Nyumbani » 30/06/2009 Entries posted on “Juni, 2009”

Hapa na pale

Vikosi vya Uangalizi vya UM katika Georgia (UNOMIG) vimesitisha rasmi shughuli zao kuanzia tarehe 16 Juni 2009, baada ya Baraza la Usalama liliposhindwa kupitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni hizo. Wanajeshi wa UNOMIG wameshaanza kuondoka Georgia kwa hivi sasa. Taarifa ya KM iliyashukuru makundi husika kwa ushirikiano wao na vikosi vya UNOMIG tangu pale vilipoanza operesheni zake katika 1993. KM alisema UM upo tayari kutumika kwenye shughuli nyenginezo za kuimarisha amani katika Georgia. Kwa kulingana na pendekzo hilo KM amemtaka Mjumbe Maalumu wake anayehusika na UNOMIG, Johan Verbeke kuendelea kuiwakilisha UM kwenye majadiliano ya Geneva yanayozingatia usalama na ututlivu wa eneo husika, mazungumzo yanayozingatia pia suala la kuwarudisha makwao wahamiaji waliopo nje na wale wa ndani ya nchi.

30/06/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mataifa yanajiandaa kubuni mfumo mpya wa kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa

Mkutano wa Tatu wa Dunia juu ya Udhibiti Bora wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (WCC-3) unatarajiwa kufanyika Geneva, Uswiss kuanzia tarehe 31 Agosti hadi Septemba 04, 2009.

30/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tiba ya majaribio dhidi ya usubi imeanzishwa rasmi katika nchi tatu za Afrika, imeripoti WHO

river blindness 06a

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuanzisha majaribio ya tiba mpya dhidi ya maambukizi ya maradhi ya usubi, katika mataifa matatu ya Afrika – yakijumlisha Ghana, Liberia na JKK.

30/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uamuzi wa Tanzania kuongeza muda wa makazi kwa Waburundi wapongezwa na UNHCR

Nemba ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limekaribisha uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kuruhusu muda zaidi wa kukaa nchini, kwa baadhi ya wahamiaji wa Burundi 36,000 wanaotaka kurejea makwao, kwa khiyari, kutoka kambi ya Mtabila iliopo wilaya ya Kasulu, kaskazini-magharibi katika Tanzania, kambi ambayo ilipangwa kufungwa mnamo tarehe 30 Juni 2009.

30/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA imeripoti 170,000 wahajiri Mogadishu kufuatia mfumko mpya wa mapigano

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mapigano yalifumka tena katika wilaya za Mogadishu za Karaan na Hodan mnamo mwisho wa wiki iliopita.

30/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

KM anatarajiwa kuzuru rasmi Myanmar kuanzia tarehe 03 – 04 Julai, kwa kuitika ombi la Serikali. Atakapokuwepo huko atakutana, kwa mashauriano ya ana kwa ana, na viongozi wakuu wa Serikali ambapo wanatarajiwa kuzungumzia masuala kadha yenye umuhimu kwa UM na jamii ya kimataifa. Alitilia mkazo kwenye mazungumzo yao mambo matatu yatapewa umuhimu wa hadhi ya juu, kwa kulingana na hali ya kisiasa ilivyo nchini kwa hivi sasa. Masuala hayo yanahusu, awali, kuachiwa wafungwa wote wa kisiasa, ikijumlisha Daw Aung Suu Kyi; kurudisha mazungumzo ya upatanishi kati ya Serikali na Wapinzani; na kusailia maandalizi ya uchaguzi wa taifa ulio huru na wa haki.

29/06/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

KM ameingiwa wasiwasi juu ya mripuko wa vurugu Honduras

KM Ban Ki-moon ametangaza taarifa ilioelezea kuwa na wasiwasi kuhusu mtafaruku uliozuka katika taifa la Honduras, la Amerika ya Kati ambapo inasemekana Raisi José Manuel Zelaya Rosales aliondoshwa madarakani kwa nguvu majuzi.

29/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bodi la Utawala UNCTAD kutathminia ufufuaji wa kilimo Afrika

UNCTAD logo UNCTAD/UN Radio Spanish

Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) linatarajiwa Ijumanne jioni kukutana Geneva, kufanya tathmini kuhusu juhudi za kufufua kilimo katika bara la Afrika, huduma ambazo zimezorota katikati ya kipindi kilichopambwa na athari haribifu zilizoletwa na mizozo ya uchumi dhaifu kwenye soko la kimataifa.

29/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Kundi la Kazi la UM kwa waliopotezwa na kutoweka wahitimisha kikao cha 88 Rabat

Forced disappearances

Wajumbe wa Kundi la Kufanya Kazi la UM juu ya Watu Waliolazimishwa Kupotea na Kutoweka baada ya kukukamilisha ziara yao ya siku nne katika Morocco walikutana kwenye mji wa Rabat na kukamilisha kikao cha 88 kilichofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Juni walipozingatia masuala yanayohusika na watu kukamatwa kimabavu na kutoweka wasijulikane walipo.

29/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICRC inasema miezi sita baada ya mashambulio ya Israel Ghaza inaendelea kusumbuka na kuteseka kimaisha

Ripoti mpya ya Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) iliotangazwa hii leo, inaeleza ya kuwa umma wa eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza, unaendelea kusumbuka na kuteseka kimaisha, miezi sita baada ya operesheni za kijeshi za Israel kuendelezwa dhidi ya eneo hili la Mashariki ya Kati.

29/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa UM umepitisha ratiba mpya kupunguza athari za miporomoko ya uchumi duniani

Wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mzozo wa Uchumi na Fedha Duniani na Athari zake kwa Maendeleo, wameafikiana Ijumaa ratiba mpya ya mpango wa utendaji, utakaotumiwa na Mataifa Wanachama kipamoja, kupunguza makali na kasi ya miporomoko ya uchumi katika nchi zinazoendelea.

29/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

KM alikutana na viongozi wa kundi la Wapatanishi wa Pande Nne juu ya Mashariki ya Kati kwenye mji wa Trieste, Utaliana na walizingatia masuala matano muhimu: mwelekeo unaofaa kuchukuliwa kufufua majadiliano ya amani kati ya Israel na Falastina; kuwasaidia wenye mamlaka wa KiFalastina (PA) kutawala bora kwenye maeneo yao na kukuza uchumi; hali katika Tarafa ya Ghaza; suala la kuleta amani kamili kati ya Israel na Syria, na Israel na Lebanon; na kusailia Mkutano Mkuu wa Moscow utakaofanyika baadaye kutathminia uwezekano wa kurudisha amani katika Mashariki ya Kati.

26/06/2009 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya Ushikamano wa Kimataifa na Walioathirika Mateso

Tarehe ya leo, 26 Julai, inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Ushikamano Kimataifa na Wathirika wa Mateso.

26/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WTO/UNEP yametoa ripoti inayothibitisha fungamano hakika kati ya biashara na mabadiliko ya hali ya hewa

OMT Logo Organizacion Mundial Turismo / World Tourism Organization UNWTO OMT / Spanish Radio

Shirika la Biashara Duniani (WTO) na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) yametangaza bia ripoti mpya yenye kuelezea, kwa mara ya kwanza, fungamano ziliopo baina ya biashara ya kimataifa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

26/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hifadhi bora kwa raia walionaswa kwenye mapigano inazingatiwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limefanyisha kikao cha hadhara Ijumaa kuzingatia ulinzi wa raia kwenye mazingira ya mapigano na vurugu.

26/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa waliong’olewa makazi Usomali waendelea

Vile vile kuhusu Usomali, Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuwa na wasiwasi juu ya athari kwa umma, kuokana na mripuko wa mapigano yaliosababisha mzozo mkubwa wa watu kung’olewa makazi kujiri kwa hivi sasa katika Usomali.

26/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mfuko wa CERF kuifadhilia IOM msaada wa kuhudumia makazi ya muda wahamiaji wa Usomali

IOM Bus

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti kuwa litapokea msaada wa dola milioni 2.6 kutoka Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF, fedha zitakazotumiwa kuwasaidia kupata makazi ya dharura wahamiaji 12,700 wa Usomali ambao wanabanana hivi sasa kwenye kambi za Kakuma, ziliopo Dadaab, kwenye jimbo la kaskazini-mashariki ya Kenya.

26/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mzozo wa Fedha Duniani watia kikomo

Mkutano Mkuu juu ya Mzozo wa Uchumi na Fedha Duniani na Athari Zake Kwa Maendeleo umekamilisha majadiliano Ijumaa alasiri.

26/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNCTAD azingatia suluhu ya kukabiliana na matatizo ya uchumi na kifedha kwa Afrika

Takwimu za UM zimethibitisha kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya umma wa Afrika, bado unaishi katika hali ambayo matumizi ya kukidhi mahitaji ya kimaisha, kwa siku, ni chini ya dola moja.

26/06/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

View of the United Nations Building UN Spanish Radio

Tume ya Umoja wa Afrika (UA) kwa Darfur, inayoongozwa na Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki imeripotiwa kukamilisha vikao vya siku 10, kusikiliza kauli za umma, ili kutafuta njia za kuharakisha suluhu ya mpango wa amani katika Darfur na kuandaa mazingira ya kuleta upatanishi miongoni mwa makundi yanayohasimiana na pia haki katika Darfur. Wajumbe wa Tume walikutana na wawakilishi wa vyama vya kisiasa, jumuiya za kiraia, makundi ya waasi, makundi ya kikabila na pia makundi ya wahamiaji wa ndani waliong’olewa makazi katika Khartoum na kutoka miji sita ya jimbo la Darfur. Taarifa hii ilitolewa na Shirika la Mchanganyiko la UM-UA kwa Darfur (UNAMID).

25/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano ya kikabila Kenya yamesababisha maelfu ya wakuria kung’olewa makazi

Shirika la UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) limetangaza kupamba hali ya wasiwasi mkuu kwenye wilaya ya Kenya ya Kuria Mashariki, karibu na mpaka na Tanzania, ambapo majuzi watu 6,000 waling’olewa makazi kwa sababu ya mapigano yaliozuka miongoni mwa jamii ya makabila ya Kuria.

25/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zimbabwe yashuhudia uzalishaji mkubwa wa kilimo, lakini wasiwasi bado umeselelea juu ya akiba ya chakula

Mashirika mawili ya UM – yaani FAO, linalohusika na chakula na kilimo, pamoja na WFP, linaloshughulikia miradi ya chakula – yamewakilisha bia ripoti ya tathmini halisi juu ya maendeleo ya kilimo katika Zimbabwe.

25/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM wamehadharisha wajumbe wa Kikao cha BK juu ya Mzozo wa Uchumi kutosahau kufungamanisha haki za binadamu kwenye maamuzi yao

Magdalena Sepulveda

Magdalena Sepúlveda na Cephas Lumina, Wataalamu Huru wawili wa UM wanaohusika na masuala ya haki za kibinadamu kwenye mazingira ya umaskini uliovuka mipaka na kuhusu athari haribifu za madeni, wametuma taarifa maalumu kwenye Mkutano wa Baraza Kuu juu ya Mizozo ya Uchumi na Kifedha, iliohimiza Mataifa Wanachama “kuchukua hatua za dharura, zitakazosaidia kuendeleza ufufuaji wa muda mrefu wa shughuli za kiuchumi na fedha, kwa kutunza haki za kimsingi kwa umma mamskini wenye kusumbuliwa zaidi na matatizo haya ya kiuchumi” kwa kupatiwa huduma za jamii.

25/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa BK juu ya Mzozo wa Kifedha na Uchumi Duniani waendela New York

Mkutano Mkuu juu ya Mzozo wa Uchumi na Fedha Duniani na Athari Zake Kwa Maendeleo umeingia siku ya pili Alkhamisi ya leo, ambapo wawakilishi wa kutoka karibu nchi 150 wanaendelea kujadilia uwezekano wa kusuluhisha mizozo hii kwa “maamuzi yatakayokuwa na natija, kwa kiasi kikubwa, na kwa muda mrefu, miongoni mwa umma wa kimataifa.”

25/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Chinese Unit

KM Ban Ki-moon amewatumia viongozi wa Kundi la G-8 barua maalumu, iliyoorodhisha masuala ambayo angelipendelea kuona yanapewa umuhimu kwenye Mkutano Mkuu utakaofanyika mwezi Julai kwenye mji wa l’Aquila, Utaliana. Aliyataka mataifa yenye maendeleo ya viwandani yaahidi kupunguza kwa kiwango cha baina ya asilimia 25 mpaka 40 vitendo vya kumwaga hewa chafu kwenye anga, itakapofika 2020, kama ilivyopendekezwa na Tume ya Kimataifa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (IPCC). Vile vile aliwataka viongozi wa G-8 kuandaa ratiba na utaratibu wa kuchangisha mabilioni ya dola zinazohitajiwa kuyasaidia mataifa dhaifu na masikini kujirekibisha ili kukabiliana na matatizo yaliozushwa na mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka ijayo. Alikumbusha pia kwamba kiwango cha mchango wa kila mwaka unaotakiwa kuyasaidia mataifa ya Afrika kupata uwezo wa kuyakamilisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) kwa wakati, bado ni kidogo sana, chini ya kima cha dola bilioni 20 zilioahidiwa kuchangishwa kwenye Mkutano wa Gleneagles.

24/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa mpya juu ya homa ya mafua ya A(H1N1)

Nembo ya WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) leo limetangaza ripoti mpya kuhusu maambukizi ya homa ya mafua ya
A(H1N1) katika ulimwengu katika kipindi cha sasa.

24/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM amehuzunishwa sana na uvamizi wa kunajisi kimabavu wanawake wafungwa katika JKK

KM Ban Ki-moon ametangaza kuhuzunishwa sana na ripoti alizopokea karibuni, kuhusu tukio la uvamizi na vitendo vya kunajisi kimabavu, wafungwa wanawake 20 waliojaribu majuzi kukimbia kutoka gereza kuu la Goma, liliopo katika eneo la mashariki ndani ya JKK.

24/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Janga la Nzige Wekundu ladhibitiwa Afrika Mashariki: FAO

Juhudi za dharura, zinazoungwa mkono na UM, kudhibiti bora tatizo la kuripuka janga la Nzige Wekundu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimeripotiwa karibuni kufanikiwa kuwanusuru kimaisha mamilioni ya wakulima, baada ya kutumiwa, kwa kiwango kikubwa, ule utaratibu wa kuangamiza kianuwai vijidudu hivi vinavyokiuka mipaka na kuendeleza uharibifu wa kilimo pamoja na kuzusha njaa.

24/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano mkuu wa UM juu ya athari za mizozo ya Uchumi na Kifedha Duniani waanza rasmi makao makuu

Baraza Kuu la UM limeanzisha rasmi, Ijumatano ya leo, Mkutano Muhimu juu ya Mzozo wa Uchumi na Fedha Duniani na Athari Zake Kwenye Huduma za Maendeleo ambao utafanyika kwa siku tatu kwenye Makao Makuu ya UM yaliopo mjini New York.

24/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

KM Ban Ki-moon alitangaza Ijumatatu alasiri taarifa maalumu ilioleza kuwa aliingiwa wasiwasi na fadhaa, juu ya kufumka kwa fujo na vurugu katika Jamhuri ya KiIslam ya Iran, kufuatia uchaguzi wa uraisi ulioendelezwa nchini humo wiki za karibuni.Alisema alishtushwa na matumizi ya nguvu dhidi ya raia, hali ambayo ilizusha vifo na majeruhi kadha. Aliwasihi wenye madaraka kusitisha, halan, vitendo vyote vya kutumia nguvu dhidi ya raia, na kusimamisha vitisho pamoja na kuwashika watu bila hatia. Alitumai “matakwa ya kidemokrasia ya umma wa Iran yatahishimiwa kikamilifu” na wenye mamlaka.

23/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNODC inajiandaa kutangaza ripoti ya 2009 juu ya tatizo la madawa ya kulevya duniani

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) litawakilisha Ijumatano ripoti mpya kuhusu tatizo la madawa ya kulevya ulimwenguni katika 2009.

23/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi kubwa ya wakazi wa eneo la mapigano katika JAK wamehajiri mastakimu: OCHA

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mashambulio yaliotukia Ijumapili alfajiri, tarehe 21 Juni, kwenye mji wa Birao, kaskazini-mashariki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yamesababisha idadi kubwa ya wakaazi kuhama kidharura eneo hilo.

23/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR ina wasiwasi na kunyanyuka kihadhi kwa vyama baguzi vipingavyo wageni katika EU

Musina on the South African border with Zimbabwe. UNHCR/J.Oatway-UN Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetoa mwito maalumu wenye kuisihi Serikali ya Sweden kutumia wadhifa uliokabidhiwa nao sasa hivi, wa uraisi wa Umoja wa Ulaya (EU), kutilia mkazo umuhimu wa nchi wanachama kusimamia shughuli za mipaka yao, kwa kuzitekeleza kanuni za huruma za kuruhusu wahamaji wa kigeni kupata hifadhi, kama ilivyoidhinishwa na haki za kimsingi za kiutu.

23/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi kubwa ya wahamaji wa Usomali na Ethopia wanaotoroshwa Afrika Kusini huteswa na wafanya magendo, inaripoti IOM

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limetoa ripoti mpya kuhusu “uhamaji usio wa kawaida” ambao huwatesa wale watu wanaotoroshwa kimagendo kutoka Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, wanaopelekwa Afrika Kusini.

23/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limepokea rasmi katika wiki iliopita maofisa wapya wa polisi 95 kutoka Gambia – wanaume polisi 92 na askari wanawake watatu, askari ambao wanatarajiwa kuenezwa katika sehemu mbalimbali za Darfur baada ya kumaliza mafunzo ya utambulisho yatakayofanyika kwenye mji wa El Fasher.

22/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UN-HABITAT atunukiwa “Tunzo ya Goteberg”

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT), Anna Tibaijuka, ametangazwa kuwa ni mmoja wa washindi watatu wa Tunzo ya Göteberg, kwa michango yao ya kitaifa na kimataifa, katika maamirisho ya huduma ya maendeleo yanayosarifika.

22/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afya ya wahamiaji dhidi ya UKIMWI inazingatiwa na bodi la UN-AIDS,linalokutana rasmi Geneva

Nembo ya UNAIDS

Bodi la la Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) limeanza rasmi Geneva kikao cha 24, kilichokusudiwa kuzingatia mahitaji ya umma unaohama hama, ukijumuisha wahamaji na wahamiaji wa ndani na nje ya mataifa yao.

22/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICTR imetangaza kifungo cha miaka 30 kwa mtuhumiwa Kalimanzira

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imetangaza hukumu ya kifungo cha miaka 30, kwa Callixte Kalimanzira, aliyekuwa ofisa Mkurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Rwanda katika 1994, ambaye alipatikana na hatia ya jinai ya mauaji ya kuangamiza makabila, na pia makosa ya kuchochea watu kuendeleza mauaji ya halaiki.

22/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO inasema mamilioni ya hekta za savana Afrika zipo tayari kuvuna natija kuu za kibiashara ya kilimo

Ijumatatu Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza kwamba sehemu kubwa ya ardhi ya savanna, iliotanda katika mataifa 25 barani Afrika, pindi itadhibitiwa na shughuli za kiuchumi kama inavyostahiki, itamudu kuzalisha bidhaa za chakula, kwa wingi kabisa, hali ambayo italiingiza eneo miongoni mwa maeneo yatakayoongoza biashara ya bidhaa za kilimo kwenye soko la kimataifa.

22/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya kisayansi kuonya walimwengu, mabadiliko ya hali ya hewa duniani sio mzaha

Wataalamu wa kimataifa wa katika fani ya sayansi, juzi waliwasilisha ripoti mpya yenye kusisitiza kwamba mabadiliko ya hali ya hewa, yalioripotiwa kujiri kimataifa katika miaka ya karibuni, ni matukio hakika kwenye mazingira na sio mnong'ono wala makisio.

22/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limeripoti karibuni limeshuhudia idadi kubwa ya waliokuwa waasi wa Ki-Hutu wa kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) kurejea makwao Rwanda. Wafuasi wa zamani 57 wa kundi la FDLR na wahamiaji wengine 26 waliokuwa wakiishi kwenye eneo la wasiwasi na mapigano la kaskazini-mashariki, katika JKK, walirejea Rwanda, kwa hiyari, wakisaidiwa na UM. Kadhalika, tangu mwanzo wa 2009, watoto wapiganaji wa umri mdogo 1,650 ziada nao pia walihamishwa kutoka majeshi ya mgambo na kurudishwa kwa wazee wao. MONUC ilieleza ya kuwa vikosi vya kulinda amani vya UM vilianzisha utaratibu unaotumia werevu maalumu, unaowawezseha kutoa hadhari ya mapema, na kufuatilia kwa ukaribu zaidi, vitimbi haramu vya makundi yenye silaha yaliopo Kivu Kaskazini, pale wanapoendesha operesheni zao za kijeshi shirika na vikosi vya taifa vya JKK. Operesheni hizi ziliimarishwa zaidi wiki hii baada ya kufunguliwa kituo kingine cha 8 kinachotumiwa kuratibu shughuli zao hizo.

19/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku Kuu ya Wahamiaji Duniani 2009

African refugees return

Ijumamosi ya tarehe 20 Juni 2009, itahishimiwa rasmi na UM kuwa ni 'Siku ya Wahamiaji Duniani’. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Mahitaji Hakika, kwa Umma Halisi”.

19/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Iran inamtia wahka Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amenakiliwa akieleza ya kuwa ameingiwa wahka juu ya ripoti alizipokea zenye kudai wenye madaraka Iran wanatumia nguvu mno kudhibiti vurugu liliozuka nchini kufuatia matokeo ya uchaguzi wa uraisi uliofanyika wiki moja iliopita.

19/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kudhibiti athari za maafa wapendekeza vifo vipunguzwe kwa nusu 2015

isdr-disaster-gde

Mkutano wa Kimataifa Kupunguza Hatari Inayoletwa na Maafa umemalizika mjini Geneva leo Ijumaa, ambapo kulitolewa mwito maalumu unaowataka viongozi wa kisiasa katika Mataifa Wanachama kuchukua hatua za dharura kupunguza, angalaukwa nusu idadi ya vifo vinavyosababishwa na maafa ya kimaumbile itakapofika 2015, .

19/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wenye njaa kukiuka bilioni 1 duniani katika 2009, inasema FAO

Jacques Diouf,

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza jumla ya watu waliopo kwenye ukingo wa kubanwa na matatizo ya njaa ulimwenguni katika 2009, inakaribia watu bilioni 1.02 – sawa na sehemu moja ya sita ya idadi nzima ya watu duniani.

19/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya Waziri wa Usalama Usomali yaichukiza sana jumuiya ya kimataifa

map of Somalia

Waziri wa Usalama wa Usomali, Omar Hashi Aden, aliuawa Alkhamisi wakati akizuru mji wa Beledwenye, uliopo kaskazini ya Mogadishu na baada ya kuhujumiwa na shambulio la bomu la kujitolea mhanga liliogheshwa ndani ya gari moja kubwa.

19/06/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Photo

Alain Le Roy, Naibu KM wa Idara ya Operesheni za Ulinzi Amani za UM (DPKO) amezuru Abuja, Nigeria Alkhamisi ikiwa miongoni mwa maeneo anayozuru katika Afrika Magharibi. Alifanya mazungumzo na maofisa wanaohusika na masuala ya nchi za kigeni, maofisa wanaowakilisha wizara ya ulinzi pamoja na kukutana na Mshauri Mkuu wa Masuala ya Usalama wa Taifa. Vile vile alionana na Rasisi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi wa Mataifa ya Afrika Magharibi, Dktr Mohamed Ibn Chambas.

18/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kilimo hujiokoa zaidi na mizozo ya kiuchumi kushinda sekta nyenginezo, inasema ripoti ya FAO/OECD

Ripoti ya pamoja iliotolewa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), iliowakilishwa rasmi Ijumatano, imeeleza kwamba ilivyokuwa uchumi wa kimataifa hautarajiwi kufufuka na kuota mizizi ya kuridhisha mpaka baada ya miaka miwili/mitatu ijayo, wataalamu wanaashiria mporomoko wa muda wa bei za bidhaa za kilimo kimataifa utakuwa wa wastani.

18/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanariadha wa kimataifa kushiriki kwenye miradi ya kupiga vita njaa ulimwenguni

Jarno Trulli na Timo Glock, madereva wa mashindano ya mbio za gari, wenye kuwakilisha kampuni za Panasonic na Toyota, wanatazamiwa kuvalisha na kupamba gari zao na alama ya kitambulisho ya lile Shirika UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), pale watakaposhiriki kwenye mashindano ya gari Uingereza mnamo Ijumapili ijayo.

18/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mawasiliano ya simu za mikononi yatazamiwa kuhamasisha mapinduzi kwwenye utabiri wa hali ya hewa Afrika

Baraza juu ya Misaada ya Kiutu Duniani, na Raisi wake, KM wa UM mstaafu Kofi Annan, akijumuika na kampuni ya mawasiliano ya Ericsson, Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO), na vile vile kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi, Zain, pamoja na Taasisi ya Huduma za Maendeleo Duniani ya Chuo Kikuu cha Columbia, Marekani wote pamoja wametangaza, leo hii, taarifa ya kufadhilia mradi mkuu, unaojulikana kama “Mradi wa Taarifa za Hali ya Hewa kwa Wote”, ambao ukitekelezwa una matumaini ya kuwasilisha mapinduzi ya kuridhisha katika kuimarisha zaidi uwezo wa kusimamia mtandao wa utabiri wa hali ya hewa, hususan kwenye yale mazingira yanayoendelea kuathiri hali ya hewa barani Afrika.

18/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO-UNICEF yasisitiza jitihadi kuu zahitajika kuhifadhi mahospitali na skuli penye maafa

Mashirika ya UM juu ya afya na maendeleo ya watoto, yaani mashirika ya WHO na UNICEF, yametoa mwito wa pamoja wenye kuzihimiza serikali za kimataifa, kuchukua hatua madhubuti, katika sehemu nne muhimu zinazohitajika kupunguza athari za maafa katika mahospitali na maskuli.

18/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Henry Anyidoho, Naibu Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UM-UA kwa Darfur (UNAMID), Ijumanne alizuru Darfur Magharibi na kukutana na wahamiaji waliorejea makwao vijijini katika siku za karibuni. Wakati huo huo, Tume ya Umoja wa Afrika kwa Darfur, inayoongozwa na Raisi mstaafu wa Afrika Kuisni, Thabo Mbeki, ikijumlisha vile vile waliokuwa viongozi wa mataifa yao – Pierre Buyoya wa Burundi na Abdulsalami Abubakar wa Nigeria – nao pia walizuru Darfur ya Kaskazini na kukutana na makamanda wa tawi liliojitenga la Abdul Wahid kutoka kundi la waasi la SML.

17/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM atoa mwito wa kuzikomesha chuki za kwenye uwanda wa intaneti

Ijumanne, kwa siku nzima mfululizo, Idara ya Habari ya UM kwa Umma (DPI) ilifanyisha warsha maalumu kuzingatia taratibu za kusitisha zile kurasa za mitandao ya kompyuta zenye kuchochea chuki.

17/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yathibitisha kesi kwa aliyekuwa naibu-raisi wa JKK

Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) imethibitisha kuwa kuna ushahidi wa kuridhisha wa kuanzisha kesi ya kumtuhumu Jean-Pierre Bemba Gombo, aliyekuwa naibu-raisi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), kwamba alishiriki kwenye makosa ya vita na jinai iliotengua haki za kiutu.

17/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Dunia Kupiga Vita Kuenea kwa Jangwa

Tangu 1995 UM unaihishimu tarehe 17 Juni, kila mwaka, kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Kuenea Kwa Jangwa. Ripoti za UM juu ya tatizo la kueneza majangwa, kutokana na matumizi badhirifu ya ardhi, inaashiria watu milioni 200 watalazimika kuhama makazi katika mwaka 2050 kutakakosababishwa na mabadiliko ya katika mazingira.

17/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uadui dhidi ya watumikia misaada ya kiutu Usomali wahatarisha maisha ya watoto na wanawake, imehadharisha UNICEF

Kaimu Mwakilishi wa Shirika la UNICEF kwa Usomali, Hannan Sulieman amenakiliwa akisema, kutokea Nairobi, kuwa “ameudhika sana” na kuongezeka kwa mawimbi mapya ya mashambulio, uchokozi na uadui uliotanda siku za karibuni, dhidi ya wafanyakazi wanaohudumia misaada ya kiutu katika Usomali.

17/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Ripoti mpya iliotolewa leo na UM inaeleza kwamba asilimia 30 ya vijana wa Afrika, kati ya umri wa miaka 17 mpaka 25, huogopa kutoa maoni au kujieleza hadharani. Kutokana na bayana hii, Shirika la UNICEF na washiriki wenzi wameamua kupanua zaidi, na kuimarisha ule ukurasa wa jukwaa lao la intaneti/wavuti, wenye mada isemayo “Zungumza kwa Uwazi Afrika”, ulioandaliwa hasa kwa madhumuni ya kuwasaidia vijana wa Afrika kushiriki kwenye majadiliano yenye maana kuhusu masuala muhimu yanayoathiri bara lao.

16/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNIDO na kampuni ya HP wafungua vituo vya mafunzo katika Afrika na Mashariki ya Kati

unido

Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) ikishirikiana na kampuni ya teknolojiya ijulikanayo kama HP, yametangaza kufungua vituo 20 vya mafunzo katika Afrika na Mashariki ya Kati, vitavyotumiwa kuilimisha vijana wa umri wa baina ya miaka 16 mpaka 25, mafunzo yanayohusika na ujasiriamali na teknolojiya ya mawasiliano ya kisasa.

16/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Afya bora ndio msingi wa kufikia MDGs’, asihi KM

Risala ya KM kufunga warsha maalumu kuhusu Afya ya Kimataifa kwenye mazingira ya mizozo, iliotolewa Ijumatano, ilisisitiza kwamba uwezo wa jumuiya ya kimataifa kuyafikilia, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia, (MDGs) unafungamana kimsingi na matokeo mazuri kwenye zile juhudi za kuendeleza afya ya jamii.

16/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa kwa Mtoto wa Afrika

Tarehe ya leo, Juni 16, inaadhimishwa na UM kuwa ni “Siku ya Kimataifa kwa Mtoto wa Afrika.” Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza ya kuwa kuna baadhi ya nchi katika Afrika, zilizoonyesha maendeleo makubwa ya kutia moyo, kwenye zile juhudi za kuhudumia watoto wachanga kuishi.

16/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

‘Watu milioni 42 waling’olewa makwao duniani 2008′: UNHCR

ACNUR UNHCR logo refugiados refugees ACNUR / Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) leo imewasilisha ripoti ya mwaka ambapo imeeleza idadi ya watu waliolazimika kuyahama mastakimu, kwa sababu ya mateso, fujo na vurugu ulimwenguni, mnamo mwisho wa 2008, ilifikia wahamiaji milioni 42.

16/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Chinese Unit

Kwenye mkutano na waandishi habari uliofanyika kwenye Makao Makuu, KM Ban Ki-moon alitangaza kumteua rasmi Raisi mstaafu wa Marekani, Bill Clinton kuwa Mjumbe Maalumu wa UM kwa Haiti. Mkutano ulihudhuriwa na Raisi Clinton pamoja na Waziri wa Nchi za Kigeni wa Haiti, Alrich Nicolas. Clinton aliwaambia wanahabri ya kwamba licha ya dhoruba kadha wa kadha zilizopiga Haiti mwaka uliopita na kusababisha uharibifu mkubwa ndani ya nchi, sasa hivi taifa hilo limo kwenye mazingira yenye matumaini ya kufufua, kwa mafanikio, huduma za kiuchumi na kijamii nchini.

15/06/2009 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IAEA inaripoti matumaini kuhusu mazungumzo ya Iran-Marekani, na wasiwasi kufuatia majaribio ya kinyuklia ya DPRK

nuclear testing Russian Radio

Ripoti ya Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Kinyuklia (IAEA), Mohamed ElBaradei iliowakilishwa kwenye Bodi la Magavana, imebainisha kuwa na matumaini ya kutia moyo, katika kuanzisha mazungumzo baina ya Teheran na Washington, kuzingatia masuala ya miradi ya kinyuklia inayoendelezwa na Iran hivi sasa pamoja na mada nyeginezo.

15/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nusu ya vifo vya barabarani huathiri wenda kwa miguu, wapanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki

Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) umethibitisha ya kuwa nusu ya watu milioni 1.27 wanaokadiriwa kufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, ni watu wanaokwenda kwa miguu, na wale wanaopanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki.

15/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uongozi mpya unahitajika kukabiliana na mizozo ya ajira duniani. inasema ILO

Juan Somavia-ILO

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) alipohutubia kikao cha ufunguzi wa Mkutano Mkuu juu ya Masuala ya Mizozo ya Ajira Duniani, uliofanyika Geneva, amependekeza kuwepo "uongozi mpya katika viwango vyote vya kiuchumi na kijamii” ili kusuluhisha vyema mizozo ya ajira kimataifa. Mkuu huyo wa ILO, alisema ulimwengu hauwezi tena kusubiri uchumi ukuwe, kwanza, kwa miaka kadha kabla ya kuamua kuzalisha ajira.

15/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa WHO ahimiza haki kwenye sera za kimataifa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dktr Margaret Chan aliwaambia wajumbe wa kimataifa, waliohudhuria warsha maalumu uliofanyika Makao Makuu ya UM, kuwacha ile tabia ya "kuamini, bila kuelewa, madai yanayojigamba ustawi wa uchumi na natija zake kimataifa ndio mambo yatakayofanikiwa kumaliza na kuponya matatizo yote ya maisha duniani."

15/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

KM amemteua Moustapha Soumaré wa Mali kuwa Naibu Mjumbe Maalumu mpya atakayeshughulikia kitengo kinachohusika na Ufufuaji wa Huduma za Jamii na Uchumi na Utawala Bora kwenye Shirika la UM juu ya Operesheni za Amani Liberia (UNMIL). Soumaré pia atashika wadhifa wa Mratibu Mkaazi wa UM na Mshauri wa Misaada ya Kiutu wa UM kwa Liberia.

12/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulimwengu sasa umo kwenye mkumbo wa awali wa maambukizo ya janga la homa ya A(H1N1), yahadharisha WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki hii limepandisha kiwango cha tahadhari ya maambukizi ya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1) kutoka daraja ya 5 mpaka ya sita.

12/06/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Dunia Dhidi ya Ajira ya Watoto Wadogo

Kwenye kumbukumbu ya miaka 10 ya Siku ya Dunia dhidi ya Ajira ya Watoto wa Umri Mdogo, siku ambayo huadhimishwa tarehe ya leo kulitolewa mwito maalumu na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), likijumuika na mashirika wenzi wa kuhimiza jamii ya kimataifa kukabiliana na sababu za msingi zenye kuchochea umasikini na ufukara, hali ambayo inaaminika ndio yenye kuwalazimisha watoto wenye umri mdogo kutafuta ajira ya kumudu maisha.

12/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo kupatikana kwenye mkutano wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Mkutano wa UM uliofanyika Bonn, Ujerumani mwezi huu, kuzingatia masuala yanayohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, umemalizika Ijumaa ya leo na iliripotiwa kumepatikana mafanikio ya kuridhisha katika maandalizi ya waraka wa ajenda ya majadiliano, kwa kubainisha dhahiri matarajio ya serikali wanachama kutoka Mkutano ujao wa Copenhagen, ili kuharakisha udhibiti bora wa taathira za mabadiliko ya hali ya hewa kimataifa.

12/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano Usomali yazusha msururu was maafa, mamia ya majeruhi na uhamisho wa lazima

OCHA logo OCHA/UN Spanish UNit

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mapigano makali yalioshtadi katika mji mkuu wa Mogadishu, Usomali mnamo miezi ya karibuni, yamewacha nyuma msururu wa uharibifu na maangamizi, majeruhi kadha wa kiraia na kusababisha mamia elfu ya watu kulazimika kuhama makazi na kuelekea maeneo tofauti ya nchi yenye hifadhi bora.

12/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

BU laamrisha vikwazo ziada dhidi ya DPRK

Baraza la Usalama limekutana leo adhuhuri, na kupitisha, kwa kauli moja, azimio 1874 (2009) liliopendekeza kuchukuliwa hatua kali za kuweka vikwazo dhidi ya miradi ya kutengeneza silaha za kinyuklia na makombora katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea/Korea ya Kaskazini (DPRK).

12/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Wajumbe wa Baraza la Usalama walikutana kwenye kikao maalumu cha faragha, hii leo, kusikiliza ripoti ya Mike Smith, mkuu wa Kurugenzi ya Utendaji Dhidi ya Ugaidi, ambapo pia walisailia shughuli za miezi ya karibuni ya bodi hilo.

11/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Homa ya mafua ya A(H1N1) yatambuliwa na WHO kuwa janga la ugonjwa wa kuenea kimataifa

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ilani maalumu yenye kuthibitisha kwamba Homa ya Mafua ya A(H1N1) sasa inatambuliwa rasmi kuwa ni janga la ugonjwa wa kuenea kimataifa – hii ni aina ya ilani ambayo inatangazwa tena kwa mara ya kwanza na WHO baada ya kipindi cha miaka 40.

11/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS kuuzindua umma wa kimataifa, VVU ni washiriki bubu wa maafa ya dharura

Mumtaz Mia, mshauri wa Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) kwa ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, amenakiliwa akitahadharisha ya kwamba mara nyingi, hasakatika mataifa yanayoendelea, huduma ya kuzuia maambukizo ya virusi vya UKIMWI huwa haipewi umuhimu unaostahiki, hasa baada ya kuzuka mizozo kadhaa ya dharura katika majiraya karibuni.

11/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kuonya, mizozo ya fedha duniani hupalilia njaa kwa mafukara

Ripoti mpya ya uchunguzi, iliotolewa na Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo imeeleza ya kuwa mzozo wa kifedha uliozuka katika miezi ya karibuni, katika soko la kimataifa, umeathiri zaidi watu maskini na wale wenye njaa – umma ambao hali yao ya kimaisha inaashiriwa itaharibika zaidi katika siku zijazo.

11/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID imepoteza mlinzi amani Darfur

Askari wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) ameripotiwa kufariki Ijumatano, kufuatia ajali ya gari katika Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini, baada ya kukamilisha doria ya kulinda raia kieneo.

11/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

View of the United Nations Building UN Spanish Radio

Asubuhi wajumbe wa Baraza la Usalama walikutana, kwa ushauri, kuzingatia nakala ya kwanza ya azimio kuhusu suala la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (DPRK). Azimio hilo linatarajiwa kupitishwa na wajumbe wa Baraza mnamo siku chache zijazo.

10/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Treky wa Libya ateuliwa kuwa raisi wa 64 wa Baraza Kuu

Dktr Ali Abdessalaam Treky wa Jamhuri ya Kiarabu ya Libya, aliye Katibu wa Masuala ya Umoja wa Afrika taifani mwao, amechaguliwa leo na wajumbe wa kimataifa, na bila kupingwa, kuwa raisi wa kikao kijacho cha 64 cha Baraza Kuu la UM, kikao ambacho kitaanza shughuli zake mwezi Septemba (2009).

10/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICRC inasema mifumko ya mapigano Kivu inakithirisha mateso kwa umma dhaifu

Goma, Nord kivu, refugees MONUC website

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) imeripoti mifumko mipya ya mapigano katika sehemu za Kivu ya Kaskazini na Kusini, katika JKK, inazidisha hali ya wasiwasi na kihoro miongoni mwa zile jamii dhaifu, raia ambao tangu awali hushuhudia hali ya mtafaruku na vurugu kila siku kwenye maeneo yao.

10/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa ICG juu ya Usomali waihimiza jumuiya ya kimataifa kutekeleza ahadi zao

Kikao cha 15 cha siku mbili, cha nchi wanachama wa Kundi la Kimataifa juu ya Suluhu ya Usomali (ICG), kilikhitimisha majadiliano yake Alkhamisi ya leo, kwenye mji wa Roma, Utaliana, kikao ambacho kiliongozwa na Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah.

10/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wa fedha wa Afrika wahimiza kuchukuliwa “hatua za kijasiri” kutatuta mizozo ya kiuchumi nchini mwao

Ramani ya Afrika

Mawaziri wa Fedha na Uchumi kutoka Mataifa ya Afrika wametoa mwito maaulumu unaotaka kuchukuliwe “hatua za kijasiri na za haraka” na nchi zao, kukabiliana na athari haribifu zinazotokana na mizozo ya kifedha na uchumi, iliotanda hivi sasa kwenye maeneo hayo.

10/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulio ya magaidi Pakistan yalaumiwa vikali na KM

KM Ban Ki-moon ameshtumu, kwa kauli kali, shambulio la magaidi liliofanyika Ijumanne kwenye Hoteli ya Pearl Continental, iliopo kwenye mji wa Peshawar, Pakistan ambapo watu 18 waliuawa, ikijumlisha pia watumishi wawili wa UM.

10/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

unflaghq0425r

Taarifa ya Baraza la Usalama kwa vyombo vya habari, iliotolewa Ijumanne ya leo, ilipongeza maendeleo yaliojiri karibuni nchini Burundi katika kutekeleza mpango wa amani, hasa ule mpango wa kunyanganya silaha kundi la waasi la FNL, kundi ambalo pia sasa hivi limejiandikisha rasmi kutambuliwa kuwa ni chama cha kisiasa, na limeridhia kujiunganisha na taasisi za kitaifa, na kuwaachia wale watoto wapiganaji waliohusiana nao hapo kabla.

09/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raisi wa Gabon aombolezwa na KM Ban

KM Ban Ki-moon ametoa taarifa maalumu, kwa kupitia msemaji wake, inayobainisha masikitiko yake makubwa juu ya kifo cha Raisi Omar Bongo Ondimba wa Gabon.

09/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP inahadharisha, Pembe ya Afrika inakabiliwa tena na mwaka wa njaa

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa onyo maalumu leo hii kutoka ofisi zake ziliopo Roma, Italiana, linalohadharisha kwamba mamilioni ya watu wanaoishi katika Pembe ya Afrika wanakabiliwa, kwa mara nyengine tena, na mchanganyiko maututi wa ukame ulioselelea, mvua haba na mizozo isiokwisha, katika mazingira ambayo bei ya chakula, hususan kwenye nchi nyingi zinazoendelea, nayo pia bado inaendelea kuwa ya juu kabisa.

09/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali katika Usomali inasailiwa na kundi la ICG kwenye mkutano wa Roma

Ahmedou Ould- Abdallah 13a.jpg

Kuanzia tarehe 09 mpaka 10 Juni (2009) wawakilishi kutoka nchi 35, wakichanganyika na wale wa kutoka mashirika ya kimataifa wamekusanyika mjini Roma, Utaliana kuhudhuria kikao cha 15 cha lile Kundi la Kimataifa la Mawasiliano ya Suluhu ya Usomali (ICG), kikao kitakachoongozwa na Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah.

09/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano ya Mogadishu yasababisha raia 117,000 kung’olewa makazi: UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti mnamo mwisho wa wiki iliopita maelfu ya raia walilazimishwa kuyahama mastakimu yao, kufuatia mapigano makali yalioshtadi kwenye mitaa ya mji mkuu wa Mogadishu, Usomali, hali ambayo ilisababisha umwagaji damu mkubwa kabisa. UNHCR inakadiria watu 117,000 waling’olewa makazi kwa sababu ya mapigano haya.

09/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Helen Clark, Mkuu wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) Ijumanne ataanza ziara ya awali katika Afrika tangu kuchukua madaraka ya kuiongoza taasisi hiyo ya UM. Atayatembelea mataifa ya Liberia, JKK na Ethiopia kutathminia maendeleo kwenye utekelezaji wa miradi ya UNDP huko, na pia atakutana na maofisa wa vyeo vya juu wa serikali za mataifa anayoyazuru.

08/06/2009 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nabarro ahadhirisha, afya isiotunzwa ya mifugo huathiri wanadamu kwa mapana na marefu

Ganado / Cattle / Livestock / FAO UN Spanish Radio

Mratibu wa Mradi wa UM Kupambana na Homa za Mafua na Mzozo wa Chakula Duniani, Dktr David Nabarro, amenakiliwa akihadharisha, kutokea Vienna, Austria ya kwamba afya ya mifugo ni muhimu sana katika kudumisha maisha bora kwa wanadamu.

08/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya huduma za kiutu yataka kuanzishwe miradi ya kuhifadhi raia na athari za mabadiliko ya hewa

UNEP. Climate Change in Africa. UNEP/UN Spanish Radio

Mashirika 18 ya UM yenye kuhudumia misaada ya kiutu, yakichanganyika na mashirika wenzi mengineyo yalio wanachama wa ile Kamati ya Kudumu ya Jumuiya Zinazotegemeana (IASC), yamependekeza kujumuishwa kwenye mkataba utakaofuatia Mkataba wa Kyoto, yale masuala yanayohusu athari haribifu dhidi ya wanadamu, zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

08/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Udhamini wa Utajiri wa Baharini

Tarehe ya leo, Juni 08, inaadhinmishwa na UM kuwa ni 'Siku ya Kudhibiti na Kutunza Utajiri wa Baharini'.

08/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walimwengu waandamana kuunga mkono juhudi za WFP kupiga vita njaa duniani

Ijumapili ya tarehe 07 Juni (2009) makumi elfu ya watu, katika sehemu mbalimbali za dunia, walikusanyika kwenye miji kadha ya kimataifa, na kuandamana kuunga mkono juhudi za Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) katika kupiga vita tatizo la njaa ulimwenguni, hususan miongoni mwa watoto wadogo.

08/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yatoa mwito wa kubuniwa mfumo imara dhidi ya njaa

FAO. Food Prices. FAO/Alessandra Benedetti - UN Spanish Radio

Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) ametoa mwito maalumu, uitakayo jamii ya kimataifa kuimarisha mfumo wa utawala bora wa kukabiliana na matatizo ya njaa, kwa kuhakikisha akiba ya chakula katika ulimwengu itadhaminiwa kwa taratibu zitakoridhisha na kutimiza mahitaji ya chakula ya muda mrefu kwa umma wa kimataifa.

08/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Shambulio la bomu liliotukia Ijumaa kwenye msikiti wa wilaya ya Dir ya Juu katika Pakistan, liliosababisha vifo vya watu 30, ni kitendo karaha kilicholaumiwa vikali na KM. Kwenye taarifa juu ya tukio hili KM alisisitiza, kwa mara nyengine tena kwamba vitendo vyote vya kutumia mabavu na fujo za kihorera dhidi ya raia ni uhalifu unaostahiki kupingwa na kulaaniwa kimataifa. Aliwatumia mkono wa pole kwa aila zote za waathirika wa tukio hilo pamoja na Serikali ya Pakistan.

05/06/2009 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wawakilishi wa tamaduni za kijadi Afrika Mashariki wazingatia kikao cha mwaka juu ya haki za wenyeji wa asili

Maasai from Tanzania

Wiki hii tutakamilisha makala ya pili ya yale mahojiano yetu na wawakilishi wawili wa jamii za makabila ya wenyeji wa asili kutoka Afrika Mashariki, ambao karibuni walihudhuria kikao cha nane cha ile Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili Duniani kilichofanyika Makao Makuu.

05/06/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama wa kigeugeu Kivu Kaskazini inaitia wasiwasi OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali ya usalama wa raia, ulioregarega Kivu Kaskazini, inaitia wasiwasi mkubwa wahudumia misaada ya kiutu waliopo katika JKK.

05/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhamisho wa raia Usomali unaendelea kukithiri wakati mapigano yakishtadi

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti idadi ya raia waliolazimika kuyahama makazi katika mji wa Mogadishu, tangu mapigano kuanza mnamo tarehe 08 Machi (2009), imekiuka watu 96,000 kwa sasa.

05/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP kuanzisha mradi mpya kuhishimu wajasiri wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limeanzisha mradi maalumu wa kuihishimu 'Siku ya Mazingira Duniani' utakaowatambua wale watu wanaoshiriki kwenye juhudi mbalimbali za uvumbuzi mpya na usio wa kawaida wa kuamsha hisia za umma kutunza mazingira.

05/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Mazingira Duniani

English Unit

Siku ya leo, tarehe 05 Juni (2009) huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni ‘Siku ya Mazingira Duniani’. Lengo hasa la siku hii ni kuendeleza mwamko unaofaa, miongoni mwa umma wa kimataifa, kuhusu mazingira, kwa ujumla, na kufahamishana hatari inayokabili maumbile haya, na pia kuwahamasisha wanadamu kuwa mawakala wa kuwasilisha mabadiliko yatakayosaidia kuhifadhi mazingira na kudumisha maendeleo.

05/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

United Nations Logo UN SPANISH RADIO

Baraza la Usalama lilikutana asubuhi kuzingatia shughuli za Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Vita katika Yugoslavia ya Zamani (ICTY) na Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR). Mwendesha Mashitaka wa ICTY, Serge Brammertz kwenye taarifa aliowasilisha kwenye kikao hicho, alikumbusha 2009 ni mwaka wa mwisho wa Mahakama kuendeleza shughuli kamili kabla kuanza kupunguza watumishi wake katika 2010. Vile vile Hasan Jallow, Mwendesha Mashitaka wa ICTR ameliomba Baraza la Usalama kusaidia kuyahimiza mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kuwashika na kuwapeleka kwenye Mahakama ya ICTR wale watoro wanaotafutwa na waliotuhumiwa makosa ya jinai. Jallow alisema fungu kubwa la darzeni ya watuhumiwa hao hivi sasa wanaishi Kenya na katika JKK, mataifa ambayo serikali zao zinawajibika kuwashika na kuwahamisha kwenye Mahakama ya ICTR iliopo Arusha, Tanzania kukabili haki.

04/06/2009 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

KM kupongeza risala ya Raisi wa Marekani kukuza uhusiano mwema na ulimwengu wa Waislam

Barack Obama 05a

KM Ban Ki-moon, kwa kupitia msemaji wake, ameripotiwa kuipongeza hotuba ya Raisi Barack Obama wa Marekani, alioiwakilisha kwenye Chuo Kikuu cha Cairo Alkhamisi ya leo, ambapo alizingatia uhusiano mpya baina ya Marekani na mataifa ya KiIslam. .

04/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UN-HABITAT/UNIFEM yatashirikiana kupiga vita udhalilishaji na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake

Cancer affects everyone – the young and old, the rich and poor, men, women and children – and represents a tremendous burden on patients, families and societies. Cancer is one of the leading causes of death in the world, particularly in developing countri WHO-OMS / Spanish Radio

Mashirika mawili ya UM, yaani lile shirika juu ya makazi, UN-HABITAT, na lile shirika linalohusika na mfuko wa maendeleo kwa wanawake, UNIFEM, yameshirikiana rasmi kujumuika bia kukabiliana na tatizo la udhalilishaji na matumizi ya mabavu dhidi ya wanawake na watoto wa kike, katika miji ya mataifa yanayoendelea.

04/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO inasema akiba ya chakula duniani imetulia mwaka huu

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetoa ripoti yenye kuashiria mavuno ya nafaka, na akiba ya chakula kwa mwaka huu, hayatodhurika kiuchumi katika soko la kimataifa, kama ilivyotukia katika 2008, ambapo bei ya juu ya chakula ilisababisha mtafaruku na hali ya hatari kimataifa.

04/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IFAD inayahimiza mataifa Afrika kukipa kilimo umuhimu kupambana na matatizo ya fedha

FAO. Sustainable farming. Agricultura sostenible. FAO/UN Spanish Radio

Kanayo F. Nwanze, Raisi wa Shirika la UM linalohusika na ukomeshaji wa ufukara na umaskini wa vijijini, yaani Shirika la Kimataifa juu ya Maendeleo na Kilimo (IFAD) ameshauri kwamba serikali za Afrika, zenye kutunza na kuhudumia kimaendeleo sekta ya kilimo, ndizo zitofanikiwa kudhibiti, kwa wastani, athari mbaya zinazoletwa na migogoro ya fedha duniani.

04/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

BK kupitisha azimio la kutiaka UM kuchunguza athari hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa dhidi ya usalama

climate change 06b

Ijumatanao, Baraza Kuu (BK) la UM, kwenye kikao cha wawakilishi wote lilipitisha, kwa kauli moja, azimio lenye kuyahimiza mashirika na taasisi zote za UM kufanya uchunguzi wa kuzingatia uwezekano wa kuzuka madhara haribifu dhidi ya usalama na amani duniani, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, pindi jumuiya ya kimataifa itashindwa kuyadhibiti maafa hayo mapema.

04/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti ya kuwa itamudu kukidhi mahitaji ya msingi ya chakula kwa wahamiaji wa ndani (IDPs) milioni 2.6, katika miezi ya Juni na Julai, waliopo kwenye maeneo ya mapigano katika Pakistan. UM inasema umepokea asilimia 43 tu ya zile fedha zinazotakikana kuhudumia mahitaji hayo, kati ya jumla ya dola milioni 280 ya maombi ya chakula. Kadhalika, akiba ya madawa muhimu inatazamiwa kumalizika katika mwisho wa mwezi, na misaada ya dharura itahitajika kuhudumia afya ya umma mnamo miezi sita ijayo. Halkadhalika, imeripotiwa kuwepo upungufu mkubwa wa vifaa vya huduma ya afya pamoja na ukosefu wa sabuni kwa watu waliopo kwenye kambi za IDPs. Vile vile Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kwamba kati ya mama wajawazito 50,000, wanaotarajiwa kuzaa katika miezi sita ijayo, wajawazito 5,000 wanakadiriwa watahitajia kupelekwa hospitali kupata matunzo ya dharura mazuri juu ya uzazi.

03/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za kilimo ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani: FAO

Juhudi za kufarajia maendeleo yanayosarifika kwenye sekta ya kilimo, hasa katika nchi zinazoendelea, ndio kadhia muhimu pekee yenye uwezo wa kudhibiti bora mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa duniani, na katika kupunguza njaa na ufukara, imeeleza Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO).

03/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takwimu mpya juu ya homa ya mafua ya A(H1N1)

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa linazingatia kupandisha juu kipeo cha hadhari ya maambukizo ya homa ya mafua ya A(H1N1) ulimwenguni, kutoka daraja ya tano hadi daraja ya juu kabisa ya sita, kwa sababu ya kuendelea kwa maambukizo ya ugonjwa huu katika dunia.

03/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR inasema wahamiaji 86,000 wamen’golewa makazi Mogadishu

UNHCR imeripoti kwamba kuanzia tarehe 08 Machi mwaka huu, hadi hivi sasa, jumla ya raia waliokosa makazi katika mji wa Mogadishu, Usomali kutokana na mapigano imefikia watu 86,000.

03/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR haikuridhika na hatua ya Rwanda ya urejeshwaji wa kimabavu kwa wahamiaji wa Burundi

Burundi map

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeeleza kuwa na wasiwasi juu ya hatua iliochukuliwa na serikali ya Rwanda, ya kuwarudisha Burundi, kwa nguvu, wale wahamiaji waliokuwa wakiishi Rwanda kwenye kambi ya Kigeme.

03/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisa wa MONUC anafafanua binafsi maana ya ‘Sikukuu ya Walinzi Amani’

Tarehe 29 Mei huadhimishwa na UM kuwa ni ‘Sikuu ya Kuwakumbuka Walinzi Amani wa Kimataifa’ waliochangisha ujuzi wao, na wengine hata kujitoleea mhanga wakati waliposhiriki kwenye zile huduma za kulinda amani, katika kanda mbalimbali za dunia zilizoghumiwa na migogoro, fujo, vurumai na vurugu. Taadhima za mwaka huu zililenga zaidi mchango wa watumishi wa kimataifa wa kike kwenye opersheni za amani za [...]

03/06/2009 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti idadi ya watu wenye njaa duniani inaendelea kuongezeka. Ilikadiria katika miaka miwili iliopita, watu milioni 150 walijiunga na safu za wenye kusumbuliwa na tatizo la njaa ulimwenguni. Taarifa ya WFP ilikumbusha vijana wa siku hizi wana hamu kubwa ya kujiilimisha juu ya tatizo la upungufu wa chakula kimataifa. Kwa hivyo, WFP imebuni ukurasa maalumu kwenye mtandao wa shirika hilo, utakaowapatia vijana taarifa na ilimu inayofahamisha vizuri zaidi matatizo ya njaa ulimwenguni, na ni aina ya mtandao wenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kimataifa, kwa ujumla, kuchukua hatua za kupambana na njaa katika ngazi ya umma wa kikawaida.

02/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazotunza vinasaba vya mimea anuwai kufadhiliwa msaada wa fedha na taasisi ya kimataifa

Mkutano wa Hadhi ya Juu wa wajumbe wa Bodi la Utawala la Taasisi ya Kutekeleza Mkataba wa Kimataifa Kutunza Rasilmali ya Vinasaba vya Mimea kwa Chakula na Kilimo, unaofanyika hivi sasa mjini Tunis, Tunisia umetangaza kuwa mataifa yanayoendelea 11 yanayotekeleza ile miradi ya kuhifadhi akiba ya mbegu za mimea kwa chakula na kutunza vinasaba vya mazao makuu, yatafadhiliwa msaada wa dola 500,000.

02/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupotea kwa ndege ya Ufaransa Brazil inaashiriwa kumesababishwa na mchanganyiko wa vipengele, yasema WMO

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeeleza kwamba ndege ya Ufaransa ya aina ya rakamu 447, iliopotea wakati ikiruka kutoka Rio de Janeiro, Brazil kuelekea Paris, Ufaransa, ilipitia ukanda wa eneo la kitropiki penye mkusanyiko mkali wa dhoruba za radi ya mvua.

02/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC inazingatia ombi la kufuta kesi ya jinai ya vita katika JKK

International Criminal Court logo

Mapema wiki hii, Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), iliopo mjini Hague, Uholanzi ilianza kusikiliza hoja za wakili wa utetezi wa mtuhumiwa Germaine Katanga, aliyekuwa kamanda wa jeshi la mgambo katika JKK, hoja ambazo zilisisitiza ushahidi uliotolewa kuanzisha tena kesi dhidi ya mshitakiwa huyo haziwezi kutumiwa kuunganisha kesi mbili kisheria, na ushahidi huo usiruhusiwe wala kukubaliwa na Mahakama.

02/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mizozo ya ajira duniani inasailiwa na ILO kwenye mkutano wa mwaka Geneva

Shirika la UM juu y Haki za Wafanyakazi (ILO) litaanzisha Mkutano wa Mwaka mjini Geneva hapo kesho, tarehe 03 Juni, ambapo majadiliano yake yataendelea hadi Juni 19.

02/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Uturuki umekabidhiwa uraisi wa duru wa Baraza la Usalama kwa mwezi Juni, baada ya Shirikisho la Urusi kukamilisha uongozi wa shughuli za Baraza kwa mwezi Mei. Wajumbe wa Baraza la Usalama watakutana Ijumanne asubuhi kuzingatia mpango wa kazi na ajenda ya mikutano ya mwezi Juni. Baada ya hapo, Balozi Baki Ilkin wa Uturuki atafanya mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa wa Makao Makuu, kuelezea masuala yatakayopewa umuhimu kwenye mijadala ya Baraza la Usalama chini ya uongozi wa Uturuki.

01/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya FARDC katika JKK vasaidiwa na MONUC kukabiliana vyema na waasi wa Kihutu nchini

Waasi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Mnamo mwisho wa wiki iliopita, Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limeripoti kushirikiana na vikosi vya taifa vya FARDC, kwenye operesheni maalumu za kuwafyeka kutoka mafichoni wapiganaji wanamgambo wa Kihutu, waliokuwa wakiendeleza vitendo vya ukatili wa aina kwa aina nchini dhidi ya raia.

01/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa yaanza rasmi Bonn

Duru ya pili ya Mazungumzo ya UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani imeanza rasmi majadiliano Ijumatatu ya leo, kwenye mji wa Bonn, Ujerumani ambapo kutazingatiwa, kwa mara ya kwanza, waraka wa ajenda iliofikiwa na nchi wanachama karibuni, ya kudhibiti bora taathira za mageuzi ya mazingira yanayoletwa na hali ya hewa ya kigeugeu.

01/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zimbabwe itahitajia dola milioni 719 kuhudumia kidharura umma

money, investment Russian Radio

UM imeripoti Zimbabwe inahitajia wahisani wa kimataifa kuchangisha msaada wa dharura, kwa mwaka huu, unaokadiriwa dola milioni 719 kukidhi mahitaji ya kiutu kwa umma na kufufua uchumi nchini, baada ya shughuli hizo kuporomoka nchini karibu miaka kumi.

01/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe Malumu kwa Sudan ameingia wasiwasi juu ya usalama wa kusini

Press Conference: Mr. Ashraf Qazi Special Representative for Sudan UN PHOTO / Spanish Unit

Kadhalika, baada ya ziara ya siku mbili Sudan Kusini, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, Ashraf Qazi, ambaye vile vile ni Mkuu wa Shirika la Ulinzi Amani la UM kwa Sudan Kusini (UNMIS) alisema ameingiwa wasiwasi juu ya kuharibika kwa hali ya utulivu kwenye eneo hilo mnamo miezi ya karibuni, kwa sababu ya mapigano ya kikabila yaliofumka kwenye majimbo ya Nile ya Juu na Jonglei.

01/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM imepeleka mkono wa taazia kwa kifo cha raisi wa zamani wa Sudan

Sudanese refugee women prepare their luggage for the trip back to South Sudan, Kakuma camp, Kenya. UNHCR

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, Ashraf Qazi, leo amepeleka mkono wa taazia kwa umma wa Sudan pamoja na aila ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo, Raisi Jaafer Nimeiri, baada ya magazeti kuripoti rasmi taarifa iliotolewa na Serikali Ijumamosi kuhusu kifo cha Raisi Nimeiry. Marehemu Nimeiry alikuwa na umri wa miaka 79 na aliugua kwa muda mrefu ugonjwa usiotambulika.

01/06/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031