Nyumbani » 31/08/2009 Entries posted on “Agosti, 2009”

Hapa na pale

Tarehe 31 Agosti ni siku ya mwisho ya uraisi wa duru wa Baraza la Usalama kwa Uingereza. Kuanzia tarehe mosi Septemba uraisi wa Baraza la Usalama utakabidhiwa Marekani. Ijumatano Balozi Susan Rice wa Marekani anatarajiwa kutangaza mradi wa kazi na ajenda ya Baraza la Usalama kwa mwezi Septemba.

31/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa WCC unazingatia utaratibu mpya wa kueneza taarifa za hali ya hewa kote duniani

Mkutano Mkuu wa Dunia juu ya Hali ya Hewa (WCC-3) umefunguliwa rasmi Geneva Ijumatatu ya leo, ambapo wataalamu na wanasiasa kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu, wanakutana kwa mashauriano ya kuhakikisha umma wa kimataifa huwa unapatiwa uwezo wa kutabiri hali ya hewa pamoja na taarifa nyengine kama hizo, ili kukabiliana vyema na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa.

31/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID imepokea maofisa polisi ziada kutoka Nepal na Nigeria

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limepokea maofisa wa polisi 26 kutoka Nepal na polisi 30 wa Nigeria waliowasili kwenye mji wa El Fasher leo Ijumatatu.

31/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umma wa Dungu watishwa kila siku na mashambulio ya LRA, anasema Mkuu wa UNICEF

Ann Veneman Unicef 019a

Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kwenye siku ya mwisho ya ziara ya siku tano alioendeleza katika JKK alipata fursa ya kukutana na wale watoto waliotoroshwa na waasi wa Uganda wa kundi la LRA.

31/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi wa Haki za Binadamu aisihi Zambia kwamba “ufukara hauondoshwi na ufasaha wa lugha bali vitendo”

Magdalena Sepulveda

Baada ya kukamilisha ziara yake katika Zambia, Mtaalamu Huru wa UM anayetetea haki za binadamu na umaskini uliovuka mipaka, Magdalena Sepúlveda, kwenye mahojiano na waandishi habari mjini Lusaka alionya kwamba “ufukara mkubwa uliopamba nchini Zambia haotofanikiwa kukomeshwa kwa ufasaha wa usemaji bali kwa vitendo halisi.”

31/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

KM Ban Ki-moon wiki ijayo atafanya ziara ya siku mbili katika Svalbard, Norway, ili kujionea binafsi athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika eneo la Kaskazini ya dunia la Akitiki (Arctic). Kwanza KM atakwenda eneo la Ny-Alesund, liliopo Kaskazini kwenye fungu la visiwa vya Svalbard, ambapo atazuru steshini ya uchunguzi juu ya mazingira ya ncha ya dunia, kabla hajaelekea Kaskazini juu zaidi ambapo atapatiwa taarifa mpya za kisayansi kuhusu namna majabali ya barafu yanavyodhibiti na kurekibisha shughuli za Bahari ya Akitiki na kuathiri mabadiliko ya hali ya hewa ya ulimwengu.

28/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Taarifa juu ya hali ya maambukizi ya A/H1N1 katika dunia

Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye taarifa ya wiki kuhusu hali ya maambukizo ya homa ya mafua ya A/H1N1 llimeeleza ya kwamba katika nchi za kizio cha kusini ya dunia, ikijumlisha Chile, Argentina, New Zealand na Australia maambukizo ya maradhi yameshapita kilele na hivi sasa yameselelea kwenye kigezo wastani, wakati mataifa ya Afrika Kusini na Bolivia yanaendelea kukabiliwa na ongezeko la homa ya mafua.

28/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kituo cha kuwasaidia wahamiaji jirani kupata ajira chafunguliwa mpakani Afrika Kusini: IOM

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limetangaza kufunguliwa Kituo cha Wahamaji wa Ajira katika Afrika Kusini, kwenye mji wa mipakani wa Beitbridge.

28/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku 100 zimesalia kabla ya Mkutano wa COP-15 kudhibiti taathira za mabadiliko ya hali ya hewa

UM umetoa mwito maalumu wenye kuwataka mamilioni ya umma wa kimataifa kutia sahihi zao, kwenye mtandao, ili kuidhinisha lile ombi la kuzihimiza serikali wanachama Kukamilisha Makubaliano juu ya waraka wa Mkutano wa COP-15, yaani ule Mkutano Mkuu utakaofanyika mwezi Disemba katika mji wa Copenhagen, Denmark kuzingatia mkataba mpya wa udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

28/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vurugu la waasi wa LRA lasabibisha raia 125,000 ziada kuhama makazi katika JKK

lra1215r

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kutoka Geneva, kwamba kundi la waasi wa Uganda, wanaojiita Jeshi la Upinzani la MUngu (Lord Resistance Army/LRA) bado wanaendeleza, kwa kiwango kikubwa vitendo vya ufisadi, uharibifu na kusababisha uhamisho uliovuka mipaka wa watu katika eneo la mashariki la JKK.

28/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisa wa UNHCR anasailia mzozo wa makazi kwenye kambi za wahamiaji za Dadaab, Kenya

Dadaab; refugee; Kenya; Somalie; Somalia UNHCR

Katika miezi ya karibuni, vurugu na mizozo ya kihali ilikithiri kwa wingi katika Usomali, hali iliosababaisha maelfu ya raia kuamua kuhama makwao na kuelekea mataifa jirani kutafuta hifadhi na usalama.

28/08/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Mkutano wa Kupunguza Silaha wajitahidi kufikia mapatano kwenye mradi wa kazi

Disarmamnet conference hall. UNOG/UN Spanish Radio

Alkhamisi, wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Kupunguza Silaha Duniani, unaofanyika Geneva kwa hivi sasa, bado wanaendelea na juhudi za kusuluhisha mvutano juu ya mradi wa kufanya kazi wa kikao hicho.

27/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabatamzinga wa Chile wakutikana na virusi vya H1N1

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetoa taarifa yenye kueleza wafugaji kuku na ndege ulimwenguni wameingiwa wasiwasi mkuu baada ya kugunduliwa homa ya mafua ya A/H1N1 miongoni mwa mabatamzinga wa katika taifa la Amerika Kusini la Chile.

27/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwanasheria wa Afrika Kusini ameteuliwa kutetea haki za wanawake waathirika wa matumizi ya nguvu

Taarifa iliotolewa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) imeleza kwamba wakili kutoka Afrika Kusini, Rashida Manjoo, ameanza rasmi kazi ya Mkariri (Mtetezi) Maalumu mpya wa UM atakayehusika na huduma za kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake, na kuendeleza kampeni za kudhibiti sababu na taathira za udhalilishaji wa kijinsiya.

27/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Asubuhi Baraza la Usalama limepitisha, kwa kauli moja, azimio la kuidhinisha operesheni za Vikosi vya UM vya Uangalizi wa Kusitisha Mapigano Lebanon (UNIFIL) ziendelee kwa miezi 12 zaidi katika eneo husika. Baada ya hapo wajumbe wa Baraza walisikiliza taarifa ya fafanuzi kutoka Jun Yamazaki, Mdhibiti Fedha wa UM, juu ya ripoti ya KM kuhusu Mfuko wa Maendeleo kwa Iraq. Kufuatia mashauriano hayo, kwenye taarifa iliotolewa kwa waandishi habari baadaye, wajumbe wa Baraza walibainisha kuingiwa wasiwasi kuhusu namna fedha za Iraq zinavyosimamiwa, na walisema wangelipendelea kuona marekibisho yanafanyika, haraka, kwenye utaratibu huo ili kuhakikisha Serikali ya Iraq inapewa madaraka zaidi kwenye matumizi ya rasilmali yao kutoka Mfuko wa Maendeleo.

27/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

KM alishtushwa na alishangazwa, halkadhalika, kuhusu shambulio liliotukia Ijumanne usiku kwenye mji wa Kandahar, Afghanistan ambapo ilripotiwa raia zaidi ya arobaini waliuawa na tukio hilo na raia themanini wengine walijeruhiwa. KM alishtumu,kwa kauli kali, kitendo katili hiki kisofahamika. KM aliwatumia aila zote za waathirika mkono wa pole, na vile vile aliwaombea majeruhi kupona haraka.

26/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Marehemu Seneta E. Kennedy wa Marekani aombolezwa na KM na UNHCR

Viongozi wa UM leo walitoa shukrani kadha na kumkumbuka kidhati seneta wa Marekani, Edward Kennedy ambaye alifariki Ijumanne usiku akiwa na umri wa miaka 77 baada ya kuugua saratani ya ubongo kwa muda mrefu.

26/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya hali ya hewa yabatilisha historia kuwa ni kiashirio kwa wakulima, anasema Mkuu wa WMO

World Meteorological Organizacion, Secretary General Michel Jarraud. WMO - Spanish Radio

Michel Jarraud, Mkuu wa Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) amenakiliwa akisema mabadiliko ya hali ya hewa yameifanya tarikh/historia kuwa ni chombo kisio sahihi tena katika kuongoza shughuli za wakulima, pamoja na wale wawekezaji wa kwenye nishati.

26/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sekta ya ilimu Sierra Leone inapitia matatizo, UNICEF yahadharisha

UNICEF logo UNICEF/UN Spanish Radio

Shirika la UNICEF limetoa ripoti yenye kuonyesha watoto 300,000 hutoroka skuli na hawahudhurii madarasa katika taifa la Afrika Magharibi la Sierra Leone.

26/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNICEF, mchezaji wa mpira wa kikapu washiriki kwenye ufunguzi wa taasisi za matibabu ya UKIMWI katika JKK

Ijumatano, kwenye mji wa Kinshasa, katika JKK kulifunguliwa rasmi maabara mbili muhimu za kufanyia uchunguzi wa kisayansi kuhusu kinga ya maradhi pamoja na usalama wa kazini kwa wahudumia afya ambazo zitakuwepo katika Hospitali ya kisasa ya Biamba Marie Mutombo (BMMH) iliojengwa na mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu kutoka JKK, Dikembe Mutombo.

26/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wanaohitajia lishe na misaada ya kiutu imekithiri Usomali: FSNAU

Kitengo cha UM Kinachotathminia Lishe na Akiba ya Chakula katika Usomali (FSNAU) kimeripoti kwamba tangu mwezi Januari 2009, idadi ya watu wenye kuhitajia misaada ya kihali na fursa ya kupata ajira nchini Usomali imeongezeka kwa asilimia 18, kutoka watu muhitaji milioni 3.7 na kufikia watu milioni 3.57, sawa na nusu ya idadi ya watu wa katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.

25/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwanadamu anaweza kuambukiza mnyama A/H1N1, inasema WHO

Imetangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kwamba kuna uwezekano kwa wanadamu, mara kwa mara, kuwaambukiza wanyama wa mifugo, kama nguruwe, kuku na mabata yale maradhi ya homa ya mafua ya aina ya A/H1N1.

25/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa dola 500,000 wafadhiliwa na UNICEF kuhudumia miradi ya kijamii Kongo-Brazzaville

Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) ametangaza wakati anazuru Jamhuri ya Kongo (Brazzavile) wiki hii ya kuwa watafadhilia msaada wa dola 500,000 ili kuhudumia miradi ya lishe bora, afya na ilimu nchini humo, sekta ambazo ziliathiriwa zaidi na mizozo ya uchumi wa dunia na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wale raia walio dhaifu kihali.

25/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP imeomba dola milion 230 kuhudumia dharura ya chakula Kenya

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limetoa ombi la kutaka lifadhiliwe na wahisani wa kimataifa, msaada wa dola milioni 230 kuhudumia dharura ya chakula kwa Kenya katika kipindi cha miezi sita ijayo.

25/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa Juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), yaani Luis Moreno-Ocampo Ijumatatu aliwakilisha hoja zake kwa Mahakama Ndogo ya Rufaa ya kupendekeza mtuhumiwa Jean-Pierre Bemba wa JKK, abakie kifungoni mpaka mwisho wa kesi. Vile vile alitaka Bemba asiachiwe wakati ombi la Mwendesha Mashitaka linazingatiwa na Mahakama ya Rufaa. Bemba alituhumiwa kushiriki kwenye makosa ya jinai yaliofanyika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

25/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kumbukumbu ya Kimataifa juu ya Taathira za Utumwa

esclavage; slavery; JM; International day ofr the commemoration abolition of slavery adapted graphic

Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Ukomeshaji wa Biashara ya Utumwa huadhimishwa na UM kila mwaka mnamo tarehe 23 Agosti.

24/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa mkataba wa kudhibiti silaha za kibayolojia wanakutana Geneva

Wataalamu magwiji wa fani ya silaha zinazotumia vijidudu vya viumbehai wanakutana hivi sasa mjini Geneva kusaillia maendeleo katika ujenzi wa fani ya uchunguzi wa maradhi ya vijidudu hivyo, ugunduzi wake, utambuzi wa ugonjwa na udhibiti wake.

24/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nusu ya ardhi ya kilimo duniani ina funiko kubwa la miti, wanasayansi wathibitisha

Matokeo ya uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Kilimo cha Misitu Duniani, uliotumia satelaiti, ulithibitisha kihakika kwamba karibu nusu ya ardhi yote iliolimwa duniani huwa imesitiriwa na funiko muhimu la miti, licha ya kuwa shughuli za kilimo, hasa katika nchi zinazoendelea ndio zinazodaiwa kusababisha uharibifu mkubwa wa misitu.

24/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS inashauriana na mashirika ya kikanda kudhibiti UKIMWI Afrika ya Kati/Magharibi

Nembo ya UNAIDS

Majuzi katika mji wa Dakar, Senegal kulifanyika kikao maalumu cha ushauriano, kilichoandaliwa na Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) pamoja na jumuiya 30 za kiraia, kwa lengo la kubuni miradi itakayohakikisha umma huwa unapatiwa uwezo wa kujikinga na UKIMWI, na kupata huduma zinazoridhisha za matibabu, pamoja na uangalizi na misaada ya fedha inayohitajika kutekeleza huduma hizo za afya kwa waathirika.

24/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wawasihi viongozi wa dunia kuonyesha vitendo kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Vijana na Watoto wa Kimataifa wa TUNZA, uliofanyika kwenye mji wa Daejeon, Korea ya Kusini walipokamilisha vikao vyao mwisho wa wiki iliopita walitoa mwito maalumu unaowataka viongozi wa dunia kuchukua hatua kali, za dharura, kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ulimwenguni.

24/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Chong Young-jin, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Cote d’Ivoire amezuru kituo kinachotoa vitambulisho vya wapiga kura katika mji mkuu wa Abidjan. Alisema kazi inayosimamiwa sasa hivi na kituo hiki ni ile ya kukusanya taarifa zilizopokewa za usajili wa wapiga kura na utambulisho. Wiki iliopita Chong alizuru sehemu za bara na maeneo ya ndani ya Cote d’Ivoire kutathminia hali kwa ujumla.

24/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mhudumia misaada ya kiutu wa kimataifa awapatia sauti wanusurika wa madhila ya kijinsiya katika JKK

Ijumatano ya tarehe 19 Agosti (2009) iliadhimishwa na UM, kwa mara ya kwanza katika historia yake, kuwa ni 'Siku ya Kumbukumbu kwa Wahudumia Misaada ya Kiutu Duniani.’

21/08/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP imeamua kudondosha kutoka angani chakula kwa wakazi muhitaji wa JKK

WFP airplane, food aid WFP/Russian Radio

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limearifu kwamba litaandeleza operesheni za kuwapatia chakula raia 10,000 muhitaji waliopo katika eneo la Dingile, katika mashariki ya JKK kwa kuidondosha misaada hiyo kutoka kwenye ndege.

21/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulio ya LRA Sudan Kusini yachochea uhamisho wa dharura kwa raia

lra1215r

Imeripotiwa hii leo na msemaji wa KM kwamba maelfu ya raia wamekimbia makazi kwenye eneo la Equatoria ya Magharibi katika Sudan, baada ya kundi la waasi wa Uganda la LRA kushambulia eneo hili.

21/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Stockholm wasisitiza ulazima wa kujumuisha suala la maji kwenye kikao cha COP-15

Wajumbe walioshiriki kwenye mkutato unaoadhimisha Wiki ya Maji Duniani kwa 2009, unaofanyika kwenye mji wa Stockholm, Sweden wamepitisha hii leo kwa kauli moja azimio linalosema suala la maji ni laizma kujumlishwa kwenye kikao cha COP-15,

21/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa za marekibisho kuhusu A/H1N1 kuchapishwa kila Ijumaa na WHO

Paul Garwood, msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameripoti leo kutoka Geneva kwamba kuanzia wiki hii taarifa mpya kuhusu hali ya maambukizi ya homa ya mafua ya A/H1N1 ulimwenguni itakuwa inachapishwa kila Ijumaa kwenye mtandao wa WHO.

21/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNICEF kuzuru JKK wiki ijayo kusailia jinai ya kijinsiya

Ann Veneman Unicef 019a

Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) wiki ijayo, anatarajiwa kufanya ziara ya siku tano katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).

21/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripotiwa kuingiwa wasiwasi mkuu juu ya kuharibika kwa hali ya usalama Yemen, hususan athari zake kwa watoto wadogo na wanawake – kufuatia mifumko ya vurugu lilionea katika eneo la kaskazini ya nchi. Kwa mujibu wa taarifa za UNICEF watu 100,000 wameathirika na mgogoro huo, asilimia kubwa yao wakiwa watoto. UNICEF imeripoti imeshaanzisha kugawa vifaa vya kuchujia maji pamoja na majerikeni ya maji, na zana za huduma ya afya, na vile vile imegawa tembe 300,000 za kusafishia maji. Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) sasa hivi linajiandaa kupeleka misaada ziada ya chakula kwa watu 150,000 katika Yemen baada idadi yao kuongezeka kutoka mwezi uliopita. Shirika la UM linaloshughulikia huduma za wahamiaji, yaani UNHCR, limeeleza ya kwamba katika wiki mbili zilizopita watu 35,000 waling’olewa makazi kutokana mapigano yaliopamba kaskazini katika Yemen. Wakati huo huo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kwamba aila nyingi za wahamiaji wa ndani Yemen wameonekana kuambukizwa na malaria, na wengine wanasumbuliwa vile vile na maradhi ya kuharisha na mapele ya mwili.

21/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Chinese Unit

KM Ban Ki-moon, kwa kupitia msemaji wake, aliripotiwa kuupongeza umma wote wa Afghanistan – wanaume na wanawake – kwa kutekeleza haki yao ya Kikatiba na kupiga kura kwenye uchaguzi rasmi wa Uraisi na Baraza la Wawakilishi wa Majimbo, uliofanyika siku ya leo, tarehe 20 Agosti. Alisema kitendo hiki kimemthibitishia dhahiri matakwa ya umma wa Afghanistan ni kurudisha utulivu nchini mwao na kuimarisha maendeleo yenye natija kwa wazalendo wote.

20/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maofisi wa polisi wa Jordan, Namibia na Philippines wawasili Darfur kujiunga na UNAMID

Shirika la Ulinzi Amani la Vikosi vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) wiki hii limepokea kundi la awali la maofisa wa polisi kutoka Jordan, waliowasili Ijumanne kwenye jimbo hilo la Sudan magharibi. Maofisa wa polisi 280 waliosalia kutoka Jordan wanatarajiwa kuwasili Darfur mwisho wa Agosti, na wataenezwa kwenye sehemu za El Fasher na Kabkabiya, Darfur Kaskazini.

20/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miripuko mipya ya kipindupindu inaashiriwa Zimbabwe

Nembo ya UNICEF

Peter Salama, Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) katika Zimbabwe hii leo ametoa onyo lenye kuhadharisha kwamba ana hakika mripuko mpya wa maambukizo ya maradhi ya kipindupindu nchini upo njiani na hautoepukika, kwa sababu ya kuharibika kwa miundo mbinu ya nchi, hali ambayo ndio itakayochochea tatizo hilo la afya, kwa mara nyengine tena.

20/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM yahadharisha, Sudan Kusini inakabiliwa na upungufu mkubwa wa huduma za kimsingi

WFP-Logo

Kuhusu operesheni nyengine za ugawaji chakula katika Sudan, Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba tangu Maafikiano ya Jumla ya Amani yalipotiwa sahihi 2003 na makundi husika na mapigano Sudan Kusini, watu milioni 2.4 waliweza kurejea makwao. Lakini eneo hili, kwa kulingana na taarifa za WFP, ni moja ya sehemu masikini sana katika Afrika, na kuna ukosefu mkubwa wa huduma za kimsingi, kwa ujumla, kwa wakazi wake bado wanasubiri kushuhudia kile kinachotambuliwa kama “mgawo wa natija za amani”.

20/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP inasema hali ya chakula Darfur inatia wasiwasi

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), ambalo linahudumia misaada ya kihali kwa watu milioni 3.6 katika Jimbo la Magharibi la Sudan la Darfur limeripoti kukabiliwa na majukumu ziada baada ya mashirika wenzi, yasio ya kiserikali, kufukuzwa Sudan mnamo mwanzo wa mwaka huu.

20/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Chinese Unit

KM Ban Ki-moon ametoa taarifa maalumu inayowahimiza WaAfghani, wa kiume na kike wanaostahili kupiga kura, kushiriki kwenye uchaguzi ujao wa Uraisi na Baraza la Majimbo, utakaofanyika nchini tarehe 20 Agosti 2009. Alisema kushiriki kwao kwenye uchaguzi huo, utaisaidia Afghanistan kuimarisha zaidi taasisi za kidemokrasia nchini na kuongeza nguvu za mifumo ya kisiasa na, hatimaye, kuzikamilisha zile ahadi za kuchangisha ustawi na amani katika Afghanistan. Vile vile KM aliwasihi wagombea uchaguzi wote, pamoja na wafuasi wao, na mawakala wa vyama vya kisiasa, na pia waangalizi wa uchaguzi wa kizalendo na wa kimataifa, kuendelea kushirikiana na Kamisheni Huru ya Taifa Inayosimamia Uchaguzi pamoja na zile taasisi nyengine katika Afghanistan, na vile vile kushirikiana na wadau wa kimataifa wanaosaidia kwenye matayarisho ya uchaguzi, ili kuhakikisha mfumo wa kupiga kura utaendeshwa kwa mafanikio na bila ya shida.

19/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM umepokea chini ya nusu ya maombi ya msaada unaohitajika Zimbabwe

Mratibu wa misaada ya kiutu ya UM katika Zimbabwe, Augustino Zacarias ametoa taarifa iliotahadharisha kwamba “ijapokuwa Zimbabwe haikabiliwi na mapigano au vurugu, hata hivyo matishio ya kihali, mathalan, upungufu wa chakula, miripuko ya maradhi ya kuambukiza kama kipindupindu, ni matatizo ambayo bado yanaendelea kusumbua taifa.”

19/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi wa UM dhidi ya ufukara hanikiza kuzuru Zambia

Magdalena Sepulveda, Mtaalamu Huru wa UM anayetetea haki za binadamu na umaskini uliovuka mipaka, anatarajiwa kuzuru Zambia kuanzia tarehe 20 mpaka 28 Agosti 2009, kufuatia mwaliko rasmi wa Serikali ya Zambia.

19/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM inawakumbuka na kuhishimu wahudumia misaada ya kiutu duniani

Siku ya leo inaadhimishwa na UM, kwa mara ya kwanza kihistoria, kuwa ni 'Siku ya Kumbukumbu kwa Wahudumia Misaada ya Kiutu Duniani.’

19/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

KM Ijumanne amemaliza ziara yake katika Jamhuri ya Korea/Korea ya Kusini. Kabla ya kuondoka mji mkuu wa Seoul, KM alizuru madhabahu ya kuomboleza yaliopo hospitali, kumhishimu aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya Korea, Kim Dae-jung, ambaye alifariki siku ya leo.

18/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO haina uhakika wa maandalizi ya chanjo ya A/H1N1

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kutoka Geneva kwamba hivi sasa halitoweza kufanya makadirio ya jumla kuhusu dawa ya chanjo inayotengenezwa dhidi ya homa ya mafua ya aina ya A/H1N1 mpaka mwezi Septemba.

18/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watumishi wawili wa UM, miongoni mwa waliouawa na shambulio la kujiangamiza Afghanistan

Spanish Radio

Watumishi wawili wa UM katika Afghanistan walikuwa miongoni mwa watu saba waliouawa, Ijumanne ya leo, shambulio la bomu la kujitolea mhanga liliotukia katika sehemuya kati ya mji wa Kabul, siku mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa taifa kuteua wawakilishi wa baraza la majimbo na raisi.

18/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID imeanzisha kitengo maalumu kuchunguza unyanyasaji wa kijinsiya Darfur

Shirika la UM-UA juu ya Ulinzi Amani kwa Darfur (UNAMID) limeripotiwa kuanzisha kitengo maalumu cha polisi kwa makusudio ya kufanya uchunguzi na kudhibiti makosa ya jinai yanayohusika na matumizi ya nguvu na unyanyasaji dhidi ya wanawake, tatizo ambalo linaripotiwa limeselelea kwa wingi katika eneo la Sudan magharibi la Darfur.

18/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Wahamiaji waliorejea Sudan kusini wakabiliwa na matatizo magumu makwao’: IMO

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), ambalo ni miongoni mwa jumuiya za kimataifa zinazoshirikiana kikazi kwa ukaribu zaidi na UM, limewasilisha ripoti mpya iliotolewa Geneva hii leo, inayozingatia hali ya wahamiaji wa ndani ya nchi pamoja na wahamaji wazalendo waliorejea Sudan Kusini kutoka mataifa jirani na kutoka nje.

18/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR kuhamisha tena wahamiaji wa Dadaab, Kenya

Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliripoti leo kutoka Geneva kwamba taasisi yao imeanzisha rasmi, wiki hii, operesheni za kuwahamisha wahamiaji wa Usomali 12,900 kutoka kambi ya Dadaab, iliosongamana watu kupita kiasi, na kuwapeleka wahamiaji kwenye kambi ya makaazi ya muda ya Kakuma, iliopo kaskazini-magharibi nchini Kenya.

18/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Chinese Unit

KM Ban Ki-moon ameshtumu, kwa kauli kali kabisa, shambulio la kujitoa mhanga liliotumia gari, na kutukia Ijumamosi kwenye sehemu ya kati ya mji wa Kabul, ambapo watu saba wanaripotiwa waliuawa na idadi kubwa ya watu walijeruhiwa, ikijumlisha mfanyakazi mmoja wa UM. Taarifa ya KM ilisema ameingiwa wahka juu ya usalama nchini kwa sababu ya kuzuka kwa vurugu la kihorera, siku chache tu kabla ya Uchaguzi wa Raisi na Majimbo, unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 Agosti (2009). KM aliwatumia mkono wa taazia na pole kwa aila zote za waathiriwa wa tukio hilo. Kadhalika aliwatumia aila za majeruhi salamu za kuwaombea wapone haraka.

17/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya Afrika Kusini na Misiri vyawasili Darfur kuisaidia UNAMID

Mnamo mwisho wa wiki iliopita wanajeshi 95 kutoka Misri pamoja na maofisa wa polisi 79 wa Afrika Kusini waliwasili Darfur kujiunga na Shirika la Ulinzi Amani la UM-UA kwa Darfur (UNAMID).

17/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti mpya ya UM inatathminia athari ya vikwazo kwa umma katika Tarafa ya Ghaza

ocha

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imewasilisha ripoti mpya juu ya hali katika eneo la WaFalastina liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza, yenye mada isemayo “Wamo Kifungoni: Athari za Kiutu za Vikwazo vya Miaka Miwili kwenye Tarafa ya Ghaza”.

17/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Liberia: KM apendekeza operesheni za amani ziongezwe mwaka mmoja zaidi

KM amechapisha ripoti mpya kuhusu maendeleo katika kurudisha utulivu na amani nchini Liberia, iliotolewa rasmi Ijumatatu ya leo.

17/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wadogo milioni 6 kupatiwa chanjo kinga ya polio katika Cote d’Ivoire

English Unit

Serikali ya Cote d’Ivoire leo inakamilisha kampeni ya siku nne iliokusudiwa kuchanja watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano, dhidi ya maradhi hatari ya kupooza au polio, shughuli ambazo zilianzishwa rasmi tarehe 14 Agosti.

17/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM imelaani shambulio la majengo yake Usomali Kusini

Ijumapili ya tarehe 16 Agosti (2009) watu saba mpaka 10, waliobeba silaha, walishambulia majengo ya Shirika la Miradiya Chakula Duniani (WFP) katika mji wa Wajiid, katika Usomali kusini, mnamo saa sita za usiku kwa majira ya Afrika Mashariki, kwa mujibu taarifa ya Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA).

17/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) kwenye taarifa iliotoa kwa waandishi habari Ijumaa, imeeleza kwamba inakabiliwa na jukumu la kuhakikisha idadi kubwa ya wapiga kura itajumuika kwenye uchaguzi ujao wa uraisi na baraza la majimbo katika Afghanistan, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini mnamo tarehe 20 Agosti 2009. UNDP imearifu kuwa inatumia wanariadha mashuhuri na wasomi wa taaluma za uraia kusaidia kuhamasisha watu kwenda kupiga kura, na pia kuilimisha raia juu ya taratibu za kupiga kura kwenye sehemu zote za nchi. Ijapokuwa Kamisheni Huru ya Uchaguzi Afghanistan (IEC) ndio ilioidhaminiwa kusimamia kikamilifu shughuli za uchaguzi, vile vile Raisi Hamid Karzai na Baraza la Usalama wameiomba UM kuongoza na kusaidia kuratibu maandalizi ya uchaguzi katika Afghanistan, kwa kupitia Shirika la UNDP pamoja na Shirika la UM la Kusaidia Huduma za Amani Afghanistan (UNAMA).

14/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waathirika wa chuki za wageni Afrika Kusini wanasema ‘bora usalama badala ya anasa za maisha’

Migrants in South Africa Seek Assistance to Return Home  IOM

Taarifa ya Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) iliotolewa wiki hii ilielezea mvutano uliozuka kwenye kambi ya makazi ya muda ya Bluewater, katika mji wa Cape Town ambapo wanaishi wahamiaji 396 ambao mnamo mwezi Mei 2008 walifukuzwa kwenye mastakimu ya muda kwa sababu ya tukio liliodaiwa kuwakilisha chuki za wazalendo dhidi ya wageni.

14/08/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria za kiutu za kimataifa ziliharamishwa Ghaza, imeripoti UM

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay leo ametangaza ripoti yenye kuonyesha kulifanyika uharamishaji wa hali ya juu wa sheria ya kiutu ya kimataifa pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu, uliotukia baina ya tarehe 27 Disemba 2008 hadi Januari 18, 2009 katika eneo liliokaliwa la WaFalastina katika Tarafa ya Ghaza.

14/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo machache yalipatikana kwenye kikao cha Bonn, asema Mkuu wa UNFCCC

Mkutano wa wiki moja kuzingatia vifungu vya waraka wa kujadiliwa kwenye Mkutano wa Copenhagen kuhusu udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa, utakaofanyika mwezi Disemba, Ijumaa ya leo, umekamilisha mashauriano yake mjini Bonn, Ujerumani. Wajumbe wa kimataifa 2400 walihudhuria kikao hicho cha Bonn.

14/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma ndege za WFP katika Chad zafadhiliwa dola milioni moja

wfpairplane

Imetangazawa kutoka Geneva ya kwamba Ndege za Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) zitafadhiliwa msaada wa dola milioni moja kutoka Serikali ya Marekani, utakaotumiwa kuhudumia misaada ya kiutu katika Chad kwa mwezi mmoja ziada. Mnamo siku za karibuni, WFP ilikabiliwa na tatizo la kusitisha huduma hizo kwa sababu ya upungufu wa fedha.

14/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC imependekeza Bemba aachiwe kwa muda

Jean-Pierre Bemba - ICJ

Mahakama ya UM juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) leo imetangaza kumwachia huru, kwa muda, aliyekuwa naibu-raisi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Jean-Pierre Bemba Gombo mpaka wakati ambapo kesi yake itaanza kusikilizwa na mahakama.

14/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Ripoti ya Mapitio ya 2008′ kutoka IAEA

Ripoti ya Mapitio ya Mwaka 2008 ya Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) imebainisha idadi kubwa ya mataifa yamependekeza kuwa na viwanda vya kizalendo vya kinyuklia, kuzalisha umeme.

13/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhamisho wa mabavu wa raia katika Port Harcourt, Nigeria waitia wasiwasi UM

Raquel Rolnik, mtaalamu huru wa UM anayetetea haki za umma kupata makazi, ameripoti kutoka Geneva kuingiwa wasiwasi juu ya taarifa alizopokea za kuhamishwa kwa nguvu mamia elfu ya raia waliopo katika Bandari ya Harcourt (Port Harcourt), Nigeria ikiwa miongoni mwa vitendo vya utekelezaji wa sera za serikali za kufufua upya miji.

13/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF imeripoti hali ya usalama itachelewesha ugawaji wa misaada ya kunusuru maisha Usomali

Taarifa ilitoka Nairobi siku ya leo ya Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) imeeleza kuwa shirika litaakhirisha kupeleka misaada ya chakula cha kunusuru maisha ya watoto 85,000, wanaoteseka na utapiamlo hatari, katika baadhi ya sehemu za majimbo ya Usomali ya kati na kusini, kwa sababu ya kukithiri kwa uhasama dhidi ya watumishi wa mashirika yanayohudumia misaada ya kihali.

13/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Alkhamisi Baraza la Usalama limeongeza sauti yake miongoni mwa jamii ya kimataifa na kutaka wafungwa wote wa kisiasa katika Myanmar waachiwe, ikijumuisha kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi. Kadhalika Baraza la Usalama limeeleza kuingiwa wahka juu ya hukumu ya kuongeza kifungo cha nyumbani cha miezi 18 ziada, dhidi ya Aung San Suu Kyi, ambaye sasa hivi ameshakamilisha miaka 14 ya kizuizi cha ndani ya nyumba kabla ya hukumu iliotolewa wiki hii. Kwenye risala ya Baraza la Usalama iliosomwa na Raisi wake kwa mwezi Agosti, Balozi Tom Sawers wa Uingereza ilisisitiza umuhimu wa Serikali ya Myanmar kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa, na kuisihi Serikali “kuchukua hatua zinazotakikana kuandaa mazingira yanayohitajika kuendeleza majadiliano yanayoaminika na Dauw Aung San Suu Kyi pamoja na vyama vyote husika, na pia makundi ya kikabila yaliopo Myanmar ili baadaye kuleta upatanishi wa pamoja wa taifa.” Wajumbe wa Baraza la Usalama wamesisitiza kwenye risala kwamba wanaunga mkono mchango wa ofisi ya KM katika shughuli za kuleta suluhu inayoridhisha katika Myanmar kwa natija za raia wote.

13/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa kwenye ‘UM ya Majaribio’ anasailia natija za kitaaluma mkutanoni

Mpango wa mazoezi ya kisiasa, unaotambiliwa kama ‘Mradi wa UM ya Majribio’ hutekelezwa kile mwaka na wanafunzi wa maskuli na vyuo vikuu kadha wa kadha katika dunia. Lengo hasa la mazoezi haya ni kuwapatia wanafunzi wanaoshiriki kwenye mradi, fursa ya kushuhudia hali halisi ya shughuli za UM na taasisi zake mbalimbali, zinazosimamiwa na kuongozwa na raia wa kutoka kila pembe ya dunia.

12/08/2009 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Mikataba ya Geneva juu ya Hifadhi ya maisha na hishima ya wanadamu wasioshiriki kwenye mapigano – hususan, raia, wafanyakazi wa afya, wahudumia misaada ya kiutu, pamoja na wagonjwa, wanajeshi majeruhi na mateka wa vita – imetimia miaka 60 mnamo tarehe ya leo, 12 Agosti 2009. KM ameeleza kwenye taarifa aliotoa juu ya kumbukumbu hiyo kwamba kanuni ya Mikataba ya Geneva zimefanikiwa “kudumishwa na kuvumiliwa na umma wa ulimwengu kwa muda mrefu” kwa sababu ya umuhimu unaopewa sheria hizo na jumuiya ya kimataifa. KM alipendekeza kwa Mataifa Wanachama yote kuchukua hatua zinazofaa, kuhakikisha kanuni za kimsingi za Mikataba ya Geneva huwa zinatekelezwa na wote kama ipasavyo.

12/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNISDR inasema onyo la mapema linahitajika kupunguza athari za mporomoko wa ardhi

isdr-disaster-gde

Shirika la UM juu ya Miradi ya Kimataifa Kukabili Maafa (UNISDR) limetoa taarifa inayotabiri kukithiri kwa miporomoko ya ardhi duniani, kwa mwaka huu, kwa sababu ya mvua kali na mabadiliko ya hali ya hewa yaliotanda kimataifa.

12/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinzi amani wa Tanzania wawasili Darfur: UNAMID

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limetangaza kwamba wanajeshi walinzi amani 200 kutoka Tanzania leo wamewasili kujiunga na operesheni zake kwenye jimbo la magharibi la Sudan.

12/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Dhoruba timilifu ya maafa ya kiutu’ inajiandaa kupiga Sudan Kusini

Sudanese refugee women prepare their luggage for the trip back to South Sudan, Kakuma camp, Kenya. UNHCR

Naibu Mratibu wa UM juu ya Misaada ya Dharura, Lise Grande ametoa onyo maalumu hii leo, kutoka Khartoum, lenye kubashiria mripuko wa “dhoruba timilifu ya maafa ya kiutu”, katika Sudan Kusini, tofani ambayo alisema itahatarisha maisha ya asilimia 40 ziada ya wakazi wa eneo hilo la nchi.

12/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku Kuu ya Kimataifa kwa Vijana

Tarehe ya leo, Agosti 12, inahishimiwa na UM kuwa ni Siku Kuu ya Kimataifa kwa Vijana. Kwenye risala aliotoa kuadhimisha siku hii, KM Ban Ki-moon alikumbusha matatizo yaliowakabili vijana kwa hivi sasa, vijana wa kiume na wa kike duniani, huathiri bila kiasi fungu hili la umma wa kimataifa, kwa sababu ya kuanguka kwa shughuli za uchumi kwenye soko la kimataifa na kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

12/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa KM apongeza kuachiwa huru wahudumia misaada Usomali

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah, leo ametoa taarifa yenye kupongeza kuachiwa huru kwa wahudumia misaada ya kiutu wanne pamoja na marubani wawili waliotekwa nyara miezi tisa iliopita nchini Usomali.

12/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahojiano kamili ya msomi wa Kenya, Ngugi wa Thiong’o, juu ya ‘wajibu wa mataifa kulinda raia’

Mnamo mwezi Julai, kwenye kikao kiso rasmi cha Baraza Kuu, walikusanyika wataalamu kadha wa kadha walioshiriki kwenye majadiliano ya hamasa kuu, yaliozingatia ukosefu wa ari, miongoni mwa Mataifa Wanachama, ya kukabili kipamoja maovu na ukatili unaofanyiwa raia pale serikali yao inaposhindwa kuwapatia raia hawo hifadhi.

11/08/2009 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

United Nations Headquarters New York media coverage. UN PHOTO

Shirika la UM Kusimamia Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS) limeripoti kuwa limefanikiwa kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi wa kuwapokonya silaha wapiganaji wa zamani katika Jimbo la Blue Nile, liliopo Sudan kusini. Ijumatatu, kwenye mji wa Ed Damazin wapiganaji wa zamani 5,674 walisalimisha silaha kwa UM. Thuluthi moja ya wapiganaji hawa wameshakamilisha mafunzo juu ya nidhamu zinazotakikana kuwaunganisha tena na maisha ya kikawaida kwenye jamii zao ziliopo katika maeneo ya Jimbo la Nile (Nile State), Kordofan Kusini (Southern Kordofan) na katika Abyei. Mapatano ya Jumla ya Amani ya 2005, baina ya Kaskazini na Sudan Kusini yameamuru wapiganaji wa zamani 180,000 kutoka Jeshi la Sudan, majeshi ya mgambo ya PDF na SPLA kusalimisha silaha zao kwa taasisi za kimataifa kama UNMIS. Mradi huu sasa unakabiliwa na matatizo ya fedha zinazotakikana kuutekeleza kama ilivyodhaminiwa na mapatano ya makundi husika. Mkutano wa kimataifa kuchangisha msaada huo, uliofanyika mwezi Februari kwenye mji wa Juba ulikadiria kwamba wahisani wa kimataifa watahitajia kuchangisha msaada wa fedha wa dola milioni 430 kugharamia kikamilifu mradi wa kupokonya silaha wapiganaji wa zamani, na jumla iliokusanywa kwa sasa kutoka wafadhili wa kimataifa ni dola milioni 88.3 tu.

11/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO itaanza kuripoti maambukizi ya A/H1N1 kila Ijumanne

Shirika la Afya Duniani (WHO) limearifu hii leo kutoka mjini Geneva, kwa kupitia msemaji wake Fadéla Chaib, ya kuwa kila Ijumanne litakuwa likitangaza taarifa mpya juu ya maambukizi ya homa ya mafua ya A/H1N1 ulimwenguni.

11/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM alaumu kifungo ziada cha Aung San Suu Kyi kutoka mahakama ya Myanmar

Aung San Suu Kyi

KM Ban Ki-moon amelaumu uamuzi wa mahakama ya Myanmar, wa kutoa adhabu ziada ya kifungo cha nyumbani cha miezi 18, kwa kiongozi mpinzani na mpokezi wa Tunzo ya Amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi.

11/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF imeripoti kushtushwa na tatizo la utapiamlo hatari linalosumbua watoto wa JAK

Nembo ya UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetoa taarifa yenye kuelezea kushtushwa na muongezeko wa tatizo la utapiamlo hatari, tatizo linaoendelea kukithiri miongoni mwa watoto wadogo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK).

11/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Usomali yaendelea kuharibika, inahadharisha OCHA

Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) imeripoti, Ijumanne, kutoka Geneva, kwamba hali ya usalama nchini Usomali, kwa ujumla, inaendelea kuharibika wakati mahitaji ya kunusuru maisha yakizidi.

11/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kumbukumbu ya Wahudumia Misaada ya Kiutu Duniani

sergio vieira de mello 07b

Mnamo tarehe 19 Agosti (2009), UM utaadhimisha, kwa mara ya kwanza 'Siku ya Kumbukumbu ya Wahudumia Misaada ya Kiutu Duniani.’

11/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

UN Photo

KM Ban Ki-moon sasa hivi anazuru Jamhuri ya Korea (Korea ya Kusini). Ijumatatu, wakati alipokuwa kwenye mji wa Seoul alihutubia Shirikisho la Jumuiya za UM Duniani ambapo alikumbusha walimwengu tunaishi hivi sasa katika umri ulioghumiwa na mizozo ya sehemu nyingi, hali ambayo haiwezi kusuluhishwa na taifa moja pekee. Alitahadharisha ya kuwa si sawa kwa mataifa kudhania mchango wa kuzisaidia nchi maskini kukamilisha Malengo ya Manedeleo ya Milenia ni “sadaka”. Alisisitiza mchango huo huwakilisha “mshikamano wa umma wa ulimwengu uliofungamana” na humaanisha maslahi ya binafsi yenye kuthibitisha wanadamu wote wamejumuika kwenye mkondo mmoja wa kimaisha. Aliendelea kwa kuutafsiri mzozo wa Darfur kuwa ni funzo kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu mafanikio na kasoro iliopo kwenye utekelezaji wa ushirikiano mpya wa pande nyingi. Alisisitiza kwamba UM unapopewa majukumu na Baraza la Usalama, hujitahidi kuyatekeleza kwa kadri ya uwezo unaofadhiliwa nawo. Alisema majukumu hayotoweza kukamilishwa kwa mafanikio ikiwa Mataifa Wanachama yanashindwa kutekeleza ahadi zao na kuinyimwa UM vifaa, zana na fedha zinazohitajika kuhudumia, kwa ukamilifu, opersheni inazodhaminiwa nazo kuimarisha uslama na amani kwenye maeneo ya mizozo.

10/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maofisa wa zamani Usomali wakutana Washington DC kuzingatia marekebisho ya kizalendo kwenye taasisi za usalama

Mkutano uliofanyika majuzi kwenye mji mkuu wa Washington D.C. Marekani, uliojumuisha maofisa wa zamani wa kijeshi na polisi kutoka Usomali, umefanikiwa kutambua vipengele maalumu vilivyochochea taasisi za usalama nchini kuporomoka na kuchafuka.

10/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa Maziwa Makuu wahimizwa kuimarisha amani

Cameroon-Nigeria Leaders Meet in New York  Nigerian President Olusegun Obasanjo (left) and his Cameroonian counterpart Paul Biya greet each other at the start of the meeting of the Cameroon-Nigeria Mixed Commission in Greentree, Long Island in New York,

Kwenye Mkutano Mkuu wa Tatu wa Viongozi wa Mataifa na Serikali wanachama wa Taasisi ya Kimataifa juu ya Masuala ya Eneo la Maziwa Makuu (ICGLR), ambao umefanyika leo Ijumatatu katika Lusaka, Zambia, Raisi mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, aliezungumzia, kwa niaba ya KM, aliyapongeza matokeo ya mkutano wa karibuni kati ya viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda, mkutano uliokuwa na makusudio ya kuendeleza hali ya utulivu na amani kwenye eneo lao.

10/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya kudhibiti marekebisho ya hali ya hewa yameanzisha duru nyengine Bonn

Hii leo kwenye mji wa Bonn, Ujerumani wajumbe wa kimataifa wamekusanyika tena kwenye duru nyengine ya kikao kisio rasmi, kushauriana juu ya maafikiano yanayotakikana kukamilishwa kwenye Mkutano Mkuu ujao, wa kupunguza umwagaji wa hewa chafu ulimwenguni, utakaofanyika mwezi Disemba mjini Copenhagen, Dennmark.

10/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku Kuu ya Kimataifa kwa Wenyeji wa Asili

Ijumapili, tarehe 09 Agosti, ni siku inayoadhimishwa na jamii ya UM kila mwaka kuwa ni 'Siku Kuu ya Kimataifa kwa Wenyeji wa Asili Duniani’.

10/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wa Kimataifa wakusanyika Geneva kuhudhuria mazoezi ya kitaaluma kwenye UM wa kuigiza

Mradi wa ‘UM ya Majaribio’ ni aina ya mazoezi ya kitaaluma yanayoendelezwa kwenye maskuli na vyuo vikuu vya kimataifa takriban kila mwaka, katika sehemu kadha wa kadha za ulimwengu.

07/08/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mashirika ya UM yanayohudumia misaada ya kihali yalishindwa mwezi Julai kuwafikia watu 500,000 wenye njaa katika Usomali, na kuwapatia chakula. Ripoti ilisema idadi hiyo ni miongoni mwa raia milioni 3.3 wa Usomali wenye kutegemea kufadhiliwa chakula na jamii ya kimataifa, hususan wale raia waliopo kwenye mji mkuu wa Mogadishu na katika eneo la kusini kuliposhtadi mapigano kwa wingi. Wakati huo huo Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza ya kuwa kuanzia Oktoba, litakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula cha kugawia watu muhitaji kimataifa. WFP ilisema itahitaji kufadhiliwa tani za metriki 209,000 za chakula, zinazogharamiwa dola milioni 208, kuweza kukidhi mahitaji ya chakula ya umma wa kimataifa katika kipindi cha sasa hivi hadi mwisho wa Machi 2010.

07/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wamaasai wa Kenya wanatazamiwa kuhifadhi mila za kijadi kwa msaada wa WIPO

Mnamo mwisho wa Julai, kwenye sherehe ya jumuiya, iliofanyika chini ya kivuli cha mti wa mkangazi, na kuhudhuriwa na wenyeji wa asili 200, Chifu Kisio na wazee wengine wa Jumuiya ya Wamaasai wa Il Ngwesi, Laikipia, Kenya walikabidhiwa rasmi vifaa vya mawasiliano ya kisasa, vya kurikodia na maofisa wa Shirika la UM juu Ya Hakimiliki za Taaluma Duniani (WIPO).

07/08/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watathminia madawa wanabashiriwa Septemba kuidhinisha chanjo kinga mpya dhidi ya homa ya A/H1N1

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti leo kwamba linatarajia kupata idhini ya taasisi za serikali zinazosimamia utumiaji madawa, kutengeneza kwa wingi mnamo mwezi Septemba dawa ya chanjo kinga dhidi ya homa ya mafua ya A/H1N1.

07/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yafadhilia uraia Waburundi wahamiaji 3,500 ziada

Wiki hii Serikali ya Tanzania imeripotiwa kutoa uraia kwa wahamiaji 3,568 kati ya wahamiaji 162,000 wa kutoka Burundi waliopeleka maombi ya kutaka uraia baada ya kuishi nchini humo kwa zaidi ya miaka thelathini.

07/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya raia wameng’olewa mastakimu na mashambulio mapya ya LRA katika JKK

Nembo ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba muongezeko wa mashambulio ya kundi la waasi wa Uganda la LRA, kwenye Jimbo la Orientale, kaskazini mashariki katika JKK, yamesababisha raia 12,500 kung’olewa makazi mwezi uliopita.

07/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP inasema mapigano ya kikabila Sudan Kusini yakwamisha huduma za chakula kwa umma muhitaji

Msemaji wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) Ijumaa aliripoti kutoka Geneva ya kwamba mashambulio yaliotukia karibuni kwenye eneo la Akobo, Sudan kusini yatazusha tena vitendo vya fujo na mtafaruku, kwa sababu ya makundi yalionuia kulipa kisasi, hali ambayo inabashiriwa itasababisha vifo zaidi.

07/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

BU inatafakaria masuala yahusuyo ‘wanawake, amani na usalama’

Baraza la Usalama(BU) asubuhi, kwenye majadiliano ya hadhara, limezingatia ripoti ya KM kuhusu maendeleo kwenye utekelezaji wa mapendekezo ya azimio 1820 (2008), yanayoambatana na ulinzi wa wanawake kwenye mazingira ya mapigano.

07/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) limeripoti mafanikio kwenye majadiliano ya mkutano wa siku mbili, wa meza ya duru, uliofanyika wiki hii mjini New York, ambapo mashirika ya kimataifa 40 ziada ya kidini yalihudhuria. Lengo hasa la ushirikiano huu kama huu kati ya UNFPA na jumuiya za kidini ni kuendeleza hatua za pamoja kuimarisha afya na huduma za uzazi bora, pamoja na kukomesha matumizi ya mabavu dhidi ya wanawake, na vile vile kutetea haki ya wanawake kupata madaraka ya kujitegemea.

06/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dawa ya chanjo kutibu A/H1N1 ni salama kutumiwa, imethibitisha WHO

Shirka la Afya Duniani (WHO) leo limetoa taarifa maalumu inayokana madai yasio msingi, yalioenezwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa, juu ya usalama dhaifu wa zile dawa za chanjo kinga dhidi ya maambukizo ya janga la homa ya mafua ya aina A/H1N1.

06/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Masuala yanayozorotisha na kukwamisha operesheni za amani za UM yatathminiwa katika BU

Ijumatano Baraza la Usalama (BU) lilikuwa na majadiliano ya hadhara, kuzingatia vizingiti vinavyozikabili shughuli za ulinzi amani za UM ulimwenguni, kwa kulingana na mapendekezo ya ripoti, isio rasmi, iliowasilishwa mwezi uliopita na Idara ya UM juu ya Operesheni za Kulinda Amani na Huduma za Maeneo ya Uhasama (DPKO).

06/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa Usomali Kenya kufadhiliwa na UNHCR msaada wa $20 milioni

money, investment Russian Radio

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwenye ziara yake rasmi nchini Kenya wiki hii alitangaza kwamba watafadhilia msaada wa dola milioni 20 kutumiwa kukidhi mahitaji ya wahamiaji wa Usomali pamoja na jamii ya wenyeji wao waliopo Kenya

06/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulio la awali la atomiki Hiroshima lakumbukwa na Mkutano wa Kuondosha Silaha Duniani

Hiroshima. 06-08-1945.

Tarehe ya leo, Agosti 06, 2009 ni siku ya ukumbusho wa kutupwa kwa bomu la kwanza la atomiki, na vikosi vya anga vya Marekani, katika mji wa Hiroshima, Ujapani miaka sitini na nne iliopita.

06/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

Tiébilé Dramé, mshauri mkuu wa UM juu ya masuala ya kisiasa ya Bukini ameripotiwa kuwa miongoni mwa wapatanishi waliokusanyika Ijumatano kwenye mji mkuu wa Maputo, Msumbiji kusimamia mazungumzo ya kusuluhisha mzozo wa kisiasa uliojiri Bukini kwa muda mrefu sasa. Juhudi hizi za upatanishi zinafanyika kwa niaba ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na kuongozwa na Raisi mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chissano. Kadhalika mazungumzo yamejumuisha wawakilishi wa kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na wanachama wa Jumuiya ya Wazungumzaji Kifaransa (Francophonie).

05/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kusambaa kwa madawa ya kulevya Guinea kunautia wasiwasi UM

drugguinea

Shirika la Polisi wa Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai (Interpol) pamoja na Idara ya UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) baada ya kufanya ziara ya uchunguzi katika taifa la Guinea, kwa ushirikiano wa karibu na Mjumbe Maalumu wa KM kwa Afrika Magharibi, ilifichua shughuli haramu za kuzalisha, kimagendo, madawa ya kulevya huendelezwa nchini humo.

05/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres anasema mzozo wa wahamiaji wa Usomali nchini Kenya ni wa “tamthilia”

António Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, wakati alipozuru kambi ya Dadaab wanapoishi wahamiaji wanaobanana wa Usomali robo milioni, kwenye eneo liliotandawaa Kenya ya kaskazini-mashariki, alitoa mwito maalumu kwa jamii ya kimataifa kukithirisha mchango wao wa fedha zinazohitajika kuuhudumia umma huu kihali.

05/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM apongeza kuachiwa huru kwa wanahabari wa Marekani katika DPRK

Taarifa ya Ofisi ya Msemaji wa KM iliotolewa Ijumatano asubuhi imesema Bani Ki-moon ameukaribisha, kwa ridhaa, uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (DPRK) wa kuwaachia huru waandishi habari wawili wa Kimarekani, kwa sababu za kiutu, wanahabari ambao walikabidhiwa Raisi mstaafu wa Marekani Bill Clinton jana Ijumanne, alipokuwa anazuru mji mkuu wa Pyongyang.

05/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulio ya raia Sudan Kusini yamelaaniwa na BU

John Sawers, Permanent Representative of the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland to the United Nations, briefs correspondents, following the Security Council meeting on the situation in Cyprus.

Ijumanne alasiri wajumbe wa Baraza la Usalama [BU] walilaani, kwa kauli ya pamoja, “mashambulio karaha” yaliotukia mwisho wa wiki iliopita Sudan kusini, ambapo inakadiriwa watu 185 waliuawa, wingi wao wakiwa wanawake na watoto wadogo.

05/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa mpya ya WHO kuhusu A/H1N1

Shirika la Afya Duniani (WHO) leo limetangaza kutoka Geneva, takwimu mpya kuhusu maambukizo ya homa ya mafua ya A/H1N1 katika dunia.

05/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Baraza la Usalama Ijumanne limepitisha, kwa kauli moja, azimio 1882 (2009) liliolaani, kwa kauli nzito, wale watu na makundi yenye kutengua sheria ya kimataifa wanapowalazimisha watoto wadogo kushiriki kwenye mapigano. Azimio limetoa mwito maalumu wenye kumtaka KM Ban Ki-moon aongeze kwenye orodha ya wakosa wa uhalifu wa kuajiri watoto kwenye mapigano, vile vile yale majina ya watu wenye kuua watoto wadogo na kuwalemaza, pamoja na watu wanaonajisi watoto kimabavu kwenye mazingira ya mapigano na vita. Orodha hii ya KM inajulikana kama "orodha ya izara/fedheha". Azimio la Baraza la Usalama liliwataka wale wote waliomo kwenye orodha kutayarisha "mipango ya utendaji, ya muda maalumu, kukomesha haraka vitendo vyao na matumizi mabaya ya watoto." Kadhalika, Baraza la Usalama "limeyataka Mataifa Wanachama husika kuchukua hatua za dhahiri, na za dharura, dhidi ya watu wanaoendelea kukiuka sheria ambao hukandamiza watoto kwenye mazingira ya mapigano". Mataifa Wanachama yanatarajiwa kuwafikisha wakosa hawa mahakamani kukabili mashtaka kwa kuvunja sheria dhidi ya utunzaji na hifadhi ya watoto.

04/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR inaomba maskani ziada kutoka Kenya kwa wahamiaji wa Usomali

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) leo alizuru kambi ya wahamiaji ya Dadaab, iliopo katika eneo la Kenya mashariki ambapo wanaishi, kwa kubanana, wahamiaji 250,000 wa Usomali waliohajiri makwao, kufuatia mapigano yaliozuka nchini mwao mnamo miezi ya karibuni.

04/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume juu shughuli za askari wa kukodi yakamilisha ziara ya Marekani

mercenaries, private army Russian Radio

Tume ya Kundi la Kufanya Kazi la UM juu ya kanuni zinazohusu matumizi ya askari wa kukodi, limekamilisha ziara ya wiki mbili Marekani wiki hii.

04/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umeitisha kikao maalumu Bonn kuhamasisha maafikiano ya Mkutano wa Copenhagen

Imetangazwa kwamba UM karibuni utafanyisha kikao, kisio rasmi, cha mashauriano, kuzingataia taratibu za kuimarisha zaidi hatua za utendaji za ule waraka wa kujadiliwa mwezi Disemba, kwenye Mkutano wa Copenhagen wa kudhibiti bora taathira za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

04/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna wa Haki za Binadamu aingiwa wahka na ripoti za fujo Nigeria

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ametangaza hii leo kutoka Geneva ya kwamba ana wahka mkubwa kuhusu ripoti alizopokea, juu ya taathira za kufumka kwa vurugu ikichanganyika na hali mbaya ya raia iliotanda majuzi katika eneo la Nigeria kaskazini, kufuatia mashambulio ya wafuasi wa kundi la kidini linaloitwa 'Boko Haram’.

04/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Uingereza imechukua madaraka ya uraisi wa duru wa Baraza la Usalama kwa mwezi Agosti, kwa mujibu wa taarida za Msemaji wa KM. Raisi wa Baraza, Balozi John Sawers wa Uingereza alikuwa na mashauriano kadha wa kadha na wajumbe wa taasisi hiyo ambao walizingatia ajenda ya kazi kwa mwezi huu.

03/08/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO inasailia kitendawili cha suala lipi la afya lastahili misaada ya kimataifa

Jarida la Shirika Afya Duniani (WHO) liliochapishwa Geneva, siku ya leo, limeeleza kwamba masuala ya afya ya jamii hupewa umuhimu na viongozi wa kisiasa, wafadhili wa kimataifa na pia jumuiya za kiraia, kwa kutokana na namna matatizo haya yanavyojulishwa, kutangazwa na kuenezwa.

03/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

EU itaifarajia WFP Yuro milioni 34 kukuza uzalishaji wa kilimo kwa nchi maskini

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti leo kwamba litafadhiliwa mchango wa yuro milioni 34 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) ili kuwasaidia wakulima wadogo wadogo katika Afrika, Asia na Amerika ya Latina kuimarisha uzalishaji wa mazao kwenye maeneo yao.

03/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umma wa Niger wanasihiwa na KM kuonyesha uvumilivu kwenye upigaji kura ya maoni kurekibisha katiba

KM Ban Ki-moon, kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wake, juzi ametoa nasaha maalumu kwa umma wa Niger kujizuia na machafuko na vurugu nchini mwao, na kuutaka pia umma uonyeshe uvumilivu wa hali ya juu wakati wanajiandaa kushiriki kwenye kura ya maoni, yenye utata, ambayo lengo lake hasa ni kubadilisha katiba itakayomruhusu Raisi wa sasa kugombania uchaguzi kwa mara ya tatu.

03/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ashtumu vikali mashambulio ya kikatili Sudan Kusini

Darfur / Sudan map Spanish Radio

Mashambulio yaliotukia Ijumapili katika Akobo, Jimbo la Jongeli, Sudan Kusini ambapo watu 161 wanaripotiwa waliuawa, ikijumlisha wanawake na watoto 100, wanaume watu wazime 50 na askari 11 wa kundi la SPLA yamelaaniwa vikali na KM hii leo, hali ambayo imemlazimisha kulielekeza Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS), kuchukua hatua za dharura kuhudumia wale wote waliodhurika na vitendo katili hivyo, na vile vile kushirikiana na wenye madaraka kurudisha amani haraka iwezekanavyo kwenye jimbo hili la mtafaruku.

03/08/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930