Nyumbani » 31/03/2009 Entries posted on “Machi, 2009”

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

KM Ban Ki-moon amesema juhudi kubwa zaidi zinahitajika kote duniani kukomesha ghasia dhidi ya wanawake na wasichana, hasa kwa kuwahusisha zaidi wanaume na wavulana.

31/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM-uchaguzi wenye kasoro hatari kwa Afganistan

KM Ban ki-moon ameonya kwamba uchaguzi utakaokua na kasoro huko Afghanistan utaweza kurudisha nyuma maendeleo yaliyopatikana, akitoa mwito kwa jumuia ya kimataifa kusaidia juhudi za kuimarisha uthabiti katika taifa hilo linalokumbwa na ghasia.

31/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuungana na kamati kubuni mpya kazi za mazingira

Chinese Unit

Mpango huo unatokana na jibu kwa pendekezo la waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, wakati wa mkutano wa viongozi wa Jopo la Uchumi huko Davos, Uswisi mwezi Januari, wa kundwa kwa kamati maalum ya kupunguza kiwango kikubwa cha utowaji gesi za carbon.

31/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada kamili unahitaji kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria

malaria; mosquito;  The Global Fund

Ni lazima kugharimia kikamilifu Fuko la Global Fund kuweza kupambana dhidi Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria ikiwa nchi zinabidi kufikia lengo la kumpatia kila mtu Duniani uwezo wa kujikinga kutokana na HIV, matibabu, msaada na kuhuduma alisisitiza mkuu wa Shirika la UM la kupambana na Ukimwi UNAIDS.

31/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imeshtushwa na vifo vingi vya wahamiaji huko Mediterrenean

Nemba ya UNHCR

Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR limeelza kushtushwa kutokana na ripoti za kufariki na kupotea mamia ya wahamiaji nje ya pwani ya Libya walipokua wanajaribu kutafuta maisha mepya Ulaya.

31/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuzorota ghasis huko Afrika ya kati kunasababisha maelfu kukimbia makazi yao

ocha

Kuongezeka kwa mapigano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kumesababisha maelfu ya wakazi kukimbia kutoka makazi yao kufuatana na idara ya huduma za dharura ya UM.

31/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waonya kua vitongoji vya maskini kuongezeka mara tatu kutokana na mizozo ya kiuchumi

Akiufungua mkutano wa 22 wa shirika la Makazi la UM, UN Habitat, Makamu Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka alisema, kuna haja ya kusisitiza juu ya mipango na kugharimia ujenzi wa nyumba ambazo watu wa tabaka la chini wanaweza kumudu, ili kuweza kupata maendeleo ya kudumu katika miji.

30/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO kupambana na ukame pembe ya Afrika

africa drought 06b

Kwa ushirikiano na Makundi yasiyo ya Kiserekali na Umoja wa Ulaya EU, Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, linafanya kazi kukabiliana na matatizo msingi yanyosababisha njaa huko Pembe ya Afrika.

30/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atowa mwito wa msaada zaidi kwa juhudi za kupambana na UKIMWI, TB NA Malaria

Katika wakati huu wa misukosuko ya kiuchumi, kugharimia vita dhidi ya UKIMWI, Kifua kikuu na Malaria ni uwekezaji wa busara, alisema KM Ban Ki-moon hii leo alipowahimiza wafadhili kugharimia juhudi za UM kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo ya hatari.

30/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM yafungua vituo viwili vya uwokozi Bahari ya Hindi

Shirika la kimataifa la Safari za Baharini la UM IMO limefungua vituo viwili vipya vidogo vya kutafuta na kuokoa maisha ya watu baharini huko Tanzania na Ushelsheli, njee ya pwani ya Afrika ya Mashariki.

30/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Annan atoa mwito wa hatua za haraka za mageuzi Kenya

Kofi Annan U.N. Spanish Radio

Viongozi wa kisaisa kutoka Kenya na wa Mashirika yasiyo ya Kiserekali wanakutana mjini Geneva, kutokana na mwaliko wa KM wa zamani wa UM Kofi Annan kujadili juu ya matokeo ya utawala wa muungano nchini humo, baada ya ghasia zilizotokea kufuatia uchaguzi mkuu wa Disemba 2007.

30/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majadiliano muhimu ya mkataba mpya wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa yaanza

UNEP. Greenhouse gas. UNEP/UN Spanish Radio

Zaidi ya wajumbe elfu 2 kutoka serekali, biashara na viwanda, watetezi wa mazingira na taasisi za utafiti wanakutana mjini Bonn Ujerumani kuanza majadiliano ya kwanza kati ya vikao vitatu kwa lengo la kutayarisha mswada wa makubaliano utakaochukua nafasi ya mkataba wa Kyoto wa kupunguza gesi za sumu Greenhouse unaotazamiwa kumalizika 2012.

30/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi za UM za kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

Children RD Congo Monuc

Leo hii, tunazungumzia kazi za afisi inayosimamia juhudi kubwa kabisa za kulinda amani za UM huko Africa na kugharimu karibu dola bilioni moja, MONUC.

30/03/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

KM Ban Ki-moon amewahimiza watu wote kuungana na UM na mamilioni ya watu kote duniani kupeleka ujumbe kwa viongozi wa serekali zao kulinda mazingira ya Dunia kwa kuzima taa kwa saa moja Jumamosi usiku.

27/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahutubia mkutano maalumu wa Afghanistan Moscow

KM Ban Ki-moon ameonya kwamba ugaidi, biashara haramu ya madawa ya kulevya na uhalifu wa megeni ni mambo yanayozuia maendeleo ya wananchi wa Afghanistan.

27/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban anasema mataifa yanayoendelea yanahitaji dola trilioni

KM wa UM Ban Ki-moon amewambia viongozi wa mataifa tajiri kabla ya mkutano wa G20 kwamba, mataifa yanayoendelea yanahitaji dola trillion moja kuweza kukabiliana na mzozo mkubwa wa fedha duniani.

27/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko makubwa kusini mwa Afrika yasabisha hasara kubwa

floods_people

Mvua nyingi zimesababisha mafuriko huko Angola, Namibia, Zambia Madagascar Msumbiji, Malawi na Botswana.

27/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano mpya wa Finland na UM kulinda misitu

Shirika la Chakula na Kilimo FAO na serekali ya Finland zimezindua mpango mpya wa miaka minne, utakaogharimu dola milioni 14 kwa lengo la kusiadia nchi zinazoendelea kulinda rasilmali yao ya misitu na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

27/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR – Wasomali wazidi kukimbilia Kenya

Maelfu ya wa Somali wanaendelea kukimbilia kaskazini mashariki ya Kenya kutafuta hifadhi katika makambi ya wakimbizi yaliyofurika watu ya Dadaab, licha ya kuwepo na serekali mpya Mogadishu na kupunguka kwa ghasia nchini humo.

27/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Maafisa wa idara ya huduma za dharura ya UM wamepongeza ushirikiano wa maafisa wa serekali ya Sudan katika kutathmini mahitaji ya huduma za dharura katika jimbo lenye ghasia la Darfur, wakati huo huo wakionya juu ya hatari zilizopo kufuatia kufukuzwa makundi muhimu ya misaada.

26/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

AU-UM wasafirisha vifaa vya mtihani kwa wanafunzi Darfur

Afisi ya pamoja ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika AU na UM huko Darfur UNAMID imesaidia hii leo kusafirisha kwa ndege vifaa vya mtihani kwa shule za secondary za maeneo ya mbali katika jimbo hilo la magharibi ya Sudan linalokumbwa na ghasia.

26/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yasisitiza haja ya kubuniwa ajira wakati wa kufufua uchumi

Mr. Juan Somavia, Director-General of the International Labour Organization. UN PHOTO / Spanish Radio

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani ILO amezihimiza serekali za dunia kulenga mipango yao ya kuokoa uchumi katika tatizo la muda mrefu linaloendelea, la ukosefu ajira.

26/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amewasili Moscow kabla ya mkutano juu ya Afghanistan

Ban Ki-moon

KM Ban Ki-moon amewasili Moscow mji mkuu wa Rashia kabla ya kuhudhuria mkutano wa kwanza kati ya mbili juu ya Afghanistan.

26/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM, UNHCR, watoa chombo kuwaelimisha wahamiaji wepya ulaya

IOM Bus

Katika juhudi za kuwaelimisha wahamiaji wepya wanaoingia nchi za Umoja wa Ulaya EU, Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR, likishirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, na msaada kutoka EU wamezindua hii leo chombo kipya chenye jina la “Not Just Numbers” siyo takwimu pekee.

26/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuwasaidia wapiganaji wa zamani Sudan kurudi maisha ya kawaida

Waasi Sudan

Zaidi ya wapiganaji wa zamani 180 000 katika vita vya zaidi ya miongo miwili vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na kusini huko Sudan, watasaidiwa kurudi katika maisha ya kawaida, wakati zowezi la kuwapokonya silaha inaingia awmu mpya.

26/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wa mjini kupata msaada kutoka mpango mpya wa UM

U.N. Habitat logo U.N. Habitat/U.N. Spanish Radio

Kutokana na hali kwamba karibu robo tatu ya wakazi bilioni moja wa dunia wanaoishi kwenye vitongoji vya ufukara ni vijana chini ya miaka 30, shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa limeanzisha mradi mpya wa kuwezesha makundi ya kijami yanayongozwa na vijana.

25/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za kuimarisha chakula Benin zapongezwa na mtaalamu wa UM

UN Photo

Mtaalamu wa UM juu ya haki ya kupata chakula, Olivier De Schutter amepongeza juhudi za Benin kuimarisha usalama wa chakula huku akisisitiza kwamba juhudi hizo zinabidi pia kuimarisha hali ya maisha ya wakazi maskini.

25/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM atoa mwito wa kuachiwa wafanyakazi wa UM

KM Ban Ki-moon, akiungana pamoja na wafanyakazi wengine wa UM wametoa mwito hii leo kuachiliwa huru wafanyakazi 19 wa UM wanaoshikiliwa au hawajulikani walipo kote duniani.

25/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

China kusaidia mataifa yanayoendelea katika kilimo

fao-logo-gde

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, limesema kwamba China imeingia katika jumuia ya wafadhili wa kuu wa shirika hilo, kwa kutoa dola milioni 30 kuanzisha fuko maalumu la kuimarisha uzalishaji chakula katika nchi zinazoendelea.

25/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imegundua ni Wangola wachache wanaotaka kurudi nyumbani

Nembo ya UNHCR

Utafiti mpya wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la UM UNHCR, na serekali ya Zambia umegundua kwamba ni wakimbizi 251 wa ki-Angola kati ya elfu 10 katika kambi ya wakimbizi ya Mayukwayukwa, wenye haja ya kurudi nyumbani mwaka huu licha ya kampeni inayowahimiza kufikiria kurudi nyumbani.

25/03/2009 | Jamii: Habari za wiki, Jarida | Kusoma Zaidi »

Mahojiano na Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya Hassan Omar

Map of Kenya. UNICEF/Un Spanish Radio

Muasisi wa kundi la kutetea Haki za Binadamu “Oscar Foundation”, Oscar Kamau Kingara aliuliwa pamoja na mshauri wake wa habari John Paul Oulu wakiwa garini karibu na chuo kikuu cha Nairobi.

25/03/2009 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

KM amelaani shambulio la kigaidi huko Lebanon

KM Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi jana lililosababisha kifo cha Kamal Medhat, naibu mkuu wa chama cha ukombozi wa Palestina PLO huko Lebanon, na baadhi ya walinzi wake.

24/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF kuwachanja watoto Rwanda

Nembo ya UNICEF

Wizara ya afya ya Rwanda ikisaidiwa na shirika la Watoto la UM, UNICEF, imezindua kampeni ya pili ya wiki moja, kuwahi kufanywa nchini humo ya kuwapatia kinga watoto na kina mama kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiliwa kwa urahisi.

24/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu saba wapoteza maisha katika ajali nje pwani ya Yemen.

somali refugees flee to the gulf of aden, yemen

Kiasi ya wahamiaji saba wa Kiafrika walizama na kufariki mwishoni mwa wiki wakati meli ya biashara ya magendo walokua wanasafiria ilipozama muda mfupi tu baada ya kutia n’ganga kwenye bandari ya Aden huko Yemen.

24/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum apongeza mkataba na waasi huko DRC

Wakimbizi wa Dr Congo

Mjumbe maalum wa UM huko JKK amesifu makubaliano yaliyotiwa sahihi Ijumatatu kati ya serekali ya Kinshasa na kundi la waasi lililokua likiendesha mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao huko mashariki ya nchi mwaka jana.

24/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban anasema kiwango cha uwambukizaji wa kifua kikuu kinapungulia

Akiadhimisha siku ya kifua kikuu duniani hii leo, KM Ban Ki-moon amesema kasi za kupungua ugonjwa wa kifua kikuu zinakwenda pole pole na kuonya kua juhudi za kupambana na ugonjwa huo zinapunguka.

24/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

View of the United Nations Building UN Spanish Radio

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Dominique Strauss-Khan ametoa mwito wa ushirikiano mkubwa zaidi kati ya IMF na Shirika la Kimataifa la Kazi ILO, akisema ushirikiano kati ya taasisi za kimataifa ni muhimu katika kukabiliana na mzozo wa uchumi.

23/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Sudan atembelea Eritrea bila ya kukamatwa

Ocampo na Al-Bashir

Rais Omar Al-Bashir wa Sudan amabae amefunguliwa mashtaka na Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC, alipokelewa na kiongozi mwenzake Isaias Afwerki wa Eritrea na wananchi, licha ya kwamba kuna hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake.

23/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pendekezo la FAO la Mkutano wa Viongozi juu ya Mzozo wa Chakula lapata Nguvu

Nembo ya FAO

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, limesema kwamba pendekezo la kuitisha mkutano wa viongozi duniani mwishoni mwaka 2009 juu ya mzozo wa chakula, ambao unazidi kuzorota katika nchi maskini, linapata nguvu na kupewa umuhimu mkubwa.

23/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM yaadhimisha Siku ya Utabiri wa Hali ya Hewa

montage of climate change pictures

Ikiadhimisha siku ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani leo Jumatatu, Idara ya UM ya kutabiri hali ya hewa WMO, inazingatia juu ya uchafuzi wa hewa duniani, kutokana na takwimu kwamba, kiasi ya watu milioni mbili duniani hufariki mapema kutokana na hewa chafu kila mwaka.

23/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban anapongeza kuachiliwa mfanyakazi moja wa UM huko Niger

KM Ban Ki-moon amepongeza hii leo kauchiliwa huru mfanaykazi mmoja wa UM aliyetekwa nyara Niger mwishoni mwa mwaka jana na akarudia tena mwito wake wa kuachiliwa huru wafanyakazi wengine wawili pamoja na mwakilishi wa UM nchini humo, Robert Fowler kutoka Canada.

23/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM anasema ni lazima dunia kufanya kazi pamoja kutumia maji kwa busara

KM wa UM Ban Ki-moon amesisitisza umuhimu wa maji kama nguvu za kungana pamoja kuliko kiungo cha mizozo, akihimiza kwamba mustakbala wa pamoja wa dunia unategemea jinsi inavyosimamia rasilmali yake hii tunu.

23/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto, ya Tanzania Bi. Mariam Joy Mwaffisi

Wajumbe kwenye mkutano wa Kamisheni juu ya Hali ya Wanawake walijadili kwa mapana marefu namna ya kuhamasisha haja ya wanawake na wanaume kufanya kazi pamoja katika majukumu ya malezi, kuwahudumia waathiriwa wa HIV na Ukimwi, pamoja na majukumu ya nyumbani.

20/03/2009 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mahojiano na Bw M'Bisima Ntakobajira, Mtetezi wa Haki za Binadamu huko Bukavu DRC

carte geographique Sud Kivu RDC; map; DRC; South Kivu RADIO OKAPI

Abdushakur Aboud amezungumza na mtetezi wa haki za binadamu, Mwenyekiti wa Kundi la Kutetea na Kulinda Haki za Binadamu huko Bukavu, Bw M’Bisima Ntakobajira, anaethbitisha kuzorota kwa Haki za Binadamu nchini DCR.

20/03/2009 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban aondoka kwa ziara ya mataifa sita ya Ulaya na Mashariki ya Kati

KM Ban Ki-moon ataanza ziara ya mataifa sita ya Ulaya na Mashariki ya Kati akianza huko Rashia ambako mjini Moscow atahudhuria mkutano juu ya Afghanistan.

20/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mvua kali ya tishia mafuriko zaidi huko Namibia na Angola

ocha

Idara ya Huduma za Dharura ya UM OCHA, inasema mafuriko yanayotokea huko Namibia na Angola kutokana na mvua kali za wiki tano zilizopita yanahatarisha kueneza magonjwa ya kipindupindu na malaria.

20/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa ya kukomesha Ubaguzi wa Rangi

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay amesema mamilioni ya watu kote duniani wanaendelea kua wathirika wa ubaguzi wa rangi na kikabila.

20/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utawala na uthabiti unaanza kurudi Somalia asema Mjumbe Maalum wa UM

Akiliarifu Baraza la Usalama juu ya hatua za kuchukuliwa katika kutekeleza makubaliano ya Djibuti, huko Somalia, Mjumbe Maalum wa UM amesema utawala wa kisheria umeanza kurudi huko Mogadishu, kukiwepo na serekali na taasisi za utawala zinazo tambuliwa kikanda, kimataifa na idadi kubwa ya wa-Somali.

20/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR inasema mashambulio mepya ya waasi ya wakimbiza raia DRC

Dozens of Congolese refugees wait to be processed at Ishasha in Uganda. © UNHCR/J.Akena UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UM UNHCR limetangaza Ijumaa kwamba mashambulio yanayofanywa na waasi wa kihutu kutoka Rwanda yanaendelea kusababisha watu kukimbia makazi yao huko mashariki ya JKK.

20/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki za Binadamu za zorota DRC

MONUC

Mapema wiki hii naibu Kamishna wa Haki za Binadamu Kyung-wha Kang ameliambia Baraza la haki za Binadamu mjini Geneva ingawa dunia nzima imekua ikizingatia juu ya ugomvi katika eneo la mashariki lenye ghasia huko JKK, ukiukaji wa haki za binadamu umekua ukitokea katika sehemu nyenginezo za taifa hilo kubwa la Afrika.

20/03/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Mjumbe Maalum wa UM huko JKK, Alan Doss amesema, ili kukomesha udhalilishaji na utumiaji nguvu wa ngono uloenea huko mashariki ya Kongo, ni lazima kusitisha shughuli za makundi yenye silaha, lakini pia kuhakikisha vikosi vya usalama vina nidhamu kamili.

20/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wachumi wataka UM kuchukua uwongozi wa mageuzi ya kanuni za masoko huru

UNCTAD logo UNCTAD/UN Radio Spanish

Wachumi kutoka shirika la biashara la UM UNCTAD wametoa mwito kwa UM kuchukua uwongozi katika mageuzi ya masharti na kanuni za masoko huru, katika juhudi za kuufufua uchumi duniani.

19/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO inaeleza kwamba bei za chakula katika nchi maskini zingali juu

FAO logo U.N. Spanish Unit

Shirika la chakula na kilimo la UM FAO limesema takwimu za bei za chakula katika mataifa 55 yanayoendelea kuanzia Afghanistan hadi Zimbabwe zingali juu kuliko bei zilizoko katika masoko ya kimataifa.

19/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID inaeleza kuongezeka kwa uhalifu huko Darfur

Afisi ya pamoja ya UM na Au ya kulinda amani huko Darfur UNAMID, imeripoti hii leo kuongezeka kwa vitendo vya wizi wa utumiaji nguvu, uhalifu, uvamizi dhidi ya wafanyakazi wa UM na raia katika maeneo yote ya jimbo la Darfur huko Sudan.

19/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya tahadhari yatangazwa Namibia kutokana na mafuriko

Rais wa Namibia ametangaza hali ya hatari nchini mwake kufuatia mafuriko mabaya kutoka nchini muhimo na kusababisha vifo vya karibu watu 90 na elfu 5 kupoteza makazi yao.

19/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahimiza uhusiano imara kati ya UM na AU

Jopo la pamoja la UM na AU kutayarisha mkakati wa ushirikiano kati ya jumuia hizo mbili hasa katika masauala ya kulinda amani limewasilisha ripoti yake mbele ya Baraza la uUalama.

18/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unatafuta dola milioni 244 kuimarisha msaada wa chakula Kenya

Nembo ya WFP

Idara ya Chakula Duniani WFP, imetoa mwito Jumatano wa kuchangisha dola milioni 244 ilikuimarisha kazi zake huko Kenya, ambako bei za juu za chakula na ukame zimesababisha watu milioni 3 na nusu kuhitaji mdsaada.

18/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpango wa dola milioni 18 UM kusaidia mataifa matano kupunguza gesi za sumu

World Bank

Mataifa matano ya Afrika, Asia na Amerika ya Kati yatapokea jumla ya dola milioni 18 kutoka mradi mmoja wa majaribiyo wa UM wenye lengo la kupunguza gesi za sumu za greenhouse kutoka misitu na kuimarisha hali ya maisha ya wakazi.

18/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matumaini ya mafanikio kwenye mkutano wa ubaguzi mwezi ujao

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UM, BI Navi Pillay, ameeleza matumaini yake Ijumatano ya kuwepo na maridhiano miongoni mwa mataifa wanachama kwenye mkutano wa mwezi ujao wa kupambana na ubaguzi, kutokana na kutolewa mswada mpya mfupi wa rasimu ya hati ya mwisho ya mkutano.

18/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS yahimiza mipango ya mchanganyiko kupambana na UKIMWI

unaids prevention HIV 024a

Kukiwepo na zaidi ya watu 7 400 kila siku wanao ambukizwa na virusi vya HIV, shirika la kupambana na UKIMWI la UM UNAIDS, linasema ni lazima kuwepo na mkakati wa kIchanganyiko ikiwa ni pamoja na utumiaji mipra ya kondom kama chombo muhimu kuzuia kuenea kwa janga la UKIMWI.

18/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

KM Ban Ki-moon amezihimiza pande zote huko Madagascar kuhakikisha utulivu na mpito makini wa kidemokrasia kufuatia kujiuzulu kwa Rais Marc Ravalomanana.

18/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa Japan kwa kusaidia kukabiliana na athari za mzozo wachakula Africa

IOM Bus

Msaada wa dola milioni 16 kutoka kwa serekali ya Japan, utaweza kulisaidia shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, kukabiliana na baadhi ya athari kutokana na mzozo mkubwa wa chakula unaowakabili wahamiaji huko Pembe ya Afrika pamoja na Mashariki na Kusini ya bara hilo.

17/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlinda Amani wa UNAMID auliwa huko Darfur

Mlinda amani wa kikosi cha pamoja cha UM na Umoja wa Afrika UNAMID huko Drafur ameuliwa katika shambulio la kushitukiza.

17/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna wa Haki za Binadamu anatoa ripoti juu ya kazi zake DRC

Kyung-wha Kang

Naibu kamishna wa Haki za Binadam alitoa ripoti ya kamishna mkuu juu ya hali ya haki za binadam na kazi za afisi hiyo huko JKK.

17/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Madagascar astahafu na kukabidhi majeshi madaraka

KM Ban Ki-moon amezihimiza pande zote huko Madagascar kuhakikisha utulivu na mpito makini wa kidemokrasiakufuatia kujiuzulu kwa rais Marc Ravalomanana.

17/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Mkutano wa tano wa maji duniani ulifunguliwa Jumatatu mjini Istambul, Uturuki ukiwa na lengo la kuliweka suala la maji katika ajenda ya kimataifa.

17/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 53 cha CSW

Leo hii, tunaendelea na mazungumzo juu ya kikao cha 53 cha kamisheni juu ya hali ya Wanawake, kilichomalizika Ijuma tarehe 13, katika makao makuu ya UM.

16/03/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unajaribu kuachiliwa huru watumishi wake waliotekwa Somalia

Afisi ya UM ya kuratibu huduma za dharura huko Somalia inasema inatafuta njia za kuachiliwa huru bila ya masharti yeyote wafanyakazi wanne wa afisi hiyo walotekwa nyara Jumatatu asubuhi na washambulkizi wasojulikana.

16/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe Maalum wa UM apongeza juhudi za Uganda na Kongo dhidi ya waasi

Alan DOSS, SRSG DRC;  MONUC

Wanajeshi wa Uganda walianza kurudi nyumbani siku ya Jumapili kutoka JKK, baada ya operesheni ya pamoja ya miezi mitatu na jeshi la nchi na lile la kusini mwa Sudan, kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Lord Resistance Army LRA.

16/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majeshi ya UM yachukua udhibiti huko Chad kutoka kwa kikosi cha EU

Walinda amani wa UM huko Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati walichukua udhibiti wa kijeshi na usalama kutoka kwa kikosi cha Ulaya katika mataifa mawili hayo yenye kukumbwa na ghasia.

16/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waathiriwa wa vita wanahitaji kupata maji masafi na usafi

Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC, imesema ni lazima kwa jumuia ya kimataifa kufanya kazi zaidi kuhakikisha kwamba waathiriwa wa vita wanapata maji masafi na huduma za usafi.

16/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UM juu ya hali ya misitu duniani

Changamoto kutokana na mzozo wa kiuchumi na mabadiliko ya hali ya hewa, zimeleta kwenye mstari wa mbele usimamizi wa misitu miongoni mwa watalamu wa dunia.

16/03/2009 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kikao cha Kamisheni juu ya Hali ya Wanawake

img_1421_web

Leo hii, tunazungumzia juu ya Kikao cha 53 cha Kamisheni juu ya Hali ya Wanawake, kinacho malizika katika makao makuu ya UM Ijumaa tarehe 13.

13/03/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Hand shake, UN Logo Mezzabolta UN Spanish Radio

Ripoti mpya ya UM inaonya kwamba kuongezeka haraka idadi ya wakazi duniani, mabadiliko ya hali ya hewa, uwongozi mbaya wa matumizi ya rasilmali na kuongezeka kwa mahitaji ya nishati, kumezidisha mahitaji ya maji yanayokauka haraka duniani.

13/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahimiza majadiliano Madagascar mzozo ukizorota

Marc Ravalomanana; Madagascar UN photo

KM Ban Ki-moon alitoa mwito wa kuwepo majadiliano kati ya viongozi wa pande zote huko Madagascar, wakati mvutanowa kisiasa unazidi kuzorota na wasi wasi kuongezeka juu ya kugawika kwa jeshi.

13/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na AU kupambana pamoja dhidi ya uhalifu na madawa ya kulevya

Idara ya UM ya kupambana na uhalifu na Umoja wa Afrika AU, walizindua mpango wa pamoja kusaidia mradi wa miaka mitano ijayo, wa nchi za ki-Afrika kupambana na biashara haramu inayopanuka ya madawa ya kulevya na shughuli za uhalifu zinazoambatana na biashara hiyo barani humo.

13/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haja ya kurahisisha zaidi wagonjwa wa UKIMWI kupata madawa ya ARV’s

Medicine Malaria

Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la kupambana na Ukimwi la UM UNAIDS, anasema kuna haja ya kuimarisha huduma za kutibu HIV, ikiwa njia muhimu ya kupunguza uwambukizaji wa virusi kutoka kwa mama hadi mtoto.

13/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhalifu wa vita huwenda umefanywa na pande zote Sri Lanka

Sri lanka

Mkuu wa Haki za Binadamu wa UM, amelaani kuongezeka idadi ya vifo na majeruhi miongoni mwa raia katika vita vikali huko Sri Lanka ya Kaskazini kati ya majeshi ya serekali na kundi la waasi.

13/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wapiga kura milioni 5.4 wameandikishwa huko Cote d’Ivoire

cote d'ivoire voter registration

Ofisi ya UM nchini Cote D’Ivore imeeleza kama mafanikio muhimu kuelekea uchaguzi mkuu ulocheleweshwa sana huko Cote D’Ivore, ilipotangaza kwamba zaidi ya wapiga kura milioni 5.4 wameshatambuliwa.

13/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Akizungumza na kamati ya masuala ya kigeni ya bunge la Marekani KM Ban Ki-moon aliwakumbusha wabunge kwamba Marekani baado inadaiwa dola bilioni moja na Umoja huo, akisema hawawezi kufanya kazi wanaombiwa kufanya bila ya rasilmali inayohitajika.

13/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni lazima dunia kusaidia Afrika kunufaika kutokana na juhudi zake za kiuchumi

Asha-Rose Migiro

Naibu katibu mkuu Ashe-Rose Migiro amesema kwamba kwa vile hivi sasa nchi za kiafrika zimefanya mafanikio makubwa katika mageuzi yake ya kiuchumi, inabidi sasa Jumuia ya Kimataifa kuzisaidia kugeuza mafanikio hayo katika kupunguza kwa dhati umaskini.

12/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasi wasi wazidi huko Madagascar baada ya mkutano kutofanyika tena

Mkutano ulopangwa kufanyika kati ya pande zinazogombana huko Madagascar haukuweza kufanyika tena hii leo baada ya meya wa Antananarivo, Andry Rajoelina kukata kuhudhuria mazungumzo.

12/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milion 50 za Marekani kuimarisha haki za wanawake UNFPA

Barack Obama 05a

Rais Barack Obama, wa Marekani ametoa dola milioni 50 kusaidia shirika la wakazi la UM UNFPA, ili kupunguza umaskini na kuimarisha afya ya wanawake na watoto katika zaidi ya mataifa 150.

12/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM Ban ana wasi wasi kutokana na kutekwa wafanyakazi wa msaada Darfur

KM Ban Ki-moon ameeleza wasi wasi wake hii leo kutokana na kutekewa nyara wafanyakazi watatu wa huduma za dharura huko Darfur, na kwa mara nyingine tena alitoa mwito kwa Serekali ya Sudan kubadili uwamuzi wake wa wiki iliyopita, wa kuyafukuza makundi 13 muhimu ya misaada.

12/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuungana na mabingwa wa kandanda Ulaya kupambana na nja

Mabingwa wakuu wa kandanda huko Ulaya pamoja na mamilioni ya mashabiki wao wana lengo la kupachika goli dhidi ya njaa kote duniani katika kampeni ya kwanza kabisa kote Ulaya, ili kuhamasisha mzozo wa njaa unaowakumba watu bilioni moja.

11/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo kuzihusisha pande zote Afrika ya Kati kutapelekea amani

francoislonsenyfallpress

Mjumbe Maalum wa KM kwa ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ameliambia Baraza la Usalama kwamba mazungumzo yaliyokua yanasubiriwa kwa muda mrefu ya vyama vyote yameweza kuleta nafasi ya kupiga hatua kuelekea amani ya kudumu katika nchi hiyo isiyopakana na bahari.

11/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wamulika athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya

Nembo ya WHO

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya, ni suala muhimu ambalo wapanga sera wanabidi kuzingatia na kufahamu wanapopanga vipau mbele vya maendeleo na uwekezaji.

11/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM Ban na Rais Obama wajadili kuimarisha uhusiano kati ya UM na Marekani

KM Ban Ki-moon na Rais Barrack Obama wa Marekani wamekubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na UM walipokutana Ijumanne huko Washington.

11/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Idara ya UM ya kupambana na mabomu yaliyotegwa ardhini, UNMAS imetangaza kwamba serekali ya Japan itatowa karibu dola milioni 7.7 ya msaada kwa ajili ya juhudi za kuondowa mabomu yaliyotegwa ardhini huko JKK na Chad.

10/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kesi mpya za kutoweka zaidi ya watu 300 kushughulikiwa na tume ya UM

OHCHR/Roy Domingo

Kamati ya UM ya kufuatilia kutoweka kwa nguvu au kwa hiyari watu, ina mpango wa kutathmini kesi mpya za kutoweka watu wengine 326 zilizowasilishwa na habari mpya kutoka nchi 32 za dunia wakati wa kikao cha kwanza kati ya tatu ya mkutano wamwaka wiki hii.

10/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuporomoka kwa biashara duniani kunaweza kuathiri zaidi wanawake

Akifungua mkutano juu ya “umuhimu wa jinsia katika biashara” mkurugenzi mkuu wa shirika la Biashara Duniani UNCTAD Bw Supachai Panitchpakdi amezipendekeza serekali zinazo tayarisha mipango ya kujaribu kuufufua uchumi ili kukabiliana na mzozo wa kifedha duniani kufikiria juu ya kuweka hatua za kuimarisha ajira kwa ajili ya wanawake na kusaidia biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wanawake.

10/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wa UNAMID wavamiwa kwa ghafla huko Darfur

Ujumbe wa pamoja wa walinda amani wa UM na Umoja wa Afrika, UNAMID huko Sudan Magharibi, umesema walinda amani walivamiwa kwa ghafla na watu watano au sita waliokuwa na silaha Jumatatu jioni, wakati wakisafiri kwa gari karibu na mji wa EL- Geneina huko darfur magharibi.

10/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nafasi milioni 10 zaweza kubuniwa kwa kukuza misitu

Naibu mkurugenzi wa shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO amesema, wakati nafasi zaidi za ajira zinapotea kutokana na kuendelea kuzorota hali ya uchumi, kuna uwezekano wa kubuni mamilioni ya nafasi za kazi za kijani, kwa kuwepo na usimamizi bora wa misitu.

10/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Liberia yazindua mpango wa kitaifa kwa ajili ya wanawake amani na usalama

UN Photo

Tarehe 8 March ilikua siku kuu ya wanawake duniani kukiweko na sherehe mbali mbali katika kila pembe ya dunia, ili kuhamasisha haki na maendeleo ya wanawake.

09/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM aonya gharama za ghasia dhidi ya wanawake hayahesabiki

Domestic violence

Akiongeza sauti yake kwa mlolongo wa sauti za maafisa wa UM kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, KM Ban Ki-moon, alitoa mwito jana, wa kukomeshwa tabia ya ghasia zinazo wakumba wanawake na wasichana kote duniani.

09/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban na Obama kukutana Washington wiki hii

SG and Senator Barack Obama sharing a shuttle ride.

KM Ban Ki-moon atakutana na Rais Barack Obama wa Marekani huko Washington kwa mazungumzo juu ya masuala mbali mbali ikiwemo mzozo wa kiuchumi duniani, Sudan, Afghanistan na Mashariki ya Kati.

09/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wapanda Kilimanjaro kuhamasisha athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Tume ya vijana 10 kutoka Kenya, Tanzania na Ghana wamefikia kilele cha Mlima Kilimanjaro huko Tanzania ikiwa ni sehemu ya kampeni ya UM ya kuhamasisha athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa.

09/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

KM Ban Ki-moon akifuatana na rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton wako Haiti hii leo ili kuhamasisha dunia nzima juu ya mahitaji ya kukarabati na kuufufua uchumi wa taifa hilo la Caribbean.

09/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauwaji ya wanaharakati wa haki za binadamu Kenya

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Bi Navi Pillay, ametoa mwito wa uchunguzi kufanyika baada ya muasisi wa kundi la kutetea haki za binadamu kuuliwa mjini Nairobi siku ya Alhamisi, wakati wa magharibi.

06/03/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon ametoa mwito kwa serekali ya Sudan kufikiria upya kwa haraka uwamuzi wake wa kuyafukuza mashirika 13 yanayowasaidia kiasi ya watu milioni nne nukta 7 huko Darfur.

06/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA kutumia teknolojia ya nuklia kupambana na ndorobo

Wanasayansi wa idara ya Kimataifa ya Nishati ya Atomiki IAEA wanatayarisha mpango wa kudhibiti nzi wenye wa hatari wa aina ya ndorobo, kwa kutumia teknolojia ya nuklia.

06/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya wanawake Machi 8 tuungane kupambana na ghasia dhidi ya wanawake

Russian Radio

“Ubaguzi ulokithiri dhidi ya wanawake katika fani zote za jamii – kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni – unadhuru jamii kwa ujumla.”

06/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yaonya athari kubwa Darfur baada ya kufukuzwa mashirika ya misaada

Mashirika ya huduma za dharura za UM yaongeza sauti zao za upinzani kufuatia onyo la KM Ban Ki-moon, na mashirika mengine ya UM kutokana na uwamuzi wa kuyafukuza mashirika 13 ya misaada kutoka Sudan.

06/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Alston atoa mwito wa uchunguzi kutokana kuuliwa wanaharakati wa Haki za Binadamu Kenya

Mtaalamu maalum wa UM kuhusiana na mauwaji ya kiholela Profesa Philip Alston ametoa mwito wa uchunguzi wa kina kufanyika kutokana na kuuliwa kwa wanaharakati wawili wa kutetea haki za binadama huko Kenya.

06/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yalaani kudhalilishwa watoto na walimu Madagascar

Nembo ya UNICEF

Shirika la watoto la UM, UNICEF limetoa mwito wa kwa wakuu wa usalama wa Madagascar pamoja na serekali, vyama vya kisaisa na wananchi kuheshimu haki msingi za watoto na kujizuia kutokana na hatua zozote za kuhatarisha watoto.

05/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Baraza Kuu kulaani kufunguliwa mashtaka Bashir

Rais wa Baraza Kuu la UM Balozi Miguel d’Escoto Brockman, akizungumza na waandishi habari mjini Geneva amesema UM haujatengwa kutokana na kundi la mataifa tajiri na yanayoinukia G20 yanakutana kando.

05/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wahimiza watu kuunga mkono kukomesha biashara haramu ya kuwauza binadamu

UM umezindua kampeni mpya, inayowakilishwa na utepe wa bulu ulochorwa kama moyo katika lengo la kuwahamasisha watu juu ya mamilioni ya waathiriwa wa biashara haramu ya kusafirisha binadamu, na kuwapatia uungaji mkono kupambana na tabia hii ambayo na utumwa wa mambo leo.

05/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lazima kukomesha ghasia dhidi ya wanawake asema KM

KM Ban Ki-moon amerudia tena mwito wake wa dharura wa kukomesha ghasia dhidi ya wanawake akieleza ni adhabu ambayo athari zake ni uchungu usoweza kupimwa.

05/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Naibu katibu mkuu wa UM Asha-Rose Migiro amehimiza hatua za haraka kuchukuliwa kunganisha idara zote za UM zinazohusiana na masuala ya wanawake ili kuimarisha juhudi za kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kisasa, kiuchumi na kijami.

04/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Mkuu wa Idara ya Kazi za kulinda amani za UM Alan Le Roy, amesema amehakikishiwa kwamba kikosi cha pamoja cha UM na Umoja wa Afrika huko Darfur UNAMID, hakita kabiliwa na kitisho ikiwa mahakama ya uhalifu ya kimataifa itatoa kibali cha kukamatwa Rais Omar Al-Bashir.

04/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yatoa mwito wa msaada kwa Somalia

Ramani ya Somalia

Idara ya huduma za dharura ya UM huko Somalia imesema huwenda ikaanza kusitisha huduma zake huko kutokana na upungufu wa fedha.

04/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Libya itazingatia sera ya kulinda amani na Sudan wakati inaongoza Baraza la Usalama

Security Council Middle East

Libya inasema miongoni mwa masuala itazingatia mnamo mwezi huo inaposhikilia uwenyekiti wa Baraza la Usalama la UM ni sera ya kazi za kulinda amani na athari zinazoweza kutokea, kutokana na uwamuzi wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa kutoa kibali cha kukamatwa kwa Rais wa Sudan.

04/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yatoa hati ya kukamatwa Rais wa Sudan kwa uhalifu wa vita Darfur

Ocampo na Al-Bashir

Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ICC imetoa hii leo hati ya kukamtwa Rais Omar Al-Bashir kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulotendeka katika jimbo linalokumbwa na ghasia la Darfur.

04/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa Mazingira kuongoza Makao Makuu ya UM Nairobi

KM Ban Ki-moon amemteua mkuu wa Shirika la Mazingira la UM, UNEP kua mkurugenzi mkuu wa Makao Makuu ya UM huko Nairobi. Achim Steiner aliyeanza awamu ya miaka minne kuiongoza UNEP 2006, ataendelea kua mkuu wa shirika hilo na kuchukua nafasi iliyokua inashikiliwa na Bi Anna Tibaijuka, ambae ataendelea kua mkurugenzi mkuu wa Shirika la [...]

03/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baada ya mkutano wa wafadhili juu ya Ghaza msaada bado unazuiliwa

ocha

UM unaripoti kwamba licha ya mwito katika mkutano wa wafadhili wa kuruhusu bila kipingamizi chechote msaada kutoka njee pamoja na vifaa vya ujenzi kuingia katika kanda ya Gaza iliyoharibiwa kwa vita, maafisa wa uslama wa Israel wanaendelea kuzuia bidhaa muhimu kuingia.

03/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM analaani vikali mauwaji huko Guinea Bissau

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa matamshi makali kabisa limelaani mauwaji ya rais wa Guinea Bissau Bernardo Vieira na mkuu wake wa majeshi Tagme Na Waie, na kutoa mwito kwa wananchi, viongozi wa kisiasa na majeshi ya nchi hiyo kubaki makini, kujizuia na kudumisha utulivu. Akisoma taarifa ya baraza hilo balozi wa Libya Ibrahim Dabbashi, ambae ni mwenyekiti wa mwezi huu wa baraza hilo amehimiza kwa pande zote nchini humo kutanzua ugomvi wao kupitia mfumo wa taasisi za kidemokrasia na kupinga jaribiyo lolote la kubadilisha serekali kinyume cha katiba.

03/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unaeleza kua mzozo wa kifedha utazidisha umaskini

World Bank

Utafiti mpya wa Umoja Ma mataifa unaeleza kwamba mzozo wa kifedha duniani unaokumba masoko ya fedha ya Marekani na Ulaya utawathiri watu fukara duniani na kuwatumbukiza mamilioni katika umaskini zaidi na kupelekea vifo vya maelfu ya watoto.

03/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya hali ya hewa kuweza kuathiri sana uvuvi duniani

Nembo ya FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo limechapisha ripoti hii leo ikionya kwamba ni lazima biashara ya uvuvi na idara za kitaifa za uvuvi zichukuwe hatua zaidi kufahamu na kujitayarisha kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa uvuvi duniani.

02/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Simu za mkono njia muhimu ya mawasiliano kwa mataifa maskini

cellphone 24a

Sita kati ya kila watu kumi kote duniani wanasimu ya mkono ikiwa ni ishara kwamba simu hizo ndizo teknolojia ya mawasiliano iliyochaguliwa hasa katika mataifa maskini, hiyo ni kufuatana na ripoti mpya ya UM.

02/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 10 cha Baraza la Haki za Binadamu cha funguliwa Geneva

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Navi Pillay, ameyahimiza tena mataifa ya dunia kuweka kando tofuati zao na kufanya kazi pamoja kuhakikisha matokeo ya ufanisi katika mkutano wa mwezi ujao dhidi ya kutostahamiliana, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni huko Geneva.

02/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM anasema, amani ya kudumu ni lazima iwe msingi wa kuikarabati Ghaza

KM wa UM Ban Ki-moon ametoa mwito kwa wafadhili wa kimataifa kutoa fedha zinazohitajika sana kwa ajili ya kazi za kuikarabati Ghaza kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel. Bw Ban alisisitiza kwa mara nyingine tena haja ya kupatikana makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano na makubaliano jumla ya amani.

02/03/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930