Nyumbani » 31/07/2009 Entries posted on “Julai, 2009”

Baada ya kuzuru Asia KM awaonya walimwengu juu ya hatari ya taathira za mabadiliko ya hali ya hewa

Ijumatano, tarehe 29 Julai 2009, KM Ban Ki-moon alikuwa na mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa waliopoMakao Makuu kuzingatia safari ya wiki moja aliyoyatembelea mataifa mawili ya Asia, yaani Uchina na Mongolia.

31/07/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Alkhamisi KM alikuwa na mkutano makhsusi na Mjumbe wa Kudumu wa Myanmar katika UM. Kwenye mkutano wao huo KM alimuarifu Mwakilishi wa Myanmar ya kuwa ni matarajio yake, na pia ya jumuiya ya kimataifa, halkadhalika, kwamba Serikali itazingatia, kwa uangalifu mkubwa zaidi, taathira za hukumu watakayotoa kwenye kesi inayomhusu kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi, na anaamini Serikali itatekeleza jukumu lake adhimu la kumtoa kizuizini mapema iwezekanavyo.

31/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uganda imekamilisha uraisi wa BU kwa Julai

Siku ya leo, tarehe 31 Julai 2009, ni siku ambayo Uganda inakamilisha uraisi wa kusimamia shughuli za Baraza la Usalama (BU) kwa mwezi huu.

31/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika yaongoza mataifa katika kunyonyesha watoto wachanga: WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) lemeripoti kwamba bara la Afrika ni miongoni mwa maeneo machache ulimwenguni yenye kuongoza kwenye huduma za kunyonyesha watoto wachanga, licha ya kuwa eneo hili linakabiliwa na matatizo aina kwa aina ya kiafya na kiuchumi. WHO imeeleza pindi kiwango cha kunyonyesha watoto katika Afrika kitaongezeka kwa asilimia 90, inakadiriwa watoto wachanga milioni 1.3 wataokoka vifo kila mwaka.

31/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za WFP Afrika zakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha

wfpairplane

Huduma za ndege zinazotumiwa na watumishi wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Dunaini (WFP) kugawa misaada ya chakula kwa mamia elfu ya umma muhitaji, unaoishi hasa kwenye zile sehemu za mbali za Afrika zenye shida ya kufikiwa na malori au usafiri mwengineo, huduma hizi zitalazimika kusitishwa ifikapo tarehe 15 Agosti mwaka huu, kwa [...]

31/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 50,000 wameng’olewa makazi na fujo zilizoipamba JKK mashariki

Nembo ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwenye taarifa iliotangaza Geneva asubuhi ya leo katika mkutano na waandishi habari, imeripoti raia 56,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) walilazimika kung’olewa makazi katika jimbo la mashariki kufuatia fujo zilizofumka tena kwenye eneo hilo mnamo tarehe 12 Julai.

31/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Baraza la Usalama Alkhamisi limepitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni mbili za UM juu ya ulinzi amani katika Cote d’Ivoire na Darfur, Sudan. Kuhusu Cote d’Ivoire Baraza lilipiga kura kwa kauli moja kuongeza kwa miezi sita muda wa operesheni za Shirika la UM Kulinda Amani katika Cote d’Ivoire (UNOCI). Wakati huo huo Baraza limeidhinisha kibali cha kibali cha kuendeleza operesheni za Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) kwa miezi kumi na mbili ijayo, hadi Julai 2010. Kadhalika Baraza la Usalama lilimtaka KM atayarishe mradi wa utendaji wenye vigezo vya kutathminia na kufuatilia maendeleo juu ya namna maazimio ya Baraza yanatekelezwa katika Darfur.

30/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Haki za binadamu na jamii zinajadiliwa kwenye kikao cha ECOSOC

Halmashauri ya UM juu ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii (ECOSOC) inayokutana Geneva Alkhamisi ilizingatia masuala yanayohusu haki za binadamu na haki za kijamii, zenye kuambatana na huduma za maendeleo, uzuiaji wa uhalifu na mifumo ya sheria.

30/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za dharura zahitajika kupunguza shida za ajira kwa wafanyakazi wahamaji waliopo nje, inasihi UNCTAD

Nembo ya UNCTAD

Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, (UNCTAD) limearifu kwamba muongezeko wa ukosefu wa kazi ulimwenguni kwa sababu ya kuzorota kwa shughuli za kiuchumi katika soko la kimataifa, ni hali inayosababisha fungu kubwa la wafanyakazi waliohamia nchi za nje kuamua kurudi makwao.

30/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO itafadhiliwa dola milioni 2.5 na Saudi Arabia kutayarisha mkutano wa kukomesha njaa

UM umetangaza ya kuwa Saudi Arabia itafadhilia msaada wa dola milioni 2.5 kwa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) ili kuiwezesha taasisi hii kufanyisha Mkutano Mkuu juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani, utakaojumuisha wajumbe kadha wa kadha wa kutoka Mataifa Wanachama kwenye Makao Makuu ya FAO mjini Roma, Utaliana kuanzia tarehe 16 hadi 18 Novemba mwaka huu.

30/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto waliopo vizuizini Rwanda kusaidiwa mawakili na mradi wa UM

Kadhalika Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba linaunga mkono, na kuahidi pia kuusaidia ule mradi ulioanzishwa na Wizara ya Utawala wa Sheria ya Rwanda, wa kuwapatia watoto 600 ziada waliomo vizuizini, mawakili wa kuwatetea kesi zao.

30/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuisaidia Angola kuhudumia raia maji safi

Mradi wa Pamoja wa Mashirika ya UM Kuhudumia Maji na Usafi umeanzishwa rasmi karibuni nchini Angola.

30/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Ripoti mpya ya KM kuhusu maandalizi ya uchaguzi katika Sudan, uchaguzi unaotazamiwa kufanyika mwezi Aprili 2010, imeeleza kwamba ijapokuwa kumepatikana mafanikio ya kutia moyo kwenye matayarisho ya jumla, hata hivyo, hatua chache za kimsingi zimesalia kutekelezwa na Serikali ya Sudan. Ripoti ilionyesha kuna ukosefu wa kudhaminia kihakika haki za kimsingi kwa raia wakati wa kupiga kura, ikijumlisha uhuru wa kukusanyika, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kusema, ikiwa miongoni mwa masuala kadha ambayo yameyafanya baadhi ya mashirika ya kiraia kutokuwa na imani kuhusu uchaguzi ujao. KM ameisihi Kamisheni ya Uchaguzi wa Taifa Sudan kuchukua hatua halisi zitakazohakikisha raia wote waliong’olewa makazi pamoja na wahamiaji, na wale waliokosa vitambulisho, huwa wanajumuishwa kwenye miradi ya uchaguzi. KM alisema UM upo tayari kutekeleza mpango wa awamu mbili utakaotumiwa kuzisaidia kamisheni 25 za uchaguzi katika majimbo, kwa kusafirisha vifaa vye kuendesha uchaguzi kama inavyotakikana kisheria.

29/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa ‘R2P’ wahitimisha mijadala kwenye Baraza Kuu

Baraza Kuu la UM Ijumanne alasiri limekamilisha mahojiano kuhusu lile suala la 'dhamana ya Mataifa kulinda raia dhidi ya jinai ya halaiki”, rai ambayo vile vile hujulikana kwa umaarufu kama 'kanuni ya R2P.’

29/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM kwa Usomali asema msaada wa jumuia ya kimataifa unahitajika kidharura kurudisha utulivu nchini

Baraza la Usalama lilikutana leo asubuhi kuzingatia hali katika Usomali. Risala ya ufunguzi ya Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Oul-Abdallah iliwahimiza wajumbe wa Baraza kuchukua “hatua thabiti” zitakazosaidia kurudisha tena utulivu kwenye taifa hili la Pembe ya Afrika, hasa katika kipindi cha sasa ambapo mapigano ndio yameshtadi zaidi kati ya majeshi ya mgambo wapinzani ya Al-Shabaab na Hizb-al-Islam dhidi ya vikosi vya Serikali, uhasama ambao ulizuka tena upya mjini Mogadishu mnamo tarehe 07 Mei (2009).

29/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ameshtushwa na mapambano ya kimadhehebu Nigeria Kaskazini

Kadhalika, Ijumanne, KM alitoa taarifa maalumu yenye kuelezea wasiwasi wake mkuu juu ya ripoti za kuzuka, hivi majuzi, duru nyengine ya mapigano ya kimadhehebu katika Nigeria kaskazini, vurugu ambalo limesababisha korja ya vifo.

29/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban anasema ni muhimu kwa Mataifa kuhitimisha mashauriano ya mkataba wa kudhibiti hali ya hewa

KM Ban Ki-moon leo alikuwa na mazungumzo ya kila mwezi na waandishi habari wa kimataifa waliopo hapa Makao Makuu ya UM. Kwenye taarifa ya ufunguzi KM alizingatia zaidi suala la athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni na juhudi za kimataifa za kulidhibiti tatizo hili.

29/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasailia hali ya usalama katika Chad/JAK

Baraza la Usalama asubuhi lilifanyisha kikao cha hadhara kusailia hali ya usalama katika Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK). Mjumbe Maalumu wa KM anayeshughulikia huduma za ulinzi amani wa mataifa haya mawili, Victor Angelo, alipowakilisha taarifa yake mbele ya Baraza alisema jumuiya ya kimataifa inawajibika kuharakisha kufanyika majadiliano ya kidiplomasiya ili kurudisha utulivu na amani ya eneo, kufuatilia mapigano yalioripuka karibuni baina ya Chad na Sudan.

28/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizi ya A/H1N1 ni ya wastani kwa sasa, inasema WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti leo hii kwamba maambukizi ya janga la homa ya mafua ya A/H1N1 kimataifa yanakadiriwa kuwa bado ni ya wastani, na wingi wa watu wanaouguwa maradhi haya kwa sasa, kwa bahati, hawashuhudii maumivu makali na hawahitajiki kulazwa hospitali.

28/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 6.2 Ethiopia wanakabiliwa na hatari maututi ya utapiamlo, OCHA inahadharisha

ocha

Fidele Sarassoro, Mratibu wa Misaada ya Kiutu katika Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) ametangaza kwamba taifa la Ethiopia linakabiliwa kwa sasa na tatizo la kuhudumia mamilioni ya raia misaada ya kihali, kwa sababu ya upungufu wa chakula, huduma za afya, lishe bora pamoja na maji safi na usafi wa mazingira, ikichanganyika pia na matatizo ya ukosefu wa makazi ya dharura, ajira na ukosefu wa shughuli za kilimo ambazo zinahitajika kuwasaidia raia kupata riziki.

28/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano Usomali kuwalazimisha maelfu ya raia kuhajiri Yemen kutafuta hifadhi

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwenye taarifa iliyoiwasilisha Geneva, Ijumanne asubuhi, ilieleza mapigano yenye kuendelea hivi sasa kwenye mji wa Mogadishu, na katika eneo la kati la Usomali, yamesababisha maelfu ya raia kuhatarisha maisha kwa kuhama makwao, na kuamua kufanya safari hatari ya kuvuka Ghuba ya Aden, kuelekea Yemen kuomba hifadhi.

28/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) liomeripoti Kamisheni ya Uchaguzi wa Taifa Sudan imewaarifu ya kuwa imeshakamilisha kuweka mipaka ya maeneo ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Aprili 2010. Vile vile Kamisheni ilisema imeshaanzisha kamati tatu zitakazoshughulikia upigaji kura kwenye majimbo yote matatu ya Darfur. Taarifa ya Kamisheni ya Uchaguzi wa Taifa Sudan pia ilisema makundi ya kiraia yataruhusiwa kuendeleza shughuli za kuhamasisha wapiga kura kutekeleza haki zao za kimsingi, bila ya kuingiliwa kati na serikali, hususan kutoka zile idara za usalama na ulinzi au ile Kamisheni juu ya Misaada ya Kiutu, na walihakikishiwa masuala yote yenye mvutano yatapelekwa kusailiwa na Kamisheni ya Uchaguzi.

28/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Catherine Bragg, Naibu Mkurugenzi wa UM Kuhusu Huduma za Dharura na KM Msaidizi wa Misaada ya Kiutu ameanza ziara rasmi ya siku tano katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK). Ijumatatu alizuru Birao, kaskazini-mashariki ya JAK. Wakati atakapokuwepo JAK, Bragg anatarajiwa kufanya tathmini ya hali ya kiutu ilivyo nchini na kuhakikisha misaada ya kihali itahudumiwa, kwa mfululizo, lile fungu la umma muhitaji wenye kutegemea misaada ya kimataifa kunusuru maisha. Bragg analizuru eneo la Birao sasa hivi mwezi mmoja tu baada ya kuripuka mapigano ya kikabila, ambapo watu waliyanganywa mali, nyumba 600 ziliunguzwa moto na raia 3,700 walilazimika kuhajiri makazi kwa sababu ya vurugu.

27/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wapiganaji watoto Darfur wameanza kupokonywa silaha na UM

Watoto 36 waliohusiana na makundi yenye silaha katika mji wa Tora, Darfur Kaskazini, wameripotiwa na UM kwamba Ijumapili walipokonywa silaha na mashirika ya kimataifa, na baadaye kurudishwa makwao.

27/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya kimataifa yameandaa mradi wa kutoa hadhari za mapema dhidi ya miripuko ya moto

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) likijumuika na Shirika la Ulaya juu ya Anga Nje ya Dunia (ESA), pamoja na Shirika la Marekani Linalosimamia Uchunguzi wa Anga (NASA) yameripoti juu ya umuhimu wa kudhibiti haraka miripuko ya moto ilioshuhudiwa kutukia ulimwenguni katika siku za karibuni, kwenye sehemu mbalimbali za dunia, hasa yale maeneo ya karibu na Bahari ya Mediterranean, kusini ya Jangwa la Sahara, Australia na katika Amerika ya Kaskazini.

27/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko ya makazi bora Afrika Kusini yanaitia wasiwasi UN-HABITAT

U.N. Habitat logo U.N. Habitat/U.N. Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT) limeripoti kuingiwa na wasiwasi kuhusu maandamano ya machafuko yaliozuka majuzi kwenye vitongoji vya Afrika Kusini, ambapo mamia ya watu walidai wapatiwe makazi madhubuti ya nyumba, pamoja na kupatiwa huduma za maji safi ya kunywa, umeme na mazingira yalio safi.

27/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM ameyakaribisha mazungumzo ya Kamati ya JSC juu ya usalama Usomali

Imetangazwa hii leo kwamba Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah, amekaribisha ule mkusanyiko wa wajumbe wa ile Kamati ya Pamoja juu ya Usalama (JSC) uliotukia kwenye mji wa Mogadishu Ijumamosi, mnamo tarehe 25 Julai (2009).

27/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ausihi ulimwengu ujirekibishe kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

KM Ban Ki-moon, kwenye hotuba alioitoa Ulaanbaatar, mji mkuu wa Mongolia Ijumatatu ya leo, kuhusu “Marekibisho ya Kudhibiti Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani” alieleza kwamba nchi zilizozungukwa na bara husumbuliwa sana na vizingiti vinavyokwamisha juhudi za kusukuma mbele maendeleo yao, hususan katika kipindi ambacho nchi hizi zisio na pwani huwa zinaathirika pia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,

27/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limetoa mwito wenye kuyahimiza Mataifa Wanachama kutumia zile taratibu za kilimo zitakazotunza na kuimarisha, kwa muda mrefu, ardhi na mazingira, taratibu zitakazojulikana kama 'mazoezi ya kilimo cha kijani’. Utaratibu huu ukitekelezwa,kwa mujibu wa UNEP, utasaidia kuleta natija kemkem kwa idadi ya umma wa kimataifa unaozidi kukithiri kwa kasi kuu. Utaratibu huu unaashiriwa pia utasaidia kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kuondosha ummaskini na kukuza uzalishaji wa chakula, nidhamu ambayo inaweza kuwa ndio chanzo cha kupata mbao zisioharibu kilimo kwa wananchi wa mataifa yanayoendelea, baada ya miti kukatwa.”

24/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

KM ameteua Kamanda Mkuu mpya wa UNAMID kutoka Rwanda

KM amewaariifu wajumbe wa Baraza la Usalama kwamba kutokana na maafikiano na Mwenyekiti wa Kamisheni ya UA, wamemteua Liuteni Jenerali Patrick Nyamvumba wa Rwanda kuwa Kamanda Mkuu mpya wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID), kuanzia tarehe mosi Septemba, mwaka huu.

24/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa rekibisho ya maambuziki ya A/H1N1 kutoka WHO

[Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti Ijumaa, kutokea Geneva kwamba maambukizi ya homa ya mafua ya A/H1N1 bado yanaendelea kimataifa, hali ambayo imeshasababisha vifo vya wagonjwa 800 katika nchi 160 duniani, zilizoripoti kugundua maambukizi ya maradhi haya kwenye maeneo yao.

24/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban anaamini miradi ya kudhibiti uchafuzi wa hali ya hewa Uchina inaweza kurudiwa kimataifa

KM Ban Ki-moon, ambaye anafanya ziara ya siku nne katika Uchina, Ijumaa alihudhuria mjini Beijing, tukio la kuanzisha mradi bia wa UM na Serikali ya Uchina kuhimiza umma wa huko, kutumia ile balbu ya taa yenye kuhifadhi nishati na inayotumika kwa muda mrefu.

24/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suluhu ya kikanda Afrika ndio yenye uwezo wa kukomesha mizozo, inasema BK

Baraza Kuu (BK) Alkhamisi limepitisha, bila kupingwa, azimio liliobainisha umuhimu wa kutumia utaratibu wa kikanda kuzuia na kusuluhisha mizozo katika bara la Afrika.

24/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msomi wa Kenya, Ngugi wa Thiong’o, ajumuisha maoni binafsi juu ya ‘wajibu wa kimataifa kulinda pamoja raia’

Alkhamisi asubuhi, kwenye kikao cha Baraza Kuu, kisio rasmi, walikusanyika wataalamu wa kimataifa walioshiriki kwenye majadiliano yenye hamasa kuu, kuzingatia ile rai ya miaka ya nyuma ya kukomesha kile kilichotafsiriwa na wajumbe wa UM kama ni “kiharusi cha kimataifa” katika kukabili maovu na ukatili unaofanyiwa raia, ndani ya taifa, wakati wenye mamlaka wanaposhindwa kuwapatia raia hawa ulinzi na hifadhi wanayostahiki.

24/07/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya raia wang’olewa makazi na mapigano Kivu Kaskazini

Nembo ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti hali ya machafuko yaliozuka karibuni kwenye Jimbo la Kivu Kusini, katika sehemu ya mashariki ya JKK imesababisha watu 35,000 kung’olewa makazi, hasa kwenye lile eneo la uwanda tambarare la Mto Ruzizi, ambapo JKK hupakana na nchi jirani za Burundi na Rwanda.

24/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

un flags 012b

Kamati ya UM ya Kuondosha Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW) ambayo inakutana wiki hii kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York, imeanza shughuli za kusailia namna nchi wanachama zinavyotekeleza mikataba ya kimataifa ya kukomesha ubaguzi wa kijinsiya. Kamati hii ya CEDAW imetimia miaka 30 katika mwaka huu. Mwenyekiti wa Kamati ya Kuondosha Ubaguzi Dhidi ya Wanawake, Naela Mohammed Gabr wa kutoka Misri, Ijumatano aliwaambia waandishi habari wa Makao Makuu kwamba miongoni mwa masuala muhimu wanayoyazingatia kwenye kikao cha safari hii ni pamoja na ile mada inayohusu taathira za mizozo ya fedha iliopamba duniani karibuni na namna inavyochafua huduma za kimsingi za jamii. Vile vile alisema Kamati inasailia mada zinazohusu mishahara wanaopatiwa wanawake kwenye mazingira ya mizozo ya kifedha kimataifa, pamoja na tatizo la kuzidi kwa ukosefu wa kazi miongoni mwa wanawake.” Kwa mujibu wa taarifa za UM Kamati ya CEDAW hutumia taratibu mbalimbali za kuhamasisha nchi wanachama kutekeleza mapendekezo yake ya kukomesha ubaguzi wa kijinsiya, mathakan, Kamati mara nyingi huchapisha rasmi ukiukaji wa haki za wanawake katika taifa fulani, fafanuzi ambazo baadaye huutumiwa Ofisi ya Kamisheni wa UM juu ya Haki za Binadamu iliopo Geneva. Ofisi ya haki za Binadamu hujumuisha matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya CEDAW kwenye ule Mradi wa Mapitio ya Jumla kuhusu namna haki za binadamau zinavyotekelezwa katika Mataifa Wanachama 192 wa UM. Mapitio haya hufanyiwa kila taifa, mara moja katika kila miaka minne. Kwenye mkutano wa wiki hii wataalamu 22 wa Kamati ya CEDAW wanafanyia mapitio juu ya hali za wanawake katika mataifa ya Azerbaijan, Bhutan, Denmark, Guinea-Bissau, Laos, Ujapani, Liberia na pia Uspeni, Uswiss, Timor-Leste na Tuvalu.

23/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ethiopia kufadhiliwa msaada wa dharura na CERF

Ethiopia refugee camps

Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF, Alkhamisi imetangaza kutoka Geneva ya kuwa itaifadhilia Ethiopia msaada wa dola milioni 6,

23/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO imeanzisha huduma ya pamoja kupiga vita Ugonjwa wa Midomo na Miguu unaoambukiza wanyama

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limeanzisha operesheni mpya za kupambana na tatizo la kusambaa kwa Ugonjwa wa Midomo na Miguu wenye kuambukiza wanyama.

23/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya KM juu ya hali Usomali

Ripoti ya KM juu ya Usomali leo imewakilishwa rasmi hapa Makao Makuu. Ndani ya ripoti, KM alibainisha wasiwasi mkubwa alionao kuhusu majaribio ya karibuni ya makundi ya upinzani ya kutaka kupindua, kwa kutumia nguvu, serikali halali ya Usomali.

23/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwajibikaji wa taifa kulinda raia ni wazo linaloungwa mkono na Pillay

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa taarifa maalumu iliochangisha maoni ziada kuhusu mjadala unaofanyika wiki hii, hapa Makao Makuu, kuzingatia suala la “Wajibu wa Jumuiya ya Kimataifa Kulinda Raia”.

23/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafanikio ya Mkutano wa Copenhagen yatahitajia $10 bilioni, anasema de Boer

Yvo de Boer, Katibu Mtendaji anayesimamia Mfumo wa Mkataba wa Kimataifa Kudhibiti Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, amenakiliwa akisema kunahitajika mchango wa dola bilioni 10 kudhibiti, kihakika, athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

23/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building UN Spanish Radio

Utafiti mpya wa Shirika la Afya Duniani (WHO) umegundua ya kuwa mama wajawazito, walioambukizwa na virusi vya UKIMWI wakipewa mchanganyiko wa madawa ya kurefusha maisha, kuanzia kile kipindi cha mwisho wa mimba hadi miezi sita ya kipindi cha kunyonyeshwa mtoto mchanga, asilimia 40 ya watoto wanaozaliwa na mama hawo hunusurika na hatari ya kuambukizwa na virusi vya maradhi. Jumuiya Mashirika ya UM dhidiya UKIMWI (UNAIDS) imeeleza na kukumbusha ya kwamba moja ya malengo muhimu ya kazi zao ni kuhakikisha wanafanikiwa kuzuia vifo vya mama wajawazito, na pia kuhakikisha watoto wachanga wanaozaliwa na mama hawo wanahifadhiwa na maambukizi ya VVU.

22/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Walinzi amani wa UM katika Liberia wameanzisha mazoezi mapya kutunza mazingira

liberia Spanish Radio

Vikosi vya ulinzi amani vya UM viliopo katika jimbo la Kakata, Liberia Magharibi vimeanzisha mazoezi mapya mnamo mwanzo wa mwezi huu, yaliokusudiwa kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

22/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

EU inashirikiana na FAO kupiga vita njaa kwenye nchi maskini

Ripoti za UM zimethibitisha ya kuwa katika 2009 watu bilioni moja ziada husumbuliwa na upungufu wa chakula na njaa sugu katika dunia.

22/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji wa kimataifa unatarajiwa kufufuliwa tena 2010, inasema UNCTAD

UNCTAD Logo UNCTAD / Spanish Unit

Ripoti ya Tathmini ya Matarajio ya Uwekezaji Duniani kwa 2009-2011 (WIPS), inayojulikana kwa umaarufu kama Tathmini ya WIPS, imeeleza kwamba mizozo ya kiuchumi na kifedha duniani imeathiri vibaya miradi ya uwekezaji wa moja kwa moja, wa mashirika makuu ya biashara kutoka nje, katika kipindi cha muda mfupi.

22/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maamuzi ya Mahakama ya Kudumu juu ya Abyei yanakaribishwa kidhati na UM

Mahakama ya Kudumu ya Kuamua Migogoro, iliopo Hague, Uholanzi leo imetangaza hukumu yake kuhusu mipaka ya eneo la mabishano la Abyei, ambapo utawala wake unagombaniwa na Sudan Kaskazini na Sudan Kusini.

22/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Ashraf Qazi, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan na Mkuu wa Shirika la Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS) ameripotiwa hii leo kuelekea eneo la mgogoro wa mpaka la Abyei, kwenye mkesha wa kutangazwa na Mahakama ya Upatanishi wa Abyei kutoka Hague maamuzi kuhusu eneo la mfarakano baina ya Sudan Kaskazini na Kusini. Uamuzi utatolewa na Mahakama ya Upatanishi Ijumatano. Mjumbe wa KM kwa Sudan Kusini alinakiliwa akisema hatua zimeshachukuliwa na wenye madaraka, za kuhakikisha makundi yote yenye silaha, isipokuwa Vikosi vya Pamoja vya Polisi na Jeshi, yameondoshwa kutoka Eneo la Mfarakano la Ramani ya Abyei kabla ya maamuzi kutangazwa kuzuia fujo.

21/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nchi Wanachama zaweza kufarajia kupima H1N1, yasisitiza WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba nchi wanachama, hivi sasa zinazo uwezo wa kufarajia kitaifa hatua za kupima viwango vya maambukizi ya maradhi ya homa ya mafua ya A/H1N1 katika maeneo yao.

21/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO kuhadharisha Bonde la Mto Zambezi lasibiwa maradhi yanayouwa samaki

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti yake rasmi iliotolewa Ijumanne, ya kwamba kumegundulikana aina ya maradhi yenye kuua na kupunguza kwa kiwango kikubwa akiba ya samaki kwenye Bonde la Mto Zambezi, hali ambayo inahatarisha akiba ya chakula na ajira ya kujipatia rizki kwa wakazi wa vijijini wa eneo hilo, liliogawanyika miongoni mwa mataifa saba ya Afrika.

21/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usubi waweza kufyekwa Afrika Magharibi kwa dawa ya ‘ivermectin’: WHO

Nembo ya WHO

Matokeo ya utafiti mpya wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kuhusu maradhi ya usubi (river blindness) katika sehemu za Afrika Magharibi, yamethibitisha kwamba ugonjwa huu unawezekana kukomeshwa kikamilifu na wataalamu wa kimataifa.

21/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA inasema inahitaji msaada wa bilioni $4.8 kukidhi mahitaji ya waathirika maafa ulimwenguni

money, investment Russian Radio

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti leo ya kuwa kuna upungufu wa dola bilioni 4.8 za msaada wa fedha zinazotakikana, katika miezi sita ya mwanzo wa 2009, kukidhi mahitaji ya kiutu kwa watu walioathirika na maafa.

21/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya wasiwasi Usomali imekwamisha, kwa muda, huduma za kiutu

Dadaab; refugee; Kenya; Somalie; Somalia UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), kwa kupitia msemaji wake Geneva, leo limeripoti kwamba muongezeko wa hali ya wasiwasi katika Usomali unazidisha ugumu wa uwezo wa watumishi wanaohudumia misaada ya kiutu kuwafikia waathirika wa karibuni wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

21/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Viongozi wa Tume ya Uchunguzi ya UM juu ya mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Benazir Bhutto imekamilisha ziara yake ya awali katika Pakistan Ijumaa iliopita. Wafanyakazi wa kusimamia shughuli za tume wanatazamiwa kubakia Pakistan kukusanya ushahidi zaidi, na ripoti juu ya uchunguzi wao inatarajiwa kutolewa rasmi kimataifa baada ya miezi sita.

20/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Makundi ya upinzani Usomali yateka nyara mali za UM

Chinese Unit

Majengo mawili ya UM katika Usomali ya Baidoa na Wajid yalishambuliwa hii leo na wapiganaji wapinzani wa kundi la Al Shabaab na walichukua vifaa na magari ya UM, kwa mujibu wa taarifa iliopokelewa kutoka Ofisi ya UM katika Usomali.

20/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNMIS ameahidiwa wanajeshi wa Sudan Kusini wataondoshwa kutoka Abyei kungojea maamuzi ya mpaka mpya

ashrafqazispecialrep

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, Ashraf Qazi ametoa taarifa, leo hii, yenye kueleza kwamba amekaribisha ahadi ziada zilizotolewa na Chama cha NCP na kutoka lile kundi la jeshi la mgambo la SPLM, kuwa watahishimu uamuzi wa Mahakama ya Kudumu juu ya Suluhu ya eneo la mvutano, lenyo mafuta, la Abyei, au Mahakama ya PCA, ambayo inatazamiwa kutangaza uamuzi wa mgogoro wao wa mipaka Ijumatano ijayo.

20/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raisi mstaafu wa Ghana ameteuliwa na WFP kusaidia kukomesha njaa inayosumbua watoto

President John Kufuor of Ghana

Raisi mstaafu wa Ghana, John Kufuor, ameteuliwa rasmi na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) kuwa Balozi Mtetezi mpya dhidi ya Njaa Duniani.

20/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada kwa utafiti wa chanjo ya ukimwi imeteremka

Ripoti mpya kuhusu uwekezaji, kwa mwaka 2008, kwenye utafiti wa kutafuta tiba kinga dhidi ya maambukizi ya VVU, mchango huo uliarifiwa kuteremka, kwa mara ya kwanza, tangu wataalamu walipoanza kukusanya takwimu juu ya utafiti wa chanjo kinga dhidi ya UKIMWI.

20/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon ameshtumu, kwa kauli kali, mashambulio ya mabomu yaliofanyika leo Ijumaa kwenye hoteli mbili za Jakarta (Indonesia), ambapo taarifa ya kwanza inasema watu tisa waliuawa. Taarifa ya KM kuhusu tukio hili ilielezea juu ya ushikamano wake na Serikali pamoja na umma wa Indonesia, na alisisitza kwamba anatambua juhudi thabiti za Serikali ya Indonesia katika kukabiliana na matatizo ya ugaidi, kwa ujumla. Alisema anatumai Serikali ya Indonesia itafanikiwa kuwafikisha mahakamani wale waliohusika na mashambulio hayo. KM aliwatumia mkono wa taazia aila zote za waathiriwa wa mashambulio na pia kuwaombea majeruhi wapone haraka.

17/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ICRC inazingatia udhibiti wa biashara haramu ya silaha ndogo ndogo ulimwenguni

Kwa muda wa angalau miaka kumi hivi, Kamati ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) ilijishirikisha kwenye jitihadi za kuyashawishi Mataifa Wanachama wa UM, kwa ujumla, kubuni kanuni kali mpya zitakazotumiwa kudhibiti biashara haramu ya silaha ndogo ndogo duniani.

17/07/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO inasema itarekibisha utaratibu wa matangazo rasmi kuhusu A(H1N1)

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti leo kwamba ongezeko la kasi la idadi ya watu wenye kuambukizwa na maradhi ya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1), katika nchi nyingi wanachama mnamo kipindi cha sasa hivi, ni tukio lenye kutatanisha juhudi za mataifa za kuthibitisha maambukizi ya maradhi kwa raia wao, kwa kulingana na vipimo vya kwenye maabara yao ya afya.

17/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waathirika wa uhasama katika JKK wafadhiliwa $7 milioni na Mfuko wa CERF kukidhi mahitaji ya kimsingi

Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF imetangaza ya kuwa itafadhilia msaada wa dola milioni 7, kukidhi mahitaji ya dharura kwa watu 250,000 waliopo kwenye majimbo yenye matatizo ya Kivu Kusini na Kaskazini.

17/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA inasema waasi wa Uganda wanaendelea kutesa raia katika JKK

ocha

Tawi la Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) iliopo Nairobi, Kenya limetoa taarifa yenye kuthibitisha waasi wa Uganda wa kundi la LRA, waliojificha kwenye maeneo ya kaskazini-mashariki, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) wanaendelea kuhujumu na kuteka nyara, pamoja na kuua raia wa katika eneo.

17/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Juhudi ziada zahitajika kukomesha uhamisho wa mabavu Uganda Kaskazini’, aonya mtetezi wa IDPs

Mr. Walter Kälin, Representative of the Secretary-General on the human rights of internally displaced persons. UN Photo/Pierre-Michel Virot-UN Spanish Radio

Walter Kaelin, Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Kibinadamu kwa wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPs) amenakiliwa akisema ameingiwa moyo na kufurahika kwa “maendeleo aliyoyashuhudia kuhusu utekelezaji wa mahitaji ya watu waliong’olewa makazi, kwa sababu ya mapigano, katika Uganda Kaskazini, ambapo takriban asilimia 80 ya umma huo, unaojulimsha wahamiaji milioni 1.8, wamesharejea vijijini mwao kwa khiyari.”

17/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC imekabidhiwa ushahidi ziada juu ya fujo kufuatia uchaguzi uliopita Kenya

Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) ameripotiwa kupokea wiki hii taarifa ziada kuhusu vurugu na fujo zilizozuka Kenya baada ya uchaguzi uliopita.

16/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za dharura kwenye sekta ya afya zinahitajika Usomali kunusuru maisha ya waathirika wa mapigano na vurugu

Ramani ya Somalia

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kwamba mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalioshtadi nchini Usomali kwa sasa hivi, yamesawijisha na kudhoofisha sana huduma za afya pamoja na miundombinu ya kijamii, hususan kwenye maeneo ya Kati na Kusini mwa nchi.

16/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNCTAD inasisitza kunahitajika wizani bora kuhamasisha maendeleo katika LDCs

[Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD), kwenye ripoti yake iliotolewa rasmi Ijumanne, yenye mada isemayo Ripoti ya 2009 kwa Nchi Zinazoendelea - Utawala wa Kitaifa na Maendeleo, ilihimiza serikali ziruhusiwe kuongoza majukumu ya kufufua shughuli halisi za uchumi na maendeleo kwa hivi sasa.

16/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Bei za chakula kwenye nchi maskini bado ni za juu sana’ kuhadharisha FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limewasilisha ripoti mpya yenye kuhadharisha ya kuwa bei za chakula za ndani ya nchi, kwenye mataifa kadha yanayoendelea, zimesalia kuwa za juu sana, licha ya kuwa kimataifa bei za chakula, kijumla, zimeteremka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha karibuni, ambapo pia palishuhudiwa mavuno mazuri ya nafaka.

16/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

un flags 012b

Ofisi ya Msemaji wa KM imeripoti kuwa Ban Ki-moon alishtushwa sana na kuhuzunishwa na taarifa alizopokea juu ya mauaji ya Zill-e-Usman, mtumishi raia wa Pakistan mwenye cheo cha juu katika Ofisi ya UM Juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), mauaji yaliotukia kwenye kambi ya wahamiaji ya Katcha Garhi karibu na mji wa Peshawar, Pakistan. Usman alishambuliwa na watu waliojaribu kumteka nyara wakati alipokuwa anatoka kwenye kambi ya wahamiaji. Alipigwa risasi kifuani mara kadha na alifariki baadaye kutokana na majeraha aliopata kwenye tukio hili. Kadhalika, mlinzi wa kambi aliuawa kwenye shambulio, na mfanyakazi mmoja raia wa UM pamoja na mlinzi mwengine walijeruhiwa. KM amelaani vikali shambulio katili hili dhidi ya watumishi wa UM waliojitolea kusimamia misaada ya kiutu kwa umma muhitaji wa Pakistan. Licha ya tukio hili, UM umeripoti utaendelea kuhudumia mahitaji ya idadi kubwa ya waathirika wa maafa Pakistan na kuwanusuru maisha. KM aliwatumia aila zote za waathirika wa tukio hili pamoja na Serikali ya Pakistan mkono wa pole.

16/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

View of the United Nations Building UN Spanish Radio

Upande wa mashtaka, kwenye kesi ya ya mshtakiwa Thomas Lubanga Dyilo, kiongozi wa jeshi la mgambo la JKK (Union of Congolese Patriots) katika jimbo la mashariki la Ituri umeripotiwa kukamilisha kuwasilisha ushahidi wake dhidi ya mtuhumiwa, mbele ya Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) iliopo Hague. Lubanga ni mtuhumiwa wa awali kuwekwa rumande chini ya uangalizi wa mahakama, na kesi yake inawashirikisha, kwa mara ya kwanza katika historia ya sheria ya kimataifa, waathirika wa mashitaka wakati kesi ikiendeshwa, ikijumlisha vile vile watoto wapiganaji. Lubango ameshtakiwa makosa mawili juu ya jinai ya vita: kuandikisha na kuwaunganisha watoto wapiganaji, chini ya umri wa sheria, kwenye jeshi la mgambo la kundi lake, fungu ambalo lilioshiriki kwenye mapigano nchini baina ya Septemba 2000 mpaka Agosti 2003. Mnamo kipindi cha wiki 22, watu 28 walitoa ushahidi – ikijumuisha wataalamu watatu – umma ambao vile vile walidadisiwa na kuhojiwa na mawakiliwanaomtetea mshitakiwa. Takriban mashahidi wote wa upande wa mashitaka walipatiwa ulinzi, pamoja na hifadhi iliowakinga na mashambulio, mathalan, sauti zao zilibadilishwa wakati walipotoa ushahidi na nyuso zao hazikuonyeshwa na walipewa hata majina ya bandia kuficha utambulizi binafsi. Waathirika karibu 100 walishiriki kwenye kesi tangu kuanza kusikilizwa mnamo tarehe 26 Januari (2009).

15/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNOMIG yakamilisha rasmi uhamisho Georgia kufuatia kura ya vito ya Urusi

Shirika la Uangalizi wa Kusimamisha Mapigano katika Georgia (UNOMIG) limeripoti kukamilishwa, kwa leo hii, uhamisho wa waangalizi wote wa kimataifa kutoka nchini humo, kufuatia kura ya vito ya karibuni ya Urusi kwenye Baraza la Usalama, kura ambayo ilipinga rai ya UM kuongeza muda wa operesheni za kusimamia amani kwenye eneo hili.

15/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kijarida cha Benki Kuu ya Dunia chaelezea mwongozo kinga dhidi ya UKIMWI kwa sekta ya usafirishaji Afrika

HIV-AIDS logo

Kitengo cha Benki ya Dunia juu ya Maendeleo ya Sekta ya Usafirishaji katika Afrika imechapisha kijarida chenye jina refu la kichwa kinachosema “Njia za kupata maisha mazuri: Maelezo ya jumla kuhusu majukumu ya miradi ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika sekta ya usafiri na uchukuzi.”

15/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Togo kusaidiwa na Global Fund kupambana na janga la VVU/UKIMWI

Logo of the Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis and Malaria. Global  Fund / Spanish Radio

Taasisi ya Mfuko wa Kimataifa dhidi ya Ukimwi, Kifua Kikuu [TB] na Malaria (Global Fund) imetia sahihi na Togo, maafikiano ya kuipatia msaada wa dola milioni 20 ili kutumiwa mnamo miaka miwili ijayo kuhudumia juhudi za kitaifa kudhibiti maambukizi ya VVU na maradhi ya UKIMWI.

15/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa FAO wanaashiria Benin itajitosheleza mahitaji ya mpunga katika 2011

Wataalamu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) wanaashiria taifa la Benin, katika Afrika Magharibi, kutokana na mradi mpya utakaowasilishwa nchini humo katika miezi ya karibuni, taifa hilo litaweza kuzalisha mavuno ya mpunga kwa kiwango kikubwa kabisa na kupunguza gharama za kuagiza mpunga kutoka nchi za kigeni.

15/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mchango wa NAM ni muhimu kwa suluhu ya kimataifa, asema KM

KM Ban Ki-moon, ambaye hivi sasa yupo Misri, Ijumatano alihutubia Mkutano wa Hadhi ya Juu wa Jumuiya ya Mataifa Yasiofungamana na Madola Makuu (NAM), unaofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh.

15/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Wajumbe watatu wa Tume ya Uchunguzi wa kutafuta ukweli, na kusailia mazingira yaliosababisha mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Benazir Bhutto wanatazamiwa kuwasili Pakistan mnamo siku za karibuni kuenedelza shughuli zao. Tume hii ilianzisha kazi zake rasmi tarehe 01 Julai (2009), na ziara yao Pakistan itakuwa ya awali nchini humo. Madaraka yailiodhaminiwa Tume na Baraza la Usalama, baada ya kushauriana na Serikali ya Pakistan, ni kuchunguza ukweli wa mauaji ya Benazir Bhutto na sio kufanya upelelezi wa uhalifu unaohusikana na kitendo hicho. Jukumu la upelelezi wa uhalifu na kuendesha mashitaka kwa wakosaji ni dhamana ya wenye mamlaka Pakistan. Ripoti ya matokeo ya uchunguzi wa Tume inatarajiwa kukabidhiwa KM katika miezi sita ijayo – mnamo mwisho wa Disemba 2009.

14/07/2009 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ICTR imehukumu kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki Rwanda

Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) leo imemhukumu Tharcisse Renzaho, aliyekuwa kiranja wa Kigali-ville na pia Kanali wa Jeshi la Rwanda katika 1994, adhabu ya kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya halaiki, makosa ya vita na uhalifu dhidi ya utu.

14/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani ya chakula ndio msingi wa usalama wa dunia:IFAD

Kanayo Nwanze, Raisi wa Taasisi ya UM juu ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwenye mahojiano aliofanya na Redio ya UM alisisitiza juu ya umuhimu wa ile rai ya walimwengu kuhakikisha kunakuwepo akiba maridhawa ya chakula duniani.

14/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR ina wasiwasi juu ya madai wanamaji wa Utaliana waliwatendea kusio huruma wahamiaji wa Eritrea

Nembo ya UNHCR

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ameripoti leo hii, kutokea Geneva, ya kuwa watumishi wa UNHCR waliopo Libya, walifanikiwa kufanya mahojiano na watu 82 waliozuiliwa karibuni na manowari za Utaliana, kwenye eneo la bahari kuu liliopo maili za bahari 30 kutoka kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa.

14/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwezo wa kufanyiza dawa ya chanjo dhidi ya A(H1N1) ni mdogo, ahadharisha mkuu wa WHO

Imeripotiwa na UM kwamba uwezo uliopo sasa wa kutengeneza chanjo kinga dhidi ya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1) ni mdogo na hautoweza kukidhi mahitaji ya watu bilioni 6.8 waliopo ulimwenguni sasa hivi, idadi ambayo inakabiliwa na uwezo wa kuambukizwa kirahisi na kuathirika na virusi vipya hatari vya homa hiyo.

14/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Ad Melkert, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Iraq ameripoti kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulio ya karibuni nchini, ambapo Wakristo walio wachache walihujumiwa pamoja na taasisi zao za kidini na makundi yasiotambulikana. Alieleza hisia hizo baada ya makanisa kadha kushambuliwa Ijumapili katika miji ya Baghdad na Mosul, mashambulio yaliosababisha vifo vya watu wanne na darzeni za majeruhi. Melkert alisema “kampeni hii ya vurugu imekusudiwa kupalilia vitisho miongoni mwa makundi yalio dhaifu, na kwa lengo la kuzuia watu wa dini tofauti kuishi pamoja kwa amani, kwenye moja ya eneo maarufu miongoni mwa chimbuko kuu la kimataifa lenye kujumlisha anuwai za kidini na kikabila. Melkert alitoa mwito uyatakayo makundi husika yote, ikijumlisha Serikali ya Iraq, kuongeza mara mbili zaidi jitihadi zao za kuwapatia wazalendo walio wachache ndani ya nchi, hifadhi kinga na kuimarisha anuwai ya kidini, kikabila na kitamaduni iliopo katika Iraq kwa karne kadha wa kadha.

13/07/2009 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kesi ya Charles Taylor yaanza rasmi Hague

Mawakili wa utetezi wa mtuhumiwa Charles Taylor, aliyekuwa raisi wa Liberia, wameanza kumtetetea mshitakiwa hii leo mjini Hague, Uholanzi kwa kusisitiza mtuhumiwa hajahusika na mauaji yalioendelezwa na waasi wa Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshtadi nchini mika ya nyuma, na wala hajahusika na vitendo vya kujamii kimabavu raia au kulemaza watu wasio hatia.

13/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM kuanzisha Kituo cha Isange kuhudumia waathirika wa mabavu Rwanda

Russian Radio

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Wanawake (UNIFEM) limeripoti kutiwa sahihi maafikiano ya pamoja, kati ya mashirika ya UM na Serikali ya Rwanda, ya kuanzisha kituo maalumu cha kuwahudumia kihali na kiakili wale wanawake na watoto wanaoteswa na vitendo vya kutumia nguvu na mabavu dhidi yao.

13/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya Serikali Usomali vyapatiwa msaada ziada wa walinzi amani wa UA dhidi ya wapiganaji wapinzani

Kadhalika, imeripotiwa walinzi amani wa Umoja wa Afrika waliopo Mogadishu, waliingilia kati, kwa mara ya kwanza, moja kwa moja, mapigano kwa madhumuni ya kuvisaidia vikosi vya Serikali kupambana na makundi ya wapinzani.

13/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe Maalum wa KM kwa Usomali ana matumaini utulivu utarejeshwa nchini karibuni

Ahmedou Ould-Abdallah, Special Representative of the Secretary-General for Somalia

Wiki iliopita Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, Antonio Guterres, alibainisha kwamba tangu mapigano kufumka katika mji wa Mogadishu, mnamo mwanzo wa mwezi Mei, baina ya vikosi vya Serikali na makundi ya upinzani yaliojumuisha majeshi ya mgambo ya Al-Shabab na Hizb-al-Islam, watu 200,000 inaripotiwa walilazimika kuhajiri makazi, kiwango cha uhamaji ambacho kilishuhudiwa kieneo mara ya mwisho katika mwaka 2007, pale vikosi vya Ethiopia vilipoingilia kati, kwa nguvu, mgogoro wa Usomali.

13/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Siku ya Udhibiti wa Idadi ya Watu Duniani itaadhimishwa rasmi mwaka huu na UM mnamo Ijumamosi ya tarehe 11 Julai 2009; na mada ya safari hii inasema “Tuwekeze mchango wa maendeleo kwa masilahi ya wanawake na watoto wa kike.” UM unaamini uwekezaji miongoni mwa watoto wa kike na wanawake, utakaowapatia fursa ya kipato utawafanya kuwa raia wenye uwezo na madaraka ya kuzalisha matunda yatakayochangisha pakubwa kwenye zile juhudi za kitaifa katika kufufua na kukuza uchumi wa kizalendo. Kadhalika utasaidia kuwapatia watoto wao wa kike ilimu yenye natija kimaendeleo, na kuwapa taarifa kinga juu ya afya bora, uzazi wa mpangilio na madaraka ya uhuru wa kujiamulia kimaisha.

10/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Janga la chakula laikabili Sudan Kusini, inahadharisha UNMIS

UNMIS. UN Photo/Fred Noy-UN Spanish Radio

David Gressly, Mratibu wa misaada ya kiutu kwa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS) ameripoti wiki hii ya kuwa Sudan Kusini inakabiliwa na hatari ya kuzuka janga kuu la chakula, kwa mwaka huu, kwa sababu ya mvua haba ilionyesha katika majimbo kadha, na vile vile kutokana na ukosefu wa usalama, hali ambayo ilisambaratisha sana shughuli za kilimo, katika mazingira ambayo mioundombinu dhaifu iliopo nchini imezorotisha zaidi zile shughuli za mashirika ya kimataifa za kugawa misaada ya kiutu ya kunusuru maisha kwa umma muhitaji wa eneo hilo.

10/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa G-8 wameahidi msaada wa kilimo wa $20 bilioni kwa nchi masikini

Viongozi wa Kundi la G-8 waliokutana kwenye mji wa L’Aquila, Utaliana kabla ya kuhitimisha kikao chao waliahidi kuchangisha dola bilioni 20 za kuzisaidia nchi masikini kuhudumia kilimo, ili waweze kujitegemee chakula kitaifa badala ya kutegemea misaada ya kutoka nchi za kigeni, hali ambayo ikidumishwa itasaidia kukomesha duru la umaskini na hali duni.

10/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF inajumuika na mashirika ya kiraia kuhudumia waathirika wa mapigano ya Mogadishu

Nembo ya UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza kujumuika na shirika la Denmark, lenye kuhudumia wahamiaji (DRC) na pia shirika la kizalendo linalohusika na huduma za amani Usomali, SYPD, kwenye shughuli za kusaidia kaya 6,000, sawa na watu 47,000 walioangamizwa katika eneo la Mogadishu.

10/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu anaamini makosa ya vita yamefanyika Usomali

Kamishan Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ameripoti Ijumaa kwamba ana ushahidi thabiti wenye kuonyesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ulifanyika katika mapigano ya karibuni kwenye mji wa Mogadishu, ambapo pia sheria ya kiutu ya kimataifa iliharamishwa kutokana na vitendo ambavyo anavitafsiri kisheria kuwa ni “makosa ya jinai ya vita”.

10/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano ya kikabila Sudan Kusini yawalenga wanawake na watoto wasiohatia

Mapigano ya kikabila, yaliosajiliwa kupamba hivi karibuni katika Sudan Kusini, yalionyesha kulenga mashambulio yake zaidi dhidi ya fungu la umma ambao hauhusikani kamwe na mvutano huo, yaani wanawake na watoto wadogo, kwa mujibu wa taarifa iliotangazwa wiki hii na Joseph Contreras, Naibu Ofisa wa Habari kwa Umma wa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan Kusini (UNMIS).

10/07/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN flag; Iraq

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana lilimaliza Mkutano wa Dunia juu ya Iimu ya Juu uliofanyika Paris, ambapo kulitolewa mwito maalumu unaozitaka nchi wanachama kuongeza mchango wao katika juhudi za kukuza ilimu. Kwenye taarifa rasmi ya mkutano, wajumbe waliowakilisha nchi 150 walitilia mkazo umuhimu wa kuwekeza posho ya bajeti lao kwenye sekta ya ilimu, ili kujenga jamii yenye maarifa anuwai, na inayomhusisha kila raia, ambaye atapatiwa fursa sawa ya kushiriki kwenye tafiti za hali ya juu, huduma itakayowakilisha uvumbuzi na ubunifu wenye natija kwa umma.

09/07/2009 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ITU itashirikiana na Qualcomm kuimarisha mawasiliano ya dharura

Teknolojia

Shirika la UM juu ya Mawasiliano ya Kisasa (ITU) limetangaza kwamba litashirikiana na kampuni ya Qualcomm, inayotumia aina ya kisasa ya mawasiliano ya simu bila waya ili kudhibiti vyema huduma za kihali kwenye maafa.

09/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara ya silaha ndogo ndogo imeongezeka maradufu ulimwenguni katika 2009, inasema ripoti

Toleo la 2009 la Ripoti ya Uchunguzi juu ya Silaha Ndogo Ndogo Kimataifa limethibitisha biashara ya silaha hizi, pamoja na ile ya silaha nyepesi, iliongezeka kwa asilimia 28 ulimwenguni katika kipindi cha baina ya miaka ya 2000 mpaka 2006.

09/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kofi Annan ameikabidhi ICC bahasha ya ushahidi juu ya fujo Kenya kufuatia uchaguzi

Luis Moreno OCampo

Luis Moreno Ocampo, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya UM juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) leo amepokea kutoka Kofi Annan, Mwenyekiti wa Tume ya UA ya Watu Mashuhuri wa KiAfrika, bahasha iliofungwa yenye ushahidi kuhusu wazalendo waliohusika na vurugu liliofumka Kenya mnamo mwisho wa 2007 na mwanzo wa 2008, kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo.

09/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usomali inazingatiwa tena na Baraza la Usalama

B. Lynn Pascoe, Under-Secretary-General for Political Affairs at stakeout. UN Photo/Evan Schneider-UN Spanish Radio

Asubuhi Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao cha hadhara kusailia hali, kijumla, katika Usomali hususan shughuli za kulinda amani za AMISOM.

09/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM amehadharisha viongozi wa G-8 kwamba uamuzi wao wa kupunguza hewa chafu hauridhishi

KM Ban Ki-moon Alkhamisi ya leo alihutubia kikao maalumu, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Viongozi wa Mataifa Yenye Uchumi Mkuu wa Kundi la G-8, unaofanyika kwenye mji wa L’Aquila, Utaliana.

09/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM-UA kuanzisha programu ya kufuatilia mtiririko wa vitegauchumi Afrika kuwasaidia wafanyabiashara

Chinese Unit

UM na Umoja wa Afrika (UA) leo wameanzisha chombo kipya chenye madhumuni ya kusaidia kupanga ratiba ya kufuatilia mtiririko wa vitegauchumi katika Afrika, na kuwapatia wafanyabiashara taarifa thabiti wanazohitajia kufanya maamuzi imara juu ya shughuli zao.

09/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Vikosi vya Ulinzi Amani vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) vimeripotiwa wiki hii kugawa misaada ya chakula kwenye kambi ya wahamiaji wa ndani ya Dereige, msaada ambao utawahudumia chakula fungu kubwa la wahamiaji muhitaji wa kike na watoto wadogo waliopo kambini humo. Vikosi vyaUNAMID pia viligawa vifaa vya ilimu vitakavyotumiwa na watoto mayatima wa kambi hiyo. Hali ya usalama katika Darfur, kwa ujumla, inaripotiwa sasa kuwa ni ya shwari.

08/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya KM imethibitisha kukithiri ukiukaji wa haki za binadamu katika JKK

Ripoti mpya ya KM juu ya shughuli za Shirika la Ulinzi Amani la UM katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) imeeleza hali ya amani nchini humo, kwa ujumla, inakabiliwa bado na vizingiti kadha wa kadha.

08/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO latangaza umuhimu wa kuwepo mtandao wa kupambana na maradhi yasioambukiza

090527-oms-asturias

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kwamba licha ya kuwa maradhi yasioambukiza – kama ugonjwa wa moyo, kiharusi, saratani, kisukari, pamoja na magonjwa ya pumu na yale majeraha ya kikawaida – ndio maradhi yenye kujumlisha idadi kubwa ya vifo ulimwenguni, hata hivyo, wahisani na mashirika ya kimataifa bado wanashindwa kuyapa maradhi haya umuhimu yanayostahiki na kuyafungamanisha na zile sera zinazoambatana na miradi ya kukuza maendeleo.

08/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 2.3 wenye VVU wafaidika na msaada wa ‘Global Fund’ wa dawa ya kurefusha maisha

Child Aids.

Taasisi ya Mfuko wa Kimataifa Dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria – inayoungwa mkono na UM – yaani Taasisi ya Global Fund, imetangaza leo watu milioni 2.3 walioambukizwa na virusi vya UKIMWI ulimwenguni walifanikiwa kupatiwa ile dawa ya kurefusha maisha ya ARV, kutokana na miradi inayosimamiwa na Taasisi ya Global Fund. Muongezeko huu unawakilisha asilimia 31 ya watu waliohudumiwa tiba hiyo, tukilinganisha na takwimu za mwaka jana.

08/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sera za uwekezaji kwenye nchi za G-20 zaonyesha kinaa

Nembo ya UNCTAD

Ripoti ya mapitio ya Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD), juu ya uwekezaji katika vitega uchumi wa kitaifa na kimataifa, imeeleza uchunguzi wao umebainisha zile nchi wanachama wa kundi la G-20 zimejizuia, kwa sasa, kuchukua hatua za dharura kudhibiti uwekezaji ndani ya nchi na katika mataifa ya nje, licha ya kuwa ulimwengu, kwa ujumla, unakabiliwa na mizozo aina kwa aina ya kiuchumi na kifedha.

08/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Said Djinnit, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Afrika Magharibi aliwasilisha ripoti mpya ya KM mbele ya kikao cha hadhara cha Baraza la Usalama, iliosailia umuhimu wa kupungua kwa hali ya vurugu na fujo kieneo. Alisema licha ya kuwa Afrika Magharibi imeonyesha maendeleo katika kurudisha utulivu na amani, hata hivyo, alitahadharisha, hali huko bado ni ya wasiwasi mkubwa. Alieleza kuna sanjari ya mambo kadha yenye uwezo wa kuzusha mtafaruku na kukoroga mazingira ya amani kwenye eneo hilo, mathalan, vitendo vya ugaidi, utawala ulioregarega, biashara ya magendo ya madawa ya kulevya na vile vile uhalifu wa mipangilio. Baada ya hapo wajumbe wa Baraza la Usalama walikutana kwenye mashauriano ya faragha kuzingatia hali katika Afrika Magharibi.

07/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

DPRK imeshtumiwa na BU kwa kufanya majaribio ya makombora

Ijumatatu magharibi Baraza la Usalama (BU) lilitoa taarifa maalumu kwa waandishi habari wa kimataifa, ilioshtumu majaribio ya makombora yalioendelezwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea/Korea ya Kaskazini (DPRK) mnamo mwisho wa wiki iliopita, hali ambayo Baraza linaamini iliharamisha maazimio ya jamii ya kimataifa, na kuhatarisha usalama wa eneo pamoja na utulivu wa kimataifa.

07/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna wa Haki za Binadamu ameshtushwa na idadi ya majeruhi na maututi katika Xinjiang

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amenakiliwa Ijumanne akieleza kuwa ameshtushwa sana na idadi kubwa ya majeruhi na mauaji yaliotukia mwisho wa wiki iliopita, kutokana na fujo zilizofumka katika eneo la Urumqi, mji mkuu wa Jimbo la Uchina Linalojitawala la Xinjiang.

07/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano ya karibuni Mogadisho yawaong’olesha makazi 200,000 ziada, imeripoti UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti, kwa kupitia msemaji wake aliopo Geneva, kwamba muongezeko wa mapigano yaliovuma karibuni kwenye mji wa Usomali, wa Mogadishu, ni hali iliozusha athari mbaya kabisa kwa wakazi waliolazimika kuhama mastakimu yao, na kuleta usumbufu mkubwa kwa raia wa kawaida.

07/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwendesha Mashitaka wa ICC aitaka korti ya rufaa iruhusu kukamatwa raisi wa Sudan

Ocampo na Al-Bashir

Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) ameripotiwa kutangaza kwamba ana ushahidi ziada, utakaomwezesha ofisi yake kutoa hati ya kukamatwa kwa Raisi Omar Al-Bashir wa Sudan, kwa madai alihusika na mauaji ya halaiki nchini kwao.

07/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

KM ameeleza Ijumatatu, kwenye mazungumzo aliokuwa nayo na waandishi habari Geneva, kwamba alihuzunishwa sana, binafsi, na tukio liliosababisha watu kupoteza maisha wakati wanaandamanaji katika Honduras waliposhiriki kwenye mdhahara wa kumuunga mkono Raisi José Manuel Zelaya Rosales ambaye aliondoshwa madarakani kimabavu na wanajeshi katika wiki za karibuni. KM alisema raia, kokote walipo ulimwenguni, wana haki ya kutoa maoni hadharani na uhuru wa kusema, bila ya kukhofia vitisho wala hujuma za kimabavu kutoka kwa wenye mamlaka. Alisisitiza, mabadiliko yeyote ya utawala, yasiolingana na katiba, hayakubaliki katu na jumuiya ya kimataifa na hayana uhalali katika sheria za kimataifa.

06/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Taarifa mpya ya homa ya mafua ya A(H1N1) – Rakamu ya 58

Taarifa mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1), yenye rakamu ya 58, iliotolewa Ijumatatu, tarehe 06 Julai 2009, imeeleza watu zaidi ya 94,000 walisajiliwa rasmi kuambukizwa na maradhi haya ulimwenguni, na kusababisha vifo 400 ziada.

06/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamisheni ya CAC inazingatia mabadiliko ya kudhibiti kemikali zinazodhuru kwenye chakula

Kamisheni iliobuniwa bia na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), yaani Kamisheni ya CAC (the Codex Alimentarius Commission) kutathminia vipimo juu ya usalama wa vyakula, imetangaza vipimo 30 vipya vitakavyotumiwa kimataifa kuongoza ukaguzi juu ya usalama wa chakula duniani.

06/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matatizo ya uchumi duniani hozorotisha juhudi za kuzuwia na kutibu VVU katika nchi masikini

Tukiendelea na ripoti nyengine juu ya masuala ya uchumi wa kimataifa, Benki Kuu ya Dunia na Jumuiya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) leo yamewasilisha ripoti ya pamoja, yenye kuthibitisha nchi 22 katika Afrika, na kwenye maeneo ya Karibian, Ulaya na Asia ya Kati pamoja na zile sehemu za Asia na Pasifiki, yatakabiliwa na misukosuko na vizingiti kadha wa kadha kwenye utekelezaji wa majukumu yanayohusu miradi ya kutibu na kuzuia maambukizi ya VVU kwa mwaka huu, kwa sababu ya mizozo ya uchumi iliopamba duniani.

06/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM awahimiza wajumbe wa Kundi la G-8 kuharakisha misaada, hasa kwa Afrika

Kadhalika, kwenye hotuba aliotoa Ijumatatu, mbele ya wawakilishi wa Vyeo vya Juu, waliohudhuria Mkutano wa Baraza la UM juu ya Uchumi na Jamii (ECOSOC) Geneva, KM alizisihi nchi wanachama wa jumuiya ya mataifa yenye maendeleo ya viwandani, wa Kundi la G-8, kuhakarisha misaada walioahidi kuzipatia nchi masikini kwa mwaka ujao, hasa nchi za Afrika.

06/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UM inasema, mafanikio ya karibuni kufyeka njaa na umaskini yanahatarishwa na mizozo ya chakula na uchumi

UN Millennium Development Goals

“Ripoti ya UM juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs)” kwa mwaka huu, ilowasilishwa rasmi Geneva hii leo na KM Ban Ki-moon, ilitahadharisha ya kuwa mzoroto/mdodoro wa uchumi uliojiri ulimwenguni sasa hivi, na vile vile bei ya juu ya chakula ilioselelea kimataifa katika 2008, ni matukio yaliojumuika kurudisha nyuma yale maendeleo yaliopatikana miaka 20 iliopita ya kupunguza umaskini katika dunia.

06/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yafadhilia utafiti wa athari za KiIslam kwenye sheria ya hifadhi ya wahamiaji

Profesa Ahmed Abu al-Wafa, mtaalamu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Cairo, ameandika kitabu chenye jina lisemalo “Utafiti wa Kulinganisha: Haki ya Kupata Hifadhi na Usalama Baina ya Shari’ah ya KiIslam na Sheria ya Kimataifa ya Wahamiaji”.

03/07/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Raisi mstaafu wa Marekani Bill Clinton, Ijumatatu, tarehe 06 Julai atafanya ziara ya awali katika Haiti, kama Mjumbe Maalumu wa KM kwa taifa hilo. Atakapokuwepo Haiti atakutana kwa mashauriano na maofisa wa Serikali juu ya namna ya kulisaidia taifa kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na matatizo ya vimbunga, kuzalisha ajira mpya na kuimarisha huduma za kimsingi za jamii. Clinton pia atajadilia taratibu za kufungamanisha shughuli za UM, jumuiya za kiraia na jamii ya wafadhili wa misaada ya maendeleo na miradi ya Serikali katika kufufua huduma za uchumi na jamii.

02/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misri kutangaza itafungua mipaka na Ghaza mara tatu kwa mwezi kuhudumia misaada ya kiutu

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Mkuu wa serikali ya utawala wa Tarafa ya Ghaza, anayehusika na masuala ya mipaki, Ghazi Hamad, aliripoti kuwa wenye madaraka Misri wamearifu rasmi kuwa na sera mpya juu ya kivuko cha Rafah, mpakani baina ya Misri na Tarafa ya Ghaza.

02/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi wa haki za Wafalastina ashtumu utekaji nyara wa wanamaji wa Israel dhidi ya meli ya wahisani wa kimataifa

Richard Falk, Mkariri/Mtaalamu Maalumu wa UM juu ya haki za binadamu kwenye maeneo ya WaFalastina, yaliokaliwa kimabavu na Israel tangu 1967, amelaumu utekaji nyara, haramu, ulioendelezwa wiki hii na manowari za Israel, kwenye bahari kuu, dhidi ya ile meli ndogo ya wanaharakati wa amani, iliokuwa imechukua shehena ya madawa na vifaa vya ujenzi kwa umma wa Tarafa ya Ghaza.

02/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA imeteua Mkurugenzi Mkuu mpya

Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) lenye wajumbe 35, ambalo linakutana hivi sasa kwenye mji wa Vienna, Austria leo limemteua Balozi Yukiya Amano wa Ujapani kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa taasisi hii ya kimataifa.

02/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

DPRK imefyatua makombora, na kutotii mapendekezo ya BU

UM umepokea taarifa zenye kueleza kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea/Korea ya Kaskazini (DPRK) mnamo saa za magharibi kwa majira ya eneo, Alkhamisi ya leo, ilirusha makombora ya masafa madogo, yaliotambuliwa kuwa ya aina ya makombora yanayotumiwa kupiga vyombo vya baharini.

02/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

KM Ban Ki-moon ambaye yupo Ujapani kwa hivi sasa, Ijumatano alikutana kwa mazungumzo na viongozi wa taifa hilo, ikijumlisha Waziri Mkuu Taro Aso, na walisailia mwelekeo wa kufuatwa na jumuiya ya kimataifa ili “kukamilisha makubaliano yanayoridhisha” kwenye mkutano ujao wa Copenhagen juu ya udhibiti bora wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Vile vile walishauriana juu ya masuala yanayoambatana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (DPRK), Myanmar, mchango wa Ujapani katika kuendesha shughuli mbalimbali za UM, hasa katika operesheni za kulinda amani, na pia kuzungumzia taratibu za kufuatwa na wafanya biashara zitakazohakikisha kunakuwepo maendeleo yanayosarifika. Alkhamisi KM ataelekea Singapore kabla ya kwenda Myanmar Ijumaa.

01/07/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjumbe Maalumu wa Maziwa Makuu hakuridhika na maendeleo ya kurudisha amani

Cameroon-Nigeria Leaders Meet in New York  Nigerian President Olusegun Obasanjo (left) and his Cameroonian counterpart Paul Biya greet each other at the start of the meeting of the Cameroon-Nigeria Mixed Commission in Greentree, Long Island in New York,

Mjumbe Maalumu wa UM juu ya Masuala ya Maziwa Makuu, Olusegun Obasanjoaliyekuwa raisi wa zamani wa Nigeria, ambaye anazuru Mako Makuu kushauriana na wakuu wa UM kuhusu hali ya eneo, aliwaambia waandishi habari Ijumanne kwamba maendeleo ya kurudisha utulivu na amani katika eneo la vurugu, la mashariki katika JKK yanajikokota, hasa kwenye zile juhudi za kukomesha uhasama baina ya makundi ya waasi na vikosi vya Serikali.

01/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chanjo ya TB kwa watoto wachanga wenye VVU inadhuru, kuonya wataalamu Afrika Kusini

who-logo

Uchunguzi wa wataalamu wa Afrika Kusini, ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la afya la Shirika la Afya Duniani (WHO) umethibitisha kwamba ile chanjo kinga dhidi ya kifua kikuu (TB), ambayo kikawaida hupewa asilimia 75 ya watoto wachanga ulimwenguni, baada ya kuzaliwa, inakhofiwa dawa hii huleta madhara kwa watoto walioambukizwa na virusi vya UKIMWI na husababisha hata vifo.

01/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahisani wahimizwa na UNCTAD kutekeleza ahadi za kuimarisha kilimo Afrika

UNCTAD logo UNCTAD/UN Radio Spanish

Kwenye kikao cha Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) kilichofanyika Ijumanne Geneva kuzingatia mzozo wa chakula katika Afrika, wahisani wa kimataifa walihimizwa kutekeleza haraka ahadi walizotoa siku za nyuma kuimarisha kilimo bora barani humo.

01/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza kuu lapitisha azimio linalolaani vikali mapinduzi ya Honduras

Ijumanne alasiri Baraza Kuu la UM lilipitisha azimio liliolaani vikali mapinduzi haramu ya serikali yaliofanyika Honduras, taifa liliopo Amerika ya Kati.

01/07/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930