Nyumbani » 30/04/2009 Entries posted on “Aprili, 2009”

Hapa na pale

Chinese Unit

John Holmes, KM juu ya Masuala ya Kiutu na Misaada ya Dharura ameshtumu, kwa kauli kali, mashambulio ya raia yaliofanyika karibuni kwenye jimbo la Kivu Kusini, katika JKK, na kundi la waasi la FDLR.

30/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama

Security Council Middle East

Alkhamisi Baraza la Usalama asubuhi lilianza shughuli zake kwa kujadilia hali katika Cyprus, na maendeleo kuhusu mazungumzo ya kusawazisha mfarakano baina ya raia wa Kigiriki na wale wa Kituruki.

30/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uamuzi wa mahakama ya jeshi la JKK waungwa mkono na MONUC

Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM kwa JKK ameyakaribisha maamuzi ya mahakama ya kijeshi la taifa ya kuwatia hatiani maofisa 20 wa jeshi, waliotuhumiwa kushiriki kwenye makosa yanayojumlisha wizi wa mabavu, jinai dhidi ya utu na vitendo haramu vya kunajisi raia kihorera.

30/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisa wa ECA ameripoti taaluma ya sayansi Afrika ndio ngao dhidi ya migogoro

Wataalamu wa sayansi 600 kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika wiki hii Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria Kikao cha Awali cha Kamati ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia (CODIST-1) kilichoanza mashauriano leo Alkhamisi.

30/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takwimu mpya za WHO juu ya maambukizi ya vimelea vya H1N1

Dktr Keiji Fukuda, Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwenye mahojiano Alkhamisi na waandishi habari mjini Geneva, alitangaza takwimu mpya juu ya maambukizo ya homa ya mafua ya nguruwe, ambayo kuanzia leo itajulikana rasmi kama homa ya vimelea vya H1N1.

30/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti idadi ya watu walioambukizwa na maradhi ya homa ya mafua ya nguruwe imeongezeka, kwa kulingana na taarifa ilizopokea Ijumatano kutoka maabara ya uchunguzi wa kisayansi wa maradhi.

29/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Orodha ya wagombea wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu yatangazwa rasmi na IAEA

Shirika la UM Kuhudumia Matrumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limetangaza kuwa limepokea orodha rasmi ya wagombea uchaguzi wa cheo cha Mkurugenzi Mkuu mpya wa taasisi hii ya kimataifa baada ya kiongozi wa sasa Mohamed ElBaradei kutangaza atastaafu atakapomaliza muda wake mwaka huu.

29/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi saba zimegundua waathirika wa homa ya mafua ya nguruwe, WHO imethibitisha

Mkurugenzi wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Maradhi (CDC) amenakiliwa na vyombo vya habari akithibitisha ripoti inayosema mtoto mchanga wa miezi 23, katika jimbo la Texas, amesajiliwa kufariki kufuatia maambukizo ya homa ya mafua ya nguruwe. Kifo hiki ni cha kwanza kutukia Marekani, miongoni mwa wale watu waliopatwa na ugonjwa huo.

29/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUC imekanusha tetesi za BBC juu ya uhusiano wa CNDP na MONUC

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limekanusha kihakika tetesi za ripoti ya shirika la habari la Uingereza la BBC zinazodai John Bosco Ntaganda, mtuhumiwa wa jinai ya vita na kiongozi wa kundi la waasi la CNDP kwenye eneo la kaskazini-mashariki ya JKK, alishiriki kwenye operesheni za vikosi vya UM nchini mwao.

29/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya kuwakumbuka waathirika wa silaha za kemikali

KM wa UM Ban Ki-moon ameyasihi Mataifa Wanachama kuchukua hadhari kuu ili kuhakikisha silaha maututi za kemikali hazitodhibitiwa katu na makundi ya magaidi. KM aliyasema haya kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kuwakumbuka Waathirika wa Mapigano Yanayotumia Kemikali.

29/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makampuni ya madawa yanahimizwa na IAEA kuunda chombo rahisi kudhibiti saratani

Shirka la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeyahamasisha makampuni yanayotengeneza vifaa na zana za matibabu kuunda chombo kipya cha tiba ya saratani kkitakachokuwa na nguvu, chepesi, kinachobebeka, rahisi kutumia na ambacho watu wa kawaida watamudu kukinunua.

28/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakulima Afrika magharibi wanakabiliwa na athari haribifu za hali ya hewa, kuonya WMO

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeripoti wakulima wa Afrika Magharibi wanatishiwa na hatari ya kukabwa kimaendeleo kwa sababu ya athari haribifu zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye ukanda wao.

28/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa mpya za WHO juu ya homa ya mafua ya nguruwe

Umoja wa Mataifa unaendelea kushughulikia tatizo la afya lililozuka ulimwenguni hivi karibuni, baada ya kugunduliwa homa ya mafua ya nguruwe katika baadhi ya mataifa na namna ugonjwa huu ulivyoathiri wanadamu.

28/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama linasailia hali katika Cote D’ivoire

Baraza la Usalama leo limekutana asubuhi kusailia hali katika Cote d’Ivoire.

28/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

Taarifa mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO), juu ya mripuko wa homa ya mafua ya nguruwe, imesema wataalamu wa taasisi ya afya wamethibitisha virusi vilivyosababisha homa ya mafua ya nguruwe, iliogundulikana karibuni katika mataifa ya Marekani, Mexico na Kanada, ni virusi vya aina ya A/H1N1.

27/04/2009 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama linazingatia tena operesheni za UNAMID

Baraza la Usalama asubuhi limezingatia ripoti ya KM kuhusu maendeleo kwenye operesheni za kulinda amani Darfur za vikosi vya mchanganyiko vya UM na UA, yaani vikosi vya UNAMID.

27/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO kuwakumbuka waliojeruhiwa na kuuawa kwenye mazingira ya vibarua

ILO-Logo

Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) limeripoti tarehe 28 Aprili itaadhimishwa kuwa ni Siku ya Usalama na Afya ya Ajira Duniani. Mataifa Wanachama kadha pamoja na mamia ya sehemu mbalimbali za dunia, yatashiriki kwenye taadhima za kuihishimu siku hiyo, zikijumlisha kumbukumbu maalumu za wafanyakazi waliojeruhiwa au kufariki wangali wakiendeleza majukumu ya vibarua walivyoajiriwa.

27/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa Wanachama yanahimizwa kuharakisha utekelezaji wa ahadi za Brussels kuhudumia amani Usomali

Ahmedou Ould Abdalah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali ameripotiwa kutoa taarifa inayohimiza nchi wanachama zilizohudhuria Mkutano wa Brussels juu ya Usomali, uliofanyika wiki iliopita ambapo kuliahidiwa kuchangisha msaada wa dola milioni 213 ziada, kukamilisha ahadi zao haraka iwezekanavyo, ili kuviwezesha vikosi vya ulinzi amani kuimarisha utulivu nchini Usomali.

27/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO inahadharisha homa ya nguruwe inahatarisha kuenea kimataifa kama haijadhibitiwa mapema

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Afya Duniani (WHO) kwenye mahojiano na waandishi wa habari mwisho wa wiki [25/04/2009], alihadharisha mripuko wa karibuni wa aina ya virusi vya homa ya mafua – inayotambuliwa kwa umaarufu kama homa ya mafua ya nguruwe – katika maeneo ya Mexico na Marekani, inatakikana kudhibitiwa mapema, au si hivyo homa hii inaashiriwa itaenea kwa kasi na kudhuru fungu kubwa la umma wa kimataifa.

27/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

John Holmes, Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu na Mratibu wa Misaada ya Dharura anatazamiwa mwisho wa wiki kufanya ziara ya siku tatu katika Sri Lanka. Anatazamiwa kuwa na mazungumzo muhimu na maofisa wa Serikali ya Sri Lanka, ikijumlisha masuala yanayohusu uwezekano wa kuipatia UM kibali cha kupeleka watumishi wae kufanya makadirio ya hali [...]

24/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtetezi wa mazeruzeru Tanzania ahimiza UM usaidie uimarishaji wa haki zao kimataifa

Russian Radio

Kwenye wiki ya tarehe 20 mpaka 24 Aprili wajumbe kadha wa kadha kutoka Mataifa Wanachama wa UM walikusanyika mjini Geneva, Uswiss kuhudhuria Mkutano wa Maafikiano ya Durban kwa makusudio ya kutathminia, na pia kuharakisha, utekelezaji wa mapendekezo yaliopitishwa na kikao cha awali cha 2001, katika Durban dhidi ya ubaguzi.

24/04/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kupiga Vita Malaria 2009

English Unit

Ijumamosi, tarehe 25 Aprili itaadhimishwa rasmi kimataifa kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Malaria Duniani.

24/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaumu misaada ya ilimu ya msingi iliteremka 2007 katika nchi masikini

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeripoti mproromoko mkubwa wa misaada ya kuhudumia ilimu ya msingi katika nchi zinazoendelea.

24/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wa JKK wanaendelea kuhajiri vijijini kukhofu adhabu za waasi wa Kihutu

Russian Radio

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limesema lina wahka juu ya usalama wa umma ulionaswa kwenye mazingira ya uhasama katika eneo la mashariki la JKK, ambapo hali inasemekana inaendelea kuharibika. Hali hiyo imesababisha makumi elfu ya raia kuhajiri makaz, kutafuta usalama na hifadhi, katika siku za karibuni.

24/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano juu ya Mwito wa Durban Kupinga Ubaguzi wahitimishwa Geneva

Mkutano wa Mapitio juu ya Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi, uliofanyika wiki hii mjini Geneva, Uswiss ulikamilisha shughuli zake leo Ijumaa. Kwenye mahojiano na waandishi habari wa kimataifa juu ya kikao hicho, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Bindamau, Navi Pillay alisema anaamini Mkutano ulikuwa wa mafanikio makubwa, licha ya kwamba mapatano yalikuwa magumu na yalichukua muda mrefu kukamilishwa.

24/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Taarifa ya KM iliotolewa Ijumatano usiku imeeleza kwa alifurahika kwa kuachiwa wale watu wanne waliotekwa nyara Afrika Magharibi miezi michache nyuma, ikijumlisha Mjumbe Maalumu wa KM kwa Niger, Robert Fowler pamoja na msaidizi wake Louis Guay, wote wawili wakiwa raia wa Kanada. Alkhamisi alasiri Baraza la Usalama limezingatia shughuli za Shirika la UM juu ya [...]

23/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO imethibitisha vifo vya malaria Zambia vimeteremka kwa asimilia 60 ziada

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti taifa la Zambia limefanikiwa kupunguza vifo vya malaria nchini kwa asilimia 66, kwa kutumia miradi maalumu ya dharura iliosaidia kudhibiti bora ugonjwa huu maututi.

23/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Brussels juu ya Usomali waahidi mamilioni kufufua amani

Kwenye Mkutano wa Kimataifa juu ya Usomali, uliofanyika kwenye mji wa Brussels, Ubelgiji Alkhamisi ya leo, wenye kuongozwa bia na Mwenyekiti wa UA, Jean Ping na KM wa UM Ban Ki-moon, uliwahamasisha wafadhili wa kimataifa kuahidi kuchangisha karibu dola milioni 250 kulisaidia taifa husika la Pembe ya Afrika kurudisha utulivu na amani ya eneo.

23/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Abiria 35 wa mashua za magendo wameripotiwa na UNHCR kuzama Yemen

somali refugees flee to the gulf of aden, yemen

Taarifa ya Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) imeeleza kwamba watu 35 waliripotiwa kuzama Ijumatano kwenye mwambao wa jimbo la Abyan, Yemen, liliopo kilomita 250 mashariki ya Aden, baada ya moja ya mashua mbili za wafanya magendo kupinduka.

23/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei kuu ya chakula katika nchi masikini inaendelea kutesa mamilioni, kuhadharisha FAO

hike of food prices all around the world FAO

Kwenye ripoti iliotolewa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) – yenye mada isemayo 'Hali ya Chakula na Matarajiao ya Baadaye ya Mavuno’ – ilieleza kwamba bei ya juu ya chakula katika mataifa yanayoendelea inaendelea bado kusumbua na kuwatesa mamilioni ya umma masikini, raia ambao tangu mwanzo umeathirika na matatizo sugu ya njaa na utapiamlo, licha ya kuwa mavuno ya nafaka ulimwenguni, kwa ujumla, yameongezeka katika kipindi cha karibuni, na bei za chakula ziliteremka kimataifa, hali kadhalika.

23/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Kundi la FNL la waasi wa Burundi limetambuliwa rasmi na Serikali, mnamo tarehe 21 Aprili 2009, kuwa kama ni chama halali cha siasa baada ya kufanikiwa kujitenga na mapigano; na baada ya kuridhia kuwakabidhi wenye mamlaka silaha na pia kuachia huru wale watoto waliolazimishwa kushiriki kwenye mapigano. KM Ban Ki-moon alipongeza uamuzi wa kundi la [...]

22/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu linaadhimisha Sikukuu ya Mama Dunia

Baraza Kuu la UM leo limefanyisha kikao maalumu kuadhimisha siku ya kuzaliwa jumuiya za kimataifa, katika 1970, kutetea haki na hifadhi ya mazingira ulimwenguni. Tarehe ya Aprili 22 hutambuliwa kila mwaka kama ni Siku ya Kimataifa ya Kuhishimu Mama Dunia.

22/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa KM anabashiria askari watoto wataachiwa na waasi katika JKK

Secretary-General's Special Representative for Children and Armed Conflict. UN Photo/UN Spanish Radio

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM Anayehusika na Hifadhi ya Watoto kwenye Mazingira ya Mapigano ameripoti kuwepo maendeleo ya kisiasa ya kutia moyo hivi karibuni, katika JKK, ambayo alisema yamewakilisha fursa mpya itakayosaidia kuharakisha kuachiwa huru wale askari watoto waliokuwa wakidhibitiwa na makundi ya waasi wanaochukua silaha.

22/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNHCR ashtumu sera za ubaguzi dhidi ya waombao hifadhi ya kisiasa

Ijumatano, Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliwaambia wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Geneva wa Mapitio ya Utekelezaji wa Mwito wa Durban Kupinga Ubaguzi Duniani, tangu kumalizika kwa Mkutano wa Awali wa Durban dhidi ya Ubaguzi miaka saba na nusu iliopita, waathirika wa mateso ulimwenguni bado wanaendelea kunyimwa hifadhi kwenye yale maeneo yenye uwezo wa kuupatia umma huo hali ya usalama.

22/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fujo za kikabila Sudan Kusini zaitia wasiwasi UNMIS

UNMIS United Nations mission in Sudan. UNMIS/Spanish Radio

Shirika la UM Linalosimamia Ulinzi wa Amani Sudan Kusini (UNMIS) limeripoti kuingiwa wasiwasi mkuu kuhusu usalama wa eneo, baada ya kufufuka tena kwa mapigano ya kikabila kwenye Jimbo la Jonglei, ambapo inaripotiwa mnamo mwisho wa wiki iliopita darzeni za watu waliuawa, wenziwao kadha wa kadha walijeruhiwa na wengine kulazimika kukimbia makazi na kuelekea kwenye maeneo jirani.

22/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizo ya Kipindupindu kusini mwa Afrika yaripotiwa kupungua na OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kuwepo mwelekeo wa kutia moyo kuhusu udhibiti wa maradhi ya kipindupindu kusini mwa Afrika. Ripoti imeeleza ya kuwa kasi ya maambukizo ya maradhi haya kieneo yanaendelea kuteremka.

22/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Mataifa Wanachama yanayohudhuria Mkutano wa Mapitio ya Mwito wa Durban Kupinga Ubaguzi Duniani, unaofanyika wiki hii Geneva, Ijumanne yalipitisha, kwa ridhaa ya wote, ule waraka wa mkutano, hatua ambayo ilipongezwa kidhati na KM Ban Ki-moon.

21/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yaadhimisha miaka 90

ILO-Logo

Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) linajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya kutimia miaka 90 tangu kubuniwa katika kipindi ambacho walimwengu hukabiliwa na mzozo mkuu wa fedha, ukichanganyika na ukosefu wa ajira.

21/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP inatayarisha mkutano wa kuzingatia upigaji marufuku madawa 12 ya kuuwa wadudu waharibifu

UNEP. DDT. UNEP/UN Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) linatazamiwa kuandaa mkutano maalumu Geneva kusailia tatizo la afya, linalosababishwa na aina 12 za madawa yanayotumiwa kuuwa wadudu waharibifu wa mazo, madawa ya kemikali ambazo husemekana zinahatarisha afya ya wanadamu na kusababisha maradhi thakili ya saratani.

21/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya raia waliongolewa makazi na mashambulio ya waasi wa FDLR yakithiri JKK kuhudharisha UNHCR

Nembo ya UNHCR

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumanne asubuhi aliwaeleza waandishi habari mjini Geneva kwamba mnamo wiki saba zilizopita idadi ya raia waliong’olewa makazi ilikithiri pomoni, kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya waasi wa kundi la FDLR, kwenye eneo la Lubero, Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).

21/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa UM kupinga ubaguzi waingia siku ya pili

Mkutano wa UM dhidi ya Ubaguzi wa Rangi Duniani unaofanyika mjini Geneva sasa hivi leo umeingia siku ya pili ambapo wawakilishi wa hadhi ya juu wamenedelea na mahojiano yao.

21/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon na Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu wameripotiwa kuchukuziwa na hotuba ya Raisi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mahmoud Ahmadinejad aliowasilisha Ijumatatu kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mapitio ya Mwito wa Durban na Mpango wa Utendaji wa Kupiga Vita Ubaguzi wa Rangi Duniani uliofanyika Geneva, Uswiss.

20/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano Dhidi ya Ubaguzi waanza rasmi Geneva

Mkutano wa UM juu ya Mapitio ya Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi wa Rangi Duniani umeanza rasmi hii leo mjini Geneva. Kwenye risala ya ufunguzi, KM Ban Ki-moon alieleza masikitiko juu ya uamuzi wa baadhi ya nchi wanachama, wa kutohudhuria kikao hiki, licha ya kuwa ushahidi uliopo umethibitisha dhahiri kwamba ubaguzi wa rangi ni tatizo ambalo linaendelea kuselelea, na kujizatiti katika maeneo kadha wa kadha ya ulimwengu.

20/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IFAD inasisitiza ruzuku kwa wakulima masikini ndio ufunguo wa kuuvua ulimwengu na mzoroto wa uchumi

IFAD

Kanayo Nwanzeon, Raisi wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ameyasihi mataifa yenye maendeleo ya viwanda kuharakisha misaada yao maridhawa kwa wakulima wadogo wadogo, hasa wale waliopo katika nchi masikini, ruzuku ambayo anaamini ikitekelezwa kidharura itasaidia sana kwenye zile juhudi za kuuvua ulimwengu na mzoroto wa uchumi uliotanda kimataifa sasa hivi.

20/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa yanayomiliki viwanda vya nyuklia yakutana Beijing kusailia sera ya karne ya 21

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeandaa Mkutano wa Kimataifa mjini Beijing, Uchina uliokusanyisha mawaziri 30 wa nishati pamoja na wajumbe kutoka nchi 65, kwa madhumuni ya kuzingatia matumizi ya nishati ya nyuklia kwa karne ya ishirini na moja.

20/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

UN Photo

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amepongeza maafikiano yaliokamilishwa, kwa mafanikio, na Kamati ya Matayarisho ya Mkutano wa Mapitio Kuhusu Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi wa Rangi.

17/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

JKK, Rwanda na UNHCR wajumuika kusailia taratibu za kurudisha makwao wahamiaji

Nemba ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti, kwa kupitia msemaji wake mjini Geneva, kuwa na matumaini ya kutia moyo, kufuatia uamuzi uliochukuliwa wiki hii na serikali za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) na Rwanda, wa kukubali kuwasaidia raia waliohamia nchi mbili hiz kurudi makwao, kufuatia misiba kadha wa kadha iliolivamia eneo la Maziwa Makuu katika siku za nyuma.

17/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umma wa nchi masikini utafadhiliwa msaada wa tiba rahisi ya malaria

Kutoka mji wa Oslo, Norway kumeanzishwa rasmi, leo Ijumaa, ushirikiano mpya wa kimataifa wa kuwasaidia mamilioni ya watu wanaogua maradhi ya malaria duniani, hasa wale wanaoishi katika nchi za Asia na mataifa ya Afrika kusini ya Sahara. Mradi huu utawapatia umma huo uwezo wa kumudu dawa za tiba ya malaria, dawa ambazo hunusuru maisha ya mgonjwa, hususan wale watoto wa umri mdogo.

17/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ametangaza sera mpya juu ya uhusiano wa kimataifa

Kwenye hotuba aliyoiwakilisha mbele ya wajumbe waliohudhuria warsha maalumu, leo asubuhi, katika Chuo Kikuu cha Princeton, kilichopo Jimbo la New Jersey, Marekani KM Ban Ki-moon alibainisha mtazamo wa sera mpya ya kimataifa juu ya uhusiano wa pande nyingi, miongoni mwa nchi wanachama.

17/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulio dhidi ya viongozi wa Usomali yalaaniwa na UM

Ahmedou Ould-Abdallah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, amelaani vikali mashambulio ya karibuni yaliofanyika Mogadishu yaliowalenga wabunge, hujumu ambazo alisema zilikusudiwa hasa kuzorotisha juhudi za Serikali mpya ya Usomali za kupitisha Bungeni kanuni za Sharia, pamoja na kukwamisha zile jitihadi za kurudisha utulivu na amani ya eneo.

17/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utatuzi Mbadala wa Mzozo wa Chakula Duniani

Mnamo wiki hii, David Nabarro, aliyeteuliwa kuongoza Tume ya UM juu ya Mzozo wa Chakula Duniani amehadharisha kwamba licha ya kuwa,katika siku za karibuni bei za chakula duniani ziliteremka kwa kiwango kikubwa sana, tukio hilo halikufanikiwa kuuvua umma wa nchi masikini na tatizo la njaa. Mamilioni ya watu duniani bado hawana uwezo wa kupata chakula kwa sababu ya mchanganyiko wa ufukara na mporomoko, usio wa kawaida, wa shughuli za uchumi, kijumla.

17/04/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Shirika la UM juu ya Huduma za Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limefungua rasmi vituo viwili vya uratibu kwenye miji ya Sake na Kiwanja, iliopo Jimbo la Kaskazini la Kivu, eneo ambalo makundi ya waasi wa Rwanda pamoja na wale wa FDLR bado wanaendelea kuhujumu raia.

16/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakaguzi wa IAEA wapigwa marufuku Korea ya Kaskazini

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeripoti kwamba wakaguzi wa UM waliohusika na uchunguzi wa shughuli za kiwanda cha nishati ya nyuklia, kiliopo kwenye mji wa Yongbyon, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini) wamelazimika kuondoka nchini Alkhamisi ya leo.

16/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya mtetezi wa Haki za Binadamu Burundi yalaaniwa na UM

Burundi map

Akich Okola, Mtaalamu Maalumu aliyeteuliwa na Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu kuchunguza utekelezaji wa haki za kiutu katika Burundi, ameripoti kuchukizwa sana na taarifa za mauaji ya Ernest Manirumva, Naibu-Raisi mzalendo wa shirika lisio la kiserikali linaloitwa OLUCOME, mauaji yaliotukia mjini Bujumbura, nyumbani mwa Manirumva, mnamo usiku wa tarehe 08 Aprili.

16/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matishio yanayokithiri ya uhalifu wa mipangilio yanazingatiwa na Kamisheni ya UM

UNODC

Kamisheni ya UM Inayohusika na Mahakama za Kesi za Jinai na Udhibiti wa Uhalifu Alkhamisi imefungua rasmi mjini Vienna, kikao cha 18 cha wawakilishi wa kimataifa kujadilia taratibu za pamoja, kukabiliana na tishio la uhalifu wa mipangilio dhidi ya utulivu na amani duniani.

16/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Liberia imefanikiwa kupunguza madeni iliorithi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe

UN Photo

Liberia imetangaza kuwa imefanikiwa kupunguza, kwa kiwango kikubwa sana, yale madeni inayodaiwa na nchi za kigeni yanayogharamiwa dola bilioni 1.2, baada ya Serikali kuamua kuyanunua madeni ya taifa yaliobakia, kwa bei iliopunguzwa kwa asilimia 97 ya thamani halisi ya madeni hayo.

16/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

António Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM Linalohudumia Wahamiaji (UNHCR) ametoa mwito unaohadharisha ya kuwa, mara nyingi wachuuzi wa biashara haramu ya magendo ya kutorosha wanadamu hulenga mawindo ya mateka wao zaidi kutoka lile fungu la wanadamu walio dhaifu kihali, ambao huwa wanadhalilishwa na kukandamizwa mara kwa mara na jamii zao. Kwa sababu hizi [...]

15/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

EU inashukuriwa na WFP kwa ulinzi wa misaada ya chakula kwa Usomali

Ramiro Lopes da Silva, Naibu Mkuu wa Operesheni za Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) ametoa taarifa maalumu, kutokea Makao Makuu ya ofisi zao yaliopo Roma, Utaliana iliyozishukuru nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa kufadhilia manowari kadhaa zinazotumiwa kuongoza meli zilizobeba msaada wa chakula wa WFP, na kuzikinga meli [...]

15/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakaguzi wa IAEA wapigwa marufuku Korea Kaskazini

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeripoti kupokea risala rasmi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini/DPRK) inayosema kwamba kuanzia Ijumanne ya tarehe 14 Aprili, inasitisha uhusiano na ushirikiano wote na wakaguzi wa IAEA waliopo kwenye viwanda vya nishati vya kinyuklia katika mji wa Yongbyon.

15/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna wa Haki za Binadamu kuihimiza jumuiya ya kimataifa kushirikiana kukomesha uovu wa ubaguzi wa rangi

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ameyasihi Mataifa Wanachama kujiepusha na alioitafsiri kuwa ni tabia karaha inayowakilisha “mawazo finyu ya kisiasa” na “ung’anga’niaji wa uzalendo”, na badala yake kuyataka mataifa yakamilishe maafikiano yanayokabiliwa na wote, ili kuendeleza mbele juhudi za pamoja za kupiga vita utovu wa ustahamilivu wa kitamaduni na uovu wa ubaguzi wa rangi duniani.

15/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mchango ziada wa kimataifa unahitajika dhidi ya maharamia, asema Mjumbe wa KM kwa Usomali

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdalla aliwasilisha taarifa maalumu kwa waandishi habari, kufuatia tukio la majuzi kuhusu mapambano na maharamia, nje ya mwambao wa Usomali. Alisema kwenye taarifa kwamba Mataifa Wanachama katika UM yanawajibika kukuza mchango wao katika kukabiliana na kile alichokiita “msiba mkuu wa kimataifa”, msiba ambao alidai “husababisha uharibifu mkubwa wa amani ulimwenguni.”

15/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa Usomali 60,000 warejea Mogadishu

desplazadosmogadishu capital somaliacnur radio spanish

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti raia 60,000 wamesajiliwa kurejea kwenye mji mkuu wa Usomali wa Mogadishu mnamo miezi mitatu ya mwanzo ya 2009, baada ya hali ya mapigano kupungua.

14/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Taarifa iliotolewa na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) imeeleza tishio la uharamia nje ya mwambao wa Usomali, ni tukio la kila siku, hali ambayo ilisababisha ucheleweshaji mkubwa katika kupeleka misaada ya chakula Usomali, na kwenye maeneo mengine ya Afrika mashariki na Afrika ya kati. Kwa mujibu wa taarifa ya WFP, [...]

14/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Baraza la Usalama lilifanyisha kikao rasmi Ijumatatu alasiri na kupitisha maafikiano yanayojulikana kama Tamko la Raisi kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea ya Kaskazini).

13/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Coomaraswamy atazuru JKK kusailia hifadhi bora kwa watoto

Radhika Coomaraswamy, Special Representative on Children in Armed Conflict, moderates the panel discussion on "Galvanizing action towards ending violence against women", to mark the International Day for the Elimination of Violence against Women, organize

Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Hifadhi ya Watoto kwenye Mazingira ya Uhasama na Mapigano, Radhika Coomaraswamy anatarajiwa kuzuru Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) kuanzia tarehe 14 Aprili mpaka 21, kufuatia mwaliko wa Serikali.

13/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa itafanyisha mkutano wa kuzingatia haki za binadamu Darfur

Kadhalika, kwenye mji mkuu wa Jimbo la Darfur Magharibi wa El Geneina, mnamo Ijumanne ya tarehe 14 Machi (2009) kutafanyika kikao cha pili cha kuzingatia namna Haki za Binadamu zinavyotekelezwa katika Darfur.

13/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID imeripoti hali ya usalama Darfur ni shwari

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limeripoti ya kuwa hali ya usalama kieneo, kwa hivi sasa, ni shwari licha ya kuwepo vitendo vya uharamia na wizi wa magari katika baadhi ya sehemu za Darfur Kaskazini na Magharibi.

13/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malawi inasonga mbele kujitegemea chakula

Malawi Derrick Mbatha

Taifa la Malawi limepania kujitegemea kwenye zile shughuli za kuzalisha chakula, kwa madhumuni ya kuepukana na ile hali ya kigeugeu inayozisumbua zaidi zile nchi masikini zenye kutegemea kufadhiliwa mchango wa chakula kutoka mataifa ya kigeni. Kuweza kulitekeleza lengo hilo Serikali ya Malawi iliamua kuchangisha mchango maalumu kutoka bajeti ka kitaifa, ikisaidiwa na UM, kuimarisha shughuli za kilimo nchini ambazo hudhibitiwa kwa taratibu zenye kuwasaidia zaidi wakulima wadogo wadogo.

10/04/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Tume ya UM ya Kuratibu na Kukadiria Maafa katika Namibia (UNADC) imeeleza kwenye ripoti iliokabidhiwa Serikali na Timu ya Maofisa Wakazi wa Mashirika ya UM, kwamba katika ordha ya vitu vinavyohitajika kuchangishwa kidharura, kukidhi mahitaji ya umma ulioathirika mafuriko yaliotukia karibuni nchini, ni pamoja na chakula, huduma za afya, maji safi na salama pamoja na makazi na mazingira ya usafi.

09/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yaanzisha sheria ya kuhifadhi haki ya mtoto

Watoto katika kambi ya Kalma

Raisi wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit alitazamiwa leo kuthibitisha rasmi, utekelezaji wa Sheria mpya ya Haki za Mtoto kwa Sudan Kusini.

09/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisa wa Haki za Binadamu wa UM aipongeza FNL Burundi kwa kuwaachia huru watoto wadogo

Radhika Coomaraswamy Special Representative of the Secretary-General for Children and Armed Conflict. UN Photo/Eskinder Debebe-UN Spanish Radio

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto kwenye Mazingira ya Mapigano ameripotiwa kuyakaribisha maamuzi ya wanamgambo wa FNL Burundi, ya kuwatenga watoto 112, ikijumlisha watoto wa kike wawili, kutoka kundi hilo na kuwavua na hatari ya kushirikishwa kwenye mapigano.

09/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suala la JKK lazingatiwa tena kwenye Baraza la Usalama

Security Council Middle East

Baraza la Usalama leo asubuhi lilikutana kwenye kikao cha hadhara kusailia hali, kwa ujumla, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK).

09/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa KM ataka kuchukuliwe hatua kali kimataifa dhidi ya uharamia Usomali

Wapatanishi wa Kimarekani wameripotiwa kujihusisha kwenye mazungumzo na maharamia wa Kisomali, ili kumwachia kapteni wa meli ya Marekani aliyeshikwa sasa hivi kwenye mashua ya kuokolea iliopo katika Bahari ya Hindi.

09/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

un flags 012b

Mahakama Maalumu juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone leo imetoa hukumu kwa viongozi watatu wa kundi la RUF, waliokutikana na makosa ya kushiriki kwenye jinai ya halaiki dhidi ya raia wasiokuwa na hatia. Issa Sesay amehukumiwa kifungo cha miaka 52, Morris Kalon amepewa adhabu ya kifungo cha miaka 40 na Augustine Gbao amehukumiwa [...]

08/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama linazingatia hali Guinea-Bissau

Security Council Middle East

Baraza la Usalama limekutana asubuhi kuzingatia ripoti ya KM kuhusu usalama na amani katika Guinea-Bissau, na pia kusailia shughuli za Ofisi ya UM inayohusika na Ujenzi wa Amani nchini humo.

08/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya UM juu ya Askari wa Kukodi yakamilisha uchunguzi Afghanistan

Afghanistan Russian Radio

Wajumbe wa UM wa Tume ya Kazi kuhusu matumizi ya Askari wa Kukodi, inayowakilishwa na Amada Benavides de Perez na Alexander Nikitin, imekamilisha ziara ya uchunguzi, ya siku tano katika Afghanistan baada ya kujadiliana na maofisa wa Serikali pamoja na wadau wengine husika kuhusu upeo na hali halisi ya shughuli za Majeshi ya Binafsi na Kampuni za Ulinzi na Usalama ziliopo Afghanistan sasa hivi na namna shughuli hizo zinavyoathiri utekelezaji wa haki za binadamu kitaifa.

08/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa kimataifa wathibitisha nishati anuwai ya viumbehai inahitajika kukuza maendeleo vijijini

Ripoti mpya kuhusu matokeo ya utafiti wa kimataifa juu ya matumizi ya nishati kwa wanavijiji, iliotolewa wiki hii, na kuchapishwa bia na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) pamoja na Idara ya Uingereza Inayohusika na Maendeleo Kimataifa (DFID) imethibitisha ya kuwa pindi uzalishaji wa japo kiwango kidogo cha nishati kutoka anuwai ya viumbehai utatekelezewa jamii za kienyeji, kadhia hiyo ina matumaini ya kuimarisha, kwa kiwango kikubwa, shughuli za maendeleo vijijini, hasa katika nchi masikini.

08/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

B. Lynn Pascoe, Naibu KM juu ya Masuala ya Kisiasa aliwasilisha, asubuhi, kwenye kikao cha faragha cha Baraza la Usalama, ripoti fafanuzi kuhusu hali ya wasiwasi iliojiri baina ya mataifa ya Djibouti na Eritrea. Kadhalika Pascoe aliwakilisha taarifa kuhusu mtafaruku wa kisiasa uliojiri Bukini mnamo wiki za karibuni. Baada ya mashauriano ziada miongoni mwa wajumbe [...]

07/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takwimu ziada juu ya tetemeko la ardhi Utaliana

Ripoti za Ofisi ya UM juu ya Misadaa ya Dharura (OCHA) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinakadiria idadi ya vifo vnavyoambatana na zilzala kali iliopiga karibuni kwenye eneo la kati, na katika mji wa L’Aquila, Utaliana limefikia 207.

07/04/2009 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkariri wa UM kuhusu mauaji nje ya mahakama ashtumu vyombo vya sheria Kenya

Mr. Philip Alston, United Nations Special Rapporteur on extrajudicial, summary or arbitrary executions. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Profesa Philip Alston, aliye Mkariri Maalumu wa UM dhidi ya Mauaji Nje ya Taratibu za Mahakama amewasilisha ripoti ilioshtumu vikali vyombo vya sheria Kenya, ambavyo alidai hushiriki kwenye vitisho vya mpangilio na mabavu dhidi ya watetezi wazalendo wa haki za binadamu, hasa wale watetezi waliotoa ushahidi kwa tume ya uchunguzi ya UM juu ya ukiukaji wa haki hizo.

07/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kumbukumbu ya miaka 15 ya mauaji ya Rwanda kuadhimishwa na UM

Kadhalika, tarehe 07 Aprili 2009 inaadhimisha miaka 15 ya mauaji ya halaiki yaliotukia Rwanda katika 1994.

07/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Afya Bora Duniani kwa 2009

Nembo ya WHO

Tarehe ya Aprili 07, huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni Siku ya Afya Bora Duniani. Mwaka huu kumetolewa mwito maalumu na UM unaozihimiza serikali za kimataifa, kuwekeza zaidi kwenye mahospitali na kwenye vifaa na nyenzo nyengine za kutunza afya, vifaa ambavyo ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya umma wenye kuathirika na matatizo ya kiutu.

07/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Hapa na pale

06/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahudumia misaada ya kiutu Darfur watekwa nyara

Wafanyakazi wa kike wawili wenye kuhudumia misaada ya kihali Darfur Kusini, wanaowakilisha mashirika yasio ya kiserikali ya Ufaransa, Ijumapili usiku, walitekwa nyara kutoka makazi yao baada ya kushikiwa bunduki wao na walinzi, na majambazi wasiotambulika.

06/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mijadala leo katika Makao Makuu

Baraza la Udhamini leo linazingatia suala la mgogoro wa chakula duniani, na pia kujadilia sera za kutumiwa, kipamoja, na Mataifa Wanachama ili kuhakikisha haki ya mwanadamu kupata chakula hutekelezewa umma wa kimataifa kote ulimwenguni.

06/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya afya duniani 2009 kuadhimishwa 07 Aprili

World Health Day 7 April 2008

Ijumanne ya tarehe 7 Aprili huhishimiwa kimataifa kuwa ni Siku ya Afya Bora Duniani. Taadhima za 2009 zitalenga zaidi kwenye zile juhudi za kuimarisha usalama wa vifaa na nyenzo za kuhudumia afya ulimwenguni, na pia kwenye uwezo wa wahudumia afya katika mazingira ya tiba ya dharura.

06/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM asikitishwa na urushaji wa kombora angani na Korea Kaskazini

Ofisi ya Msemaji wa KM, kwenye ripoti iliotoa Ijumapili kwa waandishi habari, kuhusu kitendo cha kurusha kombora angani kilichofanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini) hapo jana, taarifa hiyo ilibainisha masikitiko aliyokuwa nayo KM Ban Ki-moon juu ya kitendo cha Korea Kaskazini, ambacho alisema ilikwenda kinyume kabisa na nasaha za jumuiya ya kimataifa.

06/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Uamuzi wa Kamisheni ya Uchaguzi wa Taifa Sudan (NEC) wa kufanyisha uchaguzi mkuu wa nchi katika mwezi Februari 2010, ni tangazo liliopokelewa kwa ridhaa kuu na KM, na amekitafsiri kitendo hicho kuwa ni kigezo muhimu katike utekelezaji wa Maafikiano ya Jumla ya Amani nchini.

03/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wa Afya wakubaliana Beijing kuharakisha udhibiti bora wa TB sugu

Russian Radio

Mkutano wa siku tatu, ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Umma wa Uchina pamoja na Taasisi za Bill na Melinda Gates, ulifanyika Beijing wiki hii, kwa makusudio ya kushauriana juu ya mradi mpya wa utendaji, utakaofaa kutekelezwa kipamoja ili kudhibiti bora maradhi ya kifua kikuu, hususan kwenye yale mataifa yanayosumbuliwa zaidi na ugonjwa huo.

03/04/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uamuzi wa Kenya kuwarejesha wahamiaji Usomali waitia wasiwasi UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kuingiwa wasiwasi kuhusu mtindo wa karibuni wa Serikali ya Kenya wa kuwarejesha kwa nguvu Usomali, wale wahamiaji wenye kuomba hifadhi.

03/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa wanachama kuashiria mafanikio ya kuridhisha kuhusu Mkutano wa Durban

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu imearifu kuwa wawakilishi wa serikali wanachama wana imani ya kupatikana mafanikio ya kuridhisha katika kikao kijacho cha mapitio kuhusu masuala ya ukabila, ubaguzi wa rangi, matatizo ya chuki dhidi ya wageni na utovu wa kustahamiliana kitamaduni.

03/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jaji wa Afrika Kusini ameteuliwa kuongoza tume ya uchunguzi juu ya ukiukaji sheria za kiutu Ghaza

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu limetangaza kumteua Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini kuongoza ile tume huru ya kuchunguza ukweli kuhusu ukiukaji wa sheria ya kimataifa juu ya haki za binadamu, na uvunjaji wa haki za kiutu, uliofanyika wakati mgogoro wa eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza ulipopamba mnamo miezi kichache iliopita.

03/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabomu yaliotegwa yaendelea kuhatarisha watoto, kuonya UNICEF

The Mine Action Programme of Afghanistan (MAPA) has cleared 38,297 anti-personnel mines, 419 anti-tank mines, 957,362 Explosive Remnants of War (ERW) and 65,361,363 square meters of land across the country.

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba mabomu yaliotegwa ardhini, pamoja na mabaki ya silaha zilizowachwa kwenye eneo la mapambano baada ya vita kumalizika, ni viripuzi vinavyoendelea babdo kuhatarisha maisha ya watoto katika kadha wa kadha ulimwenguni.

03/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

kwenye Mkutano Mkuu London na viongozi wa mataifa yenye uchumi mkuu, wanachama wa Kundi la G-20, uamuzi ambao waliahidi watachangisha furushi la dola trilioni 1.1, za kutumiwa kusuluhisha mzozo wa kiuchumi na fedha uliouvaa ulimwengu kwa hivi sasa. KM alitumai maafikiano ya G-20 yatayazipatia nchi masikini msaada maridhawa wa kufufua tena shughuli zao za maendeleo ya uchumi na jamii, kitaifa, kwenye maeneo yao.

02/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA imezikaribisha ahadi za Maraisi wa Urusi na Marekani kuzuia uenezaji wa silaha za kinyuklia duniani

Mohamed ElBaradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) ameingiwa matumaini makubwa na amezikaribisha ahadi za pamoja, zilizotolewa wiki hii na Raisi Dmitry Anatoleyevich Medvedev wa Shirikisho la Urusi pamoja na Raisi Barack Obama wa Marekani za kuchukua hatua hakika kutekeleza majukumu yao, chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Kinyuklia Duniani ili, hatimaye, kuuwezesha ulimwengu kuwa huru dhidi ya silaha za maangamizi ya halaiki za kinyuklia.

02/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wabuni sera za kimataifa wahimizwa na FAO kuwashirikisha wakulima kwenye mijadala ya Mkataba wa Kyoto

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limetoa taarifa yenye kuwahimiza wabuni sera za kimataifa kuhusu udhibiti wa athari za mabadiliko ya hali hewa duniani kujumuisha suala la kilimo pale wanapozingatia mkataba mpya utakaofuatia Mkataba wa 1997 wa Kyoto, baada ya kukamilisha muda wake.

02/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kukumbushana Ugonjwa wa Autism yaadhimishwa na UM

UM leo unaadhimisha Siku ya Kukumbushana juu ya Ugonjwa wa Akili wa Watoto au kwa Kiingereza chake ugonjwa wa autism.

02/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuchangisha msaada wa kuihudumia Namibia kudhibiti athari za mafuriko

UM unajishughulisha hivi sasa kuchangisha dola milioni 2.7 zinazohitajika kuisaidia Jamhuri ya Namibia kudhibiti bora athari za mafuriko nchini, yaliosababishwa na mvua kali za karibuni ambazo zilin’goa makazi watu 13,000 na pia kuharibu majumba na njia za kujipatia rizki kwa jumla ya watu 350,000.

02/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

View of the United Nations Building UN Spanish Radio

KM Ban Ki-moon amewasili London leo hii kuhudhuria mkutano mkuu wa mataifa wanachama wa kundi la G-20.

01/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji walionusurika mwambao wa Libya wameripoti ajali yao ilisababishwa na hewa mbaya na woga wa abiria

Wale wahamiaji waliokolewa kutoka mashua ya wafanya magendo, iliopinduka mwanzo wa wiki nje ya mwambao wa Libya, wamewaambia wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) ya kuwa boti yao ilizama kwa sababu ya matatizo ya hali ya hewa mbaya, ikichanganyika na woga pamoja na khofu kubwa iliowavaa abiria, walipogundua kuvuja kwa mashua yao.

01/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya majongoo ya pwani imepungua ulimwenguni, yahadharisha FAO

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti ya kuwa akiba ya majongoo wa pwani, au madondo, inaelekea kupungua ulimwenguni kwa kima cha kushtusha, hasa katika maeneo ya Afrika na kwenye Bahari ya Hindi ambapo uvuvi wa majongoo hawa imekiuka ada.

01/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa nchi 30 ziada wakutana Beijing kuzingatia tiba ya TB sugu

Mawaziri wa afya pamoja na wajumbe wa kutoka nchi 30 ziada wameanza kikao cha siku tatu mjini Beijing, Uchina kuzingatia namna ya kukabiliana na tatizo la kuemewa na maradhi sugu ya kifua kikuu yasiokubali dawa.

01/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNDP inayahimiza mataifa ya kundi la G-20 kuzingatia mahitaji ya umma wa nchi masikini kwenye majadiliano yao

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) wiki hii limetoa taarifa maalumu kwa viongozi wa mataifa wanachama wa kundi la G-20, wanaokutana Alkhamisi mjini London, yenye kuwakumbusha ya kuwa mgogoro wa uchumi duniani huathiri zaidi maendeleo na maisha duni ya umma uliopo katika nchi masikini.

01/04/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930