Nyumbani » 27/02/2009 Entries posted on “Febuari, 2009”

Hapa na pale

unflaghq0425r

Kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika na UM huko Darfur kiliripoti Alhamisi kwamba utulivu wa kiasi fulani umerudi katika eneo lililokua na ghasia la Magharibi ya Sudan, ingawa kungali na wasi wasi juu ya kuendelea ghasia katika baadhi za sehemu. UNAMID inasema kumekua na ripoti za uhalifu huko Darfur ya Kaskazini na wanamgambo wenye silaha wanaendelea kuwashambulia na kuwabughudhi raia huko Darfur ya Kusini

27/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UM yataka mageuzi katika kikosi cha polisi Kenya

Kenya Map UN Spanish Radio

Karibuni wapendwa wasikilizaji katika makala yetu ya ripoti ya wiki leo tutazungumzia ripoti ya mjumbe maalum wa UM kwa ajili ya mauwaji ya kiholela, inayo toa mwito kwa Rais wa Kenya kutambua na kuchukua hatua za kukomesha kile alichokieleza ni “mauwaji yanayopangwa, yaliyoenea na kufanywa kwa ustadi” na polisi wa nchi hiyo.

27/02/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasi wasi wa ghasia mpya mashariki mwa JKK

Russian Radio

Idara ya huduma za dharura ya UM, OCHA imeeleza wasi wasi wakutokea ghasia mpya dhidi ya wafanyakazi wa huduma za dharura huko jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini JKK.

27/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama maalumu ya Sierra Leone yawapata na hatia viongozi watatu wa waasi

Sierra Leona Mapa / Sierra Leone Map WPF / Spanish Radio Unit

Watu watatu walokiongoza kundi la kikatili la waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sierra Leone wamepatikana na hatia ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu na mahakama maalum inayoungwa mkono na UM huko Freetown.

27/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM amemtuma mshauri wake wa kisiasa kusaidia mzozo wa Madagascar

Haile Menkerios ASSISTANT SECRETARY-GENERAL FOR POLITICAL AFFAIRS. UN Photo/UN Spanish Radio

KM Ban Ki-moon amemtuma mshauri wake wa cheo cha juu wa masuala ya kisiasa hadi Madagascar kufuatia ombi la serekali ya Antananarivo kuutaka UM kuchukua jukumu kubwa zaidi kusaidia kukabiliana na mvutano wa kisiasa katika kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi.

27/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya Wasomali elfu 40 walokimbia makazi yao warudi Mogadishu licha ya mapigano

Somalia:  12 November 2007 -  "Civilians are more than ever bearing the brunt of the fighting in Mogadishu", says UN Emergency Relief Coordinator, John Holmes.  An additional 24,000 people have fled Somalia's capital in the last week as a result of clashe OCHA / Spanish Radio

Shirika la UM la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, linaripoti kwamba zaidi ya watu elfu 40 walokimbia makazi yao IDP’s wamerudi katika mji mkuu wa Mogadishu huko Somalia licha ya mapigano makali kutokea huko katika kipindi cha wiki sita zilizopita.

27/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ametoa mwito wa kukomesha mapigano na ghasia kote Afrika

Akiendelea na ziara yake ya Afrika, KM Ban Ki-moon alikutana Alhamisi na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania mjini Dar es Salaam, kwa mazungumzo juu ya masuala mbali mabli, kuanzia uchaguzi ujao nchini humo, mizozo ya kikanda na janga la uchumi duniani.

27/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Chinese Unit

Baraza la usalama limelaani vikali shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya kambi ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa afrika AU huko Mogadishu.

26/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM amewasili Tanzania kituo cha pili cha ziare ya Afrika

KM wa UM Ban Ki-moon, amewasili Tanzania kituO cha pili cha ziara yake ya Afrika akitokea Afrika Kusini.

26/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa dharura wahitajika Somalia

Idara ya kuratibu huduma za dharura za UM, OCHA imeonya kwamba bila ya kuongezwa haraka msaada kukabiliana na janga kubwa la utapia mlo na magonjwa huko Somalia, basi hali hiyo itazidi kuzorota.

26/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

“Kijiji Muafaka” – mradi mpya wa walinda amani huko Liberia

UNMIL, Liberia UNMIL/UN Spanish Radio

Katika juhudi za kumarisha uzalishaji na usalama wa chakula walinda amani wa UM kutoka Bangladesh huko Liberia wametenga eka 150 za ardhi kujenga kijiji kipya, kikiwa na shamba la ushirika, ufugaji wa kuku, na kidimbwi cha samaki.

26/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya UM yatoa mwito kuimarisha juhudi za huduma Zimbabwe

Tume maalum ya idara za UM huko Zimbabwe imesisitiza kwamba hali ya kibinadamu inaendelea kua mbaya sana na kuhimiza serekali na jumuia ya kimatiafa kusaidia kuimarisha juhudi za msaada wa dharura.

26/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe Maalum wa UM huko Sahara Magharibi anakamilisha mazungumzo Algeria

Mjumbe maalum wa KM kwa ajili ya Sahara Magharibi, Christopher Ross, amesema mazungumzo yake na wakuu wa Algeria yalikua ya kina, wazi na ya manufaa.

26/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaonya dawa sugu kutishia juhudi za kupambana na Malaria

Shirika la Afya duniani WHO limesema jumatano kwamba kujitokeza kwa dawa iliyo sugu dhidi ya ugonjwa wa Malaria huko Kusini Mashariki ya Asia inaweza kuhujumu vibaya sana mafanikio ya kimataifa katika kuudhibiti ugonja huo.

25/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM asema mauwaji na polisi Kenya hupandwa kwa kawaida

Mtaalamu huru wa masuala ya mauwaji ya kiholela UM Philip Alston anasema mauwaji ya kiholela yanayofanywa na polisi wa Kenya ni mambo ya kawaida, yaliyoenea na hupangwa kwa makini.

25/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum wa UM ahimiza kusitishwa mapigano kusini mwa Sudan

ashrafqazispecialrep

Mjumbe maalum wa KM wa Um huko Sudan ametoa mwito kwa pande zote kusitisha mara moja mapigano yaliyozuka jana katika mji wa kusini wa Malakal.

25/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ameanza ziara ya mataifa matano ya Afrika

KM wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliwasili Afrika Kusini siku ya Jumanne kuanza ziara yake ya nchi tano za Afrika, itakayomfikisha Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Misri.

25/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

KM wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon aliwasili Afrika Kusini siku ya Jumanne kuanza ziara yake ya nchi tano za Afrika, itakayomfikisha Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Misri.

25/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICTR yafungua Vituo vya Habari Rwanda

International Criminal Tribunal for Rwanda ICTR/UN Spanish Radio

Mahakama ya UM ya uhalifu wa vita vya Rwanda huko Arusha ICTR, imefungua vituo viwili vya habari kusini mwa nchi hiyo.

24/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 6 wazama nje ya Pwani ya Yemen

map of yemen

Inaripotiwa kwamba watu 6 wamefariki na wengine 11 hawajapatikana na huwenda wamefariki baada ya wafanyabishara wa magendo kuwalazimisha abiria kuchupa baharini njee ya pwani ya Yemen wiki iliyopita.

24/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shughuli za kulinda amani, kukaguliwa kwa kina wakati inakabiliwa na upungufu wa rasilmali

Alain Le roy. Under-Secretary-General for Peacekeeping Operations. UN photo/Un Spanish Radio

Kazi za kulinda amani za UM zinazokabiliwa na hali ambayo hayajapata kutokea na upungufu mkubwa wa rasilmali, zitakaguliwa kwa kina mnamo maka unaokuja kufuatana na mkuu wa Idara ya Kazi za Kulinda Amani DPKO.

24/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa Haki za Binadamu wa UM ahimiza mataifa kutanzua tofauti zao katika vita dhidi ya ubaguzi

Ubaguzi

Kamishina mkuu wa Haki za Binadamu wa UM Navi Pillay alisisitiza jana haja ya nchi wanachama kuweka kando tofauti zao na kufanya kazi pamoja kuushinda ubaguzi wa rangi, na chuki dhidi nya wageni kabla ya mkutano wa pili wa Durban baadae mwaka huu.

24/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM alaani vikali mauwaji ya walinda amani wa Umoja wa Afrika

KM wa UM Ban Ki-moon alilaani vikali jana shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika AU huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia, lililosabibisha vifo vya walinda amani 11 wa Burundi.

24/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

2008 Flag-raising ceremony. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Mjumbe maalum wa UM huko Somalia amesema alishutshwa na habari za shambulio dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Afrika huko Mogadishu, siku ya jumapili lililosababisha vifo vya wanajeshi 11 wa Burundi.

23/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Qatar yatoa $ milioni 40 kwa ajili ya misaada ya dharura

Qatar map

Serekali ya Qatar imetangaza hii leo kwamba imetoa msaada wa dola milioni 40 ili kusaidia mipango ya huduma za dharura ya UM kote duniani.

23/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yajadili athari za mzozo wa kiuchumi kwa wafanyakazi katika sekta ya fedha

Nembo ya ILO

Wajumbe kutoka vyama vya wafanyakazi na mashirika ya waajiri watakutana huko Geneva kesho, kwenye makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Kazi ILO kujadili athari za mzozo wa kiuchumi kwa zaidi ya wafanya kazi milioni 20 wa sekta za fedha kote duniani.

23/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majeshi ya AU na UM yaimarisha doria kuwalinda waliopoteza makazi yao

UNAMID peacekkeping, Sudan, Darfur ALBANY ASSOCIATES / STUART PRICE./Russian Radio

Kikosi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur UNAMID kimeripoti leo kwamba kikosi chake cha polisi kitafanya doria ya kwanza wakati wa usiku kutokea kituo kipya cha polisi katika jamii CPC kilichojengwa kati kati ya makambi mawili makubwa ya watu walopoteza makazi yao IDP’s karibu na mji wa El Fasher mji mkuu wa Darfur ya Kaskazini.

23/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum wa UM awataka wanamgambo wa Kihutu kuondoka Kongo

Alan DOSS, SRSG DRC;  MONUC

Mjumbe maalum wa UM huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewahimiza tena wapiganaji wa kihutu kutoka Rwanda katika jimbo lenye misukosuko la Kivu ya Kaskazini, kuweka chini silaha zao na kurudi nyumbani.

23/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu itatangaza uwamuzi wa kukamatwa au la kwa Rais wa Sudan hivi karibuni

International Criminal Court logo

Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitangaza Jumatatu kwamba itatoa uwamuzi wake kuhusu kutowa kibali cha kukamatwa Rais Omar al Bashir wa Sudan hapo march 4, 2009.

23/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM yarudia mwito wa kuachiwa afisa aliyetekwa nyara Pakistan

UM umerudia tena mwito wake wa kutaka kuachiliwa kwa afisa mmoja wa UM aliyetekwa nyara huko kusini magharibi ya Pakistan.

20/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walimaji wadogo wadogo wa Tanzania wapatiwa mkopo na UM

Logo IFAD. IFAD/UN Spanish Radio

Walimaji wa mashamba madogo madogo huko Tanzania watafaidika kutokana na mkopo wa dola milioni 56 unaopatiwa sekta ya kilimo ya serekali kutoka UM.

20/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki za Binadamu na Athari za Mzozo wa Kiuchumi Duniani

Navanethem Pillay, new Human Rights Chief

Kamishna Mkuu wa haki za binadam Navi Pillay, amezihimiza serekali na wadau wa sekta za kibinafsi kuhakikisha kwamba juhudi zao za kutanzua mzozo wa sasa wa fedha duniani hazita hatarisha haki za binadam. Bi Pillay alisema mzozo wa fedha huwenda ukahujumu uwezo wa kufanya kazi, uwezo wa kumudu chakula na makazi, huduma msingi za afya [...]

20/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juhudi za UM kudhibiti mazingira bora

Mkutano wa siku tatu kuhusu uchukuzi wa baharini, uliotayarishwa na Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD), umehitimisha mijadala wiki hii mjini Geneva kwa mwito uliohimiza wenye viwanda kuhakikisha wanaongeza juhudi zaidi kwenye ile kadhia ya kupunguza umwagaji wa hewa chafu angani.

20/02/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahimiza ulimwengu kupigania Haki za Kijamii kwa wote

Akiadhimisha kwa mara ya kwanza siku ya haki za kijamii duniani hii leo KM Ban Ki-Moon amesisitiza umuhimu wa kufuatilia haki za kijami kote duniani, akilalamika kwamba watu wengi kabisa hii leo wananyimwa haki hii, ambayo ni moja wapo ya msingi wa UM katika kazi zake za kuendeleza maendeleo na heshima kwa wote.

20/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN building

Hapa na Pale

Mji wa Copenhagen umesajiliwa Alkhamisi kuwa mshiriki wa 100 wa ushirikiano unaojulikana kwa umaarufu kama Mtandao wa Mazingira ya Hali ya Hewa Huru, ambao huongozwa na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP). Mwaka mmoja uliopita Mtandao wa Mazingira ya Hali ya Hewa Huru ulianzishwa rasmi kimataifa, kwa madhumuni halisi ya kukuza shughuli maalumu zitakazohakikisha umma wa kimataifa utaishi kwenye jamii zenye uchumi usiosumbuliwa na mazingira yaliopambwa na hewa chafu.

19/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Iran yataka silaha zote za kinyuklia kupigwa marufuku

nuclear testing Russian Radio

Balozi wa Iran, Alireza Moaiyeri amewaambia wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Kupunguza Silaha unaofanyika Geneva, ya kuwa hatua pekee yenye uwezo wa kuuthibitishia, kihakika, umma wa kimataifa usalama dhidi ya vitisho au matumizi ya silaha za kinyuklia ni kwa Nchi Wanachama kuafikiana maafikiano, yanayofungamana na maadili makuu ya kimataifa ya kuondosha, na kuangamiza kikamilifu, silaha zote za kinyuklia, kote [...]

19/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ajiandaa kuzuru mataifa matano Afrika

Russian Radio

Ofisi ya msemaji wa KM imetangaza kwamba kuanzia wiki ijayo KM Ban Ki-moon atafanya ziara ya kuyatembelea mataifa matano barani Afrika, ikijumuisha Afrika Kusini, Tanzania, JKK, Rwanda na Misri.

19/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO inaadhimisha Siku ya Haki kwa Jamii Duniani

Nembo ya ILO

Ijumaa ya tarehe 20 Februari itaadhimishwa rasmi, kwa mara ya kwanza na Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) kuwa ni Siku ya Haki katika Jamii Duniani.

19/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNMIS asikitishwa na kifo cha mwandishi wa Sudan

Ashraf Jehangir Khan, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la UM juu ya Amani Sudan Kusini (UNMIS) amenakiliwa, kwenye taarifa kwa waandishi habari, kusikitishwa sana na kifo cha mwandishi mashuhuri wa riwaya wa Sudan, Al-Tayeb Saleh kilichotukia wiki hii.

19/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

Jumuiya ya Mashirika ya UM Dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) imekaribisha uamuzi wa Bunge la Burundi la kukataa ule mswada wa sheria ya kuharamisha usenge na ukhanithi nchini. Michel Sidibé, Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS amewasifu Wabunge kukataa marekibisho hayo, na anaamini kuwa wameonyesha ari kuu ya kutunza haki za binadamu za umma wao, kitendo ambacho anahisi ni cha kupigiwa mfano kwa wabunge wengine wa kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa ya UNAIDS, uharamishaji wa tabia ya kijinsiya ya wanaume watu wazima na utenguzi wa haki za binadamu za watu wenye kuishi na virusi vya UKIMWI, ni mambo yenye kukwamisha juhudi za kudhibiti bora maambukizi ya VVU katika dunia, ambazo zinafungamana na fedheha ya uhalifu dhidi ya wasenge.

18/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kinga za Maradhi kwa Watoto zasailiwa kwenye mkutano ulioanza rasmi Makao Makuu

Washirika wa kwenye zile juhudi za kupiga vita maradhi yanayozuilika kwa chanjo, wamekusanyika kwenye Makao Makuu ya UM wiki hii, kuhudhuria kikao cha nne cha Mkutano wa Kukinga Maradhi Duniani.

18/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP imepongeza Olimpiki ya Beijing kwa kutekeleza miradi ya Mazingira Rafiki

Baraza la Utawala la Shirika la UM Juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limewasilisha matokeo ya ripoti maalumu ya utafiti wao, kuhusu utekelezaji wa huduma za kimazingira wakati wa mashindano ya Olimpiki ya Beijing.

18/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viwavi haribifu vinahatarisha kilimo Liberia, imehadharisha FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limewatangazia waandishi habari mjini Monrovia, kwamba taifa la Liberia limevamiwa na aina ya viwavi visiojulikana, na wakati huo huo vile viwavi vinavyohujumu mimea, vimegundulikana kuvuka mipaka na kuelekea taifa l Cote d’Ivoire.

18/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu watathminia umadhubuti wa miradi ya kufyeka rushwa Afrika

Corruption. Money.

Wataalamu wanaohusika na udhibiti wa ulajirushwa, kutoka mataifa kadha ya Afrika, wamekamilisha mkutano wa siku mbili uliofanyika Kigali, Rwanda ambapo kulitathminia umadhubuti na athari za taasisi za Kupiga Vita Ulajirushwa barani Afrika.

18/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Mjumbe Binafsi wa KM kwa Sahara ya Magharibi, Christopher Ross, anaelekea kwenye eneo husika kwa ushauri, baada ya kukutana na KM, wajumbe wa Baraza la Usalama na wawakilishi wa makundi husika – yaani, Chama cha Ukombozi wa Sahara Magharibi (Frente Polisario) na Morocco. Ross ataanza ziara yake ya mashauriano kesho Ijumatano katika mji wa Rabat, Morocco. Hii itakuwa ni ziara ya awali kwenye eneo, baada ya kushika rasmi wadhifa wa Mjumbe Binafsi wa KM.

17/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNESCO alaani vifo vya waandishi habari katika JKK na Bukini

GENEVA - SWITZERLAND- M Koichiro Matsuura directeur general de l UNESCO lors du debat general du 1er examen ministeriel annuel sur le renforcement de la lutte contre la pauvrete durant le Conseil Economique et Social des Nations Unies . Photo UN / Jean-Ma

Koichiro Matsuura, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) amelaani mauaji ya waandishi habari yaliotukia majuzi katika Jamhuri ya Kongo na Bukini.

17/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu litazingatia marekibisho ya mfumo wa BU

Security Council Middle East

Wiki hii, mnamo tarehe 19 Februari, wawakilishi wa Mataifa Wanachama wa Baraza Kuu watakusanyika kwenye Makao Makuu ya UM kujadiliana juu ya ile rai ya kuleta marekibisho kwenye mfumo wa Baraza la Usalama, kwa lengo la kuhakikisha kazi za taasisi hii ya kimataifa zitawakilisha, kwa usawa, na kwa haki matakwa na mahitaji hakika ya wanachama wote wa UM, yatakayolingana na hali halisi ilivyo kwenye uhusiano wa kimataifa wa karne ya ishirini na moja.

17/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP inahimiza uwekezaji wa mazingira uongezwe kuimarisha uchumi wa dunia

UNEP

Ripoti iliotolewa Ijumatatu na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) imebainisha awamu ya tatu ya furushi la mradi wa kuwekeza dola trilioni 2 na nusu, zinazohitajika kufufua uchumi wa dunia unaofungamana na mazingira bora, yalio safi na salama.

17/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshindi wa Tunzo ya Haki za Binadamu, kutokea JKK, azungumzia uokoaji afya ya wasibiwa na uhalifu wa nguvu wa kijinsia

mukwege, RDC, Kivu, women

Makala yetu maalumu, kwa leo, itazingatia juhudi za daktari mmoja shujaa, kutokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), aliyehamasishwa kiutu na kizalendo, kujishirikisha kwenye huduma za kufufua afya ya wale wanawake, na watoto wa kike, waliosibiwa na mateso ya jinai ya kunajisiwa kimabavu na kihorera, kutokana na mazingira ya vurugu kwenye eneo la mashariki ya JKK.

16/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

un flags 012b

KM Ban Ki-moon ameripotiwa kushtushwa, kwa shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya wachaMngu wa KiShia, liliotukia Ijumaa karibu na Baghdad. Kadhalika, KM alisema ameshtushwa na mashambulio mengine kama hayo yaliotukia majuzi Iraq ambayo yalisababisha darzeni za vifo na kujeruhi raia kadha wa kadha, ikijumlisha fungu kubwa la watoto wadogo na wanawake. KM alisisitiza hakuna sera ulimwenguni inayohalalisha vitendo hivi, si ya kidini wala kisiasa, na alikumbusha walimwengu wanawajibika, pote walipo, kulaani kwa lugha nzito kabisa makosa kama haya ya jinai kuu dhidi ya wanadamu. KM aliusihi umma wa Iraq kupinga kabisa jaribio katili linalotaka kuchochea fujo za kiitikadi nchini mwao, na aliwataka viongozi wa Iraq kuungana pamoja, kwa moyo wa kuhishimiana na uelewano wa kizalendo, kama walivyofanya wakati walipokwenda kupiga kura karibuni kwenye uchaguzi wa majimbo, uchaguzi ambao ulifanyika mwezi uliopita bila fujo.

14/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNODC kuhusu juhudi za UM za kukomesha uhalifu wa mipangilio

Unodc 08a

Wiki hii tutaendelea na taarifa zetu kuhusu juhudi za UM katika kukomesha uhalifu wa mipangilio, ambao huhatarisha usalama na amani ya umma wa kimataifa.

13/02/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu laitisha kikao cha kuzingatia athari za mzozo wa uchumi kimataifa

martin-uhomoibhi

Raisi wa Baraza la Haki za Binadamu, Martin Ihoeghian UHOMOIBHI, amelezea kwenye mazungumzo na waandishi habari mjini Geneva ya kuwa Baraza litaitisha kikao maalumu Ijumaa ijayo kuzingatia, kwa kina, athari za mzozo wa uchumi kimataifa, hasa katika utekelezaji wa haki za binadamu ulimwenguni.

13/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa vocha za chakula waanzishwa Burkina Faso na WFP

Nembo ya WFP

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha mradi wa kutoa vocha, au hati kwa watu wenye kufadhiliwa chakula katika mataifa ya Afrika, hasa kwa wale wakazi wa katika miji.

13/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR imefaulu kuwafikia wahamiaji wa JAK wanaohitajia huduma za dharura

Chad Map / Mapa de Chad UN Spanish Radio

Baada ya safari ya siku tatu ya timu ya Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwenye eneo la mbali la kusini-mashariki ya Chad, walifanikiwa kuwafikia wahamiaji wa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kuwapatia huduma za kihali, za dharura, kunusuru maisha.

13/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkariri anayehusika na mauaji nje ya taratibu za kimahakama atazuru Kenya

Mr. Philip Alston, United Nations Special Rapporteur on extrajudicial, summary or arbitrary executions. UN Photo/Paulo Filgueiras-UN Spanish Radio

Philip Alston, Mkariri wa UM juu ya masuala ya mauaji ya kihorera, nje ya taratibu za kimahakama, anatazamiwa kuzuru Kenya kuanzia tareh 16 mpaka 25 Februari, kwa kuitika mwaliko wa Serikali ya Kenya na atakapokuwepo huko atakutana na maofisa wa Serikali kuu na pia zile za majimbo, na vile vile atakutana kwa mashauriano na wabunge.

13/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

UN Building UN Spanish Radio

Olusegun Obasanjo, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Maziwa Makuu amearifu kwamba mamzungumzo ya upatanishi yanatarajiwa kuanzsihwa tena katika siku za karibuni baina ya Serikali ya JKK na wafuasi wa jeshi la mgambo la CNDP.

13/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 25,000 wa JKK katika Zambia waiomba UM iwarejeshe makwao

Nemba ya UNHCR

Shirika la UM Juu ya Wahamiaji (UNHCR) limeripoti asilimia 99 ya wazalendo wahamiaji 25,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), waliopo kwenye kambi za Kala na Mwanga, nchini Zambia wameomba warejeshwe makwao na UM. Kambi hizi mbili zipo katika eneo la Zambia kaskazini, kilomita 1,000 kutoka mji mkuu wa Lusaka.

12/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya ICC inakana tetesi za kufikia uamuzi wa kumshika Raisi wa Sudan

International Criminal Court

Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imetangaza taarifa maalumu, inayokana zile tetesi zilizosambaa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, zinazodai kwamba mahakimu wake wamefikia uamuzi wa kutoa hati ya kumshika Raisi Omar Al Bashir wa Sudan.

12/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna wa Haki za Binadamu aisihi Zimbabwe kufufua utaratibu wa kuhishimu sheria

UNCHR

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ametoa mwito maalumu uliopendekeza kwa Serikali mpya ya Muungano wa Taifa katika Zimbabwe, kuchukua hatua za dharura kufufua taratibu za kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa na kuhishimiwa na kila raia.

12/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uzalishaji wa nafaka unaashiriwa na FAO kuporomoka kwa mwaka huu

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limewakilisha ripoti inayozingatia hali ya uzalishaji wa nafaka, kwa mwaka huu, katika dunia.

12/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNODC imewakilisha ripoti mpya kuhusu biashara ya magendo ya kuchuuza watu wanaotoroshwa

UNODC

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) limewasilisha “Ripoti ya Dunia juu ya Utoroshaji Magendo wa Watu kwa 2007 – 2008″.

12/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na pale

unflaghq0425r

Hapa na Pale

Msemaji wa KM Ban Ki-moon, baada ya mkutano na waandshi habari Ijumatano adhuhuri, ameripoti KM kukaribisha kuapishwa kwa Morgan Tsvangirai kuwa Waziri Mkuu mpya wa Zimbabwe. Alisema kitendo hicho kilimaanisha hatua muhimu imechukuliwa na Zimbabwe, katika kutekeleza Mapatano ya Amani ya Septemba 15 (2008). Serikali mpya ya muungano wa taifa Zimbabwe ilinasihiwa kuikabili mizozo ya kiuchumi na kiutu yaliolivaa taifa, haraka iwezekanavyo, ikijumlisha tatizo sugu la mripuko wa maradhi ya kipindupindu ambayo yanaendelea kusumbua umma katika Zimbabwe.

11/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM asisitiza ulazima wa kudhibiti pamoja mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Russian Radio

Ijumanne adhuhuri KM Ban Ki-moon, alikutana na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu, na aliwaelezea kuhusu safari yake ya karibuni ambapo alitembelea yale maeneo yenye mizozo; na alizungumzia pia juu ya anuwai ya masuala yenye kukabili usalama na amani ya kimataifa.

11/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaongoza Mkutano wa Mwaka kuhusu Matumizi ya Teknolojiya ya Kisasa ya Mawasiliano

Nembo ya UNICEF

Mkutano wa mwaka wa UM kuhusu matumizi ya teknolojiya ya mawasiliano ya kisasa, kwa maendeleo, umefunguliwa rasmi hapa Makao Makuu Ijumatano ya leo. Kikao hiki cha tano, kinasimamiwa na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) na majadiliano ya mkutano yanatazamiwa kuendelea hadi Ijumaa, Februari 13 (2009).

11/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanachama wa OIF wakutana kutathminia maendeleo ya kuimarisha ujuzi wa kusoma na kuandika

Kadhalika, kuanzia tarehe 11 mpaka 13 Februari (2009) watakutana kwenye mji wa Lyon, Ufaransa wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayohusika na maendeleo ya ilimu, pamoja na wajumbe wa mashirika yasio ya kiserikali kutoka zile nchi 54 wanachama wa Shirika la Mataifa Yenye Kutumia Lugha ya Kifaransa (OIF).

11/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Mpatanishi Mkuu wa Pamoja wa UM-UA kwa Darfur, Djibril Yipéné Bassolé ametoa taarifa ya kupongeza Seikali ya Sudan pamoja na kundi la waasi la JEM, kwa kuridhia kukutana Doha, Qatar kwa mazungumzo ya kusimamisha uhasama yaliofanyika Ijumanne asubuhi. Bassolé alisisitiza juu ya umuhimu wa kuwajumuisha wadau wote wanaohusika na suala la Darfur, kwenye majadiliano ya kuimarisha amani. Hii ni mara ya kwanza kwa makundi haya mawili yanayohasimiana Sudan kukubali kukutana uso kwa uso, tangu 2007 baada ya mkutano wa upatanishi uliofanyika kwenye mji wa Abuja, Nigeria.

10/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA itaanzisha tena huduma zake Ghaza kufuatia kurudishwa kwa misaada iliotaifishwa

Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) limeripoti kwamba kundi la Hamas, lenye kushika madaraka kwenye eneo liliokaliwa la Tarafa ya Ghaza, limerudisha zile bidhaa za misaada ilioitaifishwa na wao wiki iliopita.

10/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa Bukini waiahidi UM watasawazisha tofauti zao kwa majadiliano

Haile Menkerios, KM Msaidizi juu ya Masuala ya Kisiasa ambaye hivi sasa yupo Bukini, Ijumatatu alikutana kwenye mji mkuu wa Antananarivo na Raisi wa Bukini, Marc Ravalomanana na pia kuonana na meya wa jiji hilo Andry Rajoelina.

10/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Helikopta ya UNAMID yashambuliwa risasi Darfur

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limeripoti kwamba mnamo Ijumatatu, helikopta yao ya aina ya Mi-8, ilishambuliwa kwa risasi na washambulizi wasiojulikana, kwenye eneo liliopo kilomita 70 kusini magharibi ya mji wa El Fasher, wakati helikopta hiyo ilipokuwa inapeleka vyakula kwa walinzi wa amani.

10/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wa JKK wamiminikia Sudan Kusini kukwepa ukatili wa LRA, imeripoti UNHCR

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) amenakiliwa na waandishi habari wa kimataifa waliopo katika Ofisi ya UM Geneva akisema kwamba waasi wa Uganda wa kundi la LRA walishambulia tena wiki iliopita maeneo ya JKK na kusababisha maelfu ya raia kukimbilia taifa jirani la Sudan Kusini:~

10/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Alain Le Roy, Naibu KM juu ya Operesheni za Ulinzi Amani ameripotiwa akiendelea na ziara ya kutembelea Afghanistan, ambapo alipokutana na waandishi habari alisema UM utaendelea kuongoza shughuli zake nchini humo, na utahakikisha uchaguzi utafanyika kwa wakati, kwa uwazi na kwa haki. Alisema UM utabakia kwa muda mrefu Afghanistan, kuimarisha maendeleo yaliopatikana kutokana na mchango wa wazalendo wenyewe, hususan katika kukuza afya bora, kuimarisha ilimu, na kusimamia shughuli za kufyeka mabomu yaliotegwa, huduma ambazo UM utasaidia kuzihimilia na kuziendeleza Afghanistan kwa siku zijazo.

09/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mikutano muhimu katika Makao Makuu

Baraza la Usalama lilikutana asubuhi kwenye Makao Makuu ya UM, chini ya uongozi wa Ujapani, Taifa Mwenyekiti kwa mwezi Februari, ambapo kulizingatiwa shughuli za Ofisi ya UM juu ya Ujenzi wa Jumla wa Amani katika Sierra Leone, UNIPSIL.

09/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID imeanzisha rasmi klabu ya amani kwa vijana Darfur

Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) katika mwisho wa wiki iliopita, kwenye mji mkuu wa jimbo wa El Fasher, vilianzisha klabu ya vijana kwenye Skuli ya Sekondari ya Wanawake, kwa makusudio ya kuwasaidia vijana kutumia klabu kubadilishana mawazo juu ya amani.

09/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake lazima washirikishwe kwenye maamuzi ya migogoro ya uchumi, imenasihi CEDAW

Kamati ya UM ya Kuondosha Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) juzi imewasilisha taarifa maalumu kutoka Geneva, inayozihimiza Serikali Wanachama kuwahusisha wanawake kwenye maamuzi ya kutatua mizozo ya kiuchumi iliokabili ulimwenngu kwa sasa hivi, mizozo ambayo athari zake ndizo zenye kuzorotisha mipango ya maendeleo ya kukamilisha usawa wa kijinsiya kimataifa.

09/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naibu KM wa masuala ya kiutu akutana na waathirika wa vurugu Kivu Kaskazini

Naibu KM wa Masuala ya Kiutu, John Holmes, Ijumapili alizuru jimbo la mgogoro la mashariki, katika JKK, ambapo alipata fursa ya kujionea, binafsi, athari za kimwili na kiakili walizopata raia wa kiume, wanawake pamoja na watoto, alipotembelea hospitali ya Heal Africa, iliopo Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

09/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahimiza uvumilivu baada ya maandamano Bukini kuzusha vifo

Ijumapili KM Ban Ki-moon, kwa kupitia msemaji wake, ametoa taarifa iliosihi makundi yanayohasimiana Bukini, kujitahidi kusuluhisha tofauti zao kwa amani. Alishtumu vikali fujo na vurugu lilioripuka Ijumamosi katika mji mkuu wa Antananarivo, ambapo inakisiwa watu 28 waliuawa na darzeni kadha walijeruhiwa.

08/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

John Holmes, KM Mdogo juu ya Masuala ya Kiutu na Mratibu wa Misaada ya Dharura ameruhusu kutolewe dola milioni 75 kutoka Mfuko wa UM kwa Maafa ya Dharura (CERF) ili kuzisaidia nchi 14 kudhibiti hali ya dharura ilioselelea kwa muda mrefu kwenye maeneo yao. Idadi kubwa ya mchango huo, yaani dola milioni 11, zitafadhiliwa huduma za kiutu katika Zimbabwe, ikifuatiwa na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini), Ethiopia na Usomali.~

06/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanyarwanda wa JKK waiomba UM iwarejeshe makwao

Idadi kubwa ya raia wa Rwanda wameonekana wakiibuka kutokea mafichoni kwenye maeneo ya mbali katika eneo la mashariki la JKK wakiiomba UNHCR iwarejeshe makwao, UM umeamua kuongeza idadi ya magari yatakayohitajika kuhamishia umma huo, na kumefunguliwa vituo ziada katika Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, ili kuwapatia makazi ya muda watu 500 kabla ya kuhamishiwa makwao.

06/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waomba hifadhi wa Usomali katika Ethiopia watahudumiwa kihali na UNHCR

UNHCR na mashirika wenzi yenye kuhudumia misaada ya kiutu, sasa wametuma wafanyakazi wao na misaada ya kihali kwenye sehemu ya mpaka ya Dolo-Ado, katika jimbo la kusini-mashariki la Ethiopia, wanapoishi raia wenye jadi ya Kisomali, ambapo inakadiriwa watu 10,000 wamemiminikia huko kuanzia Januari mwaka huu, kutokea taifa jirani la Usomali, wakiomba hifadhi ya kisiasa.

06/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR/Kenya wakagua maskani mapya kwa wahamiaji wa Usomali

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti Serikali ya Kenya imekubali kutenga ardhi maalumu, katika eneo la kaskazini mashariki ya nchi, ili kuwaweka wahamiaji wa Usomali, wanaomiminikia Kenya sasa hivi kwa idadi kubwa.

06/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO kuipatia Kenya msaada wa tiba kwa waathirika wa ajali ya moto

WHO imetangaza kuipatia Kenya yuro 50,000 kusaidia kutibu waathirika wa moto uliotokana na tangi la mafuta ya petroli, ajali ilioua karibu watu 100.

06/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wagonjwa 67,945 wasajaliwa kipindupindu Zimbabwe na WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kwamba kumesajiliwa wagonjwa 67,945 wa kipindukipindu katika Zimbabwe hivi sasa, na kati ya jumla hiyo watu 3,371 wameshafariki.~

06/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yasimamisha, kwa muda, misaada ya kihali kwa Ghaza

Shirika la UM Linalofarajia WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) limetoa taarifa yenye kusema wanasimamisha kuingia Tarafa ya Ghaza bidhaa zote za misaada, baada ya wenye madaraka kutaifisha mamia ya tani za msaada wa chakula mnamo usiku wa Alkhamisi ya tarehe 05 Februari (2009).

06/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM kufanya ziara ya ghafla Iraq

KM alizuru Baghdad, na kwenye risala yake alipokuwepo huko aliahidi UM utaendelea kuusaidia umma wa Iraq kwa kila njia kurudisha utulivu na kuimarisha maendeleo yao.

06/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNODC inahimiza utawala bora Afrika Mashariki

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) imeripoti kuibuka mkondo mkali wa uhalifu wa mpangilio, ulionekana kushtadi kwenye mataifa yaliopo ukanda wa Afrika Mashariki. Mkondo huu unahitajia kudhibitiwa mapema kabla haujasambaa zaidi kieneo na baadaye kuhatarisha usalama, inasema UNODC.

06/02/2009 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Vuguvugu la kisiasa, liliotanda Bukini kwa sasa, linamtia wasiwasi KM Ban Ki-moon kuhusu utulivu na amani ya taifa. Kufuatia ombi la Serikali ya Bukini, KM ameamua kumpeleka Haile Menkerios, aliye KM Msaidizi kwa Masuala ya Kisiasa kusailia hali Bukini, ambaye anatarajiwa kutathminia mchango wa UM unaohitajika kusaidia kuzuia vurugu lisisambae zaidi kitaifa na, hatimaye, kurudisha amani na utulivu nchini Bukini. Menkerios atakuwepo Bukini kuanzia tarehe 07 mpaka 10 Februari, na atakutana kwa mazungumzo na ushauri pamoja na maofisa wa Serikali na wawakilishi wa makundi yote yaliofungamana na mzozo uliofumka majuzi nchini humo.

05/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

BU lazingatia ripoti kuhusu hali Sudan

Baraza la Usalama leo limezingatia Ripoti ya KM kuhusu Hali katika Sudan. Vile vile Baraza limesailia operesheni za Shirika la UM Linalohusika na Mapatano ya Amani ya Jumla baina ya Sudan Kaskazini na Kusini. Tutajaribu kukupatieni dokezo ya kikao hicho mnamo siku zijazo.

05/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM ahimiza mataifa kujumuika kudhibiti kidharura mabadiliko ya hali ya hewa

KM Ban Ki-moon anahudhuria Mkutano Mkuu juu ya Maendeleo ya Kusarifika, unaofanyika mjini New Delhi, Bara Hindi ambapo aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliokusanyika huko ya kuwa walimwengu wanawajibika kukabili, kipamoja, tishio hatari, linaloendelea kupanuka kimataifa, linalochochewa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

05/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wenye njaa Ghaza kuhudumiwa na WFP vyakula viliopikwa

Wagonjwa na majeruhi waliowekwa kwenye hospitali za eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza, wanatarajiwa kupokea misaada ya vyakula vilivyopikwa tayari, kutoka Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), ili kuwanusuru na hatari ya njaa, kwa sababu ya upungufu wa chakula na nishati uliochochewa na mashambulizi ya karibuni ya Israel kwenye eneo hilo.

05/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP itaisaidia Kenya kumudu upungufu wa nafaka, madhara ya ukame na chakula ghali

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa wiki hii litatuma timu ya watathmini wataalamu, kukadiria mahitaji halisi ya chakula kwenye yale maeneo ya Kenya yanaosumbuliwa na upungufu wa mvua mnamo mwaka uliopita.

05/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA juu ya Operesheni za Amani kwa Darfur (UNAMID) vimeripoti kuwa mashambulizi bado yanendelea Ijumatano ya leo katika eneo la Muhajeriya. Ripoti pia imedai vikosi vya Serikali ya Sidan vilionekana vikifanya doria kwenye eneo liliopo karibu mita 500 kutokea kambi ya UNAMID. Kadhalika iliripotiwa, ndege isiotambulikana, ilionekana kutupa mabomu matatu hii leo, kilomita moja kutoka majengo ya UNAMID pamoja na mashambulizi yaliosababisha raia kukimbilia kwenye kambi za vikosi mseto vya kimataifa. Kambi ya wahamiaji wa ndani ya Al Salaam, katika Darfur Kaskazini imepokea wahamaji wapya 520 wakati Kambi ya Wahamiaji ya Zam Zam ilipokea wahajiri 1,400 waliokuwa wakitafuta hifadhi kutoka vurugu liliofumka karibuni kwenyeeneo lao. UNAMID inasema asilimia 90 ya wahamiaji wapya wa ndani hujumlisha wanawake na watoto wadogo, jamii ambayo imepatiwa mahema ya kujistiri.

04/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM unaadhimisha Siku ya Kudhibiti Saratani Duniani

UM pamoja na mashirika ya kimataifa yanaiadhimisha siku ya leo kuwa ni Siku ya Udhibiti wa Saratani Duniani.

04/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM afanya ziara ya dharura Afghanistan

Ijumatano KM Ban Ki-moon alifanya ziara ya ghafla katika Afghanistan. Alipokuwepo huko, KM aliahidi UM utaendelea kuchangia, kwa kila njia, kwenye zile huduma za maendeleo zinazotakikana, kidharura, kuimarisha usalama na amani ya taifa.

04/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO ina matumaini viwavi haribifu Liberia vitadhibitiwa

Timu ya wataalamu wa sayansi wa Shirika la FAO waliozuru, wiki iliopita, maeneo saba ya Liberia, kufanya utafiti kuhusu aina ya viwavi haribifu vilivyopamba nchini humo, leo wametangaza matokeo ya uchunguzi wao yaliosisitiza kwamba mripuko wa vijidudu haribifu hivyo, unaweza kudhibitiwa, kwa urahisi zaidi, kinyume na zile taarifa za siku za nyuma.

04/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukulima shadidi lazima urekibishwe kutimiza mahitaji ya chakula kwa vizazi vijavyo, asema mtaalamu wa FAO

Mtaalamu wa mimea kutoka Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) aliwaambia wajumbe karibu 1,000 waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Nne wa Kutunza Kilimo Bora, unaofanyika wiki hii kwenye mji wa New Delhi, Bara Hindi, kwamba mahitaji ya chakula kwa umma wa kimataifa unaoendelea kuongezeka, kwenye mazingira yalioathirika na mabadiliko ya hali ya hewa, mahitaji hayatoweza kutimizwa bila ya kwanza kurekibisha mifumo ya ukulima shadidi, inayotumiwa hivi sasa kimataifa.

04/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Ijumanne Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao cha mashauriano ya awali kuzingatia ajenda ya mwezi Februari, kikao kinachoongozwa na Ujapani, taifa linaloshika madaraka ya uraisi wa Baraza kwa mwezi huu. Kadhalika, Baraza la Usalama lilizingatia ripoti kuhusu hali katika Darfur iliowakilishwa na Edmond Mulet, KM Mdogo Msaidizi kwenye Idara ya Operesheni za Ulinzi Amani za UM.

03/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM umeanzisha kampeni ya kufufua huduma za kiuchumi na jamii Ghaza

Ijumatatu, mjini Geneva, John Holmes, Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu alianzisha rasmi kampeni ya kuchangisha msaada wa dola milioni 613, kutoka wahisani wa kimataifa, msaada unaohitajika kukidhi mahitaji ya kihali kwa waathirika wa mashambulizi ya karibuni ya vikosi vya Israel, yaliofanyika kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza.

03/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi wa bunge la Usomali wapongezwa na UM

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould Abdallah mapema wiki hii ametoa taarifa yenye kusifu namna uchaguzi wa kuteua wabunge wa Usomali ulivyoendeshwa karibuni nchini Djibouti, uchaguzi ambao alisema ulihudumiwa "kwa uwazi na bila kificho."

03/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwendesha mashitaka wa kesi ya Taylor ametangaza kukamilisha ushahidi

Stephen Rapp, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama Maalumu juu ya Jinai ya Vita katika Sierra Leone kwenye mahojiano ya Ijumatatu, na waandishi habari, hapa Makao Makuu alisema ya kwamba upande wa mashitaka umemaliza kuwasilisha ushahidi wa kesi dhidi ya Charles Taylor, aliyekuwa Raisi wa taifa jirani la Liberia.

03/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF inaomba ifadhiliwe dola milioni 34 kuhudumia waathirika wa mashambulio na uvamizi katika Ghaza

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Mendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetoa ombi liliopendekeza lifadhiliwe haraka mchango wa dharura wa kukidhi mahitaji ya kihali, kwa wale watoto na aila zao, ambao waliathirika hivi majuzi kutokana na mashambulio ya mabomu na vurugu lilioendelezwa na vikosi vya Israel kwenye Tarafa ya Ghaza.

03/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hapa na Pale

Shirika la UM Linalosimamia Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limetangaza taarifa yenye kufafanua, kinaganaga, kwamba haitoshiriki kamwe, kwenye shughuli za aina yoyote au kujihusisha na operesheni zinazoambatana na Bosco Ntangada, kiongozi wa kundi la wanamgambo katika JKK. MONUC ilikumbusha ya kuwa Ntangada sasa hivi ameshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) kwa makosa ya vita, ikijumlisha jinai ya kuajiri kimabavu watoto chini ya umri wa 15, waliolazimishwa kushiriki kwenye mapigano na uhasama.

02/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICTR imethibitisha tena kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa Karera

Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imethibitisha tena kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa François Karera, ambaye mnamo 07 Disemba 2007 alipatikana na hatia ya kushiriki kwenye mauaji ya halaiki, pamoja na maangamizi dhidi ya raia wenye jadi ya Kitutsi katika sekta ya Nyamirambo, wilaya ya Kigali Ville, na mauaji katika Kanisa la Ntarama mnamo 15 Aprili 1994, na pia kushiriki kwenye jinai dhidi ya utu iliofanyika katika kijiji cha Rushahi, kwenye Wilaya ya Kigali.

02/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makundi yanayohasimiana Sudan Kusini yaombwa yasimamishe mapigano, haraka

KM Ban ametoa mwito maalumu kwa Serikali ya Sudan na kundi la waasi la JEM kusimamisha, halan, shughuli zote za mapigano katika Darfur Kusini, na kuonya juu ya hatari inayoletwa na mapambano yao, kuhusu usalama wa raia. UM umepokea taarifa zenye kuonyesha kuwepo muongezeko wa vikosi vya Serikali na waasi kwenye eneo la karibu na Muhajeria, Sudan Kusini.

02/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KM asihi UA juu ya umuhimu wa mioundombinu kuimarisha maendeleo

Ifuatayo ni taarifa fupi juu ya risala ya KM Ban Ki-moon, alioiwasilisha mbele ya viongozi waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika unaofanyika sasa hivi katika mji wa Addis Ababa, Ethiopia.

02/02/2009 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930