Matumizi ya Amani (IAEA) leo amepokea jawabu ya awali kutoka Serikali ya Iran kuhusu pendekezo linaloitaka madini ya yuraniamu halisi, inayotumiwa kwenye Kiwanda Cha Utafiti wa Matibabu cha Teheran kupelekwa nchi za nje kusafishwa.

29/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo ya nchi zinazoibuka kutoka mapigano yatafutiwa suluhu ya kudumu na UM

Warsha Maalumu juu ya Chakula na Mizozo ya Kiuchumi kwenye Mataifa Yaliobuka kutoka Mapigano na Vita ulifanyika asubuhi kwenye Makao Makuu.

29/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unasema ‘majaribio ya mauaji ya raisi Usomali ni hujma dhidi ya raia wote’

Majaribio mawili ya karibuni ya kutaka kumwua Raisi wa Usomali, Sharif Sheikh Ahmed yalilaaniwa vikali kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliotolewa na Mjumbe Maalumu wa UM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah, ambayo aliyafananisha na mashambulio ya mauaji dhidi ya raia wote wa Usomali.

29/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkariri wa UM anayetetea haki za wateswa amefukuzwa Zimbabwe

manfred nowak

Manfred Nowak, Mtaalamu wa UM juu ya masuala ya mateso, na vitendo vyengine visio vya kiutu vyeye kudhalilisha hadhi ya ubinadamu, alkhamisi alitangaza, kutokea Johannesburg, Afrika Kusini ya kuwa ana wasiwasi juu ya madai ya kuwepo hali mbaya, iliokiuka haki za kiutu za wafungwa, katika magereza ya Zimbabwe, taarifa aliowakilisha saa 24 baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia nchini humo kuendeleza uchunguzi kuhusu madai hayo.

29/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unafanya mapitio juu ya utaratibu wa ulinzi wa watumishi wake Afghanistan

Tunaanza na taarifa kuhusu hali ilivyo sasa kwa watumishi wa UM nchini Afghanistan, kufuatia tukio la shambulio la bomu la kujitoa mhanga liliofanyika mapema Ijumatano, kwenye nyumba ya wageni mjini Kabul, ambapo, kwa mujibu wa ripoti za awali, watu wanane waliuawa, ikijumlisha watumishi watano wa UM, na sio sita, kama tulivyotangaza hapo jana.

29/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

KM amemteua Dktr. David Nabarro kuwa Mjumbe M aalumu juu ya Udhibitaji Bora wa Lishe na Chakula duniani. Jukumu la Dktr. Nabarro hasa litakuwa ni kumsaidia KM kuhimiza mataifa kutumia miradi ya kizalendo ya kujitegemea chakula maridhawa na udhibiti bora wa lishe, kwa kufuata taratibu za jumla, zenye malengo yalioratibiwa kujumuisha kipamoja mchango muhimu wa mashirika ya kimataifa, ili kukuza misaada inayohitajika kutekelza huduma hizo kwa mafanikio. Tangu mwezi Januari mwaka huu, Dktr. Nabarro alidhaminiwa madaraka ya kushughulikia masuala yanayohusu chakula, na kuandaa taratibu za kuimarisha akiba ya chakula duniani kwa madhumuni ya kutosheleza mahitaji ya umma wa kimataifa.

29/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Mfanyakazi mmoja wa Kituo cha Kufyeka Mabomu Yaliotegwa Cyprus (MACC), raia wa Msumbiji, aliuawa leo kwenye ajali iliotukia wakati akiendeleza operesheni zake. Kifo hiki ni cha kwanza kutukia. katika miaka mitano ya shughuli hizi kisiwani Cyprus. Mwaathirika wa ajali hiyo anaitwa Femisberto Novele, na alifariki baada ya bomu liliotegwa kuripuka, katika milango ya saa mbili za asubuhi, kwenye uwanja ulioambukizwa vijibomu viliotegwa ardhini, karibu na sehemu ya Geri, iliopi kilomita 10 kusini-mashariki ya mji wa Nicosia. Taye-Brook Zerihoun, Mjumbe Maalumu wa UM kwa Cyprus na mkuu wa Vikosi vya UM Kulinda Amani Cyprus (UNFICYP) alisema alishtushwa na kuhuzunishwa na ajali iliosababisha kifo cha Novele, tukio ambalo, alitilia mkazo, lilikuwa ni msiba kwa UM, unaokumbusha hatari wanayokabiliwa nayo wafanyakazi wa kimataifa wanaohudumi ufyekaji wa mabomu yaliotegwa, ambayo yamenea katika sehemu kadha katika Cyprus. Zerihoun aliwatumia mkono wa pole ukoo wa marehemu Novele, kwa niaba ya timu ya watumishi wa UM waliopo Cyprus. Mradi wa MACC husimamiwa na Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) na tangu 2004, wafanyakazi wa Kituo cha MACC walifanikiwa kuondosha na kuangamiza mabomu 14,000 yaliotegwa, na kusafisha maeneo 57 yaliotegwa mabomu, yanayojumuisha kilomita za mraba milioni 6.5 za ardhi.

28/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakulima wadogo wadogo wa Tanzania kupatiwa na FAO misaada ya kukuza kilimo na taaluma ya masoko

fao-logo-gde

Shirika la UM kuhusu Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti juu ya mradi utakaotumiwa kuimarisha kilimo katika Tanzania, unaokusudiwa kuwasaidia wakulima kuongeza uwezo wa kufikia masoko na kuuza bidhaa zao, hali ambayo itakuza akiba ya chakula nchini.

28/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Zimbabwe imemnyima Mkariri wa Haki za Bindamu ruhusu ya kuingia nchini

Manfred Nowak, Special Rapporteur on torture and other cruel, inhuman or degrading treatment or punishment. UN Spanish Radio

Serikali ya Zimbabwe imeripotiwa kuzuia ziara ya Manfred Nowak, mtaalamu wa UM juu ya masuala yanayohusu mateso, na vitendo vyengine visio vya kiutu vinavyodhalilisha hadhi ya ubinadamu.

28/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICTR imeanzisha warsha wa mafunzo maalumu kwa walimu na wanafunzi kuhusu shughuli zake

Ijumanne ya tarehe 27 Oktoba 2009, Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) imeanzisha, kwa mara ya kwanza, Warsha Maalumu wa kuwahusisha walimu na wanafunzi wa skuli za sekandari kutoka wilaya za Rulindo na Musanze, ziliopo Rwanda Kaskazini,

28/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelezo mafupi juu ya mkutano wa kila mwezi wa KM na waandishi habari

Kadhalika, leo asubuhi, kwenye Makao Makuu ya UM, KM Ban Ki-moon, alifanyisha mazungumzo ya kila mwezi na waandishi habari wa kimataifa.

28/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watumishi sita wa UM wauawa na bomu la kujitolea mhanga Kabul

Taarifa za Idara ya Habari ya UM zimeeleza kwamba watumishi 6 wa UM walikuwa miongoni mwa watu 12 waliouawa kwenye shambulio la bomu la kujitoa mhanga, liliofanyika mapema Ijumatano, katikati ya mji wa Kabul, Afghanistan, kwenye nyumba ya wageni inayotumiwa na wafanyakazi wa UM.

28/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Photo

Baraza la Usalama limekutana leo, awali, kwa mashauriano juu ya Lebanon, na kufuatiwa na mapitio kuhusu vikwazo vilioekewa Cote d’Ivoire na UM. Ripoti ya mwisho ya Tume Maalumu ya Wataalamu juu ya Cote d’Ivoire ilithibitisha mzozo wa taifa hili la Afrika Magharibi umeonekana kuchukua sura tofauti, na hauhusu tena mikwaruzano baina ya jimbo la kaskazini na kusini pekee, bali pia inajumlisha makabiliano baina ya wahusika kadha wengineo ambao baadhi yao hupinga rai ya Cote d’Ivoire kuungana, na wengine wangelipendelea kuona taifa lao linaungana. Ripoti ya Tume ilieleza vile vile eneo la kaskazini linashabihiana, sasa hivi, na mazingira ya uchumi unaoendeshwa na majemadari wa vita (warlords) badala ya sehemu ya taifa ilio chini ya himaya ya serikali. Makamanda wa vita wa kundi la waliokuwa waasi wa Forces Nouvelles wanaosimamia 'maeneo huru’ wanaoyadhibiti na kunyonya mali ya asili ya Cote d’Ivoire, ndio sehemu za nchi zinazowachumia mapato. Tume ya Wataalamu ilisema inashughulishwa na tatizo la uhamishaji wa silaha na baruti, pamoja na risasi, kutoka Burkina Faso wanazopelekewa waasi wa Forces Nouvelles, kadhia ambayo Tume ilibashiria hufungamana na biashara ya magendo ya kuuza kakao. Vile vile biashara haramu ya kuuza almasi ilikutikana kufanyika kati ya Cote d’Ivoire na Burkina Faso na Mali, kwa kupitia Guinea na Liberia, kwa sababu ya ukosefu wa udhibiti wa mipaka baina ya mataifa haya.

27/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM yajitahidi kuhamasisha Mataifa Wanachama, yatakapokutana Copenhagen, kukamilisha mapatano juu ya udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa

Janos Pastzor, Mkuu wa Timu ya Ushauri kwa KM juu ya Masuala Yanayohusu Udhibiti wa Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa alinakiliwa akiwaarifu waandishi habari waliokusanyika kwenye mahojiano yaliofanyika Ijumatatu alasiri katika Makao Makuu, kwamba UM una matarajio ya wastani kuhusu uwezekano wa kuwa na mapatano ya sheria ya kulazimisha, kutokana na mkutano mkuu ujao utakaofanyika mwezi Disemba, katika Copenhagen,

27/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO kuanzisha mashauriano ya kubuni miongozo halisi juu ya umiliki bora wa mali ya asili

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeanzisha mashauriano ya awali kihistoria, na wadau kadha wa kimataifa kusailia miongozo inayohitajika kimataifa juu ya udhibiti bora wa umiliki wa ardhi na rasilmali nyengine za kimaumbile, mathalan, maji safi, rasilmali ya uvuvi na mali ya asili ya misitu.

27/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya WHO imethibitisha ‘mamilioni ya vifo vya mapema huzuilika kukiimarishwa afya ya msingi’

Ripoti mpya iliochapishwa siku ya leo na Shirika la Afya Duniani (WHO) ilieleza kwamba mamilioni ya vifo vya kabla ya wakati duniani vinaweza kuzuiliwa, kwa kushughulikia mapema matatizo ya aina tano yenye kuhusu afya.

27/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

“Wakati umewadia, kuharakisha utekelezaji wa lengo la tano la MDGs, na kupunguza vifo vya uzazi”, asema Mkuu wa UNFPA

Thoraya Ahmed Obaid,Executive Director United Nations Population Fund. UN Photo/UN Spanish Radio

Ijumatatu kwenye mji wa Addis Ababa, Ethiopia, kulifanyika Mkutano wa Wadhifa wa Juu kuzingatia maendeleo katika utekelezaji wa suala la tano la Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kupunguza umaskini na ufukara katika mataifa yanayoendelea.

27/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Ijumapili alasiri, KM Ban Ki-moon ameripoti kuwa na huzuni kuu juu ya ripoti kuhusu shambulio la gari liliobeba bomu, lilioripiliwa katikati ya mji wa Baghdad, ambapo mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa. Alishtumu vikali vitendo hivi vya kutumia mabavu, kihorera, vitendo ambavyo mara nyingi huwalenga raia na hudhamiria kuchafua juhudi za kurudisha utulivu na amani katika Iraq. KM aliwahimiza umma wote wa Iraq kutunza maendeleo yao ya kisiasa yaliofikiwa nchini kwa sasa, licha ya kuwa wanakabiliwa na matukio ya vurugu la kukirihisha la mara kwa mara, na aliwasihi wasibadilishe tarehe ya kufanyisha uchaguzi ya 16 Januari 2010, na kutarajia upigaji kura utakuwa huru na wa haki.

26/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahakama Maalum juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone imekataa rufaa ya wahukumiwa waasi wa RUF

Hukumu ya mwisho ya Mahakama Malumu juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone, imeidhinisha adhabu iliopitishwa kabla, dhidi ya viongozi watatu wa kundi la waasi la RUF, iendelee kutekelezwa kwa kulingana na makosa waliotuhumiwa nayo, ikijumlisha makosa ya kufanyisha ndoa za kulazimishwa, kitendo ambacho kilitafsiriwa kuharamisha ubinadamu, na vile vile yale makosa ya kuhujumu walinziamani wa kimataifa – na hii ni mara ya kwanza kwa mahakama za kimataifa kuchukua hatua hii ya kisheria. Mahakama ya Maalumu ya Sierra leone ilikataa kabisa maombi yote ya rufaa ya washtakiwa, isipokuwa ombi moja la mtuhumiwa Agustine Gbao, ambaye hapo kabla alishtakiwa kuendeleza adhabu za jamii, hukumu ambayo ilibatilishwa. Hata hivyo, Gbao ataendelea kutumikia kifungo cha miaka 25 gerezani.

26/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Halaiki ya raia milioni moja ziada wang’olewa makazi kutoka maeneo ya kati na mashariki barani Afrika: OCHA

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mnamo miezi sita iliopita, kutukia muongezeko halisi wa wahamiaji wa ndani (IDPs) milioni moja ziada katika mataifa ya Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.

26/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kusailia uhusiano bora wa kulinda amani Afrika kati ya UM na UA

Asubuhi ya leo, kwenye ukumbi wa Baraza la Usalama, Manaibu KM wawili juu ya Masuala ya Ulinzi Amani – yaani Alain Le Roy, anayehusika na Operesheni za Ulinzi Amani, pamoja na Susana Malcorra, anayesimamia huduma za nje za mashirika ya ulinzi amani, waliwakilisha mapendekezo yao kuhusu hatua za kuimarisha, kwa vitendo, uwezo wa vikosi vya Umoja wa Afrika, kujenga na kudumisha amani kwenye maeneo yaliojivua kutoka vipindi vya fujo na vurugu, na vile vile walizingatia taratibu za kuimarisha uhusiano bora kati ya shughuli za UM na Umoja wa Afrika.

26/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utekaji nyara wa mtumishi wa ICRC Darfur kulaaniwa na ofisa wa UM kwa Sudan

Mratibu wa UM juu ya Masuala ya Kiutu kwa Sudan, Ameerah Haq amelaani vikali utekwaji nyara wa mtumishi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) anayeitwa Gauthier Lefevre, mwenye uraia wa Kiingereza/Ufaransa, unyakuzi uliofanyika Alkhamisi iliopita, wakati mtumishi huyo alipokuwa anarejea nyumbani kwake Al Geneina, mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi.

26/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatari ya nzige Mauritania imedhibitiwa kwa akali ya kutia moyo, imeripoti FAO

desert locusts

Shirika la UM juu ya [Maendeleo ya] Chakula na Kilimo (FAO), limeripoti ya kuwa opereshini za kienyeji, za kudhibiti miripuko ya uvamizi wa nzige katika taifa la Mauritania, zimefanikiwa kuzuia wadudu hawa kutosambaa nchini au kuenea kwenye maeneo jirani ya mataifa ya kaskazini, na kuangamiza mazao na uwezo wa wakulima kupata riziki.

26/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ijumaa usiku KM Ban Ki-moon alifungua rasmi Tafrija ya Muziki kwenye ukumbi wa Baraza Kuu, kuadhimisha Siku Kuu ya UM, ambayo kikawaida, huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 24 Oktoba. Mwaka huu Siku Kuu ya UM inaadhimishwa Makao Makuu tarehe ya leo kwa sababu, tarehe 24 Oktoba 2009 imeangukia Ijumamosi, ambapo maofisi huwa yanafungwa kwa sababu ya mwisho wa wiki. Mada ya taadhima za mwaka huu ina kaulimbiu isemayo “Tuwahishimu Walinzi Amani”. Kwenye risala yake KM alipongeza mchango muhimu wa walinzi amani wa kimataifa, waume na wake 115,000 waliojitolea mhanga kurudisha utulivu na amani katika yale maeneo ya ulimwengu yalioambukizwa na machafuko na hali ya wasiwasi. Alikumbusha walinzi amani wa UM ni miongoni mwa “mabalozi bora kabisa” wa taasisi yetu ya kimataifa.

23/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uganda: Mratibu Mkuu wa UM juu ya Misaada ya Kiutu asihi umuhimu wa kinga ya mapema dhidi ya hatari ya maafa

John Holmes, Naibu KM juu ya Misaada ya Kiutu na Masuala ya Kufarajia Misaada ya Dharura, alipozuru jimbo la Karamoja, Uganda kaskazini Ijumaa ya leo, alisihi juu ya umuhimu wa kupunguza hatari ya maafa kwa kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye sehemu hizo za nchi.

23/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ayapongeza Mataifa ya Afrika kwa kuidhinisha chombo kipya cha sheria kulinda haki za wahamiaji wa ndani

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amekaribisha, kwa furaha kuu, maafikiano ya kuwa na mkataba wa kihistoria kuhusu hifadhi ya wahamiaji wa ndani ya nchi katika Afrika, ambao uliidhinishwa leo hii kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Wakuu wa Mataifa Wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika Uganda.

23/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO imechapisha mwongozo mpya kusaidia utetezi wa haki ya kupata chakula

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limechapisha taarifa inayojulikana kama “taarifa ya utaratibu wa sanduku la vifaa” juu ya haki ya kupata chakula, mfumo ambao umekusudiwa kuzipatia nchi wanachama, taasisi za kimataifa, jumuiya za kiraia na wadau wengineo hati zinazofaa kutumiwa kutetea haki ya kupata chakula, haki ambayo ni sawa na haki za kimsingi za wanadamu.

23/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuhadharisha, watu milioni sita ziada Ethiopia wanahitajia misaada ya chakula kuwavua na janga la njaa

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti Ethiopia imezongwa na mshtuko mkuu wa maafa yenye kuathiri hali ya chakula kwa watu milioni 6 nchini.

23/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya NEPAD azungumzia mwelekeo unaohitajika kusukuma mbele maendeleo Afrika

Mapema wiki hii, kabla ya kuzungumzia kikao cha Baraza Kuu la UM, kusailia ripoti kadha za KM, na kutoka wajumbe wa kimataifa na mashirika ya UM zilizozingatia huduma za kukuza maendeleo katika Afrika, Dktr Ibrahim Assane Mayaki, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Ushirikiano Mpya wa Maendeleo kwa Afrika (NEPAD), alifanya mahojiano maalumu na waandishi habari waliopo Makao Makuu.

23/10/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Homa ya nguruwe wa Afrika imeripotiwa kutapakaa Urusi Kaskazini, imehadharisha FAO

Nembo ya FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza ya kuwa ule ugonjwa maututi wa nguruwe, wenye kutambulika kama homa ya nguruwe wa Afrika (ASF), mnamo tarehe 20 Oktoba umegunduliwa katika eneo la St Petresburg, liliopo kaskazini-magharibi katika Urusi, kilomita 2,000 kutoka kusini ya Urusi ambapo maradhi haya yalikutikana hapo kabla.

22/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waathirika milioni sita ziada wa ukame Ethiopia wanahitajia misaada ya dharura ya chakula

Serikali ya Ethiopia na mashirika ya kimataifa yenye kuhusika na misaada ya kiutu yametangaza kunahitajika mchango wa dharura ziada wa dola miilioni 175 kwa mwaka huu, kuhudumia kihali watu milioni 6.2 walioathirika sana na mavuno haba na ukame wa muda mrefu uliosakama katika Ethiopia katika kipindi cha karibuni.

22/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinzi amani wa UNAMID wasaidia kukomesha mapambano ya kikabila Darfur Kaskazini

Ofisi ya Msemaji wa KM imeripoti walinzi amani wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) walilazimika wiki hii kuingilia kati kuzuia mapambano makali ya kikabila yaliotukia karibu na eneo la Shangil Tobaya, Darfur Kaskazini baina ya makabila ya Zaghawa na Birgid.

22/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makampuni ya bima yajiunga na UM kudhibiti ‘uchumi wa kijani’

achim steiner

Kampuni za kimataifa za bima, zinazodhibiti rasilmali inayogharamiwa matrilioni ya dola, zimejiunga na wataalamu mashuhuri wa kimataifa kwenye uchunguzi, wenye kuungwa mkono na UM, wa kuhakikisha viwanda vinatumia utaratibu unaosarifika na usiochafua mazingira.

22/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IFAD inasema uhamishaji wa fedha wa wafanyakazi wa Afrika waliopo nje unaweza kustawisha maisha ya vijiji

Logo IFAD. IFAD/UN Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) limewasilisha ripoti mpya inayozingatia athari za kiuchumi zinazofungamana na uhamishaji wa malipo ya fedha, unaoendelezwa na wafanyakazi wa kutoka Afrika waliopo nchi za kigeni.

22/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

United Nations Headquarters UN PHOTO / Spanish Radio

KM Ban Ki-moon amehuzunishwa na kifo cha Brigedia Jenerali Ahmed Moinuddin, Makamu Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi Amani vya UM katika Sudan Kusini (UNMIS), ambaye aliuawa Alkhamisi, mnamo tarehe 22 Oktoba, baada ya shambulio liliotukia Islamabad, Pakistan wakati akiwa mapumzikoni. KM alitumia salamu za pole ukoo wa wafiwa, wafanyakazi wa UNMIS na kwa Serikali ya Pakistan, na alitumai watu walioendeleza shambulio, watashikwa haraka na kufikishwa mahakamani.

22/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wairaqi, Waafghani na Wasomali waongoza jumla ya waomba hifadhi katika mataifa yenye maendeleo ya viwanda

Ripoti mpya iliotolewa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kuhusu maombi ya hifadhi ya kisiasa katika nchi zenye maendeleo ya viwanda, imebainisha ongezeko la asilimia 10 ya maombi hayo katika nusu ya mwanzo ya 2009, tukilinganisha na kipindi hicho hicho katika mwaka uliopita.

21/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA imewasilisha maafikiano ya awali kuzingatiwa kuhusu nishati ya nyuklia kwa Iran

Mohamed El Baradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) leo Ijumatano aliwaambia waandishi habari wa kimataifa kwamba baada ya siku mbili na nusu ya majadiliano mjini Vienna, taasisi yao imepitisha maafikiano ya awali kuhusu taratibu za kutumiwa kuisaidia Iran kupata nishati itakayotumiwa na kiwanda chao cha kiraia cha kufanyia utafiti wa matibabu.

21/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisa wa UNICEF anasema watoto wamedhurika zaidi na athari za mgogoro sugu wa JAK

UNICEF Deputy Executive Director Hilde Johnson speaks with the mother of two severely malnourished children at a UNICEF-supported centre in Kembata Tembaro, near Ethiopia's Gurage Zone.

Hilde Johnson, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), baada ya kuzuru Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK) ameeleza kwamba matatizo yaliolizonga taifa hilo huathiri pakubwa watoto wadogo, na hali hiihuenda ikaharibika zaidi pindi wahisani wa kimataifa watashindwa kuharakisha misaada inayohitajika kidharura kuhudumia kihali watoto hawa.

21/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za ndege za UM, za kugawa misaada ya kiutu Ethiopia, zahatarishwa kusitishwa

Jumuiya ya Kundi Linalotumia Huduma za Usafiri wa Ndege za Kugawa Misaada ya Kiutu, ambalo hujulikana kama Kundi la UNHAS, imetangaza leo kwamba italazimika kusitisha operesheni zake nchini Ethiopia – hasa kwenye lile Jimbo la raia Wasomali – kwa sababu ya upungufu wa fedha kutoka wahisani wa kimataifa.

21/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi Haki za Binadamu wa UM alalama, jamii ya kimataifa yawavunja moyo wahamiaji wa ndani wa Usomali

Walter Kaelin, Mjumbe wa KM juu ya Masuala Yahusuyo Haki za Binadamu za Wahamiaji wa Ndani Waliong’olewa Makazi, amekamilisha ziara ya wiki moja nchini Usomali kutathminia hali ya umma ulionaswa kwenye vurugu liliopamba katika taifa hili la Pembe ya Afrika.

21/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Asubuhi, Baraza la Usalama lilikutana kusailia hali katika Afrika Magharibi. Haile Menkerios, KM Msaidizi juu ya Masuala ya Kisiasa alipohutubia Baraza la Usalama alizungumzia juu ya ziara yake ya karibuni katika Guinea na maeneo jirani, iliokusudiwa kuandaa utaratibu wa kulisaidia Bodi la Uchunguzi la UM kuendeleza ukaguzi wa vyanzo vya fujo ziliozuka nchini tarehe 28 Septemba mwaka huu. Alisema wadau husika wengi nchini Guinea pamoja na kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi kwa Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wote, kwa pamoja, wanaunga mkono rai ya kuanzisha Bodi la Uchunguzi la kimataifa litakaloshughulikia tukio la Septemba. Baada ya mkutano wake na Baraza la Usalama, Menkerios alizungumza na waandishi habari waliopo Makao Makuu, ambao aliwaeleza kuhusu dhamira ya KM ya kuanzisha uchunguzi wa vurugu la Guinea haraka iwezekanavyo, pindi atapatiwa idhini ya kuyafanya hayo na Baraza la Usalama. Menkerios alisema Raisi wa Guinea, Dadis Camara amemuahidi kuwa atashirikiana kikamilifu na tume ya uchunguzi ya UM.

21/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya IFAD inasema ushuru wa kutuma fedha Afrika kwa wafanyakazi waliopo nje ni mkubwa

Logo IFAD. IFAD/UN Spanish Radio

Shirika la Mfuko wa Kimataifa juu ya Huduma za Maendeleo na Kilimo (IFAD) limechapisha ripoti mpya ya utafiti ulioendelezwa na taasisi hii juu ya mchango wa malipo ya fedha wanazotuma makwao wafanyakazi wa Afrka waliopo nchi za nje.

20/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM inaunga mkono rai ya kuhishimu kikamilifu “mfumo wa kikatiba” kuambatana na uchaguzi wa Afghanistan

Hamid Karzai president of Afghanistan U.N. Spanish Unit

Asubuhi KM Ban Ki-moon aliwaambia waandishi habari waliopo Makao Makuu kuwa anaikaribisha taarifa ya Raisi wa Afghanistan Hamid Karzai, ilitilia mkazo umuhimu wa kuhishimu na kufuata kanuni za katiba kuhusu uchaguzi, ambapo pindi wagombea uraisi watashindwa kupata asilimia inayohitajika, itabidi uchaguzi urudiwe tena ili kumpata mshindi halali.

20/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR inasema wahamiaji wa Angola waliofukuzwa JKK wanahitajia misaada ya dharura ya kuwavua na janga la njaa

Nembo ya UNHCR

Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) leo asubuhi aliwaarifu waandishi habari Geneva kwamba makumi elfu ya raia wa Angola waliofukuzwa kutoka JKK, ambao sasa wamewekwa kwenye vituo kadha vya makazi ya muda kwenye mji wa Mbanza-Congo, Angola kaskazini, wapo kwenye hali mbaya na wanahitajia misaada ya dharura kunusuru maisha. UNHCR ilipeleka Mbanza-Congo, katika mwisho wa wiki iliopita, ujumbe maalumu wa kutathminia mahitaji ya wahamiaji wa Angola waliofukuzwa kutoka JKK.

20/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufukuzaji wa raia baina ya Angola na JKK waongeza kasi, imehadharisha UM

OCHA imeripoti kwaamba katika kipindi cha miezi miwili iliopita, imeshuhudia muongezeko mkubwa wa idadi ya wahamiaji wa JKK wanaofukuzwa kutoka Angola, na kulazimishwa kuvuka mipaka kurejea makwao.

20/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA inasema haki za binadamu zinaendelea kuharamishwa na makundi yanayohasimiana katika JKK

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Elizabeth Byrs, Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) leo aliwaambia waandishi habari mjini Geneva kwamba taasisi yao inalaani ukiukaji wa haki za binadamu, unaoendelezwa na makundi yanayohasmiana katika JKK.

20/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetangaza tena ilani ya kuwahadharisha walimwengu kwamba zaidi ya watu milioni 23 wanaoishi katika Pembe ya Afrika, huenda wakaathiriwa na mvua kali na mafuriko yanayoashiriwa kuchochewa na mfumo wa hali ya hewa ya El Nino. Taarifa ya OCHA ilitilia mkazo ya kuwa umma unaokabiliwa na hatari ya kudhurika zaidi na hali hiyo – katika mataifa ya Usomali, Kenya, Uganda, Tanzania na Djibouti na Eritrea na Ethiopia – ni zile jamii zinazojumlisha wafugaji, wakazi wa vijijini, wakulima pamoja na wahamiaji wa ndani na wale wa kutoka nchi za kigeni.

20/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya waliong’olewa mastakimu Kivu Kaskazini waanza kurejea makwao, imetangaza OCHA

ocha

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kwamba katika miezi miwili iliopita, inakadiria watu 110,000 waliong’olewa makazi na mapigano waliweza kurejea makwao katika jimbo la Kivu Kaskazini la JKK.

19/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Abu Garda ametuhumiwa makosa ya vita na ICC

International Criminal Court logo

Vile vile tukizungumzia Sudan, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC), ambayo inakutana leo Ijumatatu mjini Hague, Uholanzi imethibitisha kuwepo mashtaka ya makosa ya vita dhidi ya kiongozi wa waasi wa Darfur, Bahr Idriss Abu Garda ambaye anatuhumiwa kuhusika na mashambulio dhidi ya walinzi amani wa Umoja wa Afrika katika Sudan mnamo tarehe 29 Septemba 2007.

19/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID imehadharisha, mapigano huenda yakafufuka tena Darfur Kazkazini

UNAMID peacekkeping, Sudan, Darfur ALBANY ASSOCIATES / STUART PRICE./Russian Radio

Kadhalika, Shirika la UNAMID limeelezea wasiwasi mkubwa kuhusu muongezeko wa vikosi vya Serikali ya Sudan na waasi wa kundi la SLA la Abdul Wahid katika maeneo ya Sortony na Kabkabiya, yaliopo Darfur Kaskazini, vitendo ambavyo vilishuhudiwa, kihakika, na waangalizi wanajeshi wa UNAMID.

19/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majambazi wameshambulia kihorera polisi watatu wa UNAMID katika Darfur Magharibi

Mnamo Ijumamosi iliopita, kwenye eneo la Zalingei, Darfur Magharibi majambazi wasiotambuliwa waliwapiga risasi na kujeruhi walinzi amani polisi watatu, wanaowakilisha Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID), na imeripotiwa hali ya majeruhi wawili kuwa ni mbaya sana kwa hivi sasa.

19/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali za Africa zajiendeleza kiutawala, lakini rushwa bado inakithiri, inasema ripoti ya UM

ECA says Africa's relatively high growth in the past few years has a very strong global background

Ripoti mpya ya UM, iliotolewa tarehe 16 Oktoba 2009, kusailia shughuli za utawala katika bara la Afrika, ilibainisha ya kuwa katika miaka minne iliopita, maendeleo machache yalipatikana kwenye viini vya harakati za utawala, na ilidhihirisha, tatizo la ulajirushwa katika Afrika, lilifurutu ada na kuongezeka kwa kiwango kikubwa katika kipindi hicho.

19/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

un flag 011b

John Holmes, Naibu KM Mdogo juu ya Masuala ya Kiutu anatazamiwa kufanya ziara maalumu Uganda kuanzia tarehe 20 mpaka 24 Oktoba, ili kuhudhuria Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Afrika (UA) juu ya Wahamiaji, Warudiwaye Makwao na Wahamiaji wa Ndani wa Afrika. Kadhalika, wakati Holmes atakapokuwepo Uganda anatazamiwa kufanya tathmini juu ya hali nchini Uganda, ambapo jumuiya ya wahudumia misaada ya kiutu inashirikiana na Serikali kuhakikisha watu milioni mbili waliong'olewa makazi na mashambulio ya waasi wa kundi la LRA huwa wanapatiwa suluhu na utulivu wa kudumu wa kuridhisha kimaisha.

19/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti nchi ziliopo kwenye Pembe ya Afrika, ambazo karibuni zilisumbuliwa na ukame wa kihistioria, hivi sasa zinajiandaa kukabilina tena na maafa mengine yanayoletwa na majira ya hali ya hewa ya El Nino, hali ambayo inatarajiwa kuzusha mafuriko makuu kwenye eneo hilo. OCHA ilitahadharisha kuna uwezekano mkubwa mataifa ya Kenya, Usomali, Tanzania na Uganda huenda yakadhurika na miporomoko ya ardhi kwa sababu ya El Nino, mfumo wa hali ya hewa unaotarajiwa pia kuathiri na kuharibu mavuno, kuzusha maradhi yanayosababishwa na maji machafu na kuharibu mitandao ya mabarabara. Kadhalika, OCHA imesema maafa hayo huenda yakadhuru vile vile mataifa ya Djibouti, Eritrea na Ethiopia. John Holmes, Mratibu wa Misaada ya Kufarajia Dharura alidhihirisha ya kuwa watu milioni 23 sasa hivi wanapepesuka, na kusumbuka, na athari za upungufu wa chakula na maji safi na salama, na vile vile wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya malisho ya wanyama, migogoro sugu na hali ya wasiwasi ambayo huathiri sana jamii za wakulima, wafugaji na wale wenye kuishi kwenye mitaa ya mabanda ya vitongoji vya miji mikuu, na huathiri pia wahamiaji wa ndani ya nchi na kutoka mataifa jirani.”

16/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkariri Huru wa Haki za Binadamu akaribishwa kuzuru Zimbabwe kwa mara ya awali

Manfred Nowak, Mkariri Maalumu Huru wa haki za binadamu, anayelenga shughuli zake kwenye masuala yanayohusu mateso, na adhabu nyengine katili zilizokiuka utu, ameripotiwa kuwa amepokea mwaliko rasmi kutoka Serikali ya Zimbabwe kulizuru taifa hilo la kusini mwa Afrika,

16/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tarehe 17 Oktoba inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa Kuufyeka Umaskini

Mnamo Ijumamosi, tarehe 17 Oktoba, UM utaadhimisha Siku ya Kimataifa Kufyeka Umaskini.

16/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Chakula Duniani

Siku ya leo inaadhmishwa na UM kama ni Siku ya Chakula Duniani. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) watu bilioni moja ziada wanasumbuliwa na njaa sugu ulimwenguni kwa sasa, na hawana uwezo wa kupata chakula.

16/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu laidhinisha ripoti ya mashambulio ya Ghaza, na kuishtumu Israel kwa makosa ya vita

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu, leo limepitisha azimio la kuidhinisha ripoti ya Jaji Richard Goldstone ilioandaliwa na Tume ya Kuchunguza Ukweli juu ya Mzozo wa Tarafa ya Ghaza, ripoti ambayo ilituhumu vikosi vya Israel na wapambanaji wa KiFalastina kufanya makosa ya vita.

16/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya Goldstone inazingatiwa kwenye mjadala wa kila mwezi wa Baraza la Usalama juu ya Mashariki ya Kati

Ijumatano Baraza la Usalama liliitisha kikao, ambacho rasmi, kilidaiwa kuzingatia hali ya Mashariki ya Kati, kwa ujumla, kama inavyofanyika mara kwa mara, takriban kila mwezi, hapa kwenye Makao Makuu.

16/10/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya raia wa Kihutu katika JKK yalaumiwa na Mtetezi wa Haki za Binadamu

Mr. Philip Alston, United Nations Special Rapporteur on extrajudicial, summary or arbitrary executions. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Philip Alston, Mkariri/Mtetezi Maalumu wa UM juu ya Haki za Binadamu dhidi ya Mauaji ya Kihorera Nje ya Sheria, hii leo ametoa taarifa maalumu kuhusu JKK.

15/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya ICC inazingatia matukio ya karibuni Guinea

International Criminal Court

Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) leo amenakiliwa akithibitisha ya kuwa Ofisi yake imeanzisha uchunguzi maalumu kuhusu tukio la Guinea, ambapo mwezi iliopita waandamanaji wa upinzani, wanaokadiriwa 150 waliuawa huko na vikosi vya usalama, pale walipokusanyika kwenye mkutano wa hadhara.

15/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO inakhofia kunywea kwa Ziwa Chad huenda kukazusha maafa ya kiutu kieneo

lake_chad

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti juu ya kunywea kwa mali ya asili ya maji katika Ziwa Chad, hali ambayo itaathiri uwezo wa watu milioni 30 wanaoishi karibui na eneo hilo kupata rizki.

15/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Aliyekuwa ofisa wa upelelezi Rwanda kukana mashtaka ya Mahakama ya ICTR

Idelphonse NIZEYIMANA, aliyekuwa ofisa wa idara ya upelelezi katika Rwanda, amekana makosa ya kushiriki kwenye mauaji ya halaiki pale alipohudhuria Ijumatano Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR), kuandikisha jibu la kesi alioshtakiwa na mahakama hiyo.

15/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Tarehe ya leo, kwa mwaka wa pili mfululizo, inaadhimishwa kimataifa kuwa ni 'Siku ya Kukumbushana Kuosha Mikono Duniani’, siku ambayo inahishimiwa na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwea Watoto (UNICEF). Kwenye taarifa iliotolewa na UNICEF ilitilia mkazo umuhimu wa watu kuosha mikono kwa maji safi na sabuni, na kukumbusha kadhia hii ni mojawapo ya huduma za afya kinga zenye matokeo yanayoridhisha, hali ambayo kila mwanadamu anaimudu bila ya gharama kuu.

15/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAMID imelaani shambulio la vikosi vyake katika Darfur

Unamid patrol 08b

UM umepokea ripoti zenye kueleza mnamo Ijumatatu usiku, saa 3:45 majira ya Sudan, majambazi watatu, wasiotambuliwa, waliochukua bunduki, walifyatua risasi kwenye kituo cha ulinzi cha Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) katika eneo la Kutum, Darfur Kaskazini na kumjeruhi askari mlinziamani mmoja.

14/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF/WHO zimeanzsiha mradi wa kuzuia vifo vya watoto wachanga vinavyosababishwa na kuharisha

Kadhalika, Shirika la UNICEF na Shirika la Afya Duniani (WHO) yameripotiwa kuanzisha mradi mpya wa pamoja, wenye makusudio ya kukinga na kuwatibu watoto na maradhi ya kuharisha – ikiwa ni ugonjwa wa pili wenye kusababisha vifo kwa wingi zaidi miongoni mwa watoto wachanga katika nchi zenye hali duni ya uchumi.

14/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF imeingiwa wahka na kuporomoka kwa afya ya watoto wa Pembe ya Afrika

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaodhurika na ukame na njaa sugu katika eneo la Pembe ya Afrika.

14/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa Kupunguza Maafa

Tarehe 14 Oktoba huadhimishwa na UM, kila mwaka, kuwa ni Siku ya Kimataifa Kupunguza Maafa (ISDR). Kampeni ya mwaka huu ya kuihishimu siku hiyo inalenga shughuli na taadhima zake zaidi kwenye juhudi za “kuzikinga hospitali na madhara ya maafa ya kimaumbile”.

14/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO/WFP zahadharisha, mizozo ya uchumi huifanya hali dhaifu ya chakula duniani kuwa mbaya zaidi

Ripoti ya pamoja ya mashirika mawili ya UM yanayohusika na miradi ya chakula na kilimo, yaani FAO na WFP, iliotolewa leo Ijumatano, imeeleza kwamba mzozo wa uchumi uliopamba ulimwenguni kwa sasa ndio uliopalilia tatizo la njaa duniani, kwa kiwango cha hali ya juu kabisa cha kihistoria, ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu 1970.

14/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Naibu KM juu ya Masuala ya Kisiasa, B. Lynn Pascoe anatazamiwa kufanya ziara ya wiki moja katika kusini na mashariki ya Afrika kuanzia tarehe 15 mpaka 23 Oktoba, kwa madhumuni ya kuimarisha uhusiano bora na Mataifa Wanachama pamoja na mashirika ya kikanda, hususan kwenye zile juhudi za kuwahi kuzuia mizozo kabla haijafumka au kuripuka kwenye maeneo hayo, na katika kuimarisha amani na ujenzi wa mazingira ya utulivu baada ya kusitishwa mapigano kwa mafanikio. Miongoni mwa mataifa atakayozuru Pascoe inajumlisha Afrika Kusini, Angola, Burundi, Kenya na Uganda. Vile vile ofisa huyu wa UM atakutana, kwa mashauriano, na viongozi wa maeneo anayoyazuru kuhusu Rwanda, hali katika JKK, maeneo yaliodhurika na mashambulio ya kundi la waasi wa Uganda wa Lord Resistance Army (LRA) na vile atajadilia nawo juu ya utekelezaji wa mpango amani katika Bukini. Zaidi ya hayo Pascoe atakuwa na mikutano, ya vyeo vya juu, na wawakilishi wa kiserikali na wale wanaojumlisha mashirika yasio ya kiserikali; na baadaye atazuru Bujumbura, Burundi yalipo makao makuu ya shirika la UM la ujenzi wa amani la BINUB, na vile vile kuzuru Ofisi ya UM juu ya Masuala ya Kisiasa kwa Usomali (UNPOS) iliopi Nairobi, Kenya.

14/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Flag Flies at Half-Mast UN PHOTO / Spanish Radio

Matokeo ya uchunguzi uliondelezwa bia na UM pamoja na Baraza la Mataifa ya Ulaya juu ya biashara haramu ya kuuza viungo, tishu za mwili na chembe za uhai, ambayo hujulikana kwa umaarufu kama biashara ya OTC, yamethibitisha kwamba walimwengu wanahitajia, kidharura, kuunda mkataba mpya, wa lazima, wa kimataifa ili kuzuia biashara ya magendo ya kuuza viungo vya wanadamu, na kuhakikisha waathirika wa jinai hii watalindwa kisheria, na kwa wakati huo huo kuhakikisha wakosa watafikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kuendeleza unyonyaji wa watu maskini na mafukara kwa kuwalazimisha kuuza viungo vyao kufanya pesa. Utafiti umependekeza kupiga marufuku, halan, biashara hii ya kufanya fedha kwa kuuza viungo vya kutoka mwili wa mwanadamu, na ilitaka kuundwe sheria itakayotumiwa kama ndio kigezo cha kusimamia kanuni zinazohusika na uhamishaji wa kiungo cha mwili wa mwanadamu, na wakati huo huo kuhamasisha watu kuamua kujitolea viungo, kwa hiyari, wakifariki, ili kusaidia kuongeza akiba ya viungo hivyo kwenye mahospitali, hali ambayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa viungo hivyo katika shughuli za matibabu. Mshauri Maalumu wa KM juu ya Masuala ya Kijinsiya na Maendeleo ya Wanawake, Rachel Mayanja aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliokusannyika hii leo Makao Makuu kwamba alitumai Baraza Kuu la UM litaandaa haraka msingi wa mkataba wa kupiga marufuku biashara haramu ya viungo kimataifa kwaminajili ya masilahi ya umma maskini.

13/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu kuzingatia hali ya maeneo yaliokaliwa kimabavu ya WaFalastina kwenye kikao maalumu

Russian Radio

Baraza la Haki za Binadamu litaitisha kikao maalumu Geneva mnamo Alkhamisi ya tarehe 15 Oktoba (2009), kuzingatia “hali ya haki za kiutu katika Eneo Liliokaliwa Kimabavu la Falastina na katika Jerusalem mashariki.”

13/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya chakula Kenya ni ya wasiwasi kwa sababu ya ukame, kuhadharisha UM

WFP Tana River, Kenya WFP

Ripoti iliotolewa na Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) kuhusu chakula katika Kenya imeeleza kuwepo hali ya wasiwasi ya chakula nchini humo, inayoendelea kuathiri mamilioni ya raia wa Kenya, kwa sababu ya kutanda kwa ukame wa muda mrefu kwenye eneo la Pembe ya Afrika.

13/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Udhalilishaji dhidi ya wanawake bado waendelezwa kwenye maeneo ya mapigano, atahadharisha ofisa wa kamati ya CEDAW

Nembo ya CEDAW

Naéla Gabr, mwenyekiti wa kamati inayosimamia utekelezaji wa Mkataba wa UM Kuondosha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW) Ijumatatu alipohutubia Baraza Kuu aliwaeleza wajumbe wa kimataifa kwamba vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji katili wa wanawake walionaswa kwenye mazingira ya mapigano bado umeselelea duniani,

13/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makumi elfu ya wahamiaji wa ndani Kivu Kaskazini warudi makwao

IDPs on the move towards Camp Bulengo, North Kivu

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kwenye ripoti iliotolewa leo hii ya kwamba tangu maafikiano ya amani kutiwa sahihi, mnamo mwezi Machi 2009, na makundi yanayohusika na uhasama uliopamba katika jimbo la Kivu katika JKK, watu 160,363 walion’golewa makazi baada ya kuishi kwa muda na aila zilizowapokea, na waliokuwa wakiishi “rasmi” kwenye kambi sita za wahamiaji wa ndani katika mji wa Goma, waliripotiwa kurejea makwao.

13/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati ya Pamoja juu ya Usalama Usomali yakutana Nairobi na yahimizwa na Mjumbe wa KM kuendelea na majadiliano ya amani

Mjumbe Maalumu wa UM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah aliripotiwa kuzungumzia ufunguzi wa mashauriano wa ile Kamati ya Pamoja kuhusu Usalama Usomali, iliokutana Ijumatatu asubuhi kwenye mji wa Nairobi, Kenya.

12/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM asema Mpango wa Utendaji wa Cairo juu ya uzazi bora bado haujatekelezwa kama inavyostahiki

Baraza Kuu la UM limeadhimisha leo hii miaka 15 tangu Mkutano wa Kimataifa juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu na Maendeleo uliofanyika Cairo katika 1994 kupitisha Mradi wa Utendaji wa Cairo.

12/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utafiti wa ILO/WFP umethibitisha ajira isio rasmi huzinyima nchi maskini natija za biashara ya soko la kimataifa

Utafiti ulioendelezwa bia karibuni na Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) na Shirika la Biashara Duniani (WTO) umegundua kuwa ajira kubwa isio rasmi hukutikana katika nchi zinazoendelea,

12/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Diouf afungua kikao muhimu cha kuzingatia akiba ya chakula duniani katika 2050

Ijumatatu kwenye mji wa Roma, Utaliana, Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeanza majadiliano ya siku mbili kuzingatia hali ya chakula ulimwenguni katika miaka 40 ijayo.

12/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

un flags 012b

KM amewasishi wajumbe waliohudhuria Mkutano wa “Mwito wa Cotonou” uliofanyika Ijumatatu, tarehe 12 Oktoba kwenye mji wa Cotonou, Benin, kuzingatia hatari ya biashara ya magendo ya dawa za bandia, kuuhifadhi umma wao na “madhara ya siri na uharamu” wa biashara hiyo. Risala ya KM ilisomwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la UM juu ya Maendeleo ya Uchumi kwa Afrika (ECA), Abdoulie Janneh, na iliyahimiza Mataifa Wanachama “kuunganisha uwezo wao kipamoja kupiga vita jinai ya dunia ya kuuza dawa bandia kwa minajili ya masilahi ya afya ya jamii ya kimataifa.” Mradi huu wa kampeni ya kuamsha hisia za kimataifa dhidi ya biashara haramu ya dawa za bandia ni uvumbuzi uliobuniwa na raisi mstaafu wa Ufaransa, Jacques Chirac.

12/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ijumamosi ya tarehe 10 Oktoba (2009) huadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kuwakumbuka Wagonjwa wa Akili Duniani. Risala ya KM kuihishimu siku hii ilieleza siku hii huupatia umma wa kimataifa fursa ya kuhamasisha walimwengu kuchangisha fedha na misaada mengine muhimu inayohitajika kukamilisha malengo ya kutoa uangalizi bora na uuguzaji unaoridhisha wa maradhi ya akili kwa wagonjwa husika, hasa katika mataifa yanayoendelea ambapo mahitaji ya huduma hiyo ni makubwa na uwezo uliopo kukabili janga hilo ni haba sana.

10/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya mwaka ya UNICEF juu ya hifadhi ya watoto imesisitiza bidii zaidi zahitajika kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji

Ripoti ya mwaka ya UNICEF kuhusu hifadhi ya watoto kimataifa imeeleza kwamba licha ya kuwa karibuni kulipatikana maendeleo kwenye suala hilo, watoto bado wanaendelea kudhalilishwa na kukabiliwa na vitendo karaha kadha wa kadha dhidi yao.

09/10/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

KM Ban Ki-moon ampongeza Raisi Obama kwa ushindi wa Tunzo ya Amani ya Nobel kwa 2009

Leo asubuhi KM Ban Ki-moon amekaribisha kidhati tangazo la kuwa Raisi Barack Obama wa Marekani amezawadiwa Tunzo ya Amani ya Nobel kwa 2009.

09/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imeonya wahamiaji wa JKK katika Burundi wasirejee makwao kwa sababu ya hali mbaya ya usalama

Nembo ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limerudia tena onyo kwa wahamiaji Wakongomano waliopo Burundi, kutorejea makwao katika Kivu Kusini.

09/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 160,000 katika JKK watafaidika na msaada wa chakula wa WFP uliovuka kilomita 1,000

Msafara wa malori 13 yaliobeba chakula, yanayomilikiwa na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) yamewasili kwenye mji wa Dungu wiki hii, eneo la kaskazini-mashariki katika JKK, baada ya safari ya kilomita 1,000 ambayo ilianzia Uganda, na kupitia Sudan Kusini, hadi Kongo.

09/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizi ya H1N1 kwenye kizio cha kusini cha dunia yameteremka,WHO imeripoti

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti maambukizi makubwa zaidi ya homa ya mafua ya A/H1N1 yanasajiliwa kutukia sasa hivi kwenye kizio cha kaskazini chaa dunia, kwa sababu eneo hili linaingia kwenye majira ya homa ya mafua kwa sasa.

09/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya Bangkok yamezaa matokeo yenye uwazi juu ya usanifu unaohitajika kujikinga na madhara ya kimazingira

Kikao cha majadiliano ya mwisho mwisho, kilichofanyika Bangkok, Thailand kwa muda wa wiki mbili kimekamilisha mazungumzo yake leo Ijumaa, miezi miwili kabla ya Mkutano wa kihistoria juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa utakaofanyika mwezi Disemba kwenye mji wa Copenhagen, Denmark.

09/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Usomali inasailiwa tena na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama asubuhi lilijadilia suala la Usomali kwenye kikao cha hadhara. NKM juu ya Masauala ya Kisiasa, B. Lynn Pascoe na Craig Boyd, ofisa wa Kitengo cha UM Kusaidia vikosi vya Ulinzi Amani vya UA katika Usomali (AMISOM) waliwakilisha ripoti zao kuhusu maendeleo nchini humo.

08/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNFCC anasema mchango ziada wa viongozi wa kimataifa unatakiwa kukamilisha Makubaliano ya Copenhagen

Head of UNFCCC Addresses Press Conference. UN Photo/Devra Berkowitz-UN Spanish Radio

Yvo de Boer, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM kuhusu Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) ameripoti kupatikana maendeleo ya kutia moyo, kwenye mazungumzo ya matayarisho ya waraka wa kuzingatiwa kwenye Mkutano wa Copenhagen juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

08/10/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

UM watahadharisha, uwekezaji mkubwa wa kilimo unatakikana 2050 kutosheleza mahitaji ya chakula kwa watu bilioni 9.1

fao-logo-gde

Wataalamu wa UM wameripoti kwenye makala ya majadiliano, iliochapishwa rasmi siku ya leo na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) kwamba kunahitajika kufanyika uwekezaji mkubwa wa katika sekta ya kilimo, kuhudumia chakula umma wa kimataifa kwa siku za baadaye, umma ambao ilisema unaendelea kuongezeka kwa kasi kuu.

08/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

KM ameiarifu Baraza la Usalama kwamba ana nia ya kumteua HanyAbdel Aziz wa Misri kuwa Mjyumbe Maalumu kwa Sahara ya Magharibi na Mkuu wa Shirika la um Kusimamia Kura ya Maoni katika Sahara Magharibi (MINURSO). Abdel-Aziz atachukua mafasi ya Julian Harston, ambaye ameteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Ofisi ya UM Belgrade kuanzia 01 Machi 2009. Abdel-Azizi ameshaitumikia UM kwa miaka 25, ambapo pia alitumikia mashirika manane ya UM yanayohusika na ulinzi amani na huduma za kugawa misaada ya kiutu. Hivi sasa Abdel-Aziz anatumikia ni Mkurugenzi wa Huduma za Misaada wa Shirika la MONUC katika JKK (DRC).

08/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

BU litazingatia ripoti ya tume ya Baraza la Haki za Binadamu juu ya Ghaza

gaza-mapa

Wajumbe wa Baraza la Usalama Ijumatano alasiri, baada ya mashauriano yao, walikubaliana kuitisha kikao cha kila mwezi kuzingatia suala la Mashariki ya Kati,

08/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Michael Williams, Mratibu Maalumu wa UM juu ya Suala la Lebanon, Ijumatano alikuwa na mazungumzo na Waziri wa Nchi za Kigeni wa Lebanon, Fawzi Salloukh. Baada ya hapo, kwenye mahojiano na waandishi habari alieleza kwamba UM ulifurahika sana kujua utulivu umerudishwa tena Lebanon kusini, na kwamba makundi yote yanayohusika na suala hili yameahidi kutekeleza mapendekezo ya Azimio 1701 la Baraza la Usalama juu ya Lebanon. Hata hivyo, Williams alisema yeye na Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon walikubaliana kuwa kuna mambo zaidi yaliosalia yanayohitajiwa kushughulikiwa kwa lengo la kudhibiti, kwa muda mrefu zaidi, hali ya kuacha mapigano na kuimarisha utulivu na amani iliopo hivi sasa kwenye lile eneo la Msitari wa Buluu. Vile vile Williams alirudia kusema ana matumaini majadiliano yatakayoendelea nchini kwa sasa yataruhusu kuundwa serikali mpya ya muungano wa taifa haraka iwezekanavyo.

07/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

BU lashauriana kuzingatia barua ya Libya juu ya ripoti ya Tume ya Goldstone kuhusu Ghaza

Alasiri, Baraza la Usalama lilikutana kushauriana juu ya barua iliotumiwa na Ubalozi wa Kudumu wa Libya katika UM, barua ambayo ilipendekeza kuitishwe kikao cha dharura, kuzingatia ripoti ya ile tume ya kuchunguza ukweli juu ya mashambulio ya Tarafa ya Ghaza yaliotukia mwisho wa 2008 na mwanzo wa mwaka huu.

07/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan mashariki inaendelea kupokea wahamiaji wa kutoka Eritrea/Ethiopia na Usomali

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetoa taarifa ya tahadhari, yenye kueleza kwamba miaka 40 baada ya operesheni zake kuanzishwa katika eneo la Sudan mashariki hakuna dalili wahamiaji wapo tayari kurejea, kwa khiyari, makwao.

07/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bukini imeomba vikwazo vilioekewa na jumuiya ya kimataifa viondoshwe

Kadhalika, Ijumanne, kwenye mji wa Antananarivo, Bukini, Mjumbe Maalumu wa UM, Tiebile Drame, alitangaza taarifa rasmi ya kutoka Kundi la Mawasiliano la Kimataifa juu ya Bukini ilioeleza kuwa inaunga mkono ombi la Serikali ya Bukini la kutaka vikwazo vilioekewa taifa hilo viondoshwe.

07/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM amekaribisha hatua ya kuunda serikali ya mpito Bukini

Ofisi ya msemaji wa KM imeripoti Ban Ki-moon ameyakaribisha kidhati mafanikio ya karibuni nchini Bukini katika kuunda Serikali ya Muungano wa Taifa.

07/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya raia wa JKK wafukuzwa Angola, imeripoti OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti wiki hii ya kwamba maelfu ya raia wa JKK wanaendelea kufukuzwa na kuondolewa Angola kwa sasa hivi, katika mazingira ambayo ni ya kutisha na kushtusha kabisa.

07/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa Benki Kuu ya Dunia ameahidi mabadiliko yanayofaa kukabili mizozo mipya ulimwenguni

Mkutano wa mwaka wa Kundi la Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) unaofanyika wiki hii kwenye mji wa Istanbul, Uturuki unazingatia mizozo ya kiuchumi na kifedha iliokabili ulimwengu katika kipindi cha hivi sasa.

07/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ijumanne KM alihitimisha ziara ya siku sita ya kutembelea mataifa ya Uswidin, Denmark na Uswiss. Kabla ya hapo, alijumuika asubuhi kwenye majadiliano ya meza ya duru, yaliokusanyisha Wakuu wa Serikali kutoka Mataifa Wanachama na maofisa wakuu watendaji (CEOs) wa makampuni ya kibiashara, waliohudhuria mkutano wa Geneva wa Shirika la Kimataifa juu ya Mawasiliano ya Simu (ITU). Kwenye hotuba yake KM aliwasihi mameneja wa makampuni, kutumia uwezo wao kuwahamasisha viongozi wa serikali za kimataifa waonyeshe ujasiri katika kutumia teknolojiya ya mawasiliano ya kisasa (ICT) nchini mwao, mfumo utakaowasaidia pia kutatua mizozo inayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, utaratibu utaowasilisha 'uchumi wa kijani’ wenye kutunza mazingira.

06/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maisha ni magumu kwa watoto duniani, kwa sababu ya ukosefu wa ulinzi unaofaa, inasema ripoti ya UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza ripoti mpya, siku ya leo, kutokea mjini Tokyo, Ujapani kuhusu hifadhi ya watoto kimataifa.

06/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM aisihi jumuiya ya kimataifa kuisaidia Serikali ya TFG Usomali kusalia

Ramani ya Somalia

Ripoti mpya ya KM juu ya hali katika Usomali, iliochapishwa hii leo, imeeleza kwamba licha ya kuwa Serikali ya Mpito (TFG) nchini humo, inaelekea iliokoka na matishio ya kupinduliwa na makundi ya wapinzani – makundi yaliopalilia mapigano katika kipindi cha karibuni – hata hivyo serikali bado inakabiliwa na vizingiti kadha wa kadha dhidi yake, hasa kwenye yale masuala yanayohusu usalama na utulivu wa kisiasa.

06/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoro wa pili wa makosa ya jinai ya halaiki Rwanda ametiwa mbaroni na ICTR

Ofisi ya Msemaji wa KM imeripoti kukamatwa kwenye mji wa Kampala, Uganda kwa Idelphonse Nizeyimana, aliyeshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) kushiriki kwenye mauaji ya Watutsi na Wahutu wenye siasa za wastani nchini Rwanda katika 1994.

06/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa ya Bahari ya Hindi kushiriki kwenye mazoezi ya tahadhari za mapema dhidi ya dhoruba za tsunami

Tsunami Maremoto Spanish Radio

UM umetangaza kwamba mnamo tarehe 14 Oktoba, nchi 18 ziliopo kwenye eneo linalojulikana kama Mzingo wa Bahari ya Hindi zitashiriki kwenye mazoezi ya tahadhari kinga dhidi ya ajali ya mawimbi ya tsunami.

06/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imehadharisha wahamiaji waliopo Burundi kutorudi JKK kwa sababu ya vurugu

Andrej Mahecic, msemaji wa shirika la UM linalohudumia wahamiaji la UNHCR, ameripoti kutoka Geneva kwamba taasisi yao imewashauri wahamiaji 2,300 wa JKK waliopo kwenye kambi ya Gihinga, katika jimbo la Mwaro, Burundi ya kati kutorejea makwao hivi sasa, kwenye lile jimbo la vurugu la Kivu Kusini, liliopo eneo la mashariki la JKK.

06/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Tarehe ya leo ni Siku ya Makazi Bora Duniani. Mada ya mwaka huu ya siku hiyo ni ile inayosema “Maandalizi ya Miji Bora kwa Siku za Baadaye”. Taadhima za 2009 zinafanyika kwenye mji mkuu wa Marekani wa Washington D.C., na ni mara ya kwanza kwa sherehe hizi kuadhimishwa katika taifa la Marekani.

05/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

BU lasisitiza wanawake washirikishwe kikamilifu katika ujenzi wa amani

Baraza la Usalama (BU) leo limefanyisha mkutano wa hadhara, wa siku nzima, ambao wawakilishi wa kimataifa 55 walizungumzia kuhusu suala la 'Wanawake, Amani na Usalama’.

05/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku Kuu ya Kuwahishimu Walimu Duniani

Tarehe ya leo, tarehe 05 Oktoba, huadhimishwa na UM kuwa ni 'Siku ya Walimu Duniani’. Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Taasisi ya Takwimu ya Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kuanzia 2007 hadi 2015 kulihitajika kuajiriwa walimu milioni 10.3 kwa walimwengu kuweza kukamilisha, kwa wakati, lengo la kuwapatia ilimu ya msingi watoto wote wa kiume na wa kike wanaostahiki kuhudumiwa kadhia hiyo.

05/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pengo la ustawi laendelea kupanuka baina ya mataifa tajiri na maskini, imebainisha kiashirio cha HDI

Kwenye taarifa kuhusu Kiashirio cha Matokeo ya Utafiti juu ya Maendeleo ya Wanadamu, ambacho hujulikana kama Kiashirio cha HDI, iliowakilishwa mapema wiki hii, iliripotiwa kwamba licha ya kuwa nchi nyingi wanachama zilionyesha kuwa na maendeleo ya kiuchumi na kijamii mnamo miaka 25 iliopita, hata hivyo, pengo la tofauti kuhusu ustawi wa jumla, na hali njema baina ya nchi tajiri na nchi maskini, linaendelea kupanuka.

05/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa yalaani mauaji ya watumishi wa UM Islamabad

Ijumatatu mchana, kwenye mji wa Islamabad, Pakistan watumishi watano wa UM wanaofanya kazi na Ofisi ya UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) waliuawa baada ya kufanyika shambulio la bomu la kujitolea mhanga kwenye jengo lao, tukio ambalo vile vile lilisababisha makorja ya majeruhi, baadhi yao wakiwa katika hali mbaya kabisa na ambao hivi sasa wanapatiwa matibabu hospitali.

05/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Chinese Unit

Mapema Ijumaa, KM BanKi-moon alikutana mjini Stockholm na Spika wa Bunge pamoja na wawakilishi wa vyama vya kisiasa. Baada ya hapo KM alikuwa na mazungumzo na wawakilishi wa mashirika yasio ya kiserikali ya Uswidini. Kufuatia hapo KM alielekea Copenhagen, ambapo alitarajiwa kukutana kwa mazumgumzo na Waziri Mkuu wa Denmark, Lars Lokke Rasmussen, na vile vile Jacques Rogge, Raisi wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC). Ijumamosi KM atahutubia Baraza Kuu la Olimpiki ambapo aantazamiwa kujadilia ajenda ya Kamati ya IOC kuhusu Hifadhi ya Mazingira kwenye Shughuli za Michezo.

02/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa ya Kutotumia Nguvu wala Mabavu

Hii leo UM unaadhimisha Siku ya Kimataifa Dhidi ya Matumizi ya Nguvu. Risala ya KM juu ya siku hii imetoa mwito maalumu unaoutaka umma wote wa kimataifa kuiadhimisha siku hiyo kwa kukumbushana urithi wa kimaadili wa Mahatma Gandhi ambaye aliwahimiza walimwengu kutatua mifarakano yao kwa taratibu za amani, zisiotumia nguvu, mabavu wala fujo.

02/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu limeakhirisha kupitisha azimio juu ya mashambulio ya katika Tarafa ya Ghaza

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu limeakhirisha kuidhinisha ile ripoti maalumu ya Tume ya Uchunguzi juu ya Mzozo wa Tarafa ya Ghaza.

02/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano mapya Usomali huathiri zaidi raia, kuhadharisha UNHCR

Dalsan (Somalia NGO)

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti mfumko wa mapigano ya karibuni katika jimbo la Kati-Kusini la Usomali yamechochea tena wimbi la wahamiaji wapya wa ndani walioamua kuelekea maeneo jirani kutafuta hifadhi.

02/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO imeanzisha mradi wa kuotesha aina mpya ya mpunga Uganda kuwasaidia wakulima waathirika wa mapigano

Ripoti ya Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) imeeleza kwamba wahamiaji wa ndani ya nchi milioni 1.5 waliohajiri makazi yao baada ya miaka 20 ya mapigano na vurugu katika Uganda kaskazini, wameonekana hivi sasa wanaanza kurejea makwao baada ya kuishi maisha ya wasiwasi kwa muda mrefu nje ya maeneo yao.

02/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwanaharakati wa kuhifadhi mazingira ahimiza viongozi wa dunia kuharakisha mapatano ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Ripoti ya wiki hii itazingatia fafanuzi za mwanaharakati mashuhuri wa Afrika Mashariki anayetetea hifadhi ya mazingira ulimwenguni, kwa madhumuni ya kunusuru maisha ya vizazi vya siku za baadaye. Mwanaharakati huyo ni Profesa Wangari Maathai, mzalendo wa Kenya.

02/10/2009 | Jamii: Makala za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Vietnam yachukua madaraka ya kuongoza Baraza la Usalama kwa Oktoba

Kuanzia siku ya leo, Vietnam imekabidhiwa Uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba. Balozi wa Kudumu wa Vietnam katika UM, Le Luong Minh, sasa hivi anashauriana na wajumbe wa Baraza la Usalama juu ya ratiba ya mwezi huu kuhusu shughuli zao.

01/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM inaadhimisha Siku Kuu ya Kuwahishimu Watu Waliozeeka

Siku ya kimataifa ya wazee

Tarehe ya leo, Oktoba 01, inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Watu Waliozeeka. Kwenye risala aliotuma KM kuihishimu siku hii, alitoa mwito maalumu uitakayo walimwengu kukomesha tabia ya kubagua wazee wenye umri mkubwa.

01/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi wa haki za binadamu anasema mzozo wa Usomali ni msiba mkubwa wa kiutu ulimwenguni

Baraza la Haki za Binadamu linalokutana Geneva wiki hii, limearifiwa na Mtaalamu Huru juu ya haki za binadamu kwa Usomali, ya kwamba hali katika taifa hili la Pembe ya Afrika ni miongoni mwa mizozo ya kiutu mibaya mno iliojiri katika ulimwengu.

01/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa kihistoria kupiga vita H1N1 umeanzishwa na mashirika ya UM katika Zimbabwe

Kwenye warsha wa siku mbili, uliomalizika Zimbabwe leo hii, kulipitishwa mradi wa kihistoria wenye makusudio ya kuimarisha uwezo wa kukabiliana na maambukizi ya janga la homa ya mafua ya A/H1N1 ya 2009, hususan katika nchi maskini.

01/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufufuaji uchumi wapamba moto duniani, kuripoti IMF

Ripoti ya karibuni ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) juu ya hali ya uchumi duniani, imeeleza kwamba kwenye soko la kimataifa, kumeanza kushuhudiwa dalili za kutia moyo, za kukua kwa uchumi, baada ya serikali kadha kuingilia kati masoko yao ya kifedha, kwa kuchangisha msaada wa kufufua shughuli zao na kupunguza hali ya wasiwasi iliojiri, ili kukidhi bora mahitaji ya umma.

01/10/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Baada ya wajumbe wa Baraza la Usalama kusikiliza taarifa ya Haile Menkerios, KM Msaidizi juu ya Masuala ya Kisiasa, Ijumatano, kuhusu fujo zilizozuka Guinea, walitoa taarifa maalumu iliobainisha wasiwasi wao kuhusu mauaji yaliofanyika tarehe 28 Septemba pale jeshi la Askari wa Guinea liliposhambulia kwa risasi, kwenye mji wa Conakry, raia na kuua watu wanaokadiriwa 150 na kujeruhi mamia wengineo. Ripoti zilisema wanajeshi vile vile walinajisi kimabavu wanawake, kweupe mchana, kwenye mitaa. Wajumbe wa Baraza la Usalama wamelaumu kwa kauli kali vitendo hivyo, na wakatui huo huo kuwahimiza wenye mamlaka kukomesha haraka fujo na vurugu nchini mwao, na kuhakikisha watawafikisha mahakamani wakosaji wa jinai ya kijinsiya. Kadhalika walinasihiwa kuwaachia kutoka vizuizini wafungwa wote wa kisiasa.

01/10/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930