Nyumbani » 30/09/2009 Entries posted on “Septemba, 2009”

Hapa na pale

KM ameamua kumrudisha Peter Galbraith kutoka Afghanistan na kumwachisha madaraka ya Naibu Mjumbe Maalumu wa KM kwa Shirika la Usaidizi Amani la UM katika Afghanistan (UNAMA). Kwenye taarifa aliotumiwa Galbraith na KM, Ban Ki-moon alimshukuru kwa bidii yake kubwa ya kazi na mchango muhimu wa kitaalamu aliojumuisha wakati alipokuwa mtumishi wa kiraia wa kimataifa anayetumikia UM. KM alichukua uamuzi wa kumwachisha kazi Galbraith kwa maslahi bora ya shirika la UNAMA. KM alikariri kuunga mkono moja kwa moja kazi za Mjumbe Maalumu wa UM kwa Afghanistan, Kaie Eide.

30/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAMID imekamilisha thuluthi mbili ya maofisa wa polisi wanaohitajika kulinda raia

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) leo limeripoti kuwasili kwenye mji wa El Fasher, wiki hii, maofisa wa polisi 130 watakaotumiwa kuimarisha usalama kwenye kambi za wahamiaji wa ndani ya nchi.

30/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu anataka kufanyike uchunguzi wa haraka Guinea juu ya mauaji ya kihorera ya karibuni

Kamishna Mkuu wa UM kuhusu Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa mwito wa kubuniwa tume maalumu ya uchunguzi, itakayopelekwa Guinea, kutathminia ripoti inayoeleza Ijumatatu vikosi vya usalama vya Guinea viliua kihorera raia walioandamana mjini Conakry, waliowakilisha kundi la upinzani.

30/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama kupendekeza UM uwe na Mjumbe Maalumu dhidi ya unyanyasaji wa kijinsiya

Baraza la Usalama lilkutana Ijumatano kuzingatia suala la hifadhi ya raia dhidi ya vitendo vyote vya kutumia mabavu na unyanyasji wa kijinsia, kwenye mazingira ya mapigano, hususan kwa raia wanawake na watoto wadogo.

30/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wagonjwa milioni nne wenye VVU wamefanikiwa sasa hivi kupatiwa tiba ya ART, kurefusha maisha

Kuanzia mwisho wa 2008, watu milioni 4 wanaoishi kwenye nchi zenye pato la chini na la wastani, walioambukizwa virusi vya UKIMWI, walifanikiwa kupata zile dawa za matibabu za kurefusha maisha za ART. Jumla hii inawakilisha ongezeko la asilimia 36, kwa mwaka, la wagonjwa wanaotibiwa kwa dawa ya ART.

30/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raisi wa BK anatabiri ‘enzi mpya ya uhusiano wa kimataifa’ wakati wa kufunga majadiliano ya wawakilishi wote

Ijumanne mchana Baraza Kuu la UM lilikamilisha wiki moja ya majadiliano ya mwaka ya wawakilishi wote, ambapo wajumbe kutoka nchi 192 walizungumza, ikijumlisha Wakuu wa Mataifa na Serikali 107, waliowasilisha hoja kadha juu ya sera za kuendeleza uhusiano wa kimataifa.

30/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS) limekaribisha amri ya utendaji iliotangazwa na Raisi Omar al-Bashir wa Sudan kusimamisha, haraka, zile sheria za ukaguzi na uchunguzi wa magazeti katika nchi. UNMIS iliripoti pindi uamuzi huo utatekelezwa utasaidia kuendeleza na kuimarisha mapendekezo ya Mapatano ya Amani ya Jumla (CPA) baina ya eneo la kaskazini na kusini, na kuandaa mazingira bora ya kutayarisha uchaguzi wa vyama vyingi uliopangwa kufanyika Aprili 2010.

29/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

KM ameridhika na mahojiano ya awali kwenye kikao cha mwaka cha BK

KM Ban Ki-moon alifanya mahojianio na waandishi habari kwenye Makao Makuu ya UM, leo asubuhi, na aliwaambia wanahabari kwamba maendeleo makubwa yalipatikana tangu kikao cha 64 cha Baraza Kuu (BK) kuanza rasmi wiki iliopita, ambapo viongozi wa dunia walifikia maafikiano kadha kwenye juhudi zao za kutafuta suluhu ya kuridhisha ya masuala makuu yanayotatanisha ulimwengu wetu, ikijumlisha udhibiti wa madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, ukomeshaji wa silaha za maangamizi za kinyuklia na kwenye mizozo ya kifedha katika soko la kimataifa.

29/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID imelaani shambulio la Darfur Magharibi dhidi ya wafanyakazi raia na wanajeshi

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limelaani vikali shambulio dhidi ya moja ya msafara wao wa ulinzi, liliotukia Ijumatatu usiku kwenye mji wa El Geneina, mji mkuu wa Darfur Magharibi na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa ulinzi amani.

29/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP/Taasisi ya Mradi wa Vijiji vya Milenia zaungana kupunguza wenye njaa na utapiamlo Afrika

Hunger Bytes! WFP and You Tube video competiton. WFP/UN Spanish Radio

Kadhalika, mapema wiki hii Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP), likijumuika na mpango wa maendeleo unaoungwa mkono na UM, unaoitwa Mradi wa Vijiji vya Milenia, yameanzisha bia mradi mwengine mpya unaojulikana kama mradi wa “maeneo huru dhidi ya ukosefu wa chakula cha kutosha” utakaotekelezewa vijiji 80 katika nchi 10 za Afrika, kusini ya eneo la Sahara.

29/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame katika Uganda unaitia wasiwasi WFP

WFP-Logo

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti rasmi hii leo kuingiwa wasiwasi kuhusu mfululizo wa mvua haba katika Uganda kwenye majira ya mvua, hali iliosababisha watu milioni mbili kukosa uwezo wa kupata chakula na kuomba wasaidiwe chakula na mashirika ya kimataifa kunusuru maisha.

29/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Namibia kuyasihi Mataifa Wanachama kupitisha hatua kali dhidi ya serikali zinazochukua madaraka kimabavu

Majadiliano ya wawakilishi wote bado yanaendelea kwenye ukumbi wa Baraza Kuu na yameingia siku ya sita hii leo.

29/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matayarisho ya mkutano wa Copenhagen yanavuta kasi Bangkok

Wajumbe wa kimataifa wanaokutana kwa sasa mjini Bangkok, Thailand Ijumatatu walianzisha majadiliano yanayokaribia duru ya mwisho ya maandalizi ya mkutano mkuu ujao wa Copenhagen,

28/09/2009 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Utata wa kwenye mapigano ya kisiku hizi unakwamisha huduma za UNHCR, anasema Guterres

Antonio Guterres 06a

Kwenye hotuba ya ufunguzi wa kikao cha 60 cha bodi la utawala la Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), Kamishna Mkuu wa Taasisi hiyo, Antonio Guterres, alisema kuongezeka kwa mizozo na vurugu yenye utata, isiowahi kushuhudiwa katika miaka iliopita, hali hiyo imezusha mazingira yenye kuhatarisha zaidi zile juhudi za mashirika ya UM za kuokoa maisha na kunusuru waathirika wa

28/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Tume ya Kuchunguza Ukweli juu ya Mzozo wa Tarafa ya Ghaza inatazamiwa kuwakilisha ripoti ya matokeo ya ziara ya uchunguzi wao, mbele ya wajumbe wa Baraza la Haki za Binadamu, Ijumanne asubuhi, mjini Geneva. Ripoti itawakilishwa na kiongozi wa tume, Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini. Wajumbe watatu wengine wa tume wataungana na Jaji Goldstone kuwasilisha ripoti yao, ikijumlisha Bi Hina Jilani, Profesa Christine Chinkin na Kanali Desmond Travers. Kadhalika, Baraza la Haki za Binadamu litasikia ripoti nyengine juu ya Ghaza kutoka Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, ikifuatiwa na taarifa za wawakilishi wa Falastina na Israel. Mswada wa azimio la kikaohicho umeshatayarishwa na Baraza la Haki za Binadamu, na utazingatiwa kupitishwa Alkhamisi au Ijumaa.

28/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kilimo katika Afrika kinaashiria maendeleo ya kuridhisha, inasema FAO

Ripoti ya makala ya kujadiliwa, iliochapishwa hii leo na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) imeeleza kwamba utendaji hakika, wa kutia moyo, ulioshuhudiwa kufanyika hivi karibuni kwenye sekta ya kilimo katika zile nchi za Afrika ziliopo kusini ya eneo la Jangwa la Sahara, umebainisha utengano halisi na tabia za kikale, zilizopitwa na wakati, za kilimo, na kuwakilisha mwelekeo mpya wenye matarajio ya ukuzaji kilimo maridhawa kieneo, maendeleo yatakayokuwa na natija kubwa kwa umma, kwa ujumla.

28/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu laanzisha tena majadiliano ya jumla ya mataifa wanachama

UN General Assembly Hall

Majadiliano ya jumla kwenye kikao cha mwaka cha wawakilishi wote, yameanza tena rasmi leo asubuhi hapa kwenye Makao Makuu, kufuatia kikao cha siku nzima cha Baraza Kuu kilichokusanyika Ijumamosi, ambapo wazungumzaji waliowakilisha mataifa 30 waliwakilisha hoja kadha wa kadha kuhusu taratibu wa kusuluhisha masuala yenye kusumbua umma wa kimataifa.

28/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti juu ya Ushirikiano wa Viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria (ALMA)

Kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu la UM, ambacho ni cha 64, kilianza rasmi wiki hii kwenye Makao Makuu. Viongozi wa Mataifa na Serikali zaidi ya 120 walikusanyika mjini New York kuhudhuria mikutano mbalimbali juu ya shughuli za usalama, amani, haki za binadamu, huduma za maendeleo na kadhalika.

25/09/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO imeripoti kuwa uwekezaji kwenye utafiti wa kilimo ni muhimu kwa maendeleo

Ripoti iliochapishwa hii leo na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) imeeleza Mataifa Wanachama yatahitajia kuwekeza, kwa kiwango kikubwa zaidi, kwenye shughuli za utafiti ambao matokeo yake yatayawezesha mataifa, hasa zile nchi masikini, kutumia teknolojia mpya ya ukulima na kwenye matumizi ya mazao makuu tofauti yatakayosaidia kuzalisha mavuno kwa wingi zaidi.

25/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA inasema hali Yemen Kaskazini inazidi kuwa mbaya

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali katika jimbo la Kaskazini la Yemen, la Sa’ada, na katika maeneo jirani, inaendelea kuharibika kwa sababu ya kushtadi kwa mapigano baina ya vikosi vya usalama vya Yemen na makundi ya wapinzani ya Al Houthi.

25/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yatangaza taarifa mpya ya dawa ya kuzuia virusi vya A/H1N1

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kwamba uzoefu uliopatikana kimataifa kwenye huduma za kutibu janga la homa ya mafua ya A/H1N1 umethibitisha umuhimu kwa mgonjwa kupata matibabu ya mapema kwa kutumia zile dawa za kupambana na virusi vya maradhi, zinazoitwa oseltamivir na zanamivir,

25/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wa Usomali wanaelekea Kenya kunusuru maisha kufuata mapigano na ukame nchini mwao: UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba tangu mwanzo wa mwaka raia wa Usomali 50,000 ziada wamehamia Kenya kutafuta hifadhi ya maisha.

25/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa Wanachama yalioshiriki kwenye majadiliano ya mwaka kudai mageuzi ya kidemokrasia katika shughuli za UM

Majadiliano ya jumla ya mwaka kwenye kikao cha 64 cha Baraza Kuu la UM leo yameingia siku ya tatu.

25/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limetangaza leo kuwa linahitajia kupokea kutoka Iran taarifa zaidi, na ruhusa ya kuchunguza kiwanda cha fueli ya kusafishia madini ya yuraniamu, ambacho kinajengwa sasa hivi na Iran. Marc Vidricaire, msemaji wa IAEA aliripoti kwamba kwenye barua iliotumiwa taasisi yao na Iran, mnamo tarehe 21 Septemba 2009, ilielezwa kwamba Iran inajenga kiwanda kipya cha kutengenezea nishati na taarifa zaidi juu ya kadhia hiyo, zitatumiwa IAEA “katika muda mwafaka na kwa wakati upasao.” Vidricaire alisema “IAEA imeiomba Iran kuwapatia, haraka iwezekanavyo, taarifa maalumu kuhusu ujenzi huu na kuwapatia wataalamu wa IAEA ruhusa ya kuzuru na kufanya ukaguzi wa kiwanda ili kuthibitisha kama ni salama kufanya shughuli zake.” Aliongeza kusema Iran imeiarifu IAEA kwamba hakuna vifaa vya kinyuklia kwenye jengo la kiwanda kipya.

25/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

“Matatizo makubwa yataukabili ulimwengu mzima ikiwa tutashindwa kuusuluhisha mzozo wa Usomali”. Onyo hili lilitolewa na Naibu KM juu ya Masuala ya Kisiasa, B. Lynn Pascoe alipohutubia wiki hiii mkutano wa Kundi la Kimataifa la Mawasiliano juu ya Usomali (ICGS). Alisema taasisi za mpito ziliopo nchini kwa sasa hivi ndizo zenye fursa ya kurudisha tena hali ya utulivu na amani Usomali, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu 1991. Aliongeza kwa kusema ni muhimu kwa jamii ya kimataifa kufadhilia misaada hakika, na yenye maana, kwa Serikali ya Mpito Usomali ili ipate uwezo wa kuimarisha vyema utawala wake. Msaada wa kimataifa vile vile utaisaidia Serikali kuanzisha taasisi zitakazoshughulikia mahitaji ya umma na baadaye kuzalisha natija za amani. Pascoe aligutusha kwamba mashambulio ya wiki iliopita mjini Mogadishu kwenye Makao Makuu ya vikosi vya ulinzi amani vya Umoja wa Afrika, AMISOM, yanathibitisha dhahiri kuwepo haja kuu ya kujumuisha jumuiya ya kimataifa katika kuisaidia Serikali ya Mpito kudhibiti bora utawala nchini.

24/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNRWA inaadhimisha miaka 60

Viongozi wa kitaifa na mawaziri wa vyeo vya juu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walikusanyika leo hii kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York kuhishimu mchango wa Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) kuhudumia kihali umma wa KiFalastina, shirika ambalo leo limetimiza miaka 60 tangu kubuniwa.

24/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majaribio ya chanjo kinga dhidi ya maambukizo ya UKIMWI kuonesha matukio ya kutia moyo

The HIV Vaccines and Microbicides Resource Tracking Working Group, established as collaborative project to track funding for HIV vaccines and microbicide research and development,  has released a summary of the resource tracking efforts – the most up to d Chinese Unit

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka ishirini utafiti wa kimsingi umefanikiwa kutengeneza dawa ya chanjo ya majaribio, dhidi ya maambukizo ya virusi vya UKIMWI.

24/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majadiliano ya wawakilishi wote kwenye Baraza Kuu yameingia siku ya pili

Majadiliano ya jumla, kwenye kikao cha wawakilishi wote katika Baraza Kuu la UM, leo yameingia siku ya pili.

24/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukomeshaji wa uenezaji wa silaha za maangamizi watathminiwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama leo asubuhi lilikutana kwenye kikao maalumu kuzingatia uzuiaji wa uenezaji wa silaha za kinyuklia na upunguzaji wa silaha za maangamizi ya halaiki.

24/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Raisi Barack Obama wa Marekani alipohutubia Baraza Kuu la UM aliwaambia wajumbe wa kimataifa kwamba taifa lake lipo tayari kuanzisha mlango mpya kwenye uhusiano wa kimataifa na nchi wanachama. Aliyataka mataifa yajihusishe kwenye awamu yenye lengo la kukidhi masilahi ya pamoja ya umma wote wa dunia, na kwenye mazingira ambapo mataifa yatahishimiana. Aliutaka ulimwengu kuongeza juhudi zao, mara mbili zaidi, zitakazohakikisha UM utatumiwa kama ni kipengele muhimu cha kuendeleza masilahi ya pamoja ya umma wote wa ulimwengu. Alisisitiza kwamba ukubwa wa matatizo yalioukabili ulimwengu sasa hivi, bila shaka yanahitajia mchango wa Mataifa Wanachama yote, mchango utakaoipa taasisi ya UM maana hakika ya jina lake, kama ni taasisi inayosimamia masilahi ya Mataifa Yalioungana. Alisema mwelekeo huo ndio Marekani ungelipendelea kuuona unatumiwa kuendeleza uhusiano wa kimataifa katika siku za baadaye – hali itakayokuwa ya amani na yenye ustawi, ambayo walimwengu wote wanaweza kuifikia, tukitambua kwamba kila taifa lina haki na dhamana ya kutekeleza majukumu hayo. Makubaliano haya, alitilia mkazo, ndio yenye uwezo wa kuyafikia malengo yanayoridhisha katika uhusiano wa kimataifa.

23/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM watuma misaada ya dharura kwa waathirika wa mafuriko Afrika Magharibi

Mashirika ya UM yamelazimika kuongeza misaada ya dharura ya kunusuru maisha, kwa watu 600,000 walioathirika na mafuriko yalioenea katika siku za karibuni Afrika Magharibi, ambapo miundombinu iliharibiwa na kuangamizwa na mafuriko ambayo pia yaliharibu maskuli, hospitali na vile vile kugharikisha mashamba na kuangamiza mazao.

23/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulio ya kikabila Sudan Kusini yalaaniwa na KM

KM ameshtumu vikali shambulio liliotukia mwisho wa wiki liopita katika Sudan kusini, ambapo iliripotiwa watu 100 ziada waliripotiwa kuuawa, ikiwa miongoni mwa msururu wa mapigano ya kikabila yaliopamba karibuni kwenye eneo hili la Sudan.

23/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kesi ya waziri aliyetuhumiwa makosa ya jinai ya halaiki Rwanda yaanza kusikilizwa na ICTR

International Criminal Tribunal for Rwanda ICTR/UN Spanish Radio

Kesi ya aliyekuwa Waziri wa Mipango ya Maendeleo katika Rwanda, yaani Augustin Ngirabatware, imeanza kusikilizwa rasmi leo Ijumatano kwenye Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR).

23/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suluhu ya wahusika wengi ndio inayohitajika kutatua mizozo ya kimataifa, asihi Raisi wa BK

Raisi wa Baraza Kuu (BK), Ali Treiki wa Libya, kwenye risala yake ya ufunguzi wa majadiliano ya jumla, aliyahimiza Mataifa Wanachama kushirikiana, kwa ukaribu zaidi, na taasisi ya UM.

23/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 64 cha Baraza Kuu kufunguliwa rasmi

High-Level meeting on Climate Change convened in the General Assembly Hall. UN Photo/UN spanish Radio

Viongozi wa dunia 120 ziada, waliokusanyika kwenye Makao Makuu asubuhi ya leo, wameanza rasmi, majadiliano ya jumla ya kila mwaka, kwenye kikao cha wawakilishi wote katika ukumbi wa Baraza Kuu la UM, siku moja baada ya kumalizika Mkutano Mkuu juu ya mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

23/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

VVU/UKIMWI vinahatarisha usalama na amani ya kimataifa

Ripoti mpya iliotolewa bia leo hii na Baraza la Utafiti wa Sayansi ya Jamii, New York, Marekani pamoja na Tassisi ya Clingendael juu ya Uhusiano wa Kimataifa iliopo mji wa Hague, Uholanzi imethibitisha hatari anuwai ya virusi vya UKIMWI katika usalama na amani ya kitaifa na kimataifa.

22/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO inasema njaa imekithiri Afrika Mashariki

Nembo ya FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza kwamba hali mbaya ya ukosefu wa chakula katika eneo la Pembe ya Afrika itayalazimisha mashirika ya kimataifa kukithirisha mchango wao wa chakula, kwa umma muhitaji wa eneo, umma ambao idadi yao inaendelea kukithiri.

22/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya kupandisha miti bilioni duniani ilifanikiwa kupita kiasi, imeripoti UNEP

Billion Tree Campaign

Imetangazwa hii leo kwamba ile kampeni ya kimataifa ya kuotesha miti bilioni moja katika ulimwengu, kwa madhumuni ya kujikinga na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa, imefanikiwa kufikia kiwango kilichokiuka matarajio ya waandalizi wa mradi huo.

22/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa ya Visiwa Vidogo yakumbusha jamii ya kimataifa dhamana yao

Mataifa Yanayoendelea ya Visiwa Vidogo yanayowakilisha nchi 42 yametoa mwito maalumu wenye kusisitiza maafikiano ya kimataifa ya 2012 juu ya hali ya hewa, yatawajibika kudhaminia uwezo wa nchi maskini sana kupata riziki,

22/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano Mkuu juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa

climate-change-logo-k

Kwenye Mkutano wa UM juu ya Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa, unaofanyika hapa Makao Makuu, KM Ban Ki-moon aliwahimiza wakuu wa Taifa na serikali 100, waliohudhuria kikao hicho kuharakisha, kwa vitendo, zile hatua za kudhibiti bora tatizo la kuongezeka kwa hali ya joto ulimwenguni ili kuihifadhi sayari yetu kwa vizazi vijavyo.

22/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

unflaghq0425r

KM ameikaribisha hatua iliochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Kideomkrasia ya Kongo, mnamo tarehe 20 Septemba, ya kumpeleka Grégoire Ndahimana kizuizini Tanzania, kwenye Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda. Ndahimana, raia wa Rwanda aliyekuwa na cheo cha juu kwenye kundi la waasi wa Rwanda la FDLR, alikamatwa na vikosi vya JKK mnamo tarehe 10 Agosti 2009 kwenye jimbo la mashariki ya nchi. Alikuwa miongoni mwa watoro 13 walioshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) kuharamisha sheria za kiutu za kimataifa nchini Rwanda katika 1994. Kutiwa mbaroni Ndahimana na uhamisho wake kwenye Mahakama ya ICTR ni vitendo vilivyosaidiwa kwa mchango wa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC), baada ya kuitika ombi la wenye mamlaka nchini humo.

22/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi wa taasisi ya ICGLR azungumza na Redio ya UM juu ya shughuli za shirika lao

Siku ya leo, Ijumatatu tarehe 21 Septemba, ofisi za UM za Makao Makuu zimefungwa rasmi kwa sababu ya Siku Kuu ya Eid al Fitr. Kwa hivyo, badala ya taarifa za habari za kila siku, leo tumekuandalieni kipindi maalumu kuhusu shughuli za Taasisi ya Kimataifa juu ya Masuala ya Kanda ya Maziwa Makuu (ICGRL) yenye makao yake rasmi mjini Bujumbura, Burundi. Makala hii itaongozwa na mimi AWK.

21/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki za wahamaji kwenye vizuizi vya idara za uhamiaji zinahitajia marekibisho, anasema Pillay

Alkhamisi mjini Geneva, Baraza la Haki za Binadamu, kwenye pambizo za kikao chake cha mwaka, iliandaa warsha maalumu kuzingatia kwa kina, masuala yanayohusu haki za wahamiaji na wahamaji wanaowekwa kwenye vituo vya kufungia watu vya idara za uhamiaji, haki ambazo katika miaka ya karibuni zilionekana kukiukwa kihorera na mataifa pokezi ya wahamaji.

18/09/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku Kuu ya Amani Kimataifa

Tarehe 21 Septemba itaadhimishwa na UM kama ni Siku Kuu ya Amani Kimataifa. Ilivyokuwa Ijumatatu ofisi za UM zitafungwa hapa Makao Makuu kusherehekea Eid al Fitri, Siku Kuu ya Amani inahishimiwa leo Ijumaa, Septemba 18.

18/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kwenye mazungumzo na Mkuu wa UA, KM amerudia ahadi ya UM kuisaidia AMISOM Usomali

Wanajeshi wa AMISOM Somalia

Ijumaa KM Ban Ki-moon alizungumza,kwa simu, na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (UA), Jean Ping kuhusu shambulio la kujitoa mhanga liliotukia Alkhamisi kwenye makao makuu ya vikosi vya amani vya AMISOM mjini Mogadishu.

18/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna wa Haki za Binadamu ashtushwa na shambulio la kwenye kambi ya wahamiaji wa ndani Yemen

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa taarifa maalumu Ijumaa ilioleza kusumbuliwa sana na taarifa za watu walioshuhudia shambulio la ndege za Yemen, liliotukia tarehe 16 Septemba, kwenye kambi ya muda ya raia waliokimbia mapigano baina ya vikosi vya serikali na waasi wa kundi la Al Houthi, tukio ambalo limesababisha darzeni kadha za vifo vya wahamiaji hawo wa ndani ya nchi.

18/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO imekaribisha kwa mikono miwili misaada ya dawa kinga dhidi ya H1N1 kutoka mataifa tisa

Mataifa ya Marekani, Australia, Brazil, Ufaransa, Utaliana, New Zealand, pamoja na Norway, pamoja na Usweden na Uingereza yameripotiwa kuchangisha msaada wa dawa ya chanjo kinga dhidi ya homa ya mafua ya A/H1N1, mchango ambao utasaidia pakubwa kuhudumia umma wa kimataifa.

18/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upungufu wa fedha utailazimisha WFP kupunguza chakula kwa wahitaji Kenya

WFP Tana River, Kenya WFP

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba kwa sababu ya upungufu wa misaada ya fedha kutoka wahisani wa kimataifa, litalazimika kupunguza posho ya chakula wanaofadhiliwa mamilioni ya raia wanaohitajia misaada ya dharura ya chakula nchini Kenya,

18/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ijumaa kumetolewa rasmi ripoti mpya ya KM juu ya watoto walionaswa kwenye mazingira ya mapigano nchini Burundi. Alisema kuanzia Agosti 2009 UM umethibitisha kutogundua tena watoto wa umri mdogo walioshirikishwa mapigano na majeshi ya mgambo katika Burundi. Alitilia mkazo kwenye ripoti kwamba jambo muhimu la kufanyika kwa sasa hivi ni kuhakikisha watoto wote waliohusikana na makundi yenye silaha katika siku za nyuma huwa wanajumuishwa kwenye kadhia za maisha ya kikawaida kwenye jamii zao. Ripoti imependekeza kuanzishwe mfumo mpya wa kuwalinda watoto, kwa ujumla, na hatari ya kuajiriwa kimabavu na makundi ya waasi. Vile vile KM alipendekeza ndani ya ripoti kwa Kundi la Kazi la Baraza la Usalama juu ya hifadhi ya watoto kwenye maeneo ya mapigano kuzuru Burundi katika miezi ijayo, ili kufuatilia maendeleo kwenye jitihadi za kutekeleza ile miradi ya kuwahifadhi watoto Burundi.

18/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Ofisi ya UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) imetangaza kushtushwa sana na kutishwa na idadi ya vifo vilivyosajiliwa katika eneo la uhasama la Yemen. UNHCR imeshapeleka mahema zaidi, magodoro na mablangeti kwa wahamiaji 2,000 ziada waliomiminikia kwenye eneo jirani la Saudi Arabia kutafuta hifadhi. Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya taarifa ilizopokea zinazosema mashambulio ya anga yaliofanyika karibuni kwenye kambi za wahamiaji wa ndani katika Yemen kaskazini, yalisababisha vifo kadha vya raia, ikijumlisha watoto wadogo. UNICEF ilisema hali hiyo ni msiba mkubwa katika Yemen kaskazini, hususan kwa watoto wadogo ambao mwezi mmoja tangu mapigano kufumka bado hawana fursa ya kupatiwa maji safi na salama, wala mazingira yanayoridhisha au utunzaji wa afya na hifadhi wanayostahiki.

17/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNCTAD inasema FDI kwa 2009 inaendelea kupungua kimataifa

Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) limewasilisha, kutoka Geneva, Alkhamisi ripoti yake mpya iliozingatia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) kimataifa.

17/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Aliyekuwa ofisa wa serikali Rwanda akiri shtaka la makosa ya vita

International Criminal Tribunal for Rwanda ICTR/UN Spanish Radio

Michael Bagaragaza, aliyekuwa mkuu wa ofisi ya viwanda vya chai katika Rwanda leo amekiri shtaka la makosa ya jinai ya vita baada ya kutuhumiwa kushiriki kwenye mauaji ya halaiki nchini mwao katika 1994.

17/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu linazingatia athari za taka za sumu kwa raia Cote d’Ivoire

okechukwu-ibeanu-small

Mkariri Maalumu mwenye kutetea haki za binadamu, Olechukwu Ibeanu, amewasilisha ripoti mbele ya Baraza la Haki za Binadamu linalokutana Geneva, iliozingatia athari za taka za sumu zilizotupwa na makampuni ya kigeni katika Cote d’Ivoire mnamo mwezi Agosti 2006.

17/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulio ya walinzi amani Usomali yalaaniwa na KM

Wanajeshi wa AMISOM Somalia

Kadhalika KM kwenye risala yake ya ufunguzi wa mahojiano na waandishi habari KM alieleza juu ya tukio katika Usomali, ambapo Alkhamisi asubuhi, magari mawili yaliochorwa alama ya UM, yaliripotiwa kutumiwa kwenye shambulio la kujitoa mhanga liliofanyika kwenye kambi ya wanajeshi wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika (AMISOM) katika mji mkuu wa Mogadishu.

17/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM anahimiza ushirikiano wa wahusika wengi kusuluhisha matatizo ya kimataifa

KM Ban Ki-moon, kwenye mahojiano yake ya kila mwezi katika Makao Makuu, na waandishi habari wa kimataifa, alitilia mkazo haja kuu ya kufufua upya ushirikiano wenye wahusika wengi, ili kukabiliana vyema na matatizo yalioupamba ulimwengu kwa hivi sasa,

17/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Ijumatano UM umewasilisha ripoti juu ya namna nchi wanachama zinavyotekeleza ahadi za kusaidia kuyakamilisha, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia yaliokusudiwa kupunguza umaskini kwa nusu kabla ya 2015. Ripoti imethibitisha serikali zipo nyuma sana katika kutimiza ahadi za msaada wa fedha za kuhudumia mataifa yanayoendelea kuibuka kutoka kwenye mazingira ya umaskini na kukabiliana na matatizo ya njaa na masuala kadha mengineyo ya kiuchumi na jamii. Ripoti yenye mada inayosema 'Kuimarisha Ushirikiano wa Kimataifa kwenye huduma za Maendeleo katika Kipindi cha Mizozo’ ilitayarishwa na Tume Maalumu ya Kazi ya UM Kuziba Pengo la Utekelezaji wa Malengo ya MDGs. Ripoti imeangaza kwamba kuna pengo la dola bilioni 35 zilioahidiwa kuchangishwa kila mwaka na nchi zenye maendeleo ya viwandani, wanachama wa kundi la G8, kwenye mkutano mkuu uliofanyika 2005 katika Gleneagles, Uingereza. Vile vile ripoti ilisema kuna upungufu mkubwa wa dola bilioni 20 zilizoahidiwa kupatiwa mataifa ya Afrika kila mwaka ili yaweze kukabiliana na matatizo ya maendeleo. Naibu KM Asha-Rose Migiro aliwasilisha ripoti hiyo ya UM mbele ya waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu. Aliwaambia kwamba “walimwengu, katika siku za karibuni, tulifanikiwa kufanya maendeleo ya kutia moyo sana katika kuimarisha mashirikiano ya kimataifa juu ya shughuli za maendeleo … katika kile kipindi kabla ya mizozo ya uchumi na kifedha kuripuka kwenye soko la kimataifa.” NKM alihimiza kwamba tunachokihitajia kwa sasa hivi ni “msukumo tofauti mpya utakaosaidia kukabili vyema vitisho vinavyohatarisha natija za uchumi na jamii, natija zilizopatikana hivi sasa kwa jitihadi kuu kabisa.”

16/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa Kuhifadhi Funiko la Hewa ya Ozoni

Siku ya leo ni Siku ya Kimataifa kwa Hifadhi ya Funiko la/Tabaka la Hewa ya Ozoni. KM alisema kwenye risala yake kwamba maadhimisho ya siku hii yanafanyika siku 80 kabla ya kikao kijacho cha Mkutano wa Copenhagen. Alisema Siku ya Hifadhi ya Tabaka la Hewa ya Ozoni kwa mwaka huu limewakilisha tukio la kihistoria ambapo [...]

16/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yamuunga mkono KM na rai ya kuanzisha idara maalumu kwa masuala ya kijinsiya

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNIFEM) pamoja na Jumuiya Mashirika ya UM Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) yameripoti kuunga mkono ile rai ya KM ya kufungamanisha vitengo vya UM vinavyohusika na masuala ya wanawake kuwa Idara moja.

16/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Njaa imekithiri duniani na kunahitajika msaada ziada kukidhi mahitaji ya chakula, kuhadharisha WFP

WFP-Logo

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limetoa ripoti iliotahadharisha juu ya kukithiri kwa matatizo ya chakula katika ulimwengu, miongoni mwa umma wenye njaa.

16/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raisi mpya wa BK afungua kikao cha 64 kwa mwito wa kuleta mageuzi kwenye mfumo wa UM

Ijumanne alasiri, kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu (BK), yaani kikao cha 64, kilifunguliwa rasmi hapa Makao Makuu na Raisi mpya, Ali Treiki wa Libya, ambaye alirithi nafasi hiyo kutoka Raisi Miguel d’Escoto wa Nicaragua, aliyemaliza muda wake mapema wiki hii.

16/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

KM ameripotiwa kuyakaribisha maamuzi ya kikao cha 63 cha Baraza Kuu kwa kupitisha azimio linalohusu Mshikamano wa mfumo-kamili wa shughuli za UM. Alisema kwa kupitishwa azimio hilo Mataifa Wanachama yamechukua hatua muhimu katika maamirisho ya kazi za UM zinazohusika na usawa wa kijinsiya na katika kuwapatia wanawake mamlaka ya kujiamulia, hali ambayo anaamini itahakikisha shughuli za UM zitatendeka kwa ukamilifu katika kukuza maendeleo. KM alisema ameridhika zaidi baada ya kutambua Mataifa Wanachama yalimkubalia pendekezo lake la kuunganisha vitengo vyote vyenye kuhusika na masuala ya wanawake na kubuni idara moja ya pamoja, itakayotumiwa kusimamia maendeleo ya nguvu, ustawi na haki halali za wanawake kote duniani.

15/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo kupanda kwa wahamiaji Waafrika waliojaribu kuvuka Ghuba ya Aden

Mnamo saa 48 zilizopita imeripotiwa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwamba watu 16 walifariki na 49 wengine wamepotea, na kudhaniwa ni maututi kwa sababu ya matukio matatu tofauti yanayoambatana na mashua zilizokuwa zikivusha watu kimagendo kwenye Ghuba ya Aden wahamiaji waliojumlisha wale waliotoka Usomali na raia wengine wa kutoka Afrika.

15/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutoruhusu wahamiaji waliokwama baharini kuingia nchini kwaharamisha sheria ya kimataifa, ameonya Pillay

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay kwenye hotuba aliotoa Ijumanne mbele ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, aliwashtumu vikali wale wenye mamlaka pamoja na manahodha wa meli kadha wanaoharamisha sheria za kimataifa wanapowakatalia kuwachukua wale wahamiaji walioachwa kutangatanga baharini.

15/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

BK limepitisha azimio juu ya ‘haki ya kulinda raia’

Baraza Kuu la UM limepitisha, kwa pamoja, lile Azimio la ‘Wajibu wa Mataifa Kulinda Raia’ wakati wajumbe wa kimataifa walipokaribia kufunga kikao cha 63 katika Ijumatatu alasiri.

15/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya UM yagundua makosa ya jinai yalitendeka na pande zote Ghaza

gaza-mapa

Asubuhi ya leo, Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini aliyeongoza Tume Maalumu ya Baraza la Haki za Binadamu iliodhaminiwa jukumu la kutathminia taathira za mashambulio ya vikosi vya Israel katika Tarafa ya Ghaza, aliwasilisha matokeo ya uchunguzi wao kwenye mkutano na waandishi habari wa kimataifa hapa Makao Makuu.

15/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raisi wa BK anasema UM unahitajia marekibisho adhimu kikazi

Ijumatatu, wakati Baraza Kuu (BK) la UM lilipokamilisha kikao chake cha mwaka, cha 63, wajumbe wa kimataifa waliarifiwa kwenye hotuba yake ya kufunga kikao, ya Raisi wa Baraza, ya kuwa UM unahitajia kufanyiwa marekibisho ya dharura na mabadiliko ya jumla ili uweze kuendeleza shughuli zake kwa mafanikio.

15/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabwawa ya maji ya Ghaza yahatarishwa kuporomoka

Mabwawa ya maji yaliopo chini ya ardhi, ambayo WaFalastina milioni 1.5 wanaoishi katika eneo liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza hutegemea kwa kilimo na matumizi, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) mabwawa haya yanakaribia kuporomoka.

14/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Angelina Jolie ashtushwa na hali ngumu kwenye kambi ya wahamiaji wa Usomali mipakani Kenya

Angelina Jolie, msanii maarufu wa michezo ya sinema na Balozi Mfadhili wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) alifanya ziara ya siku moja, mnamo mwisho wa wiki iliopita, katika kambi ya wahamiaji ya Dadaab, iliopo kwenye mpaka kati ya Kenya na Usomali.

14/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu laanzisha kikao cha kawaida Geneva

Baraza la Haki za Binadamu leo limeanza rasmi kikao chake cha kawaida cha kumi na mbili mjini Geneva. Mkutano ulianza kwa majadiliano ya hadhi ya juu ambapo wawakilishi wa Sri Lanka, Marekani na Thailand walihutubia.

14/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shughuli za “kufufua amani” Sierra Leone zaashiriwa kukabiliwa na vizingiti ziada kwa siku zijazo

Baraza la Usalama asubuhi lilikutana kuzingatia juu ya shughuli za Ofisi ya Muungano wa Huduma za Ujenzi Amani katika Sierra Leone (UNIPSIL).

14/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa IAEA apendekeza taasisi yao ipatiwe madaraka zaidi kuendeleza shughuli zake

Kadhalika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la IAEA, Mohamed ElBaradei kwenye risala alioitoa mbele ya kikao cha 53 cha Baraza Kuu la IAEA alizisihi nchi wanachama kuipatia taasisi yao “madaraka zaidi ili kuzuia kihakika, na kwa mafanikio, uenezaji wa silaha za kinyuklia katika ulimwengu” hususan kwenye usimamizi wa utekelezaji wa kanuni za Mkataba wa NPT.

14/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 53 cha IAEA chafunguliwa rasmi Vienna

Kikao cha 53 cha Baraza Kuu la la Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) kimeanza rasmi Ijumatatu mjini Vienna, Austria na kwenye risala ya ufunguzi KM alitilia mkazo ulazima wa kuwa na mfumo unaoridhisha utakaohakikisha udhibiti bora wa silaha za kinyuklia, na kuhakikisha hazitoenezwa kimataifa.

14/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakulima wa Zimbabwe wasaidiwa na FAO kuotesha mahindi na mtama

Katika jitihadi za kuisaidia Zimbabwe kukabiliana na tatizo la njaa kwa mwaka huu, Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), likishirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) yatawapatia mbegu na mbolea baina ya asilimia 10 hadi 15 ya wakulima dhaifu nchini, sawa na wakulima 176,000.

14/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko makali Afrika Magharibi yameathiri watu 600,000 ziada

Imeripotiwa na Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ya kwamba mafuriko makali ya karibuni Afrika Magharibi yameathiri watu 600,000 hivi sasa na kusababisha vifo 159.

14/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon, Ijumatatu, kwenye mkesha wa ufunguzi wa kikao cha 64 cha Baraza Kuu la UM, tarehe 14 Septemba, alijiunga kwenye sala maalumu ya kuomba dua ya mafanikio na amani ulimwenguni. Sala hii kawaida hufanyika kwenye Kanisa la Familia Takatifu (Holy Family Church) kila mwaka kabla ya ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu, ambacho huhudhuriwa na viongozi kutoka nchi zote za dunia na hufanyika kwenye Makao Makuu ya UM kujadiliwa kipamoja miradi ya kuimarisha usalama na amani ya kimataifa. KM alikumbusha kwenye risala yake kwamba wakati UM ukijaribu kuzisaidia nchi maskini kukamilisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), haitoweza kuponesha majeraha ya zile ahli za kimataifa zinazosumbuliwa na shida na matatizo ya kiuchumi. Alitoa mwito maalumu kwa viongozi wote wa makundi ya kidini kujitahidi kuungana ili kuimarisha ule uwezo wa kuyatekeleza malengo ya UM ya kunusuru maisha ya umma, na kuusaidia ulimwengu kuelekea kwenye hali nzuri ya kuusaidia umma, kwa ujumla.

14/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR kupongeza miaka 40 ya mkataba wa kihistoria Afrika kuhifadhi wahamiaji

Alkhamisi ya tarehe 10 Septemba iliadhimisha miaka 40 ya kuanzishwa mkataba wa mataifa ya Afrika kuhifadhi wahamiaji.

11/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO imemteua Paul Ahyi wa Togo kuwa msanii mpya wa kutetea amani

Paul Ahyi

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Alkhamisi limemteua msanii wa kutoka Togo, anayeitwa Paul Ahyi kuwa mwanachama mpya wa orodha ya watu mashuhuri wanaotumia sauti zao, vipaji na hadhi walizonazo kusaidia kutangaza ujumbe wa UNESCO ulimwenguni, na kuendeleza miradi ya taasisi hii ya UM kimataifa.

11/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Usomali azuru Somaliland

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah Alkhamisi alizuru Somaliland ambapo alipata fursa ya kukutana na viongozi wa huko kwa majadiliano kuhusu mpango wa amani na mfumo wa uchaguzi kwenye eneo, pamoja na kusailia masuala kadha mengine muhimu.

11/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa za sasa za WHO juu ya kupunguza homa ya A/H1N1 kwenye maskuli

Shirika la Afya Duniani (WHO) Ijumaa limetangaza nasaha maalumu kuhusu hatua za kuchukuliwa katika maskuli, ili kupunguza athari za janga la homa ya mafua ya H1N1.

11/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

David Gressly, Mratibu wa Eneo la Sudan Kusini kwa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan (UNMIS) Ijumaa alizungumza na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu, kwa kupitia njia ya vidio, ambapo alieleza ya kuwa mashambulio ya kikatili yanayoendelezwa na kundi la waasi wa Uganda wa LRA pamoja na miripuko ya karibuni ya mapigano ya kikabila ni mambo yanayohatarisha usalama wa umma wa Sudan kusini. Alizungumzia kutoka Sudan kusini na alieleza wanajeshi wa mgambo wa LRA, ambao huteka nyara watoto wadogo na huwatumia kama wapiganaji na watumwa wa kikahaba, wameselelea na kuendelea kuongoza operesheni zao kwenye eneo la magharibi ya mbali ya Sudan kusini. Kwenye jimbo la Western Equatoria kundi la LRA linaendelea na kampeni zao za vitisho – ambapo huiba mali na kuvamia nyumba za watu, makanisa na vituo vya afya. Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO) waasi wa Uganda wa LRA wameonekana wakoiba vyakula, na kuua raia wasio hatia, na vile vile huwateka nyara watoto wadogo wa kike na kiume ambao huwalazimisha kuwatumikia kwa nji zinazoharamisha kabisa kanuni za kiutu na haki za mtoto. Gressly alitoa mfano wa uharibifu wa waasi wa LRA, ambao katika mwezi Agosti mwaka huu walishammbulia maeneo ya Western Equatoria na Central Equatoria na kuzusha tatizo kubwa la watu 80,000 ziada kung’olewa mastakimu. Kuhusu mapigano miongoni mwa makabila ya Sudan kusini, Gressly alibainisha kwamba mara nyingi uhasama baina yao hutokana na mabishano ya mali – hususan ngo’mbe, maji na ardhi. Alisisitiza kwamba suala la umiliki wa ardhi ni “tatizo kubwa linalohitajia suluhu ya kuridhisha miongoni mwa makabila ya eneo la kusini, au si hivyo fujo na vurugu zitaendelea kusababisha hali ya hatari na wasiwasi Sudan kusini.”

11/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwathirika wa mateso ya vita katika JKK azungumzia maafa aliopata na msaada anaotoa kihali kwa waathirika wengine

Yvonne Kisali

Mnamo mwanzo wa mwezi Septemba UM uliwakilisha ripoti mbili muhimu, zilizochapishwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu na pia kutoka Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC).

11/09/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Utaratibu uliofungamana kimataifa wapendekezwa na UM kukabili uharamia katika mwambao wa Usomali

Russian Radio

Imehadharishwa na mtaalamu wa UM kwamba mafanikio haba yaliopatikana katika udhibiti wa vitendo vya uharamia nje ya mwambao wa Usomali humaanisha kunahitajika mwelekeo mpya kukabiliana na tatizo hili badala ya kulenga kadhia hizi baharini pekee.

10/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Siku ya Kimataifa Kuzuia Kujiua’ yakumbukwa na UM

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaihishimu tarehe ya leo, Septemba 10, kuwa ni 'Siku ya Kuzuia Kujiua Duniani’. Katika siku hii mashirika ya kimataifa hujaribu kuamsha hisia za umma wa kimataifa juu ya tatizo hili, suala ambalo ni mwiko kujadiliwa hadharani na jamii kadha wa kadha za ulimwengu.

10/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifo vya watoto wachanga duniani vyaendelea kuteremka, inaripoti UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza takwimu mpya zilizokusanywa na wataalamu kutoka mashirika ya UM, ikijumlisha WHO, UNICEF, Benki Kuu ya Dunia na Kitengo cha UM juu Idadi ya Watu, takwimu ambazo zilionyesha viwango vya vifo vya watoto wachanga duniani, chini ya umri wa miaka mitano, viliteremka kwa asilimia 28 katika mwaka 2008.

10/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jaji mpya kutoka Urusi kuapishwa na ICTR

Mnamo siku ya leo, kwenye Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) iliopo Arusha, Tanzania aliapishwa Jaji mpya wa kutoka Shirikisho la Urusi, Bakhtiyar Tuzmukhamedov.

10/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Naibu KM wa UM juu ya Masuala ya Sheria, Patricia O’Brien aliwaambia wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Ushauri juu ya Uendeshaji wa Sheria ya Kimataifa Kuhusu Jinai, uliofanyika Makao Makuu wiki hii (09-11 Septemba), ya kwamba kuanzishwa kwa Mahakama ya Kimataifa Juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) ilikuwa ni hatua ya kihistoria kwenye juhudi za kutekeleza kanuni za kiutu za kimataifa, na kuendeleza haki kwa kuhishimu sheria kote ulimwenguni. Risala iliwakilishwa kwa niaba ya KM, na ilisisitiza kazi za UM katika kuendeleza amani, maendeleo na haki za binadamu ni kadhia zinazofungamana kwa ukaribu zaidi na kazi za Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC). Risala ya KM ilisema UM inaipa umuhimu mkubwa lengo lake la kuimarisha ushirikiano bora na ICC.

10/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

KM Ban Ki-moon amezingatia, kwa wasiwasi mkubwa, uamuzi wa karibuni wa Serikali ya Isarel wa kuidhinisha ujenzi ziada wa majumba ya walowezi kwenye Maeneo Yaliokaliwa Kimabavu ya WaFalastina. Vitendo hivi na makazi yote ya walowezi kwenye maeneo yaliokaliwa, alisema KM ni vitendo vinavyoharamisha sheria ya kimataifa na ile Ramani ya Mpango wa Amani. KM ameisihi Israel kuzingatia juhudi muhimu za kuandaa mazingira ya kuridhisha ya majadiliano ya amani kati ya WaFalastina na Waisraili, yenye uzito unaoaminika na wote. KM alirudia tena ule mwito unaoitaka Israel kusimamisha shughuli zote za maeneo ya ulowezi, ikijumlisha ujenzi unaodaiwa kuwa wa kimaumbile, na kuitaka Israel vile vile kung’oa vituo vyote vya ukaguzi vilivyojengwa kwenye maeneo yaliokaliwa ya WaFalastina tangu mwezi Machi 2001.

09/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

NKM atoa mwito wa utendaji dhidi ya udhalilishaji wa wanawake

Asha-Rose Migiro

Kwenye mkutano wa mawaziri kuzingatia masuala ya udhalilishaji na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake, unaofanyika kwenye mji wa Roma, Utaliana, hii leo, NKM Asha-Rose Migiro aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliohudhuria kikao hicho ya kuwa madhila ya kutumia mabavu dhidi ya wanawake yaliongezeka zaidi mnamo mwaka uliopita, kwa sababu ya kuporomoka kwa shughuli za soko la fedha la kimataifa.

09/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM anahadharisha juu ya hatari ya ulimwengu uliofurika silaha

KM Ban Ki-moon leo amefungua rasmi kikao cha 62 cha Mkutano wa Idara ya Mawasiliano ya Umma (DPI)-na Mashirika Yasio ya Kiserikali (NGOs) katika Mexico City, Mexico.

09/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP na Kenya waomba msaada wa kufufua misitu ya Mau

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limetoa mwito unaopendekeza kuchangishwa msaada wa dharura, wa mamilioni ya dola, utakaotumiwa kufufua na kutengeneza Maeneo ya Misitu ya Mau katika Kenya.

09/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICBL yawahimiza wanachama wa UA kusafisha mabomu yaliotegwa Afrika

landmines danger

Taasisi ya Kampeni ya Kimataifa Kupiga Marufuku Mabomu Yaliotegwa Ardhini (ICBL) imetoa taarifa maalumu kwenye mkutano wa kikanda, iliokuwa na makusudio ya kuwahamasisha wanachama wa Umoja wa Afrika (UA) kuongeza jitihadi zao kwenye huduma za kukomesha na kufyeka milele kutoka bara la Afrika, zile silaha za miripuko zilizotegwa ardhini, na pia kuhakikisha haki za wanusurika wa silaha hizo zinahishimiwa kikamilifu.

09/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti za UM zinasema, inayumkinika makosa ya vita yalitendeka katika JKK

Ripoti mbili zilizotayarishwa bia na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu pamoja na Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC), na kuwasilishwa siku ya leo, zinasema inayumkinika vitendo vya makosa ya jinai ya vita, vikichanganyika na uhalifu dhidi ya utu, viliendelezwa kwenye eneo la mashariki la JKK.

09/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Kai Eide, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Afghanistan, amesihi Kamisheni Huru ya Uchaguzi pamoja na Tume ya Mashtaka ya Uchaguzi nchini, kuongeza maradufu juhudi zao za kuhakikisha wanatekeleza msimamo mkali, usio na dosari, juu ya uchunguzi wa malalamiko ya ukiukaji wa utaratibu uliodaiwa kufanyika kwenye uchaguzi uliomalizika Afghanistan hivi karibuni. Miongoni mwa madai hayo ni zile tetesi zinazosema kuna ushahidi hakika kwamba hesabu ya mwanzo ya kura zilizopigwa zinaonyesha uchaguzi ulikiuka sheria. Eide alikumbusha kwamba uchaguzi unaoaminika na raia wote ni kadhia muhimu sana kwa utulivu wa taifa la Afghanistan na kwa washirika wenzi wa kimataifa. Anaamini kamisheni mbili hizo za uchaguzi zitatekeleza majukumu waliokabidhiwa nayo kwa viwango vya juu kabisa, na kuhakikisha matokeo ya mwisho yatawakilisha nia hasa ya umma wa Afghanistan.

08/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNHCR azuru Algeria/Morocco kusailia hali ya sasa ya wahamiaji Wasaharawi

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumatatu amewasili Algiers kuanza ziara ya siku tano katika Algeria na Morocco.

08/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miripuko ya uhasama Sudan Kusini kumtia wasiwasi KM

Ofisi ya Msemaji wa KM imetangaza Ban Ki-moon ana wasiwasi mkubwa juu ya taarifa alizopokea kuhusu mfululizo wa mashambulio, yaliofuatiwa na majibu ya mapigo, katika Sudan Kusini ambapo raia kadha wasio hatia waliuawa na baadhi yao walifukuzwa makazi.

08/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yaripoti mapigano makali yameshtadi Yemen Kaskazini

Mapigano makali yalioshtadi baina ya vikosi vya Al Houti na majeshi ya serikali Yemen kaskazini, kwenye maeneo ya mji wa Sa’ada yanaripotiwa kuendelea bila kujali usalama wala hali ya raia wa kawaida.

08/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko makali kuipamba Afrika Magharibi na kuathiri 600,000 ziada

Imeripotiwa na Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ya kwamba mafuriko makali ya karibuni Afrika Magharibi yameathiri watu 600,000 hivi sasa na kusababisha vifo 159.

08/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ayasihi Mataifa Wanachama kuharakisha mapatano ya kukomesha uchafuzi wa hali ya hewa

Wiki iliopita KM Ban Ki-moon, alizuru ukingo wa ncha ya Kaskazini ya dunia, kwenye eneo la Akitiki, ambapo alishuhudia mwenyewe athari kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa na kujionea, binafsi, namna miamba ya barafu na michirizi ya barafu inavyoyayuka kwa kasi kabisa kwenye eneo hilo, hali ambayo inachochea kina cha bahari kunyanyuka katika sehemu kadha za dunia, na kuhatarisha baadhi ya mataifa ya visiwa ambavyo huenda vikaangamia ikiwa hali hii haotidhibitiwa mapema.

07/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

KM wa UM Ban Ki-moon na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Jean Ping, wametangaza leo kumteua Mohamed Yonis wa Usomali kuwa Naibu Mjumbe Maalumu wa Pamoja kwa Operesheni na Usimamizi wa Kazi za UNAMID katika Darfur. Hivi sasa Yonis ni Mkurugenzi wa Kumudu Shughuli za UNAMID na anatarajiwa kumrithi Hocine Medili wa Algeria ambaye hivi sasa amekamilishi muda wake wa kazi katika Darfur. KM alimshukuru Medili kwa kuitumikia UM kwa miaka thelathini na saba.

04/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Timu ya uchunguzi ya UNAMA yapelekwa Kunduz kufatilia shambulio lilioua darzeni za raia Afghanistan

Ijumaa, UM umeitaka Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO) kuendeleza uchugunzi wa haraka kutokana na shambulizi la mabomu yaliotupwa kutoka angani katika wilaya ya Aliabad kwenye Jimbo la Kunduz, Afghanistan ambapo raia 80 waliripotiwa waliuawa.

04/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahimiza uundaji wa serikali mpya ya mpito Bukini

Taarifa ilitolewa Alkhamisi na Ofisi ya Msemaji wa KM juu ya suala la Bukini, imeeleza kwamba Ban Ki-moon ametoa mwito unaowahimiza wenye mamlaka nchini humo kufikia maafikiano ya haraka juu ya uundaji wa Serikali ya Muungano wa Taifa, kama ilivyoidhinishwa na Mapatano ya Kisiasa ya Maputo yaliofikiwa tarehe 09 Agosti mwaka huu.

04/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA inasema mafuriko Afrika Magharibi yameathiri watu 350,000

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti Afrika Magharibi inaathiriwa hivi sasa na mafuriko makubwa yaliofumka katika siku za karibuni.

04/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa za wiki kuhusu maambukizo ya H1N1 duniani

Kwenye taarifa iliotangazwa Geneva asubuhi ya leo, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilibainisha takwimu mpya juu ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya janga la virusi vya homa ya mafua ya A/H1N1 katika dunia, ambapo iliripotiwa jumla ya vifo vilivyosajiliwa rasmi kutokana na maradhi hayo kwa sasa katika vizio vya dunia vyote viwili, vya kaskazini na kusini, halkadhalika, ni sawa na watu 2,873.

04/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro anasailia miaka miwili ya utendaji kazi katika UM

asg_abdillahi

Dktr Asha-Rose Migiro, raia wa Tanzania, alianza kazi rasmi ya NKM wa UM mnamo tarehe mosi Februari 2007. Alikuwa ni NKM wa tatu kuteuliwa kuchukua nafasi hii tangu ilipoanzishwa rasmi katika 1997.

04/09/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

hapanapale

03/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waitaka Israel kuruhusu vifaa kuingia Ghaza haraka kufufua huduma za maji

food, distribution, humanitarian, Gaza, palestine

Mratibu wa Misaada ya Kiutu kwenye Maeneo Yailokaliwa Kimabavu ya WaFalastina, Maxwell Gaylard – akijumuika na Jumuiya za Mashirika Yasio ya Kiserikali yanayoambatana na Mashirika ya Kimataifa juu ya Misaada ya Maendeleo – wametangaza leo hii taarifa maalumu yenye kuthibitisha kufanyika uharibifu mkubwa wa vifaa vya huduma za usafi na maji katika eneo la Tarafa ya Ghaza, hali ambayo inazidisha ugumu wa maisha kwa umma wa eneo hili na kuwanyima hadhi yao ya kiutu.

03/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya Rufaa ya ICC imeamua aliyekuwa kiongozi wa JKK asalie kizuizini wakati akisubiri kesi

Jean-Pierre Bemba Gombo arrested for crimes allegedly committed in the Central African Republic  ICC

Mahakama Ndogo ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa Juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imeamua Jean-Pierre Bemba Gombo, aliyekuwa Naibu Raisi wa JKK, aendelee kuwekwa kifungoni kabla ya kesi yake kusikilizwa na Mahakama Kuu.

03/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa WCC3 waafikiana kuanzisha mfumo mpya wa kuhudumia utabiri wa hali ya hewa

Mkutano Mkuu wa Tatu juu ya Hali ya Hewa (WCC3) unaokutana hivi sasa Geneva, Alkhamisi ulipitisha Mwito wa Azimio la kuanzisha Mfumo Mpya wa Dunia Kuhudumia Utabiri wa Hali ya Hewa, utaratibu ambao utayawezesha Mataifa Wanachama kupata taarifa, kwa wakati, kuhusu mageuzi katika hali ya hewa.

03/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM asihi Mkutano wa WCC3 kuharakisha maafikiano ya kudhibiti mageuzi ya hali ya hewa.

Wajumbe kadha wa kimataifa waliokusanyika Geneva, kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tatu juu ya Hali ya Hewa (WCC3) walipata fursa ya kumsikiliza KM Ban Ki-moon akisihi, kwa bidii kuu, juu ya umuhimu wa mataifa kuhakarisha makubaliano ya mkataba mpya wa kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa katika dunia.

03/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ijumatano Naibu KM Asha-Rose Migiro alihutubia kikao cha pili cha Mkutano wa Mataifa Yalioidhinisha Mkataba juu ya Haki za Watu Walemavu uliofanyika kwenye Makao Makuu ya UM. Kwenye risala yake alisema Mkataba wa Watu Walemavu unajumlisha misingi imara ya kisheria inayotakikana kwenye zile bidii za kusukuma mbele haki za watu milioni 650 – wanawake, wanaume na watoto wanaoishi na ulemavu – kutoka sehemu zote za dunia na, hatimaye, kuwawezesha kushirikishwa na kujumuika kikamilifu kwenye maisha ya jamii zao. Naibu KM alisema inatia moyo kuona mataifa mengi yameshapitisha sheria mpya na sera kadha zinazolingana na mapendekezo ya Mkataba, mwelekeo ambao alisema utasaidia kutekeleza kanuni za Mkataba kwa ridhaa ya wahusika wote.

02/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serikali zahimizwa kutekeleza ahadi za kuwasaidia wanusurika wa mabomu yaliotegwa ardhini

Ripoti mpya ya kufanikisha yenye mada isemayo “Sauti za Kutoka Ardhini” imebainisha kwamba licha ya kupatikana maendeleo katika kuangamiza akiba ya mabomu ya kutega ardhini, kutoka ghala mbalimbali, pamoja na kuziondosha silaha hizo, hata hivyo serikali za kimataifa bado zimeshindwa kutekeleza ahadi zao za kuwajumuisha waathirika wa silaha hizo kwenye maisha ya kawaida ya jamii zao.

02/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malaria Kenya imepunguzwa na mchanganyiko wa tiba mpya

Taarifa ya jarida linalochapishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) liliotolewa kwa mwezi Septemba, limebainisha ya kuwa tiba mpya iliovumbuliwa, ya mchanganyiko, ina uwezo wa kupunguza kwa kiwango kikubwa hatari ya maambukizo ya malaria kwa watoto wadogo.

02/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji wa katika mifumo ya ikolojia una matumaini ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, inasema TEEB

Matokeo ya mradi ulioanzishwa na Ujerumani pamoja na Kamisheni ya Mataifa ya Ulaya kuhusu masuala ya hali ya hewa, unaosimamiwa na Taasisi juu ya Uchumi wa Mfumo wa Ikolojia na Viumbe Hai Anuwai (TEEB), yamethibitisha dhahiri kwamba uwekezaji kwenye huduma za kufufua mifumo ya ikolojia ni hatua yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti bora taathira za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, na ni hatua itakayoimarisha uchumi wa kimataifa, halkadhalika, pindi itatekelezwa kama inavyostahiki.

02/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahimiza mataifa kukamilisha maafikiano ya Mkutano Mkuu juu ya taathira za hali ya hewa

KM Ban Ki-moon amewasihi walimwengu kuchukua hatua za dharura ili kukabiliana haraka na athari chafuzi za mabadiliko ya hali ya hewa, na kuyahifadhi maisha ya vizazi vijavyo.

02/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

KM Ban Ki-moon leo alizuru Mzingo wa Barafu wa Ncha ya Dunia (Polar Ice Rim) wakati alipokuwa ndani ya meli ya Norway. Kabla ya hapo KM na mkewe walizuru Steshini ya Zeppelin, kituo cha Norway kiliopo Kaskazini ya dunia, kunapoendelezwa uchunguzi wa hewa ya eneo la Akitiki, utafiti ambao hufuatilia athari za hewa chafu inayomwagwa angani pamoja na vichafuzi vyengine. KM alipata fursa ya kujionea binafsi majabali ya barafu yalionywea kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, hali ambayo alisema ilimshtusha sana. Ilivyokuwa chini ya siku 100 zimesalia kabla ya kufanyika Mkutano Mkuu wa Copenhagen juu ya Udhibiti wa Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa, KM alisema safari yake ya kaskazini ya ncha ya dunia imempatia fursa ya kujionea mwenyewe athari za mazingira, hali itakayomsaidia kuwahamasisha wajumbe watakaohudhuria Mkutano wa Copenhagen juu ya dharura ya kukamilisha mapatano ya mkataba mpya wa kuhifadhi mazingira, na kudhibiti bora athari chafuzi zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

01/09/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwanajeshi wa Rwanda akabidhiwa madaraka ya Kamanda Mkuu mpya kwa Darfur

patrick_nyamvumba

Kamanda Mkuu mpya wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) kutoka Rwanda, Liuteni-Jenerali Patrick Nyamvumba ameripotiwa kuanza kazi rasmi hii leo.

01/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maharamia wa uvuvi watanyimwa makimbilio salama baada ya kufikiwa maafikiano mapya ya kimataifa

Mataifa Wanachama 91 wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) yameafikiana kuukubali waraka wa mwisho wa mkataba wa kimataifa uliokusudiwa kupiga vita uvuvi haramu kwenye maeneo yao.

01/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OHCHR imepeleka timu ya wataalamu wa haki za binadamu Gabon kufuatilia uchaguzi wa uraisi

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR) imetuma wataalamu wanne nchini Gabon, kuchunguza hali ya haki za binadamu, kwa ujumla, wakati uchaguzi wa uraisi unapofanyika katika taifa hili la Afrika Magharibi.

01/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahadharisha, mzozo mkuu wa kiutu wajiandaa kuripuka Yemen kaskazini

UM unaashiria mzozo mkubwa wa kiutu unajiandaa kufumka katika mji wa Sa’ada, uliopo Yemen kaskazini, ambapo hali huko inaripotiwa kila siku kuendelea kuporomoka na kuharibika.

01/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano makali Mogadishu yanaathiri zaidi raia, inasema OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kutoka Geneva kwamba mapigano makali yaliopamba kwenye mji wa Mogadishu, Usomali yanaendelea kuathiri kwa wingi raia.

01/09/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930